SEHEMU YA MWISHO...
Shailan, Shakrum wakiwa ndani ya boti
wakimsubiri Jegan, muda wao ulikuwa umefika
wa kile wanachokiita kutoa shukrani kwa
Watanzania , Shakrum alifungua briefcase yake
kubwa na kuanza kubofya hapa na pale akipanga
renji na kila kitu, kisha akawasha kuitafuta sakiti
aliyoitengeneza ndani ya tanki la mafuta lakini
lililojazwa gesi aina ya methane upande mmoja
na mwingine liquefied petroleum gas (LPG),
vyote vilikuwa vimeshindiliwa kwa mkandamizo
mkubwa sana kiasi kwamba zikidaka moto basi
ilo tanki lote lazima ligeuke kombora baya kuliko
kombora lenyewe.
Shakrum alipofanikiwa kupata uelekeo wa sakiti
hiyo na kuanza kuhesabu muda wa kuiwasha ili
itengeneze moto ndani ya tanki hilo, tayari Chiba
alikuwa ameyanasa mawimbi hayo, hivyo
alichokifanya hapo sasa ilikuwa ni jinsi gani ya
kuyakata, ili kusiwe na mawasiliano kati ya vitu
hivyo viwili. Chiba akaendele kucheza na
kompyuta yake, ilikuwa ngumu kuelewa ni nini
anakifanya kwa ni ni namba tu zilizokuwa
zikonekana kupishana na katika kioo cheusi cha
kompyuta. Kwa kutumia program maalum kwa
kazi hiyo ambayo Chiba aliipata wakati akiwa
katika mafunzo huko NASA alifanikiwa
kuyakamata mawimbi yale na kuyafanya
yasitende lililokusudiwa, kisha akaanza kufanya
ukaguzi sehemu mbalimbali za jengo lile.
Oooh shiiit! Shakrum alionekana wazi
kuchanganyikiwa kwa hilo, aligundua kuwa kuna
muingiliano wa mawimbi umetokea, kila
alipojaribu bado alijikuta anakwama, nywele
zikamsimama.
Washenzi wameyaingilia mawimbi yangu,
akamwambia Shailan.
Inawezekanaje? Shailan akauliza.
Itakuwa kuna mtaalam wa mambo haya ndiye
kafanya hili Shakrum akajibu.
Sasa tutafanyaje? Shailana akauliza.
Hatuna jinsi kama inawezekana hapa ni kufika
eneo husika na kutumia mbinu nyingine, mbinu
mbadala ya kulipua lile tank bila ya sisi
kudhurika, Shakrum alieleza huku akiisogeza
kompyuta byake pembeni, akakizungusha kiti na
kugeuka walipo wenzake. Mara simu ya Shailana
ikaita, alipoitazama ilikuwa namba ya Tashrini,
akajua mambo yameiva, kwa vyovyote vile.
Ndiyo Tashirini, nipe taarifa, Shailan
alizungumza kwenye simu.
Jegan yuko huru na sasa anatoka gerezani,
nasikia kelele nyingi za wafungwa wengine,
zikimsindikiza nje, Tashrin akajibu.
Mungu mkubwa, kamwe hamtupi mja wake, hii
ndiyo njia pekee ya kuwashinikiza hawa
wanaojipendekeza kwa mataifa ya Maghalibi,
Shailan alijibu huku wengine wote wakishangilia.
Saa 04:00 asubuhi Gereza la Ukonga
JEGAN Grashan aliachiwa huru, hakuwa na pingu
za mikono wala za miguuni. Alitembea kwa
hatua zake mwenyewe ijapokuwa alikuwa na
uchovu kidogo. Madam S na wakuu wengine
waliokuwa pale, walimshuhudia gaidi huyo
akiondoka taratibu katika gereza hilo, akipita
katika mlango mkubwa na kuelekea katika gari la
ubalozi lililoandaliwa huku akisindikizwa na
maofisa usalama wa ubalozi wa nchi yake,
akaingia na kufunga mkanda sawia, akashusha
kioo na kumuonesha Madam S alama hya mkono
akiashiria kuwa amemtukana tusi baya kabisa,
ile gari ikaondoka. Msafara wa gari nne zenye
namba za njano kwenye kibao cha kijani
zililiacha geti la gereza na kushika barabara ya
Nyerere kuelekea mjini.
Kamanda Amata akawasha pikipiki lake na
kuvaa kofia yake ya usalama iliyomficha uso
wake, moyo wake ulijawa na gadhabu ya
kuachiwa huru Jegan, hakupenda hata kidogo.
Liwalo na liwe, akajisemea na kuaca kati yake
na wao magari kama sita hivi kisha akaingia
barabara ni na kuondoka.
Uwanja wa maonesho sabasaba
Gina alisikia mlio wa beep kutoka eneo Fulani
lililokuwa na matanki makubwa kwa ajili ya
maonesho ya kampuni hiyo.
Chibaaaa! akamwita kwa ukelele, Chiba
akaacha kompyuta yake na kukimbilia kwa Gina,
akausikia mlio wa beep hiyo, haraka sana
akapanda juu ya tanki moja na kulifungua kwa
shida mfuniko wake, ule mlio ulikuwa
ukiongezeka. Wakati hayo yakitukia, polisi
waliokuwemo uwanjani wakisaidiana na vijana
wa skauti kutoa watu nje ya uwanja, na
kuwaweka mbali na eneo hilo, vijana wa jeshi
walirudishwa tena kuhakikisha usalama huo.
Chiba alikuwa akifungua ule mfuniko kwa tabu
maana aulifungwa kwa kifungo maalum,
haikuwezekana kukata kwa gesi maana unaweza
ukasababisha mlipuko usio wa lazima.
§§§§§
Kamanda Amata akiwa tayari kwenye pikipiki
yake aliingia barabara ni, nyuma ya msafara wa
gari zilizombeba Jegan, kichwa chake
kilishatawaliwa na gadhabu mbaya juu ya mtu
huyo, hakuamini kabisa kuwa anakuwa huru na
kuacha uovu wake, hapana, bali aliamini wazi
kuwa bado maadamu yupo hai basi ataendelea
kufanya yale anayokusudia kwa raia wengine
wasio na hasira, alivuta mafuta na kutafuta
sehemu nzuri ambayo angeweza kufanya yake,
kufanya lile alilokusudia. Kama unavyojua kasi
ya gari za ubalozi haikuwa ya kawaida, yakiwa
yamewasha vimulivimuli na kupishwa yalikuwa
yakienda kasi kwelikweli. Mara saa ya Kamanda
ikaanza kutoa kamlio hafifu, akauinua mkono na
kuisikiliza inasemaje.
Kamanda Amata, Chiba hapa, alikuwa ni Chiba
aliyekuwa akimpigia Kamanda wakati huo.
Nimekusoma chiba endelea, kamanda aliirusu
simu hiyo.
Nipo, uwanja wa maonesho wa sabasaba hapa
Mtoni Mtongani, akaendelea kusema.
Endelea, Kamanda akamruhusu aendelee
kuzungumza.
Kuna aina ya mlipuko ambayo imetegwa hapa,
sasa najaribu kutafuta chanzo lakini naona
kidogo utaalam unaniishia, pamepekuliwa kwa
mitambo ya kisasa lakini hakujaonekana bomu
wala kitu kinachofanana na hicho, nipe aidia
mpya tafadhali, Chiba alieleza lile linalomsibu.
Ok, jaribu kutazama mitungi ya gesi kama ipo
maana nayo inaweza kufanya milipuko mibaya
kuliko bomu lenyewe, hakikisha kwa amri yako
umeclear eneo lote ili kama itabidi kufa basi ufe
peke yhako kama kiapo chetu kinavyosema, niko
njiani kuja huko huko, Jegan Grashan
amekwishaachiwa huru, Kamanda Amata
alimjibu na kukata simu ile kisha akarudisha
mkono kwenye usukani wa pikipiki na kuongeza
kasi zaidi na zaidi, alikuwa akipita gari kwa
overtake za hatari mpaka madereva wa magari
walikuwa wakitukana kila mtu kwa lugha yake.
Dakika mbili baadae aliziona zile gari za ubalozi
zikiwa kasi katika eneo la Karakana karibu na
Tazara, sekunde chacahe akawa ameufikia
msafara huo.
Mtu wenu anaachiwa ninyi bado mnataka
mtulipue, sasa leo ama zangui ama zenu,
Kamanda alijisemea huku akiupita ule msafara
kwa kasi na kuwa mbele yake. Kisha kama mtu
aliyepagawa alikunja kona kali na kuwa mbele
yao, zile gari nazo zikafunga breki kali mbele ya
pikipiki hiyo zikisota na kufanya ukelele mkali
kwa msuguano wa tairi za barabara, gari mbili
za nyuma ziligongana zenyewe kwa zenyewe na
ile ya mbele almanusura imgonge Kamanda
ambaye tayari alikuwa na bastola mkononi,
alikwishaiondoa usalama na alikuwa akiitafuta
shabaha yake anayoitaka. Kidole cha shahada
kikaitekenya ile bastola, risasi tatu zilipasua kioo
na kufumua kifua cha Jegana Grashan.
Muda na saa hiyohiyo
Milipuko mikubwa ilitokea katika maeneo mawili
tofauti, mmoja katika yadi ya Bunju ya
kuhifadhia mafuta iliyokuwa ikimilikiwa na
Scolleti nay a pili yadi ya Mabibo, kwa nukta na
sekunde ileile mabomu yaliyotegwa na Kamanda
Amata yalifanya mambo yaliyokusudiwa.
Mji wa Dar es salaama ulipatwa na hekaheka
siku hiyo kwani barabara ya Ally Hassan Mwinyi
ilifunikwa na gari za zima moto na ile ya
Mandela nayo vivyo hivyo. Moshi mkubwa
ulitanda anga ya Dar es salaam.
Kama walijifan ya wao magaidi basi hawakujua
kama na mimi ni gaidi zaidi yao, Kamanda
alijisemea huku akipita vitongojo vya katikati vya
wilaya ya Temeke, akafika mahali kulikuwa na
nyumba nyingi zilizobanana, Kamanda Amata
alipinda kona na kuingia katika ua wa nyumba
hiyo, moja kwa moja akaiegesha pikipiki yake
kwenye stoo ndogo ya mkaa, akaizima, akina
mama waliokuwa wakifua na kuosha vyombo
walipiga kelele na kuwanyakua watoto wao.
Kamanda Amata akashuka na kuvua ile kofia
ngumu akaipachika juu ya kioo cha kutazamia
nyuma, akavua yale mavazi ya kuendeshea
pikipiki na kuyaweka pale juu, akabaki na suti
safi nyeusi iliyopambwa na tai ya buluu,
hakuongea na mtu alitoka haraka na alipofika nje
alipanda tax aliyoikuta barabarani.
Sabasaba tafadhali, alimwamuru dereva.
§§§§§
Watu wa usalama wa ubalozi walijitahidi
kumsaidia Jegan Grashan lakini walichelewa,
ilikuwa ni mvurugano eneo lote, wamachinga
walikimbia huku na huku , wakiijaribu kunusuru
maisha yao.
Wanausalama wa ubalozi hawakuwahi
kumkamata Kamanda Amata kwani tayari
Alishakwisha waacha mbali. Wakabaki
wakitizamana hawana la kufanya.
Muda si mrefu, Land Cruiser moja nyeusi
ilipunguza mwendo katika eneo hilo la ajali
ambapo polisi wa usalama barabarani alikuwa
tyari yuko kazini na wale maofisa wa ubalozi
wakiwa wamezagaa nje na bastola zao
mikononi. Kioo cha gari ile kikateremka taratibu,
Madam S, akatzama lile tukio, akatikisa kichwa
chake na kupandisha kioo kisha gari ikaongeza
mwendo na kupotelea mjini.
§§§§§
Habari mbaya zilimfikia Shailan na Shakrum
waliokuwa katika boti wakisubiri wenzi wao ili
watoroke na kuwaachia Watanzania vilio vikuu
ndani ya siku wanayoipenda, siku ya Julai saba.
Shailana alihisi kuchanganyikiwa, kwanza kwa
habari ya kifo cha Scolleti, pili milipuko ya yadi
zote mbili, haikumuuma sana kwani si mali yao,
ila hili la kifo cha Jegan Grashan, Shailan na
Shakrum walilia machozi huku wakiwa
wamekumbatiana, na walikuwa hawajui hatima
ya wenzao waliokuwa katika yadi hizo ambao
walikuwa wakiwasubiri pamoja na Tashirni
aliyeleta taarifa hiyo. Shakrum akaiendea
televisheni na kuiwasha, hakukosea, kioo
kilikuwa kimepamba kwa maua ya moshi mzito
na wakati mwingine kwa tukio la Kalakana pale
Tazara, hasira akazima Tv na kurudi kwenye
kompyuta yake, akaketi lakini alipojaribu
kuichezea akakuta imefungwa kwa codes
maalum ambazo hakujua ni nani aliyefunga,
Shiiiiiittttt! akapiga ukelele nan kuipiga ngumi
ile kompyuta.
Shakrum na Shailan hawakuwa na la kufanya,
walitamani waondoke peke yao lakini hawakuona
vema, akaendelea kusubiri wenzao mpaka muda
waliopanga.
Saa 4:30 asubuhi
Simu ya Kamanda Amata ikaita tena wakatyi
akiwa maeneo ya Tandika kuelekea sabasaba,
akaitazama, Madam S, akatabasamu, Lazima
kapata salamu zangu pale barabarani
akajiwazia.
Kamanda, upo wapi? akauliza kwa ukali.
Nipo Sabasaba Madam vipi? Kamanda akajibu.
Hivi we una akili kweli? Madam akafoka
kwenye simu.
Kwanini Madam? Nina akili timamu kabisa,
Kamanda akajibu.
Unajua unachokifanya wewe? Sasa
umeshaharibu na we mwenyewe unalijua hilo,
Madam akaendelea kufoka kwenye simu.
Madam tutaongea ofisini mi nipo kazini kwa
sasa, Kamanda akajibu na kukata simu.
Madam S alikasirishwa sana na kitendo
alichokifanya Kamanda Amata, alipopita katika
eneo lile la tukio na kuona hali halisi alijua wazi
ni Amata kwa sababu alikwishasema mbele yake
na alishakula yamini juu ya hilo. Alijua nini
kinakuja kumkuta Amata, Madam alilia machozi
kwa hilo, alisikitika na kuumia sana, lakini
lilikuwa limekwishatokea, hakukuwa na jinsi.
Aliendesha gari yake taratibu kuelekea uwanja
wa maonesho ya sabasaba.
§§§§§
Chiba alifanikiwa kuufungua mfuniko wa tanki
kubwa la gesi, kosa moja alilolifanya ni kuwa
hakujiandaa kwa hali hiyo, ijapokuwa aliipata
sakiti iliyofungwa chini tu ya mfuniko huo lakini
yeye mwenyewe aliathirika sana na ile gesi
mbaya. Gina alimshuhudia Chiba akianguka
kutoka katika lile tanki kwa msukumo mkubwa
sana, akajishika mdomo kwa kiganja cha mkono
wake, akili ikaja haraka, akageuka huku na kule,
na kuona kabati lenye gas mask, akalivunja na
kuchukua, akaivaa haraka kisha akakimbilia kule
aliko Chiba akiwa na mask nyingine iliyojazwa
hewa ya oksijeni na kumvika Chiba.
Msaada! alipiga kelele ndipo vijana wa jeshi
walipoona jambo lile, nao haraka wakawahi
mask na kwenda kufungaa mfuniko wa tanki lile
kwa tabu sana kwani mkandamizo wa gesi
ulikuwa ni mkubwa hivyo mvujo wake nao
ulikuwa wa nguvu sana. Bkutokana na ujasiri na
ukakamavu wa vijana hao walifanikiwa kuufunga
na kupunguza athari ya gesi hiyo.
Hali ya Chiba ilikuwa mbaya, Gina akamkokota
na kutoka nae katika eneo leneye hewa, kwa
bahati nzurti katika banda hilo kulikuwa na gari
ya wagonjwa iliyowekwa kwa ajili ya maonesho,
kmpakia Chiaba nay eye akaketi katika usukani,
na kuitoa gari hiyo kwa kasi eneo lile huku akiwa
amewasha vingora vyote. Akainua simu na
kumpigia dokta Jasmine. Dr Jasmine
akamwelekeza moja kwa moja ampeleke
hospitali ya taifa Muhimbili, Gina alitoka katika
geti la uwanja huo kwa kasi na kuingia barabara
ya Kilwa kurudi mjini.
Kamanda Amata alipishana na ile gari ya
wagonjwa lakini hakujua kuna nini ijapokuwa
dereva wa gari ile aliweza kumfananisha.
Alikimbia haraka mpaka kwenye banda husika na
kukuta vijana wa jeshi wakihaha huku na huku
kujarib u kudhibiti hali iliyokuwepo hapo.
Kamanda Amata alipofika alizuiwa kupita eneo
hilo lakini kwa kitambulisho chake alairuhusiwa
huku akipewa mask na kuivaa, akaingia ndani ya
banda hilo na kukuta baadhi ya wanajeshi
wakijaribu kutoa huduma ya kwanza kwa
wafanyakazi ambao walikuwamo ndani ya banda
hilo lakini gesi ile iliwaathiri. Kamanda Amata
akaiwahi kompyuta ya Chiba iliyokuwa juu ya
meza Fulani, ilikuwa inaendeleaa na kazi ambayo
Chiba alikuwa anaifanya. Akatazama kwenye
kioo cha kompyuta hiyo, akaelewa kilichokuwa
kinafanyika mara ya mwisho. Chiba kabla
hajaenda kutafuta sehemu ya mlipuko alikuwa
akijaribu kutafuta uelekeo wa wapi mawimbi yale
ya kielektroniki yalikuwa yakitokea, mpaka yeye
anaiacha kompyuta hiyo bado ilikuwa ikiendelea,
Kamanda Amata akasoma nyuzi (degrees)
zilizojiandika, akaelewa, kilikuwa kipimo cha
ardhi katika longitude na latitude, na eneo husika
lililolengwa kadiri ya nyuzi hizo aligundua ni
maeneo ya Kigamboni, akaendelea kuperuzi na
kwa chini kidogo, akasoma kwa makini sana
namba zile zilizokuwa zikibadsilishana hapa na
pale ili kupata uelekeo sahihi.
Kigamboni Kaskazini, akajisemea na kisha
akiinua ile kompyuta na kutoka nayo mpaka nje,
akatzama huku na kule na kuiona gari ya chiba
akaiendea, akaingi na kujifungi ndani yake, kama
anavyofanya Chiba, akaunganisha ile kompyuta
na kijimtambo maalum kilichofungwa ndani ya
gari hiyo, sasa akaweza kusoma eneo halisi kwa
kutumia screen ndogo iliyopo ndani ya gari hiyo,
akaiwasha na kutoka katika uwanja huo,
akachukua simu ya upepo iliyo ndani ya gari
hiyo na kubofya kitufe Fulani.
Madam S, Madam S, akaita kwa mtindo huo.
Nakupata Chiba, madam S akajibu.
Hapana sio Chiba, hapa ni Kamanda Amata,
akamrekebisha.
Nimekusoma nipe ripoti, akaendelea Madam.
Natoka uwanja wa maonesho wa sabasaba, hali
sio mbaya sana lakini Chiba inaonekana ana hali
mbaya ameondolewa na Gina kuelekea
hospitalini, la pili inaonekana kuna jambo
maeneo ya Kigamboni kadiri ya tafutishi
nilizozikuta katika kioo cha Chiba, niko mbioni
kuelekea huko, haraka iwezekanavyo. Kamanda
akabofya kitufe kingine katika redio hiyo.
Umesomeka Kamanda, mama anabadili uelekeo,
tukutane Kigamboni, madam S akamaliza na
kukata ile simu.
§§§§§
Simanzi na majonzi viliwajaa Shakrum, Shailan
na wengine waliokuwa ndani ya boti, ukimya
ulitawala wakati injini ya boti hiyo ikiwa
inaunguruma kwani muda ulikuwa tayari
umewadia wa kungoa nanga. Kutoka mbali
Shailani aliona kitu kama boti ndogo inayokuja
kwa kasi, akachukua darubini na kutazama
hakuamini macho yake kwa kile anachokiona,
Tashrini na wengine wawili walikuwa katika boti
hiyo wakija kwa ajili ya safari. Ingawa wao
walisalimika lakini maumivu makaubwa yalibaki
kwa ndugu yao Jegan Grashan. Dakika tatu tu
ile boti ilifika ukingoni kabisa mwa ile boti kubwa
ya akini Shakrum, wakashuka na kuhamia katika
boti hiyo kisha milango ikafungwa tayari kwa
kuondoka.
Maafa yaliyotokea ni makubwa sana, Tajan
alimweleza Shailan.
Nini? aliuliza Shakrum.
Akiba yote ya mafuta kamanda Amata kalipua
yadi zote mbili hivi tunavyoongea zinateketea
kwa moto. Scolleti amekwishauawa na Yule
mwanamke wa Kihindi, Jegan nae kapigwa risasi
na mtu asiyejulikana, Tajan alitoa ripoti.
Shakrum alikuwa amesimama akimsikiliza, mara
hiyo akajiegemeza katika moja ya nguzo zilizo
katikati ya boti hiyo akiwatazama wenzake hao.
Na mlipuko wetu umetenguliwa kule sabasaba,
wametuweza, kiukweli sikufikiri kama hawa
jamaa watakubali Jegan aondoke hivihivi,
Shakrum alieleza.
Jamani, hapa tumeshacheza pata potea, washa
mashine tuondoke, si ajabu na sisi
wakatukamata hapahapa au wakatushushia
kombola moja tu tukapotea wote, Shaiilan
aliwaeleza wenzake, injini ikawashwa, milango
ikafungwa, kiyoyozi kikaanza kuyoyoza, taratibu
chombo kikaanza kuondoka eneo hilo
kikichanganya polepole na kugeuka kuelekea
upande mwingine, kila mmoja ndani ya chombo
hicho alikuwa tayari ameketi mahala pake
aliyekuwa anafungua kinywaji sawa, aliyesoma
gazeti sawa, tayari walikuwa wamekwishaamua
kuondoka.
§§§§§
OFISI ZA UBALOZI WA KHAZAKISTAN
Gari za ubalozi ziliingia katika kiwanja cha ofisi
hizo, maofisa wa usalama wakashuka na
kuiendea gari iliyokuwa haina kioo, ndani yake
alikuwamoi Jegan Grashan.
Nilijua hawawezi kukuacha hivihivi, alisema
mmoja wa maofisa hao alipokuwa anamvua
bullet proof Jegan.
Dah! Mungu mkubwa, nashukuru mlijiandaa
Yule jamaa alikuwa ananimaliza kabisa, Jegan
alijibu huku akimkabizi Yule mwanausalama lile
koti. Jegan Grashan akateremka garini na
kukanyaga ardhi ya uraiani, kwa hatua za
polepole huku akiwa ameshikwa mkono na
mmoja wa wanausalama ambaye mkononi
mwake alikuwa amekamata short gun
alisindikizwa kuingia ndani ya jengo hilo.
Ni saa nne sasa karibu na dakika arobaini na
tano, boti itakuwa inangoa nanga, kwa vyovyote
vile wao wanajua wewe umekwishakufa, ofisa
mwingine wa ubalozi alimweleza Jegan.
Haina shaka, naweza ungana nao sasa na
kuondoka, asanteni sana, Jegan aliwashukuru
na kuwakumbatia mmoja mmoja, kisha
akakiendea chombo cha mawasiliano na
kuwasiliana na ndugu zake hao walioko ndani ya
boti.
Jegan aliingizwa kwenye chombo maalum na
kufungiwa ndani yake kisha ikabonyezwa swichi
Fulani na chombo kile kikawasha injini zake
ndani ya chumba maalumu kilichojazwa maji
ambacho moja kwa moja kinatokea kwenye
mkondo wa bahari. Dakika moja baadaye kile
chombo kikasukumwa kwa nguvu na kutoka
ndani ya jengo kwa kupitia kidirisha Fulani,
kikapaa na kujibwaga baharini kisha kwa
mwendo wa kasi kikapotelea baharini.
Ndani ya boti saa 4:45 asubuhi
Furaha na shangwe ziliijaza boti hiyo baada ya
kusikia sauti ya mpendwa wao Jegan
ikawahakikishia kuwa yuko hai, hajafa. Furaha
ilikuwa mara mbili ya ile ya kwanza pale
walipokipokea chombo maalumu kilichomhifadhi
Jegan, na walipofungua ndani walimtoa ndugu
yao huyo na sherehe ikawa sherehe, shampein,
risasi za hewani vyote vililindima katika boti
hiyo, nyimbo zikaimbwa na kuchezwa, kati yao
wote hakuna aliyepotea, wote walikutana tena
kama ndoto yao ilivyokuwa.
Nimeachiwa huru, asanteni sana kwa juhudi
zenu za kuishinikiza serikali ya Tanzania,
mmefanya lililo jema hata sasa niko nanyi.
Lakini huu sio mwisho wa mapambano, huu ni
mwanzo, lazima tuikomboe nchi takatifu kutoka
katika mikono ya watu wa Maghalibi na vibaraka
vyao. Nisingeelewa kanchi kama haka ka Afrika
mashariki kajifanye kana sauti ya kupambana na
sisi, dunia yenyewe inapiga magoti mbele yetu,
wao ni nani? Hawakujiuliza kuwa kwa nini
Amerika na washirika wake kama Uingereza,
Ufaransa na wengineo wako kimya? Wote hao
wanajua kuwa freedom fighters tunajua
tunachokifanya wanajua hilo ndo maana walibaki
kimya, Jegan Grashan alitoa hotuba ya nyodo
katika boti na kufuatiwa na nderemo za wafuasi
wake. Hakukuwa na linguine zaidi ya kuondoka,
safari ikaanza taratibu, boti ile ilikuwa ikiambaa
na maji ya bahari ya Indi ikichana mawimbi
kuelekea Mombasa ambako wenzi wao walikuwa
wakiwasubiri.
§§§§§
Kamanda Amata alijirusha majini na kupiga
mbizi, akipita chini kwa chini kuielekea ile boti
ambayo ilionekana kwa mitambo maalumu ya
kijeshi pale kigamboni. Msoma rada alieleza wazi
kuwa walikuwa wakiichunguza boti hiyo karibu
masaa kumi tangu imefika eneo hilo, hawakuitilia
nashaka kwa kuwa ilikuwa ikipepeza bendera ya
ya Tanzania. Siku hii ndipo walipogundua kuwa
haikuwa boti ya kawaida bali imeingia hapo kwa
shughuli maalumu.
Madam S alimtazama Amata akipotelea majini,
nay eye alirudi upande mwingine ambako
kulikuwa na wanajeshi wanamaji waliojiandaa
tayari kwa lolote lile. Kamanda Amata alipewa
maagizo ya kuhakikisha kuwa waliopo
wanakamatika wakiwa hai na uhai wao. Aliifikia
ile boti kwa muda mfupi tu, bahati nzuri
alipoifikia na chombo kilichombeba Jegan
Grashan kilikuwa kikiwasili, aliona pale
kilipoingilia ma yeye akajipenyeza hapohapo.
Wakiwa ndani ya boti wanashangilia ushindi huo,
ndipo Kamanda Amata alipomshuhudia Jegan
Grashan ambaye alijua wazi kuwa amemuua kule
Tazara akiwa hai mbele ya macho ya wengine.
Jambo hili lilimtia hasira na uchungu, akabadili
mpango wake haraka na kujitokeza mzima
mzima. Wakati wao wanapiga shampeini na
risasi za hewani kushangilia ushindi, Kamanda
Amata alikuwa kazimama mbela yao kama
mzuka.
Jegan Grashan, nani aliyekwambia kuwa
utaondoka ndani ya nchi hii ukiwa na pumzi
yako? Kama ulijuwa kuwa umepona sasa ndio
mwisho wa maisha yako, nafikiri hukutaka kufa
peke yako ulikuwa na akili sana na sasa mtakufa
wote pamoja kwa mkono wangu huu, wasalimie
kuzimu, mwanaharamu, mwanadamu ambaye
hukustahili hata kuzaliwa, Kamanda Amata
alishikwa na hasira kali, akisema maneno hayo
hakuna aliyeamini kama mbele yao yupo kiumbe
huyo anayeogopwa kila kona ya sayari yetu,
kabla hawajajiweka sawa wakiwa bado kwenye
butwaa, kichwa cha Jegan Grashan kilifumuliwa
kwa risasi mbili kutoka katika bastola ya Amata,
mara hii alihakikisha anakufa.
Kamanda Amata alijirusha upande wa pili na
risasi yab tatu ikamfumua Yule aliyeshika
shotgun aliyekuwa akimlenga Kamnda, hola!
Alifanikiwa kupiga viti na vyupa vya pombe
wakati Kamanda akijiviringa kuelekea upande
mwingine. Ilikuwa ni hali ya taharuki kwa
freedom fighters.
Muueni shetani mweusi! Shakrum alipiga kelele
huku akitafuta pa kujificha. Tayari watu watatu
walikuwa chini bila uhai.
Jegannnnnn!!!!!! Ilikuwa sauti ya Shailan
aliyekuwa akilia kwa uchungu aliposhuhudia
mwana mapinduzi wao akifumuka kichwa.
Dakika moja baadae wote walikuwa chali
sakafuni, Shakrum alibaki hai kwa kuwa aliwahi
kujificha. Kamanda Amata akatazamana na
Shailan.
Jicho la hasira la Kamanda Amata lilikuwa
likimwangalia Shailan aliyekuwa amemshika
Jegan mfu akilia kwa uchungu.
Kama kuna aliyewaambia kuwa mtaondoka nchi
hii mkiwa hai amewadanganya kabisa,
hamkustahili kuishi wala kuzaliwa, Kamanda
Amata aliongea hayo na kufyatua risasi moja
iliyopiga kifua cha Shailan na kumtupa nyuma.
Alipotaka kufyatua risasi ya pili akajikuta
ameishiwa risasi. Mara akajikuta akidakwa kwa
nyuma, kabla hajakaa sawa, alikabwa shingo.
Amata akafikiri la kufanya kwa haraka, akainama
na kumyanyua huyo mtu na kumbwaga mbele,
Shakrum. Hasira za Amata zikawaka maradufu,
Shakrum akanyanyuka na kumkabili Kamanda
Amata.
Nilikuwa nakutamani sana wewe kiumbe! Na
sasa umeingia mkononi mwangu, sitakupa hata
nukta ya kuomba sala ya mwisho, Shakrum
alimwambia Kamanda Amata, alipomaliza
sentensi yake alimvamia Kamanda kwa jinsi ya
ajabu, akampiga ngwara moja maridadi,
Kamanda alijirusha hewani akaichanua miguu
yake na kuipata shingo ya Shakrum, alimpiga
teke kwa mguu wake wa kulia nyuma ya shingo,
Shakrum aliyumba na kujipigiza ukutani. Akaruka
sarakasi na kusimama wima, akaweka mikono
katika mtindo wa kuvutia wa mapigo ya karate,
Kamnda Amata naye akajipanga kivingine.
Shakrum alitoa mapigo ya kasi mfululizo
kumuelekea Kamnda Amata lakini hakuna hata
pigo moja lililomfikia Amata, mapigo yote
yalipanguliwa kiufundi sana, mwisho wa yote
Kamanda Amata akajirusha sarakasi na kumpa
Shakrum nafasi ya mita kama tano kutoka
kwake. Kwa sekunde chache alizozipata Amata
alijipanga na kupeleka mapigo ya kazi ambayo
yote yalimuioshia Shakrum na kumtupa chini
akiwa hoi.
Mi nilifikiri unajua kupigana kumbe ni
mwanafunzi namna hiyo! Amata alimwambia
shakrum aliyekuwa akitambaa chini huku yeye
akimfuata kwa nyuma.
Ulipigania Jegan kuachiwa huru, sasa wewe
utakaa jela badala yake, Amata alimwambia
Shakrum na kumkamata ukosi wa fulana yake na
kumvuta kwa nguvu mpaka kijana huyo
akakohoa, akamuinua kwa nguvu na kumbamiza
ukutani. Shakrum hakuwa na la kufanya,
Kamanda Amata akatoa pingu tayari kumfunga
Shakrum lakini lo, bomu aina ya grunet
lililoondolewa pini ya usalama likaanguka kutoka
mkononi mwa Shakrum na kutua chini
liokadunda mara ya kwanza na likaelekea
kugoinga sakafu mara ya pili.
Shakrum alimshika kamanda kwa nguvu zake
zote.
Hatoki mtu hapa, kama wewe umeua ndugu
zangu, lazima nawe ufe na sisi, Shakrum
alimwambia Amata.
Kamwe haiwezekani! Kamanda Amata akajibu
na kumpiga kichwa cha nguvu kilichomfanya
Shakruma amwachie. Kamanda Amata
hakupoteza sekunde, alikimbia kwa kasi yake
yote, hakukuwa na mlango ila dirisha kubwa la
kioo mbele yake, alichumpa na kutanguliza
kichwa akakipiga kioo nay eye mwenyewe kutoka
nje kupitia hapo. Nyuma yake ulitokea mlipuko
mkubwa, ile boti yote ikateketea kwa moto.
§§§§§
Madam S alijishika kichwa baada ya
kuushuhudia mlipuko ule kupitian chomb o
maalumu katka kambi ya jeshi la wanamaji
Kigamboni.
Oooh! My son! ( Oooh Kijana wangu! ) alipiga
kelele.
Moyo ulimwenda mbio hakujua afanye nini.
Akikumbuka Chiba kaumizwa na gesi, sasa
Kamanda ndani ya mlipuko, Madam S alijikuta
anabaki peke yake, machozi ya uzee
yalimdondoka huku mikono yake ikifunika kinywa
chake kwa uchungu.
Chumba kizima walichokuwa maofisa wa Jeshi
pamoja na Madam S wakishuhudia tukio lile
kilikuwa kimya, hakuna hata aliyekohoa. Madam
S alihisi akishikwa bega. Akageuka na
kumtazama aliyemshika, alikuwa waziri wa ulinzi
aliyefika muda huo katika kambi hiyo ya
wanamaji.
Pole Madam, lakini vijana wetu wamekufa
kishujaa! alimwambia Madam S.
Nani aliyekwambia vijana wangu wamekufa?
madam S alijikuta akipiga kelele kupingana na
kauli hiyo. Mara kelele zikaibuka katika chumba
kile, Madam alipogeuka alimuona Kamanda
Amata akiogelea majini baada ya kuibuka.
Mpe msaada haraka! ilikuwa ni sauti ya waziri
wa ulinzi, na mara hiyo hiyo boti iendayo kazi
ikaanza safari yake na kumfuata Kamanda
Amata.
Madam S alijikuta akifurahi kwa tukio hilo,
hakuamini kabisa anachokiona mbela yake.
Mungu mkubwa! alishukuru.