THE SPIRIT THINKER
JF-Expert Member
- Sep 9, 2019
- 419
- 654
SEHEMU YA NANE
Theresa alitoa karatasi moja na kuigeuza upande ambao ninaweza kuisoma kabla ya kunipatia. Ilikuwa imeandikwa kwa mkono majina ya mashahidi. Yalikuwa ni majina manne. La kwangu, jumlisha Rodriguez, Flrlujlov na Mbele.
“Abiria wanne.” Alisema.
Nilianza kuongea, “Mimi nilikuwemo kwenye treni na niliwahesabu. Nina uhakika kulikuwa na abiria wangapi.”
Halafu nikaanza kuliangalia tukio kwenye kichwa changu. Namna tulivyoshuka kwenye treni, tukiwa tunawasubiria askari. Na mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kukamatwa.
“Labda jamaa alitoroka.” Nilisema.
Dochery alisema, “Huyo jamaa ni nani?”
“Jamaa tu. Hakuna cha zaidi kwake, ila alionekana tu sio maskini.”
“Waliwasiliana kwa namna yeyote na marehemu?”
“Hilo sikuona.”
“Yeye ndiye alimpiga risasi huyo mwanamke?”
“Hapana. Yule mwanamke alijipiga mwenyewe.”
“Basi huyo jamaa hana umuhimu wowote. Labda hataki kuhusishwa na hili sakata kuepusha ugomvi na mke wake muda kama huu alikuwa anatokea wapi kupanda treni. Haya mambo yanatokea sana.”
“Jamaa ametoroka, lakini mnamwacha aende na sababu mnamtengenezea ila mmenikamata mimi?”
“Si umekiri mwenyewe kuwa hakuhusika?”
“Na mimi pia sikuhusika.” Nilijibu.
“Hayo umesema wewe.”
“Kwahivyo unaamini ushuhuda wangu kuhusu mtu mwingine, ila hauamini ushuhuda wangu kuhusu mimi mwenyewe?” Halafu nikaongeza, “Hapa tunapotezeana muda.”
Na ni kweli tulikuwa tunapotezeana muda, halafu nikagundua kitu. Nikagundua Theresa na Dochery walikuwa wananifanyia huruma fulani. Hili jambo lote lilikuwa limepangwa.
Kuna zaidi ya kinachoweza kuonwa kwa macho.
Niliongea, “ Huyo mwanamke alikuwa ni nani?”
“Kwani lazima awe nani?” Theresa aliongea.
“Kuna sikielewi. Najua kuna mtu kawaambia mniweke hapa hadi afike. Ndiyo maana hakuna mnachokifanya zaidi ya kuniweka hapa na huu upuuzi wenu.”
“Kusema kweli upo sahihi.”
“Kwahivyo huyu msichana alikuwa ni nani?”
“Inavyoonekana alikuwa anaifanyia kazi serikali. Na hapa kuna bwana mmoja wa F.B.I yupo njiani anakuja kuzungumza na wewe.”
Walipomaliza kuniambia hivyo walinyanyuka na kuniacha peke yangu. Chumba chenyewe kilikuwa kipo sawa tu. Kulikuwa na meza na viti vitatu. Viwili kwaajili ya maafisa na kimoja kwaajili ya mhojiwa. Wakati mwingine ni vigumu kutabiri nini humtokea mtu anayewekwa kwenye chumba kisichokuwa na madirisha.
Nilianza kuhesabu muda kwenye kichwa changu. Saa la kwanza likapita, na la pili. Hawa watu waliokuwa wanakuja kuniona lazima walikuwa wanatokea D.C. Niliacha kufikiria nikainua miguu yangu kwenye meza na kusinzia.
Alfajiri ya saa kumi na moja, jamaa watatu wakiwa ndani ya suti nyeusi walikuja na kuniamsha. Walikuwa na nyuso za upole. Suti zao zilikuwa ni za gharama. Nywele zao ilionesha wametoka kuzinyoa siku sio nyingi. Niliomba kuona vitambulisho vyao, lakini walinisomea sherfia moja kuwa walikuwa hawaruhusiwi kujitambulisha. Nilianza kufikiria kuwasumbua, lakini ni kama waliyasoma mawazo yangu na kunipatia mstari mwingine ambao ulinipatia picha moja tu, kwamba endapo ningeleta usumbufu kuna matatizo makubwa yalikuwa yananisubiria mwisho wa barabara. Kusema kweli mimi ni muoga wa vitu vichache sana, lakini kwa vitimbwi vya leo, ilinipaswa niwe mpole. Kwahivyo niliinua mabega juu na kwaambia waendelee na maswali yao.
Walianza kwa kusema walikuwa wanatambua rekodi yangu ya jeshi na walikuwa wanaiheshimu pia. jambo ambalo lilimaanisha walikuwa wananipaka mafuta kwa mgongo wa chupa au wao pia walikuwa ni askari wa wanajeshi. Na hakuna mtu anamheshimu askari wa wanajeshi isipokuwa askari wa wanajeshi mwenzake. Halafu wakaniambia watakuwa wananiangalia kwa ukaribu sana kujua kama nilikuwa nasema uongo au naongea ukweli. Ambao nao ulikuwa ni uongo mtupu. Kwasababu ni wachache kati yetu tunaoweza kufanya hivyo, na kama wao wangekuwa ni wazuri kwa kiwango hicho basi wangekuwa wapo nyumbani wamelala kuliko kuwa hapa asubuhi hii na mapema.
Lakini sikuwa na jambo lolote la kuficha, hivyo niliwaambia waendelee na maswali yao.
Walikuwa na maeneo matatu makuu waliyotaka kujua. Kwanza: Je, Nilikuwa nafahamiana na yule mwanamke aliyejiua? Nilikuwa nimewahi kuonana naye hapo kabla?
Niliwajibu, “Hapana.” Jibu fupi na tamu, kwa utaratibu ila kwa mkazo pia.
Hawakufuatisha maswali. Jambo ambalo liliniambia wao walikuwa ni akina nani haswa. Walikuwa ni timu B ya mtu fulani. Walikuwa wametumwa kwa kazi moja ya kufunga uchunguzi wa jambo lililokuwa linaendelea. Walikuwa wanazika kila kitu. Walikuwa wanataka jibu hasi kwenye kila swali walilokuwa wananiuliza, ili faili lifungwe na jambo lizikwe kabisa. Basi.
Swali la pili lilikuwa: Je, nilikuwa namfahamu mwanamke anayeitwa Lila Hoth?
Nilijibu, “Hapana,” Kwa sababu ni kweli nilikuwa simjui. Kwa wakati huo.
Swali la tatu lilileta mjadala kidogo. Aliyeliuliza alikuwa ni kiongozi wao. Alikuwa mzee kidogo. Pengine na mwenye akili kuliko wale wengine. Alianza kwa kusema, “Ulimfuata yule mwanamke kwenye treni.”
Sikusema neno lolote. Nilikuwa pale kujibu maswali, na sio kutoa hoja zangu kwenye maoni yake.
“Ulimsogelea kwa ukaribu kiasi gani?”
“Futi sita,” Nilijibu. “Umbali wa kuweza kupokea au kutoa kitu kwa mtu.”
“Ulimsogelea kwa ukaribu wa kuweza kumgusa?”
“Hapana.”
“Kwa mfano angenyoosha mkono wake, na wewe ukafanya hivyo pia, mngeweza kugusana mikono?”
“Labda,” Nilijibu.
“Nichukulie jibu lako kama ndiyo au hapana?”
“Lichukulie kama labda. Ninaufahamu urefu wa mkono wangu. Lakini sifahamu urefu wa mikono ya yule mwanamke.”
“Sawa. Je, alikupatia kitu chochote?”
“Hapana.”
“Je, ulichukua kitu chochote kutoka kwake alipokufa?”
“Hapana.”
“Je, kuna mtu mwingine labda alichukua kitu chochote kutoka kwake.”
“Sikuona hilo tukio.”
“Uliona labda akiangusha kitu chochote kutoka kwenye mkono, kwenye begi, au kwenye nguo zake?”
“Hapana.”
“Je, alikuambia jambo lolote?”
“Hakuna cha maana alichoniambia.”
“Je, aliongea na mtu mwingine?”
“Hapana.”
Yule mwanaume akatulia kidogo kabla hajaniambia, “Kama hautojali, toa mifuko yako ya suruali.”
Nilikubali. Sikuwa na kitu au jambo lolote la kuficha. Nilitoa mifuko yangu yote na kuweka kila kilichokuweko mfukoni juu ya ile meza. Kulikuwa na kiasi kidogo cha pesa zilizokunjwakunjwa. Passport yangu kuukuu. ATM card na mswaki wangu wa kukunja. Na business card ya Theresa Lee.
Yule mwanaume akakagua vitu vyangu kwa kidole kimoja na kutikisa kichwa chake kama ishara ya kuwaambia vijana wake wasogee kunikagua vizuri. Walinikagua kwa umakini bila kupata kitu chochote,
Yule bwana akasema, “Asante, bwana Kichaka.”
Halafu wakatoka nje wote watatu. Nilishangazwa kidogo, lakini pia nilifurahi. Niliweka vitu vyangu mfukoni na kuelekea ulipo mlango nitoke nje. Nilimuona Theresa akiwa kwenye dawati lake. Halafu Dochery alikuwa anaongea na bwana mmoja ambaye alionekana amechoka usoni kwa kukosa usingizi. Theresa aliniona nilivyokuwa nimemkazia macho yule mwanamume.
“Huyo ni kaka yake na yule mwanamke.” Theresa aliniambia. “Tulizipata namba kwenye waleti ya marehemu tukampigia aje. Yeye pia ni askari polisi.”
“Maskini.”
“Tumemshauri asihangaike kuutambua mwili maana una hali mbaya sana. Tumemshauri achukue tu jeneza. Na ameelewa.”
“Kwahivyo mna uhakika ni dada yake?”
“Tumechukua alama za vidole.”
“Kwani alikuwa ni nani haswa?”
“Siruhusiwi kusema.” Theresa alinijibu.
“Kwahivyo mimi naruhusiwa kuondoka?”
“Kwani wale wamemalizana na wewe?”
“Nadhani.”
“Basi wewe nenda tu.”
Nilipiga hatua kadhaa hadi kwenye ngazi ya kutokea halafu akaniita. Nilipogeuka akasema, “Niliposema wewe ndiyo chanzo cha kifo chake sikuwa ninamaanisha.”
“Ulimaanisha.” Nilisema. “Na unaweza ukawa ulikuwa upo sahihi.”
Niligeuka na kuanza kupiga hatua za kuondoka. Nilipokunja kona ya mtaa wa 35 nikajiambia hapa umemaliza. Upo huru. Lakini kumbe sikuwa huru. Kwenye kona hiyohiyo niliyokunja, kulikuwa na mabwana wengine wanne wanasubiria kuongea na mimi. Walikuwa wanafanania kama wale niliomaliza kuongea nao, ila hawa suti zao zilikuwa ni ghali mno.