kidi kudi
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 2,489
- 2,106
- Thread starter
- #201
NGUVU YA RUSHWA--IV
Bibiane alipomaliza kuoga alimkuta Willy
amemtengea kikombe.
"Kahawa au chai?"
"Kahawa."
Willy alimmiminia kahawa na alipotaka
kumwekea sukari Bibiane alikataa.
"Bila sukari," alisema.
Kwa mara ya kwanza vilevile Bibiane
alimuangalia Willy vizuri na kumuona
mwanaume mzuri sana, na alipofikiria
namna alivyowasambaratisha akina
Xavier na kundi lao, mwili wake mara
moja ulisisimuka. Halafu, palepale
akamfikiria Jean na jinsi alivyompenda na
kumfanyia kila kitu lakini akaamua
kumuua. Hasira ilimpanda sana, na
akaapa kiroho kuwa kwa vile yupo hai
atalipiza kisasi.
"Unafikiri nini?" Willy alimwuliza Bibiane.
"Ahera."
"Umeshapona sasa?".
"Xavier alisema mimi na wewe tutaonana
ahera baada ya masaa machache, akili
yangu inafikiri huenda tupo ahera." wote
walicheka.
"Uko tayari kuzungumza lolote," Willy
alimuuliza Bibiane huku sauti yake ikiwa
imebadilika ghafla na kuwa sauti yenye
uzito fulani.
"Niko tayari, nimekuambia kila
unachotaka," Bibiane alijibu kwa sauti ya
mahaba.
"Wewe ni nani?" Willy alimwuliza.
"Mimi naitwa Bibiane Habyarimana, ni
Mnyarwanda, na wewe?".
Willy alishtuka namna alivyo mjibu na
kuzidi kuimarisha hisia zake kuwa huyu
msichana vilevile alikuwa si mtu wa
hivihivi ila alikuwa mtaalamu katika
nyanja kama yake. Mara ya kwanza
alipohisi, ilikuwa jinsi alivyojirusha nyuma
ya kochi pale nyumbani kwake baada ya
yeye kuwapiga risasi wale watu wawili, na
alivyochupa dirishani kumfuata Xavier.
Kwanza alifikiri alikuwa na mafunzo ya
kijeshi tu, lakini kutokana na jinsi ya
majibizano yao aligundua alikuwa na
utaalamu zaidi.
"Willy Gamba, Mtanzania," alijibu na wote
wakaangaliana kama wanapimana saizi.
"Ningependa nijue historia yako nzima, na
usinifiche kitu, mpaka kufikia uhusiano
wako na hawa wauaji na hasa huyu
aliyekuhukumu kifo bwana Jean", Willy
alimwambia Bibiane.
"Nimeshatoa kauli yangu kuwa
nitakueleza kila kitu unachotaka niseme.
Hivyo, usiwe na wasiwasi nitakueleza, ila
itabidi uwe na subira maana ni hadithi
ndefu", Bibiane alijibu.
Bibiane alimweleza Willy kwa kirefu
maisha yake ya utoto, maisha ya shule,
juu ya baba yake na mama yake na
akaendelea, "Mwaka nilipoanza kazi
baada ya kuhitimu digirii ya kwanza ya
lugha katika Chuo Kikuu cha Kigali,
wazazi wangu wote wawili walikufa kwa
ajali. Nilikuwa nimeanza kazi Wizara ya
Mambo ya Nje kama mkalimani.
"Inasemekana kuwa wazazi wangu
hawakufa kwa ajali ya kawaida ila
waliuawa na vikaragosi vya Watutsi
ambao walifikiri kuwa baba yangu alikuwa
ndugu yake na Rais. Hivyo waliwaua
wazazi wangu ili kumkomoa Rais. Kitendo
hicho kiliniuma sana nikawachukia sana
Watutsi", Bibiane alieleza.
"Pole sana", Willy alisema kwa sauti ya
huruma.
"Kwa kunisikitikia kutokana na
yaliyowakuta wazazi wangu, serikali
ikanihamishia ofisi ya Rais, huko ndiko
nilipokutana na Jean Yves Francois, yeye
ni Mfaransa anaishi Paris lakini alikuwa
rafiki kipenzi na Rais. Tulionana naye
nyumbani kwa Rais ambako alikaribishwa
na tulianza urafiki siku hiyohiyo", Bibiane
alieleza Willy huku akimwangalia kwa
jicho la kuiba.
"Huyu Jean Yves Francois ndiye
aliyekufundisha ujasusi?", Willy
alimuuliza.
"Umejuaje?".
"Nimehisi".
"Jean ni mfanyabiashara na alikuwa
akifanya biashara na kundi la marafiki wa
Rais pamoja na familia ya Rais, wakati
mimi nafahamiana naye serikali ilikuwa
imeanza kuwa na matatizo kwani Watutsi
waliokuwa humu ndani na nje, nchini
kwenu na Uganda walikuwa wakipigana ili
waiangushe serikali. Jean ndiye aliyekuwa
akimsaidia Rais kwa kumjenga kijeshi,
kiusalama na kiutawala. Huyu Jean ana
utajiri usio kifani, kwani ndiye
anayezifadhili serikali na wakuu wengi wa
nchi za Afrika. Kwa vile mimi pia nilikuwa
kwenye himaya yake alinipeleka kwenye
mafunzo ya kiusalama sehemu
mbalimbali duniani".
"Na ukahitimu vizuri", Willy alidakia.
"Vizuri sana".
"Ehee, endelea".
"Si ni wewe unanikatisha".
"Huu utajiri aliupataje?", Willy aliuliza.
"Sijui mwenyewe ameupataje, ila
anashughulika na mambo ya silaha. Hapa
alikuwa analeta silaha, halafu anachukua
chai yote na kahawa inayolimwa katika
nchi. Hili suala ni moja ya malalamiko
mengi ya wananchi maana Jean ndiye
aliyekuwa akipanga bei anayotaka, na
hakukuwa na mtu wa kusema kitu, maana
alikuwa akifanya biashara na Rais na
kundi lake, lililokuwa likiitwa Akazu.
Kusema kweli Jean na hilo kundi la Akazu
ndio waliokuwa wanatawala na si baraza
la mawaziri au Bunge", Bibiane aliendelea
huku sasa Willy akimsikiliza kwa makini
zaidi.
"Huoni kuwa hiyo haikuwa sawa?", Willy
aliuliza.
"Mimi ningefanya nini, nilibaki kufanya
kila nilichoagizwa kama ilivyokuwa kwa
wengine wengi maana sasa hii ndio
ilikuwa namna ya maisha. Ama uko na
Akazu, vinginevyo hupati kitu cha aina
yoyote, iwe mali, elimu au kazi ya aina
yoyote Rwanda".
"Kwa hiyo rushwa ndio ilitawala utawala
uliopita?", Willy aliuliza.
"Inategemea unavyotafasiri rushwa",
Bibiane alijibu huku akiwa kama haelewi
anasema nini.
"Rushwa ni pale vyombo vya serikali
vinaposhindwa kufanya kazi zake, kwa
sababu hiyo kushindwa kutoa haki kwa
wananchi wake, na kuwafanya wananchi
wengi wapoteze imani, utu, uhuru na
maadili kwa serikali yao kwani wote sasa
huishi kama wanyama ambapo mwenye
nguvu na pesa ndiye anayepata
anachohitaji", Bibiane alisema.
"Hivyo ndivyo, maana nchi inakosa
maendeleo kwani mapato yote ya nchi
badala ya kuendeleza watu wote huingia
kwenye mifuko ya watu wachache. Na
kama ulivyosema uhalali wa serikali
kama chombo cha watu unakwisha,
badala yale wale wanaofaidika ndio
wanakuwa na nguvu zaidi ya serikali
yenyewe", Willy alitafasiri rushwa.
"Kwa tafasiri hiyo nakubali kuwa rushwa
ndiyo imetawala. Na sasa Watutsi na
Wahutu walipoanza kudai demokrasia
isingewezekana maana Jean na Akazu
hawakutaka kusikia kitu kama hicho kwa
vile kingeweza kuingila maslahi yao. Na
ndio sababu Watutsi walipokazana na
kusikia eti wako tayari hata kupigana na
Akazu, kwa kufadhiliwa na Jean, walianza
kulifundisha jeshi la wahutu lililoitwa
Intarahamwe ili liweze kuwadhibiti Watutsi
wa ndani na nje ya Rwanda".
"Kwa hiyo huyu bwanako Jean ndiye
alikuwa Rais hapa?".
"Si hapa tu, mimi najuwa nchi nyingi
ambako amewakamata wakuu wa nchi na
viongozi wa ngazi za juu serikalini na
anawajaza mapesa kila wakati".
"Huoni kuwa yeye ndiye ananufaika zaidi,
maana anajaza mapesa watu wachache
lakini yeye anachukuwa mali za wananchi
wengi", Willy alijaribu kumwelimisha
Bibiane.
"Najuwa, maana hata huko kwenu
Tanzania pia amewakamata wakubwa,
ndio sababu nchi yenu imekuwa ikisita
juu ya suala hili la Rwanda".
Willy alisitushwa na taarifa hii lakini
hakutaka kujionyesha maana kweli
msimamo wa serikali ya Tanzania ulikuwa
unalegalega kabla na hata baada ya
mauaji.
"Ina maana maamzi yoyote ilikuwa lazima
Jean akubaliane nao?".
"Ndiyo, na mapesa yalitembea sana
kuhusu swala hili na viongozi wengi
wamenufaika. Unafikiri kama swala hili
lingefanyiwa maamuzi mapema mauaji
yangetokea!", Bibiane alimwambia Willy
kwa njia ya kushangaza.
"Kwa hiyo huyu Jean ndiye aliamru
mauaji haya?".
"Baada ya Rais kuonekana kwamba
angekubali mkataba wa Arusha. Jean na
Akazu walikasirika sana maana
hawakutaka, kama nilivyosema mwanzo,
kugawana madaraka na mtu mwingine.
Hii ingegusa maslahi yao. Kwa hiyo,
kwanza ndio waliamru Rais auawe na pili
tayari walikuwa wamewatayarisha na
kuwahamasisha Wahutu kuwamaliza
Watutsi wote asibaki mtu ili wajihakikishie
uwezo wa kutawala milele. Mpango
ulikuwa kwamba hata kama jeshi la RPF
la Watutsi lingeshinda jeshi lao lazima
baada ya kuchukuwa nchi wangeshindwa
kutawala maana wangemtawala nani
huku Watutsi wote wakiwa
wameshauawa, waliobaki ni Wahutu
watupu ambao hawawaungi mkono.
Hivyo, ingewachukuwa siku chache
kuuangusha na kuutokomeza kabisa
utawala wa RPF. Hii ingebaki nchi ya
Wahutu chini ya utawala wa Jean na
Akazu.
Bibiane alipofika hapa ndipo Willy
alipoanza kuelewa kwa undani mambo
yalivyokuwa. Kumbe mauaji yote haya
yalitokana na watu wachache kutaka
kulinda maslahi yao ya kunyonya mali ya
wananchi, na kutumia hiyo mali kuweza
kuwachochea wananchi kuuana!.
Kwa mara ya kwanza Willy aliona jinsi
ambavyo nchi zote za Afrika zilivyo
hatarini kutokana na rushwa. Kwa vile
viongozi wa nchi hizi kuabudu rushwa,
hivyo Willy akaamini kuwa tukio kama la
Rwanda kumbe linaweza kutokea mahali
pengine katika Afrika!.
"Baada ya RPF kushinda na mipango ya
Jean kushindwa, wana mikakati gani
sasa?", Willy alihoji.
"Kama nilivyosema hawajashindwa. Wewe
ndiye umeingilia ndani ya mipango yao,
kuna mpango kabambe wa
kuisambaratisha serikali ya RPF kutokea
jimbo la Kivu, Zaire. Akazu wamekuwa
wakiliimarisha jeshi lao katika makambi
ya wakimbizi kule Goma na Bukavu,
Zaire, huku Jean akiwatumia rafiki zake
kutoka Afrika Kusini hasa waliowahi kuwa
katika idara ya ujasusi ya makaburu,
alikokuwa akinunua silaha na kuzipitishia
Angola ya UNITA, Zaire na Zambia kwa
kutumia viongozi wa ngazi za juu za
serikali za nchi hizo ambao wako kwenye
orodha ya malipo kutoka kwa Jean. Kwa
hiyo mambo bdo sana Willy, vita ndio
sasa karibu vitaanza".
"yaani dunia inafikiri kuwa kambi zilizoko
Zaire ni za wakimbizi kumbe ni kambi za
jeshi".
"Ni kambi za jeshi na serikali ya Zaire
inajua na ndio inayosaidia hata mafunzo.
Hata katika kambi zilizoko kwenu
Tanzania kuna wanajeshi wa jeshi la
zamani na Intarahamwe, na kuna watu
wazito katika serikali yenu ambao
wanalipwa na huyu Jean ili kuwasaidia
hawa watu, kwa hiyo hili si dogo. Kama
ulivyosema pesa ni kitu kibaya sana,
watu hawaoni tena madhara ya mauaji
yaliyotokea bali wanaona pesa tu".
"Swala la rushwa ni swala linalohujumu
haki za binadamu, yapaswa lichukuliwe
hatua kimataifa katika uzito huo wa haki
za binadamu", Willy alijibu kwa hasira.
Bibiane alikaa kimya bila kujibu kitu.
"Wewe ulikuwa uwasaidie vipi Jean na
Akazu katika kutekeleza huu mpango wao
wa kuivamia tena Rwanda", Willy aliuliza.
"Usije ukanipeleka kwenye mahakama ya
mauaji ya Arusha maana mauaji yale
sikuyajuwa pia sikushiriki, nilikuwa
Nairobi nikitokea kwenye mkutano Arusha.
Ila juu ya hili la sasa Jean amekuwa
akinituma kupashana habari kati ya
kambi za wakimbizi ambazo ni kambi za
jeshi lao huko Zaire, yeye na Akazu.
Vilevile kuna wanajeshi na viongozi wa
RPF ambao tayari wamenunuliwa na wako
upande wa Akazu, mmoja wao ndiye
anayetarajiwa kuchukua madaraka mara
tu jeshi la Akazu litakapotwaa madaraka
tena".
Willy hakuamini masikio yake kuwa tayari
hata ndani ya RPF kuna wasaliti.
Mara moja Willy alielewa jinsi alivyotaka
kuuawa na akagudua kuwa kweli kama
anavyosema Bibiane kuna kiongozi wa
juu na karibu sana katika serikali ya
Tanzania amabye anamtumikia Jean na
kundi la Akazu.
"Utasaidia kunipa majina ya watu wote
unaowajuwa kuwa wanahusika, maana
hiyo ndio njia pekee tunaweza kulikosha
jina lako", Willy alimuasa Bibiane.
"Swala la Jean kunisaliti mimi, na
kunihukumu kifo, bila kujali yote
niliyomtendea kwa hali na mali ikiwa
pamoja na kumpa mwili wangu auchezee
atakavyo, na jinsi nilivyojitoa
kumstarehesha. Willy mimi niko upande
wako, kama uko tayari kupambana nao
nihesabu na mimi. Jean akishaambiwa
kuwa umenichukua ninavyomjua atataka
apambane na wewe yeye mwenyewe,
ikifika hapo niachie mimi. Majina na
mipango yao yote ni juu yako na uongozi
wa RPF mjuwe la kufanya kwani jeshi la
Akazu, likisaidiwa na viongozi wa nchi
kadhaa ambao ni marafiki na Jean
watakuwa tayari kuingilia kati. Ni lazima
liwahiwe mapema kabla halijajiimarisha
sawasawa", Bibiane alieleza.
"Nafikiri swala la vita si letu, ni la serikali
ya Rwanda na RPF, mimi nipe hayo
majina na kutokea hapo ndipo nitajua
kama kazi yangu imeisha au ndio kwanza
inaanza", Willy alieleza taratibu.
Bila kuwa ameandika mahali popote,
Bibiane alitoa kichwani jina hadi jina
akianza na kundi la Akazu mpaka
viongozi wa nchi mbalimbali wanaolipwa
na Jean huku Willy akiyaandika chini kwa
mshangao mkubwa, kwani watu
waliokuwa wanatarajiwa wengi wao ni
viongozi wanaoheshimika Afrika na kote
duniani. Alishangaa zaidi Bibiane
alipotaja jina la yule waliyekuwa
wakimwita JKS wa Tanzania.
"JKS, hii imenishangaza sana, maana
huyu ndiye anayetegemewa kugombea
urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu
unaokuja," Willy alimweleza Bibiane.
"Najua kabisa, na tayari Jean
ameshamtengea mamilioni ya dola za
Kimarekani zitakazo msaidia katika
kampeni hiyo ya uchaguzi kuusaka urais.
Nia ya Jean ni kuwa na marais vibaraka
kote Afrika ili yeye na wenzake huko
Ulaya, waweze kufanya vile wanavyotaka
katika nchi hizi. Jean anaongoza kundi la
wafanyabiashara wakubwa wanaomiliki
makampuni makubwa ya kimataifa. Na
nia yao ni kuhakikisha kuwa Afrika
inakuwa soko lao tu, na hata siku moja
Afrika isisimame kiuchumi. Ingawaje nchi
zao zinapigia kelele rushwa, lakini nchi
hizohizo ndizo zinazoyasaidia
makampuni makubwa kwa madogo kutoa
rushwa kwa nchi zinazoendelea, maana
makampuni hayo yakitoa hongo, hongo
hii huchukuliwa kama gharama na
kutolewa kwenye kodi ya mapato. Hii yote
inaonyesha unafiki wa nchi za magharibi,
na kila wakati Jean alikuwa akinieleza
kuwa kelele zote hizi kuhusu rushwa,
demokrasia na soko huria ni kelele za
kinafiki tu, lakini huku nyuma katika vikao
vya viongozi wa nchi za magharibi ni
kuchochea rushwa. Wanajuwa kuwa
rushwa ikiisha Afrika basi demokrasia na
soko huria vitashamiri na hivyo uchumi
wa nchi hizo utakua haraka sana, kitu
ambacho hawataki kitokee. Jean
anasema, rushwa ndiyo sera inayotumiwa
kuendeleza umaskini katika nchi za Afrika
ili nchi zilizo endelea ziendelee kuitawala
Afrika kiuchumi. Kwa hiyo, iwapo JKS
ataitawala Tanzania rushwa itazidi mara
dufu, na kutokana na fedha alizotengewa
na Jean lazima atashinda, kwani kila
walipoweka mtu wao hajawahi kushindwa
uchaguzi", Bibiane alieleza.
Sasa Willy alikuwa na picha kamili namna
JKS alivyokuwa anahusika na swala zima
la Rwanda. na sababu za Tanzania
kutokuwa na msimamo dhabiti juu ya
swala hili na kuweza kuyumbisha
mikutano kule Arusha kiasi cha kutofikia
maamzi kwa muda mrefu maana swala
hili la Rwanda kwa muda mrefu lilikuwa
chini ya Tanzania kwa muda mrefu na
JKS alikuwa mmojawapo wa viongozi
walioonyesha kuchoshwa na mauaji ya
Rwanda. Na alifanya hivyo kwa shinikizo
la Jean aliyekuwa akimlipa pesa nyingi na
uchu wake wa kutaka madaraka kwa njia
ya ruswa ili aweze kuyatumia kwa faida
yake na kujinifaisha yeye na rafiki zake.
Na ni hii rushwa iliyowanyima
Wanyarwanda haki yao mpaka kufikia
hatua ya kuuawa vibaya namna ile kweli
ni aibu! Aibu sana kwa Afrika nzima.
"Vizazi vijavyo vitakapoyasoma na
kuyaelewa matukio haya, hakika
hawataamini, watajuwa sisi wote tulikuwa
wendawazimu kabisa, kwani ni sisi wote
ndio tulioachia hali hii ikafikia hapo ilipo,
kwa kuwapa walarushwa madaraka kwa
gharama ndogo ya kuuza kura zetu na
wao kutumia madaraka tuliyowapa kwa
malipo ya fedha kidogo, lazima
wayatumie kutuangamiza", Willy alisema
kwa uchungu huku akikuna kichwa chake.
Mara moja Willy alimkumbuka Malisa wa
Arusha, aliyekuwa mshauri wa JKS katika
masuala ya uhusiano wa Kimataifa kabla
hajarudi Chuo Kikuu. Hivyo basi, alijuwa
Malisa ndiye aliyemweleza JKS kuhusu
msimamo na mipango ya PAM na
kuteuliwa kwa Willy kufuatilia jambo hili.
Willy aliamini kuwa JKS ndiye aliyetoa
taarifa za safari ya Rwanda kwa Jean na
kundi lake na ndi sababu ndege
aliyopanda ikapigwa kabla ya kutua
uwanja wa ndege wa Kigali.
"Kwa hiyo JKS ndiye aliyotoa habari
zangu zote kwa Jean?", Willy aliuliza kwa
shauku.
"Ndio, na ndio sababu Col. Gatabazi
aliamru ndege hiyo ipigwe kabla ya kutua
uwanja wa ndege, lakini kwa bahati na
umahiri wako ukawaponyoka", Bibiane
alijibu huku akimwemwesa. Mara mlango
wa mbele ukafunguliwa na Col. Gatabazi
akaingia ndani.
Willy alipoangalia saa yake ilikuwa yapata
saa tisa usiku. Wote walisimama, na Willy
akawatambulisha.
"Pole Kanali, leo tumepata mgeni na
anaitwa Bibiane, na Bibiane huyu ndiye
mwenyeji wetu. Col. Rwivanga, kiongozi
katika serikali mpya ya RPF".
"Nashukuru kumfahamu", Col. Rwivanga
alijibu.
"Nami nimefurahi kukuona leo, nimekuwa
nikisikia sifa zako nyingi kwa muda
mrefu, toka kwa Col. Gatabazi kuwa wewe
ni mpiganaji hodari, hongera", Bibiane
alijibu kwa tabasamu akimwangalia Col.
Rwivanga.
"Asante kwa sifa hizo zilizotoka katika
kinywa cha msichana mrembo kama
wewe", Col. Rwivanga alijibu akaendelea,
"Ehe, imekuwaje Willy, hebu nipe habari
kamili, maana kazi tumeiona kwa Bibiane,
sasa halafu ikawaje hivi", Col. Rwivanga
alionekana kuwa wasiwasi na Bibiane.
"Mimi naomba nikalale ili mzungumze
vizuri, nionyeshe chumba cha kulala",
Bibiane aliomba.
Willy na Col. Rwivanga aliangaliana na
Willy ndiye alikuwa wa kwanza kujibu,
"Kwa vile nyumba hii ina vyumba viwili tu
vya kulala, basi kalale chumbani kwangu,
maana tayari hata kuoga umeoga huko.
Mimi nitalala hapa sebuleni kwenye kochi
hamna taabu".
"Asante", Bibiane aliwaaga na kuelekea
chumbani huku wote wakimwangalia.
Kisha wakatazamana na kutabasamu.
"Ehe, hebu nipe mambo".
Willy alichukua muda mrefu kumweleza
mambo yalivyotokea na mambo mengine
yote aliyoelezwa na Bibiane. Col.
Rwivanga akasimama na kumshika
mkono Willy kwa hatua aliyofikia haraka
na kwa umakini mkubwa.
ITAENDELEA
Bibiane alipomaliza kuoga alimkuta Willy
amemtengea kikombe.
"Kahawa au chai?"
"Kahawa."
Willy alimmiminia kahawa na alipotaka
kumwekea sukari Bibiane alikataa.
"Bila sukari," alisema.
Kwa mara ya kwanza vilevile Bibiane
alimuangalia Willy vizuri na kumuona
mwanaume mzuri sana, na alipofikiria
namna alivyowasambaratisha akina
Xavier na kundi lao, mwili wake mara
moja ulisisimuka. Halafu, palepale
akamfikiria Jean na jinsi alivyompenda na
kumfanyia kila kitu lakini akaamua
kumuua. Hasira ilimpanda sana, na
akaapa kiroho kuwa kwa vile yupo hai
atalipiza kisasi.
"Unafikiri nini?" Willy alimwuliza Bibiane.
"Ahera."
"Umeshapona sasa?".
"Xavier alisema mimi na wewe tutaonana
ahera baada ya masaa machache, akili
yangu inafikiri huenda tupo ahera." wote
walicheka.
"Uko tayari kuzungumza lolote," Willy
alimuuliza Bibiane huku sauti yake ikiwa
imebadilika ghafla na kuwa sauti yenye
uzito fulani.
"Niko tayari, nimekuambia kila
unachotaka," Bibiane alijibu kwa sauti ya
mahaba.
"Wewe ni nani?" Willy alimwuliza.
"Mimi naitwa Bibiane Habyarimana, ni
Mnyarwanda, na wewe?".
Willy alishtuka namna alivyo mjibu na
kuzidi kuimarisha hisia zake kuwa huyu
msichana vilevile alikuwa si mtu wa
hivihivi ila alikuwa mtaalamu katika
nyanja kama yake. Mara ya kwanza
alipohisi, ilikuwa jinsi alivyojirusha nyuma
ya kochi pale nyumbani kwake baada ya
yeye kuwapiga risasi wale watu wawili, na
alivyochupa dirishani kumfuata Xavier.
Kwanza alifikiri alikuwa na mafunzo ya
kijeshi tu, lakini kutokana na jinsi ya
majibizano yao aligundua alikuwa na
utaalamu zaidi.
"Willy Gamba, Mtanzania," alijibu na wote
wakaangaliana kama wanapimana saizi.
"Ningependa nijue historia yako nzima, na
usinifiche kitu, mpaka kufikia uhusiano
wako na hawa wauaji na hasa huyu
aliyekuhukumu kifo bwana Jean", Willy
alimwambia Bibiane.
"Nimeshatoa kauli yangu kuwa
nitakueleza kila kitu unachotaka niseme.
Hivyo, usiwe na wasiwasi nitakueleza, ila
itabidi uwe na subira maana ni hadithi
ndefu", Bibiane alijibu.
Bibiane alimweleza Willy kwa kirefu
maisha yake ya utoto, maisha ya shule,
juu ya baba yake na mama yake na
akaendelea, "Mwaka nilipoanza kazi
baada ya kuhitimu digirii ya kwanza ya
lugha katika Chuo Kikuu cha Kigali,
wazazi wangu wote wawili walikufa kwa
ajali. Nilikuwa nimeanza kazi Wizara ya
Mambo ya Nje kama mkalimani.
"Inasemekana kuwa wazazi wangu
hawakufa kwa ajali ya kawaida ila
waliuawa na vikaragosi vya Watutsi
ambao walifikiri kuwa baba yangu alikuwa
ndugu yake na Rais. Hivyo waliwaua
wazazi wangu ili kumkomoa Rais. Kitendo
hicho kiliniuma sana nikawachukia sana
Watutsi", Bibiane alieleza.
"Pole sana", Willy alisema kwa sauti ya
huruma.
"Kwa kunisikitikia kutokana na
yaliyowakuta wazazi wangu, serikali
ikanihamishia ofisi ya Rais, huko ndiko
nilipokutana na Jean Yves Francois, yeye
ni Mfaransa anaishi Paris lakini alikuwa
rafiki kipenzi na Rais. Tulionana naye
nyumbani kwa Rais ambako alikaribishwa
na tulianza urafiki siku hiyohiyo", Bibiane
alieleza Willy huku akimwangalia kwa
jicho la kuiba.
"Huyu Jean Yves Francois ndiye
aliyekufundisha ujasusi?", Willy
alimuuliza.
"Umejuaje?".
"Nimehisi".
"Jean ni mfanyabiashara na alikuwa
akifanya biashara na kundi la marafiki wa
Rais pamoja na familia ya Rais, wakati
mimi nafahamiana naye serikali ilikuwa
imeanza kuwa na matatizo kwani Watutsi
waliokuwa humu ndani na nje, nchini
kwenu na Uganda walikuwa wakipigana ili
waiangushe serikali. Jean ndiye aliyekuwa
akimsaidia Rais kwa kumjenga kijeshi,
kiusalama na kiutawala. Huyu Jean ana
utajiri usio kifani, kwani ndiye
anayezifadhili serikali na wakuu wengi wa
nchi za Afrika. Kwa vile mimi pia nilikuwa
kwenye himaya yake alinipeleka kwenye
mafunzo ya kiusalama sehemu
mbalimbali duniani".
"Na ukahitimu vizuri", Willy alidakia.
"Vizuri sana".
"Ehee, endelea".
"Si ni wewe unanikatisha".
"Huu utajiri aliupataje?", Willy aliuliza.
"Sijui mwenyewe ameupataje, ila
anashughulika na mambo ya silaha. Hapa
alikuwa analeta silaha, halafu anachukua
chai yote na kahawa inayolimwa katika
nchi. Hili suala ni moja ya malalamiko
mengi ya wananchi maana Jean ndiye
aliyekuwa akipanga bei anayotaka, na
hakukuwa na mtu wa kusema kitu, maana
alikuwa akifanya biashara na Rais na
kundi lake, lililokuwa likiitwa Akazu.
Kusema kweli Jean na hilo kundi la Akazu
ndio waliokuwa wanatawala na si baraza
la mawaziri au Bunge", Bibiane aliendelea
huku sasa Willy akimsikiliza kwa makini
zaidi.
"Huoni kuwa hiyo haikuwa sawa?", Willy
aliuliza.
"Mimi ningefanya nini, nilibaki kufanya
kila nilichoagizwa kama ilivyokuwa kwa
wengine wengi maana sasa hii ndio
ilikuwa namna ya maisha. Ama uko na
Akazu, vinginevyo hupati kitu cha aina
yoyote, iwe mali, elimu au kazi ya aina
yoyote Rwanda".
"Kwa hiyo rushwa ndio ilitawala utawala
uliopita?", Willy aliuliza.
"Inategemea unavyotafasiri rushwa",
Bibiane alijibu huku akiwa kama haelewi
anasema nini.
"Rushwa ni pale vyombo vya serikali
vinaposhindwa kufanya kazi zake, kwa
sababu hiyo kushindwa kutoa haki kwa
wananchi wake, na kuwafanya wananchi
wengi wapoteze imani, utu, uhuru na
maadili kwa serikali yao kwani wote sasa
huishi kama wanyama ambapo mwenye
nguvu na pesa ndiye anayepata
anachohitaji", Bibiane alisema.
"Hivyo ndivyo, maana nchi inakosa
maendeleo kwani mapato yote ya nchi
badala ya kuendeleza watu wote huingia
kwenye mifuko ya watu wachache. Na
kama ulivyosema uhalali wa serikali
kama chombo cha watu unakwisha,
badala yale wale wanaofaidika ndio
wanakuwa na nguvu zaidi ya serikali
yenyewe", Willy alitafasiri rushwa.
"Kwa tafasiri hiyo nakubali kuwa rushwa
ndiyo imetawala. Na sasa Watutsi na
Wahutu walipoanza kudai demokrasia
isingewezekana maana Jean na Akazu
hawakutaka kusikia kitu kama hicho kwa
vile kingeweza kuingila maslahi yao. Na
ndio sababu Watutsi walipokazana na
kusikia eti wako tayari hata kupigana na
Akazu, kwa kufadhiliwa na Jean, walianza
kulifundisha jeshi la wahutu lililoitwa
Intarahamwe ili liweze kuwadhibiti Watutsi
wa ndani na nje ya Rwanda".
"Kwa hiyo huyu bwanako Jean ndiye
alikuwa Rais hapa?".
"Si hapa tu, mimi najuwa nchi nyingi
ambako amewakamata wakuu wa nchi na
viongozi wa ngazi za juu serikalini na
anawajaza mapesa kila wakati".
"Huoni kuwa yeye ndiye ananufaika zaidi,
maana anajaza mapesa watu wachache
lakini yeye anachukuwa mali za wananchi
wengi", Willy alijaribu kumwelimisha
Bibiane.
"Najuwa, maana hata huko kwenu
Tanzania pia amewakamata wakubwa,
ndio sababu nchi yenu imekuwa ikisita
juu ya suala hili la Rwanda".
Willy alisitushwa na taarifa hii lakini
hakutaka kujionyesha maana kweli
msimamo wa serikali ya Tanzania ulikuwa
unalegalega kabla na hata baada ya
mauaji.
"Ina maana maamzi yoyote ilikuwa lazima
Jean akubaliane nao?".
"Ndiyo, na mapesa yalitembea sana
kuhusu swala hili na viongozi wengi
wamenufaika. Unafikiri kama swala hili
lingefanyiwa maamuzi mapema mauaji
yangetokea!", Bibiane alimwambia Willy
kwa njia ya kushangaza.
"Kwa hiyo huyu Jean ndiye aliamru
mauaji haya?".
"Baada ya Rais kuonekana kwamba
angekubali mkataba wa Arusha. Jean na
Akazu walikasirika sana maana
hawakutaka, kama nilivyosema mwanzo,
kugawana madaraka na mtu mwingine.
Hii ingegusa maslahi yao. Kwa hiyo,
kwanza ndio waliamru Rais auawe na pili
tayari walikuwa wamewatayarisha na
kuwahamasisha Wahutu kuwamaliza
Watutsi wote asibaki mtu ili wajihakikishie
uwezo wa kutawala milele. Mpango
ulikuwa kwamba hata kama jeshi la RPF
la Watutsi lingeshinda jeshi lao lazima
baada ya kuchukuwa nchi wangeshindwa
kutawala maana wangemtawala nani
huku Watutsi wote wakiwa
wameshauawa, waliobaki ni Wahutu
watupu ambao hawawaungi mkono.
Hivyo, ingewachukuwa siku chache
kuuangusha na kuutokomeza kabisa
utawala wa RPF. Hii ingebaki nchi ya
Wahutu chini ya utawala wa Jean na
Akazu.
Bibiane alipofika hapa ndipo Willy
alipoanza kuelewa kwa undani mambo
yalivyokuwa. Kumbe mauaji yote haya
yalitokana na watu wachache kutaka
kulinda maslahi yao ya kunyonya mali ya
wananchi, na kutumia hiyo mali kuweza
kuwachochea wananchi kuuana!.
Kwa mara ya kwanza Willy aliona jinsi
ambavyo nchi zote za Afrika zilivyo
hatarini kutokana na rushwa. Kwa vile
viongozi wa nchi hizi kuabudu rushwa,
hivyo Willy akaamini kuwa tukio kama la
Rwanda kumbe linaweza kutokea mahali
pengine katika Afrika!.
"Baada ya RPF kushinda na mipango ya
Jean kushindwa, wana mikakati gani
sasa?", Willy alihoji.
"Kama nilivyosema hawajashindwa. Wewe
ndiye umeingilia ndani ya mipango yao,
kuna mpango kabambe wa
kuisambaratisha serikali ya RPF kutokea
jimbo la Kivu, Zaire. Akazu wamekuwa
wakiliimarisha jeshi lao katika makambi
ya wakimbizi kule Goma na Bukavu,
Zaire, huku Jean akiwatumia rafiki zake
kutoka Afrika Kusini hasa waliowahi kuwa
katika idara ya ujasusi ya makaburu,
alikokuwa akinunua silaha na kuzipitishia
Angola ya UNITA, Zaire na Zambia kwa
kutumia viongozi wa ngazi za juu za
serikali za nchi hizo ambao wako kwenye
orodha ya malipo kutoka kwa Jean. Kwa
hiyo mambo bdo sana Willy, vita ndio
sasa karibu vitaanza".
"yaani dunia inafikiri kuwa kambi zilizoko
Zaire ni za wakimbizi kumbe ni kambi za
jeshi".
"Ni kambi za jeshi na serikali ya Zaire
inajua na ndio inayosaidia hata mafunzo.
Hata katika kambi zilizoko kwenu
Tanzania kuna wanajeshi wa jeshi la
zamani na Intarahamwe, na kuna watu
wazito katika serikali yenu ambao
wanalipwa na huyu Jean ili kuwasaidia
hawa watu, kwa hiyo hili si dogo. Kama
ulivyosema pesa ni kitu kibaya sana,
watu hawaoni tena madhara ya mauaji
yaliyotokea bali wanaona pesa tu".
"Swala la rushwa ni swala linalohujumu
haki za binadamu, yapaswa lichukuliwe
hatua kimataifa katika uzito huo wa haki
za binadamu", Willy alijibu kwa hasira.
Bibiane alikaa kimya bila kujibu kitu.
"Wewe ulikuwa uwasaidie vipi Jean na
Akazu katika kutekeleza huu mpango wao
wa kuivamia tena Rwanda", Willy aliuliza.
"Usije ukanipeleka kwenye mahakama ya
mauaji ya Arusha maana mauaji yale
sikuyajuwa pia sikushiriki, nilikuwa
Nairobi nikitokea kwenye mkutano Arusha.
Ila juu ya hili la sasa Jean amekuwa
akinituma kupashana habari kati ya
kambi za wakimbizi ambazo ni kambi za
jeshi lao huko Zaire, yeye na Akazu.
Vilevile kuna wanajeshi na viongozi wa
RPF ambao tayari wamenunuliwa na wako
upande wa Akazu, mmoja wao ndiye
anayetarajiwa kuchukua madaraka mara
tu jeshi la Akazu litakapotwaa madaraka
tena".
Willy hakuamini masikio yake kuwa tayari
hata ndani ya RPF kuna wasaliti.
Mara moja Willy alielewa jinsi alivyotaka
kuuawa na akagudua kuwa kweli kama
anavyosema Bibiane kuna kiongozi wa
juu na karibu sana katika serikali ya
Tanzania amabye anamtumikia Jean na
kundi la Akazu.
"Utasaidia kunipa majina ya watu wote
unaowajuwa kuwa wanahusika, maana
hiyo ndio njia pekee tunaweza kulikosha
jina lako", Willy alimuasa Bibiane.
"Swala la Jean kunisaliti mimi, na
kunihukumu kifo, bila kujali yote
niliyomtendea kwa hali na mali ikiwa
pamoja na kumpa mwili wangu auchezee
atakavyo, na jinsi nilivyojitoa
kumstarehesha. Willy mimi niko upande
wako, kama uko tayari kupambana nao
nihesabu na mimi. Jean akishaambiwa
kuwa umenichukua ninavyomjua atataka
apambane na wewe yeye mwenyewe,
ikifika hapo niachie mimi. Majina na
mipango yao yote ni juu yako na uongozi
wa RPF mjuwe la kufanya kwani jeshi la
Akazu, likisaidiwa na viongozi wa nchi
kadhaa ambao ni marafiki na Jean
watakuwa tayari kuingilia kati. Ni lazima
liwahiwe mapema kabla halijajiimarisha
sawasawa", Bibiane alieleza.
"Nafikiri swala la vita si letu, ni la serikali
ya Rwanda na RPF, mimi nipe hayo
majina na kutokea hapo ndipo nitajua
kama kazi yangu imeisha au ndio kwanza
inaanza", Willy alieleza taratibu.
Bila kuwa ameandika mahali popote,
Bibiane alitoa kichwani jina hadi jina
akianza na kundi la Akazu mpaka
viongozi wa nchi mbalimbali wanaolipwa
na Jean huku Willy akiyaandika chini kwa
mshangao mkubwa, kwani watu
waliokuwa wanatarajiwa wengi wao ni
viongozi wanaoheshimika Afrika na kote
duniani. Alishangaa zaidi Bibiane
alipotaja jina la yule waliyekuwa
wakimwita JKS wa Tanzania.
"JKS, hii imenishangaza sana, maana
huyu ndiye anayetegemewa kugombea
urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu
unaokuja," Willy alimweleza Bibiane.
"Najua kabisa, na tayari Jean
ameshamtengea mamilioni ya dola za
Kimarekani zitakazo msaidia katika
kampeni hiyo ya uchaguzi kuusaka urais.
Nia ya Jean ni kuwa na marais vibaraka
kote Afrika ili yeye na wenzake huko
Ulaya, waweze kufanya vile wanavyotaka
katika nchi hizi. Jean anaongoza kundi la
wafanyabiashara wakubwa wanaomiliki
makampuni makubwa ya kimataifa. Na
nia yao ni kuhakikisha kuwa Afrika
inakuwa soko lao tu, na hata siku moja
Afrika isisimame kiuchumi. Ingawaje nchi
zao zinapigia kelele rushwa, lakini nchi
hizohizo ndizo zinazoyasaidia
makampuni makubwa kwa madogo kutoa
rushwa kwa nchi zinazoendelea, maana
makampuni hayo yakitoa hongo, hongo
hii huchukuliwa kama gharama na
kutolewa kwenye kodi ya mapato. Hii yote
inaonyesha unafiki wa nchi za magharibi,
na kila wakati Jean alikuwa akinieleza
kuwa kelele zote hizi kuhusu rushwa,
demokrasia na soko huria ni kelele za
kinafiki tu, lakini huku nyuma katika vikao
vya viongozi wa nchi za magharibi ni
kuchochea rushwa. Wanajuwa kuwa
rushwa ikiisha Afrika basi demokrasia na
soko huria vitashamiri na hivyo uchumi
wa nchi hizo utakua haraka sana, kitu
ambacho hawataki kitokee. Jean
anasema, rushwa ndiyo sera inayotumiwa
kuendeleza umaskini katika nchi za Afrika
ili nchi zilizo endelea ziendelee kuitawala
Afrika kiuchumi. Kwa hiyo, iwapo JKS
ataitawala Tanzania rushwa itazidi mara
dufu, na kutokana na fedha alizotengewa
na Jean lazima atashinda, kwani kila
walipoweka mtu wao hajawahi kushindwa
uchaguzi", Bibiane alieleza.
Sasa Willy alikuwa na picha kamili namna
JKS alivyokuwa anahusika na swala zima
la Rwanda. na sababu za Tanzania
kutokuwa na msimamo dhabiti juu ya
swala hili na kuweza kuyumbisha
mikutano kule Arusha kiasi cha kutofikia
maamzi kwa muda mrefu maana swala
hili la Rwanda kwa muda mrefu lilikuwa
chini ya Tanzania kwa muda mrefu na
JKS alikuwa mmojawapo wa viongozi
walioonyesha kuchoshwa na mauaji ya
Rwanda. Na alifanya hivyo kwa shinikizo
la Jean aliyekuwa akimlipa pesa nyingi na
uchu wake wa kutaka madaraka kwa njia
ya ruswa ili aweze kuyatumia kwa faida
yake na kujinifaisha yeye na rafiki zake.
Na ni hii rushwa iliyowanyima
Wanyarwanda haki yao mpaka kufikia
hatua ya kuuawa vibaya namna ile kweli
ni aibu! Aibu sana kwa Afrika nzima.
"Vizazi vijavyo vitakapoyasoma na
kuyaelewa matukio haya, hakika
hawataamini, watajuwa sisi wote tulikuwa
wendawazimu kabisa, kwani ni sisi wote
ndio tulioachia hali hii ikafikia hapo ilipo,
kwa kuwapa walarushwa madaraka kwa
gharama ndogo ya kuuza kura zetu na
wao kutumia madaraka tuliyowapa kwa
malipo ya fedha kidogo, lazima
wayatumie kutuangamiza", Willy alisema
kwa uchungu huku akikuna kichwa chake.
Mara moja Willy alimkumbuka Malisa wa
Arusha, aliyekuwa mshauri wa JKS katika
masuala ya uhusiano wa Kimataifa kabla
hajarudi Chuo Kikuu. Hivyo basi, alijuwa
Malisa ndiye aliyemweleza JKS kuhusu
msimamo na mipango ya PAM na
kuteuliwa kwa Willy kufuatilia jambo hili.
Willy aliamini kuwa JKS ndiye aliyetoa
taarifa za safari ya Rwanda kwa Jean na
kundi lake na ndi sababu ndege
aliyopanda ikapigwa kabla ya kutua
uwanja wa ndege wa Kigali.
"Kwa hiyo JKS ndiye aliyotoa habari
zangu zote kwa Jean?", Willy aliuliza kwa
shauku.
"Ndio, na ndio sababu Col. Gatabazi
aliamru ndege hiyo ipigwe kabla ya kutua
uwanja wa ndege, lakini kwa bahati na
umahiri wako ukawaponyoka", Bibiane
alijibu huku akimwemwesa. Mara mlango
wa mbele ukafunguliwa na Col. Gatabazi
akaingia ndani.
Willy alipoangalia saa yake ilikuwa yapata
saa tisa usiku. Wote walisimama, na Willy
akawatambulisha.
"Pole Kanali, leo tumepata mgeni na
anaitwa Bibiane, na Bibiane huyu ndiye
mwenyeji wetu. Col. Rwivanga, kiongozi
katika serikali mpya ya RPF".
"Nashukuru kumfahamu", Col. Rwivanga
alijibu.
"Nami nimefurahi kukuona leo, nimekuwa
nikisikia sifa zako nyingi kwa muda
mrefu, toka kwa Col. Gatabazi kuwa wewe
ni mpiganaji hodari, hongera", Bibiane
alijibu kwa tabasamu akimwangalia Col.
Rwivanga.
"Asante kwa sifa hizo zilizotoka katika
kinywa cha msichana mrembo kama
wewe", Col. Rwivanga alijibu akaendelea,
"Ehe, imekuwaje Willy, hebu nipe habari
kamili, maana kazi tumeiona kwa Bibiane,
sasa halafu ikawaje hivi", Col. Rwivanga
alionekana kuwa wasiwasi na Bibiane.
"Mimi naomba nikalale ili mzungumze
vizuri, nionyeshe chumba cha kulala",
Bibiane aliomba.
Willy na Col. Rwivanga aliangaliana na
Willy ndiye alikuwa wa kwanza kujibu,
"Kwa vile nyumba hii ina vyumba viwili tu
vya kulala, basi kalale chumbani kwangu,
maana tayari hata kuoga umeoga huko.
Mimi nitalala hapa sebuleni kwenye kochi
hamna taabu".
"Asante", Bibiane aliwaaga na kuelekea
chumbani huku wote wakimwangalia.
Kisha wakatazamana na kutabasamu.
"Ehe, hebu nipe mambo".
Willy alichukua muda mrefu kumweleza
mambo yalivyotokea na mambo mengine
yote aliyoelezwa na Bibiane. Col.
Rwivanga akasimama na kumshika
mkono Willy kwa hatua aliyofikia haraka
na kwa umakini mkubwa.
ITAENDELEA