Riwaya: UCHU

Hawa jamaa ni janga kubwa. kidi kudi kaleta riwaya mbovu isiyo na viwango ya Mwalongo. Siyo kwamba tunanjaa kiasi cha kula kila kitu, tuna standard zetu jamani. please guys naomba mmalizie hii UCHU. Nakosa imani kama mtaleta sawa na orodha mliyoitoa.

kidi kudi kesha kuwa star hapa entrainment forums, hivyo anatuburuza kama ilivyo kawaida ya ma superstar wa bongo.
 
kidi kudi 10:28 11th January 2015
UCHU
By A.E Musiba
SURA YA KWANZA

riwaya gani ya kuchukua siku 5 hayajaisha
 
kidi kudi kesha kuwa star hapa entrainment forums, hivyo anatuburuza kama ilivyo kawaida ya ma superstar wa bongo.

Kama vp shusha wewe hiyo riwaya...maana sio unabwabwaja tu wakati hujui A wala B ya source ya riwaya hizi. Kingine kidi kudi kutupa hizi riwaya ni privilege tu sasa sisi tunataka kugeuza kuwa right. "Watu bwana"(Just a song done by joint mob)
 
Ni kweli mkuu kwamba kidi kudi na wengineo wametufanyia hisani tu kutuletea hii hadithi.....lakini kwa vile wameianza wanawajibika kumalizia vinginevyo wanakuwa wanatukosea...wanatutia ham af wanasepa aaah sio haki kabisa
 
Last edited by a moderator:

mpagani bwana!!!!
 
Yan hawatufanyii fair Mi kila nikikaa mawazo uchu tu bora mmalizie tu wakuu
 
kidi kudi kesha kuwa star hapa entrainment forums, hivyo anatuburuza kama ilivyo kawaida ya ma superstar wa bongo.
Siamini kama kuna mtu tena timamu kichwani aamue kuja kuutafuta usupa staa Jf. Atakua hajitambui
 
Ni kweli mkuu kwamba kidi kudi na wengineo wametufanyia hisani tu kutuletea hii hadithi.....lakini kwa vile wameianza wanawajibika kumalizia vinginevyo wanakuwa wanatukosea...wanatutia ham af wanasepa aaah sio haki kabisa

Muungwana utamjua tu kwa maneno yake, mkuu Khantwe wewe ni GT. Heshima kwako.
 
Last edited by a moderator:
Shusheni basi Riwaya hiyo maana imeleta kiu na uchu Willy Gamba 1 please dondosha riwaya
 
Hatuna sababu ya kumlaumu yeyote tena particularly kidi kudi nakumbuka kama alisema atakua anatoa mara 1 kwa siku ila ilimbidi yeye na TECHMAN kuileta kadri mlivyoomba. Naamini kile kidi kudi alichokisema awali kwamba anaioganaizi vizuri ili aitiririshe yote kwa mpigo.

Tumpe mda.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu kwani wewe huna hii?? Ishushe basi
 
Last edited by a moderator:
saa ngapi mtalaam? maana kila baada ya dk kadhaa nachungulia. isha kuwa utumwa eti
 
Tushushieni vitu vya uhakika na hiyo Isabel kama vipi tutumie kwa sup
 
waungwana subira inahusika hapa pia lugha yetu iwe tamu sababu kidkud kafanya uungwana kutuletea it's just like ihsani sasa isigeuke nuh'sani naamini hawezi kutufanyia ukatili wa darja hili khasa kwa wapendao riwaya angalizo tusitumie lugha ambazo zitawafanya wengine waogope kutupatia burdani hii tuwe na subra.
 
Well said mkuu...! Najua tuna "uchu" kweli na mate yanatudondoka ntamaholo vuta subra mkuu
 
Last edited by a moderator:
UCHU
NGUVU YA RUSHWA--III

Simu ilipoita Jean alikuwa amelala. JKS
alikuwa amemweleza kuwa vijana
walikuwa wamefika salama na kazi ya
kumsaka na kumuua Willy Gamba ilikuwa
ifanyike usiku ule. Alikuwa amefikiria jinsi
Bibiane angeshangaa sana baada ya
kuelezwa kuwa Jean ndiye aliyetoa amri
ya yeye kumuua. Jean alikuwa mtu
aliyefurahia uovu, alikuwa mtu katili
afadhali ya mnyama. Alifurahi kusikia mtu
akipata maumivu, na hapo ndipo roho
yake ilipopata faraja. Pamoja na miaka
yoye sita aliyokaa na Bibiane, utafikiri
walikuwa mtu na mke wake, yaani mume
na mke, bado alipomweleza Col. Gatabazi
kuwa lazima Bibiane auawe moyoni
mwake hakusikia masikitiko.
Kilichomfurahisha na kumridhisha ilikuwa
ni pesa na nguvu ya pesa, na si mapenzi.
Jean aliabudu pesa kwani aliamini kuwa
pesa ndizo zilizompatia uwezo alionao
duniani.
Kwa kutumia pesa, Jean aliweza
kuwakamata wakuu wa nchi nyingi
duniani, hasa katika Afrika na Asia, lakini
vilevile viongozi wa ngazi za juu katika
serikali za nchi za Ulaya. Alipata kila
alichokitaka kwa kutumia pesa. Hivyo,
simu ilipolia alijua analetewa habari
njema za kuuawa kwa Bibiane na Willy
Gamba maana alikuwa amesema alikuwa
amesema wakishauawa aelezwe. Kila
alipopewa taarifa ya kuuawa kwa mtu
alipata faraja ndani ya moyo wake, Ndio
sababu maelfu ya Watutsi walipouawa
alisikia raha isiyo kifani. Hakika mtu huyu
alikuwa mgonjwa, tena mgonjwa sana!.
"Jean", aliitikia kwenye simu.
"Col. Gatabazi hapa".
"Sema Col. Gatabazi".
"Kazi imeharibika".
"Nini?".
"Kazi imeharibika. Vijana wote
wameuawa. Bibiane yuko hai na
ameokolewa na Willy Gamba. mimi na
Nkubana tunaondoka kwenda Kibunda,
hatuna muda maana wakati wowote
wataanza kutusaka, afadhari tuyaandae
majeshi yetu tayari kwa vita", Col.
Gatabazi alimwambia Jean.
"Ilikuwaje", Jean aliuliza kwa sauti ya
kukata tamaa. Col. Gatabazi alimweleza
kwa ufupi kama Nkubazi alivyomweleza.
"Basi tuonane kesho Goma, saa tisa
mchana nitakuwa huko, natarajiwa kuja
na ndege yangu, lakini nitampitia rafiki
yetu Kinshasa", Jean alieleza na kukata
simu kabla hata Col. Gatabazi hajajibu
kitu.
Jean alipokata simu ya Col. Gatabazi,
alitumia muda huo kupiga simu Zambia,
Zaire, Afrika Kusini, Angola, Kenya na
kumalizia Tanzania.
"Umenipata JKS?", Jean alimuuliza JKS
baada ya kumweleza yote yaliyotokea na
maelekezo mengine huku JKS akipatwa
na shinikizo la damu.
"Nimekupata", JKS alijibu kwa sauti ya
kutetemeka.

....ITAENDELEA....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…