Riwaya: Msako wa mwehu

Riwaya: Msako wa mwehu

SEHEMU-36

Kachero Manu alikuwa amezimia kwa zaidi ya masaa 12. Alizinduka majira ya saa 7 adhuhuri akijikuta amefungwa pingu mikononi na miguu kwenye kingo za kitanda kidogo cha chuma chenye godoro la unene wa ulimi wa ng'ombe. Alijikuta hana nguo hata moja mwilini zaidi ya chupi yake tu huku nguo zake na buti zake zimetupwa pembeni ya kitanda.
Aliposhtuka kichwa kilikuwa kinamgonga vibaya sana. Alikuwa ametundikiwa dripu za kuongeza maji mwilini. Pia alikuwa ameunganishwa mwilini na mtambo unaosaidia kusoma mapigo yake ya moyo kitaalamu inaitwa "Heart Monitor" (EKG).
Alipofumbua macho vizuri akawa anajaribu kuvuta kumbukumbu amefikaje humo kwenye chumba kikubwa ambacho kina hadhi ya kuwa ni moja ya chumba cha hospitali kubwa. "Nini kimenimpata mpaka nimefika hapa?" alikuwa anajiuliza huku anatafakari. Maumivu ya kichwa yalizidi kumzonga kadri alivyokuwa anajilazimisha kuwaza. Akiwa katika hali hiyo ghafla mlango wa chumba hicho ukafunguliwa na ufunguo akaingia mtu amevaa koti jeupe, mara baada ya kuingia akaurejesha mlango huo.
Aliingia daktari mwanaume mwenye umri wa makamo, ambaye alikuja moja kwa moja mpaka kwenye zile mashine alizofungwa mwilini Kachero Manu. Kachero Manu akajifanya kufumba macho ili aonekane bado amezimia. Baada ya daktari yule kusoma vitu alivyokuwa anavyohitaji kutoka kwenye hiyo mashine akamgeukia Kachero Manu na kumuongelesha.
"Pole sana ulipoteza fahamu kwa zaidi ya si chini ya saa 12 nashukuru Mwenyezi Mungu nimepambana kuokoa uhai wako nimefanikiwa. Vipimo vinanionyesha umeshazinduka na unajitambua sasa" aliongea yule daktari huku anatabasamu akionyesha ameshtukia ujanja wa Kachero Manu.
Kisha yule daktari akachomoa dripu lile la maji ambalo lilikuwa ndio linaishia. Ikabidi hana jinsi ila afumbue macho yake. "Bwana daktari nimefikaje hapa na kilinipata nini? " aliuliza Kachero Manu kwa yule daktari wakati amempa mgongo anaandika vitu vyake kwenye karatasi zilizobanwa kwenye faili.
"Watakuja sasa hivi kukueleza wahusika wako mie sifahamu chochote juu yako zaidi ya kukutibu tu" alijibu yule daktari huku anakusanya kila kilicho chake na kuondoka zake, akafunga kile chumba kwa funguo na kuondoka zake. Alipozidi kuvuta fikra zake Kachero Manu taratibu akaanza kukumbuka matukio ya nyuma huku yanakatika hayana muendelezo. Njaa nayo ikaanza kumkung'uta barabara, mpaka akaanza kutetemeka, maana mara ya mwisho alishindia kahawa na kashata za machicha ya nazi kule kijiweni.
Haukupita muda mrefu mlango ukafunguliwa tena akaingia kipande cha mtu mwenye mwili ulioshiba mazoezi, amevaa maski usoni amebeba mkono wa kulia ana kikombe kikubwa kwa kutumia mshikio na mkono mwingine kabeba silaha. Alipofika akaweka kwenye meza ndogo kile kikombe. Na kuchomoa funguo mfukoni mwake na kuanza kufungua pingu za mkono mmoja wa kushoto. Kisha bila kuzungumza chochote akamkabidhi kikombe Kachero Manu anywe.
Kwa njaa aliyokuwa nayo alikuwa anakunywa ule mtori wa moto kama vile ni wa baridi baada ya dakika 3 kikombe kikawa hakina hata tone la mtori. "Nakuja muda sio mrefu tuongee kwa kina" alisema yule mlinzi na kuondoka zake kwa haraka. Lakini sauti yake yule adui ilimchanganya sana Kachero Manu. Hisia zake zilituma kuwa ni ya mtu kama anayemfahamu.
"Huyu ni nani? hii sauti ni ya mtu ninayemfahamu kwa kina, sio ngeni kabisa masikioni mwangu" alikuwa anawaza peke yake. "Halafu mbona hii pingu ya mkono wa kushoto aliyonifungua mbona hajaifunga tena vizuri kaiegesha tu!. Huyu ana kitu na mimi sio bure, ukisikia nyota jaa kukuangazia mchana wa jua la mtikati ndio huku sasa" aliwaza Kachero Manu. Sasa baada ya tumbo kupata chochote kitu, akili yake sasa ikatulizana na kutungamana, usicheze na njaa haina cha Rais wala raia wote wanahisi njaa.
Akaanza kuwaza namna alivyofikishwa hapo. Kumbukumbu zikamrudisha kisengerenyuma mpaka kijiwe namna alivyocheza mchezo wa bao na kisha kunywa kahawa, mpaka kuletwa na Juma Mavideo kwenye nyumba ambayo alipigwa na kitu kizito kisogoni na kupoteza fahamu. Akajilaumu kwa kutochukua tahadhari ya kutosha lakini alijipongeza kutokana na kufanikiwa kufahamu kuwa kuna siri muhimu inayotaka kufichwa kwa huyu Mwarabu.
"Kuna nini kinafichwa hapa mpaka nashambuliwa nusura kifo" aliendelea kuwaza na kuwazua Kachero Manu bila kupata majibu. Akamkumbuka dereva bodaboda Juma Mavideo, "sijui yupo salama na amesharejea nyumbani kwake?" Kwa mara ya pili tena yule mlinzi akarudi tena akionekana ana haraka sana na kama ni mtu ana wasiwasi mwingi.
"Komandoo Aboubakr anakuja mlinzi mwingine kushika zamu yangu, na usiku wamepanga wakuchukue kukupeleka kwa Bosi mkuu wa mapango ya Amboni kabla hawajakuchinja na bado hawajakutambua kama ni wewe kama wakijua umeshawahi kuishi kambini adhabu yake ya usaliti ni mbaya sana, umeshanitambua mimi nani? " alijieleza kwa haraka yule mlinzi. Kachero Manu akazidi kupigwa na butwaa. "Ina maana wamenifahamu mpaka jina langu feki..!" alikuwa anawaza kisha akajilazimisha kutabasamu, tayari alishamhisi nani anayeongea nae. "Wewe ni Akhy Abu-fadhli eeh au nakosea" aliuliza Kachero Manu kwa yule mlinzi huku akijionyesha anajiamini. Huyo Abu fadhli walikuwa wanaishi chumba kimoja kule kambini kijijini Dibungo, mara Kachero Manu alivyowasili Tanga. Kwa bahati waliochaguliwa kuja kumdhibiti Kachero Manu naye alikuwepo.
Alivyomuona tu akamgundua huyu ni Komandoo Aboubakr tena rafiki yake yupo matatizoni, huruma ikamuingia ya kumsaidia kwa mshahara wa potelea pote liwalo na liwe. "Hujakosea tumeletwa mahususi kwa ajili yako, mimi nataka nirudi atakuja mwingine kukaa na wewe mpaka saa nne usiku, kisha ataondoka watakuja sasa wengine wa kambi kuu kukupeleka Amboni, huko sasa ndio huwezi kutoka hai, jitahidi uchomoke" alijieleza yule mlinzi.
Kachero Manu alikuwa anatafakari namna ya kuchomoka. "Nimeshakufungua pingu ya mkono wa kushoto kisha nimeegesha tu makusudi, narudi kambini kwetu Dibungo nategemea utachomoka tu, pambana kwa jino na ukucha halafu tuone namna ya kuiendesha hizi kambi kwa kufuata sheria za Allah. Hawa hawapo kwa ajili ya dini wapo kwa maslahi binafsi mfano huyu Mzee uliyemfuata humu ni fuska ajabu muda mfupi niliokaa humu anafanya mambo ya ajabu tu nayashuhudia" alizungumza Abu-fadhli kwa hasira huku anapigapiga ngumi ukutani. Hakutaka kuonekana anamsaidia moja kwa moja kwa kuhofia huenda kuna watu wanaowachunguza nyendo zao mle chumbani. Kisha Abu-fadhli akaondoka zake kwa haraka sana. "Ukombozi wa kweli hauletwi kwenye sahani bali huletwa kwa mtutu wa bunduki" alijisemea Kachero Manu. Haikupita hata nusu saa mlango ukafunguliwa tena akaingia mlinzi mwingine mfupi amejazia misuli vya kutosha, kifua ngao akiwa amebeba jiko dogo la umeme na spoku za baiskeli.
Nae alikuwa amevaa barakoa usoni na singlendi nyeusi akiwa amevaa suruali ya buluu ya dangilizi iliyokatwa chini kidogo ya magoti. Chini akiwa amevalia buti kubwa za rangi ya kaki. "Wewe mbwa wa motoni, msaliti wa Jihadi, nani vibaraka waliokutuma kuhujumu Mujahidina?" alifokewa Kachero Manu kwa sauti ya kwaruza roho, huku anashindiliwa mabuti ya tumboni pale pale kitandani alipolala.
"Aaah.....Aaaah..... Nakuf .....aaaah unani....o..ne..aa bu....u... re" Alikuwa analalamika Kachero Manu huku akisubiria wakati muafaka wa kumshambulia. Akaamua amtie hasira kwa kumpa maneno mabovu. "Wewe kisonoko mtambaa na ukoko karatasi ya kuchambia chooni ya Wasomali wa Al-shabaab huwezi kuniambia kitu".
Yule jamaa akajibu kwa vitendo matusi ya Kachero, akachomeka waya wa jiko la umeme kwenye soketi ukutani, kisha akawasha swichi ili likolee moto. Kachero Manu alikuwa anamvizia ajilete kwa ukaribu amkabe kwa kutumia pingu yake ya mkono wa kushoto. Yule mjuba alikuwa kama vile ana machale anakuwa haingii kwenye mtego wa Kachero Manu. Jiko lilivyokolea moto kisawasawa akachukua spoku akawa anaipasha moto kwa kuishikilia huku mkononi amejivesha glovusi ngumu zisizopitisha moto kwa urahisi. Ile spoku ilipopata moto vizuri akaishika kwa glovusi na kumchoma nayo kachero Manu kwenye nyuma za nyuma ya ugoko wa mguu wa kulia.
"Aaaaaaaah Aaaaaah kenge wewe unaniumizaaa, kamsosi maji baridi weweee" alikuwa analalamika kwa maumivu Kachero Manu huku yule mlinzi anacheka tu kwa twezo kwani alijiandaa kumfanyia unyama wa kutisha. "Matusi hayakusaidii kitu subiri sasa spoku za moto za kwenye tundu la kupitishia mkojo ndio utakaponiheshimu".
Kachero Manu akapata wazo jipya la kufanikisha kumkaba kwa urahisi. Akakusanya makohozi kinywaji na kumtemea bonge la kohozi usoni yule adui, na kuanza kumcheka ili amtie hasira. Yule adui kuona hivyo akakasirika na kufura akawa anachemka kwa hasira. Akachukua spoku nyingine ya moto na kutaka kuja kumchoma nayo shavuni.
Hilo likawa ni kosa la majuto kwake. Wakati spoku ya moto imebakiza sentimeta chache kutua kwenye shavu la kushoto la Kachero Manu, akadakwa kiganja chake yule adui na mkono wa kushoto wa Kachero Manu kisha kwa kasi ya haraka akakigeuza kiganja chake na kusababisha spoku imuingie kwenye jicho lake mwenyewe. "Uwiiiiiiiih......Uwiiiiiih....!, jicho langu weeeeeh...!" alipiga makelele huku anagugumia kwa maumivu makali yule mjuba wa "Al-shabaab". Ama kweli mwosha huoshwa na mtenda akitendewa huona kaonewa alisahau kabisa kuwa dakika chache zilizopita alikuwa anampa mateso mwenzake, sasa kibao kimemgeukia.
Kachero Manu bila kupoteza wakati akaitumia ile fursa vizuri kwa kumvuta karibu kisha akampiga mbata moja matata sana ya kwenye paji la uso, iliyomchana vibaya na kumsababisha aangukie pale kwenye godoro huku akiwa anakoroma kwa kupoteza fahamu. Almanusra aende jongomeo kaburini ilikuwa bahati yake sana, usicheze na kupigwa kichwa na komandoo ambaye mazoezi yake kila siku akiwa nyumbani akitaka kupika wali nazi au mandondo, nazi huwa anaivunja kwa kutumia kichwa chake.
Himahima akamsachi mifukoni na kufanikiwa kupata funguo za pingu alizofungwa. Akatumia chini ya dakika 2 kuhakikisha yupo huru akavaa nguo zake haraka haraka, sasa muda ulikuwa unaonyesha ni saa 10 alasiri. Alipomaliza kuvaa akarudi tena kumsachi vizuri akamkuta ana bastola za kisasa mbili na mabomu mawili madogo ambayo ukiyalipua yanaweza kuteketeza mtaa mzima. Akabeba vile vitu na kutoka nje ya chumba kile alicholazwa. Akaanza msako wa chumba hadi chumba akiwa ndani ya nyumba ile ili kupata chochote kitu kitakachomsaidia.
 
SEHEMU-37

Mkuu wa Magaidi mikononi mwa Kachero Manu️
Mambo yalikuwa tumbitumbi kwa Kachero Manu lakini muda hautoshi ikabidi ajitahidi ayakamilishe kwa wakati. Akaingia chumba cha kwanza kinachotazamana na kile alichokuwa anateswa. Akakuta chumba kina kitanda kikubwa kilichotandikwa nadhifu huku kukiwa na kabati lenye droo zake mbili pamoja na kioo. Hakukuwa na kitu chochote kingine.
Akavunja droo ya upande wa kushoto kwa kutumia bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Ikabidi aanze kucheka kwa alichokiona ndani ya droo hiyo. Alikuta paketi za kutosha za vidonge vya kuongeza nguvu za kiume maarufu kwa jina la "Viagra", na pia kulikuwa na paketi za kutosha za mipira ya kiume maarufu kwa jina la "kondomu". Akapiga risasi droo la upande wa kulia nalo likajibu na kujimanua likawa lipo wazi. Alichokiona humo alifurahi na roho yake sana tu.
Alikuta pesa taslimu za kigeni zikiwa zimepangwa bandali bandali. Lakini kilichomfurahisha zaidi ni kuipata ramani ya kutoka walipo pale kumfikisha mapango ya Amboni walipo viongozi wakuu wa "Al-shabaab". Baada ya kujiridhisha kuwa ndio yenyewe akaisunda kwenye mfuko wa suruali yake na kutoka nje kwa tahadhari kubwa. Hakutaka yale makosa ya kutekwa kirahisi yasijirudie tena.
Mpaka sasa alikuwa bado hatambui sehemu alipo. Akasogea kwenye chumba kingine akakuta mlango umefungwa lakini taa imewashwa. Akajaribu kukifungua kitasa taratibu, mlango ukaitika kwa kufunguka. Aliyoyashuhudia ni ya kustaajabisha. Hakutegemea Babu kikongwe kama huyo ayafanye. Alimkuta Mzee Abdallah mmiliki wa "Chops Carwash & Garage" mtuhumiwa wa mauaji ya Wabunge watano na madereva wao alikuwa anakula bata, habari hana kabisa.
Jamaa huyu aliwekwa juu ya meza uchi wa mnyama, halafu kumeletwa asali iliyowekwa kwenye kisahani, halafu zile korodani zake zinawekwa kwenye kisahani huku zinapakazwa asali, kisha msichana mbichi kabisa ananyonya korodani zake kimahaba zilizolowekwa kwenye asali.
Zinaponyonywa zile kokwa hiki kibabu kinapiga kelele za kupagawa, anazungumza maneno ya ahlan wa sahalan yasiyo na mtiririko wowote wenye kuleta maana. "Yaaaaah habibiiiii.... Zubeida mimi nataka kukununulia wewe ndege, nitakujengea ghorofa katikati ya Bahri Hindi Mashaallaah...Shallalaaaaah" Babu alikuwa hajiwezi kwa raha anayopata ya kunyonywa korodani zake.
Ndio alikuwa amekaribishwa Tanga, kashakuwa limbukeni wa mapenzi baada ya kuvitoroka vyombo vya dola vinavyomsaka kwa kesi ya ugaidi. Anavyopiga kelele hizo za maneno ya mporoto, yule binti ndio anazidisha manjonjo ya kumpagawisha Babu. Kiruka njia huyo alikuwa shombe shombe, kwani licha ya ngozi yake kuonyesha kuchanganya damu, bali nywele zake zilikuwa ni za kiarabu kwani alikuwa ameiteremsha ile shungi aliyojitanda kichwani.
Kachero Manu hakutaka waendelee na starehe zao na wamgeuze yeye kuwa kozibati. "Mpo chini ya ulinzi mafuska wakubwa nyie hata aibu hamuoni" alitoa ilani halafu akabutua risasi moja kupiga kwenye dirisha. Yule Babu alishtuka mpaka akaanguka chini ya meza, miguu juu kichwa chini. Huku yule kahaba amejifunika uso wake kwa kuona aibu ya yale waliyokuwa wakiyafanya.
Yule Babu alivyoamka akachomoka nduki utasema "Alphonce Simbu'' yule mkimbiaji mahiri wa Tanzania yupo kwenye mbio za Marathoni, anakimbilia kwenye mlango mdogo uliomo mle chumbani. Kachero Manu akaikohoza kidogo tu bastola yake, akaanguka chini Babu wa watu huku damu zinamvuja gotini. Akawa anajisuwira kwa maumivu makali anayoyapata huku analalamika.
Kachero Manu akawa anamsogelea huyu Babu ambaye ni mmoja wa kiungo muhimu wa Al-shabaab na ndio aliyemfadhili "Maso Maso" kwenda masomoni Uingereza kwenda kupikwa kwenye ugaidi.
"Nitakupeleka kwenye vyombo vya dola hata ikibidi nitembee kwa miguu kutoka Tanga mpaka Dar es Salaam ukiwa mgongoni mwangu nikufikishe ukajibu tuhuma zako za ugaidi mshenzi wewe" alikuwa anafoka Kachero Manu kumwambia maneno makavu Babu Abdullah mmiliki wa "Chops Carwash & Garage" aliyekuwa bado anagaragara pale chini.
Alipozidi kumsogelea, Mzee Abdullah akaanza kucheka kicheko cha kebehi "Ha... ha... ha.. ha.. ha... ha..!" kwa sauti ya juu kisha akamwaga matusi ya kutosha kwa Kachero Manu.
Kachero Manu akashtukia kitu kisicho cha kawaida kwa Mzee Abdullah akaanza kumwendea kwa kasi akamrukia na kuwahi kumkaba shingoni, lakini alikuwa ameshachelewa tayari amezidiwa ujanja.
Mzee Abdullah alikuwa na jino bandia ambalo ni kidonge cha sumu kitaalamu kinaitwa "Lethal Pill". Ambapo kidonge hiko kinavishwa raba kwa nje kumlinda mtumiaji kama akikimeza kwa bahati mbaya. Ndani ya hilo jino bandia kuna kemikali 'Potassium Cyanide' inayohifadhiwa kwenye glasi.
Hivyo anapotaka kujiua mhusika anavunja hiyo glasi hiyo sumu kwa meno yake moja kwa moja ikiingia mwilini inaenda kusimamisha mapigo ya moyo na kuharibu ubongo. Mzee Abdullah alikuwa amechagua njia ya marhaba yeye mwenyewe hakutaka kupata mateso ya Wanausalama. Alijua watamgombania kama mpira wa kona na kumletea usumbufu wa mateso mengi atakayoshindwa kuyabeba.
"Shenzi sana kasalimie jongomeo huko utaenda kujibu katika Mahakama ya Mwenyezi Mungu, hakuna ulichokikwepa...!" alisema Kachero Manu kwa hasira za mkizi mbele ya marehemu ambazo hazisaidii kitu. "Umekuja humu kwa kupitia wapi? " aliuliza Kachero Manu kumuuliza yule kahaba, sasa kasheshe la kumkosa Mzee Abdullah lilihamia kwake yule kahaba. Yule kahaba hakumjibu kitu kwa aibu na idhilali iliyomkuta huku akiwa amejiziba uso kwa mtandio wake, akajizoazoa pale chini alipokuwa amejibweteka na kutaka kuongoza njia kuonyesha njia aliyoingilia kule kwenye nyumba ya chini ya ardhi. Kachero Manu hakutaka kumuamini moja kwa moja yule mwanamke wa mahonyo, haraka haraka akamfanyia inspeksheni ya kutosha kuhakikisha hana chochote mwilini mwake.
Alipojiridhisha ni joka la kibisa hana madhara yoyote akamruhusu aongoze njia ya kutokea akafuata mlango ule ule aliotaka atokee marehemu Mzee Abdullah. Walipoufungua mlango wakakuta kuna ngazi zinapandisha juu wakazifuata mpaka wakaja kutokeza chumba kimojawapo katika ile nyumba ya udongo aliyotekwa kachero Manu.
"Haya ongoza njia ya kurudi ulipotokea potea hapa mara moja, kabla sijabadilisha mawazo na kukuchukulia hatua kwa kushirikiana na magaidi " yule kiruka njia hakusubiri tena amri nyingine akawa anatimka kuelekea mashambani ambapo hata hakujui anapoelekea akawa anachochora tu njia mbele kwa mbele atajua huko huko, cha muhimu kwake ilikuwa kusalimika na mkono mrefu wa dola. Kachero Manu haraka haraka akarudi ndani ya jengo lile akafanya haraka kutega mabomu kwenye ile nyumba huku akitega mabomu yale yasizidi muda wa nusu saa yalipuke.
Yalikuwa ni mabomu ambayo unaweka mwenyewe mtumiaji muda unaotaka yalipuke. Alipomaliza kutega tu akawa anasikia muungurumo wa gari kwa mbali akajua moja kwa moja ndio wanakuja walinzi wengine kuja kuchukua doria kama alivyopewa taarifa na rafiki yake Abu-fadhli. Akakimbilia juu kutoka kule mafichoni hima hima akaenda kujificha kichakani akisubiri matokeo chanya ya mitego yake.
Baada ya kutimia nusu saa huku jicho lake likiwa kwenye saa yake ya mkononi halibanduki, mabomu yalianza kulipuka kwa kishindo cha kutikisa eneo zima. Kukatimka vumbi zito kama lote eneo lile kukawa kama kuna kimbunga cha mchanga. Muda ulikuwa unasoma saa kumi na mbili kasoro ya jioni, akafanya ukaguzi wa eneo hilo sasa kukawa hamna jengo lolote lililosalia, kila kitu kuliteketea.
Akatumia gari walilokuja nalo maadui zake ambalo liliegeshwa mbali na eneo la jengo kurejea nalo Jijini Tanga kujiandaa na usiku wa mwisho wa hekaheka unaokuja mbele yake. Mipango iikuwa mpaka kufika alfajiri shughuli iwe imeshakamilika. Alitaka magaidi walie kilio cha kusaga na meno kwa pigo takatifu atakalowashushia, ambalo hawatasahau kamwe maishani mwao.
 
Dope
 
Pamoja mkuu.
 
SEHEMU-38

SURA YA KUMI NA TANO
"Supu limetiwa nazi", Magaidi hatarini

Ukumbi namba -05 uliopo ndani ya moja ya mapango Amboni yasiyotumika ulikuwa umetengenezwa na kunakishiwa kwa viwango vya kimataifa. Amboni kulikuwa na mapango si chini ya 11 kwa idadi lakini ni pango moja tu ndio kinalotumiwa na serikali kwa shughuli za kiutalii. Mapango mengine ndio ambayo magaidi waliyachagua baadhi yao na kujikita humo wakijimwayamwaya kama nchi yao vile wakifanya wanavyotaka.
Hapo ndio ilikuwa kama Ikulu yao mipango yao yote inapangwa humo mapangoni. Ukumbi huo Ulipewa jina la 'VIP HALL' ambao walikuwa wanaingia viongozi 25 tu wakubwa wa "Al-shabaab" na wateule wanaowataka wao. Ulikuwa unatumika kwa matukio ya mikutano yao ya siri na wakati mwingine kwa matukio ya starehe. Ulikuwa kuta zake zinalinda sauti isitoke nje kirahisi huku ukiwa umefungwa viyoyozi vya kutosha.
Usiku wa Ijumaa hiyo tulivu kwao walikuwa wamemwalika msanii maarufu wa muziki anayetamba Afrika Mashariki na Kati kutoka Zanzibar maarufu kwa jina la "Bob Chollo". Ambaye alivyopewa mualiko wa kutumbuiza muziki mubashara alipewa ofa ya kuja na maghashi wa Mjini wasiopungua 25 wanaotikisa kwenye mitandao ya kijamii hapa nchini na wale watoto wakali wa kishua wanaotaka maisha ya ganda la ndizi. Wote malipo yao yalikuwa yanafanywa kwa Dola za Kimarekani. Kupata nafasi ya kuja huku kuhudhuria hafla za mapangoni rushwa ya ngono ilikuwa inatumika kwa wale mawakala wanaopewa kazi ya kuwatafuta hawa wasanii. Kama ni msanii wa kiume wapo waliokuwa wanaliwa kiboga na wale wa kike ndio usiseme tena, ilikuwa mtindo wa nipe nikupe. Watu mitaani walikuwa wanashangaa wasanii hao wanaishi maisha ya anasa yasiyoendana na kipato chao.
Wanaendesha magari ya kifahari na kuishi katika makasri ya kifahari lakini walisahau uzuri wote wa mti wa mkakasi ndani ni kipande cha mti tu. Onyesho moja tu kama hilo la masaa yasiyozidi matatu Bob Chollo alilipwa $40,000 taslimu bila mkopo, wakati hawa visura wenye majina yao pamoja na mpiga muziki wao "DJ" kila mmoja alilipwa $15,000 za mkono kwa mkono bila hangaisha bwege.
Lakini yalikuwa ni maonyesho ya aibu yasiyoendana na utu na utamaduni wa Mtanzania. Walikuwa wanaingia ndani ya ukumbi huo wakiwa wamevaa nusu uchi, huku wengine wakifanyiwa vitendo vya ufirauni na hao viongozi wa "Al-shabaab" ambavyo wanavumilia ili wapate chauchau yao ya kutambishia Mjini.
Wengi wao walikuwa wanatakatisha pesa zao hizo za kifirauni kwa kufungua biashara ya maduka ya kuuza nguo, viatu toka China, wengine mpaka biashara za Hoteli na Baa. Hawa viongozi wa "Al-shabaab" walikuwa sana hawapo kwenye harakati za kweli za kidini, bali dini ilitumika kama ngao ya kufichia maovu yao. Wengi walikuwa wanamiliki mali za dhulma na ufisadi wanazozipata kwenye maeneo wanayotawala huko Somalia kwa kukusanya kodi na zaka. Waliokuwa wanaoumia ni watu hohehahe wale mburumatali, mazumbukuku ulimwengu huko huku wanaotangulizwa mbele kama chambo, wakidanganywa wapo vitani kusimamisha utawala wa Kiislamu kwa mgongo wa imani zao kali.
Ndio maana matendo yao yalikuwa hayaendani kabisa na mafundisho ya uislamu. Muziki ulikuwa unaporomoshwa kwa shangwe kama zote kwenye jengo hilo lililokuwa taa zake zenye mwangaza hafifu zenye rangi tofauti zenye kumurikamurika. Ukumbi ulichangamka kwa amsha amsha ya hapa na pale, huku kila mtu akiwa na furaha usoni mwake.
Ilikuwa ni ngumu ukiwa kwenye ukumbi huo kumtambua mtu labda uwe nae kwa ukaribu zaidi. "Maso Maso" nae alikuwepo ndani ya ukumbi akiondosha msongo wa mawazo wa kushinda ndani ya mapango kwa muda mrefu, huku akiwa anavuta bonge la sigara "Siga". Kama ungemuona "Maso Maso" jinsi anavyolisakata rumba na watoto wa kishua kwa kuwabadilisha kama vile shuka, usingedhania kuwa ni namba moja hatari sana kwa ustawi wa uhai wa binadamu.
Akawa anaonekana ni kama mtu aliyepagawishwa na miondoko na swaga za uchezaji wa maghashi hao. Kutokana na kutokuwa kwake kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mrefu kutokana na kutotumia simu janja za mkononi kwa sababu za kiusalama, hivyo alikuwa zumbukuku wa starehe nyingi zinazoendelea Tanzania na duniani kwa ujumla. Wakiwa katika kilele cha starehe hizo ghafla bin vuu majira ya saa 3 usiku ikapigwa kengele ya dharura ndani ya ule ukumbi, muziki ukabidi uzimwe haraka sana.
Wale wasanii ikabidi wapitishwe mlango wa dharura na kuondolewa eneo lile mara moja kama walivyokuja walikuwa wanaingizwa kwenye magari yenye vioo vyeusi ambayo hayaonyeshi nje yanayowapeleka mpaka Tanga Mjini kutoka Amboni. Wahusika wa "Al-shabaab" kila mmoja akaingia chaka lake kujificha. Tayari disko ameingia Mmasai, supu imetiwa nazi tena imeshakuwa sio supu tena. kila kitu kilienda hobelahobela bila mpangilio, hamna tena starehe.
Taa za ukumbi zikazimwa kwa muda kukawa giza totoro kama vile hakukuwa na shamra shamra na shangwe muda mchache uliopita. Taarifa ya kutisha iliwasili mafichoni pale Amboni, kuwa wapo hatarini, adui yao anakaribia kuwateketeza kwa shambulio.

"Akhy Abu fadhli AF-Code"
"Ova Ova...!, "Nakupata vizuri kabisa AF-Code ova ova! ", Nimechomoka salama namshukuru Allah. Sasa nakuagiza nenda kwenye mtambo mkuu wa wa kulipulia mabomu ukifika nakutajia muamala wa namba za mficho ova ova!. Haina shida kiongozi nitakujuza nikifanikisha ova ova!, kazi njema ova ova!, nawe pia ova ova!". Hayo yalikuwa ni mawasiliano baina ya marafiki wawili wakitumia msimbu wa siri katika mazungumzo yao kwa kutumia redio za upepo.
Wote wenye nia na kazi moja tu kuisambaratisha "Al-shabaab" kwa malengo tofauti. Mmoja akitaka waunde kikundi kipya kitakachopigania Uislamu bila kuwashirikisha majambazi wa "Al-shabaab" na mwengine akiwa yupo upande wa serikali anakomesha uhalifu. Haikupita hata nusu saa kambi ya magaidi ya Dibungo ikawa inalipuka mabomu mtindo mmoja, ndani ya muda mfupi ikawa kambi hiyo imegeuka Somalia ndogo kwa milipuko ya mabomu.
Haya ndio yale mabomu yalitegwa na Kachero Manu enzi anaishi kambi ya magaidi ya Dibungo, akijulikana kama Komandoo Aboubakr alipokuwa mmoja wa viongozi wa kambi hiyo. Milipuko hiyo ndio iliyosababisha magaidi wakutane kikao cha siri usiku usiku huo na kuvunja starehe zote. Kachero Manu akapewa taarifa ya mafanikio juu ya tukio hilo akafurahi kupita maelezo. Akawa sasa anagombana na usukani wa gari yake barabarani anayafuata mapango ya Amboni yalipo. Akiwa katika mchepuo mkubwa wa gari lake akasikia mtetemo kwenye soli ya kiatu chake. Mtetemo aliokuwa anausubiria kuliko hata namna mama tasa anavyosubiria taarifa ya kuambiwa ni mjamzito na daktari baada ya kuitafuta mimba muda mrefu.
Mtetemeko huo wa soli ya kiatu kwake ni zaidi ya taarifa ya mgonjwa kansa aliyekuwa watu wanasubiria wa leo au kesho kupelekwa jongomeo, aambiwe sasa amepona kabisa mzima wa afya. Chapuchapu akapaki gari pembezoni mwa barabara na kuchomoa kibati chenye ukubwa simu ya kiganjani kilichokuwa kimehifadhiwa baina ya soli ya kiatu chake.
Ndani ya kibati akakitoa kifaa chenye uwezo wa kunasa mawimbi hivyo kumtambua mtu alipo au mzigo ulipo kutokana na 'microchip' iliyomo ndani yake. Hiko kifaa kinatumia teknolojia inaitwa "radio-frequency identification technology" (RFID). Alipobonyeza namba za siri anazozijua yeye akaanza kupata dira na uelekeo ambao Kachero Yasmine alikuwepo muda huo.
kifaa cha "RFID" kwa Kachero Yasmine kilifungwa kwenye chupi yake maalumu aliyotakiwa aivae anapokuwa faragha na "Maso Maso" hivyo kumpa uelekeo wapi alipo "Maso Maso" iwe rahisi kumkamata. Pia mwilini mwake Kachero Yasmine alipandikizwa 'microchip' inayotambua nyendo zake sehemu alipo kufahamu popote alipo usalama wake binafsi.
Hizo teknolojia ndizo zilimpa kiburi Kachero Yasmine kujitumbukiza kwenye mdomo wa mamba wa magaidi akiwa kifua mbele kwa kukubali kuolewa na "Maso Maso". "Hello Mr.Hamduni, Kachero Manu naongea hapa", "ahaa habari za masiku tele" alijibu Mr Hamduni.
"Tunapambana Mola anatuongoza, naomba uwape Bosi wetu mkuu wa Idara ya Usalama Bwana Omega Mtanika uelekeo wa Amboni eneo ambalo tupo kama unavyosoma mawimbi ya kiteknolojia ya Kachero Yasmine. Ningeomba pia kama ingewezekana afuatane na Waziri wa Mambo ya Ndani bila kusahau wawakilishi wa vyombo vya habari vya televisheni wawepo. Tungependa tukio hili lirushwe mubashara kwa kushuhudiwa na wananchi wote Tanzania nzima na nchi za jirani" alitoa maelekezo Kachero Manu kwa njia ya simu kumpa msiri wao Kachero mwenzao aliyopo TCRA kama "Under Cover".
Baada ya makubaliano hayo akapiga tena simu ya upepo sasa kwa rafiki yake 'Abu-fadhli'. "Umefika wapi akhy....Abu-fadhli mie ndio naelekea Amboni sasa kwenye usiku wa kufa au kupona Ova ova! " aliuliza Kachero Manu.
"Nisubirie pale kwenye eneo la ofisi za serikali ya kijiji cha Majimoto kisha tuondoke wote kwa pamoja, nimeshawapa taarifa za milipuko ya huku Dibungo hivyo nimeitwa kuhudhuria kikao cha dharura ambacho nina namba za siri za utambulisho wa kuingia humo mkutanoni Ova ova" alijibu Abu-fadhli, akimuelezea swahiba wake kuwa amealikwa mkutanoni.
Kachero Manu akakanyaga kibati cha mafuta sasa anaelekea ofisi za kijiji kumsubiria rafiki yake Abu-fadhli anayetokea kijiji cha Dibungo wakalianzishe mapangoni kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom