Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Ila kudoo me napata maumivu huyo mtoto anavyoteseka jaman,embu pindisha pindisha basi huyo mtoto atoke kwenye hicho kifungo
 
Mmh me huku nilishajitoa maana nyie wenyewe hamueleweki,leo baby kesho dada na kaka,nimepigania hii ndoa lakini nyie wenyewe vichomi sijui mlitamaniana tu
Kweli ulijitahidi ila Best akakuangusha akanikana mchana kweupee nami nikaona isiwe kesi nikachanja mbariga huyooo kumbembeleza mama kitunguu arudi nyumbani
 
Mbwa wa geti

Sehemu ya kumi na tisa

Alimwacha ndani Taus akijiandaa na yeye akaenda kuchukua gari lake lililokuwa limepaki pale uwanjani,walinzi wenzie waliona tu hekaheka za Temba aliejiita Mbwa,lakini hawakujua ni za nini hekeheka zile.

Tausi na mwanae na mkoba wenye nguo kidogo wakapanda ndani ya gari ile na kutokomea mjini huku wakipitia njia ya Area A,na katikati ya safari Temba akatoa kete mbili na kumpa Tausi aliezibugia na kumpa faraja ya ajabu huku mwili wake ukiwa umesahau maumivu.
****

Mina alikuwa anatoka ofisini kwa Rpc ndipo alipoona simu yake ikitetema,mwanzo alidhani ni Ziga,lakini alipoitoa ndipo akapigwa na butwaa,ilikuwa ni namba ya Temba.

Akiwa bado anashangaa Temba kumtafuta baada ya muda mrefu kupita,akaona ujumbe mfupi kutoka tena kwa Temba.

“Wahi Ikulu T620HHH,” mara moja Mina akaelewa ujumbe ule ni taarifa fulani ya hatari na pengine angelipuuzia kama ungelitoka kwa mtu mwingine,lakini ulitoka kwa mtu wake wa karibu na mtu wa matukio na kazi.

Haraka akarudi ofisini kwa Rpc na kuomba usafiri wa gari na difenda ya polisi yenye kasi na askari wenye ujuzi.

Rpc Mabeyo bila kuuliza akatoa magari mawili la kwake na la askari wa kawaida na msafara huo akauacha kwa Mina askari mwenye weledi wa hali ya juu .

Ziga nae alipata taarifa kutoka kwa Mina akiwa anapata taarifa kutoka kwa wenyeji wa nyumba ya Zedi na haraka akaondoka kwenda huko Ikulu ambako wote wawili hawakujua kuna kitu gani kwenye hiyo gari.

Mina ndie alikuwa wa kwanza kuliona gari lile likiwa linatembea taratibu sana haraka akatoa taarifa kwa askari wenzie waliokuwa nyuma kwenye difenda na silaha za mkononi.

“Oya kozo eeh kuna njangu nyuma wapo kishari sana” dereva wa gari lile lililokuwa likifuatwa na polisi alinwambia mwenzie aliekuwa kushoto kwake.

“mmh usitie Shaka watakuwa na ruti zao hao”

Hawakumaliza maongezi yao wakaona taa za kuwaashiria wasimame kutoka kwenye gari iliokuwa nyuma,gari ya polisi.

Dereva akasema na wenzie waliokuwa wako nyuma kama abiria wenye mizigo yao ndani ya kenta ile,nao wakajua kumekucha,haraka wakatoa silaha zao na bila kuuliza wakaanza kushambulia gari ya polisi.

Barabara ikawa haitoshi risasi zikisikia huku gari zikiwa kwenye mwendo mkali sana.

Mina hakutaka kushambulia kwanza maana alihitaji kwanza kufanya kitu haraka akahamia upande wa kulia yanakopita magari yanayotoka Dar.

Akaongeza kasi na kwa aina ya gari alilokuwa nalo haraka akaifikia ile kenta na hakutaka kupita ila akaamua kuwa nayo sambamba na kwa kutumia mkono wa kushoto akachomoa bastola yake na kulenga usawa wa dereva wa kenta ile na alipoachia risasi ikaenda kutua kwenye kichwa na gari lao likakosa mwelekeo na kwenda kujingonga kwenye mti na kubinuka.

Haraka askari wakashuka na kuwafikia watu waliokuwa kwenye kenta ile na kuwakuta baadhi wakipigania uhai wao huku mmoja kati yao akiwa amekufa tayarim.

Askari mmoja akakimbilia kwenda kufanya wokozi,lakini wakati anainama ili kumvuta mtu aliekuwa upande wa nyuma akaona kitu cha ajabu na haraka akaruka na kurudi nyuma.

Kitendo kile kilifanya wengine wajiweke tayari kwa lolote na hapo akawa amefika Mina ambae moja kwa moja bila woga akaongoza kwenda kuangalia.

Hakika hakuamiani kuona kile alichokiona.

Walikuwa ni wadudu wengi sana waliokuwa wanashambulia miili ya watu wale na waliobekana kutoka kwenye maboksi fulani ya vioo na tayari walianza kutafuta njia ya kutoka nje ya gari ile.

Ziga alisimamisha gari na kushuka haraka na bila kuuliza akawaomba askari wote warudi nyuma ni baada ya kuwaona wadudu wale waliokuwa wameanza kupanda juu ya gari ile.

Itaendelea
 
nyie wote bana ndo hakumkueleweka,mmeniudhi jaman
 
Mmh tuendeleee basi jaman kaka kudoo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom