SEHEMU-31
Huyu ni gaidi wa mapenzi pia, serikali pia imtangaze kuwa ni mtu hatari kwa akina dada na mabinti zetu mashuleni" alijisemea moyoni akiwa tayari ameshaanza taratibu kutekwa na muonekano wa "Maso Maso" na kusahau kwa muda kazi aliyotumwa. "Maso Maso" alikuwa amevalia singlendi rangi nyeupe kata mikono na bukta nyepesi ya rangi ya kahawia, iliyoacha wazi sehemu kubwa ya miundi yake isiyo na vigimbi kama wale wanaume walima matuta ya viazi wa kule Mbeya.
Alipomuona mkewe tu katika uwanda wa macho yake akanyanyuka kwenye kiti na kwenda kumkumbatia na kumsalimia. "Salaamu aleikum mke wangu, laazizi wangu wa pekee aliyekabidhiwa funguo za moyo wangu na Maulana". Kachero Yasmine alijikunyata chini ya uvungu wa kwapa ya kushoto ya gaidi "Maso Maso" kama kinda la njiwa aliyefiwa na ***** akipata jotojoto la kwapa. Kwapa ambalo lilikuwa limenyolewa nywele zake lipo kipara na laini kama unyayo wa mtoto mchanga aliyezaliwa juzi. Harufu ya kijashojasho cha kwapa ya "Maso Maso" kilichochanganyika na harufu ya unyunyu wa bei juu sana toka nchi za Ughaibuni, ulikuwa unazalisha harufu mpya ya kuvutia ambayo hajawahi kuivuta maishani mwake tokea azaliwe.
Ilikuwa ni harufu ya marashi si marashi, miski si miski ilikuwa ni baina wa baina. "Atakuwa jini mahaba huyu sio bure, najikuta nampenda kwa kila sekunde inayokatika" alijisemea Kachero Yasmine. Huku bila kujijua akajikuta tayari kwa utundu wake ameshapenyeza viganja vyake laini kama sufu chini ya singlendi ya gaidi "Maso Maso", na kuanza kupapasa nywele za malaika ya kifuani kwa "Maso Maso"' zilizokuwa zinaonyesha zimestawi barabara. "Maso Maso" alielewa anapotaka kufikishwa na Kachero Yasmine, hakutaka kuharibu mambo mesini. Himahima "Maso Maso" akamchomoa mkono kiupole kisha akakibusu kiganja cha mkewe na kumvutia mezani kwenye mlundi wa anuwai mbalimbali za maakuli na mashrabu za kila aina.
Alipokaa chini Kachero Yasmine, na "Maso Maso" nae akaenda kukaa kiti mkabala na mkewe huku anamkazia macho, kitendo ambacho Kachero Yasmine alikuwa anaona aibu na soni iliyopitiliza mipaka. Pale pale mezani "Maso Maso" akabinya kengele iliyopo chini kidogo ya meza ile. Ilipolia tu kengele baada ya dakika moja wakajitokeza watumishi wapya machoni mwa Kachero Yasmine wapo wawili. Kila mmoja akabeba sahani yake na kuwafuata waajiri wao kuwauliza maakuli wanayotaka. "Mtukufu Seyyidat mke halali wa kiongozi wetu utapenda kula nini na kunywa mashrabu gani usiku huu"? aliulizwa Kachero Yasmine kwa sauti nyororo ya kubembelezwa na yule mtumishi. "Nipatie sharubati na kipande kimoja cha keki" alijibu kwa kujitutumua Kachero Yasmine, huku moyoni akilaani na kuujutia mchezo alioamua kuucheza.
Wote wakaandaliwa chakula kisha wale watumishi wakawaacha peke yao ndani ya mesi ile yenye kila kitu cha kifahari kuanzia vikombe, sahani, visu, vijiko na masufuria ya kisasa ya kuhifadhia chakula. Kila mmoja akawa ametingwa na harakati za kushibisha tumbo lake. Alikuwa ni "Maso Maso" aliyewahi kumaliza, kisha akamsubiria mkewe amalize, akaenda kumnyanyua kutoka kitini na kumpeleka hadi kwenye sinki la kunawia maji na kumnawisha kisha akamfuta na kitambaa safi.
"Maso Maso" akarudi mezani akachukua sahani maalumu iliyotengwa na kukatwa nyama steki iliyochomwa kwa ustadi na kupakwa vumbi vumbi jeupe juu yake. Akafungua chupa ya tomato sosi akanyunyizia na kuanza kutafuna vipande kama viwili kwa kutumia uma, kisha akaweka ile chupa ndogo ya tomato ndani ya sahani akashika sahani mkono wa kulia huku mkono wake wa kushoto ameuviringa kwenye kiuno cha Yasmine. Akawa anaukandamiza shadidi kwa kukitomasa kiuno cha Yasmine huku kichwa cha Yasmine na nywele zake nyingi za shombe shombe la Kipemba zimeegemea kwenye bega la "Maso Maso".
Tayari "Maso Maso" alikuwa ameshampa shakawa kubwa ya joto la mapenzi Yasmine ambaye dalili zilionyesha kabisa hajiwezi tena, ameshamfanyia ugaidi wa mapenzi hapindui tena. Lakini karata muhimu ya kukamatwa kwa "Maso Maso" kwa namna ramani ilivyochorwa na Bosi wake Kachero Manu alikuwa ameishikilia Kachero Yasmine. Vinginevyo watatwanga maji kwenye kinu. Wakawa wameshafika chumbani kwao, "Maso Maso" akafungua mlango kisha wakaingia wote chumbani na kufunga mlango kwa funguo.














Yasmine alivyoingizwa chumbani alikuwa nusu chizi wa mapenzi tayari. Hasa ukichukulia alikuwa hajawahi kuchapwa na fimbo ya Musa tokea azaliwe. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza maishani kujifungia na mwanaume shababi, ghulamu mwenye viwango vyake kama "Maso Maso"
Akashajiika kujaribu walau leo tu siku moja aikonge na kuisuuza roho yake, kisha baada ya hapo akili ikishamkaa sawa atatekeleza majukumu yake. "Kazi na dawa, ananiona nani bwana kama nimefaidi penzi la gaidi wa mapenzi" alijisemea moyoni mwake Yasmine wakati "Maso Maso" amemuachia kiuno na kwenda moja kwa moja pembezoni mwa kitanda na kuvua singlendi yake nyeupe. Yasmine akaingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo kinachoelekea bafuni. Alitaka achague vazi ambalo litampendezesha zaidi, azidi kuikoroga akili ya "Maso Maso" ili wote wawe nusu vichaa wale tunda la uzima kwa shemere bila kuwaza.
"Maso Maso" alivyobaki peke yake akaenda kwenye redio yake ya kisasa na kuweka santuri ya muziki laini iliyokusanya nyimbo za mahaba anazozipenda. Kisha akaiendea sahani yake ya vipande vya nyama iliyonyunyiziwa unga unga wa miti shamba toka nchini Congo, maarufu kama "vumbi la Congo". Unga ambao una uwezo wa kumfanya kidume adumu kwenye tendo la ndoa kwa saa nyingi bila kuchoka. Yasmine anatokeza tu chumbani anasikia mziki mororo uliochujwa kwenye vyombo vya kisasa. Wimbo uliokuwa hewani ulikuwa ni 'My heart will go on' ulioimbwa na mwanamuziki mkongwe 'Celine Dion'. Kwa namna ulivyokuwa unaimbwa utasema umetoka hivi karibuni kumbe ni wa tokea mwaka 1997.
"Maso Maso" alikuwa sasa amejilaza kitandani anamuangalia mkewe anavyokuja huku kifua chake kipo wazi, vile viriba viriba vya umbo la mstatili ambavyo vijana wanavitafuta kwa kukesha kwenye majumba ya mazoezi "six packs" vilikuwa vimejichora tumboni mwake vinaonekana dhahiri shahiri hata mtu mzima mwenye uoni hafifu unaotokana na uzee. Yasmine alivyoviona vile viriba vya tumbo la "Maso Maso" ndio vilimzidisha hanjamu yake ya kufanya mapenzi.
Yasmine alikuwa amevaa kitopu cha rangi ya nyekundu ambacho kiliyaacha mabega yake meupe ya Kipemba yakiwa wazi, ndani ya kitopu kile chepesi hakukuwa na sidiria kwani "Maso Maso" aliweza kuziona chuchu za Yasmine zikiwa zimesimama dede kama zinataka kukitoboa kile kitopu na kukifanya kijivute kwa mbele katika harakati za kuzuia mtoboko. Chini Yasmine alikuwa amejifunga mtandio mwepesi wa rangi ya maziwa ambao ulikuwa umepambwa na maua ya rangi ya zambarau. Umbo lake namba nane ya ukweli lilikuwa sasa limejichora ipasavyo kwa vivazi vile alivyovaa. Yasmine alikuwa mzuri haswa, sio vivazi hivyo ndio vilivyompaisha aonekane mlimbwende bali ni uzuri halisi aliojaliwa na Subhana. Kama kuna orodha ya wanawake 10 bora Afrika waliopata kujaaliwa uzuri huo wa shani na Rabuka, basi Yasmine alikuwemo ndani ya 3 bora.
Mziki wa taratibu uliokuwa ukipigwa ulizidisha hisia za kufanya tendo la ndoa baina yao. Yasmine katika kumchanganya akili "Maso Maso" akawa anakatika mauno taratibu kwa ufundi mkubwa kufuatisha midundo ya muziki huo.
Uzalendo ukamshinda "Maso Maso" akagutuka kitandani na kuanza kumfuata mke wake pale anapocheza. Mwanzoni mkakati wake ilikuwa hakutaka kucheza mechi yake ya kwanza katika usiku wa fungate kwa papara alijua wazi kuwa anapaswa kumfanyia haki mtoto mbichi kama Yasmine ampagawishe kisawasawa katika uwanja ule wa fundi seremala wa futi 6*8.
Yasmine sasa alikuwa anakatika aste aste huku amempa mgongo mumewe huku akitingisha makalio yake ambayo hakunyimwa alipewa ya kutosha kiasi chake. Alipomfikia mkewe kwa macho yake yenye ithibati ya 'TBS' kwa kujua kuchagua watoto wazuri akaanza kuufanyia inspeksheni vizuri ule mtandio mwepesi aliojifunga chini pasi na kuushika. Uchunguzi wake ukazaa matunda kwa kujua ulipoanzia kufungwa ule mtandio. Haukuwa umefungwa imara ndindandinda la hasha. Ulikuwa umeegeshwa tu, na kushindiliwa pindo lake ndani ya chupi ya rangi nyeupe.
Yasmine alifanya hivyo makusudi ili asipate tabu mumewe kuuvua. "Maso Maso" akafanikiwa kuingiza kidole kwenye pindo ya mtandio na taratibu kwa ncha ya vidole vyake akafanikiwa kulifumua fundo hilo. Mtandio huo ukaanguka chini mwaaaaa sasa mambo yakawa hadharani bila mficho. Makalio au vijana wa Mjini wanaita 'Chura' wawili wa mviringo walikuwa wamebebwa ndani ya chupi nyepesi. Akaanza kupapasa makalio kama anavyopasa mpiga kinanda mahiri kwenye kazi yake. Yasmine akageuza uso wake kumtazama mumewe kwa jicho la mahaba huku anatabasamu kuonyesha kufurahishwa na mpapaso huo wa kitaalamu wa makalio yake. Macho yake makubwa yalikuwa yamelegea kama mtu aliyekunywa vidonge vya usingizi halafu anailazimisha kesha kwa kuyalazimisha macho kufunguka.
"Najiona ni mwanaume mwenye bahati ya kipekee katika sayari hii ya dunia kuwa na mke mrembo kama wewe Yasmine" alijikuta "Maso Maso" anaropoka maneno hayo ya mahaba baada ya kushajiishwa vilivyo na mapenzi sheshe yale bulibuli toka kwa mkewe Yasmine. "Ahsante my love nakupenda sana" alijibu Yasmine kwa sauti ya kivivuvivu huku nafsini mwake kukiwa na majuto, kwanini alikubali kazi ngumu inayompa majaribu, anayoshindwa kuvumilia.
Walikuwa wakiendelea kucheza muziki ule kwa mtindo wa kugandana "zero distance" na kwa mahaba makubwa. Laiti ungewaona wanavyocheza kiustadi mkubwa usingekubali kuwa huyu "Maso Maso" ni mfiadini. Kumbe wachamungu wakiwa hadharani tu mbele ya macho ya watu lakini wakiwa sirini wanayajua wao na Mungu wao wanayoyafanya. Yasmine sasa alikuwa amebakiwa na chupi tupu iliyositiri kipochi manyoya chake na chura wake. Huku macho yakiwa yamemtoka "Maso Maso" hayabanduki kuangalia mapaja meupe ya binti wa Kipemba kwa uchu wa fisi.