SEHEMU YA TATU.
Pointi namba tisa. Midomo inayocheza. Hadi leo, mashambulizi mengi ya milipuko ya mabomu ya muhanga ni matokeo ya ushawishi wa dini, na dini inayohusishwa sana na mashambulizi ya aina hiyo ni uislamu.
Mashahidi ambao wameponea chupu chupu kwenye mashambulio hayo wamenukuliwa wakisema kabla ya bomu kulipuka, midomo ya mshambuliaji huwa inacheza cheza muda wote... Abiria namba nne alikuwa anachezesha midomo yake kila baada ya kupumzika kwa sekunde ishirini au zaidi kidogo. Kwa kuwa alikuwa hasikiki nilihisi labda alikuwa anajitambuliaha huko ambako alikuwa anategemea kwenda.
Treni ilisimama mtaa wa 23. Milango ilifunguka. Hakuna aliyeshuka. Hakuna aliyepanda. Nilibaki nimekaa kwenye kiti changu. Milango ilifungwa na treni iliendelea na safari.
Pointi namba 10: Begi kubwa.
Dynamite ni bomu imara sana. Halilipuki kwa bahati mbaya hivyo huwa linahitaji kuamuliwa na blasting caps imara. Hizi huwa zinafungwa kwenye Dynamite na chanzo cha umeme kama betri na swichi. Unahitaji betri kwaajili ya Volti na Ampu. Hivyo seli ndogo za AA hazifai kwaajili ya mlipuko mkubwa kama wa Dynamite. Betri lenye volti hadi tisa au zaidi ndiyo bora zaidi, na ili upate mlipuko mzuri zaidi utahitaji betri kubwa kidogo. Kubwa sana kiasi cha kushindwa kukaa kwenye mfuko wa nguo, na ndiyo maana linahitajika begi. Betri linawekwa chini ya begi, ambapo waya zinatokea humo hadi kwenye swichi.
Abiria namba nne alikuwa amevalia begi kubwa jeusi alilokuwa amelikumbatia kwenye mapaja yake. Kwa namna nilivyokuwa nimekaa, basi lilionekana tupu isipokuwa ni kama lilikuwa limebeba kitu kimoja kikubwa sana. Akili zangu ziliniambia ni betri la bomu tu!
Hatimaye treni lilisimama mtaa wa 28. Nilikuwa natakiwa nishukie hapa, lakini nilitulia tu milango ilipofunguka. Hakuna abiria aliyepanda. Hakuna abiria aliyeshuka. Milango ilifungwa na safari iliendelea.
Pointi namba 11: Mikono ndani ya begi.
Miaka ishirini iliyopita ndiyo pointi namba kumi na moja iliongezwa kwenye orodha. Kabla ya hapo kulikuwa na pointi kumi tu kwa wanawake. Lakini dunia inabadilika kwa kasi sana. Yaani tendo halafu mwitikio... Jamii ya waisraeli na watu makini waliiongeza hii kanuni. Kwanini? Kwa sababu mshukiwa wako angefanya maamuzi ya kujilipua usingeweza kukimbia. Hakuna haja kwa sababu hakuna mtu anaweza kukimbia kulishida bomu. Ulichotakiwa kukifanya ni kukimbia na kumkumbatia huyo unayemdhania. Ndiyo! Ulitakiwa kumkimbilia na kumkubatia mtu anayetaka kujilipua halafu kuishikilia mikono yake kwa nguvu ili asibonyeze kitufe. Mashambulio kadhaa yalifanikiwa kuzuiliwa kwa hiyo njia na watu wengi wakaokolewa, lakini haikuchukua muda wataalamu wa mabomu nao wakaja na mbinu yao. Waliwafundisha wanaojilipua kuweka vidole vyao muda wote kwenye kitufe, hivyo walifanya lile kumbatio kuwa butu. Na kwa kuwa kitufe kinakuwa kwenye begi, ndiyo maana inapaswa anayejilipua aweke mikono kwenye begi muda wote.
Abiria namba nne alikuwa ameweka mikono yake kwenye begi alilokuwa amelibeba. Hakuna ubishi juu ya hilo. Vidole vyake vilikuwa juu ya swichi ya bomu hivyo ni kitendo cha kunyanyua juu kidole na bomu lilipuke. Hakuna ubishi juu ya hilo pia.
Gari moshi lilisimama mtaa wa 33. Milango ilifunguka. Hakuna mtu aliyeshuka, ila wakati huu kuna abiria alipanda kwenye behewa letu. Alikuja hadi nyuma ya siti niliyokuwa nimekaa. Niligeuka nikamuangalia. Akili iliniambia nimpe ishara ya kumtaka ashuke ili aendelee kuishi. Lakini sikufanya hivyo. Kwanza, hakuwa ananiangalia na hakuwa hata anajali kama kuna mtu anamuangalia. Pili, ninaijua vyema New York. Kutoa ishara zisizoeleweka kwa mtu ambaye hamfahamiani haswa nyakati za usiku kama huu hakuna umuhimu sana. Hivyo nilitulia tu.
Milango ya treni ilikaa wazi kwa muda mrefu kidogo safari hii. Kwa sekunde kadhaa niliwaza kuwaambia abiria waliokuwemo mule watoke. Lakini sikufanya hivyo! Ingekuwa ni kichekesho. Moja, kulikuwa na vizuizi vingi ikiwemo lugha. Sikuwa najua neno lolote la kihispania, achilia mbali bomu kwa kihispania. Bomba, labda?? Hapana! Bomba ni balbu. Hivyo ningeonekana chizi mbele ya yule mwanamke wa kihispania aliyekuwa amekaa mbele yangu.
Akili yangu ilianza kubishana juu ya neno lipi la kihispania ni sahihi kulitafsiri bomu.
"Bombala." niliwaza. Labda nilikuwa sahihi? Sijui.
Pia sikuwa najua lugha nyingine yeyote ya Albania. Au lugha yeyote ya Magharibi mwa Afrika. Hata hivyo, nilihisi labda yule mwanamke mwenye asili ya Afrika alikuwa anajua kuongea Kifaransa. Na mimi pia naongea kifaransa.
"
une bombe. La femme la-bas a une bombe sous son manteau." "
Yule mwanamke pale ana bomu amevaa ndani ya mkoti wake." Ajabu nilipomuangalia yule mwanamke wa KiAfrika alikuwa amelala, ingekuwa namsumbua tu. Mwisho wa siku niliendelea kukaa kwenye kiti changu. Milango ilifungwa. Safari iliendelea.
Nilibaki namshangaa abiria namba nne. Akili yangu ilianza kuona picha ya mkono uliokuwa ndani ya begi alilokuwa amebeba. Nilianza kuona mkusanyiko wa nyaya nyingi zilizozunguka ndani ya hilo begi. Nilianza kuwaza nguvu ya bomu la Dynamite.
Kikawaida, umeme unasafiri kwa kasi sana karibu sawa na kasi ya mwanga. Kwa nguvu ya bomu kama la Dynamite ukihusanisha na mazingira ya gari moshi tulilokuwemo wote tungelipukutika tukawa vumbi ndani ya sekunde tu. Hakuna masalia ambayo yangebaki. Sana sana mifupa midogo zaidi kwenye mwili wa binadamu iliyopo kwenye masikio (anvil na stirrup) ndiyo ambayo pengine ingeponea chupu chupu.
Nilibaki kumuangalia yule mwanamke. Hakukuwa na namna ya kumfikia. Kwanza, alikuwa umbali wa takribani hatua thelathini kutoka nilipokuwa nimekaa. Kidole gumba chake, bila shaka, kilikuwa juu ya swichi kwa nchi chache tu. Nafasi zake za kuumaliza mchezo zilikuwa kubwa kuliko nafasi nilizokuwa nazo kuutuliza. Alikuwa tayari. Mimi sikuwa tayari.
Gari moshi iliendelea kuchana mawimbi. Mlio wake wa injini uliobishana na upepo ulianza kusikika masikioni mwangu.
Nilianza kujiuliza maswali mengi. Mpango wa yule mwanamke ulikuwa nini?? Kama lengo ni watu, huko tulipokuwa tunaelekea hakukuwa na mkusanyiko wa watu wengi kwa masaa yale. Ukizingatia night club nyingi tulikuwa tumekwishazipita.
Nilibaki namtazama tu kwa macho ya mkazo. Mkazo mwingi hadi alihisi kitu.
Aligeuza kichwa chake taratibu kuniangalia kama aliyekuwa akiendeshwa na rimoti.
Macho yetu yaligongana. Uso wake ulibadilika... Alikuwa amejua kuwa nimemgundua!
SEHEMU YA NNE:
BOFYA HAPA.