Riwaya: Shamba la hela

Riwaya: Shamba la hela

Niwashukuruni sana wasomaji wote tuliokuwa pamoja tangu mwanzo mpaka mwisho wa riwaya hii ya SHAMBA LA HELA.

Maoni na mitazamo yenu, nimevipokea kwa mikono miwili, tegemeeni mabadiliko hasa katika riwaya na simulizi mbali mbali zitakazokuja hapo baadae.

Ni jukumu langu kuujali sana muda wenu kwa kuwapatia kilicho bora.

Ndimi fanani wenu,
Godlove Kabati.
 
a9f939f9.jpg

Tukutane wakati ujao kwenye riwaya hii hapahapa JF...

Mshitue mwenzako, amshtue mwenzake! 😃
 
Amani na Upendo mwingi kaka.

KAZI nzuri, mnyumbuliko, mtawanyiko na muunganiko wa matukio ni wa kutukuka....Usanifu wa lugha na mpangilio wa sarufi ni wa ajabu. Hakika Fasihi umeitendea haki.
Mapungufu ni machache ila yanamezwa na mazuri mengi.

HESHIMA KAKA.
 
Amani na Upendo mwingi kaka.

KAZI nzuri, mnyumbuliko, mtawanyiko na muunganiko wa matukio ni wa kutukuka....Usanifu wa lugha na mpangilio wa sarufi ni wa ajabu. Hakika Fasihi umeitendea haki.
Mapungufu ni machache ila yanamezwa na mazuri mengi.

HESHIMA KAKA.
Oh! Asante sana ndugu yangu.
Nafanyia kazi mapungufu, wakati ujao nirejee nikiwa bora!
Shukrani sana.
 
Niwashukuruni sana wasomaji wote tuliokuwa pamoja tangu mwanzo mpaka mwisho wa riwaya hii ya SHAMBA LA HELA.

Maoni na mitazamo yenu, nimevipokea kwa mikono miwili, tegemeeni mabadiliko hasa katika riwaya na simulizi mbali mbali zitakazokuja hapo baadae.

Ni jukumu langu kuujali sana muda wenu kwa kuwapatia kilicho bora.

Ndimi fanani wenu,
Godlove Kabati.

Shukran mwandishi wa riwaya , kongole kwako riwaya imetulia 🫡
 
RIWAYA; SHAMBA LA HELA
MTUNZI; GODLOVE KABATI
WHATSAPP; 0763204351

SEHEMU YA TANO
'MZUNGU WANNE'

AKISHTUKA kutoka kwenye usingizi mzito, akagundua kuwa kichwa chake kilikuwa kizito na mwili wake ulielemewa kwa uchovu. Akajitahidi kufumbua macho yake, akaweza japo ilikuwa kwa taabu sana.
Mwanga mkali wa taa ulimuumiza kwa mara ya kwanza lakini akajitahidi kupambana nao akaweza.
Alikuwa amedhoofu na hata alipojaribu kujikusanya ili ainuke alishindwa. Akayatazama mazingira aliyokuwepo, asingeweza kuyatambua vyema kama tu usingizi na uchovu vingeendelea kumlevya. Akajipa sekunde kumi na tano za utulivu.
Akavuta pumzi na kuitoa nje, ndani kisha nje tena mara sita.

Kisha akawa makini tena na mazingira yale aliyokuwepo. Mara moja akaziona kuta zilizosilibwa vyema kwa simenti na kupambwa kwa picha za mtu aliyemfahamu. Akakaza macho yake pale, akagundua kuwa yule bwana pale pichani amemiliki sura yake yeye mwenyewe.
"Eboh! Nimefikajefikaje hapa nyumbani?!"
Akatamka huku akijikusanya kwa taabu pale juu ya kitanda. Yupo chumbani kwake na hajui ni namna gani amefika pale.

Akajiinua na kuketi juu ya kitanda huku mkono wake mmoja ukiushikilia ubavu wake wa kulia uliokuwa ukimuuma na mwingine ukikipapasa kichwa chake. Akawa hakumbuki lolote lile lililomkuta muda mchache uliopita.
"Auuu...subiri kwanza, nilifika saluni pale, halafu ikawaje sasa? Halafu sasa hivi ni usiku! Ina maana- Ah!" Akapata utata.

Jibu lake likajibiwa kwa kufunguliwa kwa mlango kutokea nje. Na Mtemi Moringo akaingia akiwa na mfuko ulioonekana kuvimba baada ya kupakiwa vitu fulani fulani.

"Eeeh! Aiseee angalau umeamka aisee. Sasa kwanza ule!" Mtemi akatamka huku akipambana kurudishia mlango wa chumba kile, uliokuwa na tabia ya kuleta ubishi linapokuja suala zima la kufungwa endapo tu mfungaji alikuwa ndani ya chumba.
"Weka chomeko tu hapo. Bila hivyo huufungi!" Akatamka Feruzi huku akiketi vyema juu ya kitanda kile.

Mtemi akafunga mlango na kufika mpaka juu ya meza ndogo iliokuwa ndani ya chumba. Akautua mfuko ule pale mezani na kupakua baadhi ya vitu ambavyo alitaka kuvitoa mule. Na vingine akaviacha ndani ya mfuko.

"Oyah! Hivi wewe nd'o umenileta hapa ndani?!" Feruzi akauliza.
"Yaani umedondoka kama mzigo we jamaa, PUUH! Tukakuzoa mpaka nje, pepea wee pepea wee, wapi! Nikaamua nikubebe mpaka hapa kwako aisee." Mtemi akamjibu huku akiendelea kuandaa chakula alichokileta.

"Yaani ina maana nimezimia? Kule saluni au? Hapana bwana...yani mimi nizimie." Feruzi akauliza swali na kujijibu mwenyewe huku akitoa tabasamu hafifu.

"Au sio? Em jiangalie vizuri kwanza. Halafu nd'o uje uongee utopolo wako huo. Haya jiangalie kwanza!". Mtemi akaiacha sentensi yake ielee, ili Feruzi ajitazame kwanza.

Feruzi akasimama kwa taabu na kujikagua mwili wake. Alikuwa na michubuko mikononi na alichafuka suruali lake kwa vumbi kiasi.
"Umezimia pale saluni. Nikamshtua Sele, akatuleta kwa taxi yake ile mpaka hapa!". Mtemi akamalizia ile sentensi yake iliyokuwa hewani.
Akaivuta ile meza mpaka pale kitandani na kumkaribisha Feruzi chakula.
"Kwa hio hata hukunipeleka hospitali. Yani nimezimia halafu we upesi ukanifikisha hapa?!" Feruzi akirejea kwenye kitanda akaketi huku akimtupia swali Mtemi.
"Tulia bhana, hayo yote tutayazungumza mzee." Mtemi akamjibu, kisha akaketi juu ya kitanda sambamba na Feruzi.
"Najua hujala tangu asubuhi, nd'o maana unazimiazimia ovyo. Haya kwanza njoo hapa tufinye halafu tutaongea vizuri make inaonekana umesababisha mabalaa leo!"

"Maba...mabalaa? Mabalaa gani hayo unayoyajua wewe?" Uso wa Feruzi ukabadilika ghafla. Nguvu zake zilizokuwa zimeenda likizo zikarejea kwa kasi mwilini mwake na uchovu ukapotea.

"Kula kwanza mzee...Hauna nguvu sasa hivi. Tuliza povu hilo ule halafu ukimaliza tutayaongea tu haya!" Akasisitiza Mtemi huku akiviringa tonge kubwa la ubwabwa kwenye kiganja cha mkono wake wa kulia.

"Aisee..ucha utani Mtemi. Yaani kama kuna kitu-". Akakatishwa.
"Kula hilo chee kwanza, halafu ujue huyo samaki nimemnunua buku tatu!" Ni mtemi ambaye anatamka, shavu lake likiwa limevimba na bado anajiandaa kuchovya tonge kubwa la ubwabwa kwenye mboga ile ya samaki aliyeungwa vyema kwa supu nzito.

Feruzi akaacha kulalamika na kuanza kula. Alimfahamu vyema rafiki yake namna ambavyo hakuwa na utani linapofika suala la kula naye kwenye sahani moja. Akaungana naye na kukifakamia chakula chote kilichokuwepo kwa pupa. Njaa iliokuwa inamtishia uhai wake ikamkimbia. Baada ya mlo wakanywa maji ya kutosha na kutulia.

"Kwenye koti lako kulikuwa na vitu vyangu viko wapi?" Feruzi akahoji.
Mtemi akamtazama kwa sekunde nne kisha akasimama na kuinama chini ya kitanda kile. Akaibuka na begi lake ambalo alilifungua na kutoka na mfuko mdogo mweusi.
Taratibu akatoa mabunda mawili ya noti za shilingi elfu kumi. Akayaweka juu ya meza ile ndogo.
"Nitataka maelezo juu ya huu mpunga wote halafu..."
Akatia mkono wake na kuibuka na leso iliokuwa imechafuliwa kwa damu. Hii aliishika kwa vidole viwili, cha kati na gumba kama mtu mwenye kinyaa. Akakiweka mezani pia.
"Nitataka na maelezo juu ya hiki kitambaa." Akatamka akiwa ameukunja uso wake kwa uchungu.

Ukimya wa haja, ukachukua umiliki ndani ya chumba kile kwa sekunde kadhaa. Kisha kwa utulivu wa hali ya juu, Feruzi akatamka kwa sauti ya kunong'ona,
"Nisikilize Mtemi." Akatoa leso ile mezani na kuirudisha ndani ya mfuko ule kisha akaurudisha chini ya kitanda.

"Nakusikiliza hapa, yaani nataka uniambie ulienda kufanya nini leo na pikipiki yangu aisee. Kama uliteka watu au uliua uniambie!" Mtemi akatamka akiwa na hamaniko.

"Tulia Mtemi tulia." Feruzi akatamka kwa kunong'ona tena. Kisha akasogea mpaka karibu na dirisha la chumba kile akahakikisha kuwa hakuna mtu aliyekuwa akiwasikiliza kwa nje akalifunga vizuri. Akafanya hivyohivyo mlangoni.
Akarudi kitandani,
"Mambo niliyoyaona jioni hii ya leo ni ya ajabu na ya kutisha sana mwanangu!" Akameza funda la mate kisha akaendelea,
"Nitakueleza mwanzo mpaka mwisho lakini sharti ni moja tu. Hii siri nataka isitoke nje ya hizi kuta nne." Akaweka angalizo.

Feruzi akamsimulia Mtemi kisa chote, namna alivyokutana na masaibu huko porini. Mpaka namna alivyopata zile fedha na akapewa zawadi ile ya leso yenye damu na yule bwana mwenye suti.
Mpaka anamaliza kusimulia mkasa wake, Mtemi alikuwa ametoa macho yake kwa woga!

"Wewee!" Akamtamka akiwa mwingi wa hofu na mshangao.
"Eeh nd'o hivyo mzee, nadhani kama nimepona kifo leo pale msituni. Basi sitakuja tena kufa kwenye mazingira ya kutisha nakuapia aisee." Akafuta jasho lililokuwa likimtiririka usoni mwake.

"Aiseee!" Bado Mtemi yuko kwenye mshangao bado amemtumbulia macho Feruzi.
"Kwahiyo huyo abiria alikuwa anaenda kuuawa kule msituni? Na akakutumia wewe."
Akamuuliza.

"Yaani mpaka mimi sielewi. Wamenicharaza makofi ya kutosha aisee..mgongo wangu ulikuwa kama ngoma ya bendi leo!" Akajibu huku akiupapasa mgongo wake.

"Yale majamaa yanajiita Dubu sijui? Yale ni majianti aisee sijawahi kuona! Yani sijui yanakula vyakula gani yale!" Akazidi kulalamika.
"Kwani wamehaidi kukufatilia tena?"
"Duh! Hapana aisee. Sema yule jamaa mwenye suti kanambia nisome Biblia sijui, Zaburi ya ngapi ile, thelathini kitu kama hicho. Eeh Zaburi ya thelathini!" Feruzi akatamka kwa unyonge.
Mtemi akatabasamu kwa mara ya kwanza.
"Yaani majambazi yamekuagiza mpaka usome baibo? Aisee Hehehehe...ili kweli kubwa kuliko." Akasindikiza sentensi yake kwa kicheko. Kicheko cha huzuni.
"Unaweza dhani anatania mwanangu, yaani jamaa akishavua tu miwani yake. Anakuwa hana utani tena! Kama utani tu kanambia nisome Baibo mzee. Zaburi ya 30, eti nimeokoka kifo leo. Nikamshukuru Mungu!" Feruzi akanong'ona. Bado Mtemi anacheka kwa masihara.
"Yaani we unacheka! Oyah. Ukiwa mbele ya huyo jamaa, utalia sana. Sikumbuki mara ya mwisho nimelia lini. Lakini leo aisee nimetoa machozi kama mtoto. Usicheze na uhai kabisa!"
Mtemi akajikakamua kisha akasema,
"Naelewa naelewa, lakini em tuwe wakweli. Wewe mara ya mwisho kuona Biblia ni lini? Tuwe wakweli kabisa kwenye hili. Wewe Feruzi tangu lini umekuwa na urafiki na Biblia?!" Bado sauti yake ina kicheko, Mtemi akazidi kumtania rafiki yake.
"Kesho ni Jumapili. Bahati nzuri kanisani sio mbali, nenda kasali aisee. Toa sadaka! Halafu umuombe mtu baibo upitie hicho kifungu kitakatifu! Hehehehe." Akarejea kwenye kicheko.
Feruzi akatamka moyoni mwake,
'Huyu bado hajakutana nao wale kina Dubu.. Hawajui vizuri huyu.'

Mtemi akahamisha macho yake kutoka usoni kwa Feruzi na kutazama juu ya meza ile,
"Ulipozimia, sikukupeleka hospitali haraka kwa sababu nilipokukagua nilikutana na hivi vitu. Nikajua tu kuwa kuna mabalaa umeyafanya!" Mtemi akatia nukta.
"Una uhakika kuwa hakuna mtu yeyote yule ambaye amekuona ukivitunza hivi vitu aisee?" Feruzi akamuuliza kwa woga.
"Hakuna aliyeniona, nina uhakika wa asilimia mia moja!" Akatetea hoja yake.
"Kweli?!"
"Sasa ni lini nimewahi kukufelisha mzee baba? Hakuna aliyeniona yaani nilikuwa mimi na Mungu wangu." Akajigamba.
Feruzi akashusha pumzi kwa uchovu.
Akaokota bunda moja pale mezani na kulipima uzito wake,
"Kumbe milioni moja huwa inalingana hivi. Yaani hii nd'o kidogo initoe uhai leo." Akatamka huku akichezea bunda lile mkononi.
"Enhe utazifanyia nini sasa hizo hela?" Mtemi akamkandamiza kwa swali.

"Duh! Yani bado siamini amini kama wamenipa hizi hela burebure yaani. Make yule fala alinipatia kwa vitisho sana." Feruzi akanena.
"Enhe alisemaje kwani."
"Alinambia kuwa hizi hela ni haramu! Na zimetokana na shughuli zisizo za halali. Nikizitumia vibaya zitanipoteza. Sasa hapo nd'o sikumuelewa kabisa."
"Mmh mmh...Oyah kwani hizi ni hela za kishirikina? Make nasikia zile huwa zinamtokea mtu puani." Mtemi akajibu kwa hamaniko huku akiketi vyema pale juu ya kitanda.
"Huenda ni hivyo...make hata alipozitoa sikuelewaelewa, walizichimba kutoka ardhini mzee. Huwezi amini yaani. Zilichimbwa kutoka ardhini! Halafu ni kama kwao ni kitu cha kawaida kabisa!" Feruzi akajibu huku akitetemeka mikono yake.
"Unasemaje? Yaani hela wanazichimba ardhini? Kwa jembe au?" Maswali mfululizo yakamtoka Mtemi.
"Eeh mwanangu, kwa jembe. Sa sijui walizifukia pale. Yaani kama wanavuna karanga tu. Jembe moja chwaa, la pili chwaa chwaa, wanaibuka na burungutu." Akatamka Feruzi.
Mchoro wa eneo hilo ukajichora kichwani kwa Mtemi kwa haraka sana.
"Yaani ujue unaniacha njia panda! Yaani unamaanisha wanafukua hela. Au wanachimba hela kama mazao?" Akauliza kwa sauti yenye mshangao.
Feruzi hakumjibu. Badala yake akakusanya kitita kile cha fedha na kukitunza chini ya godoro lake pale kitandani kisha akajilaza kitandani na kujinyoosha.
"Hii inaonyesha hawa watu wana utajiri mkubwa sana. Yani wamekuteka kimakosa halafu wanakuzawadia milioni mbili? Tena wanachimba kutoka ardhini yaani kama karanga umesema." Bado Mtemi anaongea peke yake.

"Oyah leo utalala hapa mzungu wanne au niaje? Make ni kama usiku umeenda sana." Feruzi akabadilisha mada hewani.
"Hapa..nitalala hapa leo!"

"Poa mzee mi ngoja nilale. Siku ngumu sana hii, siku nyeusi. Sirudii tena kuwa sekido aisee, pikipiki yako ina gundu." Akajilaza juu ya kitanda.
"Duh lala tu jamaa yangu. We leo umeona mambo mengi mara Dubu! Mara Jamaa mwenye sura mbaya, mara hela za ardhini. Aisee!" Feruzi akanena huku akijilaza pembeni ya Feruzi ambaye usingizi ulimchukua punde tu baada ya kujitupa pale kitandani.

Mtemi naye akalala kando katika mtindo uleule maarufu kwa jina la 'mzungu wanne', uso wake ukitazamana na miguu ya Feruzi iliyokuwa inalalamika kutooshwa kwa muda mrefu ikitoa harufu mbaya.

"Mm..oyah Feru eeh! Halafu kesho ukiamka piganisha uoge aisee. Make kilichoko huku aisee, ni changamoto!" Akalalamika huku akiugeuza uso wake upande mwingine na kutazama na ukuta.
Akili yake inawaza juu ya ardhi hiyo ya ajabu ambayo inachimbwa na kutoa hela kwa mafungu ya milioni milioni. Alichelewa sana kulala, mpaka pale usingizi ulipoona kuwa inatosha. Ukamlevya na akalala!

************

Giza jepesi limekifunika chumba kidogo kinachofanania na ofisi.
Kinafanania na ofisi japo mapambo yake hayana uhusiano wowote ule na ofisi. Ni meza, kiti pamoja na vitabu kadhaa vinavyokipa chumba hiki walau sifa kadhaa za kuitwa ofisi. Japo chumba kama kama chumba, kilikuwa ni kama ghala ndogo ya silaha za moto.
Kikimiliki makasha kadhaa ya risasi mbalimbali pamoja na mitutu ya bunduki ikiwa imetundikwa kwenye kuta zake.
Ukimya ukitawala ndani yake na kusababisha hali ya utulivu wa hali ya juu. Utulivu ambao unapafanya mahali hapa paonekane kama hakuna kiumbe hai chochote kile.
Jambo ambalo sio kweli!

Kwa maana nyuma ya meza hii kubwa ya duara iliyo ndani ya chumba hiki, kuna kiti ambacho kimekaliwa na kiwiliwili cha mtu mkubwa kiumbo. Akiwa amevaa suti nyeusi na kofia kubwa iliyoufunika uso wake kiasi cha kusababisha kivuli kiufiche uso wake.
Mikono yake iko juu ya meza akiwa kimya kama mtu anayesubiria kitu au taarifa fulani.
Na ghafla simu yake ya mezani inaita,
Bila papara, anaiokota na kubonyeza kitufe kuruhusu sauti ya mpigaji irindime masikioni mwake.
Na sauti ile inaonekana kumjibu kwa maneno fulani fulani ambayo anayasikia na anayaelewa yeye mwenyewe na mpigaji.

Hamjibu na badala yake anaokota kalamu ya wino pale mezani na kuchana kipande cha karatasi kutoka kwenye daftari mojawapo.
Kisha ananakiri kile anachoambiwa,

"Hii namba una uhakika nayo?" Anauliza kwa sauti nzito na hana haraka kwenye kuongea maneno yake.
"Ndio mkuu, na sio tu namba! Mpaka picha nimechukua." Sauti ile ikamjibu.
"Safi sana, najua kuwa umechukua tahadhari na hakuna mtu yeyote aliyekuona!" Mtu huyu wa miraba minne akatamka tena.
"Sure mkuu! Sijafanya mistake yoyote ile!"
"Well done!" Akakata simu ile.

Kisha akakitazama alichokuwa amekinakiri juu ya karatasi kwa sekunde kadhaa. Kisha akatamka kwa kunong'ona,
"Hauna maisha marefu sana Franko! Nitakufikia na zawadi nzuri sana ya kifo chako huku nikitabasamu. Damu yako ni halali yangu! Bado sentimeta chache tu. Bado sentimeta chache kukufikia ulipo, Franko Dario!"
Akatia nukta na kuitunza karatasi ile katikati ya vitabu vyake.
Kisha akasimama na kuondoka ndani ya chumba kile kidogo chenye giza. Akafunga mlango wake kwa funguo na kuacha ukimya uliopambwa kwa giza jepesi, kufuatia maneno yake ya vitisho aliyoyanuia kwa mtu aliyemfahamu!


Itaendelea...
good
SHAMBA LA HELA
Imetungwa na Godlove Kabati.
WhatsApp 0763204351.

SEHEMU YA KWANZA;

FEROOUZ HAIR CUTS


Bukoba, Kagera
Jumamosi, saa kumi jioni.


KITENDO cha kukatika kwa umeme kiliuzika uchangamfu na kufufua hali ya kupooza kwenye genge la mtaa huu.
Hii sio hali ya kawaida kabisa,
Yaani kwenye genge la mtaa huu wa Buyekera mida kama hii ya jioni kuwa kimya namna hii?
Kwa kawaida, imezoeleka hali ya uchangamfu wa anga linalotetemeshwa kwa kelele za hapa na pale.
Duka lile utasikia midundo ya muziki murua wenye ladha ya Amapiano. Mara pale kwenye maduka ya kanda za video utasikia namna spika zinavyoshindana kupaza sauti za watafsiri wa filamu mbalimbali kutoka n'gambo.
Kule utasikia vipaza sauti vya wapiga minada kusifia upungufu wa bei za bidhaa zao. Na vibanda-umiza navyo havikutaka kuachwa nyuma, hupaza sauti za watangazaji mbalimbali wa mechi.
Ni kelele mtindo moja, ili mradi tu kila mfanyabiashara, biashara yake isikike vyema zaidi ya mwingine.
Genge hili kubwa hugeuka kuwa gulio dogo. Leo mambo ni tofauti kabisa. Genge limepoa!

Kupooza huku kumefifisha hata idadi ya wanunuzi na wachuuzi mahali hapa. Kwa kawaida ardhi hii hukusanya watu wengi sana muda kama huu. Ardhi hupata suluba sana kuzibeba nyayo za viumbe hai wanaotembea juu yake. Lakini leo hali ni tofauti kidogo, genge limepoa sana. Ni kama watu wamelisaliti genge la mtaa huu.

Hakukuwa na tangazo lolote lile juu ya kukatwa kwa umeme kwa muda mrefu namna hii. Wakazi wa eneo lile walikubali kukosa umeme kwa siku moja, wakaukosa siku ya pili na sasa hii ilikuwa siku ya tatu. Siku tatu bila umeme!
Maswali na lawama vikawa vingi kwa serikali yao, lakini majibu waliyopewa yalikuwa yaleyale waliyozoea kuyasikia siku zote,

"Kuna matatizo ya kiufundi. Ambayo yanafanyiwa kazi" . Walijibiwa hivyo.

Adha hii imeyumbisha biashara za wale waliotegemea sana umeme ili kuuza bidhaa au ujuzi wao.
Tatizo hili likawa kama ngumi ya pua kwa wale wafanyabishara wasioweza kumiliki majenereta ya umeme, na shughuli zao zilitegemea umeme ili wapate kipato.

******

Nje ya jengo dogo mfano wa kibanda, kilichonakshiwa kwa rangi na mchoro mkubwa wa aliyekuwa msanii maarufu wa marekani, Tupac Shakur.
Maneno makubwa yanasomeka pale juu ya mlango wa banda hili la mbao,
FEROOUZ HAIR CUTS.

Kijana mmoja wa kiume anaonekana kuketi umbali wa hatua nne hadi tano nje kidogo kutoka kwenye banda hili. Yeye pia akiwa mmoja miongoni mwa wahanga wa tatizo hili la kukatwa kwa umeme. Ikiwa ni siku ya tatu hii amefungua saluni yake bila kutoa huduma yoyote ile.
Amekaa juu ya benchi, ameegemea ukuta wa nyumba iliyokuwa mkabala na saluni yake.

Ameketi kuuelekea mlango wa ofisi yake hii uliokuwa wazi. Ni mtulivu ameifumbata mikono yake, macho mbele ameitazama taa ndani ya saluni yake.
Alikuwa amewasha swichi akitarajia kuwa taa ile itawaka mara tu umeme utakaporudi kutoka huko ulikokuwa umeenda kutalii. Lakini taa ikabaki kimya ikinin'ginia juu ya dari.

"Aah kudadek!", ilimtoka kinywani mwake.
"Wana nini hawa?". Haikujulikana kama anajiuliza swali au alikuwa analalamika.
"Hivi wanataka tule mchanga? Au wanataka tule mwanga wa jua kama Jadu. Yaani siku ya tatu hii wamekaa kimya tu. Sema ngoja! Wata-", hakuimaliza sentensi yake.
Aligundua kuwa hata akilalamika vipi, hatakuwa na namna yoyote ile ya kuiumiza serikali.
Kwani ni matatizo mangapi yamewahi kulalamikiwa na bado wakaishi humohumo?
Alibaki kufyonza tu.
Lilikuwa sawa na dua la kuku, lisiloweza kumpata mwewe.

Anasimama na kupiga hatua tano kuingia ndani ya banda hili. Amefika ndani na kunyanyua chupa yake kubwa ya maji ambayo ilikuwa na maji nusu ya ujazo wake kamili. Anazungusha mfuniko wake kulifungua lakini anakatishwa baada ya kusikia sauti ya muito wa simu mfukoni mwake.

Anaachana na chupa la maji, anachukua simu yake na kutazama jina la aliyempigia. Mara anaishusha chini simu yake akiwa amekunja ndita usoni kwa hasira. Akaiacha iendelee kuita, huenda huyu aliyempigia amemuudhi au hakutaka kuongea naye kwa muda huo...

"Huyu demu naye atakuwa anataka hela tu sa'hivi , sijui kwa nini nilimuahidi?"
Akajisemea peke yake,
"Sipokei simu yake!"
Akaamua kupiga mafunda kadhaa ya maji kutoka kwenye chupa lile.

Mara ikasikika sauti ya mtetemo wa pikipiki ambayo ilikuwa ikijongea kuelekea jengo lake la saluni lilipo. Mtetemo ule ukazimika ghafla, karibu zaidi na saluni yake. Hii ikamjulisha kuwa kuna mtu yupo nje ya saluni.

Akajaribu kuchungulia nje kupitia dirisha lake dogo, ili aone ni nani huyu aliyesimama nje ya saluni yake, huenda akawa mteja ambaye hakumtarajia kuwa pale muda kama huu.
Alichokiona kilimfanya atabasamu.
"Kijana Mtemi Moringo...naona mambo sio mabaya sana!" Feruzi akapaza sauti yake, ambayo ilimfikia yule mtu pale nje, aliyejulikana kwa jina la Mtemi. Na yeye akatabasamu.
Mtemi akapaki pikipiki yake vizuri kisha akaanza kujongea kuingia ndani ya saluni.

"Oyaaae kijana Feruzi niaje hapa!" Akasalimiwa na huyu mgeni.
"Aah kaka, jau jau tu." Kijana huyu aliyejulikana kwa jina la Feruzi akamjibu kwa sauti iliyotangaza unyonge.

Mtemi akavua koti lake kubwa na kulitundika juu ya msumari mmojawapo uliochomoza kwenye ubao. Akaweka helmeti yake kwenye kiti kilichokuwepo pale ndani.
Kisha akajongea moja kwa moja mpaka mbele ya kioo kipana kilichokuwepo pale ndani, akachagua chanuo kubwa la nywele miongoni mwa vingi vilivyokuwepo pale kwenye shubaka. Akaanza kuchana nywele zake nyingi kichwani, zilizokuwa kwenye mtindo wa Afro, huku akijitazama kwenye kioo.

"Umeme bado hujarudi tu?!" Akatupa swali huku akiendelea kugeuzageuza kichwa chake mbele ya kioo.

"Yaani acha tu bro, siku ya tatu leo...wanataka tuwalambe miguu yao sijui?" Feruzi akatamka huku na yeye pia muda huu akiwa amekigeukia kioo akiitazama taswira yake...ambayo ilimkasirikia kama alivyokuwa amekasirika yeye.

"Lakini nasikia kuna nguzo imeanguka kule juu maeneo ya Kibeta! Huenda nd'o wanashughulika nayo muda huu" , akasema Mtemi.
"Nguzo? Ina maana muda wote huu tangu juzi wameshindwa kubadilisha? Hawajui kuwa watu huku tunakula upepo?" Feruzi, akaongea tena kwa makasiriko.

"Nd'o serikali yetu hio... siku zote mwenye shibe hamjui mwenye njaa."

"Aah hata kama bhana...unaona hapa mwanangu, leo tumbo langu halijasalimiwa na chakula chochote kile. Na sioni hata hela ya kununua hicho chakula napata wapi." Feruzi akaanza kuangusha malalamiko yake.

"Eboo! Kumbe nd'o maana una hasira. Hii yote ni kwa sababu ya njaa!" Mtemi akayasindikiza maneno yake kwa kicheko dhaifu, kilichoudhibitisha utani uliokuwepo tangu siku nyingi baina ya marafiki hawa wawili.
Maneno yake yakamfanya Feruzi ashindwe kujizuia na yeye akacheka. Japo kicheko chake kilionyesha wazi kuwa amechoka na ana njaa!

"Nimezoea muda kama huu tena wikendi! Wateja kibao sana, halafu nikifika huwa unanifukuza we fala!" Mtemi akatupa kauli nyingine ya utani.

"Duh! Hapa mwanangu unanionea! Lini nimekufukuza wewe. Wakati humu umepafanya kama sebule yako, tena huwa nakunyoa bure kabisa!" Feruzi akajitetea.

"Aah wapi we mshikaji huwa unatukataa wahuni. Sema hamna mbaya, ngoja nenge ikunyooshe kwanza! Hahaha"

Feruzi akasogea karibu na koti lililokuwa limetundikwa pale kwenye ubao.
Akalichukua na kuanza kulivaa kabla Mtemi hajamshitua,
"Oyah wee, namna gani tena? Wapi na koti langu tena"
Feruzi akalivaa koti kimya, kisha akasogelea helmeti iliokuwepo pale juu ya kiti. Akiokota na kuivaa kichwani mwake.
Muda huu wote Mtemi amemtumbulia macho akimshangaa, hajui ni nini rafiki yake amepanga kufanya.

Feruzi akamaliza kuvaa akiwa kimya. Halafu akamsogelea Mtemi na kunyoosha mkono wake,
"Em nipe funguo hapo chap, nikatafute chochote kitu."
Mtemi akaa kimya kwa sekunde tatu kisha akaangua kicheko.
"Kwa hio umeamua kuwa Sekido!" Akatamka Mtemi huku kicheko kikiendelea kumyumbisha.

(Sekido ni jina rejesta itumikayo katika jamii za wahaya, kumaanisha dereva pikipiki au bodaboda kama ilivyozoeleka na wengi)

"We leta hio kii, nikabebe wateja wawili watatu. Nipate chochote kitu." Feruzi akaendelea kusisitiza.
Ghafla simu yake ikaita tena, wote wakageuza shingo zao kutazama ni nani huyo aliyepiga.
Simu ikiwa juu ya shubaka, wakasoma jina 'Alinda'.
Wote wakatazamana na vicheko vikalipuka tena kutoka vinywani mwao.
"Unaona? Demu huyo hapo kanipigia tena, hii mara ya pili. Nilimuahidi afu tano tu ya kusuka ndo ananidai utadhani kanikopesha!" . Kwa utulivu Feruzi akajongea na kuikata simu ile, kisha akabonyeza kitufe chake kimojawapo ili aizime kabisa. Ikazimika!

"Khaa! Ndo unazima simu kabisa?" Mtemi akatoa kauli ya mshangao, bado yumo katika hali ya kicheko.
"Yaani mi sijui leo nitakula nini....halafu nimpatie demu hela ya kujiremba?! Au anadhai mi nitakula nywele zake." Akajibu Feruzi.
"Mademu zenu hao; mkiwa mnawaita gheto kuwakamia wakiwaomba hela msiwanyime! Hata hivyo ahadi ni deni."
"Eeh bwana ee...we nipe funguo nisepe bhana. Masuala ya mademu zetu tuachie sisi wenyewe!" Kwa kukasirika kidogo, Feruzi akadai funguo isiyokuwa yake ili mradi tu abadilishe mada.
Bila kusita Mtemi akachomoa funguo kutoka kwenye mkanda wa suruali lake na akampatia Feruzi huku tabasamu likiupamba uso wake.

"Kwani nina baya basi mzee? Chukua funguo hizi hapa. Nenda ukashindane na upepo sasa, tutakuokota ukiwa mifupa!!"
"Aweee tulia bhana, fundi mimi. Haya mambo madogo madogo."
"Umezoea kushevu watu tu hapa...unapindisha mashine huku na huku, kazi simpo sana hizi. Nenda kafanye kazi za wanaume barabarani mdogo wangu!" Mtemi akatamba.

"Kazi simpo eh au sio? We nikikuacha hapa hata kwa masaa mawili tu. Utatoka umevimba mikono." Feruzi akamjibu huku akipokea ufunguo ule uliokuwa umeunganishwa barabara kwenye ringi ambayo ilikusanya jumla ya funguo nne, zilizoshindana kupiga kelele kila zilipogongana.
Feruzi akatoka nje akimuacha Mtemi ndani ya saluni.

"Kwa hiyo unarudi saa ngapi sasa?",.Mtemi akapaza sauti.
"Tulia bhana....sichelewi!" Akajibiwa.
"Angalia basi usinipaki humu ndani." Akapaza sauti yake tena akilalamika japo hakuwa na hasira.
Hakujibiwa!
Alichokisikia zaidi, ni muungurumo wa ghafla na mtetemo wa sauti ambavyo vilitosha kumjulisha kabisa kuwa pikipiki imewashwa. Halafu akasikia tena sauti ile ya mtetemo ikiishia, Feruzi aliondoka na pikipiki yake.

Akachungulia dirishani kumsindikiza kwa macho mpaka alipopotea kwenye upeo wa mwisho wa macho yake. Kisha akatabasamu!
Tabasamu lake daima liliupamba uso wake, lilikuwa tabasamu ambalo halikueleweka kama lilitafsiri furaha au huzuni moyoni mwake.

Akatoka dirishani, akaketi kwenye kiti kikubwa ambacho hukaliwa na wateja wanaponyolewa.
Akastarehe kwa kuegemeza mwili wake huku akijizungusha huku na huku. Macho yake yakilikagua dari la saluni ile.
Akawaza mambo mengi sana, kuhusu yeye na rafiki yake.

Alimuamini sana na rafiki yake,
Ni mambo mengi wamesaidiana na wameyafanya pamoja tangu walipokutana hapa mjini wote wakiwa katika utafutaji. Yeye akiwa kama dereva bodaboda na Feruzi akiwa kama kinyozi. Namna yao ya kukutana ilikuwa ya ajabu, ajabu sana!
Alipotaka kuikumbuka tu,
WAAH!

Mwanga mweupe wa taa kubwa ukammulika usoni mwake. Akafumba macho yake kuukwepa. Umeme ulirudi!
Ghafla! Ndani ya sekunde chache tu, mziki mzito ukaanza kuunguruma ndani ya saluni ile.

"Aaargh, huyu naye alikuwa hajazima spika yake!" Akasimama kuelekea ilipo spika ili afanye alichotaka kufanya ambacho mimi na wewe hatukijui.
Labda alitaka kubadilisha mziki ule au kupunguza sauti au kuzima kabisa. Tumshangae tu!

Kabla hajamaliza hatua yake ya pili tu, saluni ikapata ugeni mpya. Watu wawili wakaingia wakihitaji kunyolewa. Mtemi hakupata nafasi ya kusema lolote la kuikana saluni hata kidogo, wakaongezeka watoto watatu walioonekana kuwa wa shule ya msingi .
Ikawa ni kama watu walikuwa karibu na salumi ile wakisubiri umeme useme wiiii na wao waitikie waaa, waingie ndani yake.
Tayari ulikuwa umesema wiiii na sasa wamo ndani.

Mtemi akakasirika lakini hakuwa na namna. Ilibidi amsaidie kazi rafiki yake ambaye kaenda kutafuta pia. Ilibidi wabadilishane kazi kwa muda kidogo.
Hakuwa mgeni katika kazi hii ya kunyoa watu, alikuwa na ujuzi kidogo wa kucheza na mashine ile ya kunyolea. Akavaa aproni akawasha mashine na kuanza kusuguasugua vichwa vya wateja kuondoa nywele zao.

Alikuwa na ujuzi japo hakuwa na uzoefu. Mkono ukaanza kumuuma akajizuia sana asitetemeke kuharibu vichwa vya wateja hasa wale walioonekana wanazijali sana nywele zao kuliko vichwa vyenyewe.
Kazi aliioiita 'simpo' ikamfanya avuje jasho apate na mafua ambayo hakuwa nayo dakika kumi tu zilizopita.

Tukutane wakati ujao....
Kujua ni nini kitajiri.View attachment 3250471
good
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom