Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Mbwa wa Geti


Akakichana,kisha akikipeleka chote puani na kuvuta unga uliokuwamo na hata alipomaliza akakitupa chini huku sasa akili ikimrudia kwa mbali na kutoka kwene maji na kukaa juu ya sofa huku mwili wake ukupokea burudani murua na kuleta msisimko wenye raha ya ajabu,ambayo hajapata kuiona wala kuiwazia kama utakuja kuwapo duniani.
*****
Tausi alikuwa amejikunyata kama kinda la ndege lililoachwa na *****,sasa alikuwa akiyasikia maumivu makali yakipita mwilini mwake,na hapo akakumbuka alivyosulubiwa usiku kwa mikanda,ngumi na mateke.
Alijikuta akilia kwa majuto ndani ya nafsi yake,akajitazama alivyokonda na kisha akajiona alivyouchi sebleni,haraka akakimbia na kuingia chumba kilichokuwa karibu na yeye huko akalokota kanga na kujifunga kisha akakaa kwenye kitanda kilichokuwa humo chumbani na mikono yake akaipeleka katikati ya kitanda alichokikalia na hapo akakutana na joto joto ikimaanisha palikuwa na kiumbe hai aliekuwa amelala hapo na ameondolewa muda mfupi uliopita.
Tausi alitambua tayari mwanae amepelekwa asikotaka apelekwe.
Kilio cha kwikwi kikamkamata na akabaki akijikamua machozi tu maana hayakumpa ushirikiano wa kutoka na hapo akakumbuka ya kuwa hiyo ni dhambi ya usaliti inamtafuna.
Nafsi yake ikamlilia mungu,huku akiomboleza kwa kuomba msamaha,alimwomba mungu angalau amwondolee adhabu mwanae na amtwishe yeye alieyafanya yote yale,hakika Tausi alilia kilio cha mbwa koko.
Akiwa katikati ya majuto,mlango wa kile chumba alimo ukafunguliwa na yeye akanyanyua kichwa kutazama,alikuwa anatazamana na Kabah,mwanaume aliempenda kwa muda mfupi na pia mwanaume aliemchukia kwa muda mfupi vilevile,kabah alikuwa anatabasamu,Tabasamu ambalo lilikuwa ni chukizo kwa Tausi.
“hali yako mpenzi”
Tausi alitamani atukane tusi zito,lakini alimwogopa Kabah,alimwogopa kwa kuwa alijua ni muda wa kupokea kipigo nae hakutaka hilo litokee hivyo akakaa kimya huku akiwa na uchungu wa kupindukia.
“Usijali mwanao atarudi salama,lakini kubwa tambua mwanao ni punda wangu mdogo na wewe ni MBWA WA GETI,lakini wewe mbwa kula kwako kunategemeana na kazi atakayo ifanya punda,hakikisha unalinda hapa nyumbani kwa uangalifu”
Yalikuwa ni maneno makali yaliokuwa yanaupasua moyo wa Tausi bila kisu,sasa machozi yalitoka na hata wakati Kabah anaendelea kuzungumza Tausi hakumsikia kabisa kilio kilikuwa ni faraja yake,lakini hilo halikuwa zuio kwa Kabah asitoe ya moyoni mwake
“…..nakuachia hii chakula nadhani itakutosha kwa mchana huu na siku nitakazo kuwa sipo,,,afu jana nimeona Temba alikupa dawa usiku,haaha mi nilitaka ufe,lakini mungu bado anakupenda naondoka nitarudi hakikisha nakukuta usijaribu ujinga hutafika popote”
Kabah aliupigiza mlango wa chumba kile na kuondoka huku akiwa amemwachia kilo kadhaa za madawa ya kulevya kitandani,Tausi alizitizama lakini hakuwa na cha kufanya..
******
Kiza kilianza kuingia na tayari ilionekana jua limeshaihama mashariki na lilikuwa magaribi,hadi wakati huo Zedi hakuwa amekiona chakula,wala hakuwa ameona walau wenzie wakipata chakula.
Kwa uzoefu wake alikuwa ameshagundua baadhi ya mateka wenzie wanapoteza maisha kila muda na sasa alikuwa amesalia na hesabu ya watu saba tu waliokuwa hai akiwemo yeye.
Akili yake ilimtuma kufanya jambo na haraka akaanza kufanya jitihada za kujikunja ili angalau meno yake yaweze kufikia fundo moja la kamba liliokuwa limefungwa mkononi.
Akiwa bize na zoezi hilo akasikia mtu akikohoa na alipotizama mbele yake akaona kuna mtu akijitikisa kwenye kiti na mtu yule alikuwa akimtizama kwa macho yalioashiria kuwa azidi kufanya jitihada.
Nguvu zikaanza kumrudia na akataka kuendelea na zoezi lake la kuzingata kamba,lakini kabla meno hayajafikia kamba zile mtu yule akakohoa tena na hapo Zedi akanyanyua kichwa tena na akaona kitu katika uso wa mtu yule
Mtu yule ni kama alikuwa anamuita kwa ishara amfuate.
Kwa uzoefu wa kazi za kijasusi,Zedi alitambua kabisa mtu yule alihitaji kumwambia jambo na tena yaeza kuwa jambo la maana.
Zedi akaachana na zoezi la kujifungua kamba,na akaanza kuruka ruka na kiti,ilikuwa kama mchezo wa kuigiza,lakini ilikuwa ni hatua ya mtu kuhama sehemu moja kwenda nyingine kwa namna ile.
Zedi alifanikiwa kufika mbele ya mtu yule na hapo akapata kuona tabasamu la mtumaini la mtu yule likichanua kwenye uso uliochoka,uso uliokata tamaa .
Zedi akazisikia pumzi za mtu yule zilivyokuwa zikitoka kwa tabu,lakini bado aliona nia ya mtu yule ikiwa ipo pale pale,mtu yule alitaka kumpasha jambo,jambo gani hilo hakujua.
“Kenya yetu ipo kwenye matatizo..”
Zedi alikunja sura kwa kushindwa kuelewa yupo Kenya au Tanzania,hapo roho yake ikabaki juu na akazishusha pumzi nyingi kwa wakati mmoja na na hapo akaona mtu yule alikuwa akimtizama kwa jicho la kukata roho japo uso wake ulionesha alitaka kusema kitu na haraka Zedi akatumia ujuzi wake na kumfikia karibu kabisa na kisha akawa makini kusikia kile alichotaka kusema mtu yule.
“Kanya yetu ipo shakani,bado uko na nguvu,fanya hima,toka hapa kwenda Nairobi Kaviba stereat,nyumba namba 150,tumia 0258,waeza okoa Kenya….”
Yule mzee hakumaliza maelezo yake na akawa amekata roho na punde mwanga ukawepo mle ndani ya godauni na kisha macho ya Zedi yakapata kuona watu sita wakiingia pale ndani na nyuma yao alikuwapo mzungu yule aliekuwa ameingia kwa mara ya kwanza na wadudu wa ajabu na mara hii alipata kuona akiwa na mfuko mkubwa kiasi cha kilo hamsini hivi na alisaidiana na mtu mwingine ambae bunduki ilikuwa inanginia kifuani pake .
Safari hii Kabah hakuwepo na hata sura za hawa walinzi zilikuwa ni mpya.
Walikitua kifurushi kile na kisha wakamshusha mtu mmoja aliekuwa anabembea kwenye kamba kichwa chini miguu juu.
Walipokwisha kumshusha,wakamlaza chali,japo alifanya jitihada za kujinasua mikononi mwa watu wale lakini alishindwa mwili ulikuwa dhoofu.
Alifunikwa na bangaloo jeusi mithili ya maiti iondelewayo mochwari kisha wakawa wanaifunga zipu na walipofika kifuani,wakasogeza kiroba kile kisha kwa tahadhari wakakifungulia nusu na kuwa kama wanatoa kitu na waliporidhika na kiasi walichotaka haraka dokta yule akachukua kispray na kupuliza ndani ya bangaloo lile na haraka wakafunga zipu.
Zedi alishuhudia tu mtu yule akitikisika kidogo na ukelele kwa mbali kisha akatulia.
Dokta yule aliwambia kitu watu waliokuwa wameomgozana nae na haraka wakanyanyua mtu yule na kumfunga tena kamba akiwa ndani ya bangaloo lile na walipohakikisha ananginia ,taratibu wakaanza kugungua zipu ile na kwa tahadhari kubwa sana kisha wakaliondoa kabisa bangaloo lile.
Kwa mara nyingine tena,Zedi alipata kuona jambo gumu kuamini,ila ndivyo ilikuwa.
Wadudu weusi ti walikuwa wanaushambulia mwili kwa kasi ya ajabu na ndani ya dakika zile mbili tayari nyama zote zilikuwa zimelika na ilikuwa imebakia mifupa na wadudu walikuwa wengi mithili ya mzoga wa mbwa uliwavyo na siafu.
Damu ilimsisimka kwa kile alichokiona na alikiri kuna watu wanaroho ngumu ajabu.
Wadudu wale walikuwa wanakula ajabu na walkies na uwezo wa ajabu.
Baada ya kuhakikisha zoezi lao limekwenda sawa,dokta yule akachukua tena,spray na akapuliza kwenye mwili wa mtu yule na wale wadudu walianza kudondoka mmoja mmoja na walipokwisha ilikuwa imebaki ni mifupa tu bila hata tone la damu na hapo wakapongezana kisha wakanyanyuka na kuondoka.
Zedi alibaki akitetemeka na alijua watu wale wanafanya majaribio na ipo siku watamfanyia na yeye hivyo asipofanya jitihada basi anaweza kufia hapo.
Meno yake yaliendelea kufanya kazi na kwa asilimia kadhaa alifanikiwa kulipata fundo la kamba zile.
Wakati akiwa yupo ukingoni mwa kazi yake,mara akaja mlinzi mmoja na kumfunguwa zile kamba bila kumsemesha,na punde akamwamuru anyanyue mikono juu na aongoze njia nae akatii.
Walitoka hadi nje ya godauni lile na hapo ndipo akaona kumbe si godauni,walikuwa wapo ndani ya jengo la wazi lililoko chini ya ardhi.
Na hata walipofika juu hapo ndipo alishangaa zaidi,alikutana na majengo yamejengwa kama shule na kile kona palikuwa na mlinzi akiwa na bunduki yake mkononi.
Alipelekwa hadi kwenye jengo moja lililokuwa na taa nyingi zenye mwanga mkali na hata kabla hajafika ndani alisikia makelele ya mtu akiwa anapitia mateso makali hadi wakati huo.
Akajilegeza kidogo na kujikwaa na akaenda hadi chini,kisha akaanza kunyanyuka taratibu,yule mlinzi akamfuata kwa kasi kwa lengo la kumpiga na kitako cha bunduki lakini hakuwa amejua hila ya Zedi na tayari zedi alikuwa ameona pa kutorokea na hakutaka kuwa mzembe wakati amefuzu kozi nyingi za ukomando,njaa hakuisikia tena

Itaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom