RIWAYA: Siku ya graduation

RIWAYA: Siku ya graduation

Aisee, sijui sasa ile safari ya kwenda kwa waziri mkuu kama itafanikiwa, dah! Uzuri Ntahondi na huyu jamaa lazima wataoana!
 
Sasa muziki ndio unataka kuanza, very nice story
 
RIWAYA: SIKU YA GRADUATION
MTUNZI: MAUNDU MWINGIZI

SEHEMU YA TISA

Baada ya kuagana na Wazee pale kijini safari ya kuelekea mjini ikaanza, Tulitembea kwa umbali mrefu bila ya kuona nyumba zingine tofauti na zile za awali tulipokua tumepata hifadhi, sikuweza kutambua tulikua katika kijiji gani kwa maana sikupata hata nafasi ya kufanya hivyo kutokana na Shauku na kiu yangu ya kufika mjini ili nijue nini kinafuata ili kuona haki ikitendeka , Hamu yangu kuu ni kuona Ramla na huyo hawara yake Pablo Mwaki wakiadhirika mbele ya macho yangu kwa uovu na unyama waliotutendea japo hatukustahiki kutendewa yale,

Wakati safari ikiendelea nilikua nikitafakari na kujenga darasa huru kichwani mwangu kufuatia kadhia hii iliyotukumba, japo nimepata taabu na kuteseka sana bado kuna vitu nilivichukulia kama sehemu ya darasa kubwa katika maisha yangu na katika maisha ya mtu mwngine yeyote atakaebahatika kuipata kwa kina simulizi ya haya yaliyotokea, kila nilipomuangali Ntahondi ambae alionekana kua bado hajamini kua walau sasa tuko kwenye mikono salama nilifikiri mambo mengi sana, nilianza sasa kuitambu a Nguvu ya Wanawake katika baadhi ya mambo muhimu, niliamini kua bila Ntahondi nisingekua pale muda ule..

Safari ilikua ndefu na sasa hatimae tukatokea katika wilaya ya bagamoyo mkoa wa pwani na hapo ndipo nikaanza kupata picha sasa ya Muelekeo wa tunapotoka na tunapoelekea, Gari ilishika kasi barabara kuu ya kuelekea sasa jijini Dar Es Salaam, nilifarijika sana kuanza kuyaona mandhari ya mji ambayo kwangu sikutegemea tena kuyaona maana kuponyoka kwa wale Maharami ni sawa na Ngamia kupenya kwenye Tundu la sindano, Mwl Honde kila alipojaribu kutuongelesha tulimjibu tu ili mradi tumemjibu lakini kila mtu alikua akiwaza yake kichwani.. kilichonishtua zaidi ni pale Honde alipotuambia kua kwa sasa Ramla ni mjamzito na kila mtu ameshajua pale chuoni, ni mimba ya Pablo. Japo siku na hamu tena ya kua na Ramla ila roho ilizidi kuniuma tu..

Baada ya Safari Ndefu tuliingia sasa jijini Dar na moja kwa moja msafara ukaendelea kwa kasi kuelekea maeneo ya Msasani, na baada ya magurudumu ya Gari kuzunguka kwa kasi nzuri tu hatime breki zilipigwa mbele ya Nyumba moja kubwa, Nzuri, na ya kifakhari iliyo zungushiwa Fance kubwa iliyonakshiwa kwa kila aina ya mapambo, baada ya kusimama pale akateremka Mwl Honde na kwenda moja kwa moja Getini kuongea na Askari walinzi waliokua pale Mlangoni kasha baada ya mazungumzo yao mafupi walifungu geti kasha gari yetu ikaingizwa ndani, tulipofika ndani ya geti hili kubwa Tukapokelewa na kijana mmoja Mrefu, maji ya kunde, aliyeonekana kujazia vizuri misuli yake licha ya Suti aliyokua ameivaa lakini bado alionekana vema kua ni mwana mazoezi mzuri tu, baada ya kutupokea akatuongoza ndani kabisa ya Mjengo ule

Tulietembea katika korido ndefu mpaka katikati ambako wote tulisimama na kisha kijana huyo mwenye Suti nyeusi akagonga Kengele, wakati huu sasa tulia wane tu Mimi, Ntahondi, Mwl Honde, na huyu kijana alievaa suti nyeusi, wale Askari walibaki nje wakiwa pamoja na Oscar na baada ya kama dakika mbili hivi mlango ukafunguka kisha tukaingia ndani, tulpofika ndani tukapokelewa na watu waliokua mule ndani, kwa haraka haraka niliweza kuwatambua wawili tu kwa kua nilikua nikiwaona mara kadhaa kwenye vyombo vya habari, wakwanza alikua ni Mhe Abraha Honde waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzani, na wapili ailiku ni Mhe Stanley Kalokola KalokolaWaziri wa Mambo ya ndani, huyu watatu sikumtmbua kwa haraka. Baada ya mapokezi hayo tukakaribishwa kwenye viti kasha tukaketi, Waheshimiwa hawa walionekana kuumizwa na kusononeshwa na kitendo kile cha sisi kuteswa kikatili kiasi kile maana hapo tulipokua tulikua Tumepauka vuu kama nyani, michiirizi ya damu ikiwa imeganda mwilini, mimi nikiwa na jeraha kubwa kichwa nillolipata wakati ule tunakirikishana na Yule Baunsa kule Msituni, Ntahondi akiwa kaumia zaidi miguuni kutokana na kukanyaga visiki vikavu vya miti wakati tunakimbia kule Porini,

Baada ya kuketi tu kijana huyu alianza kututambulisha kwa waheshimiwa hawa, na hapo ndipo nikamjua huyu mtu wa tatu, aliitwa Mhe Florent Samwel ndie Mkurugenzi mkuu wa idara ya Usalama wa taifa baada ya hapo nae akajitambulisha kwetu kua ni Captein John Makala, kilinishangaza kijana huyu alionekana kutujua vizuri maana alipomaliza kutupa utambulisho wao sasa akatutambulisha sisi kwa Mhe Waziri kwa kututaja majina mpaka na ubini, alianza kwa kunitaja mimi kua ni Naufal Mpodobakshi kisha akafuatia kwa Ntahondi Salum na baada ya hapo akamuachia nafasi ya kuongea Mhe Waziri Mkuu ambae akaanza kuongea kwa utulivu mkubwa

"Kwanza poleni sana kwa matatizo yaliyowakuta, hizo ni changamoto katika maisha ya kila mwanadamu na ili mkabiliane nazo inabidi kwanza mzikubali, Matatizo yaliyowakuta pia yametusaidia sisi kuzidi kumpeleleza sana huyo anaedhaniwa kuhusuika na matatizo haya na sasa tunavitu vingi sana tumevipata kama ushahidi wa umafia na uharamia wa huyu mtu" ila kabla hatujafika mbali zaidi hebu tuambieni ilikuaje huko mlikotekwa maana wewe Naufal huku pia una kesi ya kujibu kuhusu tuhuma za kukutwa na mwili wa Yule dereva wa Tax alieuwa" Nikaanza mimi kuelezea Story nzima jinsi ilivyokua, kwa kweli hadithi ilikua ni ndefu ya kuumiza na kusisimua nilielezea kwa ufasaha bila kuruka hata nukta moja, story hii ilionekana kumuingia sana Mhe Waziri wa Mambo ya ndani nikaona anaingiza mokono mfukoni na kutoa Leso kisha akawa anafuta machozi, ksha baada ya hapo ikawa zamu ya Ntahondi ambae aliongea mengi sana mpaka siku aliyokamatwa na kuteswa kinyama japo alishindwa kuimalizia story hii akaanza kulia, ikabidi Waziri Mkuu ambembeleze na kasha akaanza sasa kuonge waziri wa mambo ya ndani

"Huyu Pablo ni mtu hatari sana, ana pesa chafu nyingi zisizojulikana hata amezipata wapi lakini kwa uchunguzi wa kina tulioufanya tuligundua kua huyu bwana mwaka 1998 alifungwa jela kwa kosa la mauaji ya Muuza Madini kutoka mererani, inasemekana alimuua na kumdhulumu pesa nyingi sana Lakini mwaka 2000 alikata rufaa na kushinda kesi yake ambayo nasikia alihonga pesa nyingi sana kwa baadhi ya mahakimu, baada ya kurudi huku uraiani akawa anajihusisha sana na Biashara za wizi wa magari kabla ya kuanza kujihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya. Mtu huyu ni hatari sana amewanunua watu wengi sana katika vitengo tofauti ambao ni vibaraka wake kila kona, anao mapolisi, waandishi wa habari, mahakimu, nk na kesi zote za mauaji aliyoyafanya tuna ushahidi wote juu ya meza, sasa na hiyo ya kumuua huyo dereva wa Tax nayo tunaiingiza kwenye List" Mhe Waziri alikua akiongea kwa hasira sana iliyotamalaki usoni machoni mwake
"Habari tulizo nazo ni kwamba zimebaki wiki mbili tu ifanyike hiyo Graduation ambapo PABLO anataka kumvisha pete ya Uchumba huyo binti aitwae Ramla ambae nae anapaswa kukamatwa kwa kushiriki tendo haram la utekaji, mauaji na utesaji, hivyo mipango inasukwa ya kuwakamata siku hiyo na kuwapeleka mbele ya vyombo vya Sheria, na siku hiyo itapaswa na ninyi wawili muwepo hapo japo mtaku ndani ya gari maalum mpaka mtakapohitajika, tutakua na ulinzi mkali sana eneo hilo kwa sababu PABLO ni mtu hatari sana na anashirikiana na baadhi ya Maofisa wa Polisi wasio waadilfu, mipango yote inatakiwa ifanyike kwa uangalifu na usiri mkubwa, hata ndugu zenu hawapaswi kujua kua mko hapa;;" kisha akamiliza kuongea, nilimuelewa vizuri huyu Waziri alikua akijaribu kututahadharisha juu ya Nguvu za Pablo na inaonekana siku hiyo inawezekana akaja na vijana wake wa kazi ni mwisho tukashindwa kumtia nguvuni..

Baada ya mazungumzo haya Waziri mkuu akamwambia mdogo wake Mwl Honde kua atupeleke vyumbani tukaoge na kubadili nguo kasha tupewe chakula halafu tupumzike na kwamba yeye angerudi pale kesho yake, Laikini kabla hatujatoka tukaombwa tupige Picha kama ushahidi wa kila tukio linaloendelea sasa, tukapiga picha tukiwa vile vile na damu zetu kasha tukatoka kwenda vyumbani tulikopelekwa na Mwl Honde, baada ya kuoga, kubadili Nguo, na kupata chakula cha nguvu tulikaa pamoja Seating Room tukiwa Mimi, Ntahondi na Mwl Honde ambae alijaribu kutufurahisha na kututoa hofu kabisa kua tupo sehemu yenye usala mkubwa na kwamba hakuna yeyote atakaeweza kuja kutudhuru mahala pale baada masaa kama mawili Mwalimu Honde akatuaga na kuondoka zake..

Tuliishi mule ndani kwa Raha mustarehe, tukiwa na amani na furaha, huku tukiisubiri kwa hamu SIKU YA GRADUATION, Japo huku sisi tukiisubiri siku hiyo kwa lengo la kuustaajabisha umma kwa kuwatia nguvuni Pablo mwaki, Ramla, na wapambe wao, hali ilikua tofauti huko Nje ambako Graduation hii ilionekana kusubiriwa kwa hamu na watu wengi wakiwamo wanafunzi, waalimu, na watu wengine ili kushuhudia tukio lilosisimua wengi la kitenda cha PABLO Mwaki kumvisha pete ya uchumba Ramla.. amaa kweli pesa ilipasua mlima nasikia tayari mwaki alishakua kawalipa na baadhi ya waandishi wa habari kutoka katika baadhi vya vyombo vya habari kwa ajili ya kuripoti tukio hilo

Tukiwa mule ndani Ntahondi mara kwa mara alikua akilalamika kua asingeweza kuendelea kuishi peke yake kule Chumbani kwani kila ikifika usiku mkubwa alikua akishtuka na kuogopa sana, ikabidi siku moja ikabidi aje kulala huku kwangu kwa kua vyumba vyetu vilikua karibu karibu, Tuliendelea kuishi na kulala pamoja japo sasa Uzalendo ukanishinda nikajikuta nasema jambo
"Ntahondi, kuna jambo nataka kukuambia"
"Niambie tu Naufal"
"Mimi na wewe tumeteseka sana, na tumeumizwa sana na mkasa huu wote, naamini Mungu alikua na agenda yake kutukutanisha kua karibu zaidi"
"Ni kweli kabisa"
"Sababu ya mateso yote haya ni mapenzi lakini pamoja na hayo huu sio mwisho wa kupenda"
"Ni kweli, na mie nakuombea kwa Mungu umpate mwingine mwenye mapenzi ya dhati akufute machozi ya kila kilichokikumba"
"Mie nahisi tayari nimeshampata mwenye mapenzi ya dhati" baada ya neon hilo tukajikuta tumecheka wote kasha akaniuliza swali la kichokozi
"Nani tena huyo mwenzetu? "
"Ni Ntahondi" nilijikaza na kutamka tu, Ntahondi akabaki ananiangalia kama mtu ambae hakufikiria kitu hicho, nikaona niendelee kutoa maneno kuntu ili anielewe
"Ntahondi naamini kuna kitu cha ziada mpaka Mungu kutukutanisha ki mtindo huu, naomba unikubalie, na kama utanielewa nataka tukimaliza tu zoezi la kumtia nguvuni Mwaki na muuaji mwenzie Ramla nikuvishe Pete ya Uchumba na hapo sasa tujiandae rasmi kwa ajili ya Ndoa" Ntahondi alionesha wasiwasi mkubwa wa kukubali jambo hili ila baada ya maongezi marefu tulifikia muafaka na kukubaliana kufunga ndoa


Ngekewa ram angelca chacha patrick showtie amina mabata mlyn Angelicious culbby muuza ubuyu princetx
 
[FONT=Helvetica, serif]RIWAYA:SIKU YA GRADUATION[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]MTUNZI:MAUNDU MWINGIZI[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]SEHEMUYA KUMI
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Sikuzilizidi kuyoyoma kuelekea kwenye siku ya Graduation, sikuinayosubiriwa kwa hamu na watu wengi kila mmoja kwa namna yake, hukukwetu mimi na Ntahond[/FONT][FONT=Helvetica, serif]ihuba lilizidi kukolea na sasa ikawa kila siku ni mipango yetu ya Ndoatu kama tutalimaliza salama zoezi hili, mara kwa mara alikua anakujaMwl Hondekupiga Story nasi, Tulicheka na kufurahi kwa pamoja, Pia MwlHonde alitumia fursa hiyo kunishauri jambo huku akinitania[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Kakaumeteseka sana kwa ajili ya yule kahaba, waswahili wanasema Kuvujakwa pakacha nafuu kwa mchukuzi, sasa Ntahondi yuko mikononi mwakoKamata Fursa hiyo kaka, take a chance brother.."[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"haaha ha kaka acha zako bhana mie bado nina stress zangu, hapa naisubirikwa hamu Graduation.."[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Aukaka bado ka moyo kapo kwa Ramla?!.." Swali hili sasa lilinipahasira japo nilijikaza ili asielewe, akaendelea kunipa somo ambalonimeshalitekeleza kimya kimya[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Wazungu wanasema Some people stick with you only because they have noone to stick with, but when they found someone else they will justleave you" akiwa na maana kwamba Kuna baadhi ya watu wanakua pamojana wewe kwakua tu hawana mtu mwingine wakua nae karibu na endapo sikuwakipata mtu mwingine wewe watakutelekeza tu, nilimuelewa vema MwlHonde kua anamaanisha Ramla alikua na mimi kwa kua alitaka kupatamsaada tu ambao kwa wakati ule hakua na mtu mwingine wa kumpa na sasakampata ndo maana kanifanyia yote yale, kisha Mwl Honde akaendelea"Kama utakua na Ntahondi hiyo itavuta hisia za wengi, nakutengeneza historia ya kipekee hata kwa vizazi vyenu" alijaribukunishawishi ..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Sikumoja zikiwa zimebaki siku mbili tu, Nikiwa na Ntahondi tumeketisebuleni tukipiga soga za hapa na pale ndani ya Mjengo wa Mhe WaziriMkuu, aliingia Mwl Honde akiwa na yule kijana alietupokea siku iletulipowasili , kijana huyu aliitwa Captein John, walipofikatuakasalimiana na bila kuchelewesha muda ikaanza mipango yamaandalizi ya kuvamia ukumbi katika siku hiyo ya Graduation,CaptainJohn alisema kua yeye ndie atakae kua Kiongozi wa hiyo Oparationnzima na tayari kuna vijana wao wa usalama wa taifa wanaosoma paleChuoni wameshajiweka tayari kwa tukio hilo, tukapewa Ramani nzima yajinsi zoezi litakavyokua kisha jamaa akasema kua wao wataanguliamapema ukumbini kisha sisi tutakuja mpaka nje na gari yetu kishatutasubiri kuitwa tu[/FONT][FONT=Helvetica, serif] [/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Kwasasa mtapaswa kutulia hivyohivyo, na hata siku hiyo ikifika mtakuandani ya gari tu kabla ya kushuka maana hamtakiwi kuonekana mapemahasa wewe Naufal si unajua unatafutwa kwa tuhuma za mauaji ya yuleTax Driver sasa kama utajitokeza mapema utakamatwa na kusababishazoezi hili ku feli" maneno hayo yalinichoma tena upya nakunitonesha jeraha langu moyoni kuona pamoja na kutekwa, kuteswa, nakuumizwa vibaya lakini bado PABLO Kanichafua na kwenye vyombo vyahabari kwa tuhuma za uongo kua nilihusika na mauaji, nilisononekanasana lakini niliyakumbuka maneno haya yalipatwa kutamkwa naMwanamuziki mkongwe Afrika Kofii Olomide[/FONT][FONT=Helvetica, serif] [/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Lokutaeyaka na ascenseur, kasi verite eyei na escalier mpe ekomi" akiwana maana kwamba Uongo hutumia lift kupanda Ghorofa(Hivyo unawahi sanakuwafikia watu) Na ukweli hutmua ngazi kupanda ghorofa(Hivyoutachelewa kufika), Japo Ukweli ukifika uongo hujitenga, baada yamazungumzo marefu kutoka kwa captain John akatoka zake na kutuachasisi tukiwa na Mwl Honde,[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]MwlHonde akaendelea kutupa hali ilivyo huko nje,[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Nimeongeana kaka yako ameniambia kua mama yako anaingia leo kutoka Tabora naLengo lake kuu ni kuja kuhudhuria hiyo Graduation ili apate nafasi yakumkabili huyo Pablo hapo hapo atamuanzishia vuruga ya hatari, kakayako kajaribu kumkanya lakini amegoma amesema siku hiyo ndoatamuonesha ilipo maiti ya mwanae kipenzi" Tukacheka wote kwa kwapamoja kusikia kua Mama alikua akijua tayari nitakua nimeshauawa,Japo nawahurumia sana mama yangu na kaka jinsi wanavyohangaika kwaajili yangu wakiwa hawajui nilipo, kisha Mwl Akaendelea kuongea hukuakiwa amejilaza kiubavu pale kwenye sofa "Mbaya zaidi Mama yake naRamla nae nasikia amekatiwa ticket na PABLO anapanda Ndege leo kujakuhudhuria hiyo Graduation haha ha na katoa maneno mabaya sana kuhusuwewe dah angejuaa!" tulikua tukisikiliza maneno ya Mwl Honde hukutukicheka , Honde akaendelea kutiririka "Huku nako Mama yake naNtahondi nae kamtukana Mkuu wa kituo na kumtuhumu kua anajua kilakitu kuhusu sakata la kutekwa kwa mwanae halafu hataki kumkamatamtuhmiwa, nae kasema atakuja siku hiyo Graduation hapo chuo KumnangaPablo Mwaki"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Storyilikua tamu sana hasa unapoona watu wako wakipambana kwa ajili yako,nasi tuliendelea kujidhadhatiti hasa kufuatia taarifa tunazopewa kuaPABLO ni mtu hatari hivyo zoezi la kumkamata si la lele mama, basibaada ya Mazungumzo marefu Honde akatuaga na kuondoka zake nakutuacha tukiwa tumepumzika pale Sebuleni..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Hatimaesiku ya Tukio ikawadia, siku ya kipekee kwetu, siku nzito, Tuliamkamapema sana siku hiyo kuliko siku zote na kisha tukajiandaa kwakuogana na kimavazi mapema, Ama kwa hakika siku hii tulikuatumependeza sana, Ntahondi alikua anang'aa kama Noti mpya ya Elfukumi mpaka nikatamani kua hii ndo ingekua siku yetu sisi ya kuvishanapete, kisha Tukaenda zetu juu yea meza kuu kupata kifungua kinywakizito kwa ajili ya kujiweka fiti kimapambano, Na baada ya kupatakifungua kinywa tulirudi kuketi juu ya makochi huku tkiendeleakuangaliana kwa macho ya ushindi.. Haikuchukua muda Mrefu majira yasaa moja asubuhi ziliwasili Gari mbili Nyeusi, Moja walishuka waleaskari watatu waliokuja kule kijijini kutuijia wakiwa na CapatainJohn Makala, na Gari ya tatu walishuka Mhe Waziri Mkuu Abraha Honde,Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Stanley Kalokola, na Mhe Florent Samwelambae ni Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa nao wote wkaja kujumuika nasipale Seating room, baada ya Salamu na Mazungumzo nikawa namsikiaCaptein John Akitoa maelezo ya ya utaratibu wa utekelezaji wa mpangokazi wetu na kisha tukapewa baraka zote na viongozi hawa ambaohawakukaa sana wakaondoka..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Tukabakindani sisi na mashushushu hawa tukiendelea kushibishana mbinu nautaratibu wa zoezi zima na baada ya kuelewana vema Sasa ikawa nimawasiliano tu yakiendelea kati ya Mwl Honde na Captain John kuhusuhali ya sherehe ikoje pale chuoni, na baada ya kupokea taarifa zaawali kua Sherehe inafanyikia katika ukumbi wa nje kutokana na kupatawahudhuriaji wengi sana, ikabidi wale Askari watatu waanze kuondokaharaka ili wawahi nafasi muhimu pamoja na kuyaelewa mazingira, sisitukabaki na Captain na ilipofika majira ya saa tatu nasi tukatoka njena kuingia kwenye gari moja sikumbuki ni aina gani ilikua kama Pajerohivi, Mimi na Ntahondi tukakaa seat za nyuma na Captain John akakaaSeat ya mbele na safari ikaanza, hapo sasa kila mtu akawa kimyaakilifikiria tukio la huko tuendako , Tulipokua sasa tunakaribiakuingia barabara hii inaotokea Chuoni IFM ambako ndiko sherehe hizizinakofanyiwa ghafla kwambele ya Ukumbi wa makumbusho ya taifa ambakoni jengo lililokaribu kabisa na cho hiki nikaona gari nyekunduimesimama pembeni ya barabara, nilipozidi kukaza macho nje ya garihiyo nikawaona vijana watatu wamesimama huku wameiegamia gari hiyo,mmoja nilimjua vema, alikua ni Yule Baunsa mweupe wa kule Msitunituliepambana nae na kutoroka, nikamgeukia Ntahondi ili nimuoneshe naeharaka akawa kumbe ameshamng'amuaTukamueleza Captein naeakamuangalia kwa makini kisha hakusema kitu, tulipoipita Gari ileCaptain John akatoa simu yake na kumpigia mmoja wa vijana wake wakazi na kumwambia awe karibu na watu wale kisha gari ikaingi kwenyeviunga vya Chuoni hapa inakofanyikia sherehe hii[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Watuwalikua ni wengi sana, wakionesha kua na furaha kubwa, huku spikazikitema mziki kisawa sawa na kumbe tayari shughuli ilikuaimeshaanza, Gari hatukuipaki mbali bali dereva aliisogeza mpakakaribu na upande wa jukwaa kuu kisha Captain akamwambia asimame, vioovote vikapandishwa juu halafu kiyoyozi kikaachiliwa vizuri, kwa kuavioo vilikua ni vya Tinted hivyo tuliona kila kitu kinachoendelea nahatukua na hofu ya kuonekana na mtu yeyote.. Tayari wale askariwaliotangulia kuja huku walikua wamekaa High table wakiwa wamevaliajeans na mashati ya mikono mirefu japo yalikua ni ya rangi tofautitofauti, tukiwa ndani ya Gari sasa niliweza kumuona vizuri RAMLAAlieonekana kushauka kisawasawa kuliko hata wenzie bila shaka kwa kuaalikua anafuraha mbili zaidi ya wenzie na kile Kitumbo chake chamimba ya PABLO MWAKI kilianza kuonekana kwa mbaali, wakatitukiendelea kuwa enjoy wahudhuriaji waliokua tayari ukumbini nawalioendelea kuingia ghafla tukamuona Mama yake na Ntahondiakipokelewa na vijana nadhifu walioandaliwa kwa kazi hiyo kisha naekapewa nafasi nzuri tu karibu na meza kuu,[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Ratibailikua ikiendelea kwa mbwembwe, Mc Alizikonga nyoyo za wahudhuriajikwa maneno yake matamu yenye kuvutia, Wakati shughulia ikiendeleakulipuka kwa Shangwe za waalikwa wakati msanii mmoja mwanadada wamuziki wa Bongo Flavour akikata mauono yake Stajini ndipo ikaingiaGari moja nzuri sana aina ya Hummer na kisha ilipopaki wakashuka watuwatatu, sikuwajua wote japo niliwakazia macho, nikamuona Ntahondiakiniangalia kisha akaniambi haya ulisema humjui Pablo Mwaki huyohapo wa katikati, nilihisi kusisimka mwili mzima, Nywele zikajizoa,Alikua ni Mtu mzima kiasi chapo si sana, mweupe, ana mwili wawastani, akiwa amevali Suti moja kali sana bila shaka hawa wawiliwalikua ni wapambe wake, Nao wakapokelewa mpaka meza kuu ambako watuwalisimama na kumpa mikono kwa heshma, akapewa nafasi karibu yaCaptein john Makala japo Captain hakusimama kumpa mkono, Shughuliikawa inaendelea kwa kila aina ya burudani huku waalikwa wakipewaJuice na Kitafunwa..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Wakatimahafali ikiendelea ghafla jicho langi Likatua kwa Bi Shammy, Mamayangu mzazi akiwa nae ameketi vizuri upande wa wazazi sikujua hataameingia saa ngapi, nilishtuka sana nikawa najihisi majonzi na furahakwa pamoja kumona mama yangu huyu, nikamuonesha Ntahondi naeakafurahi kumuona. Ikafika zamu sasa ya kupokea vyeti na zawadi,ambapo sasa tukawa tayari kushuhudia Ramla akipewa zawadi ya Gari nakuvishwa Pete ya Uchumba na Pablo ili nasi sasa tufanye yetu,Wahitimu wakawa wanaitwa majina yao kwa kuzingatia Alphabet zaowakati zoezi likiendelea ghafla akaingia Mama Ramla akionekana nafuraha, na pia akiwa ni kama mtu anaewashwa shari mwili mzima naeakapokelewa na kupewa nafasi upande wa pili wa meza kuu walikokuawamekaa wazazi pia..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Nahatimae alphabeti sasa zikafika kwa herufi za R, Ndipo nikamsikia McAkimwita kwa madaha na madolido yote RAMLA utadhani alikua akijuakinachoendelea ukumbini hapo, zikalipuka kelele za shangwe navigeregere kumshangilia binti huyu Msaliti, japo kuna Ishara niliionakwa baadhi ya vijana waliokua pale ukumbini kutokumshangilia kabisaRamla, sikushangaa sana kwa kua tulikua tumeshadokezwa na Mwl Hondekua kuna fununu zimeshaanza kuongewa pale Cho kua Ramla ameusukampango wa kutekwa kwenu, Basi ramla akaenda mpaka pale Mbele kwamwendo wa mbwembwe kabisa, kisha akenda meza kuu na kupewa vyetiyake, huku upande wa kulia tayari wageni wameshasimama kumpa zawadi,Pablo akiwa kwa nyuma yao, mkoni ameshika box[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Wakatitukio la kumvisha mataji Ramla pamoja na zawadi zingine zingiendelea,nikamuona mama Ramla nae akisogea na Box lake la zawadi, huku nakosasa Mc akaanza kumtambulisha Mwaki "Mabibi na mabwana baada yakumpa zawadi Ramla pia kuna zawadi yake maalum ya Gari pamoja nakuvishwa rasmi pete ya uchumba kutoka kwa mchumba wake PABLO.. hapotukamuona sasa Pablo akisogea mbele ya kundi akiwa na Box lake dogonadhani ndani yake ndo kuna ile Pete na Funguo ya Gari..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Ghaflatukamsikia Mama Ramla akipiga yowe kubwa kuashiria hali yatatizo[/FONT][FONT=Helvetica, serif] [/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"NOOOO"Watu wote wakashtuka na kushangaa Mama huyu akaendeleakulalama[/FONT][FONT=Helvetica, serif] [/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Haiwezekani,nasema haiwezekani hata kidogo, mama weweee aibu gani hii" watuwote walionekana kuduwaa, Tukiwa ndani ya Gari yetu tukamuona sasaCaptain John akisogea karibu ya Mwaki huku nae akionesha kushangazwana kitendo cha mama huyu kulalamika kwa sauti, Tayari Mama Ntahondina mama yangu mimi nao walikua wamesimama eneo la tukio NADHANIWALIKUA TAYARI KUMUANZISHIA VARANGATI Pablo lakini nao wakashangazwana hali ya sintofahamu kutoka kwa mama Ramla , ghafla Mama Ramlaalimsogelea na kumkwida shati PABLO MWAKI huku akilia kwa uchungu,cha ajabu Pablo Mwaki nae alikua kama haelewi elewi ndipo tukamuonaMkuu wa Chuo amesogea pale na kmuhoji mama huyu..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Kwanitatizo nini mama? We ni nani hasa na huyu Mzee unamjua?"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Miminaitwa Ayman Gamba ni mama yake mzazi na Ramla, Na huy anaitwa AlexMwakimbusu ndie Baba yake mzazi na Ramla" watu wote wakashangaa nakubutwaika ikabidi Mkuu wa chuo amuulize vizuri mama huyu kuhusuhicho anachokisema na kama anamjua kweli Pablo au anamfananisha"Namjua vizuri sana wala sijamfananisha huyu, na wala sikujua kamamwanangu leo ameniitia laana hii, mie nimekuja kushuhudia graduationya mwanangu ambae pia nikaambiwa anataka kuolewa na mfanya biasharamaarufu anaeitwa Pablo, mimi sikujua kama ni huyu Shetani.." kishamama huyu akaendelea kuliaa huku akihangaika kama mtu anaetaka kufa,ikabidi tena Mkuu wa chuo ajaribu kumbembeleza ili aendeleekusimulia, baada ya muda akaendelea kumwaga data[/FONT][FONT=Helvetica, serif] [/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Huyusio pablo ila anaitwa Alex Mwakimbusu ni mwanaume mshenzi, Nilikutananae Tabora mwaka 1989 Tukapendana sana, sikumjua alipotokea lakininilitokea kumpenda sana baada ya muda mfupi akanipa ujauzitonilichanganyikiwa sana maana Baada ya Baba yangu kugundua alinifukuzanyumbani nikawa sina ujanja ikabidi niende Mpaka alipokua amepangaMwakimbusu nae akanipokea na kuahidi kua ataitunza mimba nikawanaishi nae kwake baada ya Muda tukahama Tabora na kwenda Songeatulipofika huko akanishawishi nibadili dini ili anioe nikakubalikwakua sikua na pakukimbilia lakini kila siku visa vikawa vinazidiMara anipige, mara anilaze njaa, ikawa ni shida juu ya shida nabaadae nikaletewa taarifa kua Mwaki ana mahusiano na mwanamke Fulanimfanyabiashara kutoka Bukoba ambae alikua anasadikiwa ni muathirikawa ugonjwa wa Ukimwi, hapo sasa nikashindwa kuvumilia nikaamuakuondoka, Mwakimbusu akajaribu kunibembeleza nikakataa, tukakubalianakua tukapime kwanza afya ndo tuweze kuendelea kua pamoja, tukaendakupima na kweli tukakuta Mwakimbusu ameathirika lakini mimisnimeathiri na hapo ndo ikawa mwisho wetu mie na mwakimbusu, miminikarudi kwetu kuwaomba msamaha wazazi nao wakanielewa na kunipokeatena"[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]ENDELEA...[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Mudawote wakati mama huyu akiendelea kuongea huku analia kwa uchungu watuwote walikua kimya wakimsikiliza mpaka Mama yangu aliejipangakuanzisha vurugu alikua bado kama haamini kinachoendelea, hata hukuna sisi Mimi na Ntahondi tulikua kama vile tunaangalia movie, kishamama Ramla akaendelea kusimulia huku akili kwa kusikuka[/FONT][FONT=Helvetica, serif] [/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Nikamzaamwanagu ambae ni Ramla mwaka 1990 na nikamlea peke yangu bila yakujua hata alipokimbilia huyu Mwakimbusu, sikujua anaishi wapi tenana bade nikasikia alifungwa kifongo cha maisha jela kwa kesi yamauaji, Sasa mwanangu Ramla ameniita leo kumbe ana mahusiano na babayake mzazi, tena ameshampa na ujauzito" wakati Mama huyu akiliahuku akisaga saga miguu yake pale chini nikamuona mama yangu sasaakisogea na kumwambia Mama Ramla[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Amaakweli malipo ni duniani Akhera inakwenda hesabu tu, kwa jinsiulivyofurahia kitendo cha mwanao Ramla kushirikiana na huyu Ibilisiwako kumteka mwanangu ili waoane sasa mungu kakufedhehesha leo"Ghafla akasogea Mama yake na Ntahondi na kumkwida Mzee Mwakimbusualmaarufu kama Pablo Mwaki na kumwambia[/FONT][FONT=Helvetica, serif] [/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Namimi utanionesha alipo mwanangu leo habari zako zote ninazo jambazimkubwa we" Basi hali ikawa ya tafrani pale watu wakawawanashangilia, wengine wanashangaa hawaamini, wengine kina mama watuwazima wakifuta machozi kwa tukio hili la Laana..[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Wakatimama Ntahondi akiwa kamwikida Pablo Mwaki Ghafla Ramla aliekua kabakimdomo wazi muda wote akaanguka chini na kupoteza fahamu, shereheikageuka kilio na fedheha, ghafla akatokea yule Baunsa aliekuaanatutesa kule msituni na kumsukuma mama Ntahondi kisha akamwambiaPablo apite mbele waondoke huku akitoa maneno machafu[/FONT][FONT=Helvetica, serif] [/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"watotowenu makahaba na wengine majambazi wanatekana huko halafu mnatakakuwasingizia watu.." kabla hajamaliza kusema tu akasukumwa kwa tekemadhubuti kutoka kwa Captain John Makala akaenda mpaka pale chini naakatoa kitambulisho chake cha kazi na kujitambulisha kua ni afisa wajeshi la Polisi na kuanza kusema[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"WewePablo na huyu Mbwa mwenzio ndio mliowateka vijana wa watu,mkawapeleka msituni huko na kuwatesa sana na kama haitoshi mkamuuayule dereva tax ili asije kutoa siri huku mjini, halafu we Mbwaunatoa maneno machafu, angalia sasa Laana iliyokukumba kumbe mpenzimwenyewe ni mwanao wa kumzaa, Kuanzia sasa wote mko chini ya ulinzi"watu wakawa wanazidi kutaharuki kufuatia tukio hilo kisha Captainakaendelea[/FONT][FONT=Helvetica, serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]"Nakwa taarifa yako vijana uliowateka tayari tumeshawaokoa na tunao"baada maelezo hayo Captain akageuka na kuangalia usawa wa Gari nakutupa Ishara kua sasa tuteremke kwenye gari, Tukatetremka mimi naNtahondi tukiwa smart na wenye kuvutia tukateremka kwenye gari natukaanza kutembea kusogea Eneo la tukio[/FONT][FONT=Helvetica, serif]

[/FONT]
[FONT=Helvetica, serif]Lilikuani tukio la kipekee, tukio la ajabu, Wapo walioshangilia, wapowaliokua wakilia, Macho ya Yule Baunsa hayakuamini kutuona pale,nikamuangali mama yangu nae hakujua hata afanyeje, huku nako MamaNtahondi alikua ameduwaa..


[/FONT]
Ngekewa ram angelca chacha patrick showtie amina mabata mlyn Angelicious culbby muuza ubuyu princetx
 
Back
Top Bottom