Riwaya konki: Adili na Nduguze

Riwaya konki: Adili na Nduguze

SURA YA 11

Wokovu wa Adili


Adili alipotupwa alizama kama jiwe katika kilindi cha bahari ambacho urefu wake haukutambulikana. Viwambo vya masikio yake vililia akadhani maji yalipenya sikio hata sikio, na mianzi ya pua yake ilijaa maji yaliyozuia pumzi. Macho yake yalipofumbuka vimemeta kama nyota mbinguni vilionekana katika maji, vimemeta hivyo vilifanywa na mtikiso wa mwili wake. Kutumbukia baharini usiku wa giza ni hatari ya kutisha sana.


Kasi ya kutupwa ilipokoma alijitatamua akakata vifungo vya kamba iliyotatizwa mwilini mwake. Sasa mikono na miguu yake ilianza kufanya kazi. Nusu ya nguvu yake ilikuwa imetumika, lakini matumaini yake yalikuwa kamili. Adili alikuwa si mkata tamaa, na kabla pumzi yake haijakwisha alikusudia kuebuka. Jaribu lake lilikutana na fanaka, maana kabla moyo wale haujakoma alijiona anaelea juu ya bahari. Aliinua kichwa juu ya maji akahema kwa nguvu kama gari moshi. Kulipopambazuka alikuwa katika bahari iliyoghadhibika kwa dhoruba kali, na halibyake ilikuwa taabani. Kutazama hatari usoni kunavunja moyo wa mtu lakini alijikaza kiume.


Mara ile palikuja ndege aliyekuwa na umbo la kutisha akamwopoa Adili majini. Kama koleo, miguu ya ndege ilimshika kwapani akaruka naye. Fikiri wewe mwenyewe hofu aliyokuwa nayo Adili. Binafsi yake alijiona ameokoka kuliwa na papa akawa chakula cha tai. Ndege mwenyewe alipaa juu mpaka Adili alipotelewa na fahamu. Fahamu yake ilipomrudia alijiona katika nyumba kubwa sana iliyokuwa nzuri ajabu. Wasichana warembo na walio changamka walikuwa watumishi katika nyumba hiyo . Miongoni mwao palikuwa na bibi mmoja aliyejipambanua kama malkia, huyo alikaa juu ya kiti cha enzi kilichopambwa na majohari mbalimbali. Rangi ya mavazi yake ilikuwa fua, na kichwani alivaa taji lililopigisha moyo mshindo kwa uzuri.Yule ndege alikuwapo, lakini mara ile alijigeuza msichana wa utanashati mkubwa. Msichana mwenyewe alikuwa yule aliyezama ardhini, baada ya kuokolewa na Adili, alipokuwa katika umbo la tandu na kushambuliwa na nyoka jabalini.


Malkia alimwuliza msichana mtu aliyemwokoa baharini alikuwa nani, na kwa nini aliletwa mbele yake.

Msichana alieleza kuwa mtu yule alikuwa mfadhili wake mkubwa. Zamani maisha yake yalipokuwa katika hatari ya nyoka alipata wokovu kwake. Alimwokoa na kumleta mbele yake kwa sababu aliahidi kulipa fadhili yake.

Kusikia vile, Malkia alisimama akampa mkono Adili aliyeupokea huku amepiga magoti chini. Malkia alimwinua akamkaribisha kuketi kitini akisema, "Starehe, mwanangu. Hali yako ni hali yetu".

Kisha msichana alimwuliza Adili kama aliweza kumtambua yeye alikuwa nani. Adili alijibu kuwa hakuweza.

Msichana alieleza kuwa yeye alikuwa tandu katika jabali fulani zamani akakaribia kuuwawa na nyoka, lakini aliokolewa.

Adili alikubali kuwa alikumbuka kuona tandu jeupe, nyoka mweusi, na msichana aliyezama ardhini.


Tandu lilikuwa yule msichana. Naye alikuwa Huria binti Kisasi. Kisasi alikuwa mfalme wa Majini. Aliyekaa kitini alikuwa mama yake. Jina lake lilikuwa Mjeledi, Malkia wa Majini. Nyoka aliyepigana naye Huria alikuwa waziri wa Ngazi. Alijulikana kwa jina la Hunde. Hunde alikuwa kiumbe cha mwisho katika wanaume waliokuwa na sura mbaya. Siju moja katika matembezi Huria alikutana na Hunde. Alikuwa hatazamiki kwa ubaya, licha ya yeye kumtazama mtu. Pale pale Hunde aliingiwa na shauku kubwa juu ya Huria. Wanawake hukutana na mikasa mingi mibaya duniani. Mioyo yao hulemewa na haja zisizokubalika; masikio yao hutiwa uziwi kwa maombi ya haraka; na miili yao ni mawindo ya jeuri daima.


Hunde alikwenda kwa Kisasi kumposa Huria. Kisasi alijibu Hunde alikuwa ni sufu kwa binti yake ijapokuwa alikuwa waziri wa Ngazi, na kwamba asingalithubutu mbele yake haja kama ile. Tangu siku ile alikomeshwa tamaa ya kuposa mabinti wafalme. Aliudhika akatisha kumwonyesha Huria uwezo wake. Na tangu alipotisha hivyo hakumpa nafasi hata ya uzi kupenya tundu la sindano.


Kila mahali Huria alipopita , Hunde alifuata nyayo zake mpaka aligundua alikokuwa. Iliendelea hivyo mpaka Kisasi akapigana naye. Alishindwa akakimbia. Huria alipotaka kutembea alijigeuza umbo la mnyama. Kila alipojigeuza na yeye alijigeuza vile vile akanusa harufu yake kama mbwa. Alipojigeuza panya, yeye alikuwa paka, alipojifanya paka, yeye alijigeuza chui; na alipokuwa chui, yeye akawa simba. Kila alipoingia yeye alipajua kwa kufuata nyayo zake. Wanaume wana inda mbaya ufisadi unapowapofusha.


Siku aliyojigeuza tandu , yeye alikuwa nyoka akamfukuza. Alipochoka kukimbia alimkamata. Kabla hajamhasiri, Adili alimpiga jiwe akafa. Alijigeuza mtu akaonekana na Adili kwa macho yake. Kabla ya kujizamisha chini aliahidi kulipa wema kwa Adili.


Huria aliomba dua siku zoye ya kuweza kutimiza ahadi yake kwa Adili. Siku aliyotoswa baharini na ndugu zake alikuja upesi kumwokoa katika hatari. Ilipasa wazazi wake, Mfalme na Malkia wa Majini kumkirimu mfadhili wake.

Alimwambia mama yake kwa deni alilowiwa na Adili lilikuwa kubwa sana. Hakudai lilipwe lote lakini lipunguzwe kama lilivyowezekana.


Mjeledi alimwambia Adili kuwa wema wake haukuoza. Kwa kumwokoa Huria aliwatendea wazazi wake fadhili na heshima kubwa nchi ya Majini. Ilikuwa zamu yao kumkirimu walivyoweza sasa.


Adili aliyenyamaza kwa muda mrefu alijibu, "Deni langu limekwisha lipwa lote. Niliokoa maisha ya binti yako, naye ameokoa yangu. Hapana deni tena kati yetu."


Malkia wa Majini alitabasamu akasema, "Usiseme kikembe mwanangu. Wema wako ulikuwa asilia, nawe ulitangulia kuutenda; wa binti yangu ulikuwa wa kuigiza, naye ameutenda nyuma. Asili na uigaji ni vitu mbalimbali. Havilinganiki wala havitalinganika milele."


Adili alipelekwa katika hazina ya majini iliyokusanya utajiri wote wa ulimwengu. Johari ndogo katika hazina hiyo ilikuwa na uzito usiochukulika kwa Adili. Alipochaguzwa kuchukua alichopenda hakuweza kuchagua kitu chochote.

Malkia alisikitika akasema, "Haidhuru!" Alishika simu akauliza" Naweza kusema na mfalme wa majini?"

Jibu lilikuja , " Naam, Kisasi huyu! Nani mwenzangu?" " Mjeledi , Malkia wa majini ndiye asemaye. Adili amechaguzwa apendacho katika hazina yetu, lakini ameshindwa kuchukua hata kitu cha uzito wa sindano moja. Wanadamu hawajaweza kutumia uwezo waliopewa kama Majini. Nataka msaada wako."

" Vema. Mlete hapa," kengele iliishilia.


Adili alikwenda katika halmashauri ya Majini. Alipofika mfalme alikuwa amekaa kitini kwa juu kuelekea hadhara kubwa ya mawaziri. Joho la mfalme lilikuwa la rangi ya fua, na kichwani alivaa taji la zari. Mawaziri walivaa majoho meusi, na vichwa vyao vilikuwa wazi. Hadhara nzima ilisimama Adili alipotokeza . Ilipokaa kitako tena alipewa kitabu cha hawala ya hazina ya majini. Kwa kila hawala iliyoandikwa na kutiwa sahihi ilipochomwa Adili aliweza kupata alichotaka katika hazina ya majini. Alifurahi kwa zawadi ile. Ilikuwa nyepesi kuwekeka, rahisi kutumika, nayo si nzito kuchukulika. Alimshukuru mfalme wa majini akarudi kwa Huria.


Adili aliyageukia Manyani akauliza kama yaliyosemwa yalitokea au hayakutokea . Manyani yaliziba nyuso zao kwa viganja vya mikono yao kwa aibu.
 
Uchambuzi wa jumla wa “ADILI NA NDUGUZE”
Utangulizi
Adili na nduguze ni riwaya iliyotungwa na SHAABAN Robert; mwandishi mashuhuri
(maarufu) kutoka Tanzania. Riwaya hii ilitungwa mnamo 1952. Katika riwaya yake
anashughulika na mambo mengi kuhusu tabia mbalimbali za watu. Mtunzi anatueleza kuwa
tushinde uovu kwa kutenda mema yaani “Wema hauozi”. Adili alimwokoa Huria wakati
alipokaribia kuuwawa na Hunde. Kutokana na wema huo, Huria naye alimwokoa Adili
wakati alipotoswa baharini na ndugu zake. Haya yanazingatiwa na msemo wa Kiswahili
“kinifaa huangua, nitakufaa kwa mvua” au methali isemayo “Mwosha huoshwa”.
1. Mandhari
Mandhari ya riwaya hii ni ya nchi ya Ughaibu, yaani nchi ya mbali. Nchi hiyo ni ya kufikirika
kwa kuwa haipo katika mazingira ya kawaida. Kuna vituko vichache vilivyotokea katika
nchi za kigeni zisizotajwa kwa majina na vingine vilitukia katika nchi ya majini.
2. Wahusika
Wahusika wa SHAABAN Robert katika riwaya ya Adili na Nduguze, aliwapa majina
yanayowiana na tabia zao. Wale ambao hawakubadilika kitabia kama Adili, Mfalme Rai ni
wahusika bapa vielezo. Wahusika Huria, Hasidi na Mwivu ambao walibadilika kitabia ni
wahusika duara.
3. Wahusikana tabia zao
- Adili: shauri; onyo.
- Hasidi: mtu mwenye tabia ya kutofurahia mafanikio ya mwingine (husada)
- Mwivu: mtu menye kijicho; asiyependa mafanikio ya mwingine
- Mfalme Rai: wazo au maoni ya mtu juu ya jambo fulani
Kurai: kusema na mtu kwa maneno mazuri kwa madhumuni ya kumtaka akubali kutimiza
linalotarajiwa.
 
(I) kibali: ruhusa, idhini
- Mwelekevu: mtiifu; mwenye urahisi wa kukubali maelezo (mwongozo)
- Huria: mwenye uhuru wa kutenda kila jambo analotaka
- Mrefu: mwenye kimo (kipimo) kilichozidi kingine (cha kawaida)
- Mfalme Tukufu: mheshimiwa, mtu mwenye madaraka au cheo cha juu
- Malkia Enzi: utawala, utukufu
- Hunde: kiumbe cha ajabu kinachitisha
- Mfalme Kisasi: malipo kwz ajili ya tendo bayaalilofanyiwa mtu#fadhila (au fadhili).
• Adili: ni mhusika mkuu wa riwaya hii. Alikuwa mwema, mwenye huruma,
msamehevu, mvumilivu, jasiri na mfanyabiashara hodari. Tabia yake ile
haikubadilika toka mwanzo hadi mwisho wa hadithi. Kwa hiyo, tabia yake ni
mhusika bapa kielelezo.
• Hasidi na Mwivu: ni ndugu zake Adili. Walikuwa watu wakatili, wenye tamaa,
choyo kikubwa na wabadilifu kitabia, kwa hiyo ni wahusika duara.
• Mfalme Rai: alikuwa mtawala wa nchi ya Ughaibu ambaye aliiletea nchi yake
ustawi wa kiuchumi kutokana na uongozi mzuri, ufuatilizi bora wa kazi na
ushauri wa kuwahimiza raia kuwa wachapakazi.
• Ikibali: ni mshauri wa Mfalme Rain a Halmashauri yake. Alikuwa mcheshi na
mtu aliyechukuana na watu kutokana na kuwatunzia haki zao.
• Mwelekevu: ni msichana mwenye upendo wa kweli, mrembo na mwaminifu
kidini na kindoa.
• Huria: ni jini lililokuwa na uwezo mkubwa wa kutenda kila jambo lililotaka na
kujigeuza sura kwa utashi wake (mhusika duara)
• Mfalme Tukufu na Malkia Enzi: ni watawala ambao walipuuzi/walidharau
ujumbe wa Mola, wakaadhibiwa kugeuzwa mawe, mji wao na raia wao.
• Mfalme Kisasi: ni mfalme wa majini aliyewaelekeza raia wake majini kutii
uongozi wa binadamu.
 
3. Dhamira kuu
“Mapendeleo yakiachwa mbali nuru ya fikra humulika siku zote juu ya kweli kuliko uongo,
juu ya haki kuliko dhuluma na juu ya wema kuliko uovu”.
4. Dhamira ndogo ndogo
a. Uongozi mzuri na ufuatilizi bora wa kazi wa Mfalme Rai uliomwezesha kuistawisha
nchi ya Ughaibu katika mifugo,
b. Uchunguzi mzuri wa Ikibali uliomfanya agundue hila za Adili kuwaadhibu vikali
manyani,
c. Ukalili uliochanganywa na huruma dhidi ya manyani ambao zamani walikuwa
nduguze Adili,
d. Utetezi wa Adili mbele ya Mfalme Rai na kukieleza kisa cha baba yao Faraja kuwazaa
ndugu watatu, Adili, Hasidi na Mwivu,
e. Mvuto wa faida za biashara safarini baada ya mgawo wa urithi wa Adili na nduguze
waliofilisika,
f. Wokovu wa Tandu aliyeshambuliwa na nyoka na bahati ya Adili kupata maji safi,
g. Mji wa mawe uliokuwa na mali isiyo kadiri
h. Mapenzi ya Adili na Mwelekevu, msichana aliyekutwa hai katika mji wa mawe,
i. Habari ya mji na watu wake kugeuzwa mawekutokana na ibada ya mizimu,
j. Wivu wa nduguze Adili kumwona na mchumba na kumtosa baharini,
k. Wokovu wa Adili aliyeokotwa na Huria,
l. Marejeo ya Adili jahazini na nduguze kugeuzwa manyani,
m. Adhabu kali kwa manyani baada ya Adili kuadhibuwa mwenyewe kwa kutotii amri ya
Huria.
n. Jitihada za Mfalme Rai kuokoa manyani waliokuwa nduguze Adili,
o. Ombi la Mfalme Rai lililokubaliwa na Mfalme wa majini Kisasi na bintiye Huria la
kugeuza manyani kuwa watu tena na ndoa ya ndugu wote watatu.
 
5. MHUTASARI: Adili na Nduguze
Uongozi mzuri na ufuatilizi bora wa kazi ulimfanya Mfalme Rai kuistawisha nchi yake ya
Ughaibu katika mifugo. Mshauri wake Ikibali alikuwa bingwa wa uchunguzi wa kodi za
wanyama ila alielemewa na siri ya kiongozi wa Janibu, Adili kuwaadhibu vikali manyani
waliokuwa kwake. Alishangaa kuona jinsi ukatili huo ulivyohitilafiana sana na tabia ya
wema na huruma ya Adili akaamua siri hiyo ifichuliwe mbele ya Mfalme Rai.
Alipoletwa mbele ya Mfalme Rai, Adili alijitetea akieleza kuwa wanyama hao walikuwa
zamani nduguze kwani walizaliwa na baba mmoja, Faraja. Alijulisha kuwa alilazimika
kuwagawia urithi wake wakati walipofilisika ugenini na kurejea nyumbani kwao Janibu.
Alisimulia jinsi ndugu wote watatu walivutwa na faida za biashara na kusafiri mpaka
walipoufikia mji wa mawe, Adili alipokutana na mchumba wa kuusiwa, Mwelekevu.
Hapo hapo, Adili alieleza kuwa uovu waliomfanyia nduguze ndio uliwafanya wageuzwe
kuwa manyani. Kwanza kutokana na mali aliyoleta jahazini na mwanamke huyo mrembo
kutoka mji wa mawe, nduguze walimwonea wivu na kumlia njama za kumtosa baharini.
Wakati huo huo, aliokolewa na jinni, Huria binti Kisasi, ambalo aliwahi kusaidia
lililoshambuliwa na nyoka, ama jinni jingine Hunde.
Adili aliporejea katika chombo akiwa na Huria, jinni hilo ndipo liliamua kuwafanya
manyani ikiwa ni adhabu na kutoa amri ya kuwa watapigwa kila siku kutokana na maovu
yao.
Adili aliporudi nchini mwake, Ughaibu, ndiye aliadhibiwa wa kwanza kwa kusahau
kuwapiga manyani. Tokea hapo ilkuwa mazoea yake kuwapa chakula na kuwapiga vikali
hadi siku, Ikibali aligundua siri hiyo.
Baada ya kisa hicho, Mfalme Rai almsihi Adili asiwapige tena manyani ila awatunze vizuri
na kula nao. Alijitahidi kuwaombea msamaha kwa Mfalme wa majini Kisasi na binyiye
Huria. Ombi lake lilisikilizwa na nduguze Adili waligeuzwa kutoka uhawayani na kuwa
watu tena. Siku hiyo ilikuwa ya furaha, na nduguze wote watatu walifunga ndoa pamoja.
6. Mtindo
Mtindo wa riwaya hii ni mtindo wa rejea. Mwandishi huanza kuisimulia riwaya yake
wakati Adili alifanya ukatili wa kuwaadhibu manyani (ambao walikuwa nduguze).
 
Kugundulika kwa uovu huu ndiko kulifuatiliwa na maelezo ya kisa na sababu ya nduguze
kuwa manyanina hatimaye kuwa watu tena baada ya ombi la Mfalme Rai kukubaliwa na
majini.
Lugha ya Shaaban Robert katika riwaya ya Adili na nduguze ni nzito. Ni lugha yenye
msamiati mgumu, misemo isiyo ya kawaida, nahau na methali nyingi. Pia ametumia lugha
ya ushairi, lugha ya picha na tamathali za usemi za kipekee. Kuna wakati mwandishi huyu
alipotumia lugha ya kisheri katika barua, na hayo yote ni kuonyesha jinsi ana ustadiwa
kuimudu lugha ya Kiswahili katika nyanja zake zote.
Matumizi ya lugha
a) Tamthali za usemi
- Tashbiha:
Uk. 1: Tabia yake ijigawa katika theluthi tatu mbalimbali kama rangi ya ngozi ya
pundamiliya.
Uk. 27: Aliwapenda kama penzi ya maisha yake mwenyewe.
Uk. 33: Aliwapenda kama punzi ya maisha yake.
Alikuwa na miguu mfano wa charahani.
- Sitiari:
Tamaa kwake ni gurudumu la maisha
Lugha ni pandamizi kubwa kwa watu duniani.
Adili alitamka kuwa maisha ni safari na duniani ni matembezi.
- Kipanafsi: “Moyowe ulimshinda”
Msanii amechukua moyo kama mtu.
Moyo ulimshinda ni kusema hakuweza kuzivumilia hisia za moyo wake. Kwani bila
kujitambua alinaswa na uzuri wa Mwelekevu, binti Mfalme Tukufu.
b) Matumizi ya methali na nahau
 
i) Methali
- Mali bila daftari hupotea bila habari,
- Wema hauozi,
- Asiyefurahia heri ya mwenzake shauri yake hunghadhabika,
- Mkulima alikuwa mmoja siku zote lakini walaji wengi,
- Damu nzito kuliko maji,
- Ng’ombe wa masikini hazai picha,
- Busara kubwa kichwani haina faida kama moyoni.
ii) Nahau
- Kukata tama: kupoteza matumaini
- Macho yao yalii.
c) Matumizi ya mashairi
1. Miguu ya msichana,
Na mwendo aliokwenda,
Adili alipoona,
Moyowe ulimshinda.
2. Alikuwa na miguu,
Mfano wa cherahani,
Wala ulimwengu huu,
Hajatokea kifani.
Msanii alitumia ushairi kueleza kwa usanii uzuri wa Mwelekevu.
7. Muundo
Muundo wa riwaya hii unaambatana na kisa kinachomhusu Adili na nduguze, Hasidi na
 
Mkuu kasimba123
Uchambuzi huo ungeufungulia uzi wake au ungesubiri riwaya iishe. Uzi huu haupo kwa ajili ya wanafunzi kukariri maudhui ya riwaya mkuu . Ha ha haaa.
5. MHUTASARI: Adili na Nduguze
Uongozi mzuri na ufuatilizi bora wa kazi ulimfanya Mfalme Rai kuistawisha nchi yake ya
Ughaibu katika mifugo. Mshauri wake Ikibali alikuwa bingwa wa uchunguzi wa kodi za
wanyama ila alielemewa na siri ya kiongozi wa Janibu, Adili kuwaadhibu vikali manyani
waliokuwa kwake. Alishangaa kuona jinsi ukatili huo ulivyohitilafiana sana na tabia ya
wema na huruma ya Adili akaamua siri hiyo ifichuliwe mbele ya Mfalme Rai.
Alipoletwa mbele ya Mfalme Rai, Adili alijitetea akieleza kuwa wanyama hao walikuwa
zamani nduguze kwani walizaliwa na baba mmoja, Faraja. Alijulisha kuwa alilazimika
kuwagawia urithi wake wakati walipofilisika ugenini na kurejea nyumbani kwao Janibu.
Alisimulia jinsi ndugu wote watatu walivutwa na faida za biashara na kusafiri mpaka
walipoufikia mji wa mawe, Adili alipokutana na mchumba wa kuusiwa, Mwelekevu.
Hapo hapo, Adili alieleza kuwa uovu waliomfanyia nduguze ndio uliwafanya wageuzwe
kuwa manyani. Kwanza kutokana na mali aliyoleta jahazini na mwanamke huyo mrembo
kutoka mji wa mawe, nduguze walimwonea wivu na kumlia njama za kumtosa baharini.
Wakati huo huo, aliokolewa na jinni, Huria binti Kisasi, ambalo aliwahi kusaidia
lililoshambuliwa na nyoka, ama jinni jingine Hunde.
Adili aliporejea katika chombo akiwa na Huria, jinni hilo ndipo liliamua kuwafanya
manyani ikiwa ni adhabu na kutoa amri ya kuwa watapigwa kila siku kutokana na maovu
yao.
Adili aliporudi nchini mwake, Ughaibu, ndiye aliadhibiwa wa kwanza kwa kusahau
kuwapiga manyani. Tokea hapo ilkuwa mazoea yake kuwapa chakula na kuwapiga vikali
hadi siku, Ikibali aligundua siri hiyo.
Baada ya kisa hicho, Mfalme Rai almsihi Adili asiwapige tena manyani ila awatunze vizuri
na kula nao. Alijitahidi kuwaombea msamaha kwa Mfalme wa majini Kisasi na binyiye
Huria. Ombi lake lilisikilizwa na nduguze Adili waligeuzwa kutoka uhawayani na kuwa
watu tena. Siku hiyo ilikuwa ya furaha, na nduguze wote watatu walifunga ndoa pamoja.
6. Mtindo
Mtindo wa riwaya hii ni mtindo wa rejea. Mwandishi huanza kuisimulia riwaya yake
wakati Adili alifanya ukatili wa kuwaadhibu manyani (ambao walikuwa nduguze).
 
Mwivu. Mwandishi alieleza jinsi vituko vilivyotiririka tokea mwanzo, ndugu hawa watatu
waliokuwa wakitoka familia moja, uovu ndugu wawili, Hasidi na Mwivu, waliomfanyia
Adili na malipo ya uovu huo (kama upeo wa kugeuzwa manyani na kupata adhabu ya
kupigwa kila siku). Mwishoni kabisa anaujadili msamaha waliopewa ndugu hao. Kutokana
na majuto na ahadi ya kutorudia tena uovu huo.
8. Maadili
- Wema hauozi (mt),
- Kazi ni msingi wa maendeleo (ms),
- Tendo hukidhi haja maridhawa (ms),
- Hulka njema sawa na mali (ms),
- Damu nzito kuliko maji (mt),
- Mali bila daftari hupotea bila habari (ms),
- Mbwa wa msasi mkali ni wakali pia (mt),
- Mapendeleo yakiachwa mbali nuru ya fikra humulika siku zote juu ya kweli kuliko
uongo, juu ya haki kuliko dhuluma na juu ya wema kuliko uovu (ms),
- Turufu huenda siku zote kwa mchezaji (mt),
- Chama chema huvikwa pete (mt),
- Wema utashinda na ubaya utashindwa.
9. Uhakiki
Mwandishi Shaaban Robert amefaulu kuieleza hadithi yake kwa mpangilio bora wa
visa vyake akianzia kuwaletea wasomaji shauku ya kujiuliza “Manyani yanapigwa kwa
sababu gani? Na yahusiaje na watu?” Amewachora vizuri wahusika wake akiwapa majina
yanayowiana na tabia zao. Wale wenye tabia nzuri ni mfano mzuri katika jamii yaani
wanafaa kuigwa. Na wahusika wenye tabia mbaya ni mfano wa kupigwa marufuku, usiofaa
kuigwa katika jamii.
Masahihisho ya maswali
 
Mkuu kasimba123
Uchambuzi huo ungeufungulia uzi wake au ungesubiri riwaya iishe. Uzi huu haupo kwa ajili ya wanafunzi kukariri maudhui ya riwaya mkuu . Ha ha haaa.

Ni kweli, atulie au apeleke shule huko mambo ya dhima.
 
SURA YA 12
Nduguze kuwa Manyani


Baada ya Adili kutoswa, nahodha alishtuka akauliza nini kilichotumbukia baharini kwa kishindo kikubwa. Kusikia vile ndugu zake walianza kujiliza uongo kuwa ndugu yao amepotea. Nahodha alikwenda kutazama akaona Adili hayuko. Aliamuru kutua tanga na kuteremsha mashua. Lakini sasa dhoruba kali ilianza, na chombi kilichokuwa katika mrama mkubwa, kwa mawimbi makubwa ya upepo na umande, kilipakia maji, omo na tezi, na kulia ja kushoto. Giza kuu lilinyemelea roho za mabaharia. Palikuwa hapatiliki nanga. Kwa hivi tamaa ya kumuokoa Adili ilikatika.


Nahodha alipotaka kujua Adili alivyopotea, ndugu zake walimwambia kuwa ndugu yao aliamka akaenda msalani. Ghafula walisikia anguko kubwa majini. Watu wote jahazini walisikitika kupotelewa na Adili. Ndugu zake walilizana kitambo wakanyamaza. Kilio cha kujisingizia hakina machozi wala matanga.


Hasidi na Mwivu walichukua sanduku la Adili wakalifungua. Walitoa majohari yote wakagawana mafungu mawili usiku ule ule. Sasa ugomvi kati yao ulianza juu ya yule msichana mzuri aliyekuwa chomboni. Hasidi alitaka kumwoa, na Mwivu kadhalika alitaka kumwoa. Asiyefurahia heri ya mwenziwe, shari yake kumghadhibikia. Walimsahau ndugu yao aliyepotea dakika chache zilizopita kama aliyekufa miaka kumi iliyopita. Walikuwa na mioyo migumu iliyoje!


Mwelekevu, yule msichana mzuri, alikuwa hana tabasamu. Uzuri wake ulisawazika kwa machozi ya njia mbili usoni. Huzuni ilimshika vibaya, lakini alikuwa imara kutetea heshima yake. Aliwaambia wale ndugu wawili wasigombane bure. Hakuwa tayari kuolewa na yeyote kati yao. Na kabla ya sauti ya maneno aliyosema haijaishilia masikioni mwao, alijitosa baharini akatoweka vile vile.


Hasidi na Mwivu hawakujua la kutenda. Atakaye makaa ya mgomba hapati kitu ila jivu tupu. Ndugu hawa wawili walimtosa ndugu yao kwa tamaa ya kupata msichana , lakini walipata aibu tupu. Walikaa kitako wamefedheheka, walipokuwa katika hali hiyo na jahazi inakwenda mbio, Huria na Adili walitua ghafula kama ndege chomboni.


Marejeo ya Adili yalishangaza watu chomboni. Macho ya ndugu zake yalisutana. Kwa kutahamaki walimkumbatia wakajifanya kumfariji. Walisema hatari yake ilitisha, na msiba wao ulikuwa mkubwa. Watu wengine wote chomboni waligeuza macho yap kando waliposikia uongo wa ndugu zake. Walakini Adili aliwashukuru akisema bahari haiweki amana ya kitu kieleacho, kwa kuwa alielea aliokoka.


Kwa hasira kubwa Huria alinena, "kama mngalijua hatari ya kumtosa mtu baharini, au mngalikuwa na fikira za msiba, msingalijaribu kumtumbukiza ndugu yenu baharini alipolala. Wauaji ninyi hamstahili kuishi," aliwashika shingoni pamoja na mkono wa kushoto akawabana kwa nguvu ya ajabu. Mkono wake wa kulia uliinua ngumi juu tayari kuwaangukia kwa uzito mwingi. Ndimi vinywani na mboni machoni mwao zilitoka kwa hofu wakataka kuombewa.


Damu nzito kuliko maji. Hasidi na Mwivu walikuwa damu kwa Adili . Hakuvumilia kuona hilaki yao akamwomba Huria kuwasamehe. Walimtosa tu, hawakumwua. Huria alibisha kuwa walistahili kifo. Jaribu la jinai lilitosha kuhalalisha adhabu ha kifo ujinini. Adili alitaradhia kuwa jaribu la jinai halikutosha kuhalalisha kifo duniani. Kama walikufa kwa sababu yake angalikuwa mnyama wa mwitu mbele ya macho ya watu. Huria aliposikia maneno hayo alinena sheria ya wanadamu ilitatiza. Kwa sababu hiyo walikuwa hatarini milele. Walakini alikubali kuwasamehe kwa sharti ya kuwageuza wanyama. Aliwalaani watoke katika umbo la uanadamu. Mara ile ndugu zake walikuwa manyani.


Kisha Huria aliwakabili watu waliokuwa chomboni akasema. Adili alikuwa rafiki yake mkubwa. Alimjali na kumheshimu juu ya marafiki zake wote. Alipata upendo wake kwa sababu alikuwa salihi na mstahiki wa kuajabiwa na dunia nzima. Ataonana naye mara kwa mara. Mtu yeyote akifitini ataona nguvu ya mkono na uwezo wa ulimi wake. Atampatiliza kama alivyofanya kwa waovu wale wawili. Wajihadhari wapatw kujiokoa kwa sababu alikusdia kutimiza alivyosema. Aliwaonya pia watakapofika kwao wasisemw habari ile. Mtu yeyote atakayejaribu kunong'ona habari ile atakoma kusema milele.


Aliagana na Adili akasema, "Funga manyani haya kwa kamba . Ukifika Jannibu utayafunga kwa minyororo viunoni mbalimbali. Utayatia chumbani na kila moja lifungwe peke yake. Kila usiku wa manane utachukua kiboko ukafungue kila nyani ulipige mpaka lizimie. Utayapa posho na kuyaadhibu hivi daima. Kama amri hii haikutiiwa utaadhibiwa wewe." Alipokuwa akitoa amri hii alijibadilisha sura za ajabu kila dakika moja. Watu wote jahazini walishikwa na mshangao mkubwa kwa mabadiliko yake ya mfululizo, wakatosheka kuwa aliweza kubadili kitu chochote katika umbo alilotaka.


Adili aliyageukia manyani akauliza kama yaliyosemwa yalitokea au hayakutokea. Manyani yaliziba nyuso kwa viganja vya mikono yao kwa aibu.
 
Back
Top Bottom