Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Riwaya mpya: Mbwa wa geti

Mbwa wa geti

Sehemu ya Ishirini

Ziga alisimamisha gari na kushuka haraka na bila kuuliza akawaomba askari wote warudi nyuma ni baada ya kuwaona wadudu wale waliokuwa wameanza kupanda juu ya gari ile.

Ziga akaachia risasi ilioenda kulenga tank la mafuta la kenta ile na kukatokea mlipuko mkubwa uliosababisha kupotea kwa kila kitu ndani ya gari ile.

“huu mradi bado upo!!” alisema Ziga lakini sauti yake ilimfikia Mina na hapo Mina akajua Ziga anajua kuhusu kitu hicho.

Akaagiza uchunguzi zaidi ufanyike kuhusu gari ile huku Mina na Ziga wakipanda gari moja na kuelekea sehemu nyingine kukutana na mtu mwingine.

*****

Saa mbili ya usiku ilimkuta Zedi akiwa anaingia nyumbani kwa Wambui.

Wakati anaingia tu akapokelewa kwa namna ya kipekee,japo alitegemea,lakini hakudhani kama itakuwa gafla kiasi kile.

Wakati anaingia tu mlangoni akapokelewa kwa teke kali la kifua na alipojaribu kurudi nyuma ili atoke nje akashangaa kutandikwa teke la mgongo na kumfanya aingie ndani bila kupenda na huko akakutana na watu watatu wakiwa wamesimama na mitutu ya bunduki ikiwa tayari kutoa roho yake.

Akaamuliwa kunyosha mikono juu nae akatii na punde akatokea Wambui na kamba mkononi akamfunga Zedi na wakamkalisha kwenye kiti,mateso yakaanza.

Wakati watesaji wa Zedi wakidhani wao wapo salama,walikuwa wanakosea.

Kulikuwa na mtu hatua chache nyuma ya sebule ile waliokuwa wameigeuza kama uwanja wa mazoezi kwenye mwili wa Zedi.

Risasi iliotoka kwenye silaha iliofungwa kiwambo cha kuzuia sauti iliondoka na wawili kati ya wanne waliokuwa mle kisha pasipo kutarajia mlango ukasukumwa akaingia mtu kwa kasi ya ajabu huku akiachia mapigo safi yaliomfanya hadi Zedi atabasamu japo alikuwa bado amefungwa kwa kamba.

Zedi aliyaona yote na hata mtu yule alipotaka kutoa pigo la kifo kwa binti mrembo Wambui aliliona na akaachia ukulele wa kumzuia mtu yule asifanye vile.

Mtu yule kwa jinsi alivyokuwa amevaa Zedi hakupata shida kujua ndie mtu aliemwona akiadhibu watu waliokuwa wamebeba mzigo kutoka kwenye nyumba ya mzee Matare na ndie mtu aliepambana nae ndani ya nyumba hiyohiyo ya mzee Matare.

Mtu yule akajifunua sura yake na hapo Zedi akatabasamu baada ya kumjua
“Zedi nilikwambia tupatane Nairobi”

“na tumepatana Mao Waira” alizungumza huku akimalizia kujifungua kamba alizokuwa amefungwa na punde akawa huru huku jicho lake likinasa hila alizokuwa akitaka kuzifanya Wambui nyuma ya mgongo wa Mao Waira.

Haraka Zedi akaachia teke safi lililomkuta Wambui kifuani na kumtoa uhai wake kabla hata hajafika chini.

“Nilitaka kummaliza ukatetea ili umue wewe” Mao Waira alisema huku akicheka na kumpiga Zedi begani kisha wakaanza kutoka ndani ya nyumba ile huku Mao waira akipiga simu kituo cha polisi ili waje kuendelea na taratibu nyingine.

“Idara ya usalama ya Kenya,haikuwa imelala bwana Zedi,tulijua kabisa hizi ni hila za watu wenye pesa kutaka kuchukua hii nchi kihuni na hivyo tumefanya jitihada na kiasi chake tumefanikiwa kudhibiti na kuwakamata baadhi waliokuwa wakituhujumu ila bado kisa cha yote haya bado hakijajulikana japo wanaohusika wanajulikana.” Alizungumza Mao waira aliekuwa amejitambulisha kuwa ni mtu kutoka idara ya usalama ya nchini Kenya.

“Ni wewe ulifyatua smoke mashine pale KCB jana”aliuliza Zedi

“Yah tangu usiku ule tulipopambana kule NHC kwenye nyumba ya mzee yule,sikukimbia kama ulivyodhani,wakati unatoka na unarudi nilikuwa nyuma yako na ulipoamua kulala nikaacha vijana pale kukuwekea ulinzi na ulipotoka ahsubuhi nikaunga tela hadi nilipoona wale mbwa weupe wanakuja mle nikaamua kutumia uhuni wa kukusaidia japo ulivyotoka sikujua hadi nilipokukuta Langata Court kwa Jafo,nikaweka vijana wakulie rada”

Ok ahsante kwa msaada wako Waira,lakini hawa mbwa weupe ni kina nani hasa”

Itaendelea
 
Mbwa wa geti

Sehemu ya Ishirini na moja

Ok ahsante kwa msaada wako Waira,lakini hawa mbwa weupe ni kina nani hasa”

“haka kakikundi ka wapuuzi flani kazi yao ni kumwaga wale wadudu na kuua watu..anyway twende tukate mzizi wa fitina kwa Jafo anakikao usiku huu” walizungumza hayo huku wakiwa wanapaki gari yao nyuma ya NHC court,kisha wakaanza kutembea kwa miguu hadi walipoingia ndani ya uzio wa nyumba ile inayomilikiwa na Jafo.

Wakagawana

Mmoja alipita upande wa nyuma na mwingine alipita upande wa mbele
*****

Ziga alikuwa amesimama huku akimtizama Tausi aliekuwa amekaa kwenye sofa na mtoto alikuwa mikononi mwa Mina huku Temba akiwa nae kasimama.

Shemeji kilitokea nini hadi ukajikuta mikononi mwa mtu kama yule” aliuliza Ziga huku akionekana dhahiri anahasira na mwananke yule

Mwaka mmoja nyuma

Zedi alitambua ndoa yake imeingiliwa na mdudu pesa na tayari aliona kabisa mkewe Tausi haambiliki.

Uwezo wa kumpiga alikuwa nao,lakini hakutaka kufikia huko maana aliamini uwezo wake wake na kupambana si kumpiga mwanamke.

Pengine alikuwa sahihi,lakini ilikuwa ni tofauti kwa mkewe Tausi ambae alimua kuutumia huo uhuru kuutesa moyo wa Zedi ambae hadi wakati hakuwa na kauli yoyote kwa mkewe huyo aliekuwa ameanza tabia ya kuchelewa kurudi na akirudi huwa amelewa pombe chakari.

Zedi majukumu ya kulea mtoto yalikuwa juu yake huku kila mara akishuhudia mkewe akiondoka na kurudi na mabunda kadhaa ya pesa.

Sio kama hakuwa na pesa la alikuwa nayo ila hakutaka itumike vibaya kama mkewe Tausi alivyotaka.

Tausi raha za dunia zikamdanganya na nyumbani hakukumbuka tena,akaanza safari za kusafiri nchi za nje huku akiwa na bwana ake Kabah.

Siri ya safari zao Tausi aliijua,alijua wanapitisha dawa za kulevya kimagendo.

Haikuwa kusafirisha tu,akaanza na kutumia,hatimae akakolea.

Kabah amwambie nini asitake

Akashauriwa kudai taraka kwa mwanaume suruali Zedi,nae akaomba na Zedi akatoa.

Akashauriwa tena kudai mtoto, hapo ikawa pagumu,ikabidi ustawi waingilie na mwenye haki ya kuishi na mtoto akawa ni Tausi Zedi anahudumia tu.

Zedi hakutaka kukubali akataka kujua jeuri ya Kabah.Akarudi tena kwenye kazi ya upelelezi bila kupenda

Mwanzo tu wa upelezi wake akagundua biashara haramu ya Kabah,Kabah alikuwa anasafirisha watu na madawa ya kulevya.

Kitu ambacho Zedi hakujua ni kuwa Kabah aliingilia familia yake kama kulipiza kisasi maana alijua Zedi ndie aliemuulia baba yake katika mkasa uliopewa jina KIKOSI CHA PILI.

Kabah alitaka amtese Zedi kisaikolojia kabla hajamuua,hilo alifanikiwa,alisambaratisha familia yake na sasa anaimiliki yeye na alikuwa ameanza kuitumia atakavyo.

Kabah aligundua nyendo zake zinafuatiliwa na komando hatari Zedi hivyo haraka akasuka mpango kabambe wa Zedi kutekwa ndani kwake,hilo nalo alifanikiwa japo kwa mbinde sana.

Tausi tofauti na alivyotegemea kupata mapenzi,akajikuta akianza kula joto la usaliti,safari za nje zikaisha huku kila mara akipigwa na kuingiliwa kingono na marafiki wa Kabah.

Kabah akamletea wanawake wengine ndani na kufanya nao ngono mbele yake.

Tausi akashuhudia Mwanae akiachishwa shule na kuanza kutumika kubeba mizigo kadhaa ya dawa za kulevya.

Alipojaribu kuzuia akaambulia kipigo na vitisho.

Akajuta,akajuta!!

Ikaja siku aliosaidiwa na Temba na sasa yupo mbele ya shemeji yake Ziga na mke mwenzie Mina aibu ilioje!!

****

Zedi ndie aliepita upande wa nyuma na kufanikiwa kuona kikao kilichokuwa kinaendelea kupitia dirishani

Zedi alishangaa kumuona kabah,ila alishangaa zaidi kumuona waziri wa uchukuzi na madini wa nchini Tanzania huku wabunge wawili nao wakiwa miongoni mwao.

Akiwa bado anatazama akashudia Mao Waira akiingia kwa kasi pale ndani na kuvamia ule mkutano na kuwaweka chini ya ulinzi watu wote.

Akiwa bado anajaribu kufungua dirisha apitie hapo akashudia Kabah akiruka na kumpiga Waira kwa pigo safi kisha hakutaka kusubiri akakimbilia nje

Zedi hakutaka kuachwa nae akatoka kasi kuwahi upande wa mbele lakini alikuwa amechelewa alikutana na moshi wa gari

Hakuhangaika nae

Itaendelea
 
Mbwa wa geti

Sehemu ya Mwisho

Zedi hakutaka kuachwa nae akatoka kasi kuwahi upande wa mbele lakini alikuwa amechelewa alikutana na moshi wa gari

Hakuhangaika nae

Akaingia ndani haraka na kuongeza nguvu pale ndani huku nje vikisikika vingora vya polisi vikipiga kelele kusogea pale.

Wahalifu wote wakatiwa pingu kisha Zedi akaomba awasiliane na Ikulu Tanzania,na alipomaliza akaomba kuwasimamia wabunge wale na waziri wao had ndege binafsi itakapo kuja kuwachukua.

Waira akabaki na kazi moja tu kuchoma maabara zote zilizokuwa chini ya mbwa weupe na wanajeshi wa Kenya walielekea Karura forest kulikokuwa na kambi ya Mbwa weupe.

Kasiki ilioibwa kutoka kwenye nyumba ya mzee matare ilimshinda Mao Waira kuifungua,akamuomba Zedi na Zedi akatumia namba 0258 alizopewa wakati akiwa ametekwa na mzee matare.
Kasiki ile ndio ilibeba siri ya mkasa ule.

Mzee matare alikuwa ni dokta na mara nyingi alijikita kufanya tafiti za wadudu na hapo ndipo akapata wazo la kutengeneza aina ya wadudu watakao kuwa kama tiba kwenye mimea yaani wadudu watakao kuwa wanakula wadudu waharibifu wa mazao

Mzee huyu alitengeneza fomula za kisayansi na hatimae akafanikiwa wadudu wale.

Furaha yake ikapata doa baada ya kupata ugeni kutoka nchi za mbali,wao wakaja na wazo la kutengeneza wadudu wala nyama.

Kadri wafadhili wale walivyokuwa wakimfadhili wakaleta na watalamu wao,nasasa Mzee matare akaanza kuona hatari na kibaya zaidi akagundua mpango uliokuwa nyuma ya yote

Mpango ulikuwa ni kuwasambaza wadudu wale maeneo yote ya nchi za Afrika mashariki,kisha wao waje na tiba ya kuwaua wadudu wale,watapata pesa nyingi sana.

Lakini kikubwa walikuwa wanamwaga wale wadudu sehemu zilizokuwa zimegunduliwa madini na mafuta na ugunduzi huo ulikuwa haujafika mikononi mwa serikali yoyote katika nchi hizo.

Maeneo athirika yote wakazi wangehama hivyo,wao wangeingia ubia na serikali kuyamiliki kwa kigezo cha kutoa dawa ya kuwaangamiza wadudu wale.

Mzee yule akafanya hila akaiba ramani ya maeneo hayo yanayolengwa na akaificha ndani kwake na wakati anafanya jitihada za kuzuia akaangukia mikononi nwa wa wasaliti hatimae akaiaga dunia mbele ya macho ya Zedi.
****

Zedi alipokelewa kama shujaa uwanja wa Dodoma na waziri mkuu,IGP na CDF bwana Salim Komba.

Watuhumiwa wakachukuliwa na kupelekwa mahabusu.

Zedi akatoa ramani nzima na mpango mzima ulivyokuwa huko Kenya ila hakuwaambia kuhusu kutoroka kwa Kabah,alimhitaji akiwa mzima au mfu yeye mwenyewe.

****

Wakati Kabah akiwa ndani kwake na kudhani yupo salama,akashangaa kuona Burizozo anaingia kwa kasi na bastola mkononi.

“Tumevamiwa asee,Temba ana…” hakumaliza kauli yake Kabah akachukua bunduki yake na kutoka nje.

Kama alidhani vita ni ya kitoto alikosea

Alipata kushuhudia watu watatu tu wakiua kama mchezo tena kwa kasi na weledi wa hali ya juu.

Akamwacha Burizozo aendelee kupambana yeye akarudi ndani na kutaka kutumia mlango wa nyuma kutoka.

Ziga alimuona wakati akijaribu kukimbia,akamfuata huku sasa burizozo akiwa amebakia kutazamana na Temba na Mina akagwaya.

Temba akamrukia kwa aina ya Tailand kiki na goti lake likakutana na kifua cha Burizozo na kumpeleka chini,haraka akatak kujinyanyua lakini akachelewa kasi ya Temba ilikuwa ni kubwa akamtandika teke la mbavu.

Temba akataka kumuua lakini Mina akawahi na kumzuia kisha akampiga pingu na punde gari za polisi zikaingia kwa fujo na kukutana na maiti kadhaa za vijana wa Mbwa wa geti.

Kitu ambacho askari wale hawakujua ni kuwa Temba ndie alikuwa kiongozi wao ,ikabaki siri ya Mina,Ziga na Temba mwenyewe.

Wakati kabah anataka kutoka nje tu akaukatana na mtu ambae hakutegemea

Zedi alikuwa kasimama wima mlangoni huku silaha ikiwa mkononi na alipomuona tu akaitupa na bila kuulizana ukaanza mkono wa adabu.

Ziga alikuwa kasi kuwahi kummkamata Kabah lakini akakuta rafiki yake akiwa anapambana na jasusi Kabah,yeye akabaki kuwa mtazamaji.

Mpambano ulikuwa ndani ya dakika tano tu lakini tayari Kabah alikuwa amevunjwa mkono na Zedi.

Zedi kwa hasira alizokuwa nazo akapaa hewani ili kummliza Kabah lakini kabla hajashuka Mina akaingia na kumpitia kwa kasi Kabah kisha akamtia pingu huku RPC Mabeyo akiingia pale na kuwapigia makofi huku akiwapongeza vijana kwa kazi waliofanya ndani ya muda mfupi sana.

Kabah alikaguliwa nyumba yake na kukutwa shehena ya dawa za kulevya na watu kadhaa waliokuwa mateka pale ndani.
***

Zedi,Ziga,Mina na Temba waliingia ndani ya nyumba waliokuwa wameweka hifadhi kwa muda na walichokutana nacho hawakukitarajia.

Tausi alikuwa amelala juu ya sofa huku povu likimtoka,mtoto nae alikuwa amekaa tu huku hajui kipi cha kufanya.

Zedi akamkimbilia mwanae,huku kwa mara ya kwanza Ziga na Mina wakilishuhudia chozi la mbabe yule.

Zedi hakuumizwa na kifo cha mkewe Zaidi aliumizwa na mwonekano wa mwanae.

Taratibu zikafanyika na mtoto wa Zedi akapelekwa soba.

****
Baada ya Wiki mbili ndani ya gereza la Isango kulitokea mauaji ya askari magereza zaidi ya hamsini huku wafungwa kadhaa wakitoroka akiwemo na Kabah,huku gereza likiachwa na maandishi makubwa MBWA WA GETI.

Taarifa hizi Zedi alizipata akiwa anamwogesha mwanae ahsubuhi huku Ziga na Mina wakizipokea taarifa hizi wakiwa ndani ya hoteli ya nyota tano huko Zanzibar.

“Karibu tena kiumeni,safari hii nakuua Kabah” alijisemea Zedi huku akilitizama kovu la mwanae tumboni.

MWISHO

Ahsanten sana kwa kuwa nami mwanzo hadi mwisho wa riwaya hii.
Yule mwenye kuhitaji kutoa wazo ama ushauri basi fanya hivyo.

Mwisho wa riwaya hii ni mwanzo wa riwaya nyingine tena ahsanten
 
Inapendeza sana...

Chapter closed...

Cc: mahondaw
 
Mkuu Kudo
Wasalaam
Riwaya zako ni nzuri sana,ushauri wangu ni kwamba huwa unakuwa na mwisho wenye mambo mengi sana kwa pamoja,yaani page moja yako inaweza kuwa page hata kumi kwa mtu meingine,una "kondensi" riwaya
Embu cheki hilo mkuu
Wasalaaam
Mweweso
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom