Riwaya: Sahii ya kifo

Riwaya: Sahii ya kifo

SEHEMU YA KUMI NA SITA
Siku kama hiyo ya jumamosi chuoni hapo kuna
kuwa na disko ndani ya ukumbi wa chuo na
baadhi
ya wanafunzi huwa wanachaguliwa kucheza
nyimbo za aina mbalimbali ilikuonesha uwezo
wao
na vipaji vyao,
Rafiki zake na victoria waliweza kugundua kuwa
victoria ameanza kumpenda david hivyo walianda
mpango na kuongea na wanachumba wenzie na
david kuwa itakapofika muda wa kucheza basi
david acheze na victoria na wengine waliobaki
watacheza na wao,
Swala hilo lilionekana jema sana kwa washikaji
zake na david maana waliona sheshe kaingia
kwenye kichaka cha simba hivyo hakuna jinsi
zaidi
ya kumlarua tu na kumla nyama, mpango huo
ulikubalika,
Mida ya saa mojamoja hivi usiku wanafunzi
walionekana kujiandaa vyema, wenye kuazima
nguo waliazima, na wenye kugongea marashi
waligongea ilimradi kila mtu aonekane maridadi
siku hiyo mbele ya wavulana na mbele ya
wasichana ndani ya ukumbi huo,
Mipango yote hiyo wakati ikiendelea david
hakuwa
na taarifa yoyote ile, yeye alijiandaa kawaida
maana hakuwa mpenzi sana wa mziki na
mipango
yake ilikuwa ni kwenda kuangalia kwa muda tu na
kumuona mtoto victoria kisha arudi zake bwenini,
sauti ile ya mziki uliokuwa unasikika ukumbini
ulianza kuwa kusanya watu eneo lile.wengi
walipendeza na nguo zao za anasa,wengine
walionesha mizuka yao kwa kucheza nje hata
kabla
ya kuingia ndani acha wale waliokuwa
wamekumbatiana kwenye giza wakiendelea na
mambo yao ya ajabu ambayo haya stahiri
kuonwa
na watoto,
yote hayo david aliyaona na kubaki kusikitika tu
na
kuendelea kuzunguka kumtafuta victoria, wakati
akiwa anashangaa ghafla alikuja msichana
mmoja
kwa nyuma ,hakika alikuwa mrembo sana,
akamshika kiuno david hali iliyomfanya ageuke
kwa
haraka sana, kitendo kile cha kugeuka haraka na
yule dada alikuwa anataka kumkumbatia basi
wakajikuta wanadondoka chini na yule dada
akiwa
juu ya david,,
watu waliwazunguka na kuanza kuwa pigia
makofi
hata wale waliokuwa mbali walitamani kutaka
kujua kuna nini eneo lile hivyo nao hawakusita
kusogelea,
umati huo uliokuwa unasogea alikuwepo na
victoria pia, ndani ya dakika chache kila mtu
aliweza kushuhudia kitendo kile na yule dada
alifurahi sana kwa tukio lile maana alikuwa
kajipatia umaarufu mkubwa kumkumbatia
mwanaume asiye kuwa na mpango na wanawake
halafu anapendwa na wengi,
david alijitahidi kumsukuma yule dada pale chini
na akafanikiwa, alinyanyuka kwa hasira na
kuanza
kuwasukuma watu wampishe ili apite andoke
zake,
alipo wamaliza ghafla mbele yake akamuona
victoria aliyekuwa anataka kuanza kulia,
kwakuwa kila mmoja alikuwa anampenda
mwenzie
hivyo nyuso zao ziliteseka kwa aibu na victoria
kuanza kukimbia eneo lile na david kumfuata kwa
nyuma, watu hawakuelewa kinachoendelea zaidi
walizidi kushangilia tu kwa kujionea filamua ya
mapenzi ya bure,
Victoria alikimbia mpaka akapotezana na david,
hivyo david akawa anazidi kumtafuta maeneo
yote
yale ya chuo lakini hakumuona kwa muda huo
Hasira za victoria zilimpeleka mpaka kwenye stoo
ya chuo ambayo ilikuwa na kiza na kuanza kulia,
alijilaumua sana kwa kuchelewa kumwambia hisia
zake mwanaume aliye mpenda kwa muda mfupi
na
akiwa ndani ya maumivu alilia sana huku
akiendelea kufikiria na maneno ya upweke
yakamtoka,,,,
“”nani ambaye atauokoa moyo wangu kwenye
mafuriko haya ya machozi eeh jaman nimechoka
kuwa mtumwa wa kumtumikia bwana maumivu,
nani aje kuwa mkombozi wangu na kunifariji kwa
kipindi hiki kigumu eeh?
Victoria alijuta kuwa na moyo wa upendo kwa
kuwa ulikosa mtu wa kuutunza, machozi hayo
alimkumbuka mtu aliye kuwa na ahadi naye ya
kukutana, na aliya kumbuka maneno matamu
aliyokuwa anatumiwa hivyo alihisi moyo wake
unaweza kupata faraja kupitia mtu huyo bila ya
kujua mtu mwenyewe ni david aliyempenda bila
kumwambia pia ndiye aliye mfanya yeye kuwa
mahali hapo ambapo si salama kwa usiku huo,
Victoria hakuwa na budi kuanza kulitafuta jina la
mtu huyo kwa jinsi alivyo liweka yeye ili ampigie
waonane, wakati anaendelea kulitafuta kumbe
david alikuwa amekaribia maeneo hayo ya stoo
na
alishtushwa na mwanga wa simu uliokuwa
unaonekana kule stoo na hisia zikaja huenda
atakuwa victoria hivyo ikabidi aufuate ili awe na
uhakika kama kweli ni victoria,
David hakuchukua muda mpaka kufika kwenye
mlango wa stoo na alianza kuchungulia mle ndani
na kugundua kuwa yule ni victoria kwa kusaidiwa
na ule mwanga wa simu uliokuwa unammulika
mrembo huyo ambaye david mwanzo alimuita
Qeen
tz,
kabla victoria hajalipata jina la mtu anayetaka
kuonana nae ghafla rafiki yake akamtumia ujumbe
ulikuwa unamuuliza,
“uko wapi”?
victoria alisonya na kuendelea kutafuta jina la
mtu
wake bila kujibu ujumbe huo ndipo rafiki yake
huyo
akaamua kumpigia na wimbo uliokuwa unaita ni
huu,,,,,,,
“I’m so lonely broken angel”
“I’m so lonely,listen to my heart”
“one and only broken angel”
“come and save me, before I fall apart”
Victoria pia hakuweza kupokea hata hiyo simu
mpaka nyimbo hiyo iliyoendana na upweke
alionao
ma iliyomuongezea machozi ilipo kata yenyewe,
David aliusikia wimbo huo pale nje na kilio cha
mtoto mzuri victoria ndipo alipojitokeza na
maneno
matamu ya mahaba yalitoka kwa sauti inayo
sisitiza upendo,,,,,
“niko hapa kukutoa upweke ulionao”
Sauti hiyo iliushtua sana moyo wa Victoria
alitamani kumjua huyo mtu aliye ingia humo
ndani
japo alihiisi kama sauti anaifahamu vile, ndipo
alipommulika usoni kwa kutumia mwanga wa
simu
na kugundua kuwa ni david,
Mdomo wenye ulimi mzuri ndani yake na
uliojaaliwa kutamka maneno mazuri ya upendo
ulitaka kusema kitu lakini ulipingwa na sauti iliyo
shiba ya shababi david kwa kauli yenye kusisitiza
mahaba,,,,,,
“Victoria moyo wako unaweza kutoka kwenye
mafuriko ya machozi kama utaruhusu kuliachia
tabasamu ulilolificha kwa muda mrefu kwa mtu
unaye mpenda na kuhisi kuwa anaweza kuwa
baharia wako atakaye kufikisha nchi ya furaha
yenye upepo na kijua cha mapendo ya dhati na
kuepukana na visamaki pamoja na vichura
vidogovidogo vilivyokuja na tamaa ya maji
ambavyo kiangazi ikifika havionekani”
“Wengi watakuhitaji kwa muda mfupi lakini ni
kwasababu ya kutaka kutimiza kiu yao ya uzinzi
tu
ila mimi david niko hapa kwa ajili ya kutaka
kulinda uzuri wako usipotee na kuharibiwa na
watu
wasio jua thaman yako fikiria leo nafuta chozi
lako
kwa maneno ya dhati toka moyoni mwangu
ambayo sijawahi kumueleza mwanamke yoyote
yule katika ulimwengu huu lakini kwako
yameweza
kutoka tena bila hata ya kujali ile namba ya siri
ambayo kwa mwanaume mwenye kujielewa ni
lazima ndio aifanye kuwa funguo ya moyo si
nyingine ni tabia pekee,, hilo kwangu sikujali
tafadhali naomba upokee maombi haya ambayo
tayari yamesha pitigwa saini ya upendo”
Victoria alizidi kuweweseka manaa hakuamini
kama angeweza kukutana na mwanaume aliye
mpenda kwa dhati katika mazingira hayo, kicheko
cha furaha kilicho changanyika na aibu kiliendelea
kumtesa moyoni mwake, miguu yake ikawa na
kazi
ya kuchimbachimba chini huku vidole vyake vya
mkono wa kulia akivinyonya kama mtoto mdogo
aliye kuwa na hamu ya ziwa la mama yake,
aliinua
uso wake uliokuwa unang’a hata kama kulikuwa
na
kiza na kumrembulia jicho david, jecho lenye kope
za asili na majimaji ndani yake ambayo yalizidi
kumfanya david kujipa asilimia 99% za kumpata
Victoria,
Miguu yao ilionekana kupiga hatua ndogo ndogo
wakisogeleana kwa hisia mpaka ku kawa na
umbali wenye mita sifuri(zero distance) na
kilichoendelea hakisimuliki,
Ndani ya muda wa kama saa moja na nusu hivi
walionekana wakitoka kwenye chumba hicho
kilichokuwa na kiza huku nyuso zao zikiwa na
furaha,
Victoria kila walipo kuwa wana tembea umbali wa
hatua tano lazima aegemee kifua cha david huku
akiachia kicheko ambacho kilimfanya david
atabasamu na kumuachia busu la msisimko
shavuni mwake,
Kutembea kwao pamoja walivutia wengi ambao
walikodoa mi macho kuwa tizama na kutaka
kuhakikisha kama yule ni david au siye, wakawa
na
kazi ya kutaniana tu na kukimbizana kwenye
viunga vya maua chuoni hapo hata habari ya
disko
wakawa wamesahau kabisa,
Moyo wa david ukawa umeingiwa na furaha ya
ajabu ambayo hakuwahi kuipata kwenye maisha
yake lakini Victoria mwanamke wa kwanza
ameweza kuibadilisha akili ya david na
kumuingiza
sehemu ambayo wengi wana lia,
Rafiki zake na Victoria waliokuwa wana mtafuta
walibaki midomo wazi walipo wakuta pamoja
wamekumbatiana huku wakiwa wameegemea mti,
kila mmoja wao alionekana kufurahia mahusiano
yao kwa kuwa waliendana sana.
Siku nyingi zilikatika na habari zili sambaa chuoni
hapo juu ya watu hao wawili kuwa katika
mahusiano ya kimapenzi, waliokuwa
wanampenda
Victoria waliumia kwa kumkosa hata yule
Emmanuely regan aliye mtenda alianza kuona
wivu
jinsi watu walivyo kuwa wana wasifia kwa
kuendana kwako,
Wasichana wengi nao walijitahidi kutaka kutoa
kasoro za Victoria kwa kuwa walikuwa
wanampenda david lakini jitihada zao ziligonga
mwamba kwa wawili hao kushikamana kupita
kiasi,
****************************************
Miaka minne ya david kukaa chuoni ikawa
imewadia ni baada ya kumaliza mtihani wao wa
mwisho na kila mmoja kuwa ndani ya mavazi
yalio
fanana kama sale ya siku hiyo maalumu ya
kuhitimu ambayo yaliandaliwa mahafali makubwa
chuoni hapo watu wengi walihuzulia wakiwemo
wazazi wa wanafunzi lakini wengi wao walikuwaa
ni wakutoka pale pale Rwanda,,
Victoria na david walikuwa miongoni mwa
wanafunzi ambao hawakuwa na watu wa
kuwasindikiza katika mahafali hayo, japo huzuni
ilimtawala sana kwa kuona wazazi wa wenzie
lakini Victoria alijua wajibu wake kwa david hivyo
alimliwaza kwa maneno matamu na kumwambia
kuwa yeye ndio mama yake, hivyo awe na mana
ndani ya moyo wake,
David alizidi kuonesha upendo kwa Victoria
maana
alipata faraja aliyoikosa kwa muda mrefu na kwa
wakati muafaka ambao alikuwa kwenye mawazo
mazito,
Watu walikusanyika eneo maalumu ambapo viti
vya wahitimu vilitengwa karibu na wazazi na vile
vya wanafunzi wengine viliwekwa kando kidogo
Meza kubwa iliyokuwa mbele aliweza kuwepo
mgeni rasmi ambaye ni rais wa nchi hiyo
muheshimiwa paul kagame akiwa ameambatana
na
familia yake ambao walikuwa wame kaa pembeni
kidogo,
Muongozaji shuhuri aliweza kusoma ratiba
itakayo
waongoza ili kukamilisha mahafalli hayo, taratibu
zote zilifuatwa na kabla ya mgeni rasmi
muheshimiwa paul kagame kusimamishwa
alitakiwa kusimama mwanafunzi mmoja kwa ajili
ya kuwa kilisha wengine kwa kusema kitu
ambacho kitaweza kuwasaidia huko mtaani
wanako kwenda na wale watakao baki chuoni
hapoa ili mgeni rasmi naye aweze kutoa mchango
wake katika chuo hiko kwa kuendeleza na kukuza
maendeleo ya elimu nchini Rwanda,,
Mkuu wa chuo alipelekewa majina matano ya
wanafunzi ili achague atakaye wakilisha
wanafunzi
wote chuoni hapo,kula ya mkuu wa chuo
ilidondokea kwa mtoto wa alfredi kazinge ambaye
ni david na jina hilo kutangazwa mbele ya
wanafunzi wote na muhusika alitakiwa kwenda
mbele ya hadhara ile ya watu wengi kwenda
kuzungumza mambo ya msingi,,,,,,
Waliokuwa wanasikia tu habari za david bila
kumjua muhusika walifurahi sana maana ndio
ilikuwa nafasi pekee ya wao kumuona, sauti za
makofi zilisikika kwa wingi kumkaribisha kijana
huyo mtanashati aliye pata bahati ya
kuzungumza
ili kumkaribisha rais wa nchi hiyo mheshimiwa
paul kagame,
Jambo hilo lilimfanya david kupata uwoga maana
hakujiamani kama ni yeye ndiye anaye hitajika
kwenda pale mbele ya hadhara ile kubwa japo
alikiri jina lililo tajwa ni la kwake, Victoria aliye
kuwa karibu alimshika began a kumuomba ajikaze
na kujiamani kama mwanaume aende,
Wengi walitamani wangeitwa wao lakini aliye
chaguliwa ni kijana aliyeonekana mnyonge sana
chuoni, vidole vingi vilikwenda kwa david na
minon’gono mingi kusikika,
makofi yalizidi david alipo nyanyuka na kuanza
kuelekea kule ilipo maiki ya kuongelea
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA SABA
Jambo hilo lilimfanya david kupata uwoga maana
hakujiamani kama ni yeye ndiye anaye hitajika
kwenda pale mbele ya hadhara ile kubwa japo
alikiri jina lililo tajwa ni la kwake, Victoria aliye
kuwa karibu alimshika began a kumuomba ajikaze
na kujiamani kama mwanaume aende,
Wengi walitamani wangeitwa wao lakini aliye
chaguliwa ni kijana aliyeonekana mnyonge sana
chuoni, vidole vingi vilikwenda kwa david na
minon’gono mingi kusikika,
makofi yalizidi david alipo nyanyuka na kuanza
kuelekea kule ilipo maiki ya kuongelea ,
Wingi wa makofi uliwafanya watoto wale wa kike
wa paul kagame kuwa na shauku ya kumuona
huyo david aliyekuwa umbali kidogo kabla haja
isogelea maiki, mwendo wa david na tabasamu
alilo kuwa analiachia lili wachanganya wasichana
wengi hata walio kuja kwa niaba ya ndugu zao
nao
mioyo yao ilikiri kuwa david ni mtu mwenye kila
sifa ya kuitwa mwanaume na kugombaniwa,,
Ndani ya hatua chache alifanikiwa kuifikia ile
maiki
iliyosimamishwa na kuanza kukohoa kidogo ili
kuwa weka watu katika umakini wa kusikiliza
kitakacho ongelewa, alipo maliza alipepesa macho
yake huku na huko kutafuta pozi la kuanzia ndipo
alipo gongana macho kwa macho na mtoto wa
rahisi paul kagame,
David akiachia tabasamu na kuonesha hana
mpango naye japo yule dada alianza kuleta mikao
ya ajabu baada ya kuangaliwa na david,
Akili ya david ilipokaa sawa na kuona kimya
kimetawala ndipo alipo anza kusema mambo ya
msingi na kwa faida ya wote kutoka moyoni
mwake baada ya kutoa salamu kwa wote,,,,,,,,,,,
,,,,,,,,,
“maisha ni kama kivuli cha mti ambacho kadri
muda unvyo sogea ndivyo kivuli huama na
kubadilika hivyo mimi na wewe wote kama
vinajana tusikubali kukatishwa tamaa na mtu wa
aina yoyote ile maana cheko la usoni wakati
mwingine linakuwa ni mlinzi wa roho mbaya
iliyokuwa moyoni, hiki tulicho kipata chuno hapa
basi kiwe ni chenye kuleta upendo kwenye familia
zetu, tusije kumzalau baba au mama kwa elimu
tulio ipata, akili zetu zinabidi zifanye kazi
ipasavyo
na kuamini kuwa hata kama baadhi ya wazazi
wetu hawajafanikiwa kupita hata katika chumba
kimoja cha darasa lakini wao ni wajuzi kuliko sisi
tulio pita madarasa mengi ambayo yanaweza
kuleta viburi mbele za watu kwa kujiona kuwa sisi
ni wathamani zaidi kuliko yule mtoto unaye
muona
kaweka mikono nyuma barabarani na kukuonesha
jicho la haruma pale unapokuwa unakula vitu
vitamu, hakupenda kuwa katika hali ya udhuni
lakini alitamani naye siku moja ashike peni na
karatasi abadilishe maisha kama wewe,
Tusimnyanyase yule msichana wa kazi mdogo
ambaye ni kama mama yako wa pili pale
nyumbani
hata kama ni mdogo maana ndiye anaye
anayekuandalia chakula na kukufanyia kazi zote
japo umri wake hauruhusu kufanya kazi zile ila in
sababu ya shida tu,
Kwanini umuone in kama mtu wa kupita hali ya
kuwa anatabia nzuri inayo mpendeza kila mtu,
tafadhali elimu isifanye kuwabagua watu maana
hatujui kesho utakuwa nani kutokana na maisha
kuwa kama kivuli cha mti”
Maneno hayo david aliyazungumza kwa sauti ya
upole na palipo stahili kukemea baya alikemea
lakini alikuwa ameanza kusindikizwa na chozi la
huruma kutokana alichokuwa anakisema alikuwa
ana maanisha,,,,,,,
“huenda huyo msichana wa kazi utakaye
mnyanyasa au kumfanya ndio mke wenu wa pili
wewe na baba yako kutokana na pesa zenu na
kumpatia ugonjwa ambao utamfanya ajute
kwenye
maisha yake anaweza kuwa ni Nisha,,,,,,,,,
“Nishaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!” sauti za hadhira
iliyokuwa pale walirudia jina hilo la nisha kwa
mshangao na kuonekana kujiuliza ni nani huku
david naye akiwa kajishtukia maana haikuwa
dhamira yake kumtaja mdogo wake kipenzi hivyo
alipatwa na mshtuko wa ghafla papo hapo na
kuachia maiki ile kishindo kizito kilisikika in baada
ya mwili wa david kufika katika ardhi---
Mama!!!!!!!!!!!! Yesu kristu!!!!!!!!!!!!!!!,
mtumeeeeeeeeeee!!!!!!!!! Maskini ni nini hiki
tena???????? Mayowe ya watu yalisikika kwa
mshangao, wapo walioshika mioyo yao na
wengine
kushika vichwa vyao, Victoria alichanganyikiwa
mkono wake ulishika ile nguo aliyo vaa yenye
urefu
uliokuwa unataka kubuluzika, machozi yalianza
kumlenga mlenga huku akiomba njia ili awahi
pale
alipo dondoka kipenzi chake ambaye aliapa
kutomuacha haka kama ardhi yote itageuka na
kuwa bahari,
Umati wa watu ulimfanya Victoria kuchelewa
kumuona david yupo katika hali gani pale alipo
dondoka ni baada ya kuwa waliokuwa karibu
kumbeba na kumuwahisha katika zahanati ya
chuo, alibaki kusimama tu kuangalia jinsi david
alivyokuwa anakimbizwa ili kwenda kuokoa
maisha
yake,
Mkuu wa chuo alisimama na kuomba radhi kwa
kilicho tokea na kusisitiza utulivu uendelee ili
wamalize shughuli salama, rafiki zake na Victoria
walikwenda kumchukua victoria pale alipokuwa
amesimama na kumrudisha kwenye kiti,
Ndali ya dakika kadhaa hali ikawa shwari kiasi
Fulani lakini kulikuwa na minong’ono midogo
midogo, wengi walikshindwa kuelewewa
kilichokuwa kinaendelea na walitamani kumjua
nisha ni nani? Hata Victoria naye alishindwa
kujielewa vile na kutulia pale alipokuwa amekaa
alitaman kunyanyuka aelekee kule alipo pelekwa
david,
Moyo wa wivu ndio uliokuwa unamsumbua
Victoria
kwa wakati huo maana naye hakumjua nisha ni
nani kutokana na david kutomuleza siri ya maisha
yake na mengi yalio mkuta, utaratibu wa mahafari
uliendelea kama kawaida na rais paul kagame
kutoa pongezi kwa david ambaye hakuwepo hapo
kwa ujumbe mzuri alio utoa kwa wenzie na
kusisitiza ufuatwe na kutekelezwa,
,
Makofi mengi yalipigwa kuashiria wapo pamoja
na
rais na kuwa watafanya kama alivyosisitiza,
Rais paul kagame alivyomaliza hotuba yake,
utaratibu ulifuatwa kama kupewa vyeti vyao,
kupata chakula na kunywa, wanafunzi walipiga
picha nyingi kwa ajili ya ukumbusho na wengine
kubadilishana namba za simu pamoja na barua
pepe kwa ajili ya mawasiliano maana waliokuwa
wanasoma hapo wengi walikuwa wanatoka
mataifa
tofauti tofauti,
Familia ya muheshimiwa paul kagame ilipata
fursa
ya kwenda kumuona david ambaye alikuwa
anaendelea vizuri baada ya kupewa huduma hapo
kituoni na kwakuwa tatizo lake lili kuwa in la
muda
mfupi tu basi aliruhusiwa na kujumuika na
wenzake, watoto wa kike wa rais waliomba
kupiga
picha na david za mapozi tofauti ambayo
mengine
yalizidi kumkera Victoria maana hawakuruhusiwa
kwa wakati huo kufanya chochote kutokana na
uwepo wa rais pale,
Baada ya rais kuondoka david akawa huru
kuungana na wenzie rasmi na kupiga nao picha,
wengi walichukua namba zake hata wale
waliokuwa wana mchukia walinyoosha mikono
kuwa wameshindwa vita nay eye hivyo
wakaendeleza amani tu, kila mtu alitoa kinyongo
chake na kukumbatiana,
Mkuu wa chuo alimletea david vyeti vyake ba
kumpiga kofi la pongezi begani kwa ujumbe mzuri
alio utoa na kumtakia kila rakheri katika maisha
yake huko anako kwenda azidi kuwa hamasisha
watu kufanya mambo ya msingi,
Na wamwisho alikuwa mama mwenye nyumba
mtarajiwa Victoria , walipiga picha nyingi sana
zilizo ashiria upendo wa dhati hata kama atakaye
ziona alikuwa hawezi kuuliza kama walikuwa
wapenzi maana zilijitambulisha zenyewe, watu
wengi walitoa machozi kwa kuachana na
ukiangalia walisha zoeana hasa rafiki zake na
Victoria ambao wengine walitokea, Ghana, Kenya
na Burundi.
Hivyo ndivyo safari na maisha ya chuo kwa david
yalivyo malizika na siku aliyofuata safari ikawa
imewadia kurudi nchini Tanzania kuendelea na
shughuli yake pevu ya kumtafuta helman.
********************************
Magari ya aina tofauti yaliegeshwa upande wa
kushoto na wa kulia kwa kutenganishwa na
barabara ndogo iliyopita kati, watu wa mataifa
mbali mbali wenye rangi nyeupe na nyeusi
walikuwa wakipishana wengine wakiingia na
wengine wakitoka, wafanya kazi wenye sale za
suruali nyeusi na mashati myeupe huku wakiwa
na
vitambulisho vya ajira yao vilivyokuwa viki
ning’inia shingoni waliendelea kusukuma
mikokoteni midogo ya kisasa iliyipakia mabegi
walizidi kupendezesha eneo hilo ambalo lilikuwa
na
miti myembamba na mirefu ambalo
lilitambulishwa
kwa jina moja la mtu anaye kumbukwa na
kutamani arudi kila siku inayo itwa,aliyepigania
uhuru wan chi hii yenye sifa ya kuitwa kisiwa cha
amani ambayo sasa inaelekea kupotea kutokana
na wapuuzi wachache waliokuwa na nia ya
kutaka
kujifaidisha wao na familia zao, ni “JULIUS
NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT” (uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius nyerere)
Kofia ya zambarau na tisheti ya zambarau vilivyo
changiwa na suruali ya jinsi nyeusi pamoja na
viatu aina ya jodani yenye uwekundu maeneo
yalio
karibia soli ya kiatu hicho ndivyo vilimfanya david
kung’aa zaidi pale uwanja wa ndege wa juliasi
akiwa kamshika mkono qeen tz wake Victoria
ambaye aling’arishwa na nywele za kizungu zilizo
iva kwa weusi na kuzibana kwa kibanio cha rangi
ya pinki iliyoendana sawa na rangi ya kiatu
alicho
vaa huku vikitoautisha na suruali nyeupe
iliyombana kiasi na kuonesha maungo yake, ile
brauzi yenye rangi ya goldi na iliyokuwa
inameremeta kwa nakshi zake hakika Victoria
zilimpendezesha sana,,
David alisimama na kutoa simu yake ambayo
kulikuwa na picha ya Victoria kwenye kioo na
kutafuta namba ya afande criss kisha kupiga na
punde ikawa imepokelewa, david alipokuwa
anataka kuuliza kuwa afande criss amesiamama
wapi kwa bahati nzuri macho yao yakagongana
na
afande criss akawa anampungia mkono huku
akionesha uso wa furaha kwa kumuona david
kwa
maranyingine tena akiwa katika muonekano
tofauti
kabisa,
Baada ya kuzunguka kutoka mle ndani
wakakumbatiana kwa furaha kila mmoja alikiri
kumkumbuka mwenzie, Victoria alibaki
akiwanshangaa tu na tabasamu lake la uchokozi,
wawili hao afande criss na david walipo maliza
kulakiana mdomo wa afande criss ilitaka kuuliza
kitu juu ya Victoria lakini alipomtazama david
walibaki kucheka tu maana afande criss alikuwa
mtu mzima aliweza kuelewa kilichoendelea kati
yao,
Wote walitembea kwa furaha na kuelekea kwenye
gari la afande criss lakini Victoria alitaka kuweka
kipingamizi kwenda kwa kina david japo
alipompigia mama yake akawa hampati kwenye
simu hivyo david alimuomba na kusaidiwa na
afande criss waeleekee kwanza kwako halafu
watampeleka Victoria nyumbani kwako, mtoto wa
kike akawa hana kipingamizi mbele ya kipenzi
chake alikubali na safari ikaanza kuelekea mabibo
external nyumbani kwa afande criss,
Baada ya purukushani za foleni huko barabarani
walipokuwa hatimaye waliweza kufika external
mabibo ambapo david alieza jinsi masomo
yalivyokuwa huko na kila kitu ambacho
alichokuwa
anakijua alimtambulisha Victoria kwa afande criss
na kumdanganya Victoria kuwa yule ni baba yake
akiwa na maana hakutaka maswali mengi hapo
baada na Victoria kuujua undani wake mapema
hivyo na baada ya kula na kunywa david ilibidi
aage na kumsindikiza Victoria mpaka kwako lakini
aligoma kuingia ndani na kuahidi kuwa atakwenda
siku nyingine,
Japo Victoria alichukia lakini hakukuwa na jinsi
david alirudi mpaka kwako ambapo afande criss
alikwenda tena kazini:
***************************
Chini ya usiku wa nyota na mwezi david akiwa
juu
ya kitanda chake baada alitafakari na kupanga
mipango yake ya kuanza kumtafuta mdogo wake
nisha na kuingia vitani rasmi maana tayari ngao
ya
elimu anayo anauwezo wa kuingia mahali popote
anapo pataka,
Aliwaza na kuwazua wapi aanzie akawa amepata
jibu nini cha kufanya alijisema moyoni,
“kesho inabidi nifanye kila linalowezekana niende
morogoro alipokuwa amefungwa mzee wangu na
kupoteza maisha na kuzikwa kama mbwa wa
mitaani aliyegongwa na gari, lakini inabidi
niifanye
kuwa siri asijue Victoria wala afande maana
wanaweza leta kipingamizi na naweza kupokea
maswali mengi kutoka kwa Victoria ukiangalia
kwa
sasa sijapnaga kumuambia chochote kile,”
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA NANE
Chini ya usiku wa nyota na mwezi david akiwa
juu
ya kitanda chake baada alitafakari na kupanga
mipango yake ya kuanza kumtafuta mdogo wake
nisha na kuingia vitani rasmi maana tayari ngao
ya
elimu anayo anauwezo wa kuingia mahali popote
anapo pataka,
Aliwaza na kuwazua wapi aanzie akawa amepata
jibu nini cha kufanya alijisema moyoni,
“kesho inabidi nifanye kila linalowezekana niende
morogoro alipokuwa amefungwa mzee wangu na
kupoteza maisha na kuzikwa kama mbwa wa
mitaani aliyegongwa na gari, lakini inabidi
niifanye
kuwa siri asijue Victoria wala afande maana
wanaweza leta kipingamizi na naweza kupokea
maswali mengi kutoka kwa Victoria ukiangalia
kwa
sasa sijapnaga kumuambia chochote kile,”
Hayo ndiyo yalikuwa mawazo ya david na
mpango
aliokuwa mauandaa, asubuhi na mapema david
aliamka na kujiandaa vyema, alipokuwa anatoka
nje alikutana na afande criss ambaye naye
alikuwa
anaelekea kazini, afande alimuulizaa swali david
baada ya kumuona amejiandaa asubuhi
subuhi,,,,,,,
“vipi david unasafari?
“ aah jana nilisahau kukwambia victoria leo
wanasherehe kwako mtoto wa baba yake mdogo
anaolewa hivyo amenialika na inawezekana
nisirudi
mpaka kesho” david alimdanganya afande criss
“Ooh hakuna shida kikubwa kuwa makini tu na
tueane taarifa kama kunatatizo na ngoja nikupatie
pesa kidogo” afande criss alizungumza
“Hapana baba pesa ninayo ya kutosha hakuna
shida labda kama itapunguwa basi nitakujulisha”
Afande criss alimuelewa david na akampa ruhusa
japo taarifa ameipata asubuhi hakujali maana
david Alisha kuwa mtu mzima sasa hivyo kila
mmoja alikwenda kivyake na david kuelekea
kwenye kituo kikubwa cha mabasi ubungo na
kuchukua gari ya kampuni ya abood iliyokuwa
inaelekea morogoro,
Huzuni ilimjia baada ya kukumbuka jinsi
alivyopotezana na mdogo wake kipenzi nisha nay
eye kunusurika kufa kwa shtuma za wizi, mpaka
gari inaanza kuondoka david mchozi mwembamba
ulikuwa unamshuka taratibu, alichukua kitambaa
na kujifuta.
**********************************
Ndani ya msaa matatu akawa amefika stendi kuu
ya mabasi ya mjini morogoro msamvu kisha
kuchukua gari ndogo kuelekea kinguluila gerezani
alikokuwa amefungwa marehemu baba yake,
Umbali wa kutoka hapo mjini mpaka kufika huko
gerezani haukuwa mkubwa sane hivyo aliweza
kufika mapema na alipoliona geti la gereza
alimkumbuka marehemu baba yake sana, alipiga
hatua mpaka kwa mlinzi na kujiandikisha kuwa
anaelekea kwa mtunza kumbukumbu wa gereza,
Mlinzi huyo alimuelekeza ofisi ya mtunza
kumbukumbu na david hakuchelewa alielekea
huko
na alipo fanikiwa kuonana naye walisalimiana na
david kueleza shida yake ambayo afisa huyo
alitaka kuipinga lakini david alimpitia kiasi cha
fedha na akaridhika,
Ndipi alipo simama afisa huyo na kwenda kwenye
droo kisha kurudi na daftari moja ambalo lilichoka
choka na kumkabidhi david na david alimuuliza,,,,,
,,,,
“Unauhakika kuwa hili ndilo daftari lililokuwa
linatumika kuandikisha watu wanaokuja
kutembelea wagonjwa kipindi hicho marehebu
baba
yangu alipo fungwa hapa?
“Ndio ninauhakika” alijibu yule afisa
Ndipo david alipoanza kulikagua taratibu na kwa
umakini wa hali ya juu klitafuta jina la mtu wa
mwisho aliye kwenda kumtembelea marehemu
baba yake kabla ya kifo chake,
Uso wa david ulibadilika ghafla na kuiva kwa
hasira baada ya kulikuta jina na sahihi iliyopigwa
ya mtu huyo wa mwisho kwenda kumuona
marehemu baba yake kabla ya kifo chake lakini
jina
lililo andikwa pale ni HELSON ambalo kila
akitafakari aliona linaendana kabisa na HELMAN
alijiuliza na kuingalia ile sahihi iliyopigwa pale ili
aweze kuikariri hata hivyo aliona bado itakuwa
kazi
kuiweka kichwani ndipo alipomzugisha yule afisa
na kumwambia,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
“nahisi umekosea hili daftari tafadhali niangalizie
lingine wakati nikimalizia kulikagua hili”\
Yule afisa aliponyanyuka na kwenda kutazama
daftari lingine david alichana ile sehemu
iliyopigwa
sahihi na kukichukua kile kipande cha karatasi.
Kisha kukiweka kwenye mfuko wa suruali yake
haraka na kujikausha kwa utulivu wa hali juu
kabisa.
“bwana mkubwa hakuna lingine zaidi ya hilo
maana yote ni ya miaka ya nyuma zaidi jaribu
kuangalia vizuri na kwa umakini zaidi”
alizungumza
yule afisa wakati ametoka kutafuta daftari lingine,
“Dah mbona kazi inataka kuwa ngumu kwa
upande
wangu maana nimeangalia kila karatasi kwa
uwangalifu lakini sijafanikiwa kuoma chochote
kile”
alizungumza david iliamradi tu afanye ukweli
kuwa
uwongo na ndipo yule afande alipo sema,,,,,
“ngoja nami nikusaidie kutazama labda naweza
kuliona huenda wewe umechoka kwa uchovu wa
safari na kuwa na papala”
“Aah usijali muheshimiwa achana tu na hiyo kazi
nitakuja siku nyingine kwa ajili ya hii kazi tu,
hivyo
usisumbuke ndugu” David alimpinga kisha
kumuongezea kiasi cha fedha na yeye kunyanyuka
na kuanza safari ya kuondoka huku yule afisa
akibaki anashangaa shangaa tu pale mezani
kwake.
Siku hiyo David alilala kwenye nyumba ya wageni
mjini Morogoro na asubuhi ilipofika akaanza
safari
ya kurudi jijini Dar es salaam akiwa na wazo
jipya
kichwani mwake la kuanza harakati za kumtafuta
Nisha dada yake kipenzi walioachana miaka mingi
huku helman akiendelea kuzunguka mawazoni
kwake kwa hasira,
Muda aliotoka Morogoro mjini David aliweza
kufika
Dar es salaam mapema sana, alishuka kwenye
gari
kisha kutafakari kwa muda na kuchukua hatua ya
kumpigia simu mpenzi wake Victoria, wazo hilo
lilimjia baada ya kutaka kuleta uhalisia kwa
afande
Criss amini kwamba kweli David alilala kwenye
sherehe nyumbani kwa kina Victoria,
Baada ya muda Victoria alikuja maeneo ya
ubungo
mataa na kukutana na David, kila mmoja alimlaki
mwenzie kwa furaha bila kujali umati wa watu
waliokuwa wanapishana, furaha ilitawala kwenye
mioyo yao maana kila mmoja alikuwa anampenda
mwenzake toka ndani ya moyo,
“Unatoka wapi mpenzi wangu saa hizi na mbona
nilikuwa sikupati kwenye simu?”Victoria
alimuuliza
David ambaye aliyekuwa anafikiria jibu la
kumpa,,,,
“ni kweli Victoria hapa ninavyo kueleza nilikuwa
kituo cha polisi baada ya kukosana na mtu lugha
na ndio sababu ya kukupigia wewe maana
nimemdanganya baba kuwa nili lala kwenu
kulikuwa na sherehe hivyo naomba msaada wako
ili aamini tulikuwa wote maana akijua kama
nilikuwa kituoni atanigombeza kwa nini
sikumpigia
simu aje kunitoa na mimi jambo hilo sikutaka
kulifanya maana mimi ndiye niliye kuwa na
makosa”
David alizidi kuwa cheza shere afande Criss na
Victoria na wote wakiaamini alayokuwa
akiyasema,
Victoria alimpatia pole nyingi david ambaye
alimdanganya bila yeye kujua kuwa anachezewa
akili,
Hawakuchuka muda kufika kutokana na umbali
mfupi uliokuwepo kutoka ubungo mpaka mabibo
external nyumbani kwa kina david hivyo nyayo
zao
zilikanyaga kikanyagio cha kufutia vumbi na
uchafu
mwingine kilichopo pale mlangoni ambapo
walikuta
viatu na David alihisi afande Criss yupo ndani,
hodi
moja ilitosha kwa afande criss kusikia na kuwa
karibisha waingie,
“ooh wanangu karibuni sana na mna bahati
maana
ndio nilikuwa nataka kuelekea kazini baada ya
kurudi mara moja” afande Criss alizungumza
kabla
hata wakina David hawaja kaa chini,
“Asante sana baba tunekaribia za tangu jana?”
David alimshukuru baba yake anaye mlea afande
criss na kumuuliza swali
“namshukuru mungu salama japo nilikuwa
mpweke
maana nilishazoea kuwa wawili na nyie poleni na
uchovu wa sherehe” alizungumza afande Criss
“Mmh tumesha poa baba lakini samahani kwa
kutokualika” Victoria naye aliingilia maongezi na
kumjibu afande criss wakati david akiendelea
kutabasamu kwa kificho baada ya kuona dili lake
linaenda sawa hakuna aliyemshtukia kama
alikuwa
Morogoro kwenye shughuli pevu.
“Uwepo wa David tu unatosha kuniwakilisha mimi
wala usiwe na hofu kabisa mwanangu”
alizungumza afande Criss,
Baada ya maongezi hayo ya kutakiana hali,
afande
Criss alimtazama David kisha kumuambia,,,,,,
“David, ni rahisi sana mtu kufa kwa maji aliyo
ridhia mwenyewe kuyanywa kuliko yule anaye
tapatapa mtoni au baharini”
Usemi huo aliozungumza afande criss uliwafanya
Victoria na David kutazamana kwa mshangao
kisha David kumuuliza afande criss,,,
“unamaana gani baba kwa usemi huo?”
“maana yangu ni kwamba aliyekuwa kwenye
mahusiano na mpenzi mmoja ni rahisi sana
kupata
magonjwa ya zinaa kama hutokuwa mwaminifu
kwa mwenza wako hivyo basi ni jambo la
kushukuru kupata mchumba mzuri kama Victoria
mimi nawatakia kila la kheri katika mapenzi yenu
maana kuna jambo zuri ambalo nataka kukueleza
mbele ya mwenzio”
afande Criss alizungumza.na David alijikusanya
na
kukaa vizuri kisha kuuliza kwa shauku,,,
“lipi hilo tena baba?”
“David kwa bahati nzuri jana nilipokuwa hapa
natazama runinga kuna rafiki yangu mmoja
alinipigia tukawa tunazungumza maongezi ya
hapa
na pale ndipo aliponieleza kuwa katika shirika
lake
linaloshungulika na masuala ya kusaidia vijana
kujikwamua kutoka katika hali tete kama uvutaji
wa madawa ya kulevya pamoja na kusaidia
watoto
yatima, sasa aliyekuwa muhasibu wake
ametoroka
na kiasi cha fedha ambacho kilitumwa kutoka
landon na wafadhili waliojitolea kusaidia shirika
hilo hivyo anashida ya muhasibu mwingine
atakaye
kuwa mwaminifu, nami nikaona sio mbaya
kumueleza sifa zako juu ya masuala ya
kibiashara
uliyosomea na ufaulu wako naye ameridhika bila
hata kuona vyeti vyako kwa kuwa ananiamini
lakini
keshokutwa utakapo kwenda kuanza kazi hiyo
ubebe na vyeti vyako kwa heshima zaidi na awe
na
uhakika kwa macho yake mwenyewe” afande
Criss
alizungumza
Habari ya kazi ni jambo jema kabisa, kila atakaye
pata taarifa ni lazima afurahi kutokana na tatizo
la
ukosefu wa ajira nchini japo kuwa vijana
wanaweza kujiajili wenyewe,
David alionekana kuwa na sura ya huzuni japo
ilikuwa sio rahisi kuigundua, lakini afande criss
aliweza kuijua kutokana na utuuzima alio kuwa
nao, Victoria naye tabasamu la kirafiki lilimtoka
huku akimwangalia david aliyekuwa anajilazimisha
kufurahi,
Jambo lililomfanya david kuwa na huzuni ni
baada
ya kusikia shirika analoenda kufanya kazi ni la
watoto yatima, ndipo mawazo mengi yaka mjia
kumkumbuka Nisha ambaye mpaka kwa muda
huo
hakujua yupo katika hali gani mzima au amekufa?
Pia ni miaka mingi imepita tangu wapotezane ni
matarajio yake kumuona akiwa msichana
mkubwa
na mwenye akili timamu kama atakuwa bado
yuko
hai.
“David vipi mbona umebadilika ghafla hukufurihia
kupata kazi?” aliuliza afande criss
“Mmh hapana baba nilikuwa najaribu kufikiria
ugumu nitakao upata maana si unajua sikuwahi
kufanya hata mazoezi ya kazi nilipokuwa
chuo?’alimjibu
“Hahahahah david usitufurahishe sisi ila usiwe na
wasiwasi ulichokisoma ndicho utakacho kitumia
na
mengine utaelekezwa hapo hapo kazini sawa
mwanangu?”
******************************
Furaha yenye huzuni ndani yake ikawa imemaliza
siku david alimrejesha Victoria kwao lakini kwa
bahati mbaya mama Victoria hakuwepo muda
ambao david yupo pale, hivyo hakukaa sane nae
ilimbidi arudi nyumbani kwao akapata chakula
cha
usiku kisha kumuaga afande criss na kuelekea
chumbani,,
Aliwasha taa na kwenda kufungua begi lake
ambayo aliweka suruali aliyoivaa siku alivyo
kwenda gerezani alikokuwa amefungwa
marehemu
baba yake miaka ya nyuma kisha kuingiza mkono
na kukitoa kile kipande cha karatasi chenye sahihi
ambayo alihisi ni ya helman japo jina alilo likuta
ni
halson, aliitazama vizuri sana kisha kukihifadhi
ndani ya pochi yake ndogo ya mfukoni na
kuamua
kujipumzikia kutokana na uchovu.
Siku iliyofuata david aliamka asubuhi na mapema
na kufanya baadhi ya kazi ndogo ndogo kama
kumyooshea afande criss sale zake za kazi na
baada ya afande kuelekea kazini naye akatoka.
Alikwenda mpaka maeneo ya ubungo stendi na
kuingia kwenye steshenari moja iliyokuwa karibu
na chuo cha the amazon kisha kuitoa chapa
nyingie ile sahihi ili ziwe nyingi hata kama moja
inaweza kupotea basi awe na akiba,
Alikotoka kulikuwa na sehemu nyingi za kutolea
chapa lakini alikwenda maeneo hayo kwa jukumu
kubwa kabisa la kuanza kumtafuta dada yake
kipenzi,
David alijitahidi kuulizia kila watu ambao
aliwaona
wakiombaomba na vikundi vya watoto wa
mitaani,
walio wakubwa na hata watoto kama wangeweza
kumfahamu nisha, lakini bila mafanikio mpaka jua
likawa linaelekea kutua upande wa magharibi,,
Ndipo David alipo amua kwenda kukaa kwenye
mgahawa mmoja na kupata chakula maana kazi
ilikuwa nzito kwake hata hamu ya kula hakuwa
nayo, wakati akiendelea kujipatia chakula chake
pale ghafla macho yake yaliweza kumuona
msichana mmoja aliyevaa nguo fupi yenye rangi
nyekundu na kichwani chake kikiwa kimepambwa
na nywele za kizungu huku moshi mwingi wa
sigara ukimtoka mdomoni david alimtazama sana
lakini hakuweza kufanikiwa kumuoni usoni kwa
umbali mchache aliokuwa amekaa nae na
hakutaka
kumkazia sana macho lakini kilicho mshangaza ni
kuona yule msichana kazungukwa na mipombe
mikali juu ya meza yake,
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA TISA
Ndipo David alipo amua kwenda kukaa kwenye
mgahawa mmoja na kupata chakula maana kazi
ilikuwa nzito kwake hata hamu ya kula hakuwa
nayo, wakati akiendelea kujipatia chakula chake
pale ghafla macho yake yaliweza kumuona
msichana mmoja aliyevaa nguo fupi yenye rangi
nyekundu na kichwani chake kikiwa kimepambwa
na nywele za kizungu huku moshi mwingi wa
sigara ukimtoka mdomoni david alimtazama sana
lakini hakuweza kufanikiwa kumuoni usoni kwa
umbali mchache aliokuwa amekaa nae na
hakutaka
kumkazia sana macho lakini kilicho mshangaza ni
kuona yule msichana kazungukwa na mipombe
mikali juu ya meza yake,
Kitendo hicho david hakukubali akili yake ilikuwa
imesha changanyikiwa kila msichana anaye
muona
yupo katika mazingira yasio eleweka basi akili
yake
inarudi kwa nisha na kujiuliza vipi huko alipo
anaishi vipi? Na ndipo alipo nyanyuka kwenye
meza yake na kwenda na kuanza kumsogelea yule
dada ambaye umri wake unaonesha si mkubwa,
sauti za hatua za david zilimshtua yule dada
ghafla yule dada alipoiona sura ya david
alionekana kutetemeka huku mikono yake
ikichukua
pochi yake iliyoendana na nguo yake nyekundu na
punde tu david alivyomkaribia yule dada
alikurupuka na kuisukuma ile meza na zile chupa
za pombe zilianguka na kuvunjika, watu
waliokuwa
pale walishtuka na kugeuza shingo zao kutaka
kujua kuna nini,
Lakini david bila kumuona vizuri usoni yule dada
alitoka mbio na miguu ya david haikusita
kuanzisha mashindano ya riadha kumkimbilia yule
dada ili apate kumjua na kwa nini alikimbia
Hatua zake yule dada hazikumfikisha mbali David
akawa amemfikia, lakini yule dada alizidi
kuonesha
uwoga kwa David baada ya kupiga magoti na
kuanza kulalamika,,
“tafadhali kaka yangu usinikamate ni shida tu
lakini sikupenda kuuza mwili wangu nipate
kipato,ndugu zangu wananitegemea na hapa
ninavyokwambia nina watoto wawili wako kwa
jirani yangu mpaka nitakaporudi ndio naenda
kuwa
chukua, hawana baba, mimi ndio baba na mimi
ndio mama hivyo kama utanikamata watazidi
kuwa
katika maisha magumu kuliko haya ya sasa”
Yule dada alimwaga mchozi wa maumivu, kilio
chake kiliweza kusimamisha watu waliokuwa
wanapita kando, ila david alishindwa kumuelewa
anazungumza nini mpaka dakika hiyo, ilimbidi
amuuinue pale chini alipokuwa amepiga magoti
na
kumjibu jibu ambalo wangeenda sawa kwanza
iliajue tatizo lilikuwa ni nini,,,,,,,
“usijali dada yangu sitokukamata, ondoa shaka
kabisa moyoni mwako twende ukaendelee na
starehe zako halafu uniambie kwa upana zaidi
naweza kukusaidia”
Yule dada hakuamini alichokisikia toka kwa david
kuwa anaweza msaidia, basi waliongozana wote
mpaka kwenye zile meza na wakaamua kukaa
meza moja ili yule dada aweze kueleza tatizo
lake,
“Unaitwa nani dada?” david aliuliza
“Mwajuma” alijibu yule dada huku akifuta mchozi
na kuingiza makamasi ndani
“Ooh jina zuri lakini kwanini ulinikimbia wakati na
kusogelea?” alizungumza David
“Akili yangu haipo sawa sasa maana ni jana tu
wenzangu wamekamatwa na askari kule buguruni
kwa ajili ya kufanya miili yao mtaji, na mimi
nilifanikiwa kuwa kimbia na wame weka baadhi
ya
picha zangu kwenye mitandao kwamba natafutwa
kwa kwenda kinyume na maadili ya kitanzania
kkuuza mwili hivyo kila anaye nisogelea na jua ni
askari tu kwani wewe sio askari maana umesema
utanisaidia? Alizungumza mwajuma na kumuuliza
swali David.
“Hapana mimi sio askari na ujio wangu pale
kwako
nilihisi unatatizo maana mtu wa kawaida hawezi
kunywa pombe nyingi vile zenye ukali”
aliungumza
David
“ni kweli kaka yangu nimefanyiwa kitu sio kizuri
kabisa kwenye maisha yangu nimezalishwa
watoto
kabla ya umri wangu lakini bora ya hivyo ila
mwanaume mwenyewe akaaamua kunifukuza na
kunitishia kuniua endapo kama nitatoa taarifa
polisi ndio maana nikaamua kujihusisha na
biashara hii ya kuuza mwili na kwasasa ninaiishi
na virusi vya ukimwi ambavyo sijaelewa nilipo
vitoa kutokana na idadi kubwa ya wanaume
niliokuwa na tembea nao tena wengine bila kinga
kwa kuwa waliniahidi kunipa pesa nyingi”
David huruma ilizidi kumuuingia moyoni mwake
maana anashindwa kujua kuwa Nisha atakuwaje
maana akiangalia sababu za huyo dada in
matatizo yalio mfanya kujiuza na nisha mdogo
wake ambaye siku ya kwanza tu kufika jijini
akapotezana nae, hajui yu hali gani mpaka sasa.
Mkono wake haukusita kuingia mfukoni na kutoa
kitambaa kufuta mchozi wa kiume uliokuwa
unachuruzika shavuni kisha kumuambia,,,
“Pole sana dada yangu kwa mataizo hayo lakini
usijali huwa kuwa binaadamu kama hujakumbana
na changamoto kama hizo na sisi wanaume
wengi
ndio tulivyo huwa tunapenda kupanda lakini
mavuno hatuyataki, na huyo mwanaume wako
yuko wapi?” david alimuuliza,
“Yuko haphapa dar es salaam na anapesa nyingi
sana pia ni mtu mzima wa makamu anamke na
mtoto mmoja wa kiume ambae hana utofauti na
wewe kwa muonekano, mimi nilikuwa kimada tu
kwake na akaamua kunizalisha ila baada ya mke
wake kuanza kugundua kuwa anamahusiano na
mimi ndipo alipo nitelekeza kwa kumuhofia
mkewe
aliposema kuwa atamhuharibia siri zake”
Akili ya david ilikaa sawa kidogo baada ya kusikia
mwajuma kataja neon siri, hivyo hakusita
kumuuliza,
“Kwani anasiri gani kubwa ambayo mpaka kufikia
hatua ya yeye kuhofia?” david alimuuliza.
“Inavyosemekana ni jambazi na swala la kuua
kwake ni kama kunywa maji kila mtu amalizapo
kula ndio maana nikaamua kukaa kimya tu ili
nami
nisije kupoteza maisha yangu na kuwaacha
watoto
wangu” mwajuma alizidi kumpasulia david undani
wa maisha yake japo david alishindwa kuamini
maana ndio mara ya kwanza wameonana na yule
dada kawa muwazi kwake.
“Mmh dah sasa huyo mzee anaitwa nani na
anaishi wapi?” david aliuliza,
“Anaishi mbezi beach yeye na familia yake yote
na
kwa jina ambalo hakuna Malaya asiye lijua
anaitwa Helman mapesa, ni hii imetoakana na
jinsi
alivyokuwa anamwaga pesa nyingi kila anapokuta
wasichana wrembo hasa wadogo wadogo ili
kuwapa tama ya kukubali kuwa na yeye”
Moyo wa david ulishtuka baada ya kulisikia jina la
mbaya wake anaye mtafuta kila kona ya jiji la dar
lakini bila mafanikio likitajwa tena kwa sifa
mbaya
ambazo hata yeye anamtafuta kutokana na ukatili
alio ufanyia familia yake, alivuta kiti mbele na
kumuuliza kwa umakini mkubwa sana,,,
“Umesema anaitwa nani huyo mzee?”
“Helman mapesa” mwajuma alimjibu
“ Unaweza kuwa na picha zake ambazo mmewahi
kupiga pamoja” david akachacha maa kumtaka
kumjua huyo helman mapesa mwenye sifa za
ukatili
“Ndio ninazo lakini zipo nyumbani kwangu”
mwajuma alimjibu
“Samahani naomba tuelekee huko nyumbani
kwako
ukanioneshe hizo picha nakuomba sana” david
alizidi kumbembeleza yule dada mpaka mwajuma
akaingiwa na wasiwasi,na kumuuliza,,
Mbona unaonekana unataka kumjua sana wewe
ni
askari nini? Mwenzio na hofia maisha
yangu,watoto wangu wasije kuishi kwa mashaka
kwa hilo sitoweza kukusaidia kaka kwaheri”
Mwajuma alivyoona maswali yanazidi kuwa
mengi
akaamua kumuacha David pale alipo na kuondoka
zake huku akimuachia kitisho,,
“ukinifuata na kuitia mwizi na kuheshimu, kama
msaada wenyewe ndio huo wa kutaka kuniingiza
kwenye matatizo basi, kama unataka kumjua
tafuta madangulo nimekwambia hakuna Malaya
asiye mjua”
David hakuwa na jinsi maana maeneo yale
anayakumbuka vizuri sane aliponusurika
kuuwawa
kwa shtuma za wizi siku ya kwanza kabisa
alipokuwa anaingia jijini, alimuuangalia yule dada
ambaye aliamua kupanda boda boda na kuishia
zake.
Alinyakuwa mkono wake na kuangalia saa
ambayo
ilimuonesha kuwa ni saa mbili kasoro, ikabidi
achukue simu yake na kumpigia afande criss
kisha
kumueleza kuwa atachelewa kurudi nyumbani
siku
hiyo, na alipomaliza mazungumzo naye
alinyanyuka baada ya kuwa ameshalipia chakula
na kupanda daladala iliyokuwa inaelekea
Buguruni,
Dereva wa dalala alijitahidi kuikwepa foleni
iliyokuwa barabarani mpaka kufika buguruni
ambapo david alishuka na kuulizia sehemu
ambayo
kuna wanawake wanao jiuza,
Watu hawakuwa na roho mbaya walimuonesha,
japo walimuuliza maswali machache na kumpa
ushauri juu ya afya yake kwa kwenda kuchukua
wanawake wanao uuza miili yao,
Wanawake walionekana ni wengi na wenye umri
mdogo waliopendezeshwa na nguo zao fupi za
anasa, david alizidi kushangaa kuona mpaka watu
wazima wenye umri ambao ungeweza kufanana
na
marehemu mama yake pia wakifanya biashara ya
kuuza miili yao lakini hakutaka kuhoji sana hilo,
aliwasogelea na kuanza kuthaminisha kama
anachagua nguo dukani mwishowe aliweza
kumpata mwanamke mmoja ambaye ni mzuri
kimuonekano lakini uzuri wake ulijitia doa kwa
biashara aliyokuwa anaifanya, walikubariana bei
na
david akaahidi kumpatia marambili yake kama
atakubali kumsaidia katika mambo yake,
Yule dada hakuwa na shida kwakuwa yupo kipesa
zaidi alikubali na kuongozana na david mpaka
kwenye nyumba moja ya wageni iliyochoka choka
japo ilikuwa inatumiwa sana na wenyeji ipo
uswahilini ambayo haikuwa mbali na kile kituo
chao cha biashara ya kuuza miili.
Dada yule ambaye alijitambulisha kwa jina la
salome akataka kuanza kaziyake ya kumfurahisha
david kwa kutaka kumpatia penzi lakini haikuwa
hivyo david alimuomba asubiri kwanza
wazungumze,ndipo alipomuuliza swali,,,
“unamjua Helman mapesa?”
Swali hilo lilimshtua yule dada na kuanza kuwa
na
hofu kidogo na kujibu,,,
“ndio na mfahamu kwanini umeniiuliza” salome
naye aliuliza swali
“Mmh ni rafiki yangu hivyo aliniambia kuwa
hakuna mtu asiye mjua hivyo nilitaka kuhakikisha
tu” alijibu david
“Helman mapesa kiukweli hakuna mtu asiye mjua
mbali na pesa zake lakini ni mnyanyasaji sana
mimba nyingi amekataa na ukimlazimisha
anakutishia kukuua hivyo wanasichana wengi
huamua kukaa kimya tu” salome alizungumza
“Aisee lakini mimi nilikuwa sijui hilo maana
sikuwa
nae muda mrefu nimekuja hivi karibuni tu kutoka
arusha, na vipi kuhusu mwajuma
unamfahamu?”david alizungumza
“Mmh mwajuma na mfahamu si yule anaye kaa
jangwani? naye ni mmoja wa wanawake ambao
wametelekezwa na Helman mapesa lakini kaka
samahani sana Helman mapesa huwa hapendi
mambo yake yatangazwe ovyo mimi naogopa.
Salome alikuwa nazungumza kwa wasiwasi sana
na ghafla hali ya hewa ikaanza kubadilika
mapanzia ya ile nyumba ya wageni yakaanza
kupepea kwa upepo mkali uliokuwa unavuma,
david alinyanyuka na kuanza kuyafunga punde si
punde mlango wa chumba hicho alichokuwa david
na salome hodi ikawa inagongwa, david aligeuka
na kuutazama mlango kwa muda na kumwambia
salome aende kuufungua,
Salome alikwenda na kufanya hivyo alipo maliza
kufungua tu ule mlango ukasukumwa kwa nguvu
na watu walio shiba wakaingia mle ndani huku
wakiwa wameshika mitutu ya bunduki
David alipokuwa anataka kuwa hoji alipigwa na
kitako cha bunduki na kudondoka chini, mikono
yake ikiendelea kusugua yale maumivu ya pale
kifuani alipokuwa amepigwa,, salome aliingiza
kichwa chake chini ya uvungu wa kitanda kwa
uwoga,,
“Ole wake mtu yoyote apige kelele humu ndani
tunammaliza hapahapa” alizungumza mmoja kati
ya wale majambazi huku wengine wawili
wikichungulia nje ambapo magari ya polisi yakiwa
yanapita kwa kasi na baada ya muda kimya cha
magari na vuguvugu la polisi kule nje wale
majambazi walitoka mbio mbio bila kuwafanya
chochote kina david.
“Hawa bila shaka watakuwa wametoka kufanya
tukio mahali sasa wanakimbizwa na
polisi”alijisem
ea david moyoni.
Salome baada ya kuona hali imekuwa tulivu
alinyanyuka na kukusanya vitu vyake huku
akijisema mwenyewe ovyo,,
“kuanzia leo mimi umalaya basi” akawa
anaondoka kwa kuchanganyikiwa,,
“ Salome chukua basi pesa yako ya usumbufu”
david alizungumza,
“Sitaki kaa nayo tu” alijibu salome wakati
anaishia
kwa kasi,
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA ISHIRINI
“Ole wake mtu yoyote apige kelele humu ndani
tunammaliza hapahapa” alizungumza mmoja kati
ya wale majambazi huku wengine wawili
wikichungulia nje ambapo magari ya polisi yakiwa
yanapita kwa kasi na baada ya muda kimya cha
magari na vuguvugu la polisi kule nje wale
majambazi walitoka mbio mbio bila kuwafanya
chochote kina david.
“Hawa bila shaka watakuwa wametoka kufanya
tukio mahali sasa wanakimbizwa na
polisi”alijisem
ea david moyoni.
Salome baada ya kuona hali imekuwa tulivu
alinyanyuka na kukusanya vitu vyake huku
akijisema mwenyewe ovyo,,
“kuanzia leo mimi umalaya basi” akawa
anaondoka kwa kuchanganyikiwa,,
“ Salome chukua basi pesa yako ya usumbufu”
david alizungumza,
“Sitaki kaa nayo tu” alijibu salome wakati
anaishia
kwa kasi,,
David naye hakuwa na jinsi ilibidi aondoke huku
akiwa amesha pajua nyumbani kwa kina
mwajuma
baada ya salome kulitaja eneo ambalo analokaa
mwajuma,
Alifika nyumbani kwao usiku sana na kumkuta
afande criss akiwa kachukua pale sebuleni baada
ya kumpa onyo,,,
“David najua umekuwa sasa lakini tabia hii ya
kuchelewa kurudi tena usiku siipendi kumbuka
bado unakazi nzito mbele yako na hujui mbaya
wako nani mpaka sasa hivyo kuwa makini”
David alitingisha kichwa kukubali na kuomba
radhi
kisha akawa anataka kuelekea chumbani kwake
kulala lakini alipogeuza mgongo tu afande criss
alimuita na kumwambia,,
“david, kumbuka kesho inabidi twende kwenye ile
ofisi ukaanze kazi hivyo jiandae vizuri na uwahi
kuamka usiku mwema”
“Sawa baba” david alijibu kwa unyonge kisha
kuelekea chumbani huku akiwa kashika ile
bahasha
yake aliyotoka nayo kutoa chapa ya sahihi
aliyotoka nayo kule gerezani.
mwili wa david ulikuwa umechoka kwa pilika
pilika
za mchana kutwa hivyo aliweza kulala fofofo.
Mpaka alfajiri alipo amshwa na hodi ambayo
ilikuwa inagongwa na afande criss kwa ajili ya
kijiandaa ili waelekee maeneo ya posta ambao
ofisi
ya shirika linaloshughulika na kukomboa vijana
kutoka hali tete na watoto yatima. Linaloitwa
“upendo toka moyoni”
David alijinyakuwa pale kwenye kitanda na
kwenda
kujiandaa na baada ya muda akawa yuko tayari
hivyo wakaongozana na afande criss mpaka
posta
kwenye shirika la” upendo toka moyoni” kisha
kuonana na bosi wa shirika ilo ambaye alifurahi
sana kuona uwepo wa david,
Bossi huyo ambaye aliweza kumtambulisha david
kwa wafanya kazi wengine ambao walikuwa
wakifanya kazi hapo kwa muda mrefu, david
alioneshwa ofisi yake ambayo ilikuwa na hadhi ya
kuitwa ofisi na baada ya hapo akaanza
kuelekezwa
jinsi ya ufanyaji wa kazi na kupewa maelezo
mengi
kuhusu shirika hilo.
Jioni ilipofika baada ya muda wa kazi kuisha,
wakati david akirudi kuelekea kwao akiwa
amepita
barabara ya morogoro aliweza kumuona mtu kwa
mbali kama mwajuma akihangaika ndipo
alipoomba ashushwe pale maeneo ya jagwani,
japo
hali ilikuwa si shwari maana maji yalikuwa
yanataka kujaa kutokana na mvua zilizokuwa
zikiendelela kunyesha kwa msimu huo,
Alimfuatilia kimyakimya na kumkuta akihamisha
baadhi ya vyombo vyake kupeleka kwa jirani
baada
ya nyumba aliykuwa anakaa maji kuingia ndani
na
baadhi ya vitu kuharibika,mwajuma alishtuka
kuona uwepo wa david pale maana hakuwahi
kumuelekeza anapoishi, alimtazama kisha
mwajuma akajifanya kama hajamuona vile na
kuamua kutaka kuondoka, david alimuita kwa
upole
na kumsogelea kisha kumuomba,,
“samahani mwajuma, jaribu kunielewa mimi sio
askari na wala sina nia mbaya ya kutaka
kukuingiza matatizoni ila ninalengo la kutaka
kukusaidia kama utanipa picha ya huyo jamaa
anayeitwa Helman mapesa”
Kabla mwajuma hajajibu chochote kile, sauti ya
mtoto wa kike ikawa inasogea huku akiwa
kambeba mtoto mdogo mgongoni ambaye
alikuwa
analia na kutetemeka na baridi kisha kusema,,,
“mama njaa inauma”
David alimwangalia mwajuma na kumuuliza,,,
“hawa ndio watoto wako?”
Swali hilo lilimfanya mwajuma kujisikia aibu
kujibu
maana hali waliokuwa nayo watoto wake ilikuwa
haiendani na uzuri wake wala kama david
alivyomuona siku ya kwanza kule kwenye
mgahawa maeneno ya ubungo, david akawa
anahuakika kuwa hawa ni watoto wa mwajuma
maana wasingeweza kuja na kumuita mama
kisha
kumlalamikia njaa, hivyo david akainama na
kumuuliza yule mkubwa amabye kidogo alikuwa
anajua kuongea,,,
“unaitwa nani mtoto mzuri?”
“Nisha” kile kitoto kilijibu jibu ambalo lilimfanya
david ashtuke kidogo na kumuuliza tena,
“Nani amekupa jina hili zuri”
“mama” kilijibu kile kitoto,
David aliingiza mkno mfukoni na kutoa elfutano
kisha kumpatia yule mtoto, na kujinyakuwa pale
alipokuwa amesimama na kuanza kuzungumza na
mwajuma,,,
“mwajuma tazama hali ya watoto wako ilivyo na
hili baridi, pia fikiria eneo hili si salama kuishi
cheki mvua kidogo tu imeweza kuingia mpaka
ndani ya nyumba yako vipi kuhusu mafuriko
yakija
huoni kama unaweza kuipoteza familia yako?
Tafadhali nioneshe hizo picha mimi nikusaidie.
Maneno hayo yaliweza kugusa moyo wa
mwajuma
lakini jibu alilompatia david lilikuwa halina faida
kwa upande wa david,,,
“kaka nashukuru kwa kuonesha moyo wa
kuguswa
na tatizo langu, nami ningeweza kukusaidia lakini
kwa bahati mbaya maji haya yalioingia ndani
yameharibu vitu vingi na albamu ya kuwekea
picha
imeharibika yani picha niliyobaki nayo ni ya rafiki
yangu kipenzi niliyo ibandika juu ya ukuta.
ambaye
sikuweza kuishi naye kwa muda mrefu akanipotea
na sijui wapi alipokwenda ni muda mrefu sana
tangu nikiwa bado msichana mdogo sana ndio
maana ilikumuenzi nikaamua jina lake kumpatia
huyu mwanangu Nisha”
David hakuamini alichokisikia ikabidi aulize tena
umesema rafiki yako alikuwa anaitwa nani?
“Nisha” mwajuma alijibu,
“Tafadhali naomba unioneshe picha ya huyo rafiki
yako nakuomba sana, nitakupa kiasi chochote
cha
fedha ambacho unataka pia nitakuhamisha hapa
ambapo unakaa tafadhali naomba unisaidie yani
hiyo ni muhimu kuliko hata hiyo iliyopotea ya
Helman mapesa” david alionesha huzuni
Mwajuma akawa anashindwa kuelewa kwanini
david kila anachotajiwa yeye anakitaka kukiona
lakini hakuwa na jinsi ikabidi waongozane na
david
mpaka chumbani ambako kulikuwa na maji
ambayo yalikuwa yanakaribia magoti huku baadhi
ya vitu ambavyo vilikuwa havija tolewa vikiwa
vinaelea juu juu,
David bila hata kujali yale maji akaingia na viatu
moja kwa moja na ndipo mwajuma aliponyoosha
kidole juu kumuonesha ile picha ndogo iliyokuwa
pale juu ya ukuta, na kwakuwa david alikuwa
mrefu hivyo aliweza kunyoosha mkono tu na
kuitoa
ile picha.
Picha ilishikwa vizuri kwenye mikono ya david na
kuanza kuitazama kwa makini kwa kuisogeza
karibu na macho yake, jicho lilibadirika na rangi
na
kuanza kudodosha mchozi wa hasira
uliochanganyika na huzuni, kiganja chake kikawa
kinapapasa juu ya uso kwenye ile picha kisha
kuinua sura yake na kumtazama mwajuma na
kumwambia,,,,,,
“mwajuma huyu ni nisha wangu kabisa”
huku mdomo ukitetemeka kwa uchungu mwajuma
hakumuelewa na akaamua kumuuliza swali,,,,
“unamaana gani kusema nisha wako na unalia
kwa
nini?”
“naamaanisha ni mdogo wangu kabisa wa
kuzaliwa naye tumbo moja na nina mtafuta leo
kesho lakini bila mafanikio mpaka sasa
nimepotezana naye muda mrefu sasa na kwasasa
anaweza kuwa na umri kama wako na huenda
akaitwa mama pia kwani wewe ulikutana naye
wapi?”david alijibu na kuuliza swali,
“nisha japotulikuwa wadogo lakini aliweza
kunisaidia nilipotaka kubakwa na wahuni majira
ya
saa 4 usiku maeneo ya manzese darajani mahali
ambapo ndipo yalipokuwa makazi yangu kabla
sijaaingia kwenye ulimwengu wa kujiuza,
alinisaidia kupiga mayowe na watu wakaja
kutusaidia na kuna mama mmoja akaamua
kutupa
hifadhi kwake lakini kumbe alikuwa anafanya
biashara ya kuuza mwili hivyo nasi tukajiunga
naye, kiukweli mimi na nisha tumeingia kwenye
biashara hii tukiwa na umri mdogo sana na
sidhani
kama nisha alikuwa amesha kuwa vizuri kwa
wakati ule lakini hatukuwa na jinsi kwa kuwa
tulikuwa hatuna pakwenda ilibidi tukubaliane na
hali, lakini nisha kitendo kile cha kuuza mwili
hakuridhika nacho japo alikuwa mdogo ila
alikuwa
na upeo mkubwa wa kufikiria ndio maana
akaamua
kutoroka na sikujua alipo elekea, nilitamani kujua
kilichomkuta lakini alikataa kunieleza kabisa”
Mwajuma aliweza kumpa maelezo david japo
yalikuwa mafupi lakini yalieleweka, mpaka
mwajuma anamaliza kusema hayo naye mchozi
ukawa unamtoka.david alijilazimisha
kumbembeleza mwajuma kisha kutoa kiasi cha
fedha kumpatia na kumwambia akachukue
chumba
kwenye nyumba ya wageni halafu kesho waonane
ili ajue atamsaidiaje kisha david kuelekea kwao.
Siku hiyo ilikatika na david siku inayofuata
alionana na mwajuma na akaamua kumsaidia
kumpangia vyumba viwili maeneo ya kimara,
kitendo hicho mpenzi wake Victoria aliweza
kukusikia na akahisi huenda atakuwa in kimada
cha david hivyo ugomvi baridi ukachukua nafasi
katika penzi lao na Victoria kumtaka
akajitambulishe kwao na ikiwezekana
waoane,swala hilo david alilikubali lakini
akamuambia asubiri kidogo mpaka atakapoweka
mambo sawa ndio atakwenda huko
kujitambulisha, ********************Â-
******************
Miaka miwili ilikatika bila ya david kuvuna
chochote kile maana hakufanikiwa kumpata nisha
wala helman japo alikuwa anamuwinda kule
maeneo ya mbezi beach alipoelekezwa kuwa
ndipo
anapoishi yeye na familia yake na mungu aliweza
kujaalia david kwakuwa alianza kujitegemea
mwenyewe kwenye nyumba nzuri ya kupanga na
kuwa na usafiri wake binafsi.
Siku moja jumatatu asubuhi bosi wa shirika hilo
aliitisha kikao cha ghafla baada ya kupokea
wageni wawili asio wajua wakisema kuwa
wanataka kuwekeza kwenye shirika hilo hivyo
wafanya kazi waliombwa wachangie mawazo yao
na david akapewa fursa ya kwanza kabisa,,,,
“bosi mimi mtazamo wangu kama muhasibu wa
shirika nafikiri kwa sasa tusiwapokee mpaka
mwaka unao fuata ili tuweze kumaliza mikataba
na
wawekezaji wengine”
David alitoa mtazamo wake lakini wafanya kazi
wengine walionekana kuupinga vikali hivyo wazo
lake likaonekana halina maana, na hapo sekretali
ikabidi aagizwe akawaite wale wageni wawili
waliokuwa wanaonekana wa heshima ila baadhi
ya
wafanyakazi wa kike wakawa wananyoosha
nyoosha vidole kwa mgeni mmoja,
Baada ya muda ikabidi mikataba iletwe
iliwaandikishahe na sehemu za kujaza zilikuwa
sehemu ya mwanaseheria upende wa mwekezaji
na upande wa mwenye shirika, sehemu ya
mwekezaji mwenyewe na bosi wa shirika na
sehemu ya mwisho ni ya muhasibu na wote
waliweza kujaza vyema na nafasi ya mwisho
ilikuwa ni ya muhasibu ambaye ni david, baada
ya
karatasi kuzunguka kwa watu wengine pale
mezani
na ikawa imemfikia yeye,
Wakati akiendelea kukagua walipo weka sahihi
wengine kabla ya yeye kuweka hakuamini alicho
kiona kwenye zile karatasi hasa pale kwenye
nafasi
ya mwekezaji mkuu, mkono wake ulitetemeka
mpaka ile peni aliyokuwa ameishika ikaanguka
chini, watu wakaanza kumshangaa usoni baada
ya
kuona sura inabadrika na kuwa ya kigaidi na
moyo
wa kinaadamu ukamtoka david ghafla ni baada
ya
kuionaa sahihi inayofanana na ile aliyotoka nayo
kule gerezani ambayo in ya mtu wa mwisho
kwenda kumuona marehemu baba yake na
yawezekana ndio alikuwa anahusikia na mauaji
ya
baba yake,
David aliinua macho yake yalionza kuloa mchozi
na
kuwatazama wale wageni kwa makini usoni kisha
kuita kwa nguvu Helmannnnnnnnnn
nnnnnnnnnnnnnnnnnnnn!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!-------------“
Sauti ile ya david ilimshtua kila mtu mle ndani,
wote waliduwaa, helman kwa mshtuko akajikuta
kaitika naam, masikio ya david yalivyosikia tu
helman kaitika na macho yake kukiri kumuona
mbaya wake, viungo vya mwili wa david
havikusita
kujipa ushirikiano kwa pamoja, baada ya matukio
yaliomtokea kujirudia kichwani mwake ghafla
david
akamrukia helman na kuanza kumpatia kipigo cha
hasira cha harakaharaka bila kujali bosi wake
aliyekuwepo pale huku maneno ya fadhaa
yakimtoka mdomoni mwake,,,,,,,
“huyu ni muuaji kabisa hastaili kuishi katika dunia
hii ya waugwana hata kidogo, baradhuli mkubwa
huyu”
watuwalijitahidi kumshikiria david wakati helman
akiwa kaumizwa kiasi na damu chache kumtoka
usoni, yule mwenzie aliye kuja na helman pale
ofisi
akaona mambo yamesha haribika hivyo akatafuta
upenyo akakimbia, kitendo kile kilmshtua bosi
wake
na david akahisi ya wezekana kweli kuna tatizo
hapo, ikabidi apige simu kituoni kilichokuwa
karibu
na posta ya zamani, huku helman akiwa
ameshikiliwa na wafanya kazi wa pale.
david alikuwa bado na hasira moyoni mwake
alikasirika sana wenzie walivyomshika kama yeye
ni mtuhumiwa vile, walipokuwa wanajisahau tu,
david alikuwa anataka kumrukia tena helman,
Helman alishindwa kumjua david mpaka dakika
hiyo japo alishajua atakuwa ni mmoja kati ya
watu
ambao Alisha wahi kuwafanyia ubaya maana ndio
ilikuwa tabia yake.
Muda si mrefu askari wakawa wamefika eneo la
tukio walivyouliza tatizo na kupewa kwa ufupi
basi
hawakuwa na jinsi wakaamua kuwafunga wote
pingu maana kulikuwa hakuna ushahidi wa
kutosha kwa muda huo na kosa alilolifanya david
in kujichukulia sheria mkononi ndio maana naye
akalazimika kufungwa pingu,
ITAENDELEA
 
MWISHO SEHEMU YA KWANZA
Helman alishindwa kumjua david mpaka dakika
hiyo japo alishajua atakuwa ni mmoja kati ya
watu
ambao Alisha wahi kuwafanyia ubaya maana ndio
ilikuwa tabia yake.
Muda si mrefu askari wakawa wamefika eneo la
tukio walivyouliza tatizo na kupewa kwa ufupi
basi
hawakuwa na jinsi wakaamua kuwafunga wote
pingu maana kulikuwa hakuna ushahidi wa
kutosha kwa muda huo na kosa alilolifanya david
in kujichukulia sheria mkononi ndio maana naye
akalazimika kufungwa pingu,
Wakati wanatoka ndani ya ofisi kuelekea kwenye
gari ya polisi kwa ajili ya safari ya kuelekea
kituoni, david alimkuta mpenzi wake Victoria
ambaye alishakuwa mjamzito wa miezi tisa na
aliishi na mimba hiyo kwa mashaka na mama
yake
maana david alikataa kwenda kujitambulisha
mapema lakini mama yake na Victoria hakutaka
kumfukuza mwanae tangu alivyogundua ni mja
mzito wa miezi miwili, na sasa baada ya kuilea
mimba mpaka kufikia miezi tisa hakutaka Victoria
ajifungue bila mwenye ujauzito kumjua, hivyo
akamlazimisha amtafute aliye mpa ujauzito na
aende naye kumtambulisha hiyo ndio sababu
iliyomfanya Victoria kwenda ofisi kwa david muda
huo,
Lakini hali aliyoikuta ilikuwa si shwari kabisa
alikosa muda wa kuzungumza na david maana
alikuwa chini ya ulinzi wa polisi, na Victoria
alishindwa kuelewa kinachoendelea maana david
hakuwahi kumueleza chochote juu ya masiha
yake
aliyopitia huko nyuma,
Macho yao yenye huzuni na upendo ndani yake
yalitazamana wakati david alivyokuwa
anapandishwa kwenye gari na Victoria akiendelea
kuwa vuta mashati wale askari kutaka kujua
mpenzi wake kafanya nini ila jibu alilopewa ni
kwamba aende kituoni huko atajua yote yaliojiri.
Victoria hakuwa na jinsi ilimbidi achukue simu
yake
huku akiwa na hofu moyoni na kuanza kumpigia
mama yake kumpatia taarifa,,,,,
“Hallo mama ,baba wa ujauzito huu amepata
matatizo na hapa naelekea kituo cha polisi
kilichopo karibu na posta ya zamani”
Mama yake naye alipata mshtuko juu ya taarifa
hizo akamjibu,,
“nakuja mwanangu sasa hivi”
Gari ya polisi ilivyoondoka na Victoria
hakuchelewa, akapanda pikipiki na kuwa fuata
kule
walipokuwa wanaelekea.
***************************
Walifika kituoni na askari wakaanza kumuhoji
david,,,
“Kwanini umechukua sheria mkononi kumpiga mtu
bila kosa” alihoji askari mmoja
“Huyu anamakosa mengi sana ambayo serikali
wanayafumbia macho,haki yake ya kuishi
imeshakwisha hapa duniani lazima awafuate
aliowatanguliza kwa hila zake na mkono wake
mwenyewe kuliko kuendelea kuishi tena kwa jeshi
hili la nchi yetu lenye sera ya mwenye pesa hana
kosa,,,,,”
David alikuwa na jazba akawa anazidi kutoa
uwozo wa serikali bila kujali eneo alilopo, kitendo
hicho askari walichukia na kuanza kumpa kipondo
kwanini anaidharau serikali lakini david
hakukubali
alizidi kutoa maneno ya kashfa huku akicheka
kicheko kilichoambatana na dharau,,,,,
“hahahahah hakuna maumivu makali kama yale
yanayohifadhiwa moyoni tena bila kujua
yanaishalini,hivyo nipigeni tu maana ndio
manafikiri suluhisho bila kuchunguza na kutaka
kujua ukweli uko wapi,
“ nini faida ya wewe kusoma? Au kuwa askari
maana yake huna utu moyoni mwako ambao
unashindwa kujua maumivu anayoyapata kiumbe
kisicho na hatia na kumtumikia yule ambaye
kesho
atakuja kukugeuka utakaposhindwa kumtimizia
jambo lake, jaribuni kutumia akili kabla hamja
fanya maamuzi”
David alizidi kuwapa maneno makali huku
akiendelea kupigwa na marumbano hayo yaliweza
kusikika na mkuu wa kituo ambayo yalionekana
kumkera sana ndipo alipotoka nje na kufanya
jambo ambalo david alizidi kushangaa,,,,,,
“Helman,,!!!!!
“Freizo!!!!!!
Mkuu wa kituo hicho alishangaa kumuona rafiki
yake kipenzi helman yupo ndani ya pingu na
helman alishangaa kumuona rafiki yake yupo pale
kituoni tena akiwa na cheo maana ni muda mrefu
sana hawa kuonana.
“vipi mbona wamekufunga pingu tatizo nini?”
aliuliza mkuu wa kituo na wakati huo Victoria
anawasili mle ndani na helman alipomuona
Victoria
akamkumbuka wakati wanapandishwa kwenye
gari
kupelekwa kituoni hivyo alijua huyu ni mpenzi
wake
na david tu japo kwa wakati huo bado hajamjua
kama ni mtoto wa marehemu alfred kazinge ndipo
alipoamua kusema,,,
“hawa vijana wa sasa hivi si unajua tena
wanataka kwenda sawa na wakubwa, niliwahi
kumuona sehemu moja ya starehe huko akiwa
kazungukwa na wanawake sasa kuna msichana
mmoja na mjua kati ya wale waliokuwa
wamemzunguka ikabidi ni muuite na alipokuja
nikamueleza nilicho muitia na nilipotaka kuondoka
akaniomba in mpatie lifti maana hakuona faida
ya
kukaa na huyu mtoto sasa nafikiri huyu kijana
alihisi kuwa nina mahusiano na yule changudoa
ndio leo tumeonana katika maswala ya kujenga
taifa akanikumbuka akaanza kunirukia na
kunishambulia vikali”
Victoria alichukia kusikia maneno yale yaliokuwa
yanazungumzwa na helman, aliamini moja kwa
moja kuwa ni kweli maana helman alikuwa mtu
mzima na muonekano wake kama humjui lazima
uwamini anachokisema, Victoria aliangua kilio
pale
kituoni, akawa anamsogelea huku mkono wa
kushoto akiwa kajishika kiuno na wakulia
kashikilia
mimba yake kubwa na kuanza kutoa maneno ya
hasira,,,,
“David kumbe ulikuwa unakataa kuja
kujitambulisha kwa sababu ya huo ujinga unao
ufanya huko sehemu za starehe? In bora
ungeniambia mapema kama huniitaji, tazama
nimegombana na mama yangu juu ya ujauzito
huu
kwa kukaa kimya bila kukutaja, kumbe wewe ni
mshenzi eeh kwanini lakini umenifanyia hivi?”
Victoria alilalamika kwa uchungu, david
akashindwa aseme lipi maana hasira zilimpanda
mpaka akawa anashindwa kuongea alibaki akiita
tu jina la helman huku jicho limemuiva alipotaka
kusema kitu ghafla waliingia watu wawili kwa
haraka, mwanaume mmoja na mwanamke mmoja
ambaye naye alikuwa mja mzito ambao
ulionekana
unalingana kabisa na ule wa Victoria,,
“Baba vipi uko salama kweli maana nilipigiwa
simu
na mtu nisiyemjua kuwa umekamatwa na polisi
na
kwa bahati nzuri sikuwa mbali mimi na mke
wangu
hivyo ndio maana nimekuja haraka tatizo nini
lakini?”
yule mwanaume kulikuwa na dalili zote kuwa in
mtoto wa helman maana alivyoingia tu alianza
kumuita baba lakini david hakuwa na uhakika
mpaka aliposibitisha kwa kauli ya helman,,,,,
“usijali john mwanangu jambo la kawaida tu na
nafikiri litaisha tu maana huyu kijana ndiye
aliyekuwa ananiletea fujo(alimnyooshea kidole
david).
ndipo john mtoto wa helman pamoja na mkewe
ambaye ni mmjamzito wakamuangalia kwa
pamoja
david ambaye mchozi ulikuwa unamtoka maana
alinyimwa kabisa nafasi ya kusema,
macho ya david yalishikwa na kigugumizi kila
alipokuwa anamtazama yule mke wa john mtoto
wa helman, alimsahili kutoka juu mpaka chini
zaidi
ya mara mbili mpaka john akamuuliza kwa ukali,,
“wewe vipi mbona mnamtazama sana mke wangu
kiasi hicho” na helman naye akapata nafasi ya
kukazia neon ambalo lilizidi kuweka uwaminifu
kwa
Victoria ni kweli david alikuwa msharati,
“Kazoea huyo maana hata mimi kanidhuru kwa
sababu ya wanawake”aliungumza helman
Kwakuwa mkuu wa kituo hicho bwana freizo
alikuwa anamfahamu helman basi askari wa hapo
walishindwa kuingilia maongezi hayo maana
hayakuwa chini yao tena ndio maana yakawa
yanaendelea kama mchezo wa kuigiza,,
“uso wako haupotei, kichwani mwangu nakiri hata
kama ungekuwa umezeeka lakini kamwe
usingeweza kutoka kichwani mwangu, tazama
ulivyokuwa sasa unafanana kabisa na mama”
david alijitahidi kunyakuwa mkono na
kumuonesha
ishara yule mke wa john kuwa amsogelee jambo
ambalo kila mtu alishangaa na kushindwa
kumuelewa kwa nini anazungumza vile na kutoa
ishara kama zile mpaka mdomo wake na ulimi
wake kushirikiana kutoa maneno ya unyenyekevu
yalioonesha upendo wa dhati kabisa,,,
“Nisha! Nisha!”
David alimuita mke wa john lakini hakuitika yule
madada, hakuchoka akamueleza,,
“Nisha mdogo wangu siamani kama bado unaishi
na leo nimekuona tena! Mimi ni kaka yako david
nisha mbona hunijibu dada? Kumbuka shida ngapi
tumepata mimi na wewe leo hii unashindwa
kuniita
kaka kama zamani tafadhali nijibu mdogo wangu,
ndoto zangu nikuwa na wewe kwenye dunia hii
maana ndiye ndugu yangu uliyebaki,sikuzote
ulizokuwa mbali lakini bado ulikuwa unaishi nami
kichwani mwangu”
Macho ya david yalikuwa na uhakika kabisa kuwa
yule mke wa john mtoto wa helman ni nisha
mdogo wake lakini alichokuwa anashindwa
kuelewa mbona hajibiwi kila akimuita ndipo
alipotaka kutoka kwa nguvu pale chini ya ulinzi
wa
polisi ili amsogelee karibu, huenda nisha
akamkumbuka david,lakini alizuiwa na askari,
hapo
sasa ndipo wakawa wamehamsha zaidi hasira za
david na mdomo wake haukusita kuongea kwa
nguvu,,,,
“umepewa nini nisha mdogo wangu hii sio familia
ya kuolewa nayo huyu helman ndio anahusika na
kifo cha baba yetu kule gerezani na ndio chanzo
cha matatizo yote haya lakini serikali
imemmfumbia macho na bado kaona haoitoshi
kaamua kukuteka kupitia mwanae,,,,,”
David kabla hajamaliza kusema yule mke wa john
alikana jina hilo tena kwa sauti ya ukali,,,
“tafadhali wewe kaka, sikujui na wala hunijui
mimi
siitwi nisha na wala sina ndugu, utakuwa
umenifananisha, jina langu naitwa “Nashrifa”
kama
umenifananisha na hao machangudoa wako
wanaokufanya mpaka uvamie wakwe za watu
hapa
umekosea upo hapo?”
Jibu la nashrifa ambaye ni mke wa john mtoto wa
helman lilizidi kumkera david na askari wote
wakacheka kwa daharau, walijasahau kuwa lile ni
jengo la serikali na haki ilikuwa inatakiwa
kufuatwa
lakini wakawa wanatazama tu yule marumbano,
david mchozi ukazidi kumtoka mpaka Victoria
mpenzi wake aliyekuwa pembeni akaanza
kumuonea huruma na alilikumbuka jina la nisha
wakati wako chuo nchini Rwandalilimfanya david
kupoteza fahamu mbele ya umati wa watu chini
ya
ugeni wa rais paul kagame, lakini hakuwa na
chakusema hapo naye akaangua kilio cha kwikwi
baada ya kuona mpenzi wake anadhalilishwa,
Na kilicho washangaza zaidi Victoria na david
pamoja na askari wengine ambao waliokuwa
wanajielewa na kujua haki ni baada ya mkuu wa
kituo ndugu freizo kutoa amri kuwa helman
afunguliwe pingu na david awekwe mahabusu
kwa
kosa la kumdhalilisha helman, david hakujali hilo
kikubwa kwa wakati huo alikuwa anamataka
nisha
wake tu ndipo aliposema,,,,
“wewe ni nisha mdogo wangu mimi sijui hilo jina
la
nashrifa umelipata vipi? Na mgongoni kwako una
alama ya kovu ambalo nilitegemea lingekuwa
pigo
kwako maana ulilipata kwenye ajali
iliyosababisha
mdogo wetu dason kupoteza maisha siku chache
baada ya kumzika mama yetu mzazi.
Mchozi ulimtoka david wakati anazungumza na
kuona bado mdogo wake nisha kama anaonekana
kutoelewa kinachoendelea, lakini maneno hayo
kwa
upande wa john yalionekana kumuingia baada ya
kuwaza,,,,
“inawezekana kuna ukweli ya haya anayoyasema
huyu jamaa maana huyu ni mke wangu mimi na
ni
kweli anahilo kovu mgongoni na hakuna mtu
ambaye angeweza kujua zaidi yangu kwakuwa
mimi ndio nina uhuru na mwili wake na hajawahi
kuvaa nguo ambayo inamuonesha mgongo kwa
kuhofia hilo kovu lisionekane,,,,,”
John mtoto wa helman alipokuwa anaendela
kuwaza jambo hilo ghafla mama Victoria na
afande
criss walionekana wanaingia kwa pamoja na
hakuna aliyekuwa anajua kama wapo safari
mmoja
kwakuwa kila mmoja alikuja kivyake na
walikutana
tu hapo mlangoni,,
Victoria baada ya kumuona mama yake
alimkimbilia na kumkumbatia huku akilia kwa
uchungu, afande criss alivyo ingia wale askari
wadogowadogo walimpa heshima yake kikamanda
kwa kuwazidi cheo,
Macho ya mama Victoria yalifanikiwa kumuona
david na nisha aliweza kumkumbuka sana
kwakuwa alikuwa mkubwa mkubwa wakati enzi
za
uhai wa mama yake alipokuwa anakwenda
kuwasabahi na aliweza kumkumbuka nisha
maana
sura yake ilikuwa inafanana kabisa na rafiki yake
kipenzi marehemu magrety,
Alihisi kama maajabu na kutoamini alichokiona
baada ya kumuona na helman pale, mama
victoria
hakusita kusema neno na kwenda kumkunja
helman,,,
“wewe muuaji cheki ulivyofanya familia hii kuwa
kama watoto wa ndege, umedhurumu mali za
wazazi wao na kuwasababishia matatizo,
“David, nisha( aliwaita) huyu ndio mwenye
malizenu na ushahidi upo wa kutosha,,,”
askari ikabidi wamtoe mama Victoria kwa nguvu
baada ya kumkunja helman na helman akaanza
kumkumbuka yule mama uwoga ukaanza
akumtawala moyoni mwake maana aliona
mwisho
wake umefika, zogo lile wakati likiendelea ghafla
kishindo kizito kikasikika na kutazama alikuwa
nisha kadondoka na povu likawa linamtoka
mdomoni,
Mama Victoria alimwachia helman na kumkimbilia
nisha pale chini alipokuwa amedondoka, david
alijiona ni mwenye kuandamwa na kivuli cha
matatizo baada ya kuona mdogo wake kipenzi
anataka kupoteza maisha mbele yake,
Kauli za majonzi zikamtoka david,,
ITAENDELEA
 
MWISHO SEHEMU YA PILI.
Askari ikabidi wamtoe mama Victoria kwa nguvu
baada ya kumkunja helman na helman akaanza
kumkumbuka yule mama uwoga ukaanza
akumtawala moyoni mwake maana aliona
mwisho
wake umefika, zogo lile wakati likiendelea ghafla
kishindo kizito kikasikika na kutazama alikuwa
nisha kadondoka na povu likawa linamtoka
mdomoni,
Mama Victoria alimwachia helman na kumkimbilia
nisha pale chini alipokuwa amedondoka, david
alijiona ni mwenye kuandamwa na kivuli cha
matatizo baada ya kuona mdogo wake kipenzi
anataka kupoteza maisha mbele yake,
Kauli za majonzi zikamtoka david,,
“ nisha siku zote ulikuwa mbali nami leo unataka
kunitoka mbele ya macho yangu!!!, tafadhali
nisubiri twende huko pamoja na familia hii iwe
imefika mwisho hakuna baba, mama wala
watoto”
Tukio hilo lilizidi kukichanganya kituo cha polisi,
raia wengine waliokuwa nje walibaki wakijiuliza
kulikoni?
David alijitahidi kumuamsha nisha kwa kumtikisa
lakini hakufanikiwa, povu ndio kwanza lilizidi
kumtoka mdomoni mwake, mama Victoria pamoja
na afande criss walipokuwa wanajitahidi kumtoa
pale chini alipokuwa amemkumbatia mdogo
wake ,hawa kufanikiwa kwa kuwazidi nguvu.
David alipoona hali ya nisha inazidi kuwa mbaya,
alinyanyuka kwa hasira na kutupa jicho la
kumtafuta helman kasimama upande gani,
alipomuona tu, alipiga hatua mbili na kurusha
ngumi yenye ujazo ili kumdhuru helman, lakini
wahenga husema hasira hasara, ngumi hiyo
ilimkosa helman na kwenda kumpata kipenzi cha
roho yake Victoria ambaye nae alikuwa mjamzito.
Papo hapo mwili wa Victoria pia ukawa chini ya
sakafu na damu kuanza kumtoka sehemu za siri.
Ghafla mwanga wa kamera ukaonekana kumulika
eneo hilo, kumbe waandishi wa habari walikuwa
wamesha wasiri eneo la tukio, afande criss alitoa
agizo kwa mkuu wa kituo hicho cha polisi kuwa
helman na david wawekwe mahabusu ila ziwe
tofauti kisha wagonjwa wa wahishwe hospitalini
haraka.
Kichwa cha kila mtu kilionekana kuchanganyikiwa
kwa kuhofia kesi kuwa kubwa na kulaumiwa kwa
uzembe hivyo afande freizo nae aliwaamuru
askari
wake kwa kuwa fokea wafanye kama agizo
lilivyotoka kwa afande criss.
John mtoto wa helman alimbeba mkewe nisha na
kumtoa nje ya kituo ili waelekee hospitali huku
nisha akiwa kabebwa na askari,
vinasa sauti vilikuwa karibu kunasa habari na
picha
kupigwa kwa wingi, baadhi ya askari
wakazungushia uzio wa kamba za njano kwa
haraka ili umati uliokuwa umekusanyika wakae
kando, hata waandishi wa habari wakawa
wanakatazwa kuchukua habari.
Mama Victoria mchozi ukawa unamtoka kama
maji
kwenye macho yake, viatu na vitu vingine
alivyokuwa amekwenda navyo aliviona vizito, hata
nguo alizokuwa amezivaa alihisi zinataka
kumvuka,
tumbo la ghafla likamshika hivyo alijikaza na
mtandio wake kiunoni kama dawa ya haraka
kwake
na safari ikawa kuelea agakani hospital ambayo
haikuwa na umbali wa kutosha kutokea hapo.
Pale kituoni zogo likawa lanaendelea kati ya
afande criss na afande freizo ambaye ni mkuu wa
kituo hicho, kutokana na uzembe ambao afande
freizo ameufanya wa kuweka kikao kisicho cha
maana na watuhumiwa bila kuchukua maelezo ya
kutosha na kufungua jarada la kesi.
Walibishana hatimaye walifikia muafaka, jarada la
kesi likafunguliwa na kuandaliwa kwa kupelekwa
mahakamani.
Afande criss baada ya kuweka kila kitu sawa
akamuachia mwenye kituo chake na kuwafuata
walio tangulia hospitali huku david akibaki na
butwaa kwa kutojua nini kitakachoendelea kwa
dada yake wa dhati pamoja na kipenzi chake cha
roho Victoria, alizidi kuhisi yawezekana pia
asitoke
gerezani kama mkewe atapoteza maisha,
kumbukumbu za kifungo cha marehemu baba
yake”
Alfred kazinge” zilimjia na kuona kinataka
kuendana na kifungo chake kwa kuwa naye
amemsababishia matatizo mkewe Victoria.
Afande criss alifika agakani hospital na kukuta
Victoria pamoja na wifi yake nisha wamesha
pelekwa kwenye vyumba vya wa mama
wajawazito” leba” tayari kwa kupewa huduma ya
kwanza, huku mama Victoria akionekana
kuzunguka zunguka kwa kuchanganyikiwa na
jicho
la hasira kumtupia john mtoto wa helman japo
hisia zao zilikuwa kwenye mlango wa wagonjwa
wao wakimsubiri dokta ili kujua usalama wa
wagonjwa wao.
“vipi jamani hali za wagonjwa wetu zinaendeleaje
hapa?” aliuliza afande criss.
“Bado si buheri, ndio wameingizwa kwenye
vyumba
vya matibabu muda mchache uliopita” alijibu john
kwa unyonge
Afande criss alipokuwa anataka kuzungumza na
mama Victoria alikatishwa na sauti ya mlango
uliokuwa unafunguliwa na dokta,
Dokta alivyotoka hakuwa na muda wa kupoteza,
alitoa macho na kurusha mikono kuongea kwa
msisitizo,,,
“ mgonjwa wenu victoria hali yake si nzuri kwa
sasa kutokana na damu nyingi kumtoka na
kupoteza kiwango kikubwa cha damu na yupo
mbioni kujifungua kutokana na mtikisiko
alioupata,
hivyo damu ya haraka yenye grupu A+ inahitajika
ili tuweze kujitahidi kuokoa maisha yake yeye na
mwanae la sivyo tunaweza kumpoteza mama au
mtoto”
Vichwa vilizidi kuwa uma, walijishauri kwa haraka
na mama Victoria kujitolea kutoa damu kuokoa
maisha ya mwanae, wote walielekea kwa dokta
kufanikisha zoezi hilo, kama ilivyo ada kifo cha
nyani miti yote huteleza, baada ya kuchukua
vipimo vya mama victoria ikaonekana damu yake
haiko kundi sawa na la mwanae, hivyo afande
criss
akajitolea pia, nae majibu ya kawa yale yale.
Aliyebaki kuchukuliwa vipimo alikuwa ni john
mtoto
wa helman, alipoombwa kutoa damu yake
alikataa
na kusema kuwa,,,
“mwacheni afe kwani mimi ananihusu nini?, yani
kwa shutma zote ulizo mpa baba yangu pale
kituoni na kumdhalilisha sasa hivi nijipendekeze
kutoa damu yangu hali ya kuwa mzee wangu
anaweza kuozea jela na msababishaji ni wewe
siwezi kufanya kitu kama hicho”, alikata kauli.
Maneno hayo yalimuumiza sana mama Victoria
na
kuwezakupandisha presha yake hatimaye
kudondoka chini na kupoteza fahamu, john
alipoona vile akataka kuondoka lakini aibu
ikamshika akarudi na kukubali kuchukua vipimo,
yawezekana maisha ya Victoria yalikuwa
mikononi
mwa john, baada ya vipimo, damu zao
zilionekana
kuendana bila shida ya aina yoyote ile, papo hapo
dokta alitoka na kwenda kwenye kile chumba
walichokuwepo wagonjwa wake na kutoa agizo la
uandilizi wa vifaa kwa ajili ya upasuaji ili waweze
kumzalisha, kutokana na hali yake ya
kutojitambua
asingeweza kujifungua kwa njia salama.
Wakati wakiendelea kumuhudumia Victoria
ambaye
hali yake ilikuwa mbaya zaidi kutokana na
kupoteza damu nyingi, nisha nae aliyekuwa
amewekewa chupa ya maji ili kurudisha fahamu
yake baada ya kupotea kwa muda, alianza kupiga
kelele za uchungu, madaktari na manesi wengine
walijikusanya na kuumuandaa nae pia kwa ajili ya
kujifungua, kwake ilikuwa al-hamdulilah maana
hakuhitaji upasuaji, njia salama ilitumika.
Siku hiyo ilikuwa kama ya miujiza kwa familia
hiyo
kutokana na matatizo waliyo pitia na mpaka
walipofikia, sauti nyembamba ilisikika ya mtoto
mchanga ikilia kwa sauti kali, nyuso za furaha
zikatawala kwa manesi na madaktari waliokuwa
wanamuhudumia Victoria, japo hali ya Victoria
ilikuwa si nzuri lakini manesi walisema
“ hongera Victoria kwa kupata mtoto mzuri wa
kike
na mwenye afya”
Hazikupita hata dakika kumi na tano upande wa
nisha alipokuwa anazalishwa sauti yenye uzito
kiasi iliyoashiria kuwa ni mtoto wa kiume
amezaliwa ilisikika, unaweza kusema kuwa ni
zaidi
ya miujiza lakini amini kuwa sauti hiyo ya mtoto
wa kiume aliyezaliwa na nisha ndio ilionekana
kurudisha fahamu ya mama Victoria na alijikuta
akiropoka,,,
“nime pata bwana ewe mungu ashukuriwe”
afande criss pamoja na john ambao walikuwa
karibu kumpepelea walishangazwa na kauli yake,
lakini mshangao uliwatoka pale sauti ya viatu vya
madokta iliposikika ikiwasogelea na kuachia
tabasamu kwa kujipongeza kwa kazi nzuri
walioifanya kisha kuwaambia,,,
“ hongereni mungu ameweza kusikia maombi
yenu,
kwa taarifa nzuri ni kwamba Victoria hali yake si
mbaya sana na amefanikiwa kupata mtoto wa
kike
mwenye afya nzuri, kisha dokta wa pili akamalizia
kwa kusema huku akimwangalia mama victoria,,,
“ mama hongera sana kwa bwana mzuri
uliyempata kutoka kwa nisha.
Furaha isiyo na kifani iliwatawala kwa muda
mfupi,
japo john alikuwa anaona haya kwa alichokifanya
na kilichokuwa kinamsaidia ni kwamba mama
Victoria baada ya kurudiwa na fahamu hakujua
kilichotokea muda mchache ulio pita hivyo wote
walijumuika kwa pamoja.
Mungu ametenda maajabu kwa familia hiyo kwa
kuwapa mapacha wa nje waliopishana dakika
chache tu katika kuzaliwa kwao, ghafla nesi
mmoja alitoka na kuwa salimu kisha
kuzungumza,,,
“mnaweza kuja kuwaona watoto mara moja
halafu
mkawaandalie wagonjwa wenu chakula pia
hamtaweza kuzungumza nao kwa kuwa bado,
wapo katika hali ya mapumziko, wote walizidi
kufurahi na kwenda kufanya hivyo, waliwashika
na
kuwa chambua kiungo kimoja baada ya kingine
na
kutoa mfanano juu ya wazazi wao na siku
ilikatika
kwa namna hiyo.
********************
Siku inayofuata asubuhi na mapema afande criss
alikwenda kituoni alikokuwa amefungwa david,
nakufuatilia utaratibu unakwendaje, taarifa
alizopewa ni kwamba jarada la kesi
limeshapelekwa mahakamani, na walikuwa
wanasubiriwa wao tu, pamoja na mashahidi
ambao kila mtuhumiwa amemtaja,
Kwa upande wa david kazinge, amesema kuwa
mshahidi wake ni mama Victoria na helman
mshahidi wake ni mwanae john, ghafla na john
mwenyewe akawa anatokea nae akapatiwa
maelezo hayo.
Afande criss hakuwa na budi kumpigia mama
Victoria na kumueleza juu ya taarifa hizo, na
mama Victoria alikubali kwenda kutoa ushahidi
huo
baada ya kutoka hospitali ambapo mkwe wake
pamoja na mwanae walipokuwa wamelazwa.
Watuhumiwa walitolewa mahabusu na kupelekwa
mahakamani, huku wakisindikizwa na jopo kubwa
la waandishi wa habari, mheshimiwa hakimu
alipowasiri watu walisimama kwa heshima kisha
kukaa na watuhumiwa kupandishwa kizimbani,
Kwa kuwa wote walikuwa ni wakristu basi
waliapishwa kwa bibilia takatifu na kuahidi
kusema
ukweli mtu,
Mahojiano yaliendelea na maelezo yalisikilizwa
kwa
pande zote mbili kwa usawa na umakini mkubwa
kabisa kisha kesi kuahirishwa mpaka saa saba
mchana kuanzia muda wa saa mbili walipokuwa
wameanza,
Saa saba ilipofika kesi ikaanza upya na mama
Victoria alikuwa amesha wasiri mahakamani hapo
tayari kwa kutoa ushahidi,
Hakimu alianza kumuita john kama mshahidi wa
upande wa mshtakiwa , nae akapamda kizimbani
kutoa ushahidi wake baada ya
kuapishwa ,aliulizwa maswali mengi na wakili wa
davdi ambayo alishindwa kuyajibu mpaka
aliporuhusiwa kwenda kuketi, na mama Victoria
kupandishwa kizimbani kama mshahidi wa
mwisho
aliyekuwa anasubiriwa,
Baada ya kupewa uwanja wa kutoa ushahidi
alimtazama helman kwa hasira na jazba ya hali
ya
juu kisha kusema haya,,,,
“ mheshimiwa hakimu mimi sina mengi ya
kuzungumza ila ni kutoa ufafanuzi tu kwa ufupi
kwa kile nilichokiona.
Wakati nikiwa kama muhudumu wa landmark
hoteli iliyopo maeneo ya riverside ubungo, nilipata
kumuona yule mheshimiwa( alimyooshea kidole
helman) akiwa na wenzie walioshiba kiasi pamoja
na wasichana wa wili ambao walikuwa na sifa za
kuwa mapacha kwa mfanano wao, wakiwasiri
pale
majira ya saa moja moja usiku na gari moja
nyeusi
kisha kuchukua chumba ambacho
kilitustaajabisha
baadhi ya wahudumu ambao tulikuwa na upeo
wa
kufikiri baada ya watu hao wasiopungua wanne
kuingia kwa pamoja katika chumba hicho, kwa
kuwa vyumba hivyo vinakamera ambazo si rahisi
kuziona na mara nyingi huzimwa mpaka pale
mteja anapokuwa na shida ya kutaka kitu flani
humohumo chumbani basi huwashwa na
kuelekezwa baada ya kuwa tayari ameshapiga
simu mapokezi,
Hivyo kwakuwa mimi nilikuwa na mashaka nao
kutokana na muonekano wao, nilikwenda kuwa
kwa siri kwenye zile swichi ambazo zipo ukutani
pale mapokezi kisha kuzima ile television
inayoonesha maeneo yote ya hoteli ili wengine
wasiweze kujua kilichokuwa kinaendelea na
kuanza
kupiga kelele kwa hofu au kuwatonya nami
nikapoteza maisha yangu.
Baada ya kukaa ndani humo kwa muda mrefu
niliwakuta wanatoka kisha kuzunguka nyuma ya
hoteli na kuchukua meza moja na kuketi lakini
huyu mheshimiwa sikumuona, kiukweli
nilipunguza
ufanisi wangu wa kazi kwa muda na sikujua kwa
nini nilikuwa ninamashaka juu yao ila nafikiri ni
uwezo na miujiza ya mungu tu kutaka kunionesha
uharifu waliokuwa wanaupanga, ilipofika majira
kama ya saa nne hivi nilimkuta mheshimiwa huyu
akitoka huku akizungumza na simu ambayo
ilionesha kuwa ni ya siri kutokana na umakini
aliouweka usoni mwake, hivyo alivyo maliza
kushusha zile ngazi na kuelekea kule walipokuwa
wenzie mimi nikawasha ile televisheni baada ya
kuhakikisha kuwa nipo mwenyewe, na
nilichokiona
na kukisikia niliogopa, ghafla nilishtuliwa na
mfanya kazi mwenzangu wa kiume aliyekuwa
nyuma yangu na nafikiri aliweza kuona lakini
hakuelewa, kutokana na uwoga niliitoa ile kanda
ya
kisasa “COMPACT DISC” ( CD) na kutoka nayo
haraka bila kujali kitakachotokea kwa bosi, toka
moyo wangu ulipokili kuwa yaliokuwa
yanazungumzwa ni mipango ya uharifu,
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA MWISHO
Baada ya kukaa ndani humo kwa muda mrefu
niliwakuta wanatoka kisha kuzunguka nyuma ya
hoteli na kuchukua meza moja na kuketi lakini
huyu mheshimiwa sikumuona, kiukweli
nilipunguza
ufanisi wangu wa kazi kwa muda na sikujua kwa
nini nilikuwa ninamashaka juu yao ila nafikiri ni
uwezo na miujiza ya mungu tu kutaka kunionesha
uharifu waliokuwa wanaupanga, ilipofika majira
kama ya saa nne hivi nilimkuta mheshimiwa huyu
akitoka huku akizungumza na simu ambayo
ilionesha kuwa ni ya siri kutokana na umakini
aliouweka usoni mwake, hivyo alivyo maliza
kushusha zile ngazi na kuelekea kule walipokuwa
wenzie mimi nikawasha ile televisheni baada ya
kuhakikisha kuwa nipo mwenyewe, na
nilichokiona
na kukisikia niliogopa, ghafla nilishtuliwa na
mfanya kazi mwenzangu wa kiume aliyekuwa
nyuma yangu na nafikiri aliweza kuona lakini
hakuelewa, kutokana na uwoga niliitoa ile kanda
ya
kisasa “COMPACT DISC” ( CD) na kutoka nayo
haraka bila kujali kitakachotokea kwa bosi, toka
moyo wangu ulipokili kuwa yaliokuwa
yanazungumzwa ni mipango ya uharifu,
haukupita muda hoteli ikawa imechafuka baada
ya
kutokea mauaji ya kijana mmoja ambaye
hakufahamika jina lake ila aliuwawa na mmoja
watu aliokuwa nao huyu mheshimiwa na hapo
ndipo nilipomuona marehemu alfedi kazinge
akiikumbatia kwa uchungu na kuililia maiti ile na
kilichoendelea hapo sikujua japo nilijengewa na
hofu huenda alfredi naye alikuwa anahusika ila
ilikuwa si kweli baada ya kwenda na kuisikiliza cd
ile kwa umakini na kugundua kuwa nae walipanga
kumuua kama atakaidi agizo lao la kushirikiana
nao katika kuweka mipango ya uvamizi wa gari la
pesa, niliamua kuacha kazi katika hoteli hiyo kwa
kutetea maisha yangu kutokana na taarifa nilizo
zipata kuwa mheshimiwa huyu amejua ukweli
kuwa
cd yenye ushahidi wa mambo waliokuwa
wanayapanga nilikuwa nayo mimi hivyo walikuwa
wananitafuta kwa udi na uvumba na kila kitu
mtajionea wenyewe katika cd hiyo ambayo
nimewapatia kama kielelezo cha kukamilisha
ushahidi, pia kinachoshangaza zaidi ni kwamba
nyumba na baadhi ya mali za marehemu alfred
kazinge zinamilikiwa na huyu mheshimiwa hali ya
kuwa familia ya marehemu imekuwa na kuishi
katika mazingila magumu sana. Hivyo
muheshimiwa hakimu naomba jambo hili lifatilie
kwa makini na adhabu kali itolewe kwa
mtuhumiwa, mpaka hapo sina cha ziada.
Pumzi nzito ilionekana kushuka kwa helman
baada
ya mama victoria kuonekana kuweka kila kitu
bayana, kutokana na aibu iliyokuwa inamtesa,
helman hakusita kuinamisha uso wake uliokosa
haya kipindi cha nyuma,
Mheshimiwa hakimu akaludi upande wa helman
na
kumuuliza,
“ mheshimiwa unachochote cha kujitetea au
kupinga ushahidi ambao umetolewa na mshahidi
upende wa mashtaka?”
“Sina mheshimiwa, ila kuna kitu naomba
kuzungumza kabla hukumu kali haijaja juu yangu
kisha maneno yangu yaje kuwa funzo kwa
wengine
wote ambao ni waumini wa tabia kama yangu” .
helman alizungumza kwa huruma huku mikono
yake ikionekana kutokauka machoni kama mtu
anayefuta machozi yaanzayo kutoka. Maneno
yake
yalimstua sana mwanae john na baadhi ya watu
wengine waliokuwa wamekuja kusikiliza kesi hiyo
ambayo ilionekana kupotea kwa muda na kuwa
tena na uzito kutokana na waandishi waliowahi
kuisikia na kuifatilia kipindi cha nyuma kuipata
tena na kutaka kuhakikisha haki inafanyika kwa
wakati huo.
“unaweza kuzungumza tu mheshimiwa helman”
hakimu aliruhusu na watu wakakaa mkao
wakusikiliza hicho ambacho mtenda dhambi na
mfitini mkubwa anachotaka kukizungumza,
Sauti nzito iliyotoka kwenye koo la helman kwa
ishara ya maandilizi ya kuongea ikaongeza
ukimya
kwa wasikilizaji na hapo maneno yake ya mwisho
yakaanza kumtoka,,,,,,
“ mheshimiwa hakimu, mwanangu john na
wengine
mnaosikiliza, mimi ni binaadamu kama nyinyi
lakini
tofauti yetu ni kwa yale niliyo yatenda, tamaa na
ukosefu wa utu moyoni ndio yalionipelekea kuwa
na kiroho ya kinyama,
leo na kili mbele ya mahakama hii tukufu na kwa
mwenyezi mungu na wote naomba mnisamehe,
mahakama hii tukufu ni haki yake kunifunga kwa
niliyoyatenda na mwenyezi mungu ni haki yake
kunichoma kwa dhambi zote zinazonihusu, labda
kwa huruma yake mungu anaweza kunihurumia
kwa kuwa ni mwingi wa kusamehe.
Niliyo mtendea marehemu alfed kazinge ambaye
nilimuua kwa sumu kali niliyomuekea kwenye
chakula chake kule gerezani kinguruila mkoani
morogoro, nikishirikiana na mkuu wa gereza hilo
ambaye nilimpatia rushwa ya kutosha ya
kuniruhusu kuingia ndani ya gereza na kufanya
yale niliyo yataka, pia nilimuua mfanya kazi wa
marehemu Alfred kazinge ambaye pia alikaidi
kushirikiana nami vilivyo. Hao ni baadhi tu ambao
nyie mnaweza kuwa fahamu ila wapo wengi
nilioweza kuwapoteza katika dunia hii pale tu
walipokaidi kutii amri yangu”
Helman alizidi kumimina yale yaliokuwa kifuani
mwake,
John mwanangu,( alimuuita kwa kumtazama)
najua umekuwa katika maisha ya kifahari na kila
raha ndani yake, lakini hukujua ni wapi mali hizo
nimezipata na hukujua baba yako nafanya kazi
gani ya kuniingizia kipato kikubwa kiasi cha
kukufanya wewe uwe na furaha na kujivunia kuwa
na baba kama mimi, leo inabidi utambue na
ujifunze na wala usijaribu kupita katika njia hii
ambayo mimi nimepita maana hutokuwa na
furaha
maisha yako yote”
Helman alipomaliza kumpa usia mwanae wa
pekee
akaendelea kusema,,
“mheshimiwa hakimu, baada ya kumfanyia vitimbi
na kumtengenezea kesi ya uporaji wa fedha,
marehemu Alfred kazinge mpaka kuhukumiwa
kufungwa kutokana na wizi huo, shirika la benki
aliyokuwa anafanyia kazi ikaamua kufanya mnada
wa kuuza mali zake ili kuweza kufidia kwa
uchache
deni hilo, lakini kutokana na roho ya kinyama
niliyokuwa nayo nikafanya mpango wa kuongea
na
meneja wa benk hiyo kisha mali zake zote
zikafanywa mnada kwangu kwa kiasi kidogo cha
fedha hivyo basi nakili kuwa mimi si mmiliki halali
wa mali hizo, naomba mahakama hii tukufu
iweshahidi na kuzirudisha mali hizo katika mikono
ya david na familia yake nami niko tayari kwa
hukumu itakayotolewa na Mahakam hii, kwa yote
niliyoyafanya” helman akawa amemaliza kutoa
uozo wake ambao ulipeleka hata ya kutokuwa na
haja ya kwenda kuitazama cd iliyotolewa na
mama
Victoria kama ushahidi,
Kila mtu alistaajabu kwa alichokizungumza
helman, hakuna aliye amini kutokana na roho
yake
mbaya ya kidharimu kama angeweza kukiri na
kusema yote aliyowahi kuyafanya,
John mchozi ukawa unamtoka kama mvua
ianzayo
kunyesha kwa kasi,baada ya nyundo kugongwa
mezani wote walikaa kimya na hakimu akaanza
kuzungumza,,,,
“kutokana na vifungu vya kesi ya mauaji na
udhurumaji wa mali, mahakama hii tukufu
inamhukumu ndugu helman kifungo cha maisha
yeye pamoja na mkuu wa gereza ambaye
walishirikiana katika kuandaa mpango wa
kumuua
Alfred kazinge, hivyo baada ya hapa askari
watakwenda mkoani morogoro na kumtia mbaroni
kisha kwenda jela moja kwa moja, na pia mali
zote
zitakabidhiwa kwa david kazinge ambaye ni mtoto
wa kwanza wa marehemu”
Hakimu aligonga nyundo mezani ya kuashiria
kuwa
kesi imekwisha, na askari walikwenda kumfunga
pingu tayari kumpeleka gerezani kwenda
kutumikia
kifungo,
Jino la furaha lilionekana kwa david ambaye
alikuwa anakumbatiana na afande criss pamoja
na
mama Victoria huku akitoa shukrani zake za dhati
kwa ushirikiano waliomuonesha,
Kilio nacho ndio kikawa rafiki wa john wakati
akimtazama baba yake akipelekwa nje kwaajili ya
safari ya gerezani,
Mawakili walipeana mikono kwa kumaliza kesi
hiyo
na waandishi wa habari wakijaribu kusogeza
kamera zao kutaka kumuhoji david maswali
mbalimbali juu ya kilichotokea, lakini ghafla umati
wote uliokuwa ndani ulishtushwa na sauti ya
risasi
pamoja na sauti ya maumivu iliyosikika,
Walipokimbilia nje kutazama kilichotokea,
walikuta
mwili wa helman ukimalizikia kukataa roho baada
ya kujipiga risasi ya kichwa mwenyewe kwa
bastola aliyo pola kwa mmoja wa askari
waliokuwa wanampeleka kumpandisha kwenye
gari
kuelekea gerezani, hilo liliendelea kuwa faida kwa
waandishi wa habari kuendelea kupiga picha, john
alizidi kuchanganyikiwa maana alimpoteza baba
yake pamoja na mali zote hakujua wapi aanzie,
David pamoja na mama Victoria waliaamua
kuondoka kwa kuwa tukio hilo lilikuwa aliwahusu
ni
kazi ya serikali, na kumuacha afande criss
akijumuika na askari wenzie kulikabili tatizo hilo
na
hatimaye mwili wa helman ulipelekwa hospitali
kwa maandilizi kisha kwenda kuhifadhiwa
mochwari kwa ajili ya mazishi baada ya
makabidhiano ya mali kukamilika.
************
Siku iliyofuata wanasheria wakiambatana na john
ambaye alikuwa na majonzi, walikwenda
kukabidhi
mali kwa david akiwa chini ya usimamizi wa
afande criss, na baada ya makabidhiano David
alipigiwa simu na mama Victoria ambaye
alidamkia
hospitali, kuwa wapo njiani wakirudi nyumbani
wamepata ruhusa toka kwa daktari,
David aliwapa maelezo huku akiwa na furaha
kuwa
waende moja kwa moja kwenye nyumba yao
tayari
wamesha kabidhiwa, na baada ya muda mchache
furaha ilizidi kuongezeka kwenye familia hiyo pale
alipo ziona sura za watu wake wa muhimu nisha
pamoja na kipenzi chake Victoria wakishuka
kwenye gari huku watoto wakiwa wameshikwa na
mama Victoria pamoja na dereva ambaye
aliwaleta
pale.
David aliwasogelea watoto na kuwa busu kama
ishara ya upendo kisha kumtazama nisha ambaye
alianza kutoa mchozi baada ya kumkumbuka
kaka
yake david, hisia zao za kindugu zilipozungumza
moyoni mwao walijikuta wakikumbatiana kwa
furaha huku mikono ya david ikifuta machozi ya
dada yake,
Kitendo hicho kilipokuwa kinaendelea john alikuwa
bado hajaondoka baada ya kuwa tayari amesha
kabidhi dokomenti zote za mali hivyo alioona
hana
chake alikwenda kwa mama Victoria ambaye
alimbeba motto wa kiume wa nisha na kusema,,,,
“ nipeni mwanangu nikaishi naye mwenyewe
nanyi
muendelee na maisha yenu”
john alizungumza hivyo huku akinyoosha mikono
tayari kwa kupokea mtoto, ghafla mambo yakawa
si mambo baada ya nisha kutoa kauli ambayo
iliwafanya kutoamini hata kama familia ya kina
john iliwatendea ubaya lakini alikuwa
amekamilisha
kauli isemayo siri ya mwana aijuaye mama,,,,
“we, we, ishia hapo hapo tena usijaribu hata
kukigusa hicho kiumbe na mikono yako haramu
uliyolisi kutoka kwa baba yako dharimu
aliyenifanya kuishi maisha ya tabu na shida,
tambua huyo mtoto hakuhusu hata kidogo, tena
john ukae mbali nami sioni hasara kukudhuru
name kupoteza maisha kwa hasira na uchungu
kila
nikikumbuka mlichotufanyia”
Nisha alizungumza kwa hasira na kujikuta
ananguvu japo ndio alikuwa anatoka hospitali,
maneno hayo david alikuwa bado hajaelewa vizuri
kuhusu huyo mtoto alipokuwa anataka kuhoji
alikatishwa na john aliposema,,
“nashrifa tambua hiyo ni damu yangu nina haki
ya
kuchukua kile nilichokipanda hivyo angalia kauli
zako isitoshe najua kabisa mimi na wewe
hatuwezi
kuendelea tena ndio maana namtaka mwanangu
nikaishi mbali nanyi”
“ sikia nikwambie we mwanaume, kwanza siitwi
nashrifa, uliniteka kiakili na kunipa jina hilo kwa
kuwa sikuwa na kumbukumbu zozote juu ya
familia
yangu na wala wewe hukujua chochote kuhusu
familia yangu, jua kuwa naitwa nisha alfredi
kazinge mtoto wa pili kwenye familia yetu, na
huyu
( alimuonesha david) ni kaka yangu kipenzi na
ninampenda sana, leo naomba utambue john, siku
uliyonikuta pale buguruni majira yale ya usiku
nilikuwa nimetoka kufukuzwa na mama mwenye
nyumba ambaye nilikuwa na mfanyia kazi zake za
ndani baada ya kugundua kuwa ni mjamzito na
aliyenipatia alikuwa ni mwanae na hata nilipotaja
kuwa ujauzito ni wa mwanae wote
walinishambulia
kwa matusi na kipigo kisha kunifukuza,
nilishindwa
kukwambia ukweli na kukudanganya kuwa
ujauzito
ni wa kwako kwakuwa nilikuwa sina pakwenda na
msaada wako nilikuwa nauhitaji kwa hilo
nakushukuru kwakuwa ulinisaidia kwa usiku ule,
nafikiri umeshajua ukweli unaweza kwenda
aliyotufanyia baba yako yanatosha usitake
kuanzisha balaa lingine”
Nisha aliweka kila kitu bayana na kila aliyeyasikia
maneno yale aliamini na hakukuwa na haja ya
kuhoji chochote kwakuwa mzazi mwenyewe
ameweza kuweka siri yote kwenye masikio ya
hadhira hata david akawa ameshajua maisha
aliyopitia dada yake kwa muunganiko wa matukio
aliyo yapata kutoka kwa rafiki wa nisha na
kuunganisha hayo ambayo mwenyewe
ameyasema
kwa muda huo,
Kiukweli john alichoka kwa kuvuta na kutoa
pumzi
kubwa, alijiona ni aliyekosa thamani mbele ya kila
mtu aliyekuwapo pale, uso wa aibu ulimshika kwa
yote aliyoyafanya marehemu baba yake helman,
haukupita muda askari wa wili walikuja na
kumkamata john huku wa kiwa na kijana mmoja
ambaye alikutwa na madawa ya kulevya akitaka
kuyasafirisha nje ya nchi, na alipoulizwa na
kupewa kibano ndipo alipomtaja john helman ndio
mmiliki wa mzigo huo hivyo john alikamatwa na
kupelekwa kituoni na kuwaacha familia
iliyopoteana kwa muda mrefu ikiingia kwenye
nyumba ambayo walizaliwa na kucheza humo
miaka mingi iliyopita, david alikumbuka mengi
sana
ambayo yaliokuwa yakifanyika ndami humo, sura
ya marehemu baba yake na mama yake zilimjia
huku zikitabasamu kwa furaha, alihisi ni ishara
kuwa sasa wanaweza pumzika kwa amani huko
walipokwenda na ndipo alipo mgeukia nisha
ambaye alikuwa ameketi kwe kochi kisha kwenda
kumnyanyua mtoto wa kiume aliyezaliwa na
nisha
na kumchukua mwanae wa kike aliyezaa na
kipenzi
chake Victoria na kuwaweka pamoja na
kusema,,,,,
“tunakushukuru mungu baba kwa kuweza
kurudisha furaha yetu kupitia mapacha hawa wa
nje ambao kila mmoja anaonekana kufanana na
mzee aliyefanana nae jinsia”
Baada ya sara hiyo fupi alianza kumyakuwa
mtoto
wa kiume wa nisha nakusogea naye mpaka
kwenye kizingiti cha mlango na kumyooshea juu
na
kusema,,,,
“nakushukuru mungu baba kwa kuweza kumpatia
dada yangu mtoto wa kiume ambaye leo hii
atakwenda kuwa mlisi wa jina la marehemu babu
yake, kuanzia leo mtoto huyu ataitwa “ALFRED”
Alipomaliza kumbatiza jina mtoto huyo alikwenda
kumkabidhi kwa mama yake nisha, kisha
kumchukua mwanae wa kike na kusogea naye
kwenye kizingiti cha mlango na kumyooshea juu
na
kusema,,,
“upole na huruma aliyokuwa nayo mama yetu,
zote
ziende kwa mtoto ambaye atalisi jina la bibi yake,
kuanzia sasa mtoto huyu ataitwa “MAGRETH”
Magreth mpya alipopewa jina lala bibi yake
alikabidhiwa kwa mama yake na wote walicheka
na
kufurahi kwa furaha.
*********
Baada ya miezi kadhaa kupita Victoria na nisha
walifunga ndoa na baadaye david alifikiria na
kuona raha ya mtoto alelewe na wazazi wote
wawili hivyo alijitahidi kadri ya uwezo wake
akamtafuta mwanaume aliyempatia ujauzito dada
yake na kumshawishi wawe pamoja na
kumwambia kuwa wememsamehe bila kinyongo
cha aina ya yoyote ile, Jackson ambaye ni baba
magreth wa sasa alikubali kuwa pamoja na nisha
na wao pia wakafunga ndoa na kusamehana yote
yalio pita,
Taarifa za ndoa ya nisha zilifanikiwa kumfikia
john
mtoto wa helman huko gerezani ambapo naye
alihukumiwa kwa kosa la uuzaji wa madawa ya
kulevya ndani na nje ya nchi, hivyo kutokana na
nguvu ya mapenzi na upendo aliokuwa nao kwa
nisha ukiachilia mbali udhalilishaji alioupata wa
kulea mimba ambayo si yak wake akaamua
kujimaliza kwa kisu walipokuwa wakifanya kazi
za
gereza na kumfuata marehemu baba yake helman
kuzimu aliko elekea.
Ama kweli mwisho wa ubaya ni ubaya, na jasho
la
mtu hali liliwi
Ridhiki anagawa mungu tafuta ya kwako nawe
utafanikiwa;
---- --------------MWISHO---------------
 
Hongera gamba nazidi kusisitiza wewe ni usein bolt wa hadithi humu jukwaani tunajua unatumia muda na rasilimali zako kuweza kututupia khabari hizi nasi kiungwana hatuna budi tukushukuru.
 
Hongera mkuu kwa hadithi hii nzuri na pia yenye mafunzo mazuri km uvumilivu,elimu,kumtumainia mungu kwa kila jambo....'09.🙂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom