Sehemu ya 20*
Zagamba akaona bora afe kuliko kusubiri kuuawa na mtu kama kepteni Zegera,alimjua nje ndani bwana yule alivyokatili akaona hana la kujitetea mbele yake,atamwambia nini ikiwa mvamizi mwenyewe alikuwa ni mmoja tu na wao walikuwa watatu fadhaa ikamkumba.
Alimtazama Zedi anavyoondoka katika nyumba ile,akaonelea bora afanye kitu ili amshawishi mwamaume mwenzake amtoe uhai katika utaritibu pasipo maumivu kuliko kutolewa uhai kwa maumivu makubwa.
Kwa taabu akaipata sauti yake nayo ikamfikia Zedi,Zedi akageuka.
"umenipiga nakubali,ukaona haitoshi ukanivunja uti wa mgongo,hata nisipokwambia ninachokijua itakuwa kazi bure maana sintoweza kujitetea kwa lolote"
Zedi akamtazama akavutiwa na maneno ya Zagamba,jambazi maarufu katika vyombo vya dola,anatafutwa kwa garama kama shilingi ya kale.
Zedi akaacha hatua zake zimfikie mhalifu yule pale chini,alipomfikia akamwinamia nae akaipata sauti yake katika utulivu wa mume kuomba unyumba kwa mkewe.
"waeza zungumza sasa nami nitakusaidia!"
"Namfahamu Zegera ni mtu anaetumia vibaya vazi lake la taifa,amekuwa akinitumia katika matukio mengi ya uhalifu,anahusika na Ibrahim wa dawa za kulevya,lakini kubwa zaidi hivi sasa anampango tikisa na kuna mtu alinikutanisha nae anaitwa Ibra Mbaya....."
"Hebu ngoja we unamjua vizuri Ibra au umetamka tu hilo jina!"
"Namfahamu nimekutana nae juzi na kesho alinambia atanipangia kazi ambayo sikuijua.
Mwonekano wake ni mrefu sawa na wewe ni mpole anapozungumza ila ni hatari na maamuzi magumu,jana to ameua mtu mbele yangu baada ya kukosea mpango fulani na hivi sasa yupo mahali anafanya jambo pamoja Zegera".
"unahisi wanafanya nini huko waliko?"
"Siwezi jua ila nahisi wapo bandarini na...... "
Zagamba hakumaliza kauli yake risasi ikatua kichwani pake na kuutawanya ubongo wake huku na huko na mwingine ukamrukia Zedi mwilini kwake.
Zedi hakuwa amempiga risasi Zagamba alishangaa risasi ilipotokea nae hakungoja akaruka upande mwingine na kuiweka sawa silaha yake lakini wakati akiijaribu bahati yake akashangaa risasi nyingine ikizipasua taa zilizokuwa zikiwaka subuleni pale.
Zedi akiwa anapambana na giza akasikia mdondoko wa kitu kama paka,wakati akijiuliza na kupambana na kulizoe giza la gafla kutoka pale alipo kwa mbali aliona kama mtu akinyata na kusogea mahali kulipokuwa na meza kisha akaruka na kulikumba dirisha la kioo na kutokomea kusiko julikana.
Zedi akaliona tukio lile akajiuliza pale mtu yule alifuata nini,hapo akakumbuka hata yeye aliona kitu pale ila hakukitilia maanani Sana,hapo akajikuta akitukana tusi zito la nguoni na kunyanyuka alipokuwa baada ya kuhisi usalama eneo lile na lengo lake ni kuwahi huko bandarini usiku huo.
Nusu saa nyuma...
Zegera alikuwa kimya ndani ya gari lake alikuwa akiiacha moroko ili aikamate kawe,huko alikuwa na miadi ya kukutana na mkurugenzai wa bandari ambapo angemchukua na kufanya nae mazungumzo kisha yeye angelienda bandarini ili kufanya hila mizigo yao iwahi kutoka lakini alikumbuka jambo.
Katika mpango tikisa huwa anahifadhi kila kitu kwenye kihifadhi kumbukumbu au kwa lugha rahisi kwa wengi Flash,na hata wakati huo alipaswa kuwa nayo ili achukue baadhi ya mambo ya muhimu kwa mkurugenzi wa bandari,akajipapasa hakuwa nayo,akapaki pembeni na kukagua gari ila hakuambulia kitu.
Kumbukumbu zake zikamwambia aliiaahau nyumbani kwake mezani na alipaswa kuifuata,ila muda haukuwa rafiki,hapo akaamua jambo,akanyanyua simu yake na kupiga
"Yes!!"
"Nenda kwangu kunamzigo upo mezani niletee kawe"
"sawa mkuu"
"ila yupo Zagamba"
'"Hapana Shaka mkuu"
"Dula fanya chapu"
"ok"
Dula hakutaka kuchelewa akajipaki ajuavyo na begi lake mgongoni akachukua pikipiki yake na kuingia barabarani.
Haikuchukua muda akawa yupo nje ya geti la nyumba ya Zegera,akataka kupiga honi afunguliwe,akasita baada ya kuona mlango mdogo ukiwa wazi,akajua kuna la zaidi hapo ndani.
Aliingiwa na hisia za jambo baya maana hakuwa mgeni katika kazi ya ushushushu,akaona asijipe tabu,anajua njia mbadala ya kuingilia pale ndani akazunguka nyuma ya nyumba ile akaangaza kushoto na kulia hakuona kitu akasimama katikati ya barabara hapo akatazamana na bampa la kuzibia mifereji ya maji machafu,akatumia nguvu kidogo akabetua bampa lile kisha akazama ndani.
Haikuwa njia ya maji machafu ila ni njia ya kuingilia au kutokea ndani ya nyumba ya kepteni zegera.
Ndani ya dakika chache akatokezea kwene chumba cha bwana zegera.
Wakati akipiga hatua ili afungue mlango akasikia miguno ya mtu aliekatika mateso,akaweka umakini zaidi na kwa kutumia utalaamu wa kijasusi akafungua mlango bila mtu kusikia hata yeye aliefungua hakusikia sauti yoyote kisha taratibu mwendo wa teja akasogea kutazama ilipo sebule,hakuamini macho yake akamwona mwanaume mrefu akiwa ameikamata vyema bastola yake huku akisikiliza maongezi flani kutoka kwa zagamba.
Alifikia maamuzi ya kumuua zagamba baada ya kuona Zagamba hana nguvu za kujiokoa hata kama yeye atakuwa kamsaidia kufanya hivyo,pia aliiona Flash ikiwa bado mezani hivyo hakuwa na namna ya kuichukua isipokuwa kucheza pata potea,akanyoosha mkono na kidole kikacheza risasi ikampata Zagamba na hapo akaona wepesi wa mtesaji yule alivyoruka kuikwepa risasi iliomlenga baada ya ile ya kwanza kumpata mhusika,l.
Dula akaona sio muda wa kujipima ubavu na kiumbe yule ila ni kuichukua flash na atamtafuta wakati mwingine kwa mchezo kama ule,na bila kupoteza muda akapiga taa ikazima kisha kwa wepesi wa moshi wa sigara akaruka na kutua kama paka na kupiga hesabu za kichwa namna ilivyokaa ile Flash mezani akaikwapua ilipojaa mkononi akatumia begi lake kulikumba dirisha la vioo na sekunde chache alikuwa nje ya nyumba ile akiipeleka flash kwa mwenyewe huku nyuma akimwacha Zedi akiwasha usafiri wake kuwahi bandarini ila ni kwa kuwa hakujua huko anapoteza atakutana na nini heri angelibakia kumtafuta Dula kwanza.
******
Nb:Maisha ni kusaidiana ukinisaidia leo niweze timiza malengo yangu huwezi jua kesho yetu Mimi na wewe itakwaje japo hatujuani.
Changia chochote ulichonacho,
Nawashukuru wale wanaochangia hadi sasa na mungu awabariki wewe ambae hujafanya hivyo hujachelewa ni Wakati wako sasa kuonesha sapoti kwa waandishi waliohai,
Usisubiri tukifa utoe pongezi kwenye mandiko yetu ikiwa hukutusapoti tukiwa hai.
0758573660
0658564341
Asalaam kudo.