Riwaya: UCHU

Riwaya: UCHU

Mkuu m2n ubarikiwe kwani hilo ndilo tunalolipenda kuona. Kama unaeza kutoa mchango unatoa
 
Last edited by a moderator:
Point noted mkuu..! Usijali ni mambo ya kawaida pindi watu wenyewe utofauti wa age,IQ, level of education,gender etc wanapokutana. Cha msingi tuwe tunafikia conclusion kwa pamoja as a team.
Lastly...ukipata/mkipata muda naomba muimalizie tu hii riwaya na zozote ambazo bado zipo hanging

Salute kwako mkuu
 
UCHU
GISENYI
Ilikuwa yapata saa kumi na mbili alfajiri
wakati Willy Gamba na Bibiane
walipokuwa wakiondoka nyumbani kwa
Bibiane kuelekea Goma, nchini Zaire.
Baada ya Bibiane kwenda kulala usiku na
kumwacha Willy akimpa habari Col.
Rwivanga kuhusu yote aliyoelezwa na
Bibiane, usiku, uleule Willy na Col.
Rwivanga waliamua kwenda haraka
kumkamata Col. Gatabazi nyumbani
kwake, baada ya kuchunguzi wa kina
waligudua kuwa nyumba hiyo imefungwa
na hakuna mtu. Mara moja Col. Rwivanga
akahisi kuwa Col. Gatabazi alikuwa
ameelekea kwenye majeshi yake huko
Kibumba karibu na Goma kama ambavyo
walikuwa wameelezwa na Bibiane. Hivyo,
waliafikiana kuwa asubuhi na mapema
Willy aondoke na Bibiane kwenda Goma,
kuwasaka Col. Gatabazi, Nkubana na
Jean.
Wakati huo Col. Rwivanga alikuwa
akijiandaa kwenda kutoa taarifa za uhalifu
huo kwa serikali ya RPF ili iandae jeshi la
kushambulia sehemu ya Kibumba na
kuliangamiza jeshi la Akazu pamoja na
Jean kabla halijaishambulia Rwanda tena.
Hivyo, Willy Gamba na Col. Rwivanga
walirudi nyumbani na Willy akatafuta
usingizi wa saa moja kwa ajili ya
kujiweka sawa. Ilipofika saa kumi na moja
alifajiri Willy alimuamsha Bibiane ili
waanze safari.
Willy akilipokuwa akijipumzisha, Col.
Rwivanga alitoka usiku huo kwenda
kumwona mkuu wa shirika la Msalaba
Mwekundu ambaye alikuwa rafiki yake na
kumwomba gari. Col. Rwivanga alipewa
gari ya Msalaba Mwekundu aina ya
Toyota Land Cruser GX ambalo alipanga
Willy na Bibiane walitumie kwenda
mpakani kwenye kambi ya wakimbizi ya
Kibumba. Vilevile Col. Rwivanga
aliwatanguliza vijana wake watatu askari
wa kikosi maalumu cha upelelezi kutoka
jeshi la RPF ili wawahi kufika Gisenyi na
kutoa taarifa za Col. Gatabazi kwa
makamanda wa RPF walioko Gisenyi. Pia
alituma taarifa ya siri kwa Meja Tom
Kabarisa, kiongozi wa waasi wa
Banyamulenge kikundi kilichokuwa
kikipigana kupinga serikali ya Zaire,
kilichokuwa na makao makuu yake
sehemu za milimani, karibu na mji wa
Goma. Hawa Banyamulenge walikuwa ni
watu wa asili wa Kitutsi ambao walihamia
miaka mingi eneo hili na Mashariki mwa
Zaire kutokana na misukosuko ya muda
mrefu ndani ya Rwanda.
Kwa muda mrefu watu hawa waliishi
kama wananchi wa Zaire, lakini miaka ya
hivi karibuni serikali ya Zaire ilianza
kuwabagua kiasi cha kuwanyima haki
hata ya kupiga kura na kisha kuwataka
wahame maeneo waliyokuwa wakiishi
ndani ya Zaire ili warudi kwao Rwanda.
Lakini walikataa katakata kutii amri hii ya
serikali ya Zaire na kuanzisha kikundi
chao cha wapiganaji ili kiweze kulinda
maslahi yao. Kikundi hiki kilikuwa na
mahusiano mazuri na maofisa wa jeshi la
RPF. Wakati na baada ya mauaji ya
Watutsi na Wahutu kukimbilia eneo hili la
Ziwa Kivu, uhusiano wa Banyamulenge na
uongozi wa RPF uliimarika zaidi kwa
sababu za kiusalama kwa pande zote
mbili.
"Mimi niko tayari kwa safari, lakini
naomba tupite pale nyumbani kwangu ili
nipate nguo za safari ya namna hii na
nyenzo nyingine ambazo zinaweza
kutusaidia katika safari yetu", Bibiane
ambaye alikuwa ametokea chumbani na
kujiegemeza kwenye ukuta alisema.
Willy na Col. Rwivanga waliokuwa
wanapanga mikakati huku wameupa
mgongo ule upande wa chumba
waligeuka na kumwangalia. Alfajiri hii
Bibiane alionekana mrembo hata zaidi ya
jana yake.
Willy na Col. Rwivanga walitazamana tena
na kutabasamu huku macho ya Col.
Rwivanga yakimweleza Willy kuwa. "Haya
kazi unayo".
"Mmenisikia?", Bibiane aliuliza tena.
"Sawa", Willy alijibu kisha kama
amekumbuka kitu akahoji, "Lakini sijui
kama pale kwako tutaweza kuruhusiwa
kuingia".
"Tutaenda wote", Col. Rwivanga alijibu.
Kisha Col. Rwivanga alimmalizia Willy
maelezo na mipango yote, wakaondoka
kuelekea nyumbani kwa Bibiane.
Kwa vile kulikuwa bado
hakujapambazuka, walipofika nyumbani
kwa Bibiane ilibidi Col. Rwivanga atoke na
kujitambulisha kwa askari wapatao wanne
waliokuwa wamejitokeza baada ya
kusikia mwungurumo wa gari. Kisha
lango la mbele lilifunguliwa wakaingiza
gari ndani. Baada ya maelezo mengine
mafupi, Bibiane aliruhusiwa kuingia ndani.
"Karibuni", Bibiane aliwakaribisha Willy na
Col. Rwivanga ndani.
Bibiane aliingia chumbani na kuwaacha
Col. Rwivanga na Willy sebuleni. Nyumba
ilikuwa bado kabisa haijakaguliwa. Hivyo,
kila kitu kilikuwa kimebaki kama
kilivyokuwa isipokuwa maiti za wale tu
ndizo zilikuwa zimeondolewa.
"Willy njoo", Bibiane alimwita Willy
chumbani kwake. Willy na Col. Rwivanga
waliangalia na kutabasamu, baada ya
sekunde kadhaa Col. Rwivanga
alimuonyesha Willy ishara aende
chumbani kama alivyoitwa.
Willy alipoingia chumbani alimkuta
Bibiane anavaa suluali lakini sehemu ya
juu yote ilikuwa bado iko wazi yaani
hajavaa kitu hata sidiria.
"Hatuna muda wa kukaa hapa hivyo
itabidi unisaidie vitu vingine ili tuweze
kuondoka mapema", Bibiane alimwambia
Willy ambaye alikuwa kama amepigwa na
butwaa. Hakika msichana huyu alikuwa
mzuri, umbo lake jinsi alivyoumbika
hutaamini kama alizaliwa kutoka tumboni
kwa mwanamke isipokuwa alishushwa
kutoka juu. Hakukuwa na maelezo ya
kutosha kueleza urembo wa msichana
huyu bali ujitahidi kumtafuta ili uthibitishe
mwenyewe kama Willy alivyojionea.
Usinitie majaribioni", Willy alisema huku
akirudisha mlango.
"Aaa mshirika, mapigo yangu nikitaka
utayaweza?. Kazi kwanza mambo
mengine baadaye. Nimekuita kwa sababu
hatuna muda wa kukaa hapa nataka
kukuonyesha kitu", Bibiane alisogea
kwenye ukuta akabonyeza sehemu na
ukuta ule ukafunguka. Willy alishangazwa
kuona kumbe ule haukuwa ukuta
isipokuwa kabati la siri lililojificha likiwa
na zana mbalimbali za kazi za kisasa
kabisa.
"Pale mwisho kuna makasha mawili
makubwa yameandikwa 'hatari', yatoe",
Bibiane alimwambia Willy huku akichukua
sidiria na kuendelea kuvaa.
Willy aliyatoa na kuyaweka chini.
"Fungua", alisema huku akiendelea kuvaa.
Willy alipofungua alikuta ni mabomu aina
ambayo hakuwahi kuyaona wala
kuyatumia kabisa.
"Haya ni mabomu aina ya teknolojia ya
kisasa kabisa, ambayo Jean aliniletea
siku chache tu zilizopita, akanielekeza
niyahifadhi mpaka nitakapopata
maelekezo zaidi. Lakini yule mtu wa DOSE
aliyeleta silaha hizi alinieleza jinsi
zinavyotumika na kweli ni aina ya
mabumu ya kisasa na hatari sana",
Bibiane alieleza huku akivaa viatu na
kutengeneza nywele zake. Alimweleza
Willy jinsi mabomu hayo yanavyofanya
kazi na kumalizia. "Hayo mabomu mawili
yana uwezo wa kulipua nusu ya mji wa
Kigali, na kwa kutumia saa hii ninayokupa
unaweza kulipua mji wa Kigali huku
umeketi mahali unakunywa chai.
"Ili mradi tu usiwe umetega na nyumba
yako au ya majirani zako", Willy alitania
na wote wakacheka.
Willy alikubaliana na Bibiane kuwa
waende na makasha yote mawili, maana
kutokana na maelezo ya Bibiane, Jean na
Akazu walikuwa wameandaa jeshi kamili
kwa ajili ya kuivamia Rwanda, wakiwa na
silaha kali na za kisasa kutoka Ufaransa
na Afrika Kusini, huku wakitumia
kisingizio cha wakimbizi. Kisha Bibiane
alitoa bastola nne, mbili zikiwa
ndogondogo sana alizoziweka kwenye
mkoba na mbili kubwa alizomkabidhi
Willy, vilevile alichukua risasi nyingi sana.
"Nafikiri sasa tuko tayari", Bibiane
alisema huku akimsaidia Willy kubeba
kasha moja na mfuko wake wa nguo.
"Ehe, vipi huko ndani?", Col. Rwivanga
aliuliza.
Kabla Willy hajajibu Bibiane
alijibu."Salama kabisa".
Wote wakacheka, kisha kwa kifupi, Willy
akamweleza Col. Rwivanga kuhusu
kilichokuwa ndani ya yale makasha
waliyotoka nayo ndani.
Baada ya hapo, Willy na Bibiane waliingia
ndani ya gari na kumtakia Col. Rwivanga
heri ya kuonana, kisha wakaanza safari
ambayo hawakuwa na uhakika kama
mambo yangeendaje huko.
"Mungu awe pamoja nanyi, naamini
atawasaidia", Col. Rwivanga aliwaaga,
askari waliokuwa wakilinda nyumba ile
waliwafungulia lango wakatoka na
kutokomea kuelekea Kibunda.
 
zamu ya mareche sasa. tunawasubiri m2n, Willy Gamba, kidi kudi waje wajazie jazie. tutafika tu
 
Endeleza mkuu mareche nina-appriciate kazi nzuri uifanyayo
 
Last edited by a moderator:
Naomba mmalizie wakukuu niliko mimi ni 6:00 usiku nisilale hivi hivi jamani.
 
Back
Top Bottom