Riwaya--Kaliii

umeipenda....

  • hapana

    Votes: 0 0.0%
  • hayakuhusu

    Votes: 0 0.0%
  • acha kihelehele

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    1

kapesly

Senior Member
Jan 1, 2017
163
108
Mtunzi:Mulabha
Msambazaji:Kapesly (Mimi)
Phn:
0-655-777-272
Kama umevutiwa nayo unaweza nniambia, your reply my responseee


Mwanzo
Nimajira ya jioni ivi, gari aina ya benz nyeusi, inaonekana ikilandalanda maeneo jirani na Benki Kuu ya Taifa hapa nchini (BOT), ndani ya gari hio wanaoneka akna Jonathan, Kenn, Joven, Isack, Paul, Kizito na Mamba, wote wakiwa na karatasi zilizo na ramani ya benki hio. Mida ya saa moja ivi, Jonathan akachukua simu yake ya mkononi alfu akabonyeza namba kadha, kisha akaiweka simu Sikioni
"Jonathan, sasa mnaweza ingia ndani ila hakisheni kila mmoja wenu anavaa, kifaa chake cha mawasiliano" aliongea jama niliyempigia, nakunifanya nami nitoe amri hio haraka kwa wenzangu
"Jamani twenzetuni, kila mmoja ahakikishe amevaa mawasiliano yake" nilizungumza kwa sauti ya juu kidogo
"Johnathan, wamesema wameshaseti kila kitu tiyari" alizungumza Kenn, huku usu wake ukionyesha wasiwasi sana katika tukio tunalokwenda kulifanya muda mfupi ujao
"yaaah, kila kitu wameseti, thusway wamesema tuingie ndani, Sikieni tunadakika thelathini tu za kufanya kazi yetu" Niliongea, kisha kila mmoja akaanza kuvaa nguo za kujisitiri na mambo tuyoweza kukumbana nayo katika kazi yetu tunayoenda kuifanya

Wote tulivyo maliza kujipanga tiyari kwa kazi nzito tunayoelekea kuifanya Katika Benki yetu kubwa hapa nchini, tukashuka ndani ya Gari nakuanza kuelekea usawa na ilipo benki hii, tulivyoifikia ilipo kila mmoja akaelekea njia yake, Hatukutaka kupitia njia kuu ya benki hii kwa sababu ya majukumu tuliyokuja kuyatekeleza ndani humo, uzuri ni kwamba kila mmoja alikua amesoma ramani ya njia atakayo pita. Mimi binafsi nilipita njia iliyokua nyuma ya benki, katika milango ya dharula waitumiayo wahudumu pindi likitokea tatizo, japo ilikua imefungwa kwa lock maalumu lakini niliweza kupita salama salmini kwasababu mfumo wa mawasiliano wa benki ulikua umekwishwa kuharibiwa na Mkuu wetu wa mawasiliano ambaye ndiye aliyenipa ruhusa ya kua tuingie ndani, Mfumo wa mawasiliano wa benki hii uliharibiwa kwa dakika zipatazo arobaini na tano, muda huo wote hakuna mtu ambaye angeweza kutuona, kwakua hata Cctv Camera zilikua hazifanyi kazi kama inavyotakiwa. Kwakua hatukua na muda wa kupoteza nilitembea harakahara mpaka sehemu ya hazina kuu ya Benki hii ya taifa, Macho yangu yalinitoka kama Bundi mara baada ya kuona pesa nyingi mahala hapa, palikua na hela za mataifa tofautitofauti, hela kama dolla, yen, kwacha, uro, shilingi ya hapa nchini nazingine nyingine
"Tiyari nimeshafika ila wenzangu bado siwaoni?" nilizungumza kwa kutumia kifaa maalumu kinachotuunganisha na mkuu wetu wa mawasilano
"Okey, Jonathan hapo ndani ya Hazani mna lidude flani, kubwa hivi nenda hapo utaona kila kitu kisha fwata maelekezo watakuja tu, kwasababu milango waliyopita wao nimeshindwa kuharibu lock zake" alizungumza Mkuu wetu katika kitengo cha Mawasiliano, nami sikufanya makosa nikaliendea dude lilo kubwa humu ndani ya hazina, nakweli maana katika kifaa hicho nikaweza kuona jinsi benki yote ilivyokaa tena nikaona mpaka sehemu walizokwama wenzangu, kupitia kifaa hicho ambacho ni lidude likubwa nikafanikiwa kufungua milango walioyokwama wenzangu.

Kumbe hata hawakuwa mbali, maana nilivyofungua tu milango hio nao wakatokeza, kila mmoja wao akashikwa na bumbuwazi mara baada yakuona jinsi hazina ya nchi yetu ilivyopambwa na hela nyingi kiasi hicho
"Jamani tuanze kazi yetu, hatuna muda wa kupoteza hapa" nilizungumza mara baada ya kuona jinsi wenzangu walivyozuba mara baada ya kuona mpunga
"walisema tuchukue zipi? Sasa Mkurugenzi" Mamba aliniuliza swali hilo
"hapa hatuchagui kitu, ila dolla ndio ziwe nyingi" nilimjibu, kisha kila mmoja akachukua begi yake alikoificha, tukaanza kuchukua hela za nchi utafikiri tumeruhusiwa kuzichukua, kila mmoja alivyohakikisha amechukua kiasi cha kutosha akasimama ili kusikiliza utaratibu unaofwata
"nadhani kila mmoja anaikumbuka vizuri ramani ya njia yake, hivyo basi tutatoka kama tulivyoiingia humu ndani, tunadakika kumi na tano tu humu ndani" nilizungumuza huku nikawa nawaangazia macho yangu, kila mmoja wao alikua haamini kama ndo tunataka tutoke tena bila kutambulika ila mimi kwa uzoefu wangu niliona ni hali ya kawaida tu, ambayo inakwenda kukamika muda mfupi ujao.

Mmoja mmoja akaanza kutoka kuelekea mlango wake aliopitia wakati anaingia humu ndani, nami ndo nikawa wa mwisho nikipitia njia yangu, njia tulizopita wote zilikua ni njia za dharula, ambapo haikuwa rahisi kutambulika. Dakika chache wote tukawa tumetoka ndani ya Benki kuu ya Taifa hapa nchini, tukiwa tumelitia hasara kubwa Taifa letu, tukaelekea mahala ilipo gari yetu, tukaingizi begi zetu zilizojaa pesa, kila mmoja alivyomaliza kuweka tukaanza kupongezana.
"daaah! Yaani hata siamini, kazi njema sena hii jamani" kila mmoja alitamka maneno hayo kwa mwenzake wakati anamkumbutia, Tukiwa hapo nje kwenye gari letu, Tumejidai kwa kufanikiwa kutoka salama salimini ndani ya benki, Mara tukaona deffender tano za polisi zikija mkuku mkuku mahala tulipo, jambo lililotuogofywa sana
ITAENDELEA

 
Yaani Mkuu Nimepaki Kamkokoteni Kangu Ka Urithi Nisome Kwa Raha Hujarudi Tu? Ngoja Nikusomee Albadir Ya Kilingala Tomboka Lisolo Ezali Na Yo Ngai Mawa Ekelamu Pona Ye Na Mee Motema Nalingi Yo Esali Pona Nde Oh Ya Nani Nakotuma Mondelle Zuwaka
 
Nasubiri nikiona 'MWISHO' ndio nitatoa maoni yangu... hilo neno 'itaendelea' nina allergy nalo...
 
Yaani Mkuu Nimepaki Kamkokoteni Kangu Ka Urithi Nisome Kwa Raha Hujarudi Tu? Ngoja Nikusomee Albadir Ya Kilingala Tomboka Lisolo Ezali Na Yo Ngai Mawa Ekelamu Pona Ye Na Mee Motema Nalingi Yo Esali Pona Nde Oh Ya Nani Nakotuma Mondelle Zuwaka
Hapana ina endelea
 
Hapana ina endelea
Mtunzi:Mulabha
Msambazaji:Kapesly (Mimi)
Phn:0-655-777-272
Kama umevutiwa nayo unaweza nniambia, your reply my responseee











Mulabha
Msambazaji:Kapesly (Mimi)
Phn:0-655-777-272
Kama umevutiwa nayo unaweza nniambia, your reply my responseee

Tukiwa tumejidai nje ya gari letu, mara baada ya kutoka nje ya benki salama salimini tukaona deffender tano za polisi zikija mkuku mkuku mahala tulipo, jambo lililotuogofya sana mimi na wenzangu
"Itakua wameshatushitukia mkuu!" aliongea Joven akiwa amejawa na woga sana, nakunifanya nami nifikilie kwa muda kabla sijamjibu
"hamna kitu kama hicho, naona wapo na mishe zao maeneo haya" niliongea kwa kujiamini kidogo, ili kuwaimarisha hawa wenzangu nilioongozana nao

Kweli bwana deffender hizo zilipita mahala tulipo kwa mwendo uleule wa farasi na sisi tukabaki tukizisindikiza kwa macho mahala zinapoelekea, hali iliyopelekea mimi na wenzangu wote tuwe na furaha ya namna yake
"Jamani hatuna muda wakupoteza hapa twenzetu" niliongea, kisha kukafwatiwa na vitendo
mmoja mmoja akaanza kuingia kwenye gari letu, namimi nikawa wa mwisho kuingia ndani ya gari, naye dereva wetu bwana Kizito hakuwa na hakufanya ajizi akalitoa gari letu kwa wa fujo eneo hili la benki. Muda mfupi baadaye tulifika makao makuu yetu

Claud White House (Ikulu ya Claud) ndiyo yalikua makao yetu makuu, ambayo yailikua ymejificha ndani ya mitaa ya Osterbey jijini dare es salaam, tulipokelewa vizuri sana na mkuu wetu bwana Claud
"vijana wangu leo naona mumefanya kazi nzuri, ndani ya benki ya wahuni" aliongea mkuu wetu bwana claud, huku akionyesha furaha aliyonayo siku hii ya leo
"Ni mambo ya kawaida tu mkuu, subiri mambo yanyoke wewe mwenyewe utafurahi" Nilizungumza maneno haya pindi mkuu aliponipatia mkono wake kunipongeza
"unazidi kunifurahisha Jonathan, naamini tukifanya kazi hii na wewe kwa miaka miwili mbele, nitakua bilionea mkubwa hapa nchini" aliongea claud, kisha akawaita wafanyakazi wake waje kuchukua pesa tulizotoka kuiba benki, wengi wa wafanyakazi wake waliokua ni wasichana warembo mno na wachache wao walikua ni wavulana wadogo ambao bado hawajafunzwa maswala ya wizi ambayo ndiyo mhimiri mkuu wa mkuu wetu claud

Muda wa saa nne usiku, kila mmoja alitawanyika kwenda kulala katika chumba chake ndani ya jumba hili lililojengwa kwa utaalamu wa hali ya juu, mpka bosi wetu akaipa jina la Claud House White (Ikulu ya Claud), kwakweli Mr claud hakukosea kabisa kuipa jina hili kwani ukiingia ndani ya jumba hili unaweza ukahisi upo china ama Uingereza, Kila kitu ndani ya jumba hili kinaendeshwa kwa kutumia umeme na kama umeme ukikata kuna jenereta za moja kwa moja zinazohisi kama umeme umekata nakuendelea kuzalisha umeme bila mtumiaji kugundua kitu chochote (Automatic generator). Geti la nyumba hii limeungunishwa na mashine ambazo zina uwezo wa kutambua gari zote za Mr claud, pindi mashine zikitambua kama gari la Mr claud lipo nje basi geti hujifungua bila ya mtu yeyote kufungua geti hilo, kama sio gari lake basi mashine hizo hutuma taarifa hizo kwenye kitengo maalumu cha mawasilano ndani ya nyumba hii, ambapo kitengo hiki cha mawasiliano hutambua jina la mtu na mutumiaji wa gari husika kisha hurudishe taarifa kwenye mashine kwamba gari lifunguliwe ama lizuiliwe. Kitengo cha mawasiliano huwa na mtu muda wote kwa sababu mawasilano ndio chanzo cha usalama katika shughuli zetu hizi chafu. Nilifika ndani ya chumba changu nikalala muda wa saa nne na nusu usiku

Usiku huu nililala sana tofauti na kawaida yangu kwasababu niliamka muda wa saa moja na nusu, wakati kawaida yangu ilikua ni kuamka muda wa saa kumi na moja kamili asubuhi, utaratibu huu nilijipangia kwa sababu ya shughuli zangu nyingi ninazozifanya. Nikachukua simu yangu mahala nilipoiweka, nikaiwasha na kufungua mtandao wa kijamii wa facebookÂ
"Hela zapotea kimahajabu benki kuu" kilikua ndicho kichwa cha kwanza cha habari nilichokutana nacho kwenye page kubwa ya Mwandishi mahiri hapa nchini Millard ayo, nikacheka kidg kwa sababu nilijua yakua wasababishaji wa tukio hilo ni sisi, sikutaka kuendelea tena kusoma habari zilizopo siku hii kwenye mtandao wa facebook hivyo ikanibidi nitoke (nilog out). Nikatoka chumbani kwangu nakuelekea sebuleni ndani ya ikulu hii ya bwana Claud

Nilishituka kidogo mara baada ya kukuta shughuli mbalimbali zikiendelea sebuleni hapa, nikaangaza macho yangu pande zote za sebule hii nikaona kila mtu yupo bize na shughuliÂ
"Jane kitu gani? Kinaendelea hapa ndani" nilimuuliza binti aliyekua mmojapowapo kati ya watu waliopo sebuleni hapaÂ
"Ooooh Jonathan, kumbe hujui? Leo kuna bonge moja la party humu ndani" alizungumza Jane, nakunifanya nitaharuki kidogoÂ
"sherehe ya nini? Tena Jane" nilizungumza kwa mshituko kidogo
"Bosi ameridhishwa na kazi yenu Jonathan ndio maana ameanda sherehe hii" alizungumza Jane, nakunifanya nimshangae Bosi huyu, nikamuaga Jane kisha nikatoka nje ya Ikulu hii ya bwana Claud. Niliwaza sherehe hiyo itakua ya namna gani? Ila sikuipatia pich, nikaamua kuingia ndani ili nikapate kifungua kinywa, muda wa saa saba sikuamini mambo niliyoyaona, yaani sebule ilikua imepambwa kwa namna ya hajabu
ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom