Riwaya: Pumbazo

labda simu imepigwa pini na mama yeyoo. mzaramo kuja huku,watu dozi haijakamilika
 
Mkuuuu leta nyingineee aseee Sie wenginee MB zina takaa kuishaaa Mkuu letaaa mamboooo
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

Ile hali ya kila mmoja kujikojolea kwa wakati wake
ilimaanisha kuwa hakuna aliyekuwa amekizoea kifo.
Ni kweli kifo kipo lakini hofu huja pale unapokiona
kikija upande wako.
“Vua nguo upesi!” nilimwambia kwa kunong’ona yule
binti naye harakaharaka kwa ustadi akalirarua gauni
lake lililochakaa, wakati anamaliza na mimi nilikuwa
uchi wa mnyama nguo nikiwa nimezitupa kando.
Ama! Asikusimulie mtu ambaye hajawahi kukutwa na
balaa la namna hii, nisikilize mimi ambaye lilinikuta
moja kwa moja.
Hakuna aliyemwonea aibu mwenzake, sasa tulitulia
tukawa sawa kabisa na wale maiti. Mimi nilifumba
macho yangu na kusubiri hatma ya jaribio lile la
kujiokoa.
Sauti ile iliyokuwa inazungumza kwenye simu sasa
ilisikika ikitoa amri bila shaka kwa walinzi ndani ya lile
chimbo.
Amri ile iliendelea kunichanganya na vile nilisema awali
kuwa sikuwa vizuri katika kusikia kiingereza hasahasa
mtu akizungumza upesiupesi, lakini bado nilisikia neno
Tanzania na mara moja walitaja jiji la Dar es salaam.
Aliendelea kuzungumza, mara nikamsikia yule binti
akiniita.
Alizungumza akiwa ametulia vilevile na mimi nikiwa
nimetulia pia.
Alinieleza kwa kiingereza chenye lafudhi ya kiafrika
magharibi zaidi nami nilielewa, alisema kuwa maiti
wote wanatakiwa kuzikwa upesi sana!
Aliposema hivyo nikajikuta nafumbua macho!
Hofu!
Ndugu msikilizaji kwangu mimi niliona ni afadhali kufa
kwa mateso lakini sio kuzikwa nikiwa hai.
Nikiwa bado sijajua cha kufanya nikasikia hatua
zikisogea kule tulipokuwa kwa kasi ya ajabu.
Sasa sikuwa na silaha yoyote bali uchi wa mnyama,
nikamsihi yule dada aitetemeke hata akiguswa pia
asikakamae bali ajilegeze.
Ikawa hivyo wale watu walivyofika pale hawakukagua
hata kama kuna viumbe bado vinapumua badala yake
walitusomba na kutupakia katika kitu mfano wa toroli
kubwa.
Ulikuwa ni mchanganyiko wa maiti nyingi, waafrika
kwa wahindi, baada tu ya kurushwa mle ndani
nikageuka na kumsisitiza tena yule binti asikubali
kuzamishwa chini ya maiti wengine, hivyo kila
iliyorushwa maiti ikawa ni kazi kuinyanyua yenyewe
iende chini nasi tuendelee kubaki juu.
Dada alijituma haswa na machoni alionekana kuwa
hakika anaupigania uhai na uhuru wake.
Yule binti akanikumbusha kitabu cha nguli wa riwaya
za taharuki nchini Tanzania, Hussein Issa Tuwa katika
riwaya ya Mkimbizi alivyomuumba Tigga Mumba, kama
msichana mpambanaji anayeipigania haki na uhai kwa
jasho, machozi na damu. Huku akifanikiwa kuwashinda
watu waliokuwa na mtandao mpana kabisa wa
kinyang’anyi nchini Tanzania.
Na kufikia pale nikambatiza jina la Tigga Mumba
bandia japokuwa sikuwahi kumueleza maana ya jina
lile na chimbuko lake.
Toroli lile lilianza kuvutwa kuelekea mahali ambapo
tulitambua kuwa shughuli za uzikaji zinafanyika.
“Tigga, ukiona wanataka kukuzika piga kelele
tusikubali kuzikwa hai.” Nilimsihi naye akatikisa
kichwa kukubali. Hakujali kuhusu jina, bila shaka hata
ningemuita jina la kiume bado angeitika ‘rabeka’
Toroli lilienda kwa muda zaidi na kila mara lilikuwa
linasimama na maiti zinaongezwa.
Ilikuwa hali ya kutisha sana kuishi na maiti nyingi
angali ukiwa hai.
Kuna baadhi ya maiti zilikuwa zinatisha kuzitazama,
na sitasimulia zilivyokuwa kimuonekano.
Eeh! Mwenyezi Mungu wasamehe walioyatenda haya.
Hatimaye tolori lilisimama kwa muda mrefu kiasi kisha
ikasikika amri.
Amri ya kutuzika!!
Toroli likabinuliwa na mara tukajikuta hewani!
Tukimwagika kwenda chini kama tipa linalomwaga
mchanga.
Tulidumu kwa sekunde takribani thelathini kabla ya
kujikuta ndani ya maji, yalikuwa maji baridi japo si
sana.
Kumbe wanatutupa kama mizoga ndo namna yao ya
kuzika!!
Nilijisemea huku nikipambana nisizame na hapo
namsaka yule binti.
Uzuri ni kwamba nilikuwa vyema katika suala la
kuogelea.
Nilifanikiwa kumuona akiwa anatapatapa majini.
Alikuwa anazama na kuibuka, nikatambua kuwa
hakuwa akijua kuogelea, nikapiga mbizi na kumfikia.
Nikafanya jitihada za kumuokoa.
Tatizo lilikuwa moja, kila nikijaribu kumwokoa
ananishika kwa nguvu sana mimindo nazama.
Hiyo ni kawaida sana linapokuja suala la majini, yule
anayeokolewa humzamisha muokoaji.
Nilipambana sikukubali kumwachia azame angali
tumetoka mbali sana. Huyu angenifaa sana katika
kusimulia mengi yanayojiri katika chimbo la umauti.
Nikafanikiwa tukalifikia bomba lililokuwa linapita juu
ya yale maji, maji tusiyojua chanzo chake.
Nilimsihi ashikilie bomba, mimi nikapanda juu ya bomba
kisha nikamvuta naye akawa juu ya bomba.
“Kaka, sitakuwa na muda mrefu wa kuishi….
Nakutakia kila la heri katika safari yako, ukifika hai
duniani tafadhali waambie Nigeria kuwa mimi nimefia
kuzimu, nimekufa nikiteseka.” Alinieleza kwa
kiingereza kinachosikika vyema.
Nilimsihi sana awe jasiri, lakini badala ya kunijibu
akatabasamu. Sote tulikuwa uchi tukipigwa na baridi
kali lililovumishwa na upepo.
“Ningeweza kuwa jasiri lakini hadi kufikia hapa nina
hitilafu nyingi sana kaka yangu…” alianza kunisimulia
mkasa wake.
Akanieleza kuwa aliletwa Oman kufanya kazi za ndani,
akajituma na kuwafurahisha waajiri wake haswa
lakini shida ilianza baada ya bosi wake wa kiume na
watoto wake kwa pamoja kuanza kumuhangaisha
wakimtaka kimapenzi, hakuwa na pa kushtaki na
alitishiwa kuwa akijaribu kushtaki atauwawa vibaya
sana. Akaanza baba kuwa anamuingilia, baadaye
watoto zamu kwa zamu…. Alimudu kuitunza siri lakini
hofu yake ilikuwa siku ambayo mke wa bosi ambaye
alimtambua kwa cheo cha ‘Madam’ wake akigundua
itakuwaje.
Siku zikaenda hatimaye akaunasa ujauzito, hakujua ni
ujauzito wa nani, je? Ni wa baba mwenye nyumba ama
mtoto mmoja wao? Maana wote waliwahi kumuingilia
tena bila kutumia kinga. Alimweleza mwenye nyumba
kuwa ule ni ujauzito wake lakini aliambulia jibu
lililotisha sana, alielezwa kuwa akithubutu kusema
popote pale kuwa ule ujauzito ameupata ndani ya
nyumba ile basi yeye na huo ujauzito wake
watasambaratishwa…. Binti akajaribu sana kujikaza
lakini utaanza vipi kuificha mimba?
Haikuwezekana, hatimaye mama mwenye mji ‘Madam’
akagundua.
Hapo ndipo alipohenyeshwa akamwagiwa maji ya moto
na kujikuta akisema muhusika wa ile mimba.
Wahusika wakamruka maili mia.
Hapo ndipo alipoelezwa kuwa kamwe hatatoka katika
kasri ile akiwa na ushahidi ule wa kujazwa mimba na
bosi wake akishirikiana na watoto.
Akiwa hana hili wala lile, ghafla usiku alivamiwa
chumbani kwake akakamatwa na klufungwa kamba na
mwisho akatupiwa katika shimo hilo la umauti ambapo
aliendelea kubakwa hadi ile siku mimba yake ilipotoka
akiwa humohumo.
“Natamani sana kuendelea kukusimulia kaka yangu
mjasiri, lakini ni roho inataka ila mwili umekataa,
baridi ni kali sana linanitafuna na litaniua hili baridi…
tafadhali ukifika duniani salama nakusihi sana
usijipeleke ubalozini, nenda kiumakini sana na
usimwamini mtu maana wana watu wao ubalozini, ndo
maana kesi zinazopelekwa hapo ubalozini, huwa
hazizai matunda…..”
Baada ya kuniambia vile huku akiwa anatetemeka sana
meno yakigongana mdomoni binti alinisihi tena na tena
kuwa nipambane hadi mwisho maana ni mimi
niliyeikaribia dunia na nimeushikilia ukweli.
Nilimsogelea na kumsihi sana asikubali kufa kirahisi,
lakini haikuwezekana.
Tigga Mumba bandia, akanifia mikononi mwangu!
Niliumia sana na kujikuta nikitokwa machozi.
Baada ya muda nikalazimika kumuachia, akazama na
kupotelea katika maji yale ambayo wenzangu walikuwa
wamezikwa tayari ndani yake.
Yaani baada ya safari ndefu vile, amekufa!!! Iliumiza.
Sasa swali likabaki kwangu nitatoka vipi katika eneo
lile hadi nifanikiwe kuingia duniani kama alivyopaita
yule binti.
Na baridi lilianza kuuzidi mwili wangu uliokuwa uchi wa
mnyama....
______

NCHINI TANZANIA

GARI ya polisi ilikuwa imeegeshwa njea ya jengo
maalumu lililotumiwa na sajenti Pilipili kwa ajili ya
kuwahoji waharifu.
Gari hili halikukaa muda mrefu sana kabla kazi yake
haijaonekana.
Sajenti Pilipili akiwa na mahabusu watatu
waliounganishwa pingu walikuwa wakiongozwa
kuelekea katika hiyo gari.
Tayari walikuwa wamehojiwa kwa kiwango cha awali
ambacho sajenti alikuwa ameridhika nachona alikuwa
amepanga kuendelea kuwahoji baadaye. Hivyo
walitakiwa kurejeshwa katika vyumba vyao vya
mahabusu.
Baada ya sekunde kadhaa tu za kutoka pale ndani
Pilipili akajikuta akishuhudia jambo ambalo mara
nyingi hulishuhudia katika filamu za mapambano. Sasa
lilikuwa linatokea mbele yake.
Ilikuwa ni ndani ya sekunde kadhaa tu. Ni kama jambo
hili lilifanywa na watu watatu lakini kwa wakati
mmoja kabisa.
Utaalamu wa hali ya juu!
Haikusikika milio ya tendo hili lakini baada ya sekunde
kadhaa, miili ya Eric Mlewa na wenzake wawili
ilianguka chini kama mizigo, ikiwa imeendelea
kuungana vilevile na pingu!
Damu ikiwa inachuruzika vibaya mno, wote walikuwa
wamepigwa risasi katika mioyo yao.
Sajenti Pilipili alizama katika kuduwaa hakuamini kuwa
risasi zilizopigwa zilipita nukta chache kutoka pale
alipokuwa.
Na kama zilipita hii ilikuwa ni salamu tosha kabisa
kuwa hawakumkosa maksudi ila lile ni onyo kali sana
kwake.
Akaanza kuhaha huku na kule akiiacha ile miili mitatu
pale chini ikitiririka damu. Akatimua mbio kuelekea
ndani alipomuacha IGP.
IGP alijikuta tumbo linaanza kumkata.
Mashahidi muhimu walikuwa wameuwawa kwa maksudi
kabisa na kwa utaalamu wa hali ya juu mno.
Nani yupo nyuma ya mambo haya?
Hili lilikuwa swali gumu sana.
Geza Ulole alivyopigiwa simu hakupokea iliita mara ya
kwanza kimya.
Mara ya pili kimya.
Mara ya tatu haikuwa ikipatikana.
IGP akishirikiana na Sajenti Pilipili wakazama katika
pumbazo wasijue ni hatua gani wanapaswa kuchukua
kwa wakati ule.
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
IGP alijikuta tumbo linaanza kumkata.
Mashahidi muhimu walikuwa wameuwawa kwa maksudi
kabisa na kwa utaalamu wa hali ya juu mno.
Nani yupo nyuma ya mambo haya?
Hili lilikuwa swali gumu sana.
Geza Ulole alivyopigiwa simu hakupoke iliita mara ya
kwanza kimya.
Mara ya pili kimya.
Mara ya tatu haikuwa ikipatikana.
IGP akishirikiana na Sajenti Pilipili wakazama katika
pumbazo wasijue ni hatua gani wanapaswa kuchukua
kwa wakati ule.
Kuona vile IGP akampa ishara Sajenti Pilipili,
wakatokea mlango wa dharula huku wakiwasiliana na
timu kubwa ya jeshi la polisi kwa ajili ya kuimarisha
ulinzi eneo lile na ikiwezekana kuwatia mikononi
waliorusha risasi zile kiustadi zikaondoka na uhai wa
watu watatu muhimu kabisa.
_____
KATIKA chumba kimoja kipana sana chenye mwanga
hafifu kisichokuwa na samani nyingi, mwanaume
mmoja alikuwa ameketi katika kiti kilichokuwa na
thamani kubwa sana. Alikuwa ametulia tuli akiwa
anawaza na kuwazua hata asipate jawabu juu ya kipi
ambacho anaweza kufanya ili kujitoa katika shida
iliyokuwa inamkabili.
Hakuwa peke yake pale chumbani kulikuwa na watu
wengine wawili, hawa hakuweza kuwashirikisha
yaliyokuwa yanapita kwa kasi kichwani mwake.
Alibaki katika utulivu uleule kwa takribani nusu saa
kabla watu wale wawili hawajafika mbele yake na
kutaka awashirikishe alichokuwa anawaza.
Akawakata jicho kali kisha akainama tena!
Wakanung’unika na kuondoka tena!
Wakarejea walipokuwa wamekaa awali.
Akawarushia tusi kwa sauti ya chini kiasi lakini
likawafikia, wakazidi kunung’unika.
_____
SIMU kutoka uhamiaji juu ya balaa lililozuka la vijana
watatu kukamatwa ilipokelewa na kijakazi na kisha
kumfikishia mkuu wake wa kazi, punde baada ya
kuzungumza na kujua kilichotokea akanyanyua simu
yake na kupiga mahali alipoamini panafaa kupiga simu
kwa wakati ule.
Akazungumza maneno machache sana huku akilitaja
jina la Pilipili.
“Hakuwa peke yake alikuwa na jamaa mwingine ila
hakuna aliyeikamata sura yake na wengi wamekiri
aliyemuona anadai ilikuwa ni mara yake ya kwanza
kuiona sura ile…” alijieleza na kisha akakata simu.
Akashusha pumzi kwa nguvu sana, kabla simu yake
haijaita akaipokea na kuzungumza maneno machache
sana.
“hakikisha ndani ya masaa kumi na mbili
wamenyamazishwa kabisa…. Zingatia kunyamazisha
wanaohusika pekee.” Akakata simu.
KUKATWA kwa simu ile kukamaanisha kuwa kuna vita
ya kimyakimya imetangazwa, Pilipi akafuatiliwa
nyendo zake zote hadi ile siku waliyowachukua Eric na
wenzake kwa ajili ya mahojiano, timu iliyoagizwa
kuwanyamazisha wahusika ikajipanga vyema kabisa
kitaalamu na kusubiri wakati ufike.
Alianza kutoka Geza Ulole mle ndani, kisha baada ya
muda wakatoka waliotakikana, viwambo vya kuruhusu
risasi zitoke vikaruhusiwa na roho tatu zikatokomea!
Wakatoweka wakiwa wameimaliza kazi!
Kwa umakini waliokuwanao hawakuweza kumuacha
Geza awe ametoka kirahisi vile mle ndani, Geza
hakutembea muda mrefu kabla hajadhibitiwa.
Wakamchukua na kumwingiza katika jumba lao
maalumu, akaingizwa katika chumba kikubwa cha wazi.
Sasa yupo katika kiti chenye thamani kubwa. Mikono
yake ikiwa imefungwa na ndani ya chumba kile kuna
wanaume wawili wanaosononeka kwa sababu Geza
hatoi ushirikiano.
Kila walipokuwa wanavutana kando huyu alisema Geza
ana matatizo ya akili mara huyu akapinga, na mara
nyingine yule anayepinga akienda kuzungumza na
Geza naye anakiri kuwa Geza ni mwendawazimu.
Laiti kama Eric Mlewa angekuwa hai awasimulie
alivyobabatizwa na teke kali la Geza Ulole akabiringita
chini kama mzigo hata wasingejaribu kumjadili jinsi
walivyomjadili.
Kuna muda Geza alianza kulia kama mtoto mdogo,
kuna muda alikuwa anakoroma kama mzee, kuna
wakati alikuwa anachekacheka bila sababu na mara
nyingine alinuna.
Mara zote hizi aliambulia vibao vikali katika shavu
lake.
Alihimiri yote haya, shavu lake kamwe halikuwahi
kusahau vibao vikali kutoka kwa askari magereza
wakati alipokuwa gerezani, na hata hakuwahi kusahau
ile suluba aliyoipata mara kwa mara alipokwa
anahojiwa kwa makosa mbalimbali aliyowahi
kuyafanya.
Lakini sasa alikuwa Geza mpya kwa ndani lakini mwili
ulikuwa uleule.
Aliisikia mikono ya watu wale ilivyokuwa laini,
akawasikitikia sana.
Akaendelea kuvumilia huku akiwangoja wafanye kosa
moja tu na kisha ajitambulishe kwa majina yake kuwa
anaitwa Geza Ulole.
Ilikuwa yapata saa nane kwa mujibu wa saa iliyokuwa
pale ukutani, saa nane usiku.
Geza kichaa akaanza kulia njaa, alilia kiasi cha
kuwakera wale wanaume wawili waliokuwa na jukumu
la kuhakikisha usalama upo tele ndani ya chumba kile.
Kelele za Geza zikawafanya wafanye maamuzi ya
kumpatia chakula.
Nani amlishe kichaa?
Lilikuwa swali lisilokuwa na jibu la papo kwa hapo.
Kung’atwa!!
Kila mmoja akawaza kwa wakati wake huku
akimuhofia sana Geza kuwa anaweza kumng’ata.
Wakakubaliana kumfungua kisha watamlinda kwa
bunduki.
“Bunduki ya nini sasa Solo…. Huyu akizingua unapiga
vitasa akifa shauri zake wanatupa sisi kichaa
kumlinda..” mmoja alibeza maneno yakamwingia
mwenzake, wakamfungua GEza na kumpatia chakula.
Ilikuwa zaidi ya kichaa, mara achukue nyama mara
aache, mara ubwabwa anakula anajipaka usoni.
Akawa anaambulia matusi mazitomazito na wakati
mwingine vibao katika mngongo wake.
Hatimaye chakula kikamalizika alikuwa ameshiba kwa
kiasi chake, angeweza kula sana lakini kwanini ajaze
tumbo wakati kuna shughuli ilikuwa inamkabili mbele
yake.
Ukafika wakati wa kufungwa kamba, kwa maksudi
akauleta ule wazimu akajifanya anasumbua kufungwa
kamba. Wakaja wote wawili ili wasaidiane, akamuona
anavyoiacha silaha yake kizembe.
Alipofika na kumkamata Geza huku akimuinamia Geza
akarudi nyuma kisha akafyatuka kwa kutumia kichwa
akalenga kwa staili ileile ya wao walivyotumia kuwaua
wale watu watatu wenye siri.
Kichwa kikatua katika mwamba wa pua, yule bwana
akatua kama mzigo bila kupiga kelele yoyote, akawa
anarusha miguu huku na kule na damu ikiruka vibaya
mno.
Yule mwingine akashtushwa na tukio lile,lakini akilini
akiamini kuwa Geza ni kichaa na tukio lile akili yake
imemtuma.
Akapoteza sekunde mbili kumtazama mwenzake,
aliporejea akapokelewa na ngumi ya kijelejele katika
kifua chake, akatua chini kama gunia.
Geza akiwa anajua analolifanya akasimama akaendea
sahani yake ya chakula akachukua lile paja la kuku
aliloliacha akalitia mdomoni akalishughulia ipasavyo
wakati anamalizia akaanza kumuhoji yule bwana
aliyekuwa amejishika kifua akisota pale chini.
“Nakuona dogounaitamani bunduki, ila ipo mbali….
Nina spidi moja ya hatari sana mimi…. Nilipokuwa
shule ya msingi nilikuwa nashinda kila siku riadha, vipi
unataka tushindane?” Geza akamuhoji huku
akijilambalamba.
“Yaani kifua kipana hako kangumi hadi sasa hivi
unagalagala…. Kwani mnalipwa shilingi ngapi
kunenepa hivyo?” alauliza kwa sauti yake ileile
iliyojaa masihara, sasa alikuwa anajifuta mikono.
Yule bwana akadhani Geza hamaanishi anachokisema,
akakurupuka ghafla kuikimbilia bunduki, Geza akapiga
tambo tatu kubwa akamfikia jamaa akamchota miguu
yote miwili jama akatua chini kwa kutumia uso wake.
“Yametoka meno mangapi hapo maana nia yangu
yatoke mawili tu ya mbele ili ukitoka humu mademu
wakucheke…” Geza aliunguruma na wala
hakujishughulisha kuishika bunduki waliyokuwa
wanaikimbilia.
“Oya! Sasa tuache utani, ehee nyie ni akina nani na
kwanini mmenikamata….. nijibu fasta maana kuna
mahali nilikuwa naenda kuonana na watu najua
watalalamika sana sijaenda na simu yangu mmechukua
mkaizima.” Alizungumza kisha akamsogelea yule
bwana. Akainama chini na kumweleza bila masihara.
“Dogo ninajua kuua sana, kila kiungo changu
kinaua…. Mwenzako yule tayari nimeua na sina haja
ya kuhakikisha, sasa wewe sitaki kukuua kwa sababu
huna meno tayari, nieleze kwa ufupi sana nyie ni akina
nani na kwanini mlinikamata.”
Hofu ilikuwa jirani kabisa na yule bwana akaanza
kuongea kwa shida sana, akaelezea juu ya mradi wao
kwa kadri alivyoweza.
Mwishowe akamtaja aliyewapa kazi ya kuua na
kumkamata yeye.
Geza akapigwa na butwaa kusikia kuwa wale mashahidi
wameuwawa wakati yeye anakamatwa.
Hapo akazidi kumchimba hadi akaelezea juu ya
biashara zao za Oman na hapo akakiri kuwa aliwahi
kwenda Oman pia mara mbili.
“Ulienda kufanya nini, ya kwanza nay a pili. Sitauliza
maswali zaidi we jibu lolote ambalo unahisi
nitauliza…” Geza alichimba mkwara.
Yule bwana ambaye Geza hakutaka walau kujua jina
lake alielezea safari yake ya kwanza, nay a pili,
akaelezea na mengine mengi aliyoyajua, Geza
akachukua ya msingi hasahasa majina ya wahusika
wakubwa katika mpango huu wa aina yake uliosukwa
miaka kumi iliyopita.
Yale majina yalimtisha sana Geza.
“Swali la mwisho….. hiyo rost ya kuku mliyoniletea
nani ameifanyia makeke.. maana dah!” alisema Geza
huku akijisukutua na ulimi wake.
Yule bwana hakujibu kitu kabla Geza hajamtandika
ngumi kali ya mgongo.
“Mamaaaa Nakufaaa!!” akapiga mayowe.
Geza akamziba mdomo kisha akamwambia, “Doh!
Uliwahi kuwa mtabiri? Maana unakufa kweli sio
masihara”
Alipomaliza kauli ile akasimama imara kisha
akaunyanyua mguiu wake na kuutuliza katika shingo
ya yule bwana kwa nguvu zote.
Hakugeuka kumuangalia akatembea hapa na pale
akalifikia sahani lilokuwa limesheheni nyama za kuku.
Geza akazifakamia huku akisifia utaalamu wa
aliyezitengeneza.
“Ndo maana haya majinga yanakuwa na vimikono laini
laini….” Akageuka tena akazimwaga zile nyama huku
akijilazimisha kutapika huku akijutia kuzila nyama zile
na masimango ya hapa na pale.
Hakuweza kutapika.
Akili ya Geza aliijua ye mwenyewe.
Akatoka pale na kutaka kuondoka, akasikia kuna kitu
kama kishindo kinasikika kwa mbali, akawa makini
akasikiliza zaidi. Ghafla kikatoweka kile kishindo,
Geza akaiendea bunduki na kuitwaa, lakini haikudumu
katika mkono wake kwa muda mrefu. Ikapigwa teke
kali.
Ile Geza anakaa sawa akapokea mapigo matatu makali
mbavuni kwake akayumbayumba.
Akajaribu kumshambulia mpinzania wake lakinihali
ilikuwa tete akapokea tena mapigo matatu kutoka
katika mguu wa yule mtu aliyeibuka ghafla katikati ya
chumba kikubwa.
Geza akaacha kudharau sasa akayapanga mapigo yake
yale yaliyomfanya aitwe kaka mkubwa au steringi
gerezani.
Akamruhusu mpinzani wake amsogelee karibu huku
akiyavumilia mapigo yake makali, baada ya lengo
kutimia akafyatuka kwa kutumia kichwa chake
akakutana na mguu wa mpigaji.
Pasi na mashaka alimtegua.
Mpigaji akapiga mayowe huku akitua chini.
Geza mwenye hasira kali akamvamia pale chini yule
mpigaji aliyekuwa anasota pale chini akishindwa
kusimama imara baada ya mguu wake ulio peku
kukutana na ujanja wa Geza wa kutega kichwa.
Geza alimfululizia ngumi kama nne za nguvu.
Akataka kupiga pigo la mwisho la kuua, mara
akajikuta akitazamana na kifua kilichochomoza kuja
juu huku kilichochomoza kikiwa hakijapachikwa.
Yalikuwa ni matiti madogo!!
Mwanamke!! Akashtuka Geza na kujitoa katika mwili
wake.
Geza alishtuka kutokana na mambo mawili, kwanza
alikuwa amehenyeshwwa na mwanamke katika
mapambano ya ana kwa ana na pili alikuwa anataka
kutoa shambulizi kali kana kwamba anataka kuua
mwanaume.
“Wewe ni nani mwananmke. Na unahusika vipi katika
mradi huu…” alihoji Geza.
Yule mwanamke alijitutumua na kuzungumza.
“Niache niondoke zangu kaka nakusihi, mmenitesa
inatosha.. naomba mniache sitasema lolote….” Alijibu
kwa kusuasua.
“Naitwa Geza Ulole…. Si mkazi wa humu, wewe ni nani
humu.”
“Naitwa Zainabu… inspekta Zainabu” alijitambulisha.
“Mungu wangu!” Geza alijikuta akilitaja jina hili
tukufu kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu
sana kupita.
Akamsogelea yule binti akaitazama sura yake
hakuweza kubaini chochote kwa sababu alikuwa
ameichakaza tayari kwa ngumi kalikali.
“Unamfahamu Pilipili na Sungura naye unamfahamu….
Sungura ni nani?” alimuuliza kwa kumjaribu.
“IGP Sungura, Sajenti Pilipili..” alijibu kwa uhakika.
Hapo sasa Geza akatambua kuwa ameipata dhahabu
bila kutarajia.
Zainabu anayedhaniwa kufa sasa yu hai mikononi mwa
Geza.
 
ndugu shyjya,tukutane tena kesho Muda na wakati kama huu.Heheheh ;-) ;-)
 
daaah yaani kuna muda nasoma hadi mapigo ya moyo yanadunda spidi.hongera mkuu bonge la simulizi
 
kuna kila sababu ya kukushtaki kwa uongozi... Kwa nini hutupii nyingine?
 
Hahahahahahah hakika hii story ni kaleeee balaaaa Safiii mzaramooo yani mfano ukaishia hapo na ukatoaa kitabu chenye mwisho wake itabidi ninunue maana hakuna namnaa tenaaa eeehh
 
Hahahahahahah hakika hii story ni kaleeee balaaaa Safiii mzaramooo yani mfano ukaishia hapo na ukatoaa kitabu chenye mwisho wake itabidi ninunue maana hakuna namnaa tenaaa eeehh
ukinitumia hela ya bando utakuwa umenisaidia pia ahaaa ahaaa
 
Yaweza kuwa mzaramo anavuta pumzi ili amalize kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…