nameless girl
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 4,195
- 2,689
Kwa wapenzi wa vitabu vya Ben Mtobwa, kwa mara nyingine napenda kuchukua fursa hii kuvitangaza vitabu vya marehemu Ben Mtobwa kwamba sasa vinapatika hapa jijini Dar es salaam, maeneo ya Posta mkabala na sanamu la askari mbele ya duka la HD pharmacy, pia Kinondoni kituo cha kanisani.
Vitabu hivi mpaka sasa vinapatikana aina kumi na tatu.
1. Mikononi mwa Nunda
2. Salamu toka kuzimu
3. Mtambo wa mauti
4. Najisikia kuua tena
5. Tutarudi na roho zetu ?
6. Roho ya paka
7. Dimbwi la damu
8. Mikataba ya kishetani
9. Malaika wa shetani
10. Dar es salaam usiku
11. Pesa zako zinanuka
Vitabu hivyo vyote vinapatikana kwa bei ya shilingi 10,000 za kitanzania.
12. Zawadi ya Ushindi 7000
13. Kiguu na njia 15,000
Kwa wale walioko mkoani unaweza kupata vitabu hivi kwa njia ya bus ambapo ukinunua kuanzia vitabu vinne na kuendelea pesa ya usafiri tutagharamia lakini ukinunua vitabu vitatu kushuka chini utagharamia usafiri kwa bei ya shilingi elfu tano.
Kwa maelezo zaidi jinsi ya kupata vitabu hivi, tafadhali tupigie kwa namba 0712504985 au 0763044459.
Lakini pia napenda kuileta kwenu riwaya ya Kiguu na njia especially kwa wale walioko mbali au hawana uwezo wa kuvipata vitabu hivi kwa namna moja au nyingine, basi riwaya hii itakujia kila siku.
Itakufundisha na kukuburisha. Kwa wale wanaokihitaji kitabu hiki pia kinapatikana.
Haki zote zimehifadhiwa, huruhusiwi kucopy au kuiuza popote pale bila idhini ya Heko Publishers Ltd.
KITABU CHA KIGUU NA NJIA
BY BEN R. MTOBWA
SURA YA KWANZA
Mwanzo wa Kisa na Mkasa
Ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona baba akitokwa na machozi. Kwa kweli, ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona mwanamume yeyote mwenye umri wa baba akilia, iwe sirini au hadharani. Kitendo cha mwanamume kutokwa na machozi, iwe kwa sababu ya maumivu au majonzi, hakikupata kukubalika katika jamii yetu.
Nakumbuka nilipokuwa mtoto mdogo, wa miaka mitatu au minne hivi, nilipojikwaa na kuumia au kupigana na wenzangu nikalia. Baba alikuwa akinicharaza bakora huku akisema, “Mwanaume gani wewe unalia? Mwanaume halii.
Babu yangu pia, mzee Karimanzila, aliwahi kunicheka sana kwa suala hilo la kulia. Siku hiyo mtego nilioutega mwituni ulikuwa umemnasa kanga mkubwa sana. Rafiki yangu mmoja tuliyekuwa naye porini aliniita kwa sauti kubwa kuniarifu juu ya kanga huyo. Lakini nilipofika kwenye mtego huo nilimkuta Katato, ambaye alituzidi sana kwa umri na umbile, akimfungua kanga huyo kwa madai kuwa ni mtego wake. Tulibishana naye sana. Kwa kunikomoa Katato alimwachia kanga wangu, ambaye aliruka na kutokomea zake mwituni. Nilijaribu kupigana naye lakini akanizidi nguvu na kunitia ngeu katika paji la uso. Nililia njia nzima hadi kijijini. Babu aliposikia habari hizo aliniita na kunidhihaki kwa kusema, “Ukiona mwanaume analia ujue ana roho ya kike. Angestahili kuvaa gauni badala ya kaptula.”
“Lakini yule alikuwa kanga wangu wa kwanza. Nimekwishanasa njiwa, hondohondo na kware. Leo nimebahatika kumnasa kanga. Ningefurahi sana kumchinja na kumla!” Nilimjibu babu.
Babu alitabasamu kidogo kisha akasema, “Kanga elfu moja utawala. Tatizo ni hayo machozi. Machozi ya mwanaume yanatakiwa kuwa adimu sana. Leo jioni uje nikusimulie kisa cha mwanaume aliyepokonywa mke kwa ajili ya machozi.”
Nilizipenda sana hadithi na simulizi za babu. Kwa ujumla, kijiji kizima na hata vile vya jirani vilipendelea sana kuja kwetu kumsikiliza babu akisimulia matukio mbalimbali yaliyomkuta katika maisha yake. Hadithi zake zilijaa miujiza na maajabu kiasi kwamba baadhi ya watu walidiriki kumwita ‘mwongo’ au ‘anatia chumvi’. Lakini yeye aliwacheka watu wa aina hiyo na kuwaambia, “Hamjaiona dunia. Dunia yenu ni kijiji hiki pekee. Mimi nimeizunguka. Nimefika upande wa pili wa dunia!”
Hiyo ilikuwa kauli yake ya mara kwa mara, kauli ambayo iliongeza utamu wa simulizi zake. Hakika babu mwenyewe alikuwa hadithi, tena hadithi ya kusisimua kuliko zile simulizi zake. Inadaiwa kuwa, utotoni, akiwa na umri wangu, alitoweka kijijini hapo kama mzuka. Alitafutwa kwa siku kadhaa bila mafanikio. Watu walidhani kuwa ameliwa na simba au mamba. Lakini alipoibuka miaka kadhaa, baadaye, akiwa na simulizi tele za ‘kuizunguka dunia,’ watu walibadilika na kuamini kuwa alichukuliwa na mashetani ya chini ya bahari.
Pamoja na kuzipenda hadithi zake, pamoja na kiu ya kusikia kisa hicho cha ‘machozi ya mwanamume’ bado hasira dhidi ya kanga wangu aliyepeperushwa kwa makusudi na maumivu toka kwenye ngeu ya paji la uso kwa mara ya kwanza vilinifanya nikatae kwenda kumsikiliza.
Hivyo, kumwona baba akilia lilikuwa jambo jipya kabisa katika maisha yangu. Alikuwa kaketi juu ya gogo, mikono yake yote miwili ikiwa imekishika kichwa chake huku macho yake yakitazama mbele yake, ingawa ilikuwa dhairi kuwa haoni kitu chochote kutokana na wingi wa machozi. Nilijikaza na kumsogelea kwa nia ya kumuuliza kulikoni. Lakini mara nilipomfikia ushujaa ulinitoka. Nikajikuta nikiambulia kukaa ubavuni mwake, juu ya gogo lilelile. Kwa mshangao wangu, baba alifanya kitu ambacho hakupata kukifanya huko nyuma. Alinikumbatia kwa mkono wake mmoja huku mkono wake wa pili ukifuta machozi ambayo yalimiminika kwa wingi zaidi.
“Mwanangu!” nilimsikia akiniita kwa sauti ndogo yenye kigugumizi.
Sikumbuki kama niliitikia au la.
Wala yeye hakuzungumza neno jingine.
Je kipi kilikuwa kikimtatiza baba ?
Tukutane tena kesho saa kumi na mbili jioni.