- Thread starter
- #101
SEHEMU YA 13
Tulibaki mule ndani Mimi na Ntahondi, japo nilikua nimefarijika kiasi lakini sikua na amani kabisa maana kengere ya hatari ilikua imeshagonha ndani ya kichwa change, haikuhitaji msaada wa Profesa wa chuo ikuu cha Havard kuja kukuambia kua Pablo aliku ni mtu hatari sana, na kwakua ameshafanikiwa kutoroka sasa itakua ni Mtanange kumpata maana nae sio mjinga kihivyo lazima atajihami kwa umakini wa hali ya juu sana japo Honde ametupa majibu ya uhakika kua atapatikana tu..
Siku hiyo iliisha kimya kimya tukiwa zetu chumbani tukipiga Story na hatimae usiku ukaingia, wahudumu wa humu kwa Mhe Waziri walikua makini kwa kila hatua, pia walikua wakarimu sana, mara kwa mara walikuja kujua usalama wetu mule ndani, na kila muda wa chakula ulipowadia walikua wanakwenda na muda vilivyo,
Baada ya kupata chakula cha usiku, tuliingia kuoga na hatimae tukarudi kulala tu, Ntahondi alionekana kuchoka sana hivyo mapema tu akawa ameshapitiwa na usingizi, lakini hali ilikua tofauti kwangu, Usingizi wote uliparama, nikawa nahesabu tu Paa, mpaka saa saba usioku ndo kwa mbali usingizi ukailainisha mishipa ya kichwa changu na ndani ya muda nikawa nakoroma!!
Asubuhi na mapema ya siku iliyofuata nilikua wakwanza kuamka licha ya kuchelewa kulala mapema, nikaoga haraka haraka, nikamuamsha na Ntahondi nae akaenda kujiswafi mwili, akili yangu ilikua na wahka wa kutaka kujua hatma ya Pablo hivyo nilikua nikisubiri miadi ya Honde kua name nitaenda katika zoezi adhimu la kumkamata Mafia Pablo Mwaki, baba mzazi wa aliekua mchumba wangu Ramla, baada ya Ntahondi kupata maji alijumuika name pale katika meza ndogo kwa ajili ya kupata ‘Stiftahi',
Tulipata kifungua kinywa kile murua tulichoandaliwa na baada ya hapo tukawa sasa tunamsubiri tu Honde
"Na mimi si nitaenda?" aliniuliza Ntahondi
"No.."
"kwanini?"
"Hii imeshakua vita mama, kaa tu utulie usije ukatekwa bure ukaniacha pabaya mimi, jana tu nilitaka kua chizi niliposikia umetekwa"
"Kwahiyo we unavyotaka kwenda huko ukitekwa utakua umeniacha mimi pazuri?"
"Tuachane na hayo, hivi unajua mie simuelewi kabisa Mwl Honde anaonesha dalili za kua nae ni afisa usalama, au we haujashtukia?"
"Kweli mie tangu jana najiuliza maana ujue ni yeye ndie aliekuja na hao vijana anaosema ni maofisa mpaka pale kwenye Tax wakatuteremsha haraka haraka, na wakati nashuka kwenye tax nikaangusha simu chini sasa Honde alipoinama kuiniokotea nikaona ana mguu wa kuku kiunoni"
"Wee, usiniambie!!" "Sure, jamaa Shushushu huyu, haiwezekani mdogo wake tu na waziri mkuu ndo ajue mambo nyeti kiasi hicho chote" "Mhh, mama ya Ngoswe.."
Tuliendelea kubadilishana Story mpaka tukachoka lakini Honde hakutokea, nikaanza kupata hofu, nikajaribu kumpigia kwa simu ya Ntahondi lakini hakupokea, tuliendelea kumsubiria bila mafanikio mpaka jioni ikaingia na giza lililoashiria kuingia kwa usiku nalo likatanda,
Tukaingia zetu kulala, basi hali ilikua hivyo kwa takribani siku nne mfululizo, tuliendelea kuishi mule ndani bila ya kupata mawasiliano ya Kaptain, Honde, wala mtu mwingine yoyote zaidi ya mawasiliano ya simu na baadhi ya ndugu zetu ili kuwatoa hofu juu ya Usalama wetu,
Baada ya siku kama tano hivi mbele ndipo Honde alikuja, kama kawaida yetu hua akifika tunaanza story za kila aina pia hua anatupa taarifa zilizopo huko nje kufuatia tukio zima
"Huko nje habari zimevuja kua Ntahondi anaolewa na Naufal, Ha ha ha mko juu.."
"Ha ha hiyo utakua umeitunga wewe maana hakuna aliewaambia hao watu" Honde na Ntahondi walikua wakitaniana, na mie nikatupia swali langu
"Kwa hiyo kuna habari gani za Pablo?"
"Habari za Pablo sio nzuri sana, kuna mawili, inawezekana ameshatoroka na kakimbilia Kenya ambako atajipanga ili apotelee Dubai nasikia ana mijengo kule, pili inawezekana akawa bado yupo humu nchini ila muda wowote atatokemea"
"Sasa nanyi maafisa usalama mmeshindwa kumtia nguvuni kweli?"
"Tafadhali Naufal, aliekuambia mimi ni Afisa usalama ni nani?"
"Ahh, samahani, kwa jinsi unavyopata data najihisi kama niko na mtu wa usalama"
"Ok jitihada zinaendelea kumsaka maana kama atafanikiwa kukimbilia ughaibuni huko na akajificha vizuri, sasa ataanza msako dhidi yenu ili awaue apoteze ushahidi ili hata akikamatwa kesi haitokua nzito sana kwake"
Maneno hayo ya Honde yalinipagawisha zaidi lakini sikua na cha kufanya,
"Kina Ramla na Yule Baunsa nao vipi?"
"Kesho ndo watapandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza kujibu tuhuma za kushiriki kuteka, kutesa, na kupanga njama za mauaji, Hii hawachomoki wale, japo namuonea sana huruma Ramla unajua tayari ujauzito wake unazidi kuchomoza sasa ndo anazidi kuishiwa nguvu"
"Ndo atakoma mshenzi Yule" alijibu Ntahondi kwa hasira
"Sasa ninyi asubuhi muwe tayari tayari kwa ajili ya kuhudhuria mahakamni na kasha baada ya kesi mtarudi huku, nadhani mnaweza kuwasiliana kina mama nao wakaja mkaonana pale mahakamani,
Tulipigasoga sana ili kuvuta muda hatimae Honde akatuaga, akaondoka, tukabaki na sisi tukiendelea kukaa ndani tu kama wafungwa
****
Hatimae siku ya kwenda mahakamani ikawadia, kama ilivyo ada tukawa tumeshaamka mapema na tuko tayari kwa kuhudhuria mahakamani, japo tulikua na hamu ya kuonana uso kwa uso na Ramla ili tumuoneshee kua Mungu ameanza kulipa lakini bado sikua na raha kabisa kwa kutopatika Pablo, haikua muda mrefu san asana ikafika gari nyeusi almaarufu kama Shangingi,
Akashuka Honde na vijana wengine wawili wakiwa wamevalia suti nyeusi, bila shaka nao ni kutoka kitengi cha TISS, Wakatuchukua na safari ya kwenda mahakamani ikaanza, ndani yadika kama thelathini za mwendokasi tulikua nje ya mahakama kuu, tukateremka na kuingia ndani huku tukiwa na watu hawa wa Usalama, tulipofika ndani ya mahakama tuingia chemba huko tukawa tumekaa kwenye viti vidogo vya mbao huku tukisubiri utaratibu, ndipo akaingizwa Ramla, na Yule Baunsa, nilipokutanisha nae macho nikamwambia
"Karibu Baunsa" nae hakunijibu kitu, sasa alikua amesharudiwa na Fahamu lakini alionekana kua mchovu sana nadhani alipewa kiminyo kikali zaidi, Kwan je ya Mahakama watu walikua wamefurika.
Kupitia dirisha dogo niliweza kumuona Mama Ntahondi akiwa amesimama na mama yangu mimi, pia Ntahondi nae aliwatambua baadhi ya wanafunzi wenzao wa IFM, tulipokua mule ndani akawasili Kaptain John Makala, akawa anasalimiana na makarani kisha akaja uswa wetu nasi tukasabahiana nae kwa furaha, na baada ya mawili matatu akamtoa faragha Mwl Honde, sikujua walichokwenda kuongea kwani baada ya muda akarudi Honde peke yake nikamuwahi kwa swali
"Vipi mbona ameondoka?"
"Inasemekana Pablo ndo anataka kutoroshwa muda huu ndo nae anaenda kwenye msako"
"Kwahiyo sisi hatuendi tena?"
"Haina haja sana" Tuliendelea kukaa plae mahakamani kwa muda mrefu bila kesi kusomwa, ikawa ni stori tu baina yetu mpaka nilipochombeza ile habari yangu ya kuokota ile Flash ya Pablo kule ndani ya gari, nilidhani kua jambo lile ni la kwaida sana lakinikumbe ilikua tofauti maana Honde alishtuka na kuniuliza kwa msisitizo "Una uhakika aliiangusha yeye?"
"Ndio.."
"Mbona hkusema muda wote huo?"
"kwani ina nini?"
"Itakua kuna data za muhimu sana mule, we have to do something right now" Honde akatoa simu na akawa anaandika massage kwa muda mrefu na muda mfupi baada ya kumaliza kutuma ujumbe huo,
Simu yake ikaita akapokea na kuongea nakawaelewa kua walikua wakiiongelea ile Flash na kasha akanigeukia mimi
"Eti hiyo Flash iko wapi?"
"Iko kule tunapolala" Baada ya mazungumzo ya Honde na huyo mtu kwenye simu kumalizika alikata simu na kurusi kwangu sasa
"Aisee hiyo Flash ni ya muhimu sana, Kaptain Makala yuko njiani anakuja kutuchuku mimi na wewe tunaenda kuiangalia hiyo flash ila Ntahondi atabaki hapa hapa" Ntahondi alikua akitusikiliza muda wote wa majibizano yetu, nae aliafiki bila kipingamizi kua atatusubiri pale pale mahakani..
Muda mfupi tukaiona gari ile aliyokuja nayo mwanzo Kaptain John Makala lakini alikuwemo dereva tu, tukatoka nje na kuingia ndani ya gari na safari ikaanza, tukarudi kule nyumbani kwa Mhe Waziri,
Tulipofika tu tukawakuta vijana watatu wakiwa wamevaa suti nyeusi, kati yao akiwemo Kaptain Makala ambae baada tu ya kutuona alituonesha kwa ishara kua tufanye hima na haraka, ikabidi tuingie mule ndani kwa mtindo wa Joging, nilipofika Sebuleni maofisa wale wote wakatangulia juu ya meza ambako tayari walikua na Kompyuta ndogo ambayo walikua wameiweka tayari kwa kazi, mie nikaingia ndani kuchukua hiyo Flash, nyuma yangu akinifuata Swahiba wangu Mwl Honde mpaka chumbani,
Nilipofika ndani nikaenda moja kwa moja mpaka kitandani, nikaivuta droo ya kitanda ili nichukue hiyo flasha, nikapigwa na bumbuwazi baada ya kukuta flasha haimo, mikono yangu ikaanza kutetemeka huku ikivuja jasho la uoga, nikainuka haraka na kwenda kwenye Pochi ya Ntahondi aliyoining'iniza juu kiti kidogo kilichomo mule chumbani, nikafungua zipu ya katikati lakini nako Haipo!! Nilizidi kuchanganyikiwa, ghafla Honde nae akanichanganya "Vipi wewe, unaleta upuuzi"
"Hapana Honde siioni flash na niliiweka kwenye droo ya Kitanda"
"Sasa hii unataka kujiletea tabu, unadhani jamaa atakuelewaje?" Sikumjibu kitu Honde, nikafungua katika zipu ya pembeni, pia Haikuwemo!nikawa kama kichaa, nikajikuta najiuliza mwenyewe
"Nani kaichukua sasa?"
"Unaemuuliza nani?" alinihoji Honde, sikumjibu, nikafungua zipu ya upande wa kulia, Nikashusha pumzi, nikaingiza mkono kisha nikaitoa Flash, bila shaka itakua ni Ntahondi ailkua ameihifadhi mule, Honde akanisogelea haraka ili aichukue, hapo hapo namie nikamuuliza "Nini?.."
"Lete haraka twende na muda" "We sio afisa usalama wa taifa, sasa nikupe kama nani?, au amekubali kua nawe ni mmoja wao?" Nikamuachia tabasamu lilionesha kuzidi kumkera halafu mie nikatoka zangu mpaka pale sebuleni, nikaenda moja kwa moja na kumkabidhi Kaptain Makala, nae bila ajizi akaenda moja kwa moja mpaka kwenye Kompyuta yake halafu akaichomeka flash ile na kuanza kuperuzi..
Sikujua Kaptain alikua akiona nini maana kila mara alikua hatulii, yaani utadhani kiti kina miba, inaonekana alikua akiona mambo makubwa nay a ajabu katika kompyuta yake,
Ghafla akamuita Honde na kumuonesha kitu katika Kompyuta yake, Honde nae alipayuka kwa sauti ya mshangao huku akitaja jina la Mhe Kigwaza huku akiitumbulia macho ile Computer, name pia nilishtuka kusikia jina lile maana nilimjua alietajwa, Mhe Andrew Kigwaza,
Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Sasa amefanyaje? Sikupata jibu nikiwa sijaelewa kinachoendelea ndani ya Laptop ile tena likatijwa jina jingine lilizidi kunipa hamu na kiu ya kutaka kujua kilichomo
"Johari Kijukuu" alitamka Kaptain, nililijua vema jina hili kwani lilikua ni jina la Jaji aliepangwa kusimamia kesi yetu sasa kama nae ameonekana kua ni mmoja kati ya wana mtandao wa Pablo sijui itakuaje!!,
Wakati wakiendelea kusoma na kupereuzi ndani ya kompyuta mpakato hiyo ghafla Kaptain akainuka na kupiga meza kwa nguvu kisha akasema kwa sauti "Pasword yake hii hapa kaificha huku mshenzi huyu, baada ya hapo akaingiza mkono mfukoni akatoka Modem ya Internet halafu akaipachika kwenye Kompyuta na kuanza kuunganisha mambo pale, Baada ya muda nrefu wa kuperuzi na kudadisi Kaptain alishtuka ten asana, bila shaka alipata jambo jingine kubwa zaidi, akasimama tena pale kwenye kiti, halafu akasema
"Mungu wangu tutwahi kweli!!"
"Wapi?"
"Air port, huyu mshenzi anaondoka asubuhi hii kwenda Kenya na ndege ya Shirika la AMNOINA, Ndege ya MHZ 6453 Ndo wanayoitumia"
"Kwahiyo tunafanyaje?"
"Haraka tuondokeni tujaribu kuwawahi" aliposema tu hivyo haraka tukatoka nje na kuingia kwenye magari yetu mawili yaliyokua yameegeshwa pale Nje, tukaondoka kwa kasi ya ajabu kuelekea Airport, tulipokua njiani nilimsikia Kaptain akimuambia Honde apige simu ofisi kuu ya usala kuomba nguvu ya ziada pale uwanjani, tulitembea mwendo wa farasi, mwendo wa kasi, na dakika chache mbele tulikua katika Viunga vya Mwl Julius Nyerere Intanational Airport,
Gari ziliposimama tu tukashuka haraka, nikamuona Kaptain akiikimbilia ndege moja iliyokua ndo kwanza inaiacha ardh na kupaa juu, wote tukamkimbilia mpaka pale lakini haikusaidia kitu MHZ6453 Ilikua ikipotelea hewani,
Abiria wengi walitaharuki wakawa wanakimbia hovyo nadhani walihisi kua sisi ni majambazi au magaidi, tukarudi mpaka pembeni kidogo kulikua na Abiria wa kike kama watano hivi wakiwa wamesiamama na Jeneza lao pembeni huku wakilia, bila shaka walikua wakisafirisha maiti,
Walikua wakiongea kwa lugha ya kingerza, kitu kilichonifanya nijue kua sio watAnzani, Na hata nilipoangalia Lile Jeneza walikua wamelifunika na Bendera ya Ghana, lakini ghafla nikamuona Kaptain akinisogelea na kuniambia nitangulie ndani ya gari, haraka nikawahi kwenye gari, nilipoingia tu nilishangazwa na nilichokiona pale nje,
Kaptain na vijana wake waliwavamia wale wafiwa na kuanza kutembeza kichapo cha nguvu ghafla wakalipitia lile jeneza wakaja nalo kwa kasi mpaka kwenye Gari yetu wakaliingiza nao wakapanda haraka ki dereva akawasha gari tukatoka kwa kasi eneo lile la uwanja wa Ndege
Llikua ni tukio la jabu sana kwa abiria na hata kwangu pia, sikujua kilichofanya Kaptain afanye jambo lile bay asana, basi tukashika kasi barabarani, lakini haikua kazi rahisi maana tayari askari wa pale uwanjani walikua wakitufukuzia kwa kasi huku wakiturushia risasi,
Mji mzima ulichafuka kwa mashambulio yale, Tuliendelea kukimbia mpaka hatimae tukaingia katika viwanja vya mahakama kuu, tukateremka haraka na hapo hapo vijana wa Kaptain wakaliteremsha lile Jeneza na Kaptain akawapa maelekezo vijana wake tukaingia nalo jeneza lile mpaka ndani,na muda huo tayari askari waliokua wakitukimbiza nao walifika mahakamni pale,
Sisi tukaingia mpaka ndani tukakuta watu wengi sana wamejaa kusikiliza kesi, tayari Ramla, Baunsa na baadhi ya viongozi wa jeshi la Polisi wakiwa wamesimamishwa kizimbani huku kesi iikiendelea mbele ya Jaji Johari Kijukuu, ikabidi Mahakam nzima itulie tulivyoingia, ikawa kimya, mara na wale Askari nao wakaingia mpaka ndani.
"Kuna nini?" aliuliza mmoja katika wazee Fulani waliokua wameketi chini ya Jaji, Kaptain hakuwajibu, akienda mpaka kwenye Jeneza hilo na kulifungua
TOBAAAAA
Alikua ni PABLO MWAKI
"Alikua akijaribu kutoroka Airport kwa njia hii ya kujifanya ni maiti, tumemkamata kwa ushirikiano wa maofisa wa Polisi wa pale uwanjani" aliongea kwa kujiamini Kaptain Makala.
Hapo ndipo nilipomvulia kofia Kaptain Makala, sikuamini tukio lile, nilijiuliza mara mbili kua aligunduaje mchezo ule,
Mahakama nzima alishtuka, haraka Mwaki akainuliwa, yeye mwenyewe hakuamini alichokiona, alikua akihema kwa mshangao na Aibu, na hopo sasa Mhe Jaji akaaihirisha kusikiliza kesi hiyo na kupanga tarehe nyingine tena ili kupata utulivu wa tukio hili, japo tulishajua kua hata yeye Johari nae ni katika wafuasi wa mtandao wa mwaki lakini tulimvutia tu Pumzi kwa ajili ya kujipanga kimapambano,
Watuhumiwa wote wakakabidhiwa kwa Askari magereza na msafara wa kwenda KEKO ukaanza huku wahudhuriaji wakitawanyika kwa mshangao na gumzo waliloliona mahakamani, Na mien a Ntahondi tukarudi kwenye gari zetu maalumu kwa ajili ya kurejea mafichoni kwetu!!!
Je nini kitaendelea?
Usikose mwisho wa riwaya hii ya kusisimua..
Ngekewa ram angelca chacha patrick showtie amina mabata mlyn Angelicious culbby muuza ubuyu princetx Giti VAN HEIST Mng'ongo chwechinyong Sangomwile