Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Riwaya mpya: Mbwa wa geti

RIWAYA: MBWA WA GETI
Na Bahati Mwamba
Simu 0758573660

Upande aliokuwa amesimama,tayari ulikuwa umeanza kuifikiwa na maji ,na hakutaka kabisa maji yale yamguse,alijitahidi kila namna kusimama kwenye kingo za njia ile ili kuyakwepa maji yale yaliokuwa yakitiririka kwa kasi na kutoa harufu kali iliokuwa ni adhabu tosha kwenye pua zake,tayari harufu ya maji yale ilikuwa imeanza kumuathiri katika mfumo wa fahamu zake,harufu ile ilikuwa imeanza kumlevya huku kichwa kikiwa kinamuuma na pua zilianza kutoa majimaji mepesi.
Hakutaka kuanguka kwenye yale maji maana aliamini kabisa hayakuwa salama kabisa,na hata alipotaka kuyaingia bado macho yake yalipata kushuhudia kile ambacho hakutaka kabisa kukiona,yalokuwa yanapitisha viungo vya binadamu.
Akili yake ilikwama hasa alipoona kichwa cha mtu kikielea,huku ubongo wake ukiwa upo nje na macho kodo,kuashiria mtu yule kabla hajakatwa kichwa aliona au alipitia mateso makali sana kabla mwili wake haujatenganishwa vipande vipande.
Alitamani kutapika,lakini tumbo halikuwa na kitu,njaa ilimsumbua,kichwa kilimuuma,pua zilianza kuziba na mwili haukuwa na nguvu japo ya kupiga hata hatua moja kutoka pale alipokuwa amesimama.
Akili yake ilifanya kazi kwa shida,lakini nafsi yake haikutaka imwache afe kizembe,nafsi ilimpa nguvu za kuendelea kupigania uhai wake kwenye lile pango.
Akili yake haikuwaza kitu kingine zaidi ya mwanae,hapo nguvu zikaurudia mwili wake,akayatazama maji yale yaliokuwa yanatiririka kwa kasi,akaona hayakuwa maji tu,yalikuwa ni maji yaliochanganyika na damu.
Miguu yake ilianza kufikiwa na maji yale,haraka akaruka juu na kuidaka mizizi iliokuwa imening’inia ndani ya njia ya pango lile na wazo la kuitumia kama ndio njia ya kupita bila kuyagusa maji yale ikamwijia na hakuwa na budi kuendelea kuikamata mizizi ile huku sasa akianza kuelekea kule maji yale yalipokuwa yanaelekea.
Baada ya mwendo mrefu kidogo huku akiwa bado anaitumia mizizi ile kama kamba ya kumvusha mle pangoni ,mikono ilianza kumsaliti ili asitimize adhima yake hiyo,mikono ilianza kuchoka kwa kuwa alikuwa amening’inia muda mrefu na bado hakuona kama kutakuwa na mwisho wa pango lile.
Alitamani kuachia mizizi ile ili akanyage ndani ya maji yale lakin nafsi yake ilimkataza,na hakuwa na la kufanya zaidi ya kuendelea kutembea huku akiwa amejishikiza na mizizi na Kama ungelitokea nyuma yake basi ungehisi ni nyani anaetembea kwa kudaka mzizi mmoja hadi mwingine.
Mikono yake ilianza kutetemeka,na hata mwili ulikuwa umeshachoka kupita maelezo na kichwa bado kilizidi kumuuma na pua bado zilikuwa zinazidi kupokea harufu kali ya maji yale ambayo hayakuwa ya uozo ila ilikuwa ni harufu kama ya acid flani ambayo hakuelewa ilitokana na nini ama ni acid ya namna gani.
Ilikuwa ni lazima ajiokoea lakini viungo vya mwili vilimsaliti,havikutaka tena kumpa ushirikiano,na akaamua kutulia tu pale alipokuwa huku macho yake yakiyatizama maji yale yaliokuwa yanatiririsha viungo vya binadamu kwa wingi sana,vingine aliona ni vya watoto na vingine vya wanawake na vingine vya wanaume.
Watu gani hawa wasio na huruma alijisemea ndani ya nafsi yake.
Mzizi aliokuwa ameshiria alisikia ukitikisika,mwanzo hakutilia shaka lakini mzizi ule ulizidi kutikisika katika namna ya ajabu na hapo akili yake ikamtuma atazame juu.
Kwa tabu sana akapata kuona kule kwenye shina mzizi ule kuna kitu kilijitikisa,kilikuwa ni kiumbe hai kilichokuwa kimeweka hifadhi pale.
“nyoka!!” alijisemea na haraka akataka kushika mzizi uliokuwa mbele yake lakini huko nako akapata kuona viumbe hai wengine,walikuwa ni popo wakubwa mithili ya mwewe wakiwa wameninginia na kwa uzoefu wake alikiri alikuwa hajapata kuwaona popo wa aina ile tangu anazaliwa hadi kufika umri wake aliokuwa nao wakati huo.
Mwili ulijaa hofu ya kushambuliwa na nyoka,lakini pia ya kushambuliwa na popo wale wakubwa,lakini aliona bora popo kuliko sumu ya nyoka.
Haraka mkono wake ukadaka mzizi wa mbele yake na kisha akafanya kudaka ya mwingine na alipotizama nyuma alipata kuona joka lile likijiachia kutoka kwenye kuta ya pango lile na kuanza kufuata ulekeo aliokuwapo,lakini si joka tu hata popo walianza kuruka huku na huko na hapo akafanya jitihada za kusonga mbele,lakini jitihada zake zilikuwa zinakwamishwaa na popo waliokuwa wameanza kuweka wingu jeusi mbele yake,walikuwa popo wengi sana na wakubwa na walikuwa wakitoa milio ya ajabu ajabu.
Alianza kupokea adha ya kupigwa na mbawa za popo wale na kitendo bila kutarajia akaona wale popo wanamshambulia yule nyoka kwa kumdonoa donoa.
Joka lile likashindwa kustahimili maumivu,likajitupa ndani ya maji na hapo ndipo aliona kile kilichokuwa kinamuogopesha kuyakanyaga maji yale.
Lile joka lilianza kuwa kama linaungua na kuanza kukatika vipande vipande,akiwa ameduwaa akashangaa kujikuta akianza kupokea maumivu ya kudonolewa na wale popo huku wakimpiga na mbawa zao,alipitia mateso makali ya kusulubiwa na popo wale na hapo mikono yake ilikuwa ikifanya jitihada za kupokezana kuwapangua popo wale huku kila akipata nafasi alikuwa akihama mzizi mmoja kwenda mwingine,hadi akafanikiwa kutoka eneo lile la wale popo lakini damu ilikuwa ikitoka mwili mzima kutokana na kunyofolewa nyama kwenye baadhi ya sehemu za mwili wake.
Alikuwa akipumua kama mtu alietoka kukimbia mbio za maratoni,na alipotizama chini hakuyaona maji yale wala hakuwa akisikia kelele zake.
Akajiachia kutoka juu ya pango lile na kudondoka chini huku akihema na alikuwa anajaribu kukabiliana na maumivu ya vidonda vyake.
Kwa kuwa alikuwa amechoka sana hakutaka kujua kama alipo ni salama au la akaamua kujipumzisha hapohapo na hapo akili yake ikamrudisha saa chache nyuma kabla hajakutana na adha ile.

Like,coment ili kila ikitoka upate notification

Tukutane jioni
daah bonge ya kitu hii
 
Mkuu Kudo900 ulituahidi asubuhi na jioni hii kitu, tupe wepesi kwa ahadi yako Chief
 
Mbwa wa geti

Sehemu ya tano

Akajilegeza kidogo na kujikwaa na akaenda hadi chini,kisha akaanza kunyanyuka taratibu,yule mlinzi akamfuata kwa kasi kwa lengo la kumpiga na kitako cha bunduki lakini hakuwa amejua hila ya Zedi na tayari zedi alikuwa ameona pa kutorokea na hakutaka kuwa mzembe wakati amefuzu kozi nyingi za ukomando,njaa hakuisikia tena
Mlinzi aliekuwa nyuma ya Zedi akahadaika kwa kasi akaanza kumfuata Zedi aliekuwa akijinyanyua kutoka chini, lakini adhima yake haikutimia na kitendo bila kutarajia akajikuta akipokea teke safi kutoka kwa Zedi ,teke lile likamrdudisha nyuma hatua kadhaa lakini akakuta akikikabiliana na ngumi za kasi kutoka kwa Zedi na ndani ya dakika moja alikuwa amejaa mikononi mwa Zedi huku walinzi wengine wakiwa wamefika pale kwa ajili ya kutoa msaada

Mitutu ya bunduki zaidi ya kumi ilikuwa imemwelekea Zedi aliekuwa nyuma ya mlinzi mmoja aliekuwa amemkaba kwa kabari matata na kisha alimweka ngao mbele yake na nyuma yake hakuwa na shaka kwa sababu alikuwa ameufanya ukuta kuwa kinga yake na aliamini hakuna wa kuweza kumshambulia kutokea nyuma hata kama angelitokea kwenye mlango wa kuingia kule walikokuwa wakielekalea mwanzo,bado angeliwaona.

Zedi alipiga hesabu za kutumia mabega ya mateka wake kuparamia paa lililokuwa kichwani pake ni wakati huo aliposikia sauti ikitokea kwenye mlango waliokuwa wakielekea kabla hajafanya manjegeka kwa bwana yule alie mikononi mwake sasa.
Kill them all
Sauti aliitambua ilikuwa ni sauti ya Kabah nae hakutaka kuona risasi za SMG zijaa kifuani kwake .
Zedi ni mchawi wa mipango ya kujiokoa na pia ni mchawi wa mapigano huwa hakati tamaa hata kama amedhoofu vipi,na hili alilidhihirisha mbele ya Kabah na genge lake.
Zedi alimsukuma yule mtu aliekuwa amemweka kama ngao na mtu yule akaelekea kuwakumba walinzi walikuwa manajiandaa kushambulia,kisha kwa wepesi wa ajali ya bodaboda akachumpa kwenda juu kidogo na guu lake la kulia likatua katikati ya mgongo wa mateka wake aliekuwa ameanza kuchezea risasi na kwa kasi ile ile akaenda juu zaidi na mikono yake ikalikamata paa la jengo lile kisha kama nyoka awindae akajivuta na kukaa juu ya paa kwa namna ya pekee kabisa hadi walinzi wale wakaacha kushambulia wakabaki wakishangaa uwezo wa Zedi,hawakuamini kama angeliweza kuwatoka kwa namna ile ya ajabu kabisa..
Kabah alicheka,sio kama alifurahi la hasha,alicheka kwa fadhaa na chuki ya kutorokwa na Zedi na huku nafsi yake iki kiri kabisa ya kuwa Zedi akifanikiwa kutoka kwenye ngome yake basi mambo yake yatamwendea kombo.
****
Zedi akiwa juu ya paa ile akaona mbele yake hakuna nyumba hata moja,lilikuwa ni pori tupu,pori lenye miti mirefu na hapo nafsi yake ikapata nguvu,alipenda michezo ya porini na huo ndio ulikuwa wakati wake.
Akachumpa hadi chini na kisha akaanza kukimbia kusonga mbele kulikokuwa na miti mingi iliofunga na tayari kiza kilianza kukolea wadudu wa usiku walikuwa wanapiga miluzi kushangilia muda wao,lakini si wote waliokuwa wakishangilia kwa furaha maana wengine walijikuta wakishangilia kwa woga baada ya kusikia vishindo vya kitu kizito kikipita karibu yao,alikuwa ni Zedi akikimbia katikati ya pori asililolijua na tayari sasa nyuma yake alikuwa akikoswakoswa na risasi za waliokuwa wakimkimbiza huku wakiwa na amri moja tu wakimpata wamuue.
Zedi alipiga hesabu maana risasi zinatoka kwenye bunduki moja,hivyo mtu aliekaribu yake bila shaka ni mmoja haraka akatoka kwenye uelekeo ule aliokuwa anaendea na akajibanza kwenye mti,lakini akagairi kujificha hivyo na kama paka akauparamia mti ule kisha kama nyoka akajigeuza na kichwa kikatazama chini huku mikono ikiwa imeukama vyema mti ule mrefu,alitulia hata pumzi zake mwenyew hakuzisikia.

Mtu yule aliekuwa anamkimbiza Zedi,akashangaa kuona anakimbia peke yake,akajua anategwa au amepigwa changa la macho usiku ule.
Akaanza kunyata huku sasa hofu ikiwa dhahiri moyoni mwake.
Alihofu vitu viwili,mosi alihofu viumbe ambao aliamini watakuwapo ndani ya pori lile usiku ule na pili alihofu kukutana na mtu yule aliemwona akidondoka kutoka juu ya paa la kambi yao,lakini kubwa zaidi akiogopa maana hakuwa na ruhusa ya kukimbiza mtu usiku ule na hata radio yake ya upepo ilikuwa haijapata uhai,hivyo ilimaanisha kazi alioifanya haikuwa na baraka zote kutoka kwa mkubwa wao.

Akagairi kuendelea mbele,

Ni wakati mlinzi yule akigeuka ili arudi alikotoka,hapo ndipo akakutana na kivuli cha mtu kikiwa kimesimama bila kutikisika.

Wakati mlinzi yule akiwa anajiandaa kushambulia,hakujua hata kimetokea nini akajikuta anaelekea kuanguka,lakini hakufika chini mkono wake wa kushoto ulikuwa umejaa kwenye mkono imara wa kivuli kile.

Mlinzi yule akavutwa kwa kasi kurudi juu na bila kutarajia akajikuta akipewa kichwa cha uso hadi akaona nyotanyota kisha likafuatia swali ambalo hakulitarajia kutoka kwa kivuli kile .

“Nioneshe njia ya kutokea katikati ya pori hili”

Mlinzi yule akawa hana cha kubisha akamweleza kinaga ubaga ya kuwa,eneo walilopo kilomita mbili mbele kuna ukuta mrefu sana,na hakuna aliewahi kuuvuka na huko pia kuna askari wengi sana.

Zedi akapagawa kuyasikia yale kutoka kwa mlinzi yule,akayarudisha macho yake kwa mlinzi yule na hapo masikio yake yakapata kusikia habari njema kidogo kutoka kwa mtu yule aliekuwa anaongea kiswahili na kiingereza kwa lafudhi ya kikenya.

Mtu yule alimwambia kuwa,njia pekee ni kupita kwenye mkondo wa maji machafu,mkondo ambao unapeleka maji yake kwenye mto Sariza,na chemba ya kupita ni moja na ipo hatua mia kutoka walipo.

Zedi ni mwanaintelejensia aliebobea,akayapima maelezo ya mtu yule na hapo akagundua jambo,mtu yule alisema ukweli,lakini kuna kitu zaidi kwenye macho ya mtu yule,alionekana kuutapika ukweli makusudi ili amwokoe Zedi,lakini kwanini atake kumsaidia,likabaki swali kichwani kwa Zedi na hakutaka kulipata,akasimama na kumwachia mtu yule kisha akaanza kupiga hatua kufuata uelekeo alioelekezwa.

Hakupiga hatua nne,akasikia mtu yule akimpa tahadhari
 
tuendelee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom