Naona jasmine anapona tena kugongwa na kimasomasoAliwe tu

Kachero many mle kwanza huyo demuSEHEMU-40
Saa 4:30 usiku Kachero Manu akiwa na sanjali wake Abu fadhli waliwasili mapangoni tayari kwa kazi. "Mie nitashuka na kuingia mkutanoni wewe usishuke kwanza hauna nguo walizovaa walinzi leo. Ila nitakuletea mboga sasa hivi itakayokusaidia kuingia ndani ya mkutano, usifunge dirisha nampa mboga ufunguo wa gari umpe mfueni wa nguvu" alisema Abu fadhli huku akikumbatiana na Kachero Manu wakaagana tayari kwa usiku wa kazi.
Abu fadhli alikuwa anatembea akiwa amevaa kombati za kijani huku juu amevaa kofia ya kijeshi mpaka alipomfikia mlinzi wa kwanza. "Hello nenda kanifungue kioo cha gari yangu nimesahau nitaukuta ufunguo kwako ninawahi kikao" alitoa amri Abu fadhli kwa yule mlinzi huku moyoni akimuonea huruma kitakachomkuta huko aendako. Yule mlinzi kwa kutaka kujipendekeza alikuwa anaenda mbio mbio bila tahadhari yoyote, kufika akaingiza funguo kwenye tundu la mlango, akautikisa kidogo ule funguo, mlango ukajibetua ukafunguka.
Akaingia ndani ya gari ile anataka kuwasha ili apandishe kioo, Kachero Manu akamgusa bega akageuka na kutumbua macho kama ameona mzimu wa Mababu. Kachero Manu hakutaka kumpa nafasi akamlamba kareti moja takatifu ya shingoni jamaa pale pale akakauka kwa kifo cha ghafla. Akamvua kombati zake za rangi ya kaki, chapuchapu akazivaa yeye na kujivika pama, ungemuona utasema ndio pacha wa yule mlinzi.
Akamvutia chini ya uvungu wa gari akachukua ile silaha ya yule mjuba akaikagua akaikuta imejaa risasi. Akatega bomu ndani ya gari lile na kuliacha kama lilivyo. Akaanza kutembea kuelekea uelekeo ule ule aliokuja nao yule mlinzi. Alipokaribia akaona kuna mlinzi mwingine amekaa kama meta 200 kutoka alipo yeye macho yake kodo upande anaotokea Kachero Manu.
"Sssss...Ssssss...Ssssss... ! " Kachero Manu alipiga mluzi kumuita yule mlinzi aliye jirani na yeye. Yule mlinzi akawa anakuja haraka haraka akijua kuna jambo limetokea alipokaribia tu Kachero Manu akajifanya kama kuna kitu kwenye kichaka kilichopo jirani na alipo. Yule mlinzi akajifanya kimbelembele kutangulia mbele ili ajinyakulie sifa za ushujaa. Kachero Manu hakumkawiza kumtanguliza njia ya marhaba, akamtandika risasi mbili za mgongoni kwa kutumia bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Sasa alipochunguza akakuta wamebaki walinzi kama wanne tu aweze kuingia ndani ya jabali kubwa lililopo umbali kidogo kutoka alipo.
Akachomoa redio yake ya upepo toka kiunoni alipoipachika akaanza kuigiza anaongea na mtu huku anawapita mutawalia. "Hello ova ova..!!eeh...nakuja ndani haraka, huku nje hali ipo shwari kabisa, dakika moja nipo hapo kiongozi ova ova...!!" wale walivyomuona mwenzao anaongea na simu hawakumtilia mashaka kabisa wakamuacha tu apite huku wengine wakionekana wana uchovu wa usingizi.
Alipowavuka tu akalivuka jabali lilitobolewa katikati. Akapenya jabali lile akatembea kwenye mwangaza hafifu kama dakika 10 akaona mbele yake maandishi 'VIP HALL-05', akajua ndio humu humu hawa manyang'au walipojichimbia. Alipofika akauchapa mlango teke ikafunguka akajirusha ndani kwa mtindo sarakasi na kuanza kushambulia kwa ghafla.
Shambulizi ambalo halikutegemewa na yoyote kuja tahamaki watu kama 10 tayari wameshalala chali wanalamba mchanga. Abu Fadhli nae akaanza kuwafyekelea mbali kwa mtutu wake, mpaka ukumbi unabakia na viongozi kama 6 tu huku damu zikiwa zimetapakaa. Mmoja wa wale maadui ambaye alijifanya amekufa akaanza kutambaa na ukuta mpaka akajiweka nafasi nzuri akafanikiwa kumlipua risasi za kifuani Abu fadhli na kumrusha hewani alipotua chini tayari marehemu wa juzi. Mziki ukabakia kwa Kachero Manu anatunguana nao kwa kuviziana.
Katika wale 6 waliobakia, 3 wakafariki dunia huku 2 wengine wakifanikiwa kutoroka ndani ya kile chumba kwa kutumia njia za panya. Kachero Manu akakimbilia kwa rafiki yake Abu fadhli akamkuta wabaridi kabisa tayari ameshafariki. Akambusu kwenye paji lake la uso, na kuiacha maiti yake mle mle ndani huku anafuata maelekezo kile kimashine chake cha "RFID" kumfuata alipo Kachero Yasmine na "Maso Maso".
Alipotoka ukumbini aliwakuta wale walinzi bado wapo pale nje hawajui kinachoendelea ndani kutokana na ukumbi kuwa hautoi sauti nje. "Hello nendeni kwenye lile gari mkatoe mzigo haraka sana unahitajika kwenye ukumbi wa mkutano nimeagizwa hivyo".
Maskini ya Mungu bila kujua wanayafuata mauti walivyokaribia kufika huku Kachero Manu alikuwa anafanya makadirio yake wakashtukia gari limelipuka na wao tena buriani maisha ya dunia imewakumba. Mlipuko ule ulikuwa mkubwa ukazusha kishindo kikubwa eneo lile, haraka haraka akawa anaelekea sasa chumbani kwa Yasmine kwenda kumtia mbaroni "Maso Maso".
"Maso Maso anayeyuka kimaajabu"
Kachero Yasmine alikuwa amepitiwa kidogo na usingizi hadi alipokurupushwa usingizi na mumewe bandia "Maso Maso". "Yasmine Yasmine tumevamiwa amka fasta" alizungumza "Maso Maso" kwa sauti ya juu. Yasmine nae akazinduka usingizini, akafikicha macho alijiona kama yupo ndotoni.
Ndipo akagutuka kuwa ni ukweli sio ndoto. Akavua haraka haraka nguo yake ya kulalia akavaa suruali dangirizi nyeusi iliyombana vilivyo na brauzi nyeupe juu. Kisha akauliza kwa sauti ya masikitiko "kwanini unavamiwa umewafanya kosa gani mume wangu?". "Sasa sogea hapa nikufundishe namna ya kutumia silaha kujilinda, nitakuambia siku nyingine kwanini wananiwinda" aliongea "Maso Maso" huku anamkabidhi bastola mkewe aliyoichomoa kwenye suruali yake pana kombati ya jeshi iliyoonekana imetunatuna bila kujua huyo ni bobezi kwa matumizi ya silaha.
Alipokabidhiwa tu bastola huko nje ya mlango kukawa kunatoka mlio kama wa kengele, ambao Kachero Yasmine alifahamu huyo ni Kachero Manu yupo nje ya chumba na kifaa chake cha "RFID" hivyo wakati umefika. "Tupa bastola chini na nyoosha mikono juu gaidi mwanaharamu wewe" Kachero Yasmine alifoka kwa sauti ya kazi sio tena ile nyororo ya kubembeleza aliyoizoea "Maso Maso". "Maso Square The Duduman" hakuamini anachokisikia katika masikio yake na wala macho yake hayakutaka kusadikisha kama kweli mke wake ndio huyo aliyembadilikia. Uso wake ulipigwa na taharuki alishatanabahi huyu mke wake kumbe alikuwa ni jasusi aliyepandikizwa kwake, lakini alishachelewa. Akatupa chini bastola yake na kutii amri ya kunyoosha mikono yake juu. "Rudi kinyumenyume usilete ujanja wowote nitakusambaratisha sasa hivi" alizidi kufoka Kachero Yasmine akihofia akiwa karibu yake anaweza kuanzisha mapigano.
Wakati anarudi kinyumenyume "Maso Maso" alikuwa uso wake umebeba tabasamu kama lote hana chembe yoyote ya hofu, mpaka Kachero Yasmine akaingiwa na hofu yeye. Ghafla Kachero Manu nae akavamia ndani baada ya kuvunja mlango kwa kutumia risasi. Hiko kishindo kilikuwa kosa kubwa sana kwao kwani Kachero Yasmine alivyopepesa macho yake kidogo tu kumuangalia Kachero Manu anavyoingia, "Maso Maso" akawa ameshafika ukutani akabonyesha swichi ya mfumo wa ulinzi wa kutumia ukungu mweupe unaosambaa kwenye chumba kama moshi mweupe.
Mfumo huo kitaalamu unaitwa "Smoke Security System"(SSS) ambao Tanzania ulikuwa bado haujaingia kabisa. Kwenye huo mfumo huo ukungu unazalishwa pindi glycerine iliyochanganyika na maji yaliyotakaswa 'distilled water' yakipashwa joto la umeme.
Ni mfumo ambao nchi zilizoendelea unafungwa kwenye mabenki makubwa, na stoo za kutunzia bidhaa za thamani kubwa. "Maso Maso" aliwachapa kibao cha teknolojia Makachero hao. Wakawa ndani hawaonani moshi mweupe na mzito unasambaa chumba kizima. "Kamata kamata huyoo anatoroka Kamata huyooo..." Kachero Yasmine alikuwa ameshapagawa anapiga kelele bila mpangilio. Kachero Manu chapuchapu akatoa miwani yake maalumu akavaa kidogo ikawa inamsaidia kuona kwa tabu.
Akaenda mpaka ukutani na kufanikiwa kuzima swichi ya mfumo huo wa ukungu. Baada ya kama robo saa hali chumbani ikatungamana, ukungu ukawa umetoweka, tahamaki wanajikuta wapo watu wawili tu, "Maso Maso" ameshatoweka hajulikani alipo.
MASO MASO JAMAJI HUYU SIJUI NI JINI LA KISOMALI??
![]()
Duuh....?SEHEMU-40

Nimeona the duduman Square,Nakuja sasa hivi leo Jmosi siendi kokote mpaka tuimalize