MTUNZI: MAUNDU MWINGIZI
SEHEMU YA 12
Ndani ya gari tulikua watu kama wanane hivi kiasi kwamba tukawa tumebanana kisawa sawa japokua Gari ilikua haikua ndogo sana , Seat ya mbele karibu ya dereva alikua amekaa Kaptain John Makala, na huku seat za nyuma tulikua tumekaa Mimi, Pablo, Ramla, na wale Askari polisi wawili ambao walitokea pale maeneo ya mnazi mmoja, pia alikuwepo Yule baunsa akiwa bado hajarejewa na fahamu!
Wote tuliku kimya ndani ya gari, hapakua na sauti yoyote zaidi ya Pablo Mwaki ambae muda wote alikua akigumia kwa sauti ya chinichini kutokana na maumivu makali katika mguu wake uliopigwa Risasi katika jaribio lake la kutoroka, moyoni niliendelea kujifariji kua sasa tuko kileleni mwa ushindi wetu dhidi ya Pablo, sasa Tulikua tumeshika barabara ya Uhuru inayokatisha maeneo ya Kariakoo na kuendelea moja kwa moja mpaka Buguruni huko, ndipo Simu ya Kaptain John Makala ilipoita,
"Hallo mkuu" Alipokea simu Kaptain lakini hatukujua alikua akiongea na nani lakini kadri alivyokua akizidi kuongea ndivyo sura yake ilivyozidi kubadilika, bila shaka alikua akipata taarifa zisizokua nzuri kabisa, tayari moyo wangu ukawa umeshapata hofu, Alipomaliza kuongea akajipiga kichwani na kuropoka kwa sauti
"Shit!!! Mambo yameshaharibika huko.."
"Nini tena kaka?" aliuliza Yule Afisa usalama alikua akiendesha gari, lakini hakupata jibu lolote kutoka kwa Kaptain ambae sasa alinigeukia mimi na kunitupia swali lililonishtua sana
"Kina Ntahondi wako wapi?"
"Nimewachukulia Tax imewapeleka nyumbani"
"Umeharibu kila kitu, Bila shaka hilo ni kosa kubwa sana ulilowahi kulifanya katika maisha yako"
"Kwanini kapteni?" nilijikuta nikitokwa na swali hilo
"Tax waliyopanda imevamiwa na tayari wamefanikiwa kumteka Ntahondi, na wameondoka nae, Lazima wamuue ili wafute ushahidi"
Moyo wangu ulipiga Paa!! Nikawa nahema kama punda, akili iliniruka kabisa, nikamuangalia Pablo mwaki kwa Hasira huku nikiwa sijui cha kufanya,
"Pamoja na haya yote bado tu unaendelea kuwatuma vijana wako wawateke watu, Si ndio?" Kaptain Makala alimuulioza swali la kebehi Pablo Mwaki, lakini kabla Pablo hajajibu chochote,
Kaptain akamgeukia kisha akamnyang'anya simu yake, Wakati anamnyang'anya ile simu kikadondoka na kitu kingine kidogo hivi, baadae nikagundua kua ilikua ni Flash, lakini kilichonishangaza Pablo aliwahi kuikanyaga ili isonekane ila mimi nikagundua ule mchezo, haraka nikainama na kuichukua kwa nguvu halafu nikaiweka kwenye mfuko wa Suruari yangu, muda huo tayari tulikua tumeshafika maeneo ya ‘Roundabout' ya Msimbazi, hapo hapo Kaptain akatoa amri kwa dereva
"Zuia gari" Dereva akasogeza gari pembeni kasha akamgeukia Kaptein "Kuna nini Boss?"
"Kuna hali ya hatari" "Nini hasa?"
"Geuza gari tunakwenda maeneo Ofisi za usalama, Ocean road, Now!!"
"NO! Naomba tuheshimu taratibu za kazi, sisi ni askari na humu tuna wahalifu hivyo hatuwezi kuendelea kupoteza tyme hapa Gari inakwenda moja kwa moja kituo cha Msimbazi" Aliongea kwa sauti ya juu mmoja kati ya wale Maaskari tuliopanda nao kwenye gari
"Pumbavu! We unaongea hivyo kama nani? Unanijua mimi wewe?" Kaptain Makala alifoka huku akiwa amemtolea macho Yule Askari
"Sina haja ya kukujua, Gari inakwenda kituoni na si vinginevyo"
Majibu ya askari huyu yalionesha kumkera sana Kaptain kiasi kwamba sasa akashindwa kuvumilia hapo hapo akaingiza mkono mfukoni, nikamuona akitoa Bastola yake, nikapatwa na hofu zaidi sikujua anataka kufanya nini!
Lakini kabla hajaitoa tu nikashangaa Yule Askari mwingine aliekua kimya muda wote wa malumbano anamrukia kichwa Kaptain, hakika kichwa kile kilimpata sawia maeneo ya kwenye kimpuma, juu kidogo ya nyusi zake za jicho la kushoto,
Kichwa kile kilimchana captain akaanza kuchuruzika damu, kilikua ni kitendo bila kuchelewa, hapo hapo Yule askari mwingine nae akaanza kumrushia makonde mfululizo bila hata ya kuuliza kitu, sasa ikabidi dereva wetu ambae ni mwenzie na Kaptain Makala ageuke nyuma ili kujaribu kumsaidi mwenzie,
Naam hilo ndio lilikua kosa kubwa, ikatokea kwa mbele yetu gari nyekundu ikaja moja kwa moja na kutugonga ubavuni upande wa dereva, ilikua ni ajali ya kijua sana, sikujua dereva wa gari ile alidhamiria nini maana sisi tulikua tumepaki pembeni kabisa ya barabara,
Wakati mpambano unaendelea kwenye gari kati ya Makala na wale Askari ghafla wakashuka vijana kama watano hivi kutoka ndani ya ile gari iliyotugonga na kisha wakaja kwa kasi mpaka ndani ya gari yetu walipofika hawakuuliza kitu zaidi ya wao kuwasaidia wale askari na kumshambulia kaptain Makala, ikawa ni kipigo juu ya kipigo,
Kaptain hakua na wa kumsaidia kwa sababu tayari dereva wetu alikua amepoteza fahamu kutokana na ajali hiyo ambapo gari ile iligonga zaidi upande wake na kumuumiza sana,
Uzalendo ukanishinda ikabidi name sasa niingilie kupambana na jamaa hawa, ikawa ni vurugu kubwa sana ndani ya gari ile kiasi kwamba baadhi ya wapiti njia wakaanza kutaharuki na kukimbia hovyo,
Sasa tulianza kupata majibu ya tukio lile kua ni la kupangwa ambalo pia lilitupa jibu kua hata hawa askari ni miongoni mwa washirika au wafuasi wa Pablo, watu walianza kuja mbio eneo lile hivyo ikabidi mmoja kati ya majambazi wale akaanza kupiga risasi hovyo ili kuwatawanya watu walioanza sasa kufurika eneo lile, wakati vurumai ikizidi kushika kasi tayari vijana baadhi walikua wameshafanikiwa kumtoa Pablo nje ya gari huku akichechemea kwa maumivu,
Wakamuingiza ndani ya gari na baada ya dakika chache vijana hawa pamoja na Askari wale wawili wakatoka kwa kasi ndani ya gari yetu na kuingia kwenye gari waliyokuja nayo na hapo hapo gari ikawashwa WAKATOKOMEA!!!
Lilikua ni zaidi ya tukio la Kimafia!!!
Uso wa Kaptain ulikua umeenea damu, mimi pia nilikua nimeumizwa vibaya kichwani hata sikujua wamenipiga na kitu gani, haraka tukatoka nje ya gari na kujaribu kuwafukuzia lakini haikua kazi rahisi maana tayari walikwashaondoka tena kwa kasi ya ajabu, pia dereva wetu alikua amepoteza fahamu
"Washenzi hawa, Hawa Askari wamejiingiza matatizoni nitawapata tu, nimekariri namba za Yule mmoja" aliongea Kaptain Makala huku akihema kwa kasi, tayari wananchi walishajaa eneo lile, Ndani ya Gari yetu walibaki watu watatu tu, Ramla, Yule Baunsa wa Pabl na Dereva wetu,
Ndani ya muda mfupi tu Wananchi walikua wamefurika pale, wengine wakijaribu kumuuliza Kaptaini juu ya kilichotokea lakini hakuwajibu kitu, muda mfupi baadae zikawasili gari mbili kwa kasi, zilipofika tu wakateremka watu wakiwa wamevaa Suti Nyeusi na mmoja akiwa amevalia gwanda za kipolisi, walipofika wakasalimiana na Kaptain, niligundua kua ni maofisa wenzie wa Usalama wa Taifa.
Haikuchukua hata dakika wakawa wameshaingia ndani ya ile gari yetu iliyogongwa, wakamtoa Ramla, Baunsa, pamoja na dereva wetu kisha wakawaingiza katika moja ya gari zile walizokuja nazo halafu gari ikaondoka haraka, ikabaki ile gari moja tukapanda mimi na Kaptain Makala nayo ikatuondoa kwa kasi eneo lile na kuiacha ile gari yetu iliyogongwa ikiwa imezungukwa na Wananchi tu,
Ndani ya gari hakukua na maongezi yeyote kati ya Kaptain na maafisa wenzie, bila shaka walikua wameshaelewa kilichotokea japo sikujua wamezipata wapi habari zile zilizotokea pale, gari yetu ilikua kwenye kasi ya ajabu,
Tukiwa ndani ya Gari kijana mmoja alitoa vitambaa vyeusi akamfunga machoni Ramla, Ramla alikua akilia huku akiniomba msamaha lakini haikusaidia kitu.
Haikuchukua muda tukawa nje ya nyumba ya Mhe Waziri Mkuu, Kule tulipohifadhiwa mwanzo, tulipofika pale wakaniteremsha na kuniacha pale halafu wao wakaondoka, sikujua wanakwenda wapi, nikaingia ndani nikiwa nimechoka sana akili na mwili, nilipofika ndani nikawa nimejilaza katika kochi pale Seating room, mawazo yakanitawa ubongo wangu
"Ahhh mkosi gani huuu" Nilijisemea kwa sauti huku nikibubujikwa na machozi kila nikimfikiria Ntahondi, nilishindwa kujizuia machozi yakawa yanazidi kutiririka,
Nilijua kua sasa mwisho wa Ntahondi umefika, niliamini kua ni lazima watamuua tu ili kupoteza ushahidi,
"Amaa kweli Mwaki ana mtandao, na atatumaliza tu" nilizidi kujisemea peke yangu kama mwehu vile, Moyo ulivilia maumivu makubwa nikajiona sina tena thamani ya kuendelea kuishi, maana kila hatua inaleta madhara makubwa,
Ntahondi ambae nilitegemea kua ndie angenifuta machozi na kuniliwaza katika kipindi hiki kigumu lakini nae kaishatoweka, Baada ya kukaa kwa muda mrefu pale Sebuleni nikaamua kuinuka na kwenda kule chumbani, kwakua nilikua tayari mwenyeji hivyo sikuhitaji muongozo wa mtu yeyote,
Nilipofika pale mlangoni bahati nzuri mlango ulikua umerudishwa tu haukufungwa na funguo hivyo nikkinyonga tu kitasa kidogo na kuufungua nikashangaa nimevutwa mkono kwa nguvu kuelekea kule chumbani, moyo wangu ulishtuka almanusura ungepasuka,
Mapigo ya moyo yalikua yakinienda mbio, nilikua nikitetemeka kwa hofu, nilipoingia tu mule chumbani mlango ukafungwa kwa nguvu, nilipogeuka nimuangalie alinivutia mule chumbani na kuufunga mlango ule, Moyo ulilipuka tena, sikuamni hata kidogo nlichokiona mbele ya mboni za macho yangu!!
Alikua ni NTAHONDI!!!
Naam, alikua ni Ntahondi mwenyewe, na nguo zake zile zile alizokua amezivaa kule kwenye Graduation, sasa amefikaje huku? Nani kamleta? Nilibaki nimeduwaa huku nimemtumbulia macho kama mjusi alibanwa na mlango, cha ajabu Ntahondi alikua akinichekea tu,
Niliendelea kupigwa na butwaa, ndipo sasa Ntahondi akanifuata na kunikumbatia kwa furaha
"Wewe imekuaje upo hapa?"
"Na wewe umefikaje hapa? Au umefuta mwanamke mwingine humu?" alinijibu huku akiachia cheko lake maridhawa
"Hebu acha mzaha bhana, mie hapa siko sawa kabisa niliambiwa kuwa umetekwa na watu wa Mwaki sasa nashangaa uko huku"
Wakati nikiendelea kumuhoji Ntahondi ghafla nikahisi kama vile kuna nyayo za mtu zimenishtua, sauti ya Nyayo hizo ilitokea mule mule chumbani maeneo ya nyuma ya kabati kubwa la nguo liliopo mule chumbani, ikabidi nimuachie Ntahondi ili nisogee kuangalia kuna nini kule nyuma ya kabati maana sasa hofu imeshanivaa, na sihitaji kumuani mtu yoyote.
Niliposogea nyuma ya kabati lile, nikapigwa na mshtuko mkali moyoni, macho yangu yakakutana na Uso wa Mwl Honde
"Nyie mbona siwaelewi?" niliwauliza huku nikimuangalia Ntahondi aliekua amesimama palepale nilipomuacha huku akiendelea kucheka kwa sauti,
Nikarudi mpaka kitandanani na kujibwaga kama kiroba maana kwa jinsi nilivyoshtuka mpaka mwili ulikua umeishiwa nguvu, Ndipo sasa Honde na Ntahondi wakaja mpaka pale kitandani, nao wakaketi
"Pole Kijana, mkeo yuko salama huyo hapo, hakuna aliemteka" aliniambia Mwl Honde
"Mmh, sasa ilikuaje? Unajua mpaka sasa sijaelewa kitu"
Niliposema hivyo Honde nae akacheka kisha ndo akaanza kunipa habari "Iko hivi pale uliposimamisha Tax ukawapakiza kina Mama pamoja na Ntahondi ilikua ni Mistake kubwa sana maana maeneo yale kulikua na vijana wa Pablo kama Nyuki na wengine ni Askari polisi, sasa wakawa tayari tayari kuivamia ile Tax ili wamteke Ntahondi, bahati nzuri kulikua na maofisa wa usalama wa taifa eneo lile wakagundua mchezo mzima hivyo wakaiwahi ile Tax wakawatoa akina Ntahondi pamoja na kina Mama kisha wakawaingiza kwenye gari zao mpaka nyumbani, lakini kwa usalama ikabidi warudi na Ntahondi mpaka huku, ila sasa wakati wanakuja huku pia wakagundua kua wale Askari Polisi mlioingia nao kwenye gari yenu nao ni vijana wa Mwaki na wameshapewa maelekezo na mkuu wao wa kazi kua wahakikisha wanamuokoa Mwaki ndipo tukampigia Simu Kaptain ili abadili muelekeo,
Kwahiyo pale alitumia mbinu tu ya kusema kua Ntahondi ametekwa ili Mwaki na vijana wake wajue kazi imefanyika" Aisee nilibaki kinywa wazi, ilikua ni tukio la kustaajabisha sana, japo Ntahondi na Mwl Honde walikua wakionesha sura za bashasha ila mimi bado sikua na amani kabisa moyoni, nikamtupia swali Mwl Honde
"Sasa na lile tukio la kule Msimbazi? Nalo ni la kuunda?"
"No lile ni kweli kabisa, na tayari wamefanikiwa kumtorosha Pablo"
"Sasa si itakua hatari imenza upya hiyo?" "Unajua Pablo si mtu mdogo kama unavyomfikiria, anakula na vigogo serikalini Yule"
"Kwahiyo tunamuacha atoroke hivi hivi? Tumekubali matokeo?"
"Hapana, Mwaki atapatikana tu ila sio kirahisi rahisi hivyo, inahitaji makini wa hali ya juu vinginevyo atakufa mtu, tumeshajua kila kitu anachojaribu kukifanya Mwaki na watu wake ili watoroke, na mpaka kufikia kesho tutakua tumeshamtia nguvuni, Operation itaanza asubuhi, ila ninyi inabidi muendelee kukaa humuhumu katika jela yenu ya hiari kwa usalama wenu maana kwa sasa mmeshakua target, mnaweza kuuawa ili ushahidi upotee. Oky?"
Kwa jinsi Honde alivyokua akiongea kwa kujiamini inaonekana anajua kila kitu
"Mhh, Ok. Lakini Honde we unapata wapi hizi Information zote? Au na wewe Usalama mzee?"
Swali hili likasababisha wote tuangue kicheko mule chumbani, nikashusha Pumzi nzito kuashiria kua nimekubali matokeo kua Mchumba wangu Ramla yuko salama, na niko nae tena Kwa Mhe Waziri Mkuu, Japo pia Pumzi zangu ziliku na maana nyingine kubwa, kwamba Aluta continua yaani mapambano yanaendelea, nilizidi kuiogopa nguvu ya Pablo, na swali kubwa llipita kichwani mwangu ni Je tutampata Mwaki? Je Haki itatendeka?, Je Maisha yangu na Ntahondi yatakua Salama?, na Je tutafunga Ndoa mimi na Ntahondi?.
Baada ya kimya cha muda mrefu sasa, Mwl Honde akatuaga kwa madai kua anaenda kule chuoni kujua kinachojiri na pia anahitaji kupumzika kwa ajili ya maandalizi ya Zoezi la kesho
"Kwani na wewe utakuwepo kesho kwenye hiyo Operation?"
"Sio mimi tu, hata wewe pia utakuwemo" Baada ya majibu hayo ya Honde akainuka na kuondoka, nikabaki mimi na kichuna change, Wawili tu ndani!! Kidogo nilifarijika!!
Je nini kitaendelea?
Ngekewa ram angelca chacha patrick showtie amina mabata mlyn Angelicious culbby muuza ubuyu princetx Giti VAN HEIST Mng'ongo chwechinyong