the_legend
JF-Expert Member
- Jan 14, 2019
- 1,612
- 7,110
- Thread starter
- #561
Usiwaze. Siwezi kuzichanganya na hii, kila moja itakua na uzi wakeKama unaanza hizo uweke uzi zake
the Legend☆
Usiwaze. Siwezi kuzichanganya na hii, kila moja itakua na uzi wakeKama unaanza hizo uweke uzi zake
Woyoooooo hapo kwenye ushindi wa simba yaani hapo acha nikupende tu mm




kesho lazima tuwanyooshe na huyo kibaraka wao ZaheraMsije kuchezeshwa .kinyantindinya...unyago wa kima ..kibwebwe mkia!kesho lazima tuwanyooshe na huyo kibaraka wao Zahera
the Legend☆
Lazima wanyookekesho lazima tuwanyooshe na huyo kibaraka wao Zahera
the Legend☆
Hahahaha, sijawahi kua na wasiwasi na Simba taifaMsije kuchezeshwa .kinyantindinya...unyago wa kima ..kibwebwe mkia!
Sent using Jamii Forums mobile app
Angalia msipigwe 5G zingineHahahaha, sijawahi kua na wasiwasi na Simba taifa
the Legend☆
Jiandae kisaikolojia...Hahahaha, sijawahi kua na wasiwasi na Simba taifa
the Legend☆
Hatimae Minja alifufuka bahariniRIWAYA : MKONO WA CHUMA
MTUNZI : ALEX KILEO
SEHEMU YA THELATHINI NA TANO.
___________________
ENDELEA..............
____________________
Dizonga alikisukuma kile kiti cha matairi mpaka nyuma ya hospital, kisha akachomoa bastola na kumuelekezea Tom usoni, kisha akatoa kichupa kidogo cha dawa kumpulizia Tom puani, Tom akazinduka na kuanza kupiga chafya mfululizo, ubongo ulipokaa sawa ndipo akagundua Kuna mtu mbele yake amemshikia bastola, Tom akashtuka na kutulia,
"nisikilize kwa umakini sana, mimi ni mbaya nimetumwa kukudhuru, ila nadhani muda wa kukudhuru bado haujafika, sasa tafuta njia yoyote huku nyuma ya hospitali, na utoroke, usikae tena mazingira ya huku hospital, na usimuamini mtu yeyote" Dizonga alimwambia Tom,
"wewe ndio mkuu wa polisi uliyenipigia simu?" Tom aliuliza kwa hofu,
"hapana, mimi sio mkuu wa polisi, wala sina uhusiano na mkuu wa polisi, ila mtu aliyefanya tupajue hapa ni mkuu wa polisi" Dizonga aliongea huku akirudishia bastola kiunoni,
"sawa, nashukuru kwa wema wako" Tom aliongea huku akiwa hamuamini kabisa mtu aliye mbele yake, alijua ndio wale wale wakina Ray Charles,
"kaka ondoka, usije ukafia humu, na usipite geti la mbele, kwa maana utanikuta tena mimi na sitokuonesha tena huruma kama ninaokuonesha sasa hivi" Dizonga aliongea na kuanza kurudi geti kubwa la mbele, alitembea kwa umakini mkubwa ili wenzake walioingia ndani ya wodi wasigundue kama aliondoka katika eneo alilopangiwa.
Dizonga alifika getini na kutoa simu yake, kisha akampigia mtu aliyemsevu kama "X soldier"
"kaka mkubwa" Dizonga aliongea baada ya mtu wa upande wa pili kupokea simu,
"niambie" Sauti ya upande wa pili iliyoonekana kama ya mtu mzee sana ilijibu,
"dogo nimemsaidia na kumpa mwanga namna ya kuondoka, akizembea atakuwa ametaka mwenyewe kujiua" Dizonga aliongea,
"sawa, umefanya vyema sana" Sauti ya upande wa pili iliongea,
"sawa, baadae basi" Dizonga aliongea,
"haya, kazi njema" Sauti ya upande wa pili ulijibu na kukata simu.
Dizonga akaendelea kuhesabu dakika tu huku akiwasubiri wenzake watoke wodini, aliwasubiri muda mrefu na hakuna kilichotokea. Mission walitakiwa waifanye ndani ya dakika kumi, lakini tayari dakika ishirini na tano zilikuwa zimeshakatika.
Dakika tano baadae, Dizonga alimshuhudia mkuu wa polisi akitoka ndani ya jengo la hospital huku akiwa na daktari, kuna kitu walikuwa wanaongea, waliongea kwa dakika mbili kisha wakaagana, mkuu wa polisi akaingia katika gari yake na kuondoka. Dizonga akamshuhudia daktari akija pale getini alipokuwepo, kisha akaingia katika kibanda cha mlinzi,
"Kuweni makini sana na watu wanaotoka ndani, inasemekana kuna mgonjwa ametoroka au ametoroshwa, bado tunafuatilia" Daktari aliongea na mlinzi ndani, ila Dizonga alisikia yale maelezo,
"sisi kazi yetu ni kufungua geti kwa ajili ya kuingia na kutoka magari, na kuruhusu watu kuingia kuona wagonjwa kwa muda sahihi, hilo suala la wagonjwa kutoroka ni jukumu la ulinzi wa ndani ya jengo" Mlinzi alisikika akijibu,
"sawa, ngoja ukweli ujulikane, walinzi wote mtashikwa, ndipo utajua nani mwenye jukumu la ndani au nje" Daktari aliongea huku akitoka nje ya kibanda cha walinzi, kisha mlinzi nae akatoka na kuangaza kushoto na kulia, Dizonga akajifanya kama anaongea na simu. Mlinzi alivyorudi ndani, Dizonga akarudisha simu mfukoni, na muda huo wale wenzake waliokuwa ndani ya jengo la hospital, walikuwa wakitoka nje huku nyuso zao zikionesha hazina furaha hata kidogo.
Dizonga akatangulia kutoka ndani na kuingia ndani ya gari, akamkuta mwenzao ambaye ni Dereva nae akishangaa
"mbona mmetumia muda mrefu" Dereva aliuliza,
"walioingia ndani ya jengo ndio wamechelewesha mchezo" Dizonga alijibu,
"wako wapi?" Dereva aliuliza,
"wanakuja" Dizonga alijibu na kipindi hicho wale wenzao wawili walikuwa wakitoka ndani ya geti la hospitali na moja kwa moja wakaingia katika gari,,
"vipi, imeshindikana?" Dizonga aliuliza,
"jamaa hatujamkuta katika ile wodi" Mmoja alijibu,
"Sasa si mngekagua mpaka vyooni" Dereva aliuliza,
"tumefanya hivyo na ndio maana tumechelewa" Mwingine alijibu,
"hospitali yote mmeamua?" Dizonga aliuliza,
"mzeebaba, tumekagua kila eneo na ndio tumetumia muda mrefu ndani, labda tukuulize wewe uliyesimama getini, hukumuona huyo dogo hakitoka? " Mmoja kati ya wale watu waliokuwa na mission ya ndani waliuliza,
"hakuna kitu kama hicho, mpaka gari ya mkuu wa polisi niliiona ilivyoingia na muda wa kutoka niliiona, aliingia ndani ya gari peke yake" Dizonga alijibu,
"huenda basi aliruhusiwa" Dereva aliongea,
"kama aliruhusiwa, mkuu wa polisi alifuata nini pale hospitali?" Dizonga aliuliza,
"Yule jamaa ameshakoswa koswa kuuawa mara mbili, naona hajiamini sasa hivi, kila anapokaa atakuwa anajichunga mwenyewe" Jamaa mwingine aliongea,
"tuondokeni sasa" Dereva aliongea,
"Rais tunaenda kumuambia nini" Mmoja kati yao aliuliza,
"tutamwambia ukweli tu, hakuna haja ya kumficha" Dizonga aliongea,
"sawa" Dereva aliongea na kuondoa gari.
***************
Siku iliyofuata saa mbili asubuhi, wale vijana wanne wa rais walikuwa katika ofisi ya Rais, mbele ya Rais,
"kwa hiyo mpaka mnaondoka hospital hamkuweza kugundua Tom yupo wapi?" Rais aliuliza huku akiandika andika katika karatasi zake mezani,
"ndio, huenda aliruhusiwa mapema kabla sisi hatujaingia pale" Kijana mmoja alijibu,
"au tuamini tu huyu dogo ana ngekewa, maana nyie mmekosa, pia Ray ndio hataki kabisa kumuua" Rais aliongea huku akiendelea kuandika,
"naamini endapo tutajua alipo kwa mara nyingine, hatutofanya kosa tena" Dizonga aliongea kwa utulivu,
"nani kajibu hivyo" Rais aliuliza huku akiwa bado anaandika,
"mimi, Dizonga" Dizonga alijibu huku mapigo ya moyo yakiongezeka,
"ooh, D, Sasa Kuna kazi moja nataka uifanye wewe. Hivi mmefuatilia na kujua kesi ya yule Dokta Smith inaendaje?" Rais aliuliza na kuinua kichwa,
"Leo inasikilizwa kwa mara mwisho, alafu watapanga siku ya hukumu" Kijana mmoja alijibu,
"tumechelewa, maana si itasikilizwa saa nne?" Rais aliongea na kumtazama yule kijana aliyejibu,
"ni saa kumi jioni" Kijana alijibu,
"basi sawa, sasa Dizonga itabidi uende ukaongee na Dokta Smith kabla ya hiyo saa kumi, mwambie unamsaidia kumtoa, ila kwa sharti moja tu, akusaidie kumtibu mgonjwa wako, sitaki ajue kama mimi nipo nyuma ya haya,
"sawa, je ataamini vipi mimi naweza kumtoa?" Dizonga aliuliza,
"akiuliza swali kama hilo, mwambie hata jioni hatoitwa mahakamani, badala yake muda wa yeye kuwa mahakamani, ndio muda ambao mkuu wa gereza atamtoa nje""Rais aliongea,
"sawa mkuu, je niende muda gani?" Dizonga aliuliza,
"Sasa hivi, rudi kwako na ukavae suti, huende kama mtu mwenye pesa, usiende kihuni huni, anaweza akagoma kukuamini,
"sawa mkuu" Dizonga alijibu,
"utaondoka na gari ya serikali, utachagua yoyote hapo nje, na Dereva nitakupatia" Rais aliongea,
"sawa mkuu" Dizonga alijibu na kisha akaaga, akatoka mpaka nje na kuchagua gari moja ya serikali iliyokuwepo ndani ya uzio wa Ikulu, kisha akaingia na baada ya dakika tano dereva akaja na kuingia, wakasalimiana na kisha Dizonga akamuelekeza anapoenda.
***********
Dokta Smith alikuwa amekaa ndani ya gereza huku mwili wake ukionekana umepungua tofauti na hapo hawali, ila hakuonekana mtu mwenye mawazo, alikuwa akiongea na kutaniana na wafungwa mbalimbali. Askari magereza akasimama mbele yake,
"Dokta Kuna mgeni wako" Askari magereza aliongea na kumfanya Dokta Smith ashangae, kwa maana tangu amehamishiwa gerezani hakuwahi kutembelewa,
"nani" Dokta Smith aliuliza,
"mimi hata simjui, ila inawezekana ni viongozi wa serikali, maana hata gari yake ina namba za serikali" Askari magereza aliongea na kufanya Dokta Smith ashangae zaidi, yaani kusikia kuwa huyo mgeni ni kiongozi wa serikali,
"sawa, twende" Dokta Smith aliongea na kisha akatangulizwa mbele na Askari akakaa kwa nyuma.
Walitembea na wakaingia katika ofisi moja ndani ya gereza, hapo Dokta Smith akazidi kushangaa zaidi, baada ya mlango wa ofisi kufunguliwa, Dokta Smith akamkuta ndani kijana mtanashati ndani ya suti bei mbaya, na mdomoni alikuwa na sigara kubwa kama wanazovutaga majambazi katika sinema za kizungu, alikuwa ni Dizonga.
Dokta Smith akabaki anatoa macho tu,
"kaa hapo, uongee nae" Askari magereza aliongea kisha akatoka nje, akamuacha Dokta Smith ndani akijiuliza huyu mtu ni nani na anataka nini,
"samahani, hii sigara huenda inakukera" Dizonga aliongea na kuitupa ile sigara chini, kisha akaikanyaga,
"hapana usijali" Dokta Smith aliongea na kutabasamu,.
"samahani sana kwa huu uvamizi wa ghafla, ila nimekuja hapa nataka nikusaidie, alafu na wewe unisaidie" Dizonga aliongea na kumuangalia Dokta Smith,
"wewe unanisaidiaje, Na mimi nakusaidiaje?" Dokta Smith aliuliza kwa umakini,
"mimi nitakupa msaada mdogo tu, wa kukutoa humu na kufuta kesi yako" Dizonga aliongea,
"na mimi nitakusaidiaje?" Dokta Smith aliuliza,
"msaada wako kwangu, ni kuwa mimi nina mgonjwa nahitaji unisaidie kumtibu, maana ana siku ya tatu leo hajaenda hospital" Dizonga aliongea
"kwanini hamumpeleki hospital?" Dokta Smith alihoji,.
"endapo utakubali kunisaidia, basi utajua sababu pindi utakapomuona mgonjwa mwenyewe" Dizonga aliongea,
"sawa, mimi nitakusaidia, nitajaribu kumtibu" Dokta Smith aliongea na kumfanya Dizonga atabasamu,
"sawa, acha niende, ila jiandae, baadae nakuja kukuchukua" Dizonga aliongea,
"itawezekama vipi wakati leo ni siku ya kusikiliza kesi yangu?" Dokta Smith aliuliza,
"muda huo unaotakiwa usikilize kesi, ndio muda ambao utaachiwa huru, jiamini Dokta" Dizonga aliongea huku akiinuka katika kiti na kumuacha Dokta Smith akimuangalia tu.
"baadae dokta" Dizonga aliongea huku akitoka nje na kupishana na Askari magereza akiingia ndani ya ile ofisi aliyetoka.
Dizonga alitembea kwa mbwembwe kama mtu mwenye wadhifa serikalini, alitembea na kuingia katika gari, kisha Dereva akaiondoa gari eneo lile la magereza.
*************
Mishale ya saa tisa unusu wakati wafungwa wakiitwa majina ili wapelekwe mahakamani, jina la Dokta Smith halikuitwa, hapo akaanza kuamini maneno ya mgeni aliyemtembelea nyakati za asubuhi.
Baada ya wafungwa walioitwa kuondoka na basi na kupelekwa mahakamani, akaja Askari magereza na kumuita Dokta Smith, akampeleka mpaka ofisi ya mkuu wa gereza, kisha akaonana na mkuu wa gereza, wakaongea mambo mawili matatu kuhusu uhuru atakaopewa, kisha Dokta Smith akaruhusiwa kutoka gerezan.
Alivyotoka tu nje ya mlango wa gereza, alimkuta Dizonga akimsubiri ndani ya gari, Dokta Smith akaenda moja kwa moja kuingia katika gari ile ya serikali,
"pole sana kwa maisha ya gerezani" Dizonga alimwambia Dokta Smith,
"asante" Dokta Smith aliongea,
"tunapitia kwanza duka la nguo, alafu kwa mgonjwa husika utaonana nae jioni" Dizonga aliongea,
"sawa" Dokta Smith alijibu.
Dereva aliendesha mpaka katikati ya mji katika maduka ya nguo na kisha akasimamisha gari nje ya duka kubwa la nguo,
"wewe ondoka tu, kazi yako imeshaisha" Dizonga alimwambia yule Dereva wa gari la serikali,
"sawa" Dereva alijibu na kisha Dizonga na Dokta Smith wakatelemka katika gari na kuingia katika duka la nguo.
Wakati Dokta Smith akichagua za kuvaa, Dizonga alikuwa anaongea na simu, alipigiwa na Rais,
"ndio mkuu" Dizonga aliongea,
"mpo wapi?" Rais aliuliza,
"tupo kwenye maduka ya nguo" Dizonga alijibu,
"Sasa itabidi uzunguke nae kwanza mpaka jioni, kwa maana huyu mwanamke tunataka kumuhamishia nyumbani kwa Ray Charles, ili huyo Dokta hasigundue kama nipo nyuma ya haya yote" Rais aliongea,
"kutokana na hali ya huyo dada si bora mngemuhamisha sasa hivi ili Dokta akaanze matibabu?" Dizonga aliuliza kwa unyenyekevu,
"ni kweli D, ila muda Kuna ugeni kutoka nje upo ikulu hapa, kwa hiyo upo ulinzi wa aina mbalimbali, kuna Kuna walinzi wa huu ugeni, na Kuna ulinzi wa kimataifa, ila tuna maongezi ya saa moja tu, yakiisha utajulishwa" Rais aliongea,
"sawa mkuu" Dizonga aliongea na Rais akakata simu.
Dizonga akakaa huku akifikiria atampeleka wapi Dokta Smith kwa muda huo, wazo likamjia,
"Dokta tayari umemaliza kuchagua?" Dizonga alimuuliza Dokta Smith,
"ndio mheshimiwa" Dokta Smith alijibu na kumfanya Dizonga atabasamu,
"twende sasa" Dizonga aliongea na kutangulia nje, kisha Dokta Smith alimfuata kwa nyuma.
Dizonga akakodi taxi, aliamua arudi nyumbani kwake huku akiwa na Dokta Smith, kwa maana nyumbani Dizonga alikuwa na mgonjwa wake.
Taxi ilitembea mpaka nje ya nyumba ya kifahari ambayo Dizonga ndipo alipokuwa anaishi, ni nyumba aliyopewa zawadi na Rais. Taxi ilisimama kisha Dizonga akatelemka na kumlipa Dereva taxi.
Dizonga akaingia ndani huku Dokta Smith akimfuata, walifika sebuleni na Dokta Smith akasalimiana na familia ya Dizonga, mke na watoto wawili wa kike,
"mgonjwa anaendeleaje" Dizonga alimuuliza mke wake,
"bado, mpeleke hospital, atatufia ndani" Mke wake aliongea kwa huruma,
"nimekuja na Dokta leo, atamtibu tu" Dizonga alijibu,
"Dokta Smith twende huku" Dizonga aliongea na kupiga hatua kuelekea upande wa vyumbani huku Dokta Smith akiwa nyuma yake.
Walienda na kuingia katika chumba kimoja cha mwisho kabisa, kilikuwa na ukubwa wa stoo,
"Karibu Dokta" Dizonga alimkaribisha dokta Smith huku akifungua mlango,
"asante" Dokta Smith alijibu huku macho yake yakimtazama mwanaume aliyekuwa amelala huku mgongo ukiwa juu na majeraha kadhaa yalionekana mgongoni mwake,
"X soldier, leo nimekuletea daktari" Dizonga aliongea huku akikaa pembeni ya yule mgonjwa,
"Daktari kutoka wapi?" Yule mgonjwa aliuliza huku akijigeuza ili amuone daktari. Mgonjwa alipojigeuza ndipo Dokta Smith nae akaweza kumuona vizuri mgonjwa mwenyewe, mgonjwa mwenyewe akatabasamu, tabasamu lake bado halikuzuia kuonesha maumivu aliyokuwa nayo,
"Karibu Dokta" Mgonjwa aliongea,
"asante, pole kwa kuumwa" Dokta Smith aliongea huku akimtazama mgonjwa yule ambaye hakuwa na jicho moja la upande wa kushoto, naam, yaani alikuwa chongo........
Nadhani mimi nimeshamjua mgonjwa, sijui nyinyi wasomaji wangu.
*********ITAENDELEA***********
the Legend☆

Barikiwa sn AnkooBaadhi ya wadau wameomba wakati tunaendelea na hii mkono wa chuma niweke pia riwaya zilizotangulia kabla ya hii.
Kimsingi kabla ya hii zilianza kuwepo 'memory card' na 'fumbo la utambuzi', baada ya hizo ndo ikafuata hii Mkono wa Chuma. That means hii mkono wa chuma ni muendelezo wa hizo za nyuma nlizotaja hapo, yani ni kama series flani hivi(memory cardfumbo la utambuzi
mkono wa chuma).
So nimefkiria wakati tunaendelea na hii ya sasa nijitahidi kuwawekea na hizo 'memory card' na kisha 'fumbo la utambuzi', ili muelewe vizuri yote yaliyojiri kabla ya mkono wa chuma, kama ishu za mikataba ya BQ ilipoanzia na kadhalika. Stay tuned...
the Legend☆
(sio zumo

Hahahahahahahaa
Sawa mzee, tubasubiri vituz...Nadhani Jumapili wakati tunaendelea kusherehekea ushindi wa Simba tutaanza na 'memory card'
the Legend☆
Nadhani majibu umeyapataJiandae kisaikolojia...
Au rahisisha kwa kuanza mazoezi ya kulia kabisa..
Simba naipinda ila wakiamua kujitoa fahamu.. ..wanajitoa kweli!
Sent using Jamii Forums mobile app
Jiandae kisaikolojia...
Au rahisisha kwa kuanza mazoezi ya kulia kabisa..
Simba naipinda ila wakiamua kujitoa fahamu.. ..wanajitoa kweli!
Sent using Jamii Forums mobile app





una la kuongeza mkuu?siusema simba hatoshinda na wewe nawe aaghrr...una la kuongeza mkuu?
the Legend☆
Hahahaha, nlisema sijawahi kua na wasiwasi na Simba kwa Mkapa..To be honest sijawahi kuona shangwe kama lile la jana uwanjani baada ya goli la pili tangu nizaliwesiusema simba hatoshinda na wewe nawe aaghrr...
kujiandaa kisaikolojia kwa michezo ni kawaida... au uliwahi hisi simba anaweza lazwa 5 bila??
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii hakuna kufanya mambo inapotolewa mpaka ipostiwe halafu mm sio chambo wako mfyuuuu


