Girland
JF-Expert Member
- Jan 24, 2016
- 1,824
- 2,841
DEDICATED TO IBRA87 RIP, Inspired by true story.
UTANGULIZI
Katika maisha mapambano hayaepukiki,Wakati wa kutunga mimba mbegu moja ya kiume hupambana na zingine milioni 45 kurutubisha yai moja,hata wakati wa kuzaliwa kiumbe hiki hupambana na mazingira mapya ya makazi yaliyo tofauti natumboni alimoishi kwa miezi tisa.Achilia mbali mapambano ya madaraka,ya vikundi vya magaidi na serikali,ya ndugu ya fikra na namna nyingine yoyote......Hii inathibitisha kwamba uwapo duniani huna budi kupambana kwa hiari au kwa lazima maana ndiyo njia pekee ya kuishi ,Lakini ni upi mtazamo wetu katika mapambano haya karibu ufuatane namimi.........
BAGAMOYO-PWANI
Hali ya hewa mahali hapa ilikuwa ya utulivu kabisa,jua lilikuwa likiendelea kukusanya makali yake,Ilikuwa ni asubuhi nyingine,Pilika zilikuwepo za hapa na pale za kujitafutia riziki ni kijana huyu pekee aliyekuwa kalala muda huu,si kwa sababu ya uvivu au kukosa kazi HAPANA
Alikuwa na mawazo,
Mawazo yaliyompelekea kutoka Nyumbani kwake maeneo ya Kinyerezi hadi hapa mjini Bagamoyo usiku wa manane.Kijana huyu aliyepitia mitihani mbalimbali maishani hakutegemea kwamba mawazo ya aina hii yangemzuia kwenda kazini kwake,Sasa aliiangalia tena saa yake ya mkononi ,09:45 Ilionyesha ,ndipo akagundua alikuwa amekaa mahali hapo zaidi ya saa 10 bila ya usingizi,ALIKESHA,akashangaa,akajaribu kujilaza kitandani apate japo usingizi kidogo ila akagutuliwa na sauti ya mhudumu aliyekuwa anataka kufanya usafi,akaanza kujiuliza maswali,au pengine kujilaumu kwa kilichotokea lakini akatamani iwe ni ndoto ,Aliwaza akawazua lakini hakupata majibu akaishika simu yake ya mkononi ndipo akagundua kuwa simu 25,meseji 10,na Email 9 zilizohitaji majibu kutoka kwa wateja wake,Alihitaji huruma kijana huyu ambaye wiki iliyopita alishinda tuzo ya kijana anayefanya vizuri katika sekta ya mitindo na ubunifu wa mavazi
OFISINI-TABATA SEGEREA
Hapo ndipo ilipokuwa ofisi ya kijana huyu,kijana wa miaka ishirini na tatu,mrefu wa wastani ,maji ya kunde kwa mwonekano ,hapa alikuwa ni mmiliki na mstendaji mkuu wa duka hili maarufu la ushonaji wa nguo.Alishona nguo za kiume na kike na hata watoto ,lilikuwa duka maarufu na wateja wengi waliamini na kuzipenda kazi zake.Leo wafanyakazi wake walikuwa tayari ofisini kama ilivyo kawaida lakini kijana huyu hakuwepo,walijaribu kumpigia lakini simu yake haikuwa ikipokelewa,Walianza kushauriana, Labda atakuwa kasafiri fundi mmoja akauliza,
"Hapana" akajibu Irene ,msaidizi wa kijana huyu anayepanga ratiba zake za siku na kusaidia mawazo ya kuiendesha biashara hii,Jana tulikuwa naye na alikuwa salama kabisa itakuwqa kapatwa na nini waliendelea kujiuliza.Mjumbe mmwingine katika kikao hicho kisicho rasmi akauliza,Irene jaribu kuwapigia marafiki zake,MMMMH,aliguna Irene rafiki yake ninayemfahamu ni mmoja tu na anafanyakazi benki kuu.Alipiga simu haikupokelewa,
Wafanyakazi wote 12 wa duka hili walibaki nje ya duka lao la ushonaji wasijue la kufanya wakapata wazo la kutoa taarifa polisi,Lakini wakati huu wakapokea simu kutoka kwa kijana huyu ambaye kwa ofisi zingine anaitwa BOSS jina ambalo kijana huyu alikataa kuitwa na badala yake kumuita kwa jina lake,NICKSON, naam,au kwa ufupi Nick ,alipopokea tofauti na siku zingine alimuita Irene na kutoa maelekezo.
"IRENE,utakaimu madaraka hapo ofisini hakikisha unafanya shughuli zote hadi hapo nitakapokwambia,kazi ziendelee kama kawaida na kama una tatizo lolote utanifahamisha"
Lakini Nick ukowapi,hakujibiwa swali lile na badala yake alishuhudia simu ikikatwa akabaki na mshangao.
**************************************************************************************
Kijana aliamka na lindi la mawazo aliyafikiria maisha yake ,lakini zaidi aliyafikiria maisha yake bila uhai na shida watakaozipata wafanyakazi wake akiondoka ,akalia,naam Mwanaume akilia kuna jambo kijana huyu jasiri leo alilia japo sauti wala kilio hakikusikika lakini macho yake yalitoa machozi.Alitamani dakika zirudi nyuma afute kumbukumbu zilizopita muda uliopita wa maisha yake ,kumbukumbu za tukio la kusikitisha aliloshuhudia kijana yule alihuzunika sana,Alikuwa kama mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na maambukizi ya ukimwi bila kushauriwa na daktari japo ni siku tu iliyopita ila kwake ilikuwa na matukio ya kutisha alitamani aende polisi akaeleze kilichotokea lakini akakumbuka onyo aliloachiwa kwenye usukani wa gari yake akatulia ,Hata kitabu cha The Alchemist alichoanza kusoma juzi hakikuwa na maana tena,Alitia huruma.
Akainuka kutoka katika kitanda cha hoteli hii maarufu hapa mjini Bagamoyo kumpisha mfanya usafi aliyemuangalia kwa jicho la huruma ,alivalia kaptula ya jeans na fulana nyeupe,akaanza kuzipanda ngazi kuelekea juu ya hoteli ile.Huku juu kabisa kulikuwa na mandhari ya kuvutia lakini kijana huyu hakuhangaika kuitazama badala yake alitafuta kiti pembezoni kabisa akaketi akayakubuka maneno ya William shakespear, "THE HELL IS EMPTY,ALL DEVILS ARE HERE" kwake yeye aliiona dunia kama sio mahali salama tena kwake Alimuomba Mungu amsaidie,akaita mhudumu mwingine na kumuagiza supu ya samaki,akainywa taratibu,lakini hamu ya chakula hakuwa nayo na hakumaliza dakika chache akaanza kushuka ngazi kurejea kwenye chumba chake,Akiwa kwenye nganzi akapishana na mmoja wa vijana alioonana nao usiku naam vijana walioweka ujumbe kwenye usukani wa gari lake,japo alikuwa kajibadilisha lakini kijana huyu alimtambua ,mapigo yake sasa yalizidi kwenda mbio kijasho chembamba kikazidi kuchuruzika aliingiwa na woga ,woga wa kumuona mbaya wake tena uso kwa uso, kijana huyu alisikitika.
OFISINI-TABATA
Leo kazi zilikuwa nyingi sana ,Irene ndiye alikuwa Incharge akipokea malipo yote ya wateja na kuzungumza nao huku mafundi wakiendelea na kazi zao,alizungumza na wateja wengi sana na mmoja wapo alikuwa Ben,rafiki mkubwa wa Nick mmiliki wa duka lile la ushonaji kijana anayefanya kazi Benki kuu hapa nchini,kijana ambaye hivi karibuni almetangaza kuwa anamtaka Irene awe mchumba wake lakini akakataa,pengine kwa sababu mbili kuu
kwanza hakuwa na hisia naye na pili alikuwa tayari ana mpenzi wake.mpenzi aliyenaye kwa mwaka sasa toka amalize chuo na Irene kupata kazi hapa dukani kwa Nick amekuwa akimtegemea kwa kila kitu.Irene alikuwa njiapanda alitamani azifuate pesa za Ben lakini upande mwingine wa akili yake ulimwambia atulie na mpenzi wake.Leo Ben alikuwa hapa dukani kwa shughuli mbili ya kwanza ni kutoa oda ya suti za wafanyakazi wenzake na pili,pengine ya muhimu zaidi ni kuonana na Irene.
Aliingia kama ilivyo ada ,akamsalimia Irene na kumueleza
"Irene sitaki kupoteza muda wako,unaona nimekuja kutoa oda tunahitaji suti za kiume 6 kwa ajili ya sherehe ndogo ya idara yetu na hivyowiki mbili ziwe tayari" alimaliza Ben,Irene akatabasamu akiandika andika kwenye kitabu chake,Ben akaongezea naomba kama utakuwa free nikupitie jioni Irene kama kawaida yake alitolea nje ofa hii.wakaagana, Ben akauliza simuoni Nick ametoka? Irene akajibu nilifikiri unajua alipo maana nimekupigia simu hujapokea,hapana akajibu kwa mkato na kuondoka.
Kijana Nick alikuwa katika lindi la mawazo,alitafakari kwa kina sababu za kupokea ujumbe ule hakuzipata hivyo akaamua kupiga simu,akapiga asikie upande ule wa pili lakini haikupokelewa....Akazidi kuwa na wasiwasi ni miaka 23 tokea kijana huyu mzaliwa wa mwanza azaliwe na miaka hii yote hajawahi kuingia katika hofu kama hii hofu iliyosababishwa na vitisho alivyoachiwa jana yake kwenye usukani wa gari yake ujumbe huu haukumtaja nani aliyeutuma lakini ulielekeza vitisho kwa Nick kwani alitajwa,akakumbuka kuipiga simu ya rafiki yake Ben ambae alimuona kama msaada mkubwa wakati wa shida ni Ben huyuhuyu anayemshauri kwenye mambo yake ya muhimu ,baada ya kupokea akamueleza ndugu yangu naomba uje hapa Bagamoyo mara moja sababu sitaweza kuondoka peke yangu ,kuna nini aliuliza Ben lakini kijana huyu alisisitiza, mmmh sawa Ben alijibu.kijana akakata simu yake.
SIKU MBILI KABLA HYATT-KIVUKONI
Kikao cha wamiliki wa Hyatt cha kutangaza kampuni iliyoshinda tenda yakushona nguo za wafanyakazi wake kwa miaka mitano kilikuwa kikiendelea wajumbe wote walikubaliana na mwenyekiti kuidhinisha kampuni ya kijana huyu Nick ikishinda zabuni na kuyaacha,makampuni mengine ya ndani na nje ya nchi.Ilikuwa ni taarifa njema kwa duka lake la ushonaji kwani huu ungekuwa mradi mkubwa wa 5 kwa mwaka huu pekee na mitatu ikiwa kushonea wafanyakazi wa ndege sare zao.Mafanikio haya yalilifanya duka lake kupata umaarufu na kukubalika pengine kuliko maduka mengine ya ushonaji.
Upande wa pili pembezoni kidogo ya barabara iendayo kibada gari aina ya Ford ranger lilikuwa limebeba wazee wawili wote wakiwa na asili ya asia walikutana mahali hapa kwakuwa hawakutaka kufahamika na hivyo kuchagua eneo hilo.walianza kujadili kwanini Hyatt imezikacha kampuni tanzu zao ambazo kwa miaka mitano iliyopita zimewapatia ukwasi mkubwa,lakini hili halikuwauma zaidi kilichowauma ni kwamba sasa wangekosa biashara halali ya kutakatishia pesa zao.Unafikiri nini kifanyike?Aliuliza mzee wa kwanza na yule wa pili akamjibu nina vijana naomba uniachie kazi hii wataimaliza.Hakikisha "they don't leave any tail behind" mzee wa kwanza akasema akikunja sura yule wapili akamjibu nice and clean.wakaagana.
******************************************************************************************************
Kijana yule aliendesha gari lake kuelekea Kivukoni kwa ajili ya kusaini hati ya makubaliano au ungeweza kuiita mkataba wa kushona nguo za hoteli hii kwa kipindi cha miaka mitano ijayo,Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwake kushuhudia dili nono kutoka hoteli hii ya kimataifa,Alifika na kukaribishwa na msaidizi wameneja na moja kwa moja wakaelekea kwenye kusaini,alipewa nakala yake kisha akampa mwanasheria wake aliyeambatana naye kwa ajili ya kuipitia baada ya kujiridhisha ,mwanasheria yule alimshauri kuwataka Hyatt kurekebisha baadhi ya vipengele kisha zoezi likafungwa.wino ukamwagwa ,picha zikapigwa.
Baada ya kutoka hapa kijana alirejea ofisini mwake ambako habari zilikuwa zishafika kila mtu alimpongeza lakini yeye aliwaambia kwamba wa kupongezwa ni nyinyi na wateja wetu ambao kila wakati wanatuamini na kutupa nafasi hii ya kufanya kilicho bora.kazi zikaendelea kama kawaida na muda wakufunga kijana huyu akafunga ofisi na kuondoka,kwenye gari lake alikuwa peke yake akisikiliza nyimbo za asili ya afrika hasa mitindo ya zouk,hii ndio ilikuwa furaha yake.Akaelekea nyumbani kwake kinyerezi alipoiacha barabara inayoelekea majumba sita akakata kulia mbele kidogo akaiona gari nyeupe ikiwa nyuma yake huwa hapendi kufuatwa akaongeza mwendo ,gari ile haikuongeza mwendo badala yake ikasimama pembeni mwa barabara kijana yule hakujali alifika nyumbani kwake geti lilikuwa wazi akashangaa,akakumbuka alilifunga vizuri asubuhi,akashuka garini na kwenda kulifunga geti majabu,
Gari ile iliyokuwa imepaki sasa iliingia getini kwake kwa kasi akaogopa,kijana huyu akashika simu yake lakini kabla hajafanya chochote akasikia sauti yenye mamlaka ikimwamrisha kuweka mikono yake juu akatii,akapigwa na kitako cha bunduki vijana wale wakaondoka kwa spidi kubwa"
Nini kiitaendelea ,tafadhali fuatilia sehemu ya piliu