RIWAYA: Siku ya graduation

RIWAYA: Siku ya graduation

Imetulia, ila usiwe unaichelewesha sana Casuist
 
Last edited by a moderator:
RIWAYA:SIKU YA GRADUATION
MTUNZI:MAUNDU MWINGIZI


SEHEMUYA NNE


TULIVYOKUTANANA RAMLA

Ilikua ni mwaka 2009, Mwaka mmoja tangu nipate kazi kwenye kampuni ya KIGWAZA inayojishughulisha na Upakiaji na upakuaji mizigo bandarini kama Muhasibu nikachukua likizo fupi kwa ajili ya kwenda kumsalimu Mama yangu mzazi Bi Shammy Naufal aishiye Tabora, niliifurahia sana safari hii kwa kua ilikua ni muda mrefu sana sijaenda nyumbani hivyo nilitaraji kuonana na Mama yangu kipenzi, Ndugu zangu, na Marafiki zangu ambao tulikua tukikaa wote kijiweni tukibadilishani story kadhawa kadha..

Niliwasili TABORA majira ya saa kumi na mbili jioni, nilipokelewa na wadogo zangu waliokuja Stand ya Mabasi kunipokea kisha tukaondoka mpaka nyumbani ambako nilipokelewa kwa shangwe na Mama na ndugu wengine waliokua pale nyumbani, ilikua ni siku ya furaha sana kwangu, kama kawaida ya wageni mambo kama Jogoo huusika kwa asilia mia wakati wa mduara wa chakula cha usiku na kila aina ya vinywaji ilipofika Saa sita kasoro(usiku) niliondoka na kwenda Chumbani kwa Mdogo wangu wa kiume na kujiandaa kwa ajili ya kulala..

Asubuhi ya siku iliyofuata niliamka mapema, na baada ya kuoga na kupata kifungua kinywa nikajipumzisha kidogo pale ukumbini na kisha nikamuaga Mama kua ninaenda kijiweni kuwasalimia jamaa zangu kisha kuna Mzigo nilipewa na Mke wa Boss wangu ili niupeleke kwa dada yake anaishi Mtaa wa Rufita anaitwa Bi Ayman Gamba, baada ya hapo nikaanza kujongea kijiweni ambako pia nilipokelewa kwa furaha sana na washikaji zangu wa kitambo niliowaacha wakati naenda Dsm, tukiwa katikati ya Story alikatiza binti mmoja ana mirindimo mithili ya Mjaluo, Mrembo, Mrefu, sio Mweupe wala si mweusi, Hips kama amefichapanya, , yaani kama we ni Rijali lazima ungegeuka mara mbili kumtazama. Huyo si mwingine alikua ni RAMLA

Baada ya kuwaulizia washikaji kuhusu binti huyu waliniambia kua anakaa mtaawa Rufita, kuhusu shughuli zake niliambiwa kua anafanya kazi za msimu katika ofisi za ATTT! Nilitamani kujua mengi zaidi yamuhusuyo binti huyu lakini washikaji walibadili mada na tukaendelea na Story zangu baada ya muda mrefu niliwaaga jamaa ili niende sasa nikamtafute huyoBi Ayman wa mitaa ya Rufita maana nilikua sipaju anapokaa, nikachukuaboda boda kisha nikaondoka zangu, nilipofika Rufita maeneo niliyoelekezwa tukasimama kisha nikateremka kwenye boda boda ilinimuulize mmoja wa vijana aliekua upande wa pili wa bara bara lakini kabla sijavuka akatokea msichana mmoja katika nyumba niliyokua nimesimama akamwaga maji nje nilipogeuka na kumuangalia alikua ni yule binti mrembo aliepita kule kijiweni

Kabla sijasema chochote akaniwahi yeye kwa kunisalimia
"Mambo"
"Poa,mzima wewe?
"Mie mzima, mara tu umefika huku?" hili swali likanishtua nikahisi amenifananisha lakini kabla sijamjibu chochote akaniwahi kwa swali jingine
"Kwani wewe si nilikupita na jamaa zako mmekaa kule Minazi mikinda?"nikajua hakua akibahatisha
"Duh una kumbukumbu sana, yeah ni mimi. sasa mie naomba kukuuliza,napaulizia kwa Bi Ayman Gamba!!" akacheka kidogo kisha akanijibu kwa Pozz
"na unaeongea nae hapa ni binti yake aitwae Ramla, karibu ndani"wote tukacheka na kisha tukaangia ndani, nikamuomba yule dereva wa boda boda anisubiri kidogo

Tulipofika ndani tulipokelewa na Bi mkubwa mmoja mnene na mweupe, na baada ya kusalimiana nae Ramla alinitambulisha kua ndie Bi Ayman Gamba,nikamsabahi na baada ya kumsabahi nikamueleza kilichonipeleka
"Mama mimi natokea Dar japo asili yangu ni wa hapa hapa Tabora, nimepewa mzigo huu kutoka kwa mke wa Boss wangu kaniambia nimkabidhi dada yake" aliupokea mzigo na kunishukuru sana Kisha mimi nikaaga zangu, wakati naondoka Ramla akaniwahi na kunitania
"Umeshamaliza shida zako hata hauniagi eeh?"
"Nilijua uko nje, haya nakusubiri unisindikize" Binti yule akanifuata kama ananisindikiza vile nikaona kama nyota ya Jaa imeniangukia,tukawa tunatoka nje huku tupiga story mbili tatu japo hazikua za msingi na baada ya utani wa hapa na pale tukaagana, Lakini kabla sijaondoka nikamchombeza kua anipe namba yake kama hatojali, nae bila ajizi akaishika simu yangu aina ya Sumsung akaandika namba yake halafu akaji beep baada ya hapo tukaagana kwa tabasamu kila upande...ISHARA NZURI

Niliporejea nyumbani akili ikawa ni kwa Ramla tu, ilipofika usiku tukaanza kuwasiliana kwa msg, tulitaniana, tulisifiana, daah basi sikulala siku hiyo,, kwa kifupi Ramla alikua ni binti mrembo alieumbika kike,anapendeza machoni, hali ilikua hivyo kwa karibu siku tatu mfulilizo mwishowe kijana wa Kinyamwezi nikajitosa kutamka maneno matamu yakuomba hifadhi ya nafsi yangu katika bustani ang'avu la moyo wake, Haikua kazi rahisi sana kutokana na mbwembwe na mapozz niliyokutana nayo kwake, haikunifanya nikate tamaa nikaendelea kila siku kumgasi Mwishowe Mtoto Ramla akinielewa na kunikaribisha sio tu sebuleni bali mpaka chini ya uvungu wa moyo wake, ikawa ni mapenzi moto moto mpaka kizunguzungu!!, Ndani ya wiki kama mbili tu za mapenzi yetu motomoto muda wangu wa kurudi Dar ulifika na nikawa sina budi kuondoka..

Nakumbuka tuliagana siku hiyo kwa furaha iliyojawa na majonzi maana Ramla alikua akilia akihisi nitamsahau nikfika mjini lakini nilimbembeleza na kumuahidi kua nikifika Dar baada ya wiki mwezi mmoja ningemtumia nauli aje ili nimfanyie mpango wa Shule maana alikua amenieleza mambo mengi kuhusu Familia yao kua wanaishi maisha ya tabu na dhiki tangu baba yake Mzazi alipoikimbia Familia yeye akiwa mdogo sana,Alinieleza kua aliishia kidato cha nne hivyo alitamani sana kuendelea na masomo lakini hali ya kiuchumi haikua nzuri kwao na Mama yakehataki Ramla aende Dar kwa huyo mama yake mdogo mke wa Boss wangu MrJimmy kwa kua yule alibadilishwa dini na Jimmy na kuolewa hivyo anahofia kua kama akiienda kukaa kule nae ataweza kushawishiwa kufanya mambo kama hayo..

Baadaya mwezi mmoja nikawasiliana na Ramla nikamtumia pesa za nauli kwa ajili ya kuja Dar na pia nikamuongezea pesa za kumuachia Mama yake pale nyumbani ili asipate taabu siku za mwanzo, kweli baada ya siku kama tatu hivi akaja Dar, ilikua ni kazi kubwa kwangu ya kumtoa tongotongo za macho kwa kumtembeza kila kona ya Jiji hili la maraha ili nae auone mji, na baadae nilimtafutia chuo pale IFM akawa anaishi pale pale katika Hostel nilijipa majukumu ya kumuhudumia kila kitupia ilibidi sasa mama yake ajue kila kitu kua kwa sasa mimi ndie niko na mwanae na ndie ninae msomesha chuo ikabidi sasa nipeleke kwao na Barua ya Uchumba ili akimaliza chuo tu nimuoe, nikawa sasa namuhudumia mpaka na mama mkwe pindi apatwapo na matatizo. nashukuru Mungu Mama huyu aliniheshimu na kunithamini sana, japo Ramla alikua anenda kwa mama yake mdogo mke wa Boss wangu Mr Jimmy lakini ilikua ni mara moja moja sana...

*****
Wakati tukiwa katikati ya mazungumzo na Ntahondi ghafla mlango ukafunguliwa kwa kasi kisha akiingi Mtu mmoja mnene bila Shaka alikua ndo PABLO MWAKI Maana mimi sikua nikimjua kwa sura zaidi ya kumjua kwa sifa zake tu...
Baadaya mlango ule kufunguliwa kwa kasi aliingia kijana mmoja Mnene,Mweupe, hakua mrefu sana ila ana kimo kiasi chake, niliendelea kuamini kua huyu ndie PABLO MWAKI Tajiri alieamua kuvunja penzi langu kwa Ramla kwa kutumia Ukwasi aliokua nao na hatimae kuniteka na kuagiza vijana wake wanitese na hatimae waniue. Baada ya Njemba hiikusogea mpaka pale chini tulipokua tumekaa tukijaribu kuwaza nakuwazua njia ya kujiokoa kutoka katika mikono ya mabaradhuli hawa,alipofika akauliza huku akiniangalia usoni
"Wendie Naufal?"
"Ndio"
"Ninani Mwingine zaidi ya huyu Ntahondi anaejua kua ulikua na matatizo na PABLO?" nikamjibu tena
"Hakuna anaejua mkuu" baada ya hapo akaja upande wangu wa kushoto Kisha akamuangalia Ntahondi usoni kisha akasema kwa kebehi nadharau
"Ntahondi,Mrembo wa IFM" Kisha akauliza kwa sauti Nyepesi
"Ninani mwingine uliempa story za PABLO zaidi ya huyu Naufal?"
"Hakunaanaejua". Baada ya maswali hayo jamaa akatoka nje...

Tulibakutumepigwa na butwaa huku tukiangaliana, binafsi nilijua fika kuawalichotaka kufahamu ni nani mwingine anapaswa kutekwa kablahajavujisha taarifa zozote zinazoendelea kati yangu na PABLO Iliwatakapotuua mambo yao yaendelee kubaki kua ni Siri. ndani ya dakikakadhaa waliingia tena mule ndani vijana wengine wawili wakiwa nakamba mikononi walipofika wakaniinua na kunifunga kamba mikononi nakisha kunining'iniza juu kama mbuzi anaesubiri kuchunwa, kisha wakajakwa Ntahondi nae wakampeleka mpaka pembezoni mwa kitanda cha Simentiambacho hua nalalia mimi, kuna kiti maalum kwa ajili ya kupewa matesoya Umeme nae wakamfunga kisawa sawa halafu wakatoka nje vijanawale...

Tulikaakatika hali ile ya Sintofahamu huku kila mmoja akiwaza yake juu yanini tulikua tunakuja kufanyiwa, sikuamini kama ndo tulikua tunauliwakwa kua nilishadokezwa na Ntahondi kua Tungeuawa siku ya Graduationya kina Ramla ambayo ingefanyika miezi miwili baadae.. nikiwanaendelea kusali sala zote mpaka sasa nikawa nachanganya dua maananilijikuta Eti nasoma dua ya kuchinjia kuku anhaa Usiombee Matatizoyakufike kooni, Ghafla akaingia tena yule Bonge aliekuja kutuhojimaswali, mara hii akiwa amevalia kihatari hatari, alikua amevaa Buktaya Jeanz, tishert nyepesi, mikononi aevaa Gloves, aliingia naKebo(waya) maalum kwa ajili ya kutolea adhabu, sindano ndefu sikujuani ya nini, mawe ya kupimia uzito kwenye mizani, na vifaa vinginevingi ambavyo sikuelewa na vya nini?, nilipogeuka upande wangu wakulia nilimuona Ntahondi maskini akilia kwa Uchungu sana..

Njembaile ikaja usawa wangu na kuniuliza
"Umekataakutaja mtu anaejua kuhusu suala hili huko nje?!" nikajibu hukunikitokwa na Machozi
"Siwezikukudanganya kaka, hakuna anaejua", akahamia kwa Ntahondi naeakamuuliza swali kama langu kilichonishangaza na ule ujasiri waNtahondi pale alipojibu pengine akiwa ameshakata tamaa ya kuishitena
"Tumechokana mateso yenu ni bora mkatuaa tu" majibu yale yalimkera Njembayule nikashangaa akipiga ngumi za nguvu kama anampiga mwanaume,Ntahondi alikua akilia kwa sauti ya Uchungu sana, nilishindwakuendelea kumuangalia tukio lile nikawa nimefumba macho, nilipofumbuamacho nilimuona Ntahondi akiwa anavuja damu uso mzima..

KishaNjemba hii ikahamia kwangu, ilipofika haikuuliza kitu, ilikua niadhabu juu ya adhabu, nilichapwa sana na waya, nikawa nachomwa na ilesindano kwenye Ncha za vodole vyangu, Kijana huyu aliendelea kunipigabila ya kunipa mapumziko huku akinisisitiza nitaje mtu anaejua mkasahuu, nililia huku nikijitetea kua hakuna anaejua, baada ya kipigo chamuda mrefu kilichoniacha na maumivu makali na majeraha, Baunsa huyuakarudi kwa Ntahondi ma kuanza kumpa sasa mateso ya Shot ya UmemeNtahondi alikua akipiga kelele nyingi sana! nikaanza kupotezamatumaini kama angeweza kustahmili ukali wa mateso yale na Pengineangemtaja Mwl Honde ambae bila Shaka ndie mtu aliebaki huko uraianiakijaribu kutupigania..

Tuliteswakwa kiwango cha ajabu bila ya kutaja chochote walichotaka na baadaekijana yule akatoka nje akiwa anavuja jasho sana kwa kazi nzito yautesaji dhidi ya viumbe wasiokua na hatia, dakika kumi baadae wakajavijana wale waliotufunga kamba kisha wakatufungua tukiwa hoi, tulikaakama saa moja hivi wakatuletea chakula kidogo sana na maji, ikabidimie nijifanye nimeshiba ili tu ale Ntahondi peke yake maana chakulakilikua kidogo kiasi kwamba kisingemtosha hata mtoto mdogo LakiniNtahondi ane aligoma kula peke yako ikabidi tule hivyo hivyo wotewawili baada ya hapo tukalala mpaka asubuhi

Haliya mateso iliendelea kila siku jioni na huku tukiambiwa kua wangeachakututesa kama tutawataja japo watu wawili wanaojua habari ile kuamimi na PABLO Tunagombania Mwanamke ambae ili nao watiwe nguvuniwasije wakavujisha siri itakayokusababisha Serikali pengine ianzekumchunguza PABLO na hatimae kumtia nguvuni, Siku moja alikua huyuBaunsa anaetutesa kila siku na kumchukua Ntahondi kisha akaondka naena sikujua alipompeleka, nilibaki na hofu kubwa nikijua kua hukopengine Ntahondi ataadhibiwa sana mpaka atatoa taarifa za watuwanaojua sakata hili, pia niljua kua wangeweza hata kumuua huko kamaangeendelea na msimamo wa kutotaja mtu hata mmoja, Lakini nashukuruMungu ilipofika saa moja na nusu jioni Ntahondi alirudishwa ikiwa saazima limepita tangu waondoke nae..

"Vipiuko salama kweli? nilijua wameenda kukuua" nilimuuliza Ntahondi,nae akajibu
"Nikosalama wangu, mie mwenyewe nilijua sitakukuta tena Thanx God tukosalama", nikaendelea kumuhoji kilichojiri huko, nae bila yakusita akaanza kutiririka
"Mwenzangusasa hapa we have to do something, kwa kifupi huyu jamaa kaniambiaananitaka kimapenzi na endapo nitamkubali hatokua anatutesa tena natutapewa chakula kizuri kila siku na atajitahidi kutufanyia mpango wakutoroka kabla ya siku ya Graduation ambayo ndo imepangwa kua PABLOAtakuja kutuua" Nilijikuta nimeshusha Pumzi nzito, nikiwa sinacha kushauri maana kutoroshwa nataka, lakini sitaki binti huyuaudhalilishe mwili wake kwa kumpa Rushwa ya penzi mtu asiemjua vema,pengine ni muathirika wa magonjwa mbali mbali ikiwemo Ukimwi, piainawezekana ni tama zake tu za ngono lakini wala asitutoroshe. nikiwabado sijajua cha kushauri Ntahondi akendelea kufunguka kua
"Naameniambia kua Leo anaenda mjini kuonana na PABLO hivyo ataachamaagizo kwa vijana wake kua watupe chakula kizur na maji na atakaahuko kwa muda wa siku tano tu halafu atarudi hivyo akirudi kasemasiku hiyo atakuja kulinda yeye peke na hawa vijana wake wataendamjini kutembea hivyo siku hiyo ndo nikalale nae..

Tukiwakatikati ya majadiliano ya nini cha kufanya, Mlango ukafunguliwaakaingia mmoja kati ya wale vijana ambao hua wanatufunga kamba kablaya kuanza kuteswa. lakini safari hii aliingia akiwa na Ndoo mbili zamaji, akaziweka chini kisha akatoka nje na kurudi na Mfuko mweusi unanguo na shuka ndani yake kisha akasema kila mtu akaoge kisha avaenguo halafu tusubiri chakula cha usiku, yaani sikuamini kinachotokeamaana karibu mwezi na Nusu sasa sijaoga zaidi ya kumwagiwa maji ilinizinduke baada ya kuzimia kutokana na kuzidiwa na kichapo kikalinachopewa mara kwa mara halikadhalika Ntahondi. tukaaingia kuoga zamukwa zamu na baada ya kupata maji ngozi sasa walau ilionekana ni yakibinaadamu japo nilikua na vidonda vilivyotokana na moto niliokuanaunguzwa kwa kutumia Misumari na Sindano zilizowivishwa kwenye moto,Ndani ya mfuko kila mtu alivaa nguo alizozikuta kutokana na jinsiayake na pia kulikua na shuka mbili za kujifunika, Ntahondi alikua naupele mwingi usoni uliotokana na Mbu waliokua wakituuma siku zotetulipokua tukilala kwenye simenti bila hata ya Shuka..

Baadaya kumaliza kuoga kijana yule kijana akatuijia na kutupeleka kwenyechumba kingine kilichokua na vitanda vidogo viwili na meza mojailiyokua na chakula juu, kisha akatuambia "Mkimaliza kula kilamtu alale kwenye kitanda chake" kisha akatoka zake, nilibakinikimtazama Ntahondi kwa macho ya mshangao wa kila kinachoendelea,walau sasa tulifarijka kwa huduma mpya tulizopewa, sikua na Furahasana kwakua niliamini kua siku tano zijazo itampasa Ntahondiawajibike kuzilipa huduma hizi kwa kumuhonga Rushwa ya Ngono yuleBaunsa mweupe, baada ya Chakula tulipumzika na kisha tukaendelea namajadiliano yetu..

Nilianza mimi kutoa ushauri wa nini cha kufanya ambapo Ntahondi aliuafiki kisawasawa ushauri huu
"Sasahuu ndo muda wetu wa kutoroka, muda wa kuokoa maisha yetu, chakufanya tuwe majasiri kwa kila hatua, kwakua siku hiyo ambayo jamaaanataka ulale nae atakua peke yake humu kama Mlinzi itatupasatuitumie fursa hiyo kumzidi akili, tumtie nguvuni sisi na hatimaetuondoka humu ndani"
"Kwa hiyo tutamuwekea sumu au? "
"Humu ndani hatuwezi kupata sumu kirahisi hivyo"
"Kwa hiyo tutafanyaje? "
"Itabidi tujue Bunduki yake anaiweka wapi ili ukiwa nae kitandani mienitaingia ghafla na kuichukuanajua kutumia Bunduki ipasavyo na hapohapo sitamkawiza nitausambaza Ubongo wake na safari itaanza, chamsingi ukishaingia nae tu Chumbani hakikisha hamjafunga mlango"
"Naufalhiyo ni hatari sana, una uhakika kua unajua kutumia Bunduki wewe?"
"Ondoa shaka, mie zamani nilikua naenda Porini kuwinda na kaka yangu huko nijifundisha kutumia Bunduki za aina nyingi tofauti"
Ntahondi aliinuka kwa fu...raha na kunikumbatia kwa wazo zuri nililitoa, na hapo tukaanza kujiandaa tu na utekelezaji


culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata binti kiziwi Nicas Mtei korino Sukula aniceth mzahula Khantwe kelcie chwechinyong ram tabibumtaratibu Ngekewa

 
Last edited by a moderator:
Haya weee.... ngoja tuone kama mtaokoka
 
RIWAYA:SIKU YA GRADUATION
MTUNZI:MAUNDU MWINGIZI


SEHEMUYA NNE


TULIVYOKUTANANA RAMLA
Ilikua ni mwaka 2009, Mwaka mmoja tangu nipate kazi kwenye kampuni ya KIGWAZA inayojishughulisha na Upakiaji na upakuaji mizigo bandarini kama Muhasibu nikachukua likizo fupi kwa ajili ya kwenda kumsalimu Mama yangu mzazi Bi Shammy Naufal aishiye Tabora, niliifurahia sana safari hii kwakua ilikua ni muda mrefu sana sijaenda nyumbani hivyonilitaraji kuonana na Mama yangu kipenzi, Ndugu zangu, na Marafikizangu ambao tulikua tukikaa wote kijiweni tukibadilishani story kadhawa kadha..

Niliwasili TABORA majira ya saa kumi na mbili jioni, nilipokelewa na wadogozangu waliokuja Stand ya Mabasi kunipokea kisha tukaondoka mpakanyumbani ambako nilipokelewa kwa shangwe na Mama na ndugu wenginewaliokua pale nyumbani, ilikua ni siku ya furaha sana kwangu, kama kawaida ya wageni mambo kama Jogoo huusika kwa asilia mia wakati wamduara wa chakula cha usiku na kila aina ya vinywaji ilipofika Saasita kasoro(usiku) niliondoka na kwenda Chumbani kwa Mdogo wangu wakiume na kujiandaa kwa ajili ya kulala..

Asubuhi ya siku iliyofuata niliamka mapema, na baada ya kuoga na kupata kifungua kinywa nikajipumzisha kidogo pale ukumbini na kisha nikamuaga Mama kua ninaenda kijiweni kuwasalimia jamaa zangu kisha kuna Mzigo nilipewa na Mke wa Boss wangu ili niupeleke kwa dada yake anaishi Mtaa wa Rufita anaitwa Bi Ayman Gamba, baada ya hapo nikaanza kujongea kijiweni ambako pia nilipokelewa kwa furaha sana nawashikaji zangu wa kitambo niliowaacha wakati naenda Dsm, tukiwa katikati ya Story alikatiza binti mmoja ana mirindimo mithili ya Mjaluo, Mrembo, Mrefu, sio Mweupe wala si mweusi, Hips kama amefichapanya, , yaani kama we ni Rijali lazima ungegeuka mara mbili kumtazama. Huyo si mwingine alikua ni RAMLA

Baadaya kuwaulizia washikaji kuhusu binti huyu waliniambia kua anakaa mtaa wa Rufita, kuhusu shughuli zake niliambiwa kua anafanya kazi za msimukatika ofisi za ATTT! Nilitamani kujua mengi zaidi yamuhusuyo bintihuyu lakini washikaji walibadili mada na tukaendelea na Story zangubaada ya muda mrefu niliwaaga jamaa ili niende sasa nikamtafute huyoBi Ayman wa mitaa ya Rufita maana nilikua sipaju anapokaa, nikachukuaboda boda kisha nikaondoka zangu, nilipofika Rufita maeneoniliyoelekezwa tukasimaa kisha nikateremka kwenye boda boda ilinimuulize mmoja wa vijana aliekua upande wa pili wa bara bara lakinikabla sijavuka akatokea msichana mmoja katika nyumba niliyokuanimesimama akamwaga maji nje nilipogeuka na kumuangalia alikua niyule binti mrembo aliepita kule kijiweni

Kabla sijasema chochote akaniwahi yeye kwa kunisalimia
"Mambo"
"Poa,mzima wewe?
"Memzima, mara tu umefika huku?" hili swali likanishtua nikahisiamenifananisha lakini kabla sijamjibu chochote akaniwahi kwa swalijingine
"Kwaniwewe si nilikupita na jamaa zako mmekaa kule Minazi mikinda?"nikajua hakua akibahatisha
"Duhuna kumbukumbu sana, yeah ni mimi. sasa mie naomba kukuuliza,napaulizia kwa kwa Bi Ayman Gamba!!" akacheka kidogo kishaakanijibu kwa Pozz
"naunaeongea nae hapa ni binti yake aitwae Ramla, karibu ndani"wote tukacheka na kisha tukaangia ndani, nikamuomba yule dereva waboda boda anisubiri kidogo

Tulipofika ndani tulipokelewa na Bi mkubwa mmoja mnene na mweupe, na baada yakusalimiana nae Ramla alinitambulisha kua ndie Bi Ayman Gamba,nikamsabahi na baada ya kumsabahi nikamueleza kilichonipeleka
"Mamamimi natokea Dar japo asili yangu ni wa hapa hapa Tabora, nimepewamzigo huu kutoka kwa mke wa Boss wangu kaniambia nimkabidhi dadayake" aliupokea mzigo na kunishukuru sana Kisha me nikaagazangu, wakati naondoka Ramla akaniwahi na kunitania
"Umeshamalizashida zako hata hauniagi eeh?"
"Nilijuauko nje, haya nakusubiri unisindikize" Binti yule akanifuatakama ananisindikiza vile nikaona kama nyota ya Jaa imeniangukia,tukawa tunatoka nje huku tupiga story mbili tatu japo hazikua zamsingi na baada ya utani wa hapa na pale tukaagana, Lakini kablasijaondoka nikamchombeza kua anipe namba yake kama hatojali, nae bilaajizi akaishika simu yangu aina ya Sumsung akaandika namba yakehalafu akaji beep baada ya hapo tukaagana kwa tabasamu kila upande...ISHARA NZURI

Niliporejeanyumbani akili ikawa ni kwa Ramla tu, ilipofika usiku tukaanzakuwasiliana kwa msg, tulitaniana, tulisifiana, daah basi sikulalasiku hiyo,, kwa kifupi Ramla alikua ni binti mrembo alieumbika kike,anapendeza machoni, hali ilikua hivyo kwa karibu siku tatu mfulilizomwishowe kijana wa Kinyamwezi nikajitosa kutamka maneno matatmu yakuomba hifadhi ya nafsi yangu katika bustani ang'avu la moyo wake,Haikua kazi rahisi sana kutokana na mbwembwe na mapozz niliyokutananayo kwake, haikunifanya nikatae tamaa nikaendelea kila siku kumgasiMwishowe Mtoto Ramla akinielewa na kunikaribisha sio tu sebuleni balimpaka chini ya uvungu wa moyo wake, ikawa ni mapenzi moto moto mpakakizunguzungu!!, Ndani ya wiki kama mbili tu za mapenzi yetu moto motomuda wangu wa kurudi Dar ulifika na nikawa sina budikuondoka..

Nakumbukatuliagana siku hiyo kwa furaha iliyojawa na majonzi maana Ramlaalikua akilia akihisi nitamsahau nikfika mjini lakini nilimbembelezana kumuahidi kua nikifika Dar baada ya wiki mwezi mmoja ningemtumianauli aje ili nimfanyie mpango wa Shule maana alikua amenieleza mambomengi kuhusu Familia yao kua wanaishi maisha ya tabu na dhiki tangubaba yake Mzazi alipoikimbia Familia yeye akiwa mdogo sana,Alinieleza kua aliishia kidato cha nne hivyo alitamani sana kuendeleana masomo lakini hali ya kiuchumi haikua nzuri kwao na Mama yakehataki Ramla aende Dar kwa huyo mama yake mdogo mke wa Boss wangu MrJimmy kwa kua yule alibadilishwa dini na Jimmy na kuolewa hivyoanahofia kua kama akiienda kukaa kule nae ataweza kushawishiwakufanya mambo kama hayo..

Baadaya mwezi mmoja nikawasiliana na Ramla nikamtumia pesa za nauli kwaajili ya kuja Dar na pia nikamuongezea pesa za kumuachia Mama yakepale nyumbani ili asipate taabu siku za mwanzo, kweli baada ya sikukama tatu hivi akaja Dar, ilikua ni kazi kubwa kwangu ya kumtoa tongotongo za macho kwa kumtembeza kila kona ya Jiji hili la maraha ilinae auone mji, na baadae nilimtafutia chuo pale IFM akawa anaishipale pale katika Hostel nilijipa majukumu ya kumuhudumia kila kitupia ilibidi sasa mama yake ajue kila kitu kua kwa sasa mimi ndie nikona mwanae na ndie ninae msomesha chuo ikabidi sasa nipeleke kwao naBarua ya Uchumba ili akimaliza chuo tu nimuoe, nikawa sasanamuhudumia mpaka na mama mkwe pindi apatwapo na matatizo. nashukuruMungu Mama huyu aliniheshimu na kunithamini sana, japo Ramla alikuaanenda kwa mama yake mdogo mke wa Boss wangu Mr Jimmy lakini ilikuani mara moja moja sana...

*****
Wakatitukiwa katikati ya mazungumzo na Ntahondi ghafla mlango ukafunguliwakwa kasi kisha akiingi Mtu mmoja mnene bila Shaka alikua ndo PABLOMWAKI Maana mimi sikua nikimjua kwa sura zaidi ya kumjua kwa sifazake tu...
Baadaya mlango ule kufunguliwa kwa kasi aliingia kijana mmoja Mnene,Mweupe, hakua mrefu sana ila ana kimo kiasi chake, niliendeleakuamini kua huyu ndie PABLO MWAKI Tajiri alieamua kuvunja penzi langukwa Ramla kwa kutumia Ukwasi aliokua nao na hatimae kuniteka nakuagiza vijana wake wanitese na hatimae waniue. Baada ya Njemba hiikusogea mpaka pale chini tulipokua tumekaa tukijaribu kuwaza nakuwazua njia ya kujiokoa kutoka katika mikono ya mabaradhuli hawa,alipofika akauliza huku akiniangalia usoni
"Wendie Naufal?"
"Ndio"
"Ninani Mwingine zaidi ya huyu Ntahondi anaejua kua ulikua na matatizona PABLO?" nikamjibu tena
"Hakunaanaejua mkuu" baada ya hapo akaja upande wangu wa kushoto Kishaakamuangalia Ntahondi usoni kisha akasema kwa kebehi nadharau
"Ntahondi,Mrembo wa IFM" Kisha akauliza kwa sauti Nyepesi
"Ninani mwingine uliempa story za PABLO zaidi ya huyu Naufal?"
"Hakunaanaejua". Baada ya maswali hayo jamaa akatoka nje...

Tulibaki tumepigwa na butwaa huku tukiangaliana, binafsi nilijua fika kuawalichotaka kufahamu ni nani mwingine anapaswa kutekwa kablahajavujisha taarifa zozote zinazoendelea kati yangu na PABLO Iliwatakapotuua mambo yao yaendelee kubaki kua ni Siri. ndani ya dakikakadhaa waliingia tena mule ndani vijana wengine wawili wakiwa nakamba mikononi walipofika wakaniinua na kunifunga kamba mikononi nakisha kunining'iniza juu kama mbuzi anaesubiri kuchunwa, kisha wakajakwa Ntahondi nae wakampeleka mpaka pembezoni mwa kitanda cha Simentiambacho hua nalalia mimi, kuna kiti maalum kwa ajili ya kupewa matesoya Umeme nae wakamfunga kisawa sawa halafu wakatoka nje vijanawale...

Tulikaakatika hali ile ya Sintofahamu huku kila mmoja akiwaza yake juu yanini tulikua tunakuja kufanyiwa, sikuamini kama ndo tulikua tunauliwakwa kua nilishadokezwa na Ntahondi kua Tungeuawa siku ya Graduationya kina Ramla ambayo ingefanyika miezi miwili baadae.. nikiwanaendelea kusali sala zote mpaka sasa nikawa nachanganya dua maananilijikuta Eti nasoma dua ya kuchinjia kuku anhaa Usiombee Matatizoyakufike kooni, Ghafla akaingia tena yule Bonge aliekuja kutuhojimaswali, mara hii akiwa amevalia kihatari hatari, alikua amevaa Buktaya Jeanz, tishert nyepesi, mikononi aevaa Gloves, aliingia naKebo(waya) maalum kwa ajili ya kutolea adhabu, sindano ndefu sikujuani ya nini, mawe ya kupimia uzito kwenye mizani, na vifaa vinginevingi ambavyo sikuelewa na vya nini?, nilipogeuka upande wangu wakulia nilimuona Ntahondi maskini akilia kwa Uchungu sana..

Njemba ile ikaja usawa wangu na kuniuliza
"Umekataakutaja mtu anaejua kuhusu suala hili huko nje?!" nikajibu hukunikitokwa na Machozi
"Siwezikukudanganya kaka, hakuna anaejua", akahamia kwa Ntahondi naeakamuuliza swali kama langu kilichonishangaza na ule ujasiri waNtahondi pale alipojibu pengine akiwa ameshakata tamaa ya kuishitena
"Tumechokana mateso yenu ni bora mkatuaa tu" majibu yale yalimkera Njembayule nikashangaa akipiga ngumi za nguvu kama anampiga mwanaume,Ntahondi alikua akilia kwa sauti ya Uchungu sana, nilishindwakuendelea kumuangalia tukio lile nikawa nimefumba macho, nilipofumbuamacho nilimuona Ntahondi akiwa anavuja damu uso mzima..

KishaNjemba hii ikahamia kwangu, ilipofika haikuuliza kitu, ilikua niadhabu juu ya adhabu, nilichapwa sana na waya, nikawa nachomwa na ilesindano kwenye Ncha za vodole vyangu, Kijana huyu aliendelea kunipigabila ya kunipa mapumziko huku akinisisitiza nitaje mtu anaejua mkasahuu, nililia huku nikijitetea kua hakuna anaejua, baada ya kipigo chamuda mrefu kilichoniacha na maumivu makali na majeraha, Baunsa huyuakarudi kwa Ntahondi ma kuanza kumpa sasa mateso ya Shot ya UmemeNtahondi alikua akipiga kelele nyingi sana! nikaanza kupotezamatumaini kama angeweza kustahmili ukali wa mateso yale na Pengineangemtaja Mwl Honde ambae bila Shaka ndie mtu aliebaki huko uraianiakijaribu kutupigania..

Tuliteswa kwa kiwango cha ajabu bila ya kutaja chochote walichotaka na baadaekijana yule akatoka nje akiwa anavuja jasho sana kwa kazi nzito yautesaji dhidi ya viumbe wasiokua na hatia, dakika kumi baadae wakajavijana wale waliotufunga kamba kisha wakatufungua tukiwa hoi, tulikaakama saa moja hivi wakatuletea chakula kidogo sana na maji, ikabidimie nijifanye nimeshiba ili tu ale Ntahondi peke yake maana chakulakilikua kidogo kiasi kwamba kisingemtosha hata mtoto mdogo LakiniNtahondi ane aligoma kula peke yako ikabidi tule hivyo hivyo wotewawili baada ya hapo tukalala mpaka asubuhi

Haliya mateso iliendelea kila siku jioni na huku tukiambiwa kua wangeachakututesa kama tutawataja japo watu wawili wanaojua habari ile kuamimi na PABLO Tunagombania Mwanamke ambae ili nao watiwe nguvuniwasije wakavujisha siri itakayokusababisha Serikali pengine ianzekumchunguza PABLO na hatimae kumtia nguvuni, Siku moja alikua huyuBaunsa anaetutesa kila siku na kumchukua Ntahondi kisha akaondka naena sikujua alipompeleka, nilibaki na hofu kubwa nikijua kua hukopengine Ntahondi ataadhibiwa sana mpaka atatoa taarifa za watuwanaojua sakata hili, pia niljua kua wangeweza hata kumuua huko kamaangeendelea na msimamo wa kutotaja mtu hata mmoja, Lakini nashukuruMungu ilipofika saa moja na nusu jioni Ntahondi alirudishwa ikiwa saazima limepita tangu waondoke nae..

"Vipiuko salama kweli? nilijua wameenda kukuua" nilimuuliza Ntahondi,nae akajibu
"Nikosalama wangu, mie mwenyewe nilijua sitakukuta tena Thanx God tukosalama", nikaendelea kumuhoji kilichojiri huko, nae bila yakusita akaanza kutiririka
"Mwenzangusasa hapa we have to do something, kwa kifupi huyu jamaa kaniambiaananitaka kimapenzi na endapo nitamkubali hatokua anatutesa tena natutapewa chakula kizuri kila siku na atajitahidi kutufanyia mpango wakutoroka kabla ya siku ya Graduation ambayo ndo imepangwa kua PABLOAtakuja kutuua" Nilijikuta nimeshusha Pumzi nzito, nikiwa sinacha kushauri maana kutoroshwa nataka, lakini sitaki binti huyuaudhalilishe mwili wake kwa kumpa Rushwa ya penzi mtu asiemjua vema,pengine ni muathirika wa magonjwa mbali mbali ikiwemo Ukimwi, piainawezekana ni tama zake tu za ngono lakini wala asitutoroshe. nikiwabado sijajua cha kushauri Ntahondi akendelea kufunguka kua
"Naameniambia kua Leo anaenda mjini kuonana na PABLO hivyo ataachamaagizo kwa vijana wake kua watupe chakula kizur na maji na atakaahuko kwa muda wa siku tano tu halafu atarudi hivyo akirudi kasemasiku hiyo atakuja kulinda yeye peke na hawa vijana wake wataendamjini kutembea hivyo siku hiyo ndo nikalale nae..

Tukiwakatikati ya majadiliano ya nini cha kufanya, Mlango ukafunguliwaakaingia mmoja kati ya wale vijana ambao hua wanatufunga kamba kablaya kuanza kuteswa. lakini safari hii aliingia akiwa na Ndoo mbili zamaji, akaziweka chini kisha akatoka nje na kurudi na Mfuko mweusi unanguo na shuka ndani yake kisha akasema kila mtu akaoge kisha avaenguo halafu tusubiri chakula cha usiku, yaani sikuamini kinachotokeamaana karibu mwezi na Nusu sasa sijaoga zaidi ya kumwagiwa maji ilinizinduke baada ya kuzimia kutokana na kuzidiwa na kichapo kikalinachopewa mara kwa mara halikadhalika Ntahondi. tukaaingia kuoga zamukwa zamu na baada ya kupata maji ngozi sasa walau ilionekana ni yakibinaadamu japo nilikua na vidonda vilivyotokana na moto niliokuanaunguzwa kwa kutumia Misumari na Sindano zilizowivishwa kwenye moto,Ndani ya mfuko kila mtu alivaa nguo alizozikuta kutokana na jinsiayake na pia kulikua na shuka mbili za kujifunika, Ntahondi alikua naupele mwingi usoni uliotokana na Mbu waliokua wakituuma siku zotetulipokua tukilala kwenye simenti bila hata ya Shuka..

Baadaya kumaliza kuoga kijana yule kijana akatuijia na kutupeleka kwenyechumba kingine kilichokua na vitanda vidogo viwili na meza mojailiyokua na chakula juu, kisha akatuambia "Mkimaliza kula kilamtu alale kwenye kitanda chake" kisha akatoka zake, nilibakinikimtazama Ntahondi kwa macho ya mshangao wa kila kinachoendelea,walau sasa tulifarijka kwa huduma mpya tulizopewa, sikua na Furahasana kwakua niliamini kua siku tano zijazo itampasa Ntahondiawajibike kuzilipa huduma hizi kwa kumuhonga Rushwa ya Ngono yuleBaunsa mweupe, baada ya Chakula tulipumzika na kisha tukaendelea namajadiliano yetu..

Nilianzamimi kutoa ushauri wa nini cha kufanya ambapo Ntahondi aliuafikikisawasawa ushauri huu
"Sasahuu ndo muda wetu wa kutoroka, muda wa kuokoa maisha yetu, chakufanya tuwe majasiri kwa kila hatua, kwakua siku hiyo ambayo jamaaanataka ulale nae atakua peke yake humu kama Mlinzi itatupasatuitumie fursa hiyo kumzidi akili, tumtie nguvuni sisi na hatimaetuondoka humu ndani"
"Kwahiyotutamuwekea sumu au? "
"Humundani hatuwezi kupata sumu kirahisi hivyo"
"Kwahiyotutafanyaje? "
"Itabiditujue Bunduki yake anaiweka wapi ili ukiwa nae kitandani mienitaingia ghafla na kuichukuanajua kutumia Bunduki ipasavyo na hapohapo sitamkawiza nitausambaza Ubongo wake na safari itaanza, chamsingi ukishaingia nae tu Chumbani hakikisha hamjafungamlango"
"Naufalhiyo ni hatari sana, una uhakika kua unajua kutumia Bunduki wewe?"
"Ondoashaka, mie zamani nilikua naenda Porini kuwinda na kaka yangu hukonijifundisha kutumia Bunduki za aina nyingi tofauti"
Ntahondialiinuka kwa fu...raha na kunikumbatia kwa wazo zuri nililitoa, nahapo tukaanza kujiandaa tu na utekelezaji


culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata binti kiziwi Nicas Mteikorino Sukula aniceth mzahulaKhantwe kelcie chwechinyong ram tabibumtaratibu Magembeh Emmanuel Thadei
 
Weka episod nyingine basa Mkuu Casuist
Iko poa sana hii story
 
Last edited by a moderator:
RIWAYA: SIKU YA GRADUATION
MTUNZI: MAUNDU MWINGIZI

SEHEMU YA TANO

Siku zilizidi kuyoyoma kuelekea kwenye Graduation ya kina Ramla, siku ambayo mbali ya kuhitimu masomo yake pia alikua akijiandaa kuvishwa pete ya Mwanaume wake PABLO MWAKI wakati huo huo hii ndo siku iliyopangwa kwa ajili ya kutekeleza azma ya kutuua mimi na Ntahondi tukiwa hukuhuku Msituni, Hasira zilinipamba kichwani kila nikikumbuka jinsi nilivyokutana na Ramla kwa mara ya kwanza, nikamtoa Tabora na kumleta Jijini Dar Es Salaam, nikikumbuka gharama kubwa nilizokua nikizitumia kwa ajili ya kumlipia ada, malazi na Chakula bila ya kusahau jinsi nilivyokua nikituma pesa za matumizi kwa mama yake Mzazi aliebaki Tabora halafu Leo amenisaliti kisa kapata Mwanaume Tajiri na Maarufu kuliko mimi mbaya zaidi na Mama yake nilietegemea angekua ndie kimbilio langu nae kaingiwa na Tamaa ya pesa na kutaka tu Mwanae aolewe na Tajiri huyu..

Tangu aondoke yule Baunsa mweupe anaemtaka kimapenzi Ntahondi tuliendelea kuishi chini ya ulinzi mkali japokua hali ya mateso kwa sasa haikuwepo tena bila shaka ni kutokana na maelekezo waliyoachiwa vijana hawa kutoka kwa jamaa huyo anaemzengea Ntahondi, tulikua tunakula chakula ambacho kiasi ni kizuri ukilinganisha na kile tulichokua tukipewa awali, pia maji ya kunywa na kuoga tulipatiwa na hata Malazi yetu kwa sasa yalikua yana ahueni kiasi, tuliendelea kulala Chumba kimoja mimi na Ntahondi kwa kipindi chote hicho na Tuliitumia ipasavyo nafasi hii kila siku kujipanga kisawa sawa juu ya kuutekeleza mpango wetu wa kutoroka, Kila mara tulijikumbusha mipango hiyo tukihisi hiyo ndiyo njia pekee ya kutuokoa mule ndani. ilikua ni kitu kigeni kwa Mtoto wa kiume kulala chumba kimoja na mtoto wa kike, tena mtoto mweyewe ameumbika kisawa sawa Bila ya kupata hisia za mihemko ya kimapenzi Lakini kwetu haikua hivyo kila mtu alikua busy akiumiza kichwa namna ya kujiokoa ukizingatia siku za Jamaa kurudi zilikua zimekaribia..

Siku tano zilitimu tangu Njemba ile iende mjini kuonana na PABLO MWAKI Hivyo tukawa tayari tukijua siku hiyo ilikua ndo siku tuliyokua tukisubiri, Ntahondi alijitahidi kujiweka katika hali ya Urembo ili kuzidi kumchanganya jamaa atakaporejea japokua hakua katika kiwango kile cha IFM Kutokana na hali ya mazingira.. Tuliendelea kumsubiri yule Baunsa bila mafanikio ya kumuona mpaka usiku ukaingia Tukaingia kulala tukiwa na kiu ya kuutekeleza mpango wetu, Tulilala mpaka asubuhi mapema sana tuliposhtushwa na Sauti za watu wakicheka kwa shangwe nje ya Mjengo ule uliojaa kila hali ya kutisha na kuogofya, nilipojaribu kusikiliza ili nijue kua zilikua ni cheko za nini hasa niliisikia Sauti ya Baunsa aliekua mjini kwa siku sita sasa na bila shaka alikua akipokelewa na vijana wake baada ya kuingia akitokea mjini, nikainuka pole pole na kwenda mpaka katika kitanda cha Ntahondi, nikamuamsha na kumpa taarifa za ujio wa Jamaa ili awe tayari kukabiliana nae, kisha nikarudi kitandani kwangu na kujifunika shuka halafu nikatulia kama vile niko katika usingizi mzito..

Hazikupita hata dakika tano nikasikia mlango wa Chumbani kwetu ukifunguliwa, niliendelea kujifanya nimelala, kisha nikamsikia Baunsa akimuamsha Ntahondi na kumsalimia

"Hujambo binti? una lala mpaka saa hizi?"

"Sijambo, nilikua nimeshaamka ila usingizi ukanipitia tena"

"Vipi hakuna mtu yeyete aliekusumbueni tangu nilipoondoka?"

"hakuna alietusumbua, nashukuru"

"Usiogope sema kama mlipata tabu yoyote, hawa ni vijana walio chini yangu hawapaswi kukiuka maagizo yoyote nayotoa mimi" Jamaa aliendelea kujizolea masifa lukuki kutoka kwa Ntanhondi, wakati huo mie bado nimejifunika shuka yangu halafu nimetulia tuli, Ntahondi aliendelea kukataa kwa sauti ya laini na mahaba kiasi kwamba hata mimi sasa nilianza kupata 'vibration', baada ya mazungumzo hayo mafupi jamaa akuambia Ntahondi amfuate, Binti akainuka wakaanza kutoka nje, nikamsikia jamaa akiuliza

"Huyu ----- nae kalala tu kama yuko kwa baba yake humu" akimaanisha mimi

Sikujua wamekwenda wapi, ikanibidi na mimi niamke niwe tayari kwa lolote nilikaa kama dakika Ishirini bila kupata hata dalili ya kinachoendelea huko kisha kwa mbali nikasikia sauti za nyayo za miguu zikija usawa wa chumbani kwetu, nikajiegesha ukutani nikijifanya kama ndo nimetoka kuamka, nikasikia mlango ukifunguliwa na Ntahondi akaingia, mkoni ameshika sahani yenye Mkate uliopakwa Blueband na jam na mkono mwingine amebeba kikombe kikubwa cha chai ya maziwa, akanisogelea huku akiwa na tabasamu na kunikabidhi kifungua kinywa hicho, nikakipokea na kisha nikamuuliza

"Imekuaje huko?"

"Jamaa kanipeleka hadi chumbani kwake anakolala, akanipa chai ninywe, wakati nakunywa akaanza kuniuliza kama nimeafiki suala lake, na mie kwa mapozi nikamkubalia, kweli kuna wanaume wanatamaa ya Ngono Eti ndani ya Dakika tano tu nimeishaitwa majina yote mazuri mara baby, mara sweat, mara dia Hivyo tumekubaliana kua Leo jioni wake wataondoka na kwenda mitaa ya mbele huko kuna 'center' ya kijiji hivyo atabaki yeye tu kama mlinzi kwahiyo nitaenda kulala nae Chumbani kwake" baada ya maelezo hayo tukaanza sasa kuboresha mipango yetu upya ya namna ya kufanya mashambulizi na kisha kutokomea,

Kilichozidi kunifariji ni maneno ya kijasiri na kishujaa ambayo ki ukweli sikutegea kuyasikia yakitoka kinywani mwa mtoto wa kike tena mdogo kama huyu,

"Huu ni mpambano wa kuokoa roho zetu ikibidi hata kwa kutoa roho ya yeyote atakaekua mbele yetu hivyo inabidi tuwe makini, tuna aslimia 99 ya kufanikiwa kutoroka mpaka sasa ila pia tuna asilimia moja tu ya kushindwa kutekeleza mpango huu hivyo tusiiruhusu asilimia hii ikazizidi asilimia 99" Ntahondi alikua akiongea kwa maneno makali huku akionesha kujiamni, kisha akaendelea kua

"Nilipoingia chumbani kwake nimemuona akiwa na bunduki mbili, moja kubwa akiwa kaining'iniza juu ya kiti kilichopo karibu na kitanda, nyingine ni Ndogo(Pistol) alikua kaining'iniza usawa wa kiuononi kwenye suruali yake hivyo nikiwa nae chumbani we uwe tayari tayari, kwaku huyu Shetani anaonesha ni mtu wa tamaa ya mapenzi me nitamlaghai mpaka nihakikishe amelainika kama mgonjwa wa degedege, ukisikia tu nakohoa kwa sauti kubwa ujue picha iko tayari hapo hapo usichelewe uje fasta mlango sitaufunga nitauegesha tu hivyo ukifika we unaingia moja kwa moja" nilikua nikimsikiliza kwa makini mdada huyu akiwa hana hata chembe ya woga usoni mwake, nikamuuliza

"Sasa vipi kwa bahati mbaya nikishaingia halafu hizo bunduki nisizione?"

"Mimi kwakua nitakua humo humo chumbani nikau namuangalia anavyoweka kila kitu hivyo kama asipoweka maeneo hayo nilipoziona mwanzo nitaona ameweka wapi hivyo nitakupa Ishara ya haraka mahali zilipo halafu wewe utaenda moja kwa moja kuchukua, na ukishaichukua usichelewe kumfyatua" Tulipanga kila kitu mpaka mwisho tukawa tumekaa tu tunasisitizana kua makini..

Hatimae jioni ikafika, ilikua ni majira ya saa moja magharibi, hali ilikua tulivu kabisa na giza lilikua limeanza kutinga kwa kasi bila shaka ni kutokana mazingira msituni kule.. Tukiwa chumbani mimi na Ntahondi tuliwaona wale vijana wawili wakitokomea kwa mbali kupitia matundu ya dirisha wakitokomea Hivyo tukawa tayari kukabiliana na Ibilisi huyu altakaebakia peke yake, Tuliendelea kukaa mule ndani kwa muda mrefu tu mpaka ilipotimu majira ya kama saa tatu usiku tukasikia mlango wa chumbani kwetu ukifunguliwa kisha akaaingi kijana mmoja akiwa na Bunduki yake mkononi kisha akamwimbi Ntohondi "Boss anakuita chumbani kwake"

"Ok nakuja" alijibu Ntahondi kisha kijana yule akatoka nje ya chumba kile, ile hali ilitushtua sana maana tuliamini kua hakukua na mtu mwingine yeyote ndani ya mjengo ule Lakini sasa dalili sio nzuri kumbe kuna huyu kijana alieonekana ni Mlinzi pia, Ntahondi akasimama huku akiwa na mfadhaiko usoni, nikampa moyo na kumwambia

"Nenda, fanya kama tulivyokubaliana, kuhusu huyu kijana ondoa Shaka tutajua namna ya kumkabili ila mipango yote ni kama tulivyopanga" Ntahondi alitikisa kichwa kuashiria ameafiki Kisha akatoka na kwenda chumbani kwa Baunsa..

Kadri muda ulivyozidi kwenda niliendelea kupata nguvu ya kupambana, japo kibinaadamu mapigo ya moyo hayakuacha kwenda kasi, jasho jembamba liliendelea kunitiririka mwilini, kilichozidi kunitia hofu ni hali ile ya ukimya sikusikia Sauti ya Ntahondi akikohoa kama tulivyokubaliana na sasa imeshakua takribani saa moja tangu aende kule chumbani kwa Baunsa yule, nilipojaribu kucungulia nje usawa wa getini japo ilikua ni mbali na chumba hiki nilimuona yule kijana mlinzi akiwa amekaa kwenye kiti kama vile mtu aliepitiwa na usingizi, nikataka kutoka na kwenda chumbani aliko Ntahondi lakini kengere ya hatari ikalia kichwani mwangu nikakumbuka jinsi Ntahondi alivyonisisitiza kua nisiende mpaka nikimsikia anakoho kwa nguvu, ikanibidi Nishushe pumzi kisha nirudi mpaka kitandani na kujitupia..

Baada ya kama nusu saa tena nikiwa nimejilaza pale kitandani nikamsikia Ntahondi akikohoa kwa sauti kubwa kama vile mtu aliepaliwa na machicha ya nazi hapo hapo nikasimama haraka, nikaenda mpaka dirishani tena na kumchungulia yule Mlinzi kule Getini nae alikua maekaa vile vile, nikaufungua mlabgo wa chumba taratibu kisha nikatoka haraka nikiwa na kisu mkononi, kisu hiki ilikikuta pale kwenye korido juu ya pipa kubwa la maji, nikaenda mpaka kwenye chumba cha nne kutoka kile chetu, hapo ndipo walipokua Ntahondi na Huyu haramia, nilipofika mlango tu nikajaribu kuusukuma mlango wa chumbani LAA HAULA Mlango ulikua umefungwa kwa ndani, nikazidi kupata hofu nisijue la kufanya, lakini nikiwa bado sijajua nifanye nini nikamsikia Ntahondi akimwambia yule jamaa ampele msalani akajisaidie, nikashusha pumzi kisha nikarudi fasta mpaka chumbani kwetu halafu nikwa nachungulia kwa jicho moja kupitia kwenye pazia nyepesi aliyokua mlangoni..

Baada ya dakika mbili hivi nikwaona wakitoka chumbani wakielekea upande wa pili wa korido ile ndefu ambako ndiko kuna vyoo, jamaa huyo akiwa maevaa bukta huku akiwa kidali wazi, na Ramla akiwa amejifunga khanga. walipokatiza tu kuingia Maliwatoni mimi nikatumia mwanya huo haraka nikaenda mpaka pale mlangoni walipotoka nikaingia mule chumbani, nikakuta chumba cha kawaida tu, kukiwa na mwanga hafifu wa taa za kichina, haraka hara nikaanza kupepesa macho huku na kule nikitafuta silaha, 'HAMAD' Nikaiona Bunduki ikiwa pale pale kwenye kiti kilichopo mbele ya kitanda, nikaiacha na kwenda mbele tena kwenye suruali yake ya jinzi aliyokua kaitundika kwenye msumari ukutani, nilipoigeuza upande wa pili nikaiona Pistol yake nikachukua haraka kisha nikaenda mpaka pale kitandani halafu nikaingia chini ya kitanda(uvunguni) kitendo cha kama sekunde kadhaa nikwasikia wanaingia ndani..

"Funga mlango hua vizuri, unatakiwa kua makini usipende kulala bila ya kufunga mlango" ni sauti ya Baunsa akimwambia Ntahondo, nikiwa chini ya uvungu wa kitanda niliona miguu ya huyo Baunsa akienda mpaka usawa wa kiti na kuishika Bunduki yake, nikawa naomba dua zangu zote ili asiende kule alikotundika suruali yake maana angekuta hakuna Pisto yake haipo ingeanza mtanange, baada Ntahondi kutoka usawa wa malangoni karudi mpaka pale kitandani akapanda kisha akakohoa tena kwa nguvu nadhani hakujua kama tayari nipo ndani hivyo ilikua ni ishara tena ya kuniita, nikaendelea kutilia tuli, nikaiona sasa miguu ya huyu Baunsa akija mpaka kitandani nae akapanda kitandani kisha baada ya mazungumzo yao ya hapa na pale nikasikia sasa sauti za mahaba hasa hasa kutoka kwa kidume huyu hapo hapo nikaanza kutambaa taratibu kwa Tumbo mpaka mwisho kitanda wakati huo nikiwa tayari nimeshaikoki Pistol yangu kidole cha shahada kikiwa 'attention' kwenye 'trigger' kwa ajili ya kufyatua risasi muda wowote..


culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata binti kiziwi Nicas Mteikorino Sukulaaniceth mzahulaKhantwe kelcie chwechinyong ram tabibumtaratibu Magembeh Emmanuel Thadei
 
RIWAYA: SIKU YA GRADUATION
MTUNZI: MAUNDU MWINGIZI

SEHEMU YA SITA

Mwanga wa chumbani ulikua ni hafifu mno hivyo ilikua ni hali nzuri kwangu kuzidi kujiamini, sasa nikatambaa mpaka mbele ya kitanda kasha nikasimama ghafla. niliposimama tu jamaa akshtuka nae akaruka kutoka kitandani na kunirukia, me nikamkwepa hapo hapo mapambano yakaanza nikafyatua Risasi moja lakini ikamkosa jamaa alikua ni mwepesi wa viungo kuliko hata nilivyotegemea, akaenda upande wa nyuma wa kitanda nikapiga risasi ya pili nayo ikamkosa, hapo sasa hali ya tafrani ilizidi kupamba chumbani mule, nilikua naogopa kufyatua Risasi hovyo nikihofia kumdhuru Ntahondi ambae nae alikua kitndani hapo, niikaanza kuhaha sasa maana nilijua ndani ya pisto ile hapakua na Risasi zaidi ya tano ghafla nikasikia mlango wa chumbani umepigwa kwa nguvu na jamaa mwingine akaingia nilipogeuka kumuangalia ni nani hiyo ndo ilikua mistake ya kwanza Baunsa yule alinirukia na kunipiga ngumi ya kichwa nikaenda mpaka chini, pistol ikaniponyoka ikarukia kitandani.. nikaanza kazi ya mchezo wa ngumi na watu wawili sasa lakini kutokana na ile hali Mwanga mule ndani ikanisaidia kidogo maana baunsa alikua anpiga hovyo mpaka anampiga mlinzi wake..

Mpambano ulichukua takribani dakika sita ndipo nilipohamia upande wa pili karibu na kitanda na haraka Ntahondi akanipa tena ile Pistol nilipoishika tu nikamuelekezea yule Mlinzi

"Weka Silaha chini!!!" niliongea kwa ukali, wakati huo Ntahondi analia akiwa amesimama upande wa kiti kile chenye Bunduki, Mlinzi akawa bado ameshikilia vema Bunduki yake basi hapo hapo sikumkawiza nikamdungua Risasi ya karibu ya kifuani upande wa bega la kulia akaanguka chini huku akipiga kele kali za maumivu, nilipogeuka kwa Baunsa huyu nikamfyatulia Risasi Loo salaleee Risasi zilikua zimekwisha na jamaa akaligundua hilo sasa ikawa kizaa zaa mule ndani wote macho yetu yako kwenye Bunduki ya huyu Mlinzi sasa...

Ngumi zikaanza tena kwa kasi ya ajabu, kiukweli jamaa alikua akinizidia nguvu sana tu tatizo alikua kahamaki hivyo nikawa naitumia hiyo fursa kumpa mapigo ya kumshtukiza, nikiwa nagalagazana nae pale sakafuni wakati huo huyu mlinzi analia kwa maumivu makali ya Risasi, baunsa hyu akanizidia nguvu na kuniweka chini kisha akaanza kunipa makonde ya kichwa mpaka nikataka kupoteza fahamu, hapo hapo Ntahondi akaja kwa kasi ya ajabu akiwa amenyanyua kiti kidogo cha chuma na kupiga nach yule jamaa kichwani jamaa alitoa sauti moja tu kali na kisha akaenda mpaka chini akapoteza fahamu

Nikanyanyuka haraka na kujifuta damu zilizokua zikinitoka puani na upande wa kisogoni nilikua nimepasakua baada kuanguka pale chini, hara haraka tukachukua Bunduki zote mbili ile ya Mlinzi na ile ya huyu baunsa iliyokua kwenye kiti kisha tukatoka haraka mule ndani, tukaenda mpaka Getini hapakua na mtu mwingine tukafungua Geti kisha tukatoka nje kabisa na kuanza kukimbia hovyo kama kuku aliekatwa kichwa, maana hatukujua tuko wapi na tunaenda wapi, hatukujua ni mkoa gani ule wala ni wilaya gani ukizingatia na giza nene lililokutanda Msitu ule ni hatari lakini hatukukata tamaa tukaendelea kukimbia kwa kwenda mbele tu..

Tulikimbia kwa umbali mrefu tukiwa peku, majani magumu almaarufu kama Magugu yalitupasuapasua miguu, ikafika mahali Ntahondi akawa analia huku akilalama kua pumzi zimemuishia hivyo hawezi kukimbia tena, akagoma kukimbi akilalamika amechoka sana, pia miguuni alikua akivuja damu zilizotakona na kuchomwa na visiki vikavu vya miti mule Msituni na mbaya zaidi hakukua na dalili hata ya Nyumba moja licha ya umbali tuliokimbia karibu kilometa tano,Nilijaribu kumbembeleza ajikaze tuendelee na safari lakini ilishindikana Binti alikua hajiwezi ikanibidi sasa nimbebe mgongoni na safari ikaendelea japo nami nilikua hoi bin taabani ila nilijikaza tu..

Tulizidi kutembea umbali mrefu japo ilikua ni shida lakini tulijikaza, mara kwa mara tulikua tukipumzika njiani kisha tukiendelea na safari ndefu isiyojulika tuendako, baada ya Ntahondi kupata tena nguvu tukaanza tena kukimbia kuelekea hovyo hovyo tu mpaka hatimea kwa mbali tukaanza kuona kama dalili ya makazi ya watu, tulipozidi kusogea tuliona majaruba yaliyolimwa mahindi na vitu kama karanga vile hatukuweza kuona vizuri kutokana na giza totoro lililotawala maeneo yale, tulipokaribia tukaanza kuona nyumba zilizoezekwa kwa nyasi, hii ilikua ni ishara sasa kua japo tumefika kwenye makazi ya watu ila hapaku mjini kabisa, hatukujali sie tulichokua tukikililia ni ni msaada tu kutoka kwa Raia wema, tulipofika maeneo yale palikua kimya sana bila shaka watu walikua wamelala, kwa kukadiria ilikua ni mida ya saa tisa za usiku, tulijaribu kujadiliana kama tuwagongee wenyeji kisha wakitufungulia ndo tujieleze kwao na kuomba msaada lakini hatukufanya hivyo tukihofia kua wasingweza kumfungulia mtu wasiemjua na ingeleta madhara kwetu kama tungepigiwa kelele za wizi..

Tukaenda mpaka kwenye nyumba nyingeine ambayo ilikuahaina milango tukaingia mule ndani, ilikua ni kama sehemu wanayoitumia kwa kupikia, kulikua na majiko ya kienyeji, pia kulikua na viroba kama vitano hivi vyenye mabunzi ya mahindi, tukaamua kua tulale mule mpaka asubuhi kisha wenye wakija tutawaeleza tatizo letu, Naam tukaribu kulala lakini usingizi haukupita kabisa pengine kutokana na woga tuliokua nao, ikichagizwa na mbu wengi waliotusshambulia mule jikoni, baada kama ya nusu saa tulisikia mlio wa piki piki zikija kwa kasi tukaamka na kusikiliza milio ile ikua ikielekea wapi na baada ya dakika kadhaa tulikubaliana wote kua ni pikipiki za zilikua zikija kule tulipo, tukasimama haraka nikamshauri Ntahondi kua tuingie ndani ya mifuko ile yenye mabunzi ya mahindi ili tujifiche kama hatari ile itaku ni yetu..

Naam nikampakia Ntahondi katika kiroba kimoja kisha nikakiegesha vizuri ukutani kisha nikamsisitiza atulie, nami nikafanya hivyo hivyo kwenye kiroba kingine kilichokua nyuma ya jiko la kupikia, baada ya dakika kama tano sauti zile za pikpiki zilizidi kuja maeneo yale na kisha zikasimama maeneo yale ya kijiji kisha nikasikia Sauti za watu wakiongea kwa kufokezana, sikujua ni kina nanii?! baada ya Muda niliisikia Sauti ya yule Baunsa aliekua amezimia kule Mjengoni akimgongea mwenye nyumba

"Mjumbe Fungua haraka kabla sijakichoma moto hiki kibanda chako" hofu sasa ikazidi kutanda moyoni mwangu, nilijilaumu sana kwa kumuacha bila ya kummalizia Yule Baunsa, baada ya muda nikawa naona mwanga wa tochi ukimulika nje na baada ya mazungumzo marefu ya huyo mjumbe kisha wakaanza kuongoza wakija kule jikoni

"Kuna majambazi watatu mmoja mwanamke wamekuja kutuvamia kule kwenye godauni letu la nafaka wamemuua mlinzi na mimi wamenijeruhi sana, tazama damu zote hizi, kama mmewahifadhi naomba muwataje Laa sivyo mtajuta" Ilikua ni sauti ya yule Baunsa, kisha wakaja mpaka kule Jikoni

"Hii mifuko a nini?" aliuliza baunsa

"Ni mabunzi ya mahindi hua tukipukuchua mahindi ndo tuyaweka humo"

"Zungu hebu pekua pekua humo kwenye hiyo mifuko kama hakuna kitu twende na huko wanakolala"

mwanga mkali wa tochi uliendelea kumulika ndani chumba hiki cha wazi, kasha nikasikia mlio wa mifuko ile ya Sandarusi, nikaanza kulia kwa moyoni sasa nikijua tunakamatwa tena..
 
Dah iko poa sana
Mungu awasaidie wapone coz wakikamatwa wameisha ila hawata kamatwa. Mmh angejua angemmalizia ya kichwa
 
Mwenyeezi mungu atawafanyien wepesi na hawatakuwa na nguvu za kupekua hiyo mifuko na hamtskamatwa
 
[FONT=Helvetica, serif]RIWAYA:SIKU YA GRADUATION[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]MTUNZI:MAUNDU MWINGIZI[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]SEHEMUYA SABA
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Niliendeleakutetemeka kwa hofu, nilijuta hata kwanini tulikimbia bila yakuhakikisha tumem 'shoot' huyu Baunsa japo jibu nilikua nalo kwambailikua ni ha[/FONT][FONT=Helvetica, serif]makitu.. Baunsa aliendelea kuongea kwa sauti ya Ukali huku nikiisikiaSauti yake ikija usawa wangu nilizidi kuingiwa nahofu Lakininilijikaza kisabuni, "Majambazi wanatoka mjini huko wanakujakuua watu halafu wanakimbilia huku mnawaficha, dawa yenu iko jikoni"aliendelea kutoa tambo zake Baunsa huyu, nikawa sasa nasikia sautikama vile jamaa anaviangusha chini vile viroba vya mbele kule kwakuvipiga na mateke huku mwanga wa tochi ukizidi kuja usawawangu...[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Baadaya kusikia sasa nyayo zao zikija upande niliokua nimejificha miminilianza kuomba dua za kila aina ili Mungu mkuu atetende muujiza wakenaimani dua yangu ilipokelewa kwani baada ya dakika chache nilimsikiaBaunsa akimwambia huyo mjumbe kua waende wakakague na kule vyumbanimwao wanakolala, kisha wakatoka nje na hali ile ya Giza ikarejea,nilishusha tena Pumzi kwa kasi nikamshukuru Mungu japokua hali ilikuabado ni tete, nilikua nikimfikiria Ntahondi hali aliyokua nayo mulekwenye Kiroba alichojikunja kama mnyoo wa Amoeba.[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Sikujuahuko walikoenda walienda kumkagua nani! au kama waliwakaguawanakijiji wote kwa kua hawakua wengi sana pia sikujua, tuliendeleakutulia mule kwenye viroba vya mabunzi ya mahindi mpaka baadae kabisatukasikia sauti za pikipiki zikiondoka tena kwa kasi, baada ya dakikakama 20 nikatoka ndani ya kiroba kisha nikaenda kumtoa na Ntahondi,tukajifuta vumbi lililokua kwenye viroba vile ambalo kwa kiasikikubwa lilikua tayari limeganda mwilini kutokana na damu zilizokuazikituvuja. baada ya hapo sasa tukaanza kujadili tutajiokoa vipikutoka pale tulipo maana sasa Wanakijiji wameshaambiwa kua sisi niMajambazi na tulikua na Bunduki moja ambayo nayo tumeificha nyuma yajiko na ile Bunduki nyingine bila shaka tuliiangusha njiani wakatitunakuja huku na nadhani itakua waliiona ndomaana wakaamuakutufuatilia maeneo ya kule, tukafikia muafaka wa kusubiri kwanzakupambazuke ili asubuhi tujitokeze tuwaeleze ukweli tu hawa wazee wakijiji pengine watatuelewa, japo swali kubwa tulilobaki nalo itakuajeendapo watashindwa kutuelewa na kutuchukulia kua nimajambazi!!?[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Tuliendeleakukaa mule jikoni muda mrefu tu kisha baada ya muda hali ikaanzakubadilika na kua ang'avu ikiwa ni ishara tosha kulikua kunaanzakupambavuka, nilipochungulia nje kulikua na wazee wawili wakionekanakujadili vitu kwa umakini mkubwa, nikamwambia Ntahondi kua acha miminiwawahi hawa wazee nikajaribu kujieleza kabla hapajakucha nahawajajua lolote, Ntahondi alionekana sasa kua hana imani tena nahawa wana kijiji kwakua wanaonesha wameshaingiwa na hofu ya mikwaraya Baunsa na wenzie Lakini ikawa haina budi ikabidi tu nijikaze kishaniwafuate, ila nikamuambia Ntahondi yeye atulie tu pale pale aisijekwanza. Nikatoka mule ndani nikiwa hoi kwa mchoko nikaanza kuwaelekeawaliko wazee wale wawili mmoja akiwa ni ktu kirefu mkononi kama vileJambia, mwingine akiwa amevaa 'Rubega' yaani kajifunga shuka upandemmoa wa Bega lake la kulia, wazee wale waliposikia sauti za nyayozangu wote waligeuka wakaangali upande ule ninaotokea mimi hukunikichechema kwa maumivu, Mzee mmoja akanisemesha kilugha ambachosikukielewa ikanibidi tu mie niwanyooshe mikono yangu miwilikuashiria amani..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Usiku..??"mzee mmoja alitamka neno hilo ambalo nililielewa vema, Mara nyingiukikutana na mtu mida ya usiku unamuuliza 'usiku' akikujibu 'mchana'ujue anamaana ya Amani na akikujibu tofauti inaashiria ni hatari,hivyo hima nikamjibu[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Mchana!!",wazee wale wakawa wamejiweka tayari kunikabili, nilipofikawakanistopisha kwa mbali kisha wakanihoji kwa lugha ambayo sikuielewakabisa, nikawajibu kua "Siijua lugha hiyo", yule Mzeealiejifunika shuka akanihoji[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Weni nani na unatokea wapi saa hizi?"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"NaitwaNaufal, nina matatizo makubwa wazee wangu naomba mnisikilize"wote wakawa makini kunisikiliza[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Miminiko na mwenzangu tulikua tumetekwa na majambazi karibu mwezi mzimasasa na wametutesa sana na hatimae usiku wa kuamkia leo tukapambananao kisha tukawatoroka na kukimbilia huku.." kabla sijamalizakuongea yule mzee mwingine akaniwahi[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Anhaakumbe nyie ndo mliovamia kule Godown la nafaka mkataka kuiba halafummeua mtu huko mkakimbila huku kuja kutuletea matatizo"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Hapanawazee sisi sio wizi sisi ni raia wema tunatoka Dar Es Salaamtulitekwa na hata hapa sipajui ni wapi"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Mwenzioyuko wapi?"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Yukohumo ndani" nikawasontea kwa kidole kwenye lile jiko tulikokuatumejificha..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Wakatitunaendelea na mahojiano mzee aliejifunga shuka akaondoka hadi upandewetu wa kulia ambako kuna nyumba zao ndogo ndogo za kuishi kishanikamsikia akiwaita watu kwa majina na baada ya muda mfupi akarudi navijana kama sita hivi na wao wawili wakawa jumla wanane, walipofikawale viajana hawakutaka kutusikiliza kabisa zaidi ya shutuma tu juuyetu[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Hawani wezi tu wanatoka huko mjini kuja kufanya uhalifu huku, wafungenikamba tuwapeleke huko Godown walikua vunja" kijana mmoja alisemahuku akionesha kuungwa mkono na wenzie, Mwingine akakataa nakusema[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Tusipotezemuda wa kuhangaika na hawa watu tuwachome moto tu kisha tutawafukiahuko kwenye shamba la mahindi" nae alipata wenzie walio msapotikwa rai yake hiyo, sasa hapo ndo nilizidi kuchanganyikiwa wana kijijiwaligoma kabisa kunisikiliza, Mara kijana mmoja akanisogelea nakunipiga sasa makofi huku akinitaka nikae chini, nikaa chini harakakisha kijana yule aliongea kitu kwa lugha yao nisioifahamu Lakininilielewa kua anamuulizia huyo mwenzangu nae alipo maana baada yaswali lake hilo alielekezwa na Mzee yule aliewafuata kuwaamsha kuayupo mule jikoni..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Kijanayule akaenda haraka na kisha akatoka akiwa ameshika Ntahondi hukuakimvuta kwa kasi, alipomfikisha pale nae wakamshambulia kwa kichapocha makofi kisha wakamkalisha chini pale karibu yangu, tukawa sasakama wizi kweli tuliokamatwa. wakati huo hawa wanakijiji wakibishanajuu ya nini cha kufanya kufuatia rai zilizotolewa moja ni kutuchomamoto na nyingine kuturudisha kule Godown kwa wale maharamia wa PABLOMWAKI, Nilikua nikilia huku nikijaribu kujieleza lakini hawakunielewakabisa wazee hawa pamoja na vijana wao wakati wanaendelea kubishanakwa fujo kuna kijana mmoja ye akaja na kamba ngumu za katani kishaakaanza kutufunga mikono kwa nyuma ya mgongo na miguu, Ntahondialikua nae akilia kwa uchungu..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Baadaya majadiliano ya muda mrefu akaja Mzee mmoja mwenye mvi nyingikichwani, wote wakaanza kumsalia kwa hesha sana inaonekana ni mzeemwenye cheo fulani pale kijijini,[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"ShikamooMzee Ngozi" aliamkiwa na kila kijana pale kisha wakaanzakumfahamisha hali ilivyo pale[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Hawa ndo wale majambazi walioenda kuvamia na kuua kule Godown, sasatunafikiri tu kuwapeleka kule kule" yule mzee akamuangalia sanammoja wa wale vijana aliekua akimpa maelezo kisha akamuuliza kwaukali[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Hivimna akili Timamu nyini?, mna uhakika gani kama hawa ni majambazi?mmewasikiliza mkathibitisha? mnakijua walichokiiba? na hata kama nikweli ni majambazi Je huko mnakotaka kuwapeleka ni Polisi? nawakipatwa na mabalaa huko hata kuuawa hamuoni na ninyi mmeshiri?"Yaani nilitamani nimbebe huyu mzee, kundi zima likawa kimya, yuleMzee aliekua kajifunika shuka alijaribu kumuelewesha mzee mwenziehuyu lakini alizidi kuwapinga kwa hoja za msingi kutokana na kilawalichomueleza, wakafikia muafaka kua wapige simu polisi ili watuijieaskari pale na si kutuchoma moto wala kutupeleka kule Msituni ambakosasa nilianza kuelewa kua walio wengi wanaamini kua lile jengo nighala la kuhifadhia nafaka..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Simuyangu mimi haina charge karibu wiki sasa, nendeni hapo kwa Mzee Banzimkamwambie namuita hapa aje na simu yake" alitoa agizo huyuambae alikua ni kama Mkombozi wa maisha yetu kwa sasa, kishaakaendelea kutoa Amri[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Wafunguenina hizi kamba, mbona hamna huruma ninyi?! angalia huyo binti mpakamikono imeanza kuvimba jinsi mlivyomfunga kamba, na nyinyi wazeewenzangu manakosa hekma kiasi hiki?" vijana hawa walikua wakitiikila amri iliyotolewa na mzee huyu inaonekana alikua akiheshimiwasana Wakati wanatufungu kamba yule kijana alietumwa nae akawamaeshawasili akiwa na Mzee mwingine wa makamu bila shaka ndie MzeeBanzi huyo, alipofika tu mzee huyu nae akasimuliwa kila kitu kishanae kaanza kuzungumza kwa ukali[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Hilisuala limeanza kunishtua sasa unajua kwa maelezo ya hawa vijana kunakitu kinazunguka kichwani" aliakua akiongea huku akimtazama MzeeNgozi[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Unajuajuzi alikuja mwanangu kutoka mjini japo hakukaa sana ila katikamazungumzo akaniambia kua huko mjini kuna kijana ameuawa, halafu kunawengine wawili wamepotea katika mazingira ya kutatanisha naakanitajia mpaka jina la huyo Binti alietekwa sema tu nimelisahau,sasa isije ikawa ni kweli ndo hawa halafu ninyi mnataka kuwapelekahuko huko wanaposeama ndiko walikokua wametekwa" kauli hiiliwashtua wote pale, wakaangaliana kwa hofu sasa kisha Mzee Jongaaliekua akitikisa kichwa kuashiria kua anamuunga mkono mzee mwenziealiekua akiendelea kuongea[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Ngojatumpigie simu Mwanagu atutajie jina la huyo binti alitekwa kishatutajua tu na hata kama sio huyu pia tutamtuma haraka aende kituo chapolisi akatoe taarifa kisha aje nao hao polisi mpaka hapa wawachukueili haki ikatendeke huko huko mini" akamaliza kuongea Mzee huyukisha akatoa simu na kumpigia huyo mwane...[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Hallow,hebu nipigie haraka Baba simu yangu haina salio" aliongea MzeeBanzi baada ya kuitoa simu yake katika mfuko wa Kanzu yakeiliyochakaa, wakati tunasubiri huyo mwanae apige simu, huyu MzeeNgozi akawahi kumuuliza Ntahondi[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Unaitwanani Binti?" nilijua lengo lilikua ili ajue kama atakua ndieyeye ili afananishe majibu watakayopewa na huyu mtoto wao ambe badohatujamjua ni nani na Je ana tujua sisi au Laa,[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"NaitwaNtahondi", hapo hapo simu ikaita tena akapokea huyu Mzee,

Ngekewa ram angelca chacha patrick showtie amina mabata mlyn[/FONT]
 
Last edited by a moderator:
[FONT=Helvetica, serif]RIWAYA:SIKU YA GRADUATION[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]MTUNZI:MAUNDU MWINGIZI[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]SEHEMUNANE
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"eehhhujambo?..."[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"SijamboShikamoo mzee.."
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Marhaba"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Kunanini Baba mbona asubuhi asubuhi, kuna usalama kweli?"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Usalaupo, Hebu kwanza niambie yule Binti alietekwa huko mjini anaitwa nanivile?!" wote tulikua tumetega masikio kwenye simu ya Nokia yaTochi na kwakua Mzee huyu alikua ameeweka Loud Speaker hivyotuliyanasa mazungumzo yao kisawa sawa..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"AnaitwaNtahondi, kwani kuna nini Baba?" watu wote tukaangaliana usoni,Mzee Ngozi alimuangalia yule kijana aliekua anampa maelekezo kuawanataka kuturejesha kule Godown, tena alikua akimuangali kwa jicholilionesha kumsuta kwa upuuzi waliokua wakitaka kuufanya,Wakati huoMzee Banzi alikua akiendelea kuongea na simu na mwanae alieko Darjapo hatukumjua ni nani![/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Sasasikia huyo Ntahondi tuko nae hapa kijijini, ameumizwa sana na yuko nakijana mwingine hivi nae kaumizwa sana maeneo ya kichwani, sasa fanyahima kachukue Polisi uje nao huku kijijini haraka"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Babambona kama sikuelewi? una uhakika ni Ntahondi? na weumemjuaje?"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Sasahutaki? hebu ongea nae huyu hapa" Mzee Banzi kampa simu Ntahondiili aongee na huyo mwanae, nilitamani niidake mie ile simu ilinijaribu kutumia akli nimshawishi huyo kijana asiende Polisi nabadala yake nijaribu kumpa utaratibu wa kuwapata ndugu zetu kwanzamaana nilikua najua kua PABLO MWAKI ana nguvu sana ya pesa hivyoatakua kaishawanunu askari wengi tu wanaoweza kutugeuka na kutupotezakabisa ili kuficha ushahidi,[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Hallow.."aliongea Ntahondi sasa[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"EeehWe Ntahondi?"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Ndiowe ni nani?"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Mieni Oscar mlinzi hapa chuoni kwenu IFM, Pole sana na matatizo,imekuaje sasa?"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Ahsantenimekufahamu, hatuwezi kuongea mengi kwa sasa ila tuko hapa kijijinikwenu tumefika baada ya kuwatoroka wale waliotuteka, naomba umfuateharaka Mwl Honde umpe hii habari kisha umpe utupigie simu tumpemaelekezo ya kwenda Polisi kutoa taarifa" hapo hapo simu ikakatanilifarijika kidogo sasa kwa kua Ntahondi nae katumi mbinu nilioitakamimi maana nae alijua tu wakitoa taarifa ya kawaida tu kituoni huendawakazipata Askari wapambe wa MWAKI halafu itakua blaa jipyakwetu[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Baadaya simu kukatika wazee wale wakatuambia tuinuke pale chini tulipokuatumekalishwa kisha wakaanza kujadili kwa hofu kubwa juu ya hilitukio, Mzee Ngozi alizidi kuonekana na hekma sana mbele ya hawa wanakijiji wenzie, baada ya hapo wakatuchukua mpaka katika nyumbailiyokua mbele kidogo ya kichuguu kikubwa kiliconekana mpaka kuizidiurefu nyumba, tulipokua mule ndani tulijaribu kuwasimulia japo kwamukhtasar tu mkasa huu uliotukumba, wazee wale walionesha kukunwasana na stori hii. wakati tukiendelea kujadiliana ghafla simu ya MzeeBanzi ikaita tena.. akapokea[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Hallow.."[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Eehbaba, sasa tunakuja huko muda si mrefu ila msimuambie mtu yeyote hiihabari kwani nasikia huyo alie wateka ana pesa na anajuana askariwengi sana hivyo isije ikwaletea tabu hapo"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Hakunamtu ajuaje zaidi yetu sisi na wewe huko mjini"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Hayahebu mpe simu huyo dada.." Mzee akamsogelea Ntahondi na kumpasimu[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"HallowNtahondi are you oky?" ilikua ni Sauti ya Mwl Honde sasa.maskini Ntahondi akashindwa kujikaza na kuanza kulia[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"NOUsilie sasa, tuko njiani tunakuja huko, uko na nani?"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Nikona Naufal"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Wewe!!!?..are you sure?" Inaonesha Mwl Honde hakutegemea kabisa kusikiajambo lile, kabla Ntahondi hajajibu tena simu ikakatika, kuangaliahivi ilikua imeishiwa charge, hatukusikitika sana kwani tulikuatunajua sasa tuko katika mikono salama kiasi[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Tuliendeleakukaa pale mpaka majira ya mchana hivi nadhani ilikua ni saa nnekutokana na Jua lilivyokua likizidi kua kuongezeka hapo kwa mbaalitukaanza kusikia sauti ya gari ikija upande wetu, Ntahondi masikiniakasimama na kutaka kujificha akijua pengine ni wale mabedui wa PabloMwaki wanarudu tena, tulipochungulia nje tuliona Gari aina ya kama yaRange Rover ikiwa imepaki nje ya Nchumba iliyokua mbali kidogo napale tulipo, kisha wakashuka vijana watatu wakiwa na Bunduki wakiwawamevalia kiraia, kisha wakashuka tena watu wawili nilipowaangaliavizuri niliwajua alikua ni Mwl Honde, na Oscar Mlinzi wa pale chuonikwa kina Ramla na Ntahondi ambae pia kumbe ni Mtoto wa MzeeBanzi..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]NikamsikiaMzee Banzi akimwambia Mzee Ngozi "wanajua tuko kwangu,"kisha mzee Ngozi nae akamjibu "Haya basi tuwasogelee"tukasimama na kuanza kutoka nje ya Nyumba ile tuliokua tumekaa,tukiwa tuko mbele, muda wote hu kule ndani tulikua pamoja na walewazee wawili wa mwanzo walionesha kua na shaka na sisi na kutakakuturudisha mikononi mwa Maharamia wale PABLO hawakua wakichangiachochote nadhani walikua wakijilaumu kwa kila walichotaka kutufanyia.Tulipowakaribia akina Honde nikamuona Honde akija kwa kasi upandewetu na kisha akanifuata na kunikumbati huku akitokwa na machozi,kisha akaenda kumkumbatia Ntahondi, baada ya hapo tukaingia Ndani kwaMzee Banzi..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Tulipofikandani akaanza kuongea Mwl Honde[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Wazeetunawashukuru sana kwanza kwa kila jitihada zenu mlizozifanya zakuhakikisha mnawatunza vijana hawa na kututafuta sisi mpaka tumefikahapa, pili tunawaomba radhi kwa kila aina ya usumbufu mlioupata tangumlipokua na hawa vijana hapa" kisha akaendelea tena baada kuvutaPumzi[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Mimini naitwa Stephen Honde hawa watatu ni askari kitengo maalum , "nilishukuru Mungu kimoyo moyo kusikia maneno haya ya Mwl Honde kwakuasasa niliamini ukombozi hauoko mbali[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]KishaHonde akanigeukia na kuniambia kua[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"sasatunaondoka na kwenda moja kwa moja mpaka kwa Mhe Waziri mkuu mtakaapale kwa mahojiano maalum" baada ya kuongea maneno hayo Hondealiwasisitiza wazee hawa wasitoe ile siri popote kisha akawapa pesakama shukrani kisha akawaaga kwa ahadi kwamba atarudi tena kuzungumzanao siku nyingine, Wazee hawa walishukuru sana na kuahidi kuawatatupa ushirikiano wowote kama utahitajika. Tukanyuka na kuingiakwenye gari kwa ajili ya Safari ya kurudi mjini...[/FONT]
 
Back
Top Bottom