25phiri12
Senior Member
- Jun 19, 2021
- 120
- 93
- Thread starter
- #21
RIWAYA: MATEKA
MTUNZI: EMMANUEL PHIRI
NAMBA: 0758 195 890
(KIPANDE CHA KUMI)
Yalikuwa majira ya saa tatu usiku. Japokuwa ulikuwa wakati wa giza lakini mji uling`aa mataa kila kona. Giza lilipigwa kikumbo kizito na mwanga uliozalishwa na mataa ya barabarani, nyumba pamoja na vyombo vya moto vilivyokuwa vikitumiwa na raia waliokuwa wakijongea kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Mmoja wa watu waliofanikiwa kuufukuza mwanga kupitia chombo cha usafiri alikwa daktari Johnson, gari lake lilikuwa mwendo kasi kuelekea mtaa wa Bungero, mtaa alikuwa akiishi binti wa kiarabu, Nasrat Abdul al Aziz. Alihisi gari likimsaliti, japokuwa alikuwa mwendo kasi lakini alihisi akitembea kwa miguu. Alitamani gari lipae kama ndege lakini haikuwezekana. Alichukua simu yake ya mkononi kisha akampigia Nasrat Abdul al Aziz, simu iliita pasipo mafanikio. Hakuchoka, alipiga tena na tena lakini jibu halikubadilika. Hakuogopa kupata ajali alipokuwa akiendesha gari kwa mwendo kasi kwa mkono mmoja. Alirudisha simu mfukoni kisha mkono wa pili ukarudi katika usukani wa gari na safari ya kwenda kwa Nasrat Abdul al Aziz ikaendelea. Aliamini lazima amkute Nasrat Abdul al Aziz nyumbani kwake muda huo, mara nyingi Nasrat Abdul al Aziz huwa nyumbani kwake Bungero muda kama huo. Mara chache huwa katika ngome yake. Mara chache hizo ni mpaka itokee dharura iliyomuhitaji yeye mwenyewe, kwa sababu dharura zingine alimwachia Zimwi akabiliane nao. Mungu siyo Athumani, daktari Johnson alifanikiwa kufika katika nyumba ya Nasrat Abdul al Aziz. Alipiga honi mara kadhaa pasipo mafanikio. Akachukua simu yake akampigia kwa mara nyingine, mara hiyo simu ilipokelewa
“Dogo mbona hupokei simu?”
Siku zote alizoea kumuita dogo tangu enzi za uhai wa mzee Abdul al Aziz. Japokuwa Nasrat Abdul al Aziz alikuwa ndiye bosi wake lakini haikubadilisha jina la dogo, wala Nasrat Abdul al Aziz hakuumizwa wala kuchukizwa na jina hilo kwa sababu aliamini lilikuwa likimuenzi baba yake. Mara zote aliitika, na mara chache daktari yule alipomwita jina lake (Nasrat) au jina la heshima (bosi) Nasrat Abdul al Aziz alikataa kuitika na kumwambia amuite jina alilozoea kumuita tangu enzi za utoto wao. Walicheka na kundelea na shughuli iliyowakutanisha. Nasrat Abdul al Aziz alijibu hoja ya daktari Johnson
“Samahani sana daktari, nilikuwa bafuni naoga. Samahani sana”
Nasrat Abdul al Aziz alimuheshimu sana daktari Johnson, heshima hiyo ndiyo iliyoongeza upendo wa daktari kwa Nasrat Abdul al Aziz. Daktari Johnson alimwambia Nasrat kuwa yupo nje ya geti la nyumba yake, anahitaji geti lifunguliwe ili aingie. Kabla Nasrat Abdul al Aziz ajajibu kauli ya daktari Johnson alitazama saa ya ukutani ikamuonesha ilikuwa saa tatu usiku. Alishangaa kusikia daktari yupo nje ya nyumba yake muda huo, haikuwa kawaida hata kidogo. Alijibu kauli ya daktari
“Kuna kheri kweli? Au umeniongezea nguvu uliyoniambia?”
Daktari alielewa maana ya maswali ya Nasrat Abdul al Aziz kwa sababu siku iliyopita alimwambia afanye juu chini kuboresha ulinzi katika nyumba yake, alimwambia kauli hiyo baada ya kusikia Derrick Edward amekamatwa na watu wasiojulikana. Daktari Johnson alihofia usalama wa Nasrat Abdul al Aziz. Alijua Nasrat Abdul al Aziz akiongeza ulinzi katika nyumba yake atakuwa salama kwa kiasi kikubwa. Daktrari Johnson alihisi akicheleweshwa kuingia ndani, alikuwa na ujumbe mzito wa kumueleza Nasrat Abdul al Aziz. Japokuwa alikuwa ameshafika katika nyumba ya Nasrat Abdul al Aziz na angeweza kusubiri mpaka kuingia ndani ndiyo aongee dhamira ya kufika usiku ule, lakini hakuwa tayari kusubiri. Alianza kuongea kupitia simu. Alimwambia binti wa Kiarabu
“Leo nina majibu kuhusu Derrick, hakika kwa alipo Derrick hutakiwi kuishi katika makazi yako. Yakupasa kuishi katika ngome yako. Kwakweli yakupasa kuishi kule ili uweze kulindwa na kujidhatiti katika njia za kumkomboa mpenzi wako”
Kauli ya daktari Johnson ilisababisha mwili wa Nasrat Abdul al Aziz usisimke kwa hofu baada ya kusikia habari za Derrick Edward, hasa aliposikia kauli iliyomwambia suala la kumkomboa mpenzi wake. Alihisi kama alisikia vibaya lakini akili yake iliyokamilika ilimuhakikishia kuwa alisikia vizuri kwa asilimia mia moja. Alijiuliza
“Nani aliyemteka Derrick? Eti mpenzi wangu! Kuna mapenzi hapo, mapenzi na mpelelezi!”
Akili ya Nasrat Abdul al Aziz ilikataa kabisa kuhusu suala la mapenzi na askari mpelelezi aliyempenda lakini akili hiyo hiyo ikamkumbusha juu ya mtoto wa askari huyo aliye tumboni kwake. Kichwa kikawaka moto. Sasa aliamini alikuwa kwenye mtego mgumu katika maisha yake, alishindwa atetee upande gani. Alikumbuka kauli ya daktari Johnson, kauli iliyohitaji kufunguliwa geti la nyumba hiyo ili aingie kumpa taarifa kamili kuhusu Derrick Edward na watekaji. Taratibu alipiga hatua kuelekea nje ya nyumba yake, alifika getini kisha akafungua. Mwili ulikuwa mkakamavu ukichukua maamuzi lakini akili ilielemewa kwa mzigo mzito wa mawazo. Alifungua mlango wa geti lakini aliendelea kukaa katikati ya mlango huo, kitendo kile kilisababisha daktari Johnson kushindwa kuingiza gari ndani ya geti hilo. Siyo kwamba Nasrat Abdul al Aziz alipenda au alijua kama amemzuia daktari Johnson, hapana, alisimama njiani pasipo kujua. Daktari Johnson alimtazama Nasrat Abdul al Aziz akaelewa alikuwa mbali sana kimawazo, alikuwa dunia nyingine tena dunia iliyo mbali na upeo wa macho yake. Daktari Johnson alipiga honi, honi ilimshitua Nasrat Abdul al Aziz na kumrudisha katika dunia yake halisi. Nasrat Abdul al Aziz alielewa maana ya honi ya daktari Johnson, alisogea pembeni kuruhusu gari kuingia. Ndivyo ilivyokuwa, daktari Johnson aliingiza gari lake kisha akaliegesha sehemu ya maegesho, sehemu ambayo Nasrat Abdul al Aziz huegesha magari yake.
Baada ya tukio lile waliongozana mpaka sebuleni wakakaa kwenye viti vya sofa, hapo ndipo ufafanuzi ulipotolewa. Daktari Johnson alimsimulia Nasrat Abdul al Aziz kuwa Derrick Edward yupo mikononi mwa Amani Collence, hakuishia hapo bali alifafanua zaidi kuwa hali aliyomkuta nayo Derrick Edward ilieleza wazi kuwa alipigwa sana mpaka akapoteza fahamu. Walimpasua sehemu nyingi za mwili wake hasa kichwani wakasababisha apoteze damu nyingi. Daktari Johnson hakuishia hapo bali alifafanua namna alivyochukua sampuli ya damu ya Derrick Edward na kuondoka nayo kwenda kuipima katika hospitali yake, alipofahamu grupu la damu yake akarudi katika ngome ya Amani Collence na kumuongezea damu. Alifafanua zaidi kuwa alikubaliana na Amani Collence atakuwa akienda kuangalia maendeleo ya Derrick Edward kila asubuhi na usiku mpaka atakapopata nafuu au kupona kabisa. Ufafanuzi wa daktari Johnson ulimpa picha kamili Nasrat Abdul al Aziz. Aliamini Amani Collence ameanzisha vita aliyopanga siku nyingi.
Suala la Derrick Edward kukamatwa halikumuumiza Nasrat Abdul al Aziz kwa sababu Derrick Edward alikuwa adui yake kipindi hicho, kilichompa hofu aliamini Derrick Edward alikamatwa kwa ajili yake hivyo basi aliamini lengo kuu la Amani Collence siyo Derrick Edward bali ni yeye. Alifikiria hivyo kwa sababu aliamini Amani Collence hajamkamata Derrick Edward kwa kigezo cha kuwa askari mpelelezi, alijihakikishia kuwa hiyo haikuwa sababu kwa sababu Amani Collence alikuwa afahamu suala hilo. Kichwa kilimuuma sana Nasrat Abdul al Aziz. Akili ikamwambia lazima amuue Derrick Edward ili awe salama. Kwake Derrick Edward alikuwa adui mkubwa kuliko Amani Collence, aliamini Derrick Edward akiwa hai anaweza kumsumbua katika kazi zake kwa sababu askari na muuza madawa ya kulevya hawawezi kukaa zizi moja, vile vile aliamini suala la Derrick Edward kuwa hai akiwa katika ngome ya Amani Collence ni tishio la usalama wake na siri zake. Aliamini Derrick Edward anaweza kutoa taarifa zake za namna yoyote kwa Amani Collence, taarifa zinazoweza kuwa chanzo cha kutekwa au kuuliwa na kundi hilo. Aliona maamuzi ya kumuua Derrick Edward yalikuwa sahihi kwa asilimia mia moja, lakini moyo ulikataa baada ya kufikiria kiumbe kilichokuwa tumboni kwake. Alifikiria namna ya kumuua baba wa mwanae. Alijiuliza swali kichwani kwake
“Nitamwambia nini mwanangu akiwa mkubwa? Hivi nitakuwa na ujasiri wa kumwambia nilimua baba yake kwa sababu alikuwa adui yangu?”
Alikosa jibu la swali lake, lakini hakubadilisha mawazo ya kwanza. Aliamini alichopanga awali ndicho sahihi. Lazima aondoe maisha ya Derrick Edward ili ajiweka mazingira salama. Nasrat Abdul al Aziz alimtazama vizuri daktari Johnson aliyekuwa pembeni yake akichezea simu kisha akatabasamu, akainuka akachukua jagi la maji lililokuwa juu ya meza akamimina katika glasi akanywa fundo tatu. Akarudisha glasi mezani. Akatabasamu kwa mara nyingine kisha akamwambia daktari Johnson
“Yatupasa kuchukua maamuzi magumu, yatupasa kuondoa maisha ya Derrick haraka iwezekanavyo”
Kauli ya Nasrat Abdul al Aziz ilizua utata katika kichwa cha daktari Johnson, kauli ile ilimaanisha daktari Johnson achukue jukumu la kumuua Derrick Edward kwa sababu yeye pekee ndiye aliyekuwa na idhini ya kuingia na kutoka katika ngome ngumu iliyo chini ya mtukutu Amani Collence. Japokuwa daktari Johnson alikuwa bega kwa bega na Nasrat Abdul al Aziz lakini katika suala la kumuua Derrick Edward aliingiwa na hofu. Alijua lazima Amani Collence atabaini na atakuwa amejiweka wazi dhidi ya maadui zake. Kifo kingekuwa halali yake
“Unamaanisha nimuue Derrick?”
Nasrat Abdul al Aziz alitikisa kichwa juu chini akimaanisha ndicho alichomaanisha. Daktari Johnson aliinamisha kichwa chini kisha akakiinua, akamkazia macho mrembo wa Kiarabu kisha akamwambia
“Unafikiri itakuwaje endapo wakibaini kuwa nahusika na suala hilo?”
Nasrat Abdul al Aziz alicheka kwa sauti, kicheko chake kilimaanisha aliulizwa swali la kitoto. Alimjibu daktari Johnson kwa bashasha ya hali ya juu
“Hakuna atakayeweza kukugusa ukiwa katika himaya yangu, nafikiri unaelewa nguvu ya kundi langu. Nafikiri unajua kila kitu”
Daktari Johnson hakuwa na swali lolote, aliafiki kauli ya Nasrat Abdul al Aziz. Mpango wa kuumua Derrick Edward uliiva, waliafikiana daktari Johnson akienda kumuangalia Derrick Edward asubuhi ya siku inayofuata lazima atimize kazi ya mauaji. Katika makubaliana yao, Nasrat Abdul al Aziz alimwambia daktari Johnson kuwa kabla hajaondoa uhai wa Derrick Edward amfahamishe kuwa ana kiumbe chake katika tumbo la Nasrat Abdul al Aziz, lazima Derrick ajue kama ana mimba. Nasrat Abdul al Aziz alimwambia daktari Johnson suala hilo kwa sababu aliamini ni jambo la kheri Derrick Edward kufahamu juu ya mtoto wake aliye njia kuingia katika uso wa dunia.
Ndege wa angani walisikika wakipiga kelele za kuikaribisha siku mpya, hakika ilikuwa siku mpya haswa, tarehe ya jana haikuwa tarehe ya siku hiyo. Walitoka tawi moja na kuhamia tawi lingine, furaha waliyokuwa nayo haikuwa kifani. Furaha ya ndege hao ilikuwa tofauti sana na mioyo ya watu wengi, watu wengi hawakuwa na furaha hata kigodo, walikuwa kwenye mawazo mazito ya kufanya mauaji ya kijana mbichi aliye mikononi mwa Amani Collence. Ilikuwa imefika asubuhi iliyoandaliwa kuondoa maisha ya Derrick Edward, kila mpango ulioandaliwa ulikuwa ukienda kama ulivyopangwa. Dokta Johnson alikuwa akipiga hatua ndani ya ngome ya Amani Collence akielekea katika chumba alicholazwa Derrick Edward, akili yake iliwaza kuuwa na siyo kutibu. Siku hiyo alipanga kuisaliti kazi yake, kazi aliyoifanya miaka mingi ya kuokoa maisha ya watu kupitia taaluma yake. Siku hiyo alikuwa tayari kuuwa kwa kutumia sumu aina ya ‘Strychinine’. Sumu hiyo hupatikana kwenye mmea uitwao ‘Dog Button Plant’, kitaalamu mmea huo hufahamika kama ‘Strychnos nux – vomica’.
Mmea huo huzalisha sumu kali sana ambayo hushambulia misuli ya mwili mzima, hufanya misuli yote ya mwili wa binadamu kukakamaa sana na kupelekea kifo baada ya masaa mawili mpaka matatu. Mmea unaozalisha sumu hiyo hupatikana bara la Asia katika nchi za India, Sri Lanka, Australia na baadhi ya mataifa mengine yanayopatikana kwenye bara hilo. Sumu ya ‘Strychnine’ ni chungu na isiyo na rangi ambayo huweza kutengenezwa katika mfumo wa hewa (breathed in) au kama poda inayoweza kuchanganywa katika kimiminika na kuchomwa mtu katika mshipa (intravenously). Sumu hiyo ina nguvu sana kwa sababu hata kiasi kidogo sana hutosha kuondoa maisha ya watu. Mtu anayechomwa au kuvuta suu hiyo humchukua robo saa mpaka saa moja kuonesha dalili za kuathirika.
Daktari Johnson aliingia katika chumba alicholazwa Derrick Edward, alimkuta akiwa macho wazi. Suala lile lilimaanisha fahamu zake zilirudi mahala pake, alitabasamu usoni lakini moyoni alikuwa na hofu. Alitamani amkute akiwa amelala fofofo ili amchome sumu ya ‘Strychnine’ kwa urahisi pasipo kuulizwa maswali yoyote na mgonjwa huyo. Kwa upande wa pili suala la kumkuta macho Derrick Edward ilikuwa hatua nzuri ya kutimiza kazi aliyopewa, kazi ya kumfahamisha kuwa Nasrat Abdul al Aziz alikuwa ana ujauzito wake. Derrick Edward alikuwa peke yake chumbani, hapakuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuharibu mpango wa daktari Johnson. Ilikuwa furaha kwake. Daktari Johnson alifika mbele ya Derrick Edward kisha akamsalimia, Derrick Edward aliitika kwa shida sana. Kipindi Derrick Edward akiitika salamu ya daktari Johnson akilini alikuwa akiwaza wapi alipowahi kumuona mtu huyo, haikuwa sura ngeni hata kidogo. Aliumiza kichwa, kumbukumbu ikamjia kuwa alishawahi kumuona daktari huyo katika makazi ya Nasrat Abdul al Aziz. Kichwa kilimuuma zaidi, akashindwa kuelewa daktari yule anafanyaje kazi kwa mabwana wawili wenye chuki kati yao. Aliamini kuna siri nzito iliyojificha. Ghafla alishitushwa na kauli ya daktari Johnson
“Wajionaje na hali kijana?”
Derrick Edward alijibu kuwa anajisikia vizuri lakini kichwa na mbavu vinauma sana. Daktari Johnson alielewa sababu ya hali hiyo, alielewa kipigo alichokipata kilisababisha hali hiyo. Hakujali jibu la Derrick Edward, yeye alikuwa tayari kutimiza kazi iliyompeleka mahali pale, kazi ya kuondoa maisha ya Derrick Edward. Daktari Johnson alimkazia macho Derrick Edward kisha akamwambia
“Sikiliza kwa makini kijana, nina habari njema toka kwa Nasrat”
Kauli ya daktari Johnson ilimshangaza sana Derrick Edward, alishangaa kusikia kuwa daktari huyo alikuwa na habari njema kutoka kwa Nasrat Abdul al Aziz. Akili ya Derrick Edward ilienda mbali sana. Aliamini hakuwa salama hata kidogo, kauli ile ilimaanisha kifo mbele yake, aliamini Nasrat Abdul al Aziz alishafahamu kama yeye ni polisi mpelelezi hivyo basi lazima afanye mpango wa kumuua kabla ya kupambana na maadui wengine. Alitamani apige kelele za kuomba msaada kutoka kwa majambazi lakini mwili ulikataa, maumivu makali yalisambaa ghafla toka kidoleni mpaka utosini. Mapigo ya moyo yakaongezeka maradufu, macho yakamtoka pima. Derrick Edward aliamini hawezi kukwepa kifo kilichokuwa mbele yake. Alimtazama daktari Johnson kwa jicho la hasira kisha akaongea kwa tabu sana
“Coward! Today I`ll be dead, tomorrow is your time” (Mwoga! Leo nitakufa, kesho ni wakati wako)
Ilikuwa kauli ya kishujaa, kauli iliyomaanisha hakuogopa kuuliwa wala hakuogopa kifo. Kauli yake haikubadilisha mawazo ya daktari Johnson, daktari Johnson alikuwa tayari kutimiza kazi aliyopewa na Nasrat Abdul al Aziz. Alitabasamu kama mtu aliyefurahishwa na kauli ya Derrick Edward lakini tabasamu lake halikuwa na uhalisia wa aina yoyote, alijaribu kuukwepa ukweli uliotamkwa na mgonjwa, ukweli uliomaanisha kuwa alikuwa muoga. Hakika aliuona uwoga wake, uwoga wa kutimiza kauli za magaidi kuliko kufanya kazi zake. Aliendelea kutabasamu kinafiki, akakaa katika kiti alicholala Derrick Edward kisha akavua begi dogo lililokuwa mgongoni. Hakutaka kujibu kauli ya Derrick Edward kwa sababu alihofia kuharibu kila kitu, yeye alihitaji kutimiza kazi aliyopewa. Alikumbuka msisitizo wa Nasrat Abdul al Aziz, msisitizo wa kumwambia Derrick Edward kuhusu mtoto wake aliye tumboni. Daktari Johnson alimshika mkono Derrick Edward akauchezesha chezesa juu chini, Derrick Edward alilalamika kuumia kwa kitendo kile. Mwili wa Derrick Edward ulikuwa kama donda, ulimuuma sana kila uliposumbuliwa. Daktari Johnson aliurudisha mkono wa Derrick Edward mahali pake.
Siyo kwamba daktari Johnson alishika mkono wa Derrick Edward na kuuchezesha chezesha bila sababu, hapana, bali kipindi alipoushika na kuuinua macho yake yalikuwa makini kuangalia misuli ya Derrick Edward inayopatikana kwenye mkono ule, alikuwa akiangalia msuli upi autumie kupitisha dawa yake. Hakuna msuli aliouona, misuli yote ilikuwa imesinyaa kabisa. Misuli ilirudi ndani zaidi. Suala hilo halikumuumiza kichwa daktari Johnson, alijisemea moyoni kuwa ataichanganya sumu katika dripu ya maji aliyopanga kumuwekea mgonjwa wake. Hakuona sababu ya kushindwa kutimiza zoezi lake. Alitabasamu kwa mara nyingine kisha akamkazia macho Derrick Edward, akamwambia
“Sikiliza kijana, nilikwambia nina habari njema kutoka kwa Nasrat lakini kabla sijakwambia habari yenyewe ukaanza kuongea mambo ya ajabu. Mimi ni mgeni mwema kwako, nimetumwa na Nasrat nijaribu kuokoa maisha yako, lakini jambo la msingi unalotakiwa kujua ni kwamba Nasrat Abdul al Aziz ana ujauzito wako”
Ilikuwa kauli ya kumshangaza sana Derrick Edward, alimkazia macho daktari Johnson kama mtu aliyemwambia hajaelewa chochote alichomwambia lakini haikumaanisha chochote. Daktari Johnson aliendelea kutoa ufafanuzi wa kauli yake, ufafanuzi ulioendelea kumshangaza na kumstaajabisha Derrick Edward
“Nasrat anakupenda sana ndiyo maana kanituma nije kutafuta njia ya kuokoa maisha yako, nipo katika njia hiyo na nina uhakika lazima njia hiyo ifanikiwe. Baada ya masaa mawili tutakuwa nje ya jumba hili, namaanisha utakuwa kwa Nasrat”
Kauli ya daktari Johnson ilikuwa na maana tofauti sana, hakumaanisha kuwa Derrick Edward ataonana na mpenzi wake baada ya masaa mawili, hapana, bali iliamini baada ya masaa hayo lazima Derrick Edward atakuwa maiti baada ya kushambuliwa na sumu ya ‘Strychnine’. Derrick Edward aliendelea kumkazia macho daktari Johnson huku akilini akiendelea kufikiria kauli aliyoambiwa kuhusu ujauzito wa Nasrat Abdul al Aziz, alifikiria uadui ulioibuka kati yake na Nasrat Abdul al Aziz akaishiwa nguvu kabisa.
Derrick Edward hakuwa mjinga wa kuamini maneno ya daktari Johnson kuwa eti Nasrat Abdul al Aziz amemtuma kumuokoa toka kwenye mikono ya Amani Collence, aliamini kuwa siri ipo katikati. Aliamini siri hiyo itakuwa imezungukwa na kauli ya kifo, aliamini lazima auliwe japokuwa Nasrat Abdul al Aziz alikuwa na ujauzito wake. Derrick Edward alikumbuka kauli aliyowahi kuambiwa na Nasrat Abdul al Aziz kipindi mapenzi yao yalipokuwa moto, aliwahi kumwambia
“Huwa sipendi kumficha mtu kitu halisi anachotakiwa kujua, hata kama mtu huyo yupo hatua ya mwisho ya maisha yake. Lazima nifanye juu chini ajue”
Derrick Edward alitabasamu, sasa aliamini kauli hiyo ilikuwa na maana kubwa kwake siku hiyo. Aliamini Nasrat Abdul al Aziz alimtuma daktari huyo amfahamishe kuhusu ujauzito wake lakini kumfahamisha huko siyo sababu ya kuokoa maisha yake. Alielewa lazima wampoteze. Derrick Edward akamfikiria mtoto wake aliye tumboni mwa adui yake, moyo ulimuuma sana endapo akiuliwa na kumuacha mwanae katika sura ya dunia. Alijisemea moyoni
“Mungu niokoe kijana wako”
Machozi yalitengeneza mifereji katika mashavu yake, hakutoa sauti ya kilio lakini kilio kilikuwa moyoni, kilio kilimpeleka mbali sana na kumkumbusha maisha aliyopitia. Machozi yaliendelea kutiririka kama maji yateremkayo bondeni kila alipokumbuka maisha yake. Alikumbuka kauli ya shangazi yake, kauli aliyoapa kuiishi nayo mpaka siku ya mwisho ya maisha yake. Machozi yakaendelea kutiririka kama maji. Kilikuwa kitendo cha kustaajabisha na kushangaza kwa daktari Johnson, lakini aliapa kutokurudi nyuma, aliapa kutimiza kazi ya Nasrat Abdul al Aziz.
ITAENDELEA