swahiba Senior
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 2,478
- 3,630
Kimyaaaaaa,, Binafs nipo upande wa Martini nguzu Mzee wa hisia
Tayari mkuumkuu tunasubiri tuitafute alfajiri ,mie nimempenda kichaa aliye kazini
Mimi naileta kama ilivyo huko nilikoitoaTuambieni tulale au kuna chochote???halafu mbona mnakata fupi fupi sana??
KaribuNitarudi
Itaendelea leo mkuu mi nimecopy tu kama ilivyojumatano si jana mkuu au
pamoja sanaRIWAYA; MKANDA WA SIRI
MTUNZI; HALFANI SUDY
SIMU; 0674 395733
Sehemu Ya Tisa
Upande wa hali za kina Martin sasa zilikuwa nzuri. Walikuwa wamerejea katika hali zao za kawaida. Wakivuta hewa kama kawaida. Hakuna aliyeelewa nini kilichowatokea. Walienda katika viwanja vya Maisala wenyewe kwa hiari yao lakini walipelekwa hospitali na wasamaria wema bila hiari yao, wakiwa hawajitambui. Na sasa waliruhusiwa kutoka hospitali. Njiani walijadiliana kwa kina juu ya chanzo cha hali ile iliyowatokea.
"Hivi ni kitu gani kilitokea pale Maisala?" Richard alikuwa anamuuliza Martin kwa sauti yenye uchovu kana kwamba Martin alikuwa ameshuhudia kila kitu.
"Yaani hata mimi sielewi Rich....ila nahisi itakuwa tulivutishwa sumu iliyotufanya tupoteze fahamu" Martin alijibu huku akiweka wazi dukuduku lake.
"Inavyoonesha yule jamaa tuliyekuwa tunamfatilia hakuwa peke yake, alikuwa na mwenzake ama wenzake, bila shaka wakati sisi tunamfatilia nasi pia tulikuwa tunafatiliwa bila kujua..na huyo mwenzake au wenzake ndipo walipofanikiwa kutupaka au kutunusisha sumu kwa siri...na ndipo tukapoteza fahamu!"
"Nami naamini hivyo lakini kwa namna gani sasa inawezekana hiyo Rich, kwanini tulale wawili tu uwanja mzima tena kukiwa na umati wa watu..je wale wengine hiyo sumu ilikuwa haiwadhuru ama?"
"Hapo hata mimi napatwa na mashaka makubwa sana.."
"Unajua tumefanya makosa makubwa sana yaani..Tumempoteza Binunu, tumempoteza yule jamaa..na kosa kubwa zaidi ya yote tumepoteza mkanda, yaani mkanda hauko mikononi mwetu!" Richard aliongea kwa kulalama.
"Ila tusijilaumu sana, twende Maisala, sehemu tulikopoteza fahamu zetu ndipo sehemu tunapoweza pata sababu ya kupoteza fahamu zetu.."
"Daah sawa twe'nzetu"
Wakiwa njiani Richard alianzisha mjadala mpya.
"Hivi vipi Brown amewasili Bongo kutokea Moro?"
"Nilimpa kazi ya kwenda kumpokea yule mshkaji wetu wa bandarini, yule Mansour, lakini sijawasiliana nae bado"
"Nice kaka, usimpigie kwanza, ngoja tulimalize hili kwanza...maana Brown akisikia mkanda umepotea........"
"Patachimbika haki ya Mungu!"
Walipofika katika viwanja vya Maisala walikuta bado kuna umati mkubwa sana wa watu. Kina Martin safari hii walikuwa makini kupita kawaida, lakini pamoja na umakini wao na kujitahidi kutafuta sana lakini hawakufanikiwa kumuona Binunu wala yule jamaa. Walijaribu kuulizia kwa watu pale uwanjani, hawakupata lolote la maana, kila mtu alijibu sijui...sijui...sijui. Walichanganyikiwa walikuwa wamewapoteza watu wale muhimu sana...watu ambao wangeweza kuwa ni jibu juu ya mahali ulipo mkanda wa siri. Walitoka nje ya viwanja vya Maisala. Nje waliiona gari yao iliyokuwepo mahali palepale walipoiacha kabla ya kupotelewa na fahamu zao. Bila kusemashana maneno yoyote wala kudadisi waliingia ndani ya gari. Wakakaa. Richard alikuwa amekaa katika kiti cha dereva, na Martin alikaa katika kiti cha upande wa kulia, kiti cha abiria. Dakika zipatazo tatu walikuwa macho....na kuongea.
"Unakumbuka katika ‘OPS’ kule Arusha siku ile tuli--vyo--ingia ka-mbi--ni kwa wa-le jam....." Martin hakumalizia kusema alichotaka kusema. Mdomo wake ulikuwa mzito ghafla! Hali ilibadirika mle ndani ya gari, sasa majamaa walikuwa wanashindana na macho yao, macho yanataka kufumba kilazima, wao wanataka kufumbua kilazima. Ilikuwa tafrani!
'Ni nini hii Martin lakini....' Richard alijiona anasema kwa nguvu, lakini sauti haikufika hata katika sikio lake mwenyewe. Aliishia kutoa madenda tu, sauti ile ilisikiwa na ubongo wake tu. Kujua kama alikuwa anataka kuongea labda ni yale madenda yaliodondokea katika kava ya sukani ya gari, mdomo nao ulikuwa mzito! Haukuthubutu kutoa hata neno moja nje. Mashindano kati ya ubongo wao uliokuwa hautaki kuruhusu macho kufumba na macho yakiyotaka kujifumba uliendelea. Siku zote ubongo ndio huamrisha macho kufumba au kufumbua. Lakini leo macho hayakufata amri ya ile ya ubongo. Wakati ubongo ukitaka macho yasijifumbe, macho yalikuwa yanalazimisha kujifumba. Balaa!
Mpambano ule ulidumu kwa muda takribani wa dakika moja tu, na macho yakaibuka mshindi kwa mara ya kwanza katika maisha yake. Majamaa walilala usingizi mzito sana. Richard alikuwa kalalia sukani. Martin alikuwa kalalia kiti cha abiria. Kilichowalaza..... kwa maana ya chanzo cha mpambano ule, hakikujulikana!
Saa 6:09 P.M
Bandarini, Dar es salaam hali ilikuwa ya wasiwasi sana. Watu wengi walikuwa wameizunguka Range Rover Vogue moja ambayo ilianza kutoa harufu kali. Walivyoichunguza vizuri Range Rover ile waligundua kuwa kioo cha nyuma kilikuwa kimevunjika ama kimevunjwa. Hofu ya kuwa kuna kitu kibaya ndani ya ile gari ikawavaa. Haraka haraka Polisi wakapigiwa simu. Na nusu saa baadae Polisi walifika mahali pale kwa Land Rover yao nyeupe. Askari watano na bunduki zao aina ya SMG mkononi walishuka kabla hata ile Land Rover haijasimama vizuri. Polisi watatu walikuwa wanalizunguka lile gari. Huku bunduki zao zikiwa zimetangulizwa mbele, askari wawili ndio walikuwa wanaisogelea ile Range Rover kwa tahadhari kubwa. Polisi mmoja akiwa kavaa sare safi za jeshi la Polisi na kifimbo cheusi mkononi, na bunduki yake ikiwa inaning'inia begani huku yule mwengine akiwa nae amevaa sare za jeshi la Polisi lakini hakuwa na kifimbo kama yule mwenzake huku bunduki yake ilikuwa imara mkononi akiielekeza katika ile gari, waliisogelea kwa tahadhari kubwa sana. Njiani walikutana na upinzani wa harufu mbaya sana toka ndani ya Range Rover kila walivyokuwa wanaikaribia. Wakasimama kwa pamoja, wakavaa viziba pua vyeupe vilivyokuwa vinaning'inia shingoni mwao. Wakaendelea kupiga hatua kuelekea kwenye harufu kali baada ya kuridhika kuwa waliziziba vizuri pua zao. Askari yule asiye na kifimbo cheusi alifika pale dirishani. Akajipekua mfukoni na kutoa 'gloves' mbili, akazivaa katika mikono yake. Yule askari mwenye kifimbo cheusi akaitoa bunduki yake begani, akaishika imara mkononi. Akiielekeza mdomo wa bunduki garini. Alikuwa tayari kwa lolote! Askari asiyekuwa na kifimbo cheusi aliining'iniza bunduki yake begani. Sasa mikono yake yote ilikuwa huru. Akapeleka mkono wake wa kulia mlangoni, akijaribu kuuvuta mlango wa mbele wa dereva. Haukufunguka. Akapata wazo la kuchungulia ndani ya gari kupitia dirishani. Wazo ambalo alilipitisha katika halmashauri ya kichwa chake. Akitaka kufanya uamuzi sawa na alioufanya kijana Mansour na kupelekea kifo chake! Alivyotaka kuingiza tu, mwenzie akampa onyo.
"Hatari hiyo Afande hujui ndani kuna nini!" Yule askari asiye na fimbo nyeusi akarudisha kichwa chake kwa haraka! Askari wakarudi nyuma kidogo, ili kupata nafasi ya kufikiria namna mzuri ya kuufungua ule mlango wa gari.
"Funguo Malaya" Askari aliyeshika kifumbo cheusi alisema kwa kunong'ona, na sauti ile ilisikiwa vizuri na yule askari mwengine. Na alitekeleza.
Askari asiye na kifimbo cheusi akaenda haraka haraka kwenye gari yao iliyopaki kama meta thelathini kutokea pale kwenye Range Rover, huku yule askari mwenye kifimbo cheusi akibaki pale karibu na gari, yu imara na bunduki yake mkononi, masikio na macho yake yakiwa makini kuliko kawaida, yakisubiri mtikisiko wowote ule toka ndani ya ile gari autungue. Dakika moja baadae, askari asiye na kifimbo alirudi tena kwa mwendo wake uleule wa haraka, akiwa na funguo ndogo mkononi. Alienda moja kwa moja hadi katika mlango wa mbele wa Range Rover. Akiwa makini pasi na kawaida, huku yule askari mwenzie akimlinda kwa kutumia ile bunduki yake. Na midomo mengine ya bunduki tatu, za wale askari wengine zikiwa zimeelekezwa katika ile gari. Wananchi wakiwa umbali wa kama mita mia moja wakiwa makini, wanataka kuwa mashuhuda wa tukio lile. Askari asiye na kifimbo akapenyeza ile funguo malaya katika lile tundu la kupitisha funguo. Aliutekenya kidogo tu, mlango wa Range Rover Vogue ulifunguka! Pamoja na kile kiziba pua lakini ilipenya, alikaribishwa na harufu kali sana, askari asiye na kifimbo cheusi ambaye ndiye aliufungua mlango wa ile Range Rover alitanguliza mdomo wa SMG mbele huku mwili wake ukiwa nyuma. Tayari kuishambulia hatari yoyote atakayokutana nayo ndani ya Range Rover. Haikuwa kama walivyofikiria, hakukutana na hatari yoyote ya kuwashambulia, alikutana na hatari isiyoshambulia,maiti ya binadamu ikiwa imevimba vibaya sana, huku ikiwa imezungukwa na inzi wa kutosha! Kizungumkuti!
"Kuna maiti tu humu afande!" Askari asiye na kifimbo alimtaarifu mwenzio kwa sauti iliyotokea puani (nasal sound), hii ni kutokana na kile kiziba pua alichokitumia kuzibia pua yake.
"Hakuna kitu kingine chochote cha hatari?" Askari mwenye kifimbo cheusi nae aliuliza.
"Hapana afande, ni maiti tu"
Taratibu za kiusalama zikafuatwa. Na mwili wa wa ile maiti iliyokuwa imeanza kuharibika ukatolewa ndani ya gari. Vijana wa Bandarini walikuwa umbali wa mita mia moja tokea pale Range Rover Vogue ilipo, lakini waliona. Wengi wa vijana wale waliropokwa kwa sauti kali wakati mwili wa jamaa ukitolewa ndani ya gari.
"Mansoouuur!"
Maiti ya Mansour ikabebwa msobemsobe na kupelekwa hospitali. Na mara moja upelelezi wa sababu ya mauaji ya Mansour ulianza. Askari waliokabidhiwa upelelezi wa kifo kile cha kutatanisha ni walewale, askari mwenye kifimbo cheusi na mwenzie, askari asiye na kifimbo cheusi. Hatua ya kwanza walioichukua ni kuitafuta kadi ya gari. Lengo ni kumpata mmiliki wa gari ile. Walishaelezwa na vijana wa bandarini kwamba Mansour hakuwa na gari, kwa maana hiyo aliuwawa na kutelekezwa ndani ya gari. Kwanini auwawe? Ile gari ni ya nani? Je kuna uhusiano kati ya mwenye gari na ile maiti? Ili kuyajibu maswali hayo na mengine kadhaa yaliyowazungukakichwani mwa askari wale. Askari wakaamini ili wajue chanzo cha mauaji au mtu anayejua lolote kuhusu mauaji ya mtu yule ni kumtafuta mmiliki wa ile gari. Lazima atawapa mwanga wa kitu gani kilichotokea. Hawakupata shida. Nakala ya kadi ya gari waliikuta mlemle ndani ya gari!
"Mmiliki wa ile gari tulioikuta maiti anaitwa Martin Nguzu" Askari asiye na kifimbo alisema wakiwa ofisini. Huku mkononi akiwa ameshikilia nakala ya kadi ya gari.
"Martin Nguzu! Sio jina geni katika masikio yangu...nimelisikia wapi hiviiii?" Askari mwenye kifimbo aliuliza huku akikuna kichwa kujaribu kuvuta kumbukumbu.
"Mimi sijawahi kulisikia hili jina kwa kweli" askari asiye na kifimbo cheusi alisema.
"Hebu tuangalie katika database yetu ya wahalifu, kama tutalikuta hilo jina...ila jina lake si geni kabisa katika masikio yangu....Martin Nguzu..."
"Sawa Afande. Ngoja tuwasiliane na Mtunza kumbukumbu za Wahalifu tuone kama ataliona hilo jina?
" Nusu saa baadae majibu toka kwa Mtunza kumbukumbu za Wahalifu yalikuwa mezani kwao. Hakukuwa na mtu mwenye jina hilo katika orodha ndefu ya wahalifu waliokamatwa na walio katika orodha ya kutafutwa katika jeshi la Polisi nchini Tanzania.
"Itabidi twende TRA kupata maelezo zaidi ya mtu huyu...kwa kuwa hii gari imesajiliwa haitotupa shida sana" Askari mwenye kifimbo alitoa wazo.
"Sawa Afande, hakika kule tutapata mambo mengi muhimu kuhusu huyu mtu aitwaye Martin Nguzu"
Nje ya viwanja vya Maisala.....Zanzibar Martin na Richard walikuwa wamelala fofofo ndani ya gari. Hawakuwa wanajitambua kabisa, hawakujua jinsi hatari ikivyojitengeneza huko Dar es salaam kwa kasi kubwa sana ili isafiri na kwenda kumvaa Martin Zanzibar. Sumu aina ya Rox iliyokuwemo ndani ya gari lao iliwalaza kwa mara ya pili. Kumbe kabla Malkia hajaingia katika viwanja vya Maisala alianza kupulizia Rox ndani ya gari ile, kisha ndipo alienda ndani ya viwanja vya Maisala. Alifanya hivyo makusudi. Endapo angewakosa kuwapulizia ile sumu kule ndani ya uwanja, basi waje kukutana nayo ndani ya gari yao. Na Malkia alifanikiwa kwa asilimia mia...Rox iliwapata ndani, Rox imewapata nje...walikuwa na saa tatu zingine za kulala, huku kina Malkia wakiendelea na harakati za kutafuta hatma ya mkanda wa siri. Hivi vilikuwa vita vya akili, vilivyokuwa vinahitaji watu wenye akili kuvicheza, na Malkia alikuwa mwanamke wa kipemba aliyejaaliwa akili hizo, akili za VITA. Na ndomana Chifu mwenye akili aliamua kumuoa Malkia mwenye akili, kwakuwa Chifu siku zote alikuwa mtu wa vita na alikuwa anajua ya kwamba vita vyahitaji akili sana!
Sasa kwanini asimuoe mtu mwenye akili?
***
Askari mwenye kifimbo cheusi na askari asiye na kifimbo cheusi waliwasili katika makao makuu ya ofisi za TRA. Baada ya kufuata taratibu zote za kiofisi maaskari walipewa anuani ya mmiliki wa ile Range Rover Vogue, Martin Hisia, pamoja na namba yake ya simu. Askari walitoka nje na kuingia ndani ya gari yao, wakiwa na matumaini tele ya kufumbua utata wa kifo kile cha kitata. Askari mwenye kifimbo cheusi ndiye aliyechukua jukumu la kuipiga ile namba ya Martin.
Simu ya Martin iliita, ikakata, akaipiga tena, ikaitaa weee mpaka ikakata, akapiga tena matokeo yakawa yaleyale, akapiga tena na tena, lakini simu ya askari mwenye kifimbo cheusi haikupokelewa.
"Jamaa hapokei simu.." Askari mwenye kifimbo cheusi alisema huku akimwangalia mwenzake.
"Labda yupo mbali na simu, lakini la msingi namba yake inapatikana, anaweza kutupigia yeye atakapoikuta 'missed calls' katika simu yake, asipopiga tutampigia baada ya muda kidogo" Askari asiye na kifimbo cheusi alishauri.
"Ahaa wazo zuri, twende kwanza kituoni tuisubirie simu ya jamaa, tukiona kimya twende moja kwa moja nyumbani kwake"
"Sawa afande"
Waling'oa gari yao na kurejea kituoni.
Zanzibar bado wajanja wanausaka mkanda wa siri...Dar es salaam upelelezi wa kifo cha Mansour waanza huku mshukiwa namba moja akiwa ni Martin Hisia.. Bado fumbo halijafumbuka!! Kwa wanayoitaka yote riwaya hii inapatikana WhatsApp namba ya mwandishi ni 0674 395733 bei ni 3000 tu.
Good morning
Usirudie kufanya hivo tena mkuu unasumbua wanao tumia cmpamoja sana
Subiri ifikie ndio ushukuru huwa wanaishiaga njiani hawaAsante sana hadithi iko vizuri.tunasubiri muendelezo.
Ni ujinga ku-quote uzi mrefu hivi, unaweza comment tu bila ku-quote. Ni kero.pamoja sana