Riwaya: 'J u l y 7'

Riwaya: 'J u l y 7'

kidi kudi

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
2,630
Reaction score
2,298
JULAI 7

story by richard MWAMBE

Dunia inakumbwa na wimbi la ugaidi,
matukio ya kutisha yanayopoteza maisha
ya walio wengi katika pande mbalimbali
za dunia ikiwemo Afrika hususan
Tanzania. Nchi zinazoendelea
zinajumuishwa kuwa na mahusiano na
mataifa beberu ya Maghalibi.
Idara za usalama za Tanzania
znafanikiwa kumtia mkononi Jegan
Grashan akihusishishwa na mlipuko wa
ubalozi wa USA, Dar es salaam. Swahiba
zake wanaishinikiza serikali imuache huru
kwa kutekeleza milipuko kadhaa, wanaipa
siku saba iwe imekamilisha hilo. Je
litawezekana?
Tiririka na mkasa huu mwingine
unaomhusisha Kamanda Amata.
1
MVUA KUBWA ilikuwa ikinyesha katika jiji la Dar
es salaam, jiji linalosifika kwa joto kali
linalowafanya watu wake kujutia kila siku kwa
nini wanaishi hapo, lakini bado kuhama
hawataki. Radi za hapa na pale ziliendelea
kumulikan ardhi yote ya eneo la Tazara katika
makutano ya barabara zenye majina ya viongozi
wakubwa Africa, barabara ya Nyerere na ile ya
Mandela, umeme ulikuwa umekatika na giza
lilitawala kila mahali jioni hiyo, haikuwa usiku
sana kwani ndiyo kwanza kipindi cha majira
kutoka RTD kilikuwa kikianza, hakuna aliyeweza
kuvuka katika makutano hayo, magari yalijaa kila
upande mpaka kule kwenye service road, kelele
za honi zilitawala na matusi ya hapa na pale,
wengine wakijifanya ndiyo askari kuongoza
magari lakini bado hali ilikuwa tete, si wakwenda
Buguruni, wala Ukonga wote walitua pale, mvua
iliendelea kunyesha kwa fujo na ngurumo
zikitawala.
Katikati ya makutano yale kulikuwa na gari aina
ya Peugeot imesimama hali inaunguruma, dereva
wake alishuka na kupiga kelele za hapa na pale
akiwaomba wengine wampishe lakini hakuwapo
wa kumpisha, kwa hasira yule bwana aliubamiza
mlango wa gari na kujichanganya na vijana
waliojaa eneo lile, haikupita dakika mbili mlipuko
mkubwa ulitokea katika gari ile, anga lote
lilifunikwa na rangi nyekundu iliyochanganyika na
moshi mweusi, watu walitawanyika huku na kule
wengine wakitokea katika madirisha ya daladala,
ilimradi tu kujiokoa. Vilio vilisikika huku na kule
watu waliumia sana na wengine kupoteza
maisha, gari zaidi ya ishirini zilidaka moto eneo
lile.
Gari za zimamoto kutoka kampuni binafsi na lile
la jiji yalifika huku polisi wa kutuliza ghasia
wakiwa tayari kusaidia majeruhi kuwakimbiza
hospitali ya Dar Group, Temeke na wengine
Muhimbili moja kwa moja, kazi ilikuwa ngumu
kwa kila mtu aliyekuwa pale, wananchi wote
walisogezwa mbali na eneo la tukio ili kupisha
shughuli za uokoaji. Baada ya takribani dakika
arobaini na tano gari ya jeshi ilisimama karibu
kabisa na jengo la S.S Bakhresa, wakashuka na
vifaa vyao kuelekea pale palipotokea mlipuko
walilizungushia gari lile utepe maalum na
kukusanya kila kilichoonekana na uhusiano na
mlipuko ule kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Hali
iliendelea kuwa tete eneo lile kila mtu alilia
kivyake.
* * *
“Ingia kaka, umemaliza kazi” bwana mmoja
alisema huku akiufungua mlango wa Toyota
prado na kumruhusu huyo aliyemwita kaka
kuingia kwenye gari hiyo, kasha ikageuza na
kuchukua barabara ya Mandela kuelekea
Buguruni.
“Bado, kazi ndiyo kwa nza inaanza” yule bwana
aliwaeleza wenzake huku gari ile ikitokomea kwa
kasi maeneo ya Sukita kuielekea Ubungo.
“Hii ni vita ya tatu ya dunia, na tunaiendelezea
hapa Tanzania, kwa kuwa ulinzi wan chi hii
hauko makini” aliongea bwana mmoja
aliyeonekana kama ndiyo kiongozi wao.
* * *
Mlio mkali wa simu ulimshtua madam S
usingizini, alisonya na kuiinua simu ile huku
akiwa bado kitandani mapema namna hiyo.
“Hey, nani?” aliuliza kwa hasira.
“Madam S, washa runinga yako TBC kasha
nitakupia baadaye kidogo” sauti ya upande wa
pili ilitoa ombi, madam S bila kuchelewa
aliichukua rimoti na kuiamuru runinga ile kufanya
kazi. Alipigwa na butwaa na moyo ukaanza
kumuenda mbio, ukizingatia na umri nao ulikuwa
umekwenda, aliifutailia habari ile, na kwa mbali
macho yake yalianza kujaa machozi. ‘Oh my
God’ alijisemea moyoni, ‘Nini tena hii?’ alijiuliza
mwenyewe wakati akimfuatilia Grace Kingalame
akitoa maelezo ya moja kwa moja kutoka eneo
la tukio. Madam S alinyanyuka kitandani na
kuutafuta mlango wa bafu, baada ya kujiweka
sawa alivalia suruali yake nadhifu na fulana yake
nyeupe iliyoandikwa Naipenda Tanzania , na juu
yake alijitupi kijikoti cheusi, bastola yake
aliipachika sawia katika mkanda wa suruali
aliyovaa na kutoka moja kwa moja aliiendea gari
yake aina ya Toyota Spacio na kuondoka
akiiacha nyumba yake ikibaki na mlinzi tu. Njia
nzima madam S alikuwa akilaani kilichotokea
hapo Tazara, kama kawaida yake alitamani huyo
mtu amkamate mara moja ili amuoneshe
shughuli nene kwa kufanya jambo kama hilo.
Alifika eneo la tukio na kukuta shughuli
zikiendelea hasa zile za uchunguzi, pale
alikutana na wakuu wa polisi na vyombo vingine
vya usalama kila mmoja akiwa hana la kusema
juu ya tukio hilo, laana za kumlaani aliyetenda
hilo na vizazi vyake vyote ndizo zilikuwa
midomoni mwao.
“Atakamatika tu” Madam S alimwambia IGP
walipokuwa katika mazungumzo huku
wakiangalia shughuli ile ikikaribia kufika
ukingoni.
Madam S aliinua simu yake na kuitazama,
ilikuwa yapata saa tano usiku, aliwaaga wenzake
na kuondoka eneo lile mara moja huku akiwa na
mawazo lukuki kichwani mwake.
Siku iliyofuata
“Miranda!” sauti nzito iliita kutoka mlango wa
pili, ilikuwa ni sauti ya waziri wa ulinzi ambaye
ndiyo kwanza alikuwa akiingia ofisini kwake
asubuhi hiyo. Miranda alitii wito huo mara moja
alikiacha kiti chake na kuufuata mkango mkubwa
wa kioo uliokuwa kushoto kwake na kuufungua.
“Nimefika mzee!” aliitikia. Bwana Sixtus Maige,
waziri mwenye dhamana ya ulinzi katika serikali
ya Tanzania aliinua sura yake iliyoonekana
usawajika kwa mawazo na kujawa mikunjo ya
hasira na uchungu.
“Naomba uniitie Madam S, kitengo maalum
usalama wa Taifa tafadhali, fanya hilo sasa hivi”
aliamuru na Miranda mara moja alitii agizo
alilopewa. Ndani ya ofisi yake aliandika fax ya
haraka na kuituma kunakohusika, kisha akatulia
akiendelea na majukumu yake mengine.
Dakika kumi na tano zilikuwa nyingi, mlango wa
katibu muhtasi wa waziri wa ulinzi miss Miranda
ulifunguliwa na mwanamama wa makamo
aliingia ndani na kumtazama binti yule aliyekuwa
anajitazama kwenye kioo huku akipaka rangi ya
mdomo. Miranda alistuka aliposikia mlango
ukifunguliwa na kugeuka haraka.
“Nimepata ujumbe msichana, mzee yupo?”
madam S aliuliza na Miranda bila kujibu
alimuonesha ishara ya kuingia katika ofisi ya
mheshimiwa.
“Karibu sana madam S, nilikuwa nakusubiri kwa
hamu kubwa, kwa kukuona tu nahisi kazi
imekwisha” waziri wa ulinzi mheshimiwa Maige
alimkaribisha mgeni wake na kumuonesha kiti
cha kukaa naye bila kusita akafanya hivyo,
kasha mheshimiwa akaendelea, “Madam S najua
wazi kuwa unafahamu lile nililokuitia, sina haja
ya kulieleza maana jana sote tulikuwa kule
Tazara kwenye lile tukio. Wito wangu hapa ni
kutaka kuona pamoja nawe jinsi ya kulimaliza
hili swala na kuwakamata wahusika,
mheshimiwa Rais amesema lifanyike mara moja,
na mi nikaona kuwa wewe ndiye unaejua jinsi ya
kuifanya kazi hii kwa utaalam”
“Ooh mheshimiwa, nimekusikia, nimetafakari
sana juu ya hili swala tangu jana, lakini akili
yangu haisomi”
“Kwa nini?”
“Sasa hivi sina watu, TSA 1 tumetuma huko
China kwa ajili ya ile issue ya madawa ya
kulevya, TSA 2 naye yupo kule Malawi kwa ajili
ya kuweka mazingira tayari kwa ile kazi yetu,
tufanyeje mheshimiwa, serikalai itakalosema sisi
tutatii” madam S aliongea kwa msisitizo
mkubwa.
“Ok! Nimekuelewa vizuri, sasa naomba TSA 1,
kamanda Amata arudi mara moja kwa ajili ya
kazi hii” waziri maige alitoa oda.
“Sawa mheshimiwa, litatekelezwa mara moja”
madam S alijibu kwa heshima.
“Akifika nchini naomba moja kwamoja uje nae
hapa” mheshimiwa aliongeza. Madam S aliinua
mkono wake na kuitazama saa yake kasha
akabonyeza kitufe Fulani na kuendelea
kubonyeza vijitufe vingine juu ya saa hiyo aina
ya casio, kasha akatulia na uendelea na
mazungumzo na waziri Maige wakijadili hali
halisi ya tukio zima lililotukia usiku wa jana.
Hong Kong – China
Cheung Sha beach, Lantau
Kamanda Amata alikuwa juu ya kitanda safi
kilichotengenezwa kwa plastick huku akiwa
amejilaza kifua chake alikiruhusu kipigwe na
upepo wa pwani, akiitazama bahari tulivu
iliyokuwa na mawimbi kiasi, pembeni yake
mwanadada mrembo alikuwa amejilaza pamoja
nae wakiongea mawili matatu.
Baada ya mazungumzo yao yaliyokuwa marefu
kiasi na kujawa na vicheko vya mahaba,
walinyanyuka kutoka kwenye vitanda hivyo na
kuelekea hotelini alikofikia kamanda Amata kwa
ajili ya kuendeleza mazungumzo yao kwa
vitendo. Akiwa anakaribia katika ngazi za
kuingilia mapokezi ya hotel hiyo alipishana na
mtu mmoja aliyekuwa akimtazama sana, Amata
hakumtilia maanani mtu huyo, mkono wake wa
kuume ukiwa kiunoni mwa mwanadada akili yake
isingeweza kuwa makini tena katika jambo
lingine. Walipanda ngazi kadhaa na kuufikia
mlango wa chumba chake, Amata alikitazama
kitasa cha mlango ule na kumrudisha kwa
nyuma yule mwanadada kisha akatumbukiza
ufunguo wake na kuufungua ule mlango, kwa
hatua za hadhari aliingia ndani ya chumba ile,
aliangaza huku na huku lakini hakuona dalili ya
mtu ndani mle, lakini kila alipopiga hatua kwenda
ndani alihisi damu ikikimbia na nywele
kumsimama, alisogea kwa ndani ili kwenda
kuichukua bastola yake aliyoificha chini yam to,
hamad! Teke la nguvu lilitua tumboni mwake,
kwa wepesi wa hali ya juu, Amata aliudaka ule
mguu upande wa kanyagio na kuuzungusha kwa
nguvu mpaka akauvunja, yowe la uchungu
lilimtoka yule mtu, Amata alimsukuma na
kumbamizia ukutani, akageuka nyuma haraka
kumtazama yule mwanadada ndipo alipokutana
na bastola iliyokwishatolewa usalama ikiwa
mikononi mwa yule mwanadada ikimlenga yeye,
Amata alijirusha kwa haraka na risasi iliyotoka
ilichimba ukuta, kwa haraka aliuzungusha mguu
wake na kumpiga ngawala safi yule mwanadada
ambaye alipaa juu na kutua katika meza kubwa
ya kioo huku bastola ikimtoka mkononi, iliokotwa
na kamanda Amata na kushikwa barabara
mikononi mwake. ‘Sina muda wa kupoteza,’
alijiwazia na kuifyatua ile bastola, risasi moja
alifumua kichwa cha yule jamaa na nyingine
ilizama moyoni mwa yule mwanadada,
‘Wanaharamu’, mara akasikia kamlio kadogo
kama ka mashine ya typewriter kakilia kutoka
katika kitu kama kitabu juu ya droo ya kitanda,
alikawahi na kutoa kijikaratasi kirefu kilichokuwa
na maandishi machache.
“Hali siyo nzuri, rudi haraka mgonjwa anahitaji
msaada wako, Tena Sana Aisee” alikirudisha kile
kikaratasi katika ile notebook bandia kumbe
ilikuwa ni fax mashine akaifungua tena ile fax
machine yake na kurudia kusoma kile kikaratasi,
akabaki akishangaa ‘Nini kimetokea?’ alijiuliza
kwa kuwa kazi aliyotumwa huko ilikuwa ndiyo
kwanza imepamba moto, alinyanyauka na
kufungua kabati la nguo kasha akapaki kila kitu
begini, alipokamilisha akaitazama ile miili ya
wale viumbe wawili waliotaka kuiondoa roho
yake, akatoka taratibu katika chumba hicho na
kujipanga kwenda uwanja wa ndege tayari kwa
safari.
Dar es salaam
Kamanda Amata alikaribishwa na vichwa vya
habari vya kutisha katika magazeti siku hiyo,
‘Mlipuko mkubwa waitikisa Dar es salaam’ na
lingine likaandika, ‘Ugaidi waigubika Dar’ , na
mengine mengi yaliandika kila moja kwa jinsi
zake.
Kamanda Amata aliinua uso wake na kumtazama
waziri wa ulinzi kasha akamtazama madam S na
kushusha pumzi ndefu.
“Yes, Kamanda, hiyo ndiyo hali halisi iliyoukumba
mji wetu, taifa lipo kwenye maombolezo ya siku
tatu, bendera nusu mlingoti. Serikali inaiomba
ofisi yenu wewe pamoja na madam S
kuikamilisha kazi hii kwa haraka na ufanisi
mkubwa, tuko tayari kuto msaada wowote pale
utakapoitajika, nawatakia mafanikio mema katika
hili na Mungu awatangulie” waziri wa ulinzi mh
Maige alimaliza rai yake
“Amin!” kamanda Amata alijibu na kumtazama
madam S. akiwa ndani ya suti yake nyeusi
Amata alinyanyuka kitini na kuongozana na
madam S kutoka katika ofisi hiyo, walipita pale
alipo Miranda na kugana nae, jicho la kamanda
Amata lilimtazama kwa tuo mwanadaa huyo
ambaye daima utamkuta akitengeneza kama
siyo nywele basi rangi ya midomo kupitia kijikioo
kidogo alichokihifadhi katika motto wa meza.
“Hata usipojiremba, we bado ni mrembo tu”
Amata alianza uchokozi wa maneno kwa
mwanadada Yule.
“Mmmmm kamanda, kuna warembo nitakuwa
mimi?” alimjibu huku akiyarembua yale macho
yake makubwa, “Nitoe lunch leo,” alitupa ombi
huku akiendelea kujitazama kiooni.
“Usijali, mrembo kama wewe hakuna mwanaume
atakayekunyima lunch, hata dinner kabisa”
Amata alijibu huku akiwa ameushika mlango
tayari kutoka.
Piipiiii, honi za gari ya madam S zilimshtua
kamanda kwenye maongezi yale.
“Unaitwa na mama yako huko uende,” Miranda
alimwambia Amata
“Ok Beibi, nitakucheki mida” alijibu na kutoka
nje.
Aliingia garini na kuketi, kasha akajifunga
mkanda wa usalama.
“Hivi hii tabia yako utaiacha lini? Wengine wake
za watu hao!” madam S alimueleza Amata.
“Aaa bibi, hata mimi mtu jamani” alijibu kwa
utani.
“Shauri yako hivi vingine vitakugharimu sana”
“Shaka ondoa”
* * *
“Hili bomu lilikuwa ni bomu la masaa, bomu
ambalo hutegwa makusudi kwa malengo
maalum, kwa hiyo siyo mlipuko wa kawaida ni
wa kukusudiwa” kapteni Savana alikuwa akimpa
ripoti ya kwanza ya uchunguzi kamanda Amata
walipokutana pale makao makuu ya jeshi
Upanga.
“Kwa hiyo unataka kuniambia mlipuaji alitega
kwa malengo maalum?”
“Ndiyo”
Kamanda Amata alitazama lile faili lililo mbele
yake na kuligeuzageuza. Baada ya mazungumzo
ya kina waliagana na Amata akaenda mahali
pengine kwa uchunguzi. Breki ilikuwa katika
kituo cha polisi cha Tazara kuitazama gari ile
iliyotumika kwa mlipuko ule. Mezani mbele yake
alikutana na ASP Majegero.
“Kuna lolote mmepata kuhusu hii gari iliyobeba
mlipuko?” lilikuwa ni swali la Amata kwa ASP
majegero.
“Aaa hapana ila bado tunaendelea na uchunguzi
ukizingatia gari yenyewe imeungua vibaya
inakuwa ni ngumu kutekeleza hilo kwa wakati”
“Ok, hebu nilione.” Wote wawili walitoka na
kuzunguka uani kuiona gari ile, Amata aliitazama
jinsi ilivyochakaa, aliizunguka na mara
akakutana na kile alichokuwa akikitafuta….
Plate namba ya gari hiyo iliyoungua vibaya kwa
moto, Amata aliing’oa na kuitazama kisha bahati
nzuri namba zake zilikuwa za kugongwa siyo zile
za kupuliza, Amata alisoma namba zile kiurahisi
na kuziandika kwenye kijitabu chake kidogo
kasha akaagana na Yule askari polisi na
kuondoka zake. Breki ya kwanza ilikuwa katika
jingo la TRA pale Samora evenue, alishuka na
kufika mapokezi ambapo aliomba kuonana na
ya kuperuzi katika mtandao wao.
“Kadiri ya namba hii hiyo ni gari inayomilikiwa
na mama mmoja anaitwa Miss Jesca Mdachi”
Yule dada alimjibu Amata.
“Ok, maelezo yake mengine tafadhali” Kamanda
Amata aliomba
Yule mwanadada aligeuka kwenye kompyuta na
kuprint karatasi Fulani akarudi na kumpatia
Amata.
“Kila kitu kimeandikwa hapa” alimwambia Amata
“Ok asante sana mrembo” Amata alishukuru.
“Kuna linguine tafadhali?” Yule dada alihoji kama
kuna lingine anahitaji msaada nalo. Amata
alimtazama Yule dada kwa uchu alivutiwa na
kifua chake kilichobeba matiti yaliyojaa vizuri.
“Hapana kingine zaidi ya namba yako ya simu,
kama upo radhi” Amata alitoa ombi lingine la
binafsi, Yule mwanadada alimtabasamia Amata
kisha akauvuta mkoba wake na kutoa business
card na kumpatia, kisha Amata akaondoka zake.
USIPITWE NA RIWAYA HII SEHEMU YA PILI......
 
JULAI 7 - 02

story by richard MWAMBE


Plate namba ya gari hiyo iliyoungua vibaya kwa
moto, Amata aliing’oa na kuitazama kisha bahati
nzuri namba zake zilikuwa za kugongwa siyo zile
za kupuliza, Amata alisoma namba zile kiurahisi
na kuziandika kwenye kijitabu chake kidogo
kasha akaagana na Yule askari polisi na
kuondoka zake. Breki ya kwanza ilikuwa katika
jingo la TRA pale Samora evenue, alishuka na
kufika mapokezi ambapo aliomba kuonana na
ya kuperuzi katika mtandao wao.
“Kadiri ya namba hii hiyo ni gari inayomilikiwa
na mama mmoja anaitwa Miss Jesca Mdachi”
Yule dada alimjibu Amata.
“Ok, maelezo yake mengine tafadhali” Kamanda
Amata aliomba
Yule mwanadada aligeuka kwenye kompyuta na
kuprint karatasi Fulani akarudi na kumpatia
Amata.
“Kila kitu kimeandikwa hapa” alimwambia Amata
“Ok asante sana mrembo” Amata alishukuru.
“Kuna linguine tafadhali?” Yule dada alihoji kama
kuna lingine anahitaji msaada nalo. Amata
alimtazama Yule dada kwa uchu alivutiwa na
kifua chake kilichobeba matiti yaliyojaa vizuri.
“Hapana kingine zaidi ya namba yako ya simu,
kama upo radhi” Amata alitoa ombi lingine la
binafsi, Yule mwanadada alimtabasamia Amata
kisha akauvuta mkoba wake na kutoa business
card na kumpatia, kisha Amata akaondoka zake.
EPISODE 02
* * *
“Hatutawaacha hai hata mara moja, kila
tutakapoamua kulipua tutahakikisha
tunaua watu zaidi ya hamsini. Kosa lenu
mnalijua, kuingilia mambo yasiyowahusu,
vita ya watu wa Maghalibi na sisi, ninyi
haviwahusu, kwa nini mnaingilia. Sasa
tunasema kwa sauti moja, tutawaua na
tutawaua mpaka mtakapomuachia huru
ndugu yetu Jegan Brashan mliyemfunga
katika magereza yenu huko Tanzania.
Tunawapa siku saba mumuwache huru
zikipita bila kutekeleza mlipuko mwingine
utatokea karibu kabisa na pua zenu…”
Waziri wa ulinzi bwana Maige aliizima cd ile
iliyokuwa ikitoa ujumbe huo katika luninga
kubwa iliyofungwa ofisini hapo, kisha aligeuka
kuwatazama Amata na madam S pamoja na
watu wachache waliokusanyika ofisini hapo
baada ya wito wa dharula kutoka kwa waziri
huyo.
“Hii cd imeletwa na Miranda ameikuta katika
sanduku letu la posta asubuhi hii,” waziri Maige
alilieleza lile jopo. Madam S alitoa kitambaa
chake na kujifuta jasho ilhali hakuwa na jasho
ilimradi tu akili yake ilikosa utulivu.
“Kazi tunayo, tena siyo ndogo” madam S
alisema kwa utulivu.
“Sasa wewe mama ukisema hivyo sisi
tutasemaje?” aliuliza mjumbe mwingine
aliyekuwa katika kikao hicho. Wote wakabaki
kimya kwa muda wakitafakari hili na lile.
“Lakini hawa ni nani? Al Qaeda, Al-Shabab, Boko
Haram au ni nani?” alitupa swali mtu mwingine.
“Mimi na wewe hatujui, ndiyo maana niliwaita ili
ninyi kama watu wa juu wa usalama wa nchi hii
mlipatie ufumbuzi” waziri Maige alijibu.
“Ina maana baada ya siku saba tutegemee
mlipuko mwingine sivyo?” aliuliza mjumbe
mwingine.
“Ndiyo maana yake, hapa hatujui tunapigana na
nani na wangapi na wako wapi, katika medani za
ijeshi tunasema, adui mbaya ni yule aliye ndani
yako. Sasa adui huyu tayari yuko nchini mwetu,
tufanye juu chini kabla ya wiki tuwe
tumefanikisha hilo” Madam S alizungumza kwa
jazba.
“Wanataka tumuachie huru Jegan Brashan na
wao wasitishe malipuzi yao, ninyi mnasemaje?”
waziri aliuliza.
“Dunia itatushangaa sana kwa kufanya hilo,
kumuachia Jegan! Hilo sijahafiki hata kidogo,
tuone kwanza hii wiki moja tunafikia wapi,”
madam S alijibu.
“Kamanda Amata mbona uko kimya sana? Huna
la kuzungumza?” waziri alimuuliza Amata
“Jegan Brashan, hawezi kuwa huru hata iweje,
hata iwe vita ya tatu ya dunia, mimi Amata TSA
namba 1 sitalikubali, labda itoke maiti yake lakini
si yeye kamili” alimaliza kwa kauli tata.
“Amata, unazungumza nini? Tunataka tupate
muafaka wa hili,” waziri Maige alimkaripia
kidogo Amata.
“Kwanza hiyo cd imenipa mwanga, nataka
nianze na Jegan Brashan kisha hapo nitajua
wapi pa kuendelea, naomba mnipe muda wa siku
tano kisha tuone tena pamoja” Amata alimaliza
kusema. Wote waliafikiana nae na kupeana kazi
mbili tatu kisha wakatawanyika.
Gereza la Ukonga
“Jambo afande!” Amata alisalimu
“Jambo!” alijibu askari mmoja liyekuwa getini
akiangalia usalama wa eneo hilo ambalo
limehifadhi watu hatari kwa usalama wa taifa
hili. Aliliendea gari la Amata na kuzungumza nae
machache kisha akafunguliwa geti na kuingia,
aliiacha ile njia inayoelekea chuo cha maafisa na
kukunja kushoto kuufuata mlango amkubwa wa
gereza hilo, baada ya mwendo wa kama mita
mia mbili hivi aliegesha gari yake na kuteremka,
alirekebisha tai yake na kujiweka koti lake vizuri
kisha akauendea mlango ule na kutikisa kichuma
Fulani, mara kajimlango kalikokuwa katikati ya
ule mlango mkubwa kakafunguliwa naye
akajitoma ndani.
“Naweza kuonana na bwana jela?” aliwauliza
wale maafisa aliyowakuta pale.
“Bila shaka, nifuate…”
Kamanda Amata alimfuata yule askari na mara
wakafika kwa bwana jela, yule askari akarudi na
Amata akabaki pale.
“Naitwa Amata,” akajitambulisha na kutoa
kitabulisho chake na kumkabidhi.
“Ndiyo bwana Amata, karibu sana chuo cha
mafunzo, nikusaidie nini tafadhali?”
“Yah nahitaji kumuona mfungwa wa kigaidi
bwana Jegan Grashan, nina mazungumzo nae”
“Bila shaka, je una kibali maalum? Maana huyu
mfungwa hatakiwi kuonana na mtu yeyote wala
kuona mtu yeyote”
“Nimetumwa na serikali, na kitambulisho changu
ndiyo kibali” Amata alijibu kwa tindo huo.
“Ok, ngoja nikupe vijana wakupeleke, ila uwe
makini sana tusije kupata lawama”
Baada ya dakika tatu hivi vijana wanne
waliovalia sare nadhifu ya magereza, wenye
maumbo ya kipiganaji hasa, mabegani mwao
walikuwa na vile vibaka vya kijani, Amata mara
moja alijua wale ni vijana wa kazi KMKGM.
Jegan Grashan, kijana anayekadiriwa kuwa na
umri wa miaka thelathini hivi, alitokea kuwa gaidi
tishio katika ukanda wa Africa Mashariki, akiwa
anafanya kazi na kundi kubwa linaloendesha
shughuli hizo sehemu mbalimbali za dunia.
Alipitia mafunzo ya kijeshi huko Pakistan na
kuwa mpiganaji hodari, lakini baada ya muda
Fulani aliai jeshi na kujiunga na vikundi
vinavyoendesha mapinduzi kwa njia za kigaidi
ndani na nje ya Pakistani mapaka alipojikuta
kwenye mtandao mkubwa na wa kimataifa na
kutekeleza mauaji mengi sehemu mbalimbali,
japokuwa dunia ilikuwa ikimsaka kwa udi na
uvumba huko Mashariki ya kati, kumbe kijana
huyu hatari alikuwa ameweka makazi yake Africa
ya Mashariki katika mji wa Mombasa, Kenya,
wakati dunia imeanza kumsahau kwa unyama
wake, Jegan aliibuka tena mwaka 1998 Tanzania
na Kenya, alipopanga milipuko iliyopishana
dakika kumi tu, ule wa Dar es salaam ulitokea
saa 4” na ndipo dunia ilipostuka na kutambua
kuwa mtu huyu bado yupo asakwe mpaka
apatikane. Ilipita miaka kadhaa serikali ya
Tanzania na Kenya zikishirikiana na shirika la
upelelezi la marekani (FBI) walimtia mkononi
Jegan katika viunga vya mji wa Tanga akiwa
mbioni kutorokea ughaibuni. Ndipo Marekani
ilipowaacha Kenya na Tanzania kuamua hatima
ya mtu huyo, na Tanzania ilimchukua na
kumuweka jela katika gereza kuu la Ukonga
akiwa anasubiri hatima yake isiyojulikana ni lini
ingetimia.
* * *
Jegan Grashan aliketishwa katika kiti cha chuma
huku akiwa amefungwa minyororo madhubuti
katika kiti kile, wale vijana wa KM wa magereza
walitakiwa kusubiri nje ya chumba cha
mahojiano, ndani alibaki Kamanda Amata na
Jegan, wawili tu walioketi kwa kutazamana.
Jegan alimtazama Amata kwa jicho la chuki na
hasira, lakini Amata alikuwa akimtazama kwa
jicho la upendo na ukarimu.
“Jegan, rafiki zako wametuomba tukuachie huru,
upo tayari?” Amata alianza kumuuliza swali la
kizushi.
“Usinifanye mimi mtoto, ninajua leo ni tarehe
ngapi na ni nini kimetukia juzi” Jegan alijibu kwa
sauti ya kukwaruza.
“Ok, je hiyo ndiyo njia ya wao kuomba uwachiwe
huru?” Amata aliendelea
“Naam, na mtakwisha ninyi vibaraka wa
Maghalibi, hii vita hamuiwezi kamwe, wao
wanataka mimi niachiwe huru lakini mimi
nimetumwa kwa Wamarekani nina ujumbe wao
na wao wanaufahamu” Jegan alijibu huku
akimwangalia Amata kwa gadhabu.
“Kwa hiyo ujumbe wao uliusafirisha kwa milipuko
ya mabomu?”
“Ha ha ha ha Kamanda Amata, we ni mtoto
mdogo sana na jina lako tunalo kati ya watu
wanaotakiwa wachinjwe” Amata aliingiwa na
hofu kidogo aliposikia mtu huyu akilitaja jina lake
tena kwa ufasaha.
“Niambie ninyi ni nani na mna uhusiano gani na
vitendo vya kigaidi vinavyosambaa duniani kote
hivi sasa?”
“Usiniambie hujui kitu wewe mwana Intelijensia,
hii ni vita kaka, tunapiga kila walipo adui zetu,
1998 tumepiga pale Dar, ile ilikuwa ni onyo na ile
ilikuwa ni opereshen al – aqsa, ilipangwa kaka,
na ile ya Nairobi ilikuwa ni opereshen kama hiyo,
nakwambia haya yote nikijua wazi hutoyafikisha
popote kaka. Kama wewe ni mwana historia
kumbuka mlipuko wa bomu ulikuwa tarehe 7
august 1998 ambao ilikuwa ni miaka nane kamili
tangu majeshi ya Marekani yaikalie Saudi Arabia.
Una swali lingine?”
Amata alijikuta ameduwaa kwa kuwa mambo
yale hakuwahi kuyaunganisha namna hiyo katika
kazi zake na wala hakujua kama yana uhusiano
mkubwa namna hiyo.
“Swali langu la msingi ni kuwa nani
anayewatuma na kuwafadhili?”
“Kamwe sintokwambia, kwa kuwa haitakusaidia,
lakini kwa kifupi mabosi wenu walioko Maghalibi
ndiyo wanaotutma”
Ilipita takribani saa nzima ya mahojiano kati ya
wawili hawa, kamanda Amata alipata majibu
mengi sana ya maswali ambayo labda
angeyauliza miaka kumi liyopita ila yale
aliyoyataka leo hakuyapata kabisa kwa wepesi.
7 august, 1998
Gari aina ya Nissan Atlas iliyokuwa imepakiwa
mlipuko wenye uzito wa kilogram 900 ambapo
madini aina ya TNT yaliunganishwa na mitungi
kumi na tano ya hewa ya Oxygen na
kuzungukwa na mifuko minne ya amonium
nitrate , kisha waya uliounganishwa kutoka
katika bomu hilo mpaka katika betri zilizokuwa
upande wa nyuma wa gari hiyo na kisha switch
yake kuunganishwa chini ya dashboard ya gari
hiyo. Gari hiyo ilikuwa iliegeshwa nje ya jengo la
ubalozi pale katika barabara ya bagamoyo,
mlipuko wake haukuleta maafa sana kwa kuwa
eneo lile hakukuwa na makazi ya watu jirani
yake tofauti na Nairobi Kenya.
* * *
Ilikuwa ni kizaazaa katika eneo hilo watu
walitawanyika ovyo, vioo vya madirisha
vilivunjika, gari za uokoaji na zile za zima moto
hazikuchelewa kufika, taharuki iliukumba mji
waote wa Dar es salaam.
Jegan Grashan alimaliza kazi yake aliyoikusudia
na bila kuchelewa alipanda boti inayoelekea
Pemba na kutokomea uko akisikilizia ni nini
kitaendelea. Vyombo vya dola vilianza uchunguzi
wake mara moja kutafuta chanzao cha mlipuko
huo, FBI kutoka Marekani nao walifika haraka
sana kusaidia, na baada ya miezi kadhaa Jegan
Grashan alikamatwa na kuhusishwa moja kwa
moja na uandaaji wa milipuko hiyo
(masterminds) , baada ya kesi yake kuunguruma
huko Amerika iliamuriwa arudishwe Afrika
Mashariki na hapo ndipo alipohifadhiwa katika
gereza la Ukonga.
Kamanda Amata aliondoka eneo la gereza kurudi
mjini, aliitazama saa yake ya mkononi,
ilimuashiria kuwa ni saa saba mchana,
alikanyaga mafuta kuwahi mjini kwani alikuwa
na miadi na kimwana Miranda kwa chakula cha
mchana, alipoanza kuteremka mlima wa
magereza kuelekea Banana alisikia kishindo
kikubwa na gari yake ilianza kuyumba kushoto
kulia, alijaribu kuiongoza vema lakini bado
ilikuwa ikiyumba, kutokana na mafunzo yake
maalumu aliyopewa ya kujilinda aliiendesha gari
hiyo kwa umakini mkubwa na alipoweza kuweka
sawa alikutana uso kwa uso na lori la mchanga
kishindo kikubwa kilisikika, gari ya Amata
iligongwa na kukanyagwa vibaya.
Kitendo bila kuchelewa, Subaru moja nyeusi
ilifika eneo hilo na kusimama jirani, watu wanne
walishuka haraka na kuelekea kunako gari ya
Amata, walichungulia huku na huku lakini
hawakuona kitu wala mtu, mara ghafla kutoka
upande wa pili wa gari ile ya mchanga kamanda
Amata alijirusha na kumpiga double kick mmoja
wao ambaye alidondokea katika michongoma
iliyo jirani tu na barabara, kabla hajakaa sawa
tayari Beretta 92 bastola ya kiitaliano ilishafanya
yake na yule mtu kuitwa marehemu, yule wa pili
alijikuta ana kwa ana na kamanda Amata
alijaribu kujitete lakini wapi, mateke ya
kuzunguka ya Amata yalimfanya apoteze
network na kuyumba vibaya alisimama na
kujipanga kimapigano huku wale wenzake
wakitafuta upenyo wa kuiondoa gari yao maana
tayari gari zilikuwa zimejaa eneo lile, alirusha
ngumi ambayo ilikwepwa na Amata, kisha Amata
alijibu mapigo kwa makonde kadhaa ya mbavuni
na kummaliza pumzi, wakati Amata anataka
kupeleka mashambulizi mengine jicho moja
liliwaona wale wanaotaka kutoroka mmoja akiwa
na bastola tayari akimlenga na alipoifyatua tayari
Amata alitoka eneo lile kwa kujiviringa chini na
kupita uvungu wa lori na kuacha risasi ile ikipita
kifuani kwa yule mwenza wao akipaishwa
nakudondoka kama mzigo.
Amata alitokea upande wa pili tayari hima hima
bastola yake mkononi tena alisikia kelele za tairi
ya gari ikijigeuza barabarani lakini walichelewa
bastola ya Amata alipasua kioo cha nyuma cha
gari hiyo na kumjeruhi vibaya mmoja wao lakini
dereva aliendelea kuiondoa gari ile kurudi uelekeo
wa Pugu, kamanda Amata alitazama huku na
huku akamfuata mwanamama mmoja aliyekuwa
hapo na gari yake aina ya Toyota Harrier na
kumtoa kwenye usukani kisha kukaa na
kuiondoa kwa kasi kuifuata ile Subaru. Mwendo
ulikuwa si wa kawaida, walipita mbele ya gereza
la Ukonga na kuelekea pande za Gongo la Mboto,
Amata alifanya juu chini asiipoteze ile Subaru
ambayo ilikuwa ikienda kasi sana huku ikifanya
ovateki za hatari, Amata naye alihakikisha
anakwenda sambamba nalo, walipoimaliza
Gongo la mboto na kuianza Pugu, tayari magari
mengi yalipungua, Amata alikaza mguu na ile
Harrier ilitii, dakika chache tu alikuwa anaikaribia
ile Subaru. Kwa kasi ileile walipandisha mlima
wa Pugu tayari Amata alishaanza kuipita ile
Subaru mara ghafla akanyonga usukani upande
wa kushoto na kuigonga ile gari kwa nyuma
kidogo ya ubavu wake na kuifanya ile gari
kuyumba upande wa kushoto na kupoteza
muelekeo mara ikatumbukia na kubingirika katika
bonde la mlima huo. Amata alishuka katika gari
yake bastola mkononi na kuifuata kule chini
mpaka ilipokwama, alitazama ndani na kumuona
yule dereva akiwa hoi pale kwenye usukani,
akauvuta mlango kwa nguvu na kumtazama kwa
makini yule bwana aliyejiinamia huku usukani ule
ukiwa umembana kifuani, damu zilimtoka
kinywani na puani, hakuna msaada, yule
mwingine tayari alikwishakufa maana alionekana
kuvurugwa kichwa chote kwa risasi ya kamanda
Amata iliyofumua ubongo wake na
kusambaratisha kichwa chake, alimsogelea yule
aliyekuwa dereva wa gari ile na kumtazama
vizuri, akamzaba kofi la shavu lililomfanya
pamoja na maumivu yake kugeuka.
“Ninyi ni nani?” alimuuliza huku akimuwekea
bastola kichwani, yule jamaa alionekana
kutetemeka, “Sema, usipoteze muda!” aling’aka
kamanda Amata huku akivuja damu sehemu ya
paji la uso ambapo palichanika kwa vioo katika
ajali ile. Yule jamaa alikuwa akihema kwa tabu
sana, mara simu ya Amata ikaita, akaingiza
mkono mfukoni na kuitoa alipotazama kwenye
kioo aliona jina la ‘Miranda’ likiwakawaka,
akabonyeza kitufe chekundu na kuirudisha
mfukoni, alipogeuka kwa yule jamaa alimkuta
tayari ameshakufa akiwa
anamwagika povu na damu kinywani. Kamanda
Amata aliirudisha bastola yake mahali pake na
kumpekuwa yule jamaa, bahasha ya khaki
ilikuwa katika mfuko wake, vitambulisho kadhaa
na kadi za kibiashara, alipoona vinatosha
alivihifadhi mfukoni mwake na kupanda kile
kilima kuifuata ile gari aliyoiacha pale juu.
Akajikung’uta vumbi na kujihifadhi ndani yake,
aliiwasha na kuigeuza kisha taratibu kuifuata
barabara ya Nyerere kurudi mjini, mbele kidogo
alikutana na gari za polisi wakamuwashia taa
kwa ishara ya kusimama nae akatii.
Amata alimuona yule mama aliyemnyang’anya
gari akiwa na wale polisi wakimfuata, akashuka
na kuwasubiri.
“Kijana tunakuweka chini ya ulinzi kwa kuwa
umepora gari ya watu na kufanya mauaji” polisi
mmoja alimwambia Amata huku akitoa pingu
zake mfukoni mwake, Amata alinyoosha mikono
yake na kufungwa zile pingu huku shati lake
likiendelea kulowa kwa damu tiririka zilizokuwa
bado zinadondoka kwenye jeraha lake.
Akaingizwa kwenye gari Land Cruiser ya polisi
na kuamuriwa alale chini kisha wale polisi
wakasimama juu yake na ile gari ikageuzwa
kurudi mjini huku polisi mmoja na yule mama
wakiingia katika ile harrier na kuwafuata
nyuma....
UASIKOSE SEHEMU YA 03 YA RIWAYA HII KALI
UJUE NINI KILIENDELEA...
 
JULAI 7 - 03


.....Akajikung’uta vumbi na kujihifadhi ndani
yake, aliiwasha na kuigeuza kisha taratibu
kuifuata barabara ya Nyerere kurudi mjini, mbele
kidogo alikutana na gari za polisi wakamuwashia
taa kwa ishara ya kusimama nae akatii.
Amata alimuona yule mama aliyemnyang’anya
gari akiwa na wale polisi wakimfuata, akashuka
na kuwasubiri.
“Kijana tunakuweka chini ya ulinzi kwa kuwa
umepora gari ya watu na kufanya mauaji” polisi
mmoja alimwambia Amata huku akitoa pingu
zake mfukoni mwake, Amata alinyoosha mikono
yake na kufungwa zile pingu huku shati lake
likiendelea kulowa kwa damu tiririka zilizokuwa
bado zinadondoka kwenye jeraha lake.
Akaingizwa kwenye gari Land Cruiser ya polisi
na kuamuriwa alale chini kisha wale polisi
wakasimama juu yake na ile gari ikageuzwa
kurudi mjini huku polisi mmoja na yule mama
wakiingia katika ile harrier na kuwafuata nyuma.
endelea...
EPISODE 03
Mabatini polisi, Stakishari
“Weka ndani jambazi hili, linapora magari ya
watu tu,” yule polisi alimwambia mwenzake huku
akimsukumia Amata nyuma ya kaunta.
“Vua mkanda, vua viatu uingie pale kwa wakora
wenzio” aliamuru polisi aliyekuwa nyuma ya
kaunta karibu kabisa na WP mmoja aliyekuwa
akiandikaandika katika daftari kubwa, aligeuka
na kumuangalia Amata kwa makini juu mpaka
chini, kisha akasonya.
“Unashangaa nini si umeambiwa uingie huko
ndani” yule WP naye aliongea huku akibetua
midomo yake.
“Tafadhali afande nakubali, ila naomba nimpe
taarifa mke wangu ili ajue niko wapi” Amata
aliomba
“Haya we afande Mary, msaidie ombi lake kisha
aende huko ndani” amri ilitolewa na yule polisi
aliyemleta Amata pale kaunta.
WP Mary alimtazama Amata kwa mara ya pili na
kubetua midomo yake kinafiki.
“Unaomba tu upige simu unajua anayezilipia ni
nani? Haya taja namba haraka watu tuna
mambo mengi,” WP Maria alimueleza Amata kwa
sauti kali, Amata alimtajia namba ile yenye
takribani tarakimu saba, WP Maria alizungusha
tarakimu zile kisha akaweka kile chombo sikioni.
“Haya inaita, ongea haraka,” WP Maria
alimwambia Amata.
“Hello mama, mimi kijana wako, nakupa taarifa
kuwa nimekamatwa na polisi nipo hapa kituo
cha Mabatini Stakishari Ukonga, msaada wako
tafadhari” Amata alirudisha simu kwa WP.
“Ongea na mama tafadhali” alimwambia
“ (…) Ee tumemkamata mwanao we njoo ndiyo
utajua kosa lake, hatuna muda wa kuongea
kwenye simu” WP Maria alimaliza na kukata
simu.
“Haya ingia huko ndani,” alimwambia Amata,
naye bila shida aliingia na kufungiwa selo
pamoja na vijana wa kihuni wa kila aina ndani
humo.
* * *
“Jambo afande!” OCD Masoketi aliwasabahi
polisi waliokuwa katika kaunta ya kituo hicho na
wote wakakauka kwa kusalute kwa mkuu wao
wa kazi, walionbekana wazi kujiweka sawa hapa
na pale maana hawakutegemea ujio huo kwa
muda wa adhuhuri kama ilivyotoke. OCD
Masoketi alisimama karibu na ile kaunta na
kuwaangalia wale vijana walioonekana busy na
kazi mbalimbali.
“Afande, kuna mtu mmemkamata na kumuweka
ndani hapa mida hii?” OCD akauliza
“Ndiyo mkuu, ni jambazi aliyepora gari ya huyu
mama tunayemchukua maelezo sasa,” alijibu WP
Maria
“Mna uhakika gani kama ni jambazi?”
“Kwa maelezo ya huyu mama, ni kuwa gari yake
alinyang’anywa katika eneo la ajali pale karibu
na Banana na kabla ya hapo anasema huyu
mtuhumiwa alikuwa anarushiana risasi na watu
wengine. Na hapa tumemkuta na bastola aina ya
Berreta 92 vyote vimehifadhiwa mkuu” alijibu
polisi mwingine aliyemleta Amata pale kituoni.
“Muwe makini na kazi yenu nyie vijana,
nimeshawaambia mara nyingi jinsi ya kumhiji na
kumchunguza mtuhumiwa, au hamjajifunza CCP?
Haya nifungulieni huyo mtu haraka mniletee
ofisini kwangu” OCD Masoketi aliongea huku
akiwanyooshea mkono uliokuwa na redio call
mkononi. Kamanda Amata alifunguliwa kutoka
selo na kuongozwa na WP Maria mpaka ofisini
kwa OCD.
“Karibu kamanda, keti kitini, WP mletee kinywaji
baridi tafadhali” OCD alitoa oda na kutekelezwa
na WP kwa haraka, huku kichwani mwake
akitafakari ni nani huyu anayeitwa kamanda.
Mazungumzo yalifanyika ofisini mle kwa dakika
chache tu na yule mama alipewa maelekezo ya
kufuata ili kesho yake apewe gari ingine kwa
kuwa ile ilikuwa imeharibika sana upande wa
mbele, baada ya kumaliza kila kitu alirudi kaunta
na kurejeshewa vitu vyake vyote alipovikagua
viko salama, akachomoa kadi yake moja ya
biashara na kumtupia WP Maria.
“Baadae unitafute,” alisema huku akiteremka
ngazi na kusimama kwa muda. Yule mama
aliondoka na tax aliyolipiwa na Amata na
kuiacha ile gari yake pale kituoni, akiwa bado na
mazungumzo na OCD mara freelander ya kijivu
ilisimama kando kidogo ya mti mkubwa uliokuwa
hapo, wakaagana na OCD kisha akaiendea ie
gari na kuingia ndani.
“Amata nini tena? Mbona una majanga kijana?”
ilikuwa sauti nyororo ya Gina, katibu wake
muhtasi katika ofisi yao ya AGI International-
clearing and forwading.
“Ah Gina we acha tu, hebu nipeleke hospitali
kwanza kisha tukapate lunch mahali”
“Kwanza nashangaa kukuona hapa, we si
ulikuwa China!?”
“Nimerudi jana ila sikukwambia makusudi ilikuwa
surpries tu,” kisha wote wakacheka na kugonga
viganja vya mikono yao.
“Haya bwana nimefurahi kukuona tena nilikuwa
mpweke kweli bora umerudi mtu wa kunipa
faraja” Gina aliongea huku akiingiza gari
barabara ya Nyerere na kuiacja ile ya Segerea.
“Mmm unataka nipigwe na Malick?” Amata
akamtania Gina huku wakipotelea mjini.
≈ ≈ ≈
Betram aliinua mkono wake na kutazama saa
yake ilikuwa tayari saa tisa na dakika kadhaa,
akiwa bado amesimama katika dirisha la ghorofa
ya tano akiangalia chini getini labda atawaona
vijana wake wakirudi haikuwa hivyo, moyo wake
ulianza kukumbwa na wasiwasi, alitoka pale
dirishani na kuindea meza kubwa yenye
kompyuta na vitu vingine vya mawasiliano
ambapo kulikuwa na mtu mmoja wa makamo.
“Kaka! Hawa jamaa sidhani kama wamefanikiwa
misson tuliyowatuma naona muda unakwenda,
vipi unawapata kwenye GPS?” Betram alimuuliza
Shakrum mtaalamu wao wa mawasiliano.
“Hapana hata huku siwaoni kabisa nafikiri kwa
vyovyote watakuwa wamepata tatizo maana
hata simu zao hazipatikani kabisa” Shakrum
alijibu, huku akijaribu kubofyabofya tena simu
iliyopo pale mezani akijaribu kuwatafuta swahiba
zao hao. Alipojaribu kupiga ile simu kwa mara
nyingine iliita kwa muda mopaka ikakatika, moyo
ukaanza kumuenda mbio, kabla hajasema lolote
simu ya mezani iliita akainyakuwa kwa shauku.
“Fungua TV yako utazame TBC” sauti ya upande
wapili ilimwambia kisha simu ikakatika. Shakrum
alinyanyuka haraka na kuindea TV kubwa iliyopo
hapo sebuleni na kuiwasha kisha kuchagua ile
channel aliyoambiwa.
“Mama yangu mzazi!” Betram alitamka kwa
sauti huku mikono yake ikiwa kichwani kwa
mshangao, walitazama ile habari ya wakati huo
ikionesha ajali iliyotokea mchana ule na nini
kiliendelea, kisha gari iliyokutwa katika bonde la
mlima wa Pugu na maiti za watu wawili ambazo
hazikutambulika kwa mujibu wa polisi.
“Shakrum, fanya haraka funga vitu vyako
tuondoke hapa siyo pa kukaa tena, twende
Mombasa tukajipange upya tuendeleze kazi yetu,
hatukati tamaa” Betram alimweleza Shakrum
kwa kumsisitizia huku akiingia chumbani kwake
na kukusanya kila kinachomhusu, ndani ya nusu
saa walikuwa tayari kwenye gari yao aina ya
Toyota Prado tayari kwa kuondoka. Mara simu
ya Betram ikaita
“Ee ndiyo tunaondoka sasa na jamaa zetu wane
wameuawa katika sakata hilo wameshindwa
kufanikisha mission yetu (…) yeah nimekusikia
boss, tutakuwa hapo alfajiri ya kesho.”
* * *
Usiku huo Kamanda Amata aliegesha gari yake
karibu na barabara ya kuingia hosteli za chuo
kikuu zilizopo Mabibo, kisha akateremka na
kutembea kwa tahadhari akiufuata ukuta
unaotenganisha kiwanda kimoja na magenge ya
wauza mboga, ilikuwa kama saa nane hivi eneo
lote lilitawaliwa na ukimya wa hali ya huu, watu
walishalala zamani waliobaki nje ni makahaba,
wezi, wachawi na wale tu wenye kazi maalum.
Aliendelea kuambaa ambaa na ule ukuta mpaka
upande wa nyuma na hapo alijikuta karibu na
jingo refu la ghorofa kama saba hivi lililojengwa
ndani ya wigo ule, sauti za watu zilisikika
zikitoka upande wa ukuta ule kule alikotoka, kwa
utulivu mkubwa alijibana kati ya ukuta na nguzo
kubwa ya umeme, hakuweza kuonekana na mtu
hasa kutokana na mavazi yake meusi
yaliyomfanya afanane na kiza cha usiku huo.
Vijana kama watatu walipita eneo lile wakiwa na
vitu mbalimbali wamevibeba huku wakionekana
kulaumiana kwa jambo Fulani, vibaka. Walipopita
tu, taratibu Amata alikwea ile nguzo ya umeme
na kujikuta juu ya ukuta, kisha akatua ndani
taratibu na kuchuchumaa kwa ustadi
uliowafanya walinzi wa eneo lile wasistuke kama
kuna kiumbe kimeingia. Kisha akatazama huku
na huku ili aone wapi pa kuelekea, mlinzi mmoja
alipoenda upande wa pili Amata alikimbia kwa
tahadhari na kujificha nyuma ya matank ya maji
yaliyowekwa pembezoni mwa jengo lile,
alitazama mlango wake wa kuingilia ndani kisha
akauendea na kupachika ile funguo yake maalum
kisha akaingia na kuufunga nyuma yake, ngazi
ndefu zilikuwa zikimsubiri, akapanda ya kwanza
na ya pili akakutana na milango kadhaa, hakujua
hasa mlango gani anaoukusudia, alisimama
kidogo kisha akatoa simu yake na kuipiga namba
Fulani, akasikia mlio wa simu inaita ghrofa ya
juu, akaikata na kutulia kidogo kisha akaendelea
kupanda ngazi hadi gorofa mbili zinazofuata na
kukuta mlango mmoja tu, akatoa funguo zake na
kupachika tunduni alipozungusha tu mlango
ulilegea na kufunguka. Sebule kubwa
lilimkaribisha lililojazwa vitu vya thamani vya
kisasa aliichunguza ile sebule kwa macho kisha
akaenda kwenye meza kubwa iliyokuwa na
kompyuta juu yake akaiwasha na kujaribu
kupekuwa hapa na pale lakini hakuna cha maana
alichokiona, akaiacha na kuingia chumbani
hakuna mtu, akafikiri kwa muda akaona windo
lake alilolitegemea amelikosa akageuka
kuondoka, lakini macho yake yakavutwa na
karatasi moja iliyo chini ya kabati, akaiendea na
kuiokota akaifungua harakaraka ilikuwa ni tiketi
ya ndege ya iliyobeba jina la Shakrum Shakran,
raia wa Khazakistan, aliyeingia nchini siku nne
nyuma kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar,
kamanda Amata aliitia mfukoni tiketi ile na
kutoka katika jengo lile kwa mtindo uleule.


2
Kenya Bay Beach Hotel – MOMBASA
UKIMYA ULITAWALA katika meza moja ya duara
iliyozungukwa na watu takribani saba waliokaa
kwa kutazamana, hakuna aliyeongea kabisa
ilionekana kama wote wamepatwa na mshangao.
Aliyeonakana kama kiongozi wao alikohoa kidogo
na kuwatazama wenzake walioonekana kama
wamegutushwa kwa kukohoa huko.
“Leo ni siku ya tatu tangu tutekeleze ule mlipuko
pale Dar, tunawasikiliza kama watatimiza takwa
letu la kumuacha huru Jegan Grashan, lazima
tumkomboe mwanamapinduzi wetu kwa damu
iwayo yote. Tanzania wametuchokoza, kuwaua
vijana wetu wane kwa siku moja ni dharau
kubwa sana, tutahakikisha tunalipiza kwa mamia
ya damu. Sasa tusuke mpango mwingine wa
kuwamaliza mpaka aikulu yao itikisike kwa hofu”
aliongea kwa jazba na kupiga meza kwa ngumi.
Kila mmoja lionekana kushusha pumzi nzito.
“Mbaya zaidi yaani mtu mmoja awamalize watu
wanne, watu waliofuzu mafunzo ya kijeshi, ya
upiganaji wa silaha na ana kwa ana, bado
sijaamini, Betram, inawezekanaje?”
Betram alitulia tuli hakuwa na jibu la uhakika
kwa maana kama ni taarifa alikwishaifikisha jinsi
ilivyo.
“Aah inaonekana walifanya makosa kidogo, kwa
sababu tulipofika Tanzania kwanza tulianza
kufanya uchunguzi wetu wa wapi pa kuanzia,
tukagundua kwamba kuna mtu wao mmoja
ambaye ni matat sana katika kugundua hujuma
kama hizi, kwa hiyo nikawapanga kumshambulia
na kumpoteza mara moja, lakini ndiyo hivyo
badala yake ni yeye pekee aliyewamaliza wote
wanne.” Betram alijibu.
“Ok, sasa tunabadilisha mbinu, nitakuongezea
wtu wawili wa juu, ambao wao wanaijua kazi
yao sawasawa na hawaweai kufanya makosa
kama hayo. Sasa hebu Shakrum, weka hiyo DV
cam niwape onyo kali” yule kiongozi wao
aliyejulikana kwa jina la Beishal alitoa amri na
mara moja ile mashine ya kurekodia ikategwa
tayari kwa kumrekodi, kama kawaida akavaa ile
sox yake usoni.
“…Imebidi kuwapa onyo hili mapema kwa
kuwa mmetupotezea wapiganaji wetu
wanne ambao mtawalipia kwa damy nyingi
kutoka kwa wananchi wenu wasio na
hatia, tunakuja tena kwa nguvu mpya
badala ya zile siku saba sasa mlipuko
mkubwa muutegemee ndani ya saa 48 tu.
Vijana wetu wane thamani yao ni sawa na
wananchi wenu mia moja, kaeni tayari,
hatutawaacha kwa kuwa mmejiingiza
kwenye vita isiyowahusu, na kwa tukio la
jana mmechokoza nyuki, tutawauwa
mpaka mumuachie huru kaka yetu Jegan
Grashan mpigania haki asiyechoka…”
Kama kawaida yao wakaituma ile DVD kwa njia
ya DHL ili ifike kwa haraka zaidi.
“Betram, nakubadilisha nafasi yako, wewe
utakwenda Somalia na Shailan wa Somalia
ataongoza vita baridi huko Tanzania na vijana
wengine watatu nitawaongeza, mmoja nitamtoa
Mali mwingine Afghan na Pakistan nina uhakika
watamaliza kazi ndani ya wakati kwa mbinu
yoyote ile” Beishal alimaliza na kuwtaka kila mtu
kurejea katika kazi yake na mapinduzi yaendelee
kama yalivyopangwa.
Dar es salaam
Waziri wa ulinzi alionekana wazi akitetemeka
baada ya kuitazama DVD ile iliyowafikia mchana
wa jua kali la saa saba, alishika remote na
kuitoa katika ile mashine maalumu kwa kazi
hiyo, aliirudisha kwenye kasha lake na kuiweka
mezani kisha akamtazama IGP aliyekuwa
ameketi hapo.
“Unafikiri wapi hawa jamaa watalenga kwa
sasa?” sauti ya kitetemeshi kutoka kwa waziri
Maige.
“Aaa hapa nikujipanga kila kona yenye
mikusanyiko ya watu, inabidi CID wetu wafanye
kazi ngumu ya kujichanganya na watu, na sasa
hatuwezi kuilinda Dar peke yake wanaweza
kwenda kulipua Kigoma, hawa jamaa hawana
mana kabisa” IGP alimueleza waziri.
“Mwisho wa yote ni nini?” alitupa swali na waziri
wa mambo ya ndani akajibu.
“Hawa jamaa wana mtandao mkubwa sana, kwa
hiyo kupambana nao inabidi kutumia vyombo
vyetu vyote vya usalama nchini kwa sababu
hujui watatokea wapi.”
Maazimio ya kikao hicho yalipitishwa na kila
kona kulimwagwa polisi wa kutosha na ukaguzi
kila sehemu zenye mikusanyiko ya watu, hakika
hali ilikuwa tete, ilikuwa ni sawa na kupigana na
gizani maana humuoni unayemshambulia,
ilmradi tu kila sehemu kulikuwa na ulinzi wa
kutosha.
≈ ≈ ≈
Amata alishusha simu yake kutoka sikioni na
kuiweka mezani kwake kisha akainua kikombe
cha kahawa na kupiga funda moja. Akavuta
gazeti mojawapo lililokuwa hapo mezani na
kusoma habari nzito iliyobeba kurasa ya kwanza
(good copy) iliyosomeka
‘Magaidi watoa kitisho kingine,
kuishambulia Dar es salaam muda
wowote’
aliisoma habari ile kwa kina sana na kuielewa
vizuri, kichwani mwake mawazo mengi
yalimzunguka akifikiri nini cha kufanya kwenye
sakata hilo wakati wakiwa wamebakiwa na siku
nne tu walizopewa na magaidi wale. Alivuta
kitabu chake cha kumbukumbu na kufungua
karatasi kadhaa alizokuwa akiandika andika na
kusoma mambo Fulani, mara simu yake ikaita,
akainyanyu kwa haraka.
“Yes hello! (…) Ok asante (…) sasa hivi natuma
mtu” aliishusha simu yake na kumuita Gina
ambaye muda huo alikuwa akichapa kazi Fulani
katika computer yake ndogo.
“Niambie kaka” aliitika wito
“Kuna kazi kidogo, nenda pale ofisi za Qatar
airways kuna mzigo watakupatia uniletee
haraka” alitoa maagizo. Gina bila kuchelewa
aliiacha ofisi na kukodi bajaji ili aweze kuwahi
kazi aliyotumwa.
Ofisini alibaki Amata peke yake akiumiza kichwa
kujua jinsi ya kulimaliza swala hilo mara kengele
ya mlango ikalia, akafikiri kidogo na kuivuta droo
yake, akatoa bastola yake aina ya Beretta 92 na
kuitia katika mfuko wa koti huku ameishikilia
tayari tayari maana hakuna kuaminiana nyakati
hizo, aliuendea mlango na kuufungua kwa
tahadhari ya hali ya juu, hakuyaamini macho
yake, mwanadada mrembo alisimama mbele
yake akiwa amevalia vazi refu kutoka juu mpaka
chini, alimtazama Amata kwa jicho la mahaba na
kutaka kuingi ofisini mle, Amata alibaki tu
kumtazama msichana yule aliyekadiriwa kuwa na
umri kama wa miaka 28 hivi.
“Karibu sana, wewe ni nani?” kamanda Amata
aliuliza
“Nimeagizwa kuleta mzigo ofisini kwako, bila
shaka wewe ni kamanda Amata” alijibu yule
msichana. Kengele za hatari kichwani mwa
Amata zikagonga.
“Nipe tafadhali na uniambie ni nani aliyekutuma”
Amata alimwambia.
“Sawa twende ndani,” akisema yule msichana
huku akivuta hatua kuingia ofisini kwa Amata,
Amata alijikuta akimruhusu kupita ofisini kwake
na moja kwa moja akaketi katika kiti
kinachotazamana na kile alichoketi Amata, mara
akasikia mlio wa alarm ukitoka kwenye saa yake
ambayo alikuwa ameivua na kuiweka mezani
hapo kwa muda mrefu. Mlio ule ulizidi kuwa
mkali, Amata akachomoa bastola yake na
kumuelekezewa yule msichana.
“Simama haraka, haraka” alimuamuru. Yule
msichana akataka kuwa mbishi.
“Nitakufumua kichwa chako sasa hivi, shetani
wewe simama” alimuamuru tena na ile saa ilizidi
kupiga kelele kuashiri imeditect aina ya mlipuko
ulio jirani sana na eneo ilipo....
NINI KITAENDELEA?
USIKOSE CHAPISHO LA NNE...
 
CHAPISHO LA 4


Amata aliona anapoteza muda na kifo kilikuwa
dhahiri mbele yake, hakupenda kumpoteza kwa
risasi kiumbe yule mrembo mwenye sura ya
kuvutia, alirudisha bastola yake kiunoni na
kumtandika makofi mawili ya haja mpaka yule
msichana akasimama.
“Vua hilo nguo lako haraka?” alimuamuru, yule
msichana alichomoa bastola kutoka kwenye ile
nguo yake na bila kusita aliiondoa usalama
tayari kufyatua, lakini alichelewa, ticktack
iliyopigwa na Amata iliitoa ile bastola mkononi
mwake na kufyatuka ikiwa hewani, ngumi moja
ya usoni ilimchanganya yule msichana kabla
hajakaa sawa, teke moja lililopigwa nyuma ya
magoti yake lilimfanya apige magoti, Amata kwa
wepesi alimvua lile gauni lake refu kwa kulivuta
juu na kumuacha msichana yule chuchu nje
akibaki na chupi tu. La haula la kwata bomu
lilitegwa kwa saa lilikuwa limefungwa kuzunguka
tumbo lake dogo, likiwa na milipuko kadhaa, na
saa ya kidigitali ilikuwa ikiwakawaka kuonesha ni
dakika mbili tu zilibakia. Kwa wepesi wa ajabu
alichukua kiberiti chake na gazeti alilokuwa
akisoma akaliwasha na ule moshi wake
akauruhusu uwende kwenye sensa maalum ya
kusensi moshi, punde tu kengele kali zikalia
jengo zima na na vifaa maalum vya kumwaga
maji kusaidia uzimaji moto vikafunguka kila kona
maji yalimwagika tayari kuzima moto wowote
ambao upo eneo lile, watu walitawanayika
milango ilibamizwa wote wakitaka kutoka nje
kuokoa maisha yao. Kwa kisu chake cha kukunja
alikata ule mkanda maalum uliofungiwa lile
bomu na kufanikiwa kulitoa tumboni mwa yule
msichana, kwa haraka akatoka nalo likiwa
mkononi kuelekea nje huku akiwapiga vikumbo
watu waliokuwa koridoni wakikimbia kuokoa
maisha yao. Alifanikiwa kufika katika ngazi za
kushuka chini au kupanda juu, aliitazama saa ya
lile bomu ilisoma bado sekude 55 tu, aliingia
kwenye lifti na kuiamuru ipande ghorofa ya juu
kabisa nayo ikatii. Sekunde 40 alikuwa juu
kabisa ya jengo la JM MALL, aliisoma ile saa
hakuwa na ujanja, alijaribu kufanya anachoweza
ilipotimu bado sekunde 2 alilirusha juu lile bomu
na kisha kulala chini, mlipuko mkubwa ulitokea
angani watu waliochini walishtuka hawakujua
nini kimetokea, moshi mzito ulitawanyika juu na
mtikisiko wake ulifanya baadhi ya vyoo vya
madirisha ya majengo mengine kupasuka na
kutawanyika barabarani, watu walikuwa
wakikimbia ovyo huku na kule. Kamanda Amata
aliinuka kutoka pale alipolala na kushuhudia
mshikemshike uliokuwa huko chini, alirudi haraka
kwenye lifti na kuingia kisha kuimauru iteremke
mpaka pale pale alipopandia.
Aliusukuma mlango wa ofisini kwa nguvu na
kuingia kwa minajiri ya kumuwahi yule msichana,
peupe, hakuna msichana wala nguo yake,
altazama huku na huku hamna mtu, aliichomoa
bastola yake na kuwahi chini ya jingo lile
ambapo vurugu kubwa ilikuwa pale katika korido
kubwa karibu na supermarket ya Shopprite,
ailisimama na kutazama huku na kule asimuone,
akasogea karibu na barabara kubwa, barabara
ya Samora, huku na huko alimuona mtu aliyevaa
vilevile akamkimbilia na kumkamata, sio yeye,
Amata alichanganyikiwa, akendelea kusaka huku
na huko, hakuna mtu, kila mtu alimuona kama
amechnganyikiwa.
Gari za polisi zilianza kuingia eneo lile kwa
mbwembwe zikifuatiwa na zile za zimamoto,
tayari askari wa usalama barabarani
walishaifunga barabara ya Samora kuanzia
mnara wa sasa mpaka makutano na barabara ya
Morogoro ili kuruhusu shughuli za uokoaji
kuendelea kama inabidi. Kamanda Amata akiwa
na bastola yake mkononi aliteremka ngazi na
kufika barabarani ambako kulikuwa na vurugu za
watu tu wakikimbia na kukanyagana kelele za
‘bomu, bomu’ zikitawala eneo lote hilo.
Watu wa zimamoto waliingia ndani ya jengo hilo
tayari kwa kazi yao ya uokoaji, watu waliobakia
ndani walikuwa wakitolewa na kupakiwa kwenye
gari za wagonjwa kwa kukimbizwa hospitalia.
Amata alirudisha bastola yake kiunoni na
kusimama sehemu akitazama pilikapilika
zilizokuwa zikiendela huku macho yake yakipepes
kiufundi kuangalia kila anayeingia au kupita eneo
hilo. Moyo ulimpiga kwa nguvu alipoona
wafanyakazi wawili wa zimamoto wakiwa
wamemshika msichana mmoja wakitoka naye
nje katika harakati za kuuokoa lakini cha
kushangaza msichana yule hakupakiwa kwenye
gari la wagonjwa bali walimpakia kwenye gari ya
zimamoto kisha wale jamaa nao wakapanda, ile
gari aina ya Dennis iligeuzwa na kuanza
kuondoka eneo lile ikichukua barabara ya
Samora kuelekea picha ya askari kisha kuifuata
barabara ya Maktaba.
Kamanda Amata aliijua ile ni trick na alijua kuwa
kwa vyovyote ilikuwa ni mbinu ya kumuokoa
binti huyu, hakuwa na muda wa kujiuliza
maswali mara mbili, alitazama huku na huko na
kumuona askari mmoja aliyekuwa na Honda ya
kipolisi 350 CC, alimfata na kumuamuru ashuke
mara moja, kisha akakaa juu ya lile pikipiki na
kuingiza gia ya kwanza, alilizungusha kwa ufundi
mkubwa na kuiacha barabara ya Samora na
kuichukua ile ya Morogoro, alipofika barabara ya
Bibi Titi alikunja kulia kwa kutumia upande usio
sahihi ili kuikabili ile gari ya zimamoto,
hakukosea kwani aliiona ikija upande huo mara
moja akaitoa ile bastola yake ya kiitaliano na
kulenga tairi ya ile gari, shabaha ya kwanza
haikuwa sahihi, dereva wa gari ile aliliona hilo
akayumbisha gari na kufanikiwa kuiepa ile risasi,
Amata aliuma meno, wakiwa jirani kabisa kabla
hajafanya lolote, kishindo kiliskika , pikipiki ya
kamanda Amata ilikanywagwa na
kupondwapondwa kabisa, Amata alijirusha
pembeni upande wa jingo la wizara ya Vijana na
kutua sawia kwa goti moja bastola mkononi,
shabaha ya pili ilipiga tairi ya nyuma na
kuifumua vibaya, ile gari iliyumba barabarani na
kusababisha ajali kadhaa lakini hakuna
aliyefuatilia, jamaa waliijua vyema kazi yao, ile
gari ikaacha barabara ya Bibi Titi pale kwenye
mataa ya DIT na kukunja kulia kuelekea Faya,
kamanda Amata alibaki chini barabarani hana la
kufanya ile lori imeshaondoka, ‘Hayawani
wakubwa hawa’ aliwatukana kimoyomoyo na
kujinyanyua lakini alijikuta akirudi chini na
maumivu makali kwenye bega lake la kulia,
aliiokota bastola yake na kuiweka mahali
salama, watu walianza kujaa wakijuwa kuwa hilo
ni jambazi wengine walitwaa mawe tayari
kumpiga, kamanda Amata aliona hiyo ni hatari,
aliichomoa bastola yake na kufyatua risasi
kadhaa hewani na kuwafanya watu wale
kutawanyika, kwa haraka alinyanyuka pale alipo
licha yakuwa alikuwa na maumivu alijikokota na
kuifikia tax ya jirani na kuomba apelekwe eneo la
tukio na mara yule dereva akfanya hivyo.
≈ ≈ ≈
Madam S, alitulia tuli kama maji ya mtungini
huku akili yake ikizunguka kwa kasi, akitafakari
jaribio lile ambalo kama si Amata basi jengo la
JM MALL lingekuwa likiteketea na kusababisha
vifo vingi hasa cha kamanda Amata ambaye ofisi
yake ya siri iko hapo katika jengo hilo. Hakuwa
anajielewa sawasawa, mbele yake mezani
kulikuwa na mafaili kadhaa ambayo labda alitaka
kuyafanyia kazi au sijui alitaka afanye nini nayo.
Aliinuka na kupekua faili moja baada ya jingine
kisha akachukua moja na na kulitia katika begi
maalum na kufunga ofisi, alijipakia katika gari
yake na kuondoka eneo lile.
Breki yake ilikuwa mbele ya ofisi ya wizara ya
ulinzi, moja kwa moja aliingia ofisini kwa
mheshimiwa Maige na kulitoa lile faili kisha
kulitupia mezani kwa waziri huyo.
“Mheshimiwa, mi naona ili tuifanye kazi yetu
vizuri, muachilie huyu mtu huru” madam S
aliongea kwa jazba.
“Oh! Madam, vipi tena? Mbona hasira mchana
huu?” waziri Maige aliongea huku akiwa
amesimama.
“Hivi leo wangekufa watu mamia, kama si Amata
kufanya aliloweza, msichana yule alitaka kujitoa
mhanga kwenye ghorofa ya ngapi sijui, hapana
mheshimiwa, mpe removal order huyo mtu
atoke arudi kwao”
Juu ya meza ya waziri Maige faili lililoandikwa
‘JEGRAN GRASHAN’ lilikuwa limetulia likisubiri
amri ya waziri ili lifanyiwe kazi. Waziri Maige
aliliangalia faili lile na kutikisa kichwa chake
kuonesha kama hajakubaliana na kitu Fulani.
“Madam!” hili swala lipo juu ya uwezo wangu,
inabidi mheshimiwa Rais ndiye aamue juu ya
huyu mtu kama kutoka au la”
“Mheshimiwa waziri, naomba ulishughulikie hili
haraka iwezekanavyo. Mi nafikiri tukimuachia
huyu, tutakuwa katika hali ya utulivu sana hapo
tunaweza kuwasaka hawa jamaa kwa taratibu tu
mpaka tuwakamate”
Gereza la Ukonga
“Kwa nini watu wako wanafanya milipuko ya
namna hii? Wanafikiri kwa kufanya hivyo ndiyo
tutakuwacha huru?” kamishna wa Magereza
Tanzania alikuwa akimuuliza Jegran, huku akiwa
na jopo la watu wengine, waziri Maige na
madam S walikuwa miongoni mwao.
“Kwa nini mnaniuliza swali kama hili? Ninyi
wenyewe mnajua na wamekwishawaambia
wanataka nini, mkitekeleza wanalotaka mtakuwa
huru dhidi ya mashambulizi haya, msipotekeleza
mtaendelea kuangamia,” Jegran alijibu kwa sauti
yake kavu nay a upole.
“Serikali ya Tanzania inataka kukuacha huru!
Uko tayari?” waziri wa ulinzi bwana Maige
alimuuliza.
“Hata mi nashangaa kwa nini mmenifunga bila
kosa, sina kosa mimi” Jegran alijibu.
“Huna kosa!? Kuulipua ubalozi wa Marekani
hapa nchini si kosa?” Madam S aliuliza kwa
jazba
“Nililipua ubalozi wa Marekani, wangenikamata
Wamarekani, sasa ninyi mmenikamata kwa kosa
gani? Ndiyo maana mnapata misukosuko, na
sasa jiandaeni kwa maangamizi”
Madam S alishikwa na hasira na kuuma meno.
Baada ya mazungumzo hayo na tayari
wakikubaliana kumuachia huru gaidi huyo, jopo
hilo lilitoka katika eneo hilo na kuondoka zao.
≈ ≈ ≈
Akiwa na bandage yake mkononi, kamanda
Amata alitembea taratibu pembezoni mwa
barabara ya Morogoro katika eneo la Jangwani
ambapo ile gari ya zimamoto ilikuwa
imetelekezwa hapo na jeshi la polisi lilikuwa
likifanya jitihada za kuiondoa katika eneo hilo.
FK Security Group, ilikuwa ni nembo iliyong’aa
sana katika ubavu wa gari ile, kamanada Amata
aliitazama nembo ile na kuipiga picha kwa
sababu mbalimbali za kazi yake, kisha bila
kuongea na mtu yeyote aliingia kwenye tax na
kuomba kupelekwa eneo la Mikocheni.
FK Security Group
Taratibu aliuendea mlango ulioandikwa FK
Security na kubofya kitufe cha kengele,
alipoitikiwa aliufungua na kuingia ndani.
Msichana mrembo alikuwa nyuma ya kompyuta
kubwa akiendelea na kazi.
“Karibu kiti kaka, nikusaidie nini?” alimuuliza
Amata.
“Naitwa Stephen Amalutwa, muandishi wa gazeti
la Dar es salaam leo, nimekuja hapa kuulizia juu
ya sakata la gari lenu la zima moto kutumika
katika jaribio la kigaidi pale JM MALL ghorofa ya
saba” alijitambulisha huku akiweka kitambulisho
chake mezani, kitambulisho cha uandishi wa
habari.
“Gari yetu sisi, imetumika? Ipi hiyo, mbona mi
sina taarifa na nadiye ninaeratibu shughuli zote
za ofisi hii?” aliuliza yuke dada.
“Inawezekana, lakini gari ile ni ya kwenu,”
Amata, muandishi bandia akatoa simu yake na
kumuonesha ile picha ya gari hiyo na namba
zake za usajiri, yule dada alipatwa na mshtuko
na akanyanyuka na kumwambia Amata asubiri,
kisha akaenda na kuingia katika ofisi Fulani, na
baada ya dakika kadhaa alitoka na kurudi pale
alipokuwa mwanzo.
“Bwana Amalutwa, haya ingia ofisi namba tatu
pale utapata majibu yako yote” aliambiwa.
Kamanda Amata aliinuka na vifaa vyake, na
kuelekea katika ofisi aliyoelekezwa.
Mbele yake aliketi bwana mmoja mnene kidogo
ambaye alikuwa na ndevu nyingi zilizouzunguka
uso wake kwa upande wa mashavuni,
walitazamana na Amata kisha wakasabahiana
na kuanza mazungumzo yao.
“Kutokana na maelezo yako bwana Amalutwa,
sisi hatuna gari ya uokoaji yenye namba hizo,
gari zetu zote ni hizi hapa” aliongea yule bwana
aliejitambulisha kwa jina moja tu, Scoletti. Alitoa
faili kubwa na kufungua kadi original za usajiri
wa magari yale, Amata alitazama na kweli
hakuona gari iliyosajiriwa kwa namba hizo.
“Na unasemaje kuhusu hii nembo yenu ya
kampuni katika gari ile?” alimuuliza
“Aaaa itakuwa ni wahuni tu wameamua kutumia
jina letu tu ili kutuharibia biashara, kama
unavyojua sisi ndiyo kampuni ya kwanza ya
binafsi kuanza kutoa huduma hii” Scoletti alijibu
huku akirudisha lile faili. Kwenye shelf maalum
lililo katika kabati moja kubwa pembezoni mwa
ukuta. Amata aliandika vitu Fulani katika kijitabu
chake, kwa macho ya kipelelezi aliiangalia ofisi
ile na kuona sehemu zote zenye ulinzi na vifaa
vya ulinzi moyoni mwake aliahidi kurudi usiku
huo kwa upekuzi zaidi. Waliagana na kuondoka
katika ofisi hiyo.
Scoletti alitoka ofisini kwake akiwa amefura kwa
hasira mapaka kwa secretary wake.
“Wewe, nikwambie mara ngapi unielewe?
Nimeshakwambia sitaki umruhusu mtu au
uongee na mtu kitu usichokijua, wengine hawa
wanatupeleleza, utasababisha kampuni hii
kufungwa wewe. Sasa nakupa likizo ya mwezi
mmoja na malipo yote yanayokustahili, utarudi
kazini baada ya mwezi mmoja” alimkemea yule
dada.
“Lakini Boss, yule si ni mwandishi wa habari nae
alikuwa katika majukumu yake ya kazi?” aliuliza
yule dada.
“Nani aliyekwambia? Yule ni mpelelezi wa
serikali, mpelelezi anayetegemewa hapa
Tanzania. We unaruhusu watu tu waingie,
tunaweza kuuawa humu ndani na we usijue”
kisha akampa sonyo refu. Baada ya dakika mbili
akaja na hawala ya fedha mkononi na
kumkabidhi yule dada.
Yule secretary hakuwa na la kufanya, likizo ya
dharula ilikuwa mezani kwake, hawala ya fedha
kwa likizo ilikuwa mkononi mwake, milioni mbili
zilisainiwa, machozi yalikuwa yakimlenga yule
dada kwa kosa alilolifanya, aliichukuwa ile barua
na ile hawala kisha akaagana na boss wake na
kuondoka. Alisimama nje katika barabara ya
Bagamoyo, akaangalia kushoto kulia hakuona
anachokitafuta. Mara akatoa kadi ya kibiashara
na kuitazama juu yake iliandika kwa wino
mweusi na maandishi ya kuremba Mr Stephen
Amalutwa, ikifuatiwa na namba kadhaa za mtu
huyo, aliinua simu yake na kupiga namba Fulani
kisha akaweka sikioni.
“Halo, yeah mimi ni secretary wa FK Security,
sijui naweza kukuona kaka yangu (…), hapana we
nambie nikuone wapi mi nitakuja” aliongea na
simu ile na miadi ya kukutana saa kumi nambili
jiono ilikuwa dhahiri kwake, kukutana na
mwandishi bandia Mr Amalutwa. Moyoni mwake
yule dada alikuwa na uchungu wa kupewa likizo
ile maana alijua anaweza kufuatiwa na barua ya
kuachishwa kazi muda wowote, lakini milioni
mbili alizopewa zilikuwa zikimfariji na kumfuta
machozi katika hilo.
JAMBO LIMEZUA JAMBO.... KWA NINI
MWADAWA APEWE LIKIZO YA DHARULA? JE
ATAFANIKIWA KUONANA NA KAMANDA AMATA?
 
JULAI 7 - 5

Ilipoishia...
Alisimama nje katika barabara ya Bagamoyo,
akaangalia kushoto kulia hakuona
anachokitafuta. Mara akatoa kadi ya kibiashara
na kuitazama juu yake iliandika kwa wino
mweusi na maandishi ya kuremba Mr Stephen
Amalutwa, ikifuatiwa na namba kadhaa za mtu
huyo, aliinua simu yake na kupiga namba Fulani
kisha akaweka sikioni.
“Halo, yeah mimi ni secretary wa FK Security,
sijui naweza kukuona kaka yangu (…), hapana
we nambie nikuone wapi mi nitakuja” aliongea
na simu ile na miadi ya kukutana saa kumi
nambili jiono ilikuwa dhahiri kwake, kukutana
na mwandishi bandia Mr Amalutwa. Moyoni
mwake yule dada alikuwa na uchungu wa
kupewa likizo ile maana alijua anaweza
kufuatiwa na barua ya kuachishwa kazi muda
wowote, lakini milioni mbili alizopewa zilikuwa
zikimfariji na kumfuta machozi katika hilo.
EPISODE 05
Gari aina ya Toyota V8 yenye vioo vya giza
iliinga katika geti kubwa la jingo Fulani huko
maeneo ya Mabibo. Vioo vyake vya tinted
havikuruhusu mtu wa nje kuona kilichopo ndani
ya gari hiyo, kwa mwendo wa taratibu
iliegeshwa na milango yake ikafunguliwa vijana
wawili na mtu mwingine wa makamo
wakateremka na kuufungua mlango wa nyuma,
mwanadada mmoja akateremshwa na kupelekwa
ndani ya ghorofa iliyopo ndani ya wigo huo.
“Ni mwanamke mjinga sana wewe!” ilikuwa sauti
ya yule mtu wa makamo aliyetambulika kwa jina
la Shailan aliyekuja kuchukua nafasi ya Betram, “
Tumekulipa pesa nyingi, tumekupa mafunzo ya
kujitoa mhanga, sasa umefanya nini? Unazidi
kutuingiza matatizoni, kaa hapo na leo hii
tunakuchinja kwa sababau wewe tayari
umeshakufa” alimalizia luongea kwa jazba
kubwa.
Yule msichana alisukumiwa ndani ya chumba
fulani chenye giza na kufungiwa. Kisha akaketi
na wenzi wake pale mezani.
“Bora mmempata, maana wangempata wao, sijui
tungemwambia nini Beishal, na ameshaamuru
huyu msichana auawe mara moja, kwa hiyo
baadae hiyo kazi ifanyike na mwili wake mtajua
mtautupa wapi”
“Lakini kwa nini tusimuache kwanza tumbane
atueleze kama kuna chochote alichoongea na
hawa watu, ili tujue labda tuna la kufanya”
aliongea kijana mwingine.
“Lakini pia ni wazo zuri, tumbane kwanza
tukishapata tunachokitaka ndiyo tummalize”
aliongezea Shailan, akanyanyuka katika kiti kile
alichokalia na kuelekea katika chumba kile
walichomfungia yule msichana, wakaufungua
mlango na kuwasha taa,
“We mwanake mjinga, uliyeahirisha kifo
ulichokiuza mwenyewe sasa utakipata kwa
maumivu makali” Shailan alimueleza huku
akilifuta jambia lake lililokuwa liking’aa huku na
huku kutoka katika ala yake.
Yule msichana alikuwa ameketi kinyonge katika
kona ya chumba hicho akiwatazama wanaume
wale kwa huzuni.
≈ ≈ ≈
kuhusu FARJAH
FARJAH, msichana yatima kutoka Mombasa
aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu huko
Mombasa, baada ya mama na baba yake kufa
katika ajali mbaya ya gari, msichana huyu
alibaki bila msaada huku akiwa ameachiwa
wadogo zake wane wa kuwalea bila msaada
wowote, akiwa katika harakati hizo alijikuta
akiingia katika biashara haramu ya ukahaba ili
kujipatia chochote kwa minajiri ya kusomesha na
kusaidia wadogo zake kimaisha.
Siku moja usiku wa manane akiwa kwenye moja
ya miahngaiko yake ndani ya club maarufu ya
usiku ya ‘Mombasa by Night’ ndipo alipokutana
na Shakrum Shakran ambaye alimtongoza
mrembo huyo na kwenda kulala nae katika hoteli
moja kubwa ambayo alifikia. Huko ndiko
alikosuka mpango huo na kumshawishi Farjah
kukubali mpango huo kwa malipo ya pesa nyingi
sana ambazo zingeweza kusomesha wadogo
zake na kuwaweka katika mazingira mazuri kwa
miaka ishirini mpaka watakapoweza kujitegemea
wenyewe, aliposaini pesa hiyo wadogo zake
walijengewa nyumba kubwa na kuwekewa kila
kitu na kulipiwa ada ya masomo yao, kisha
Farjah alimuomba shangazi yake awalee wadogo
zake hao wakati yeye anaenda nje ya nchi kwa
muda mrefu, shangazi yake alikubali na Farjah
alisafirishwa kwenda Somalia kupata mafunzo
maalum ya kujitoa mhanga, mafunzo ya
kutoogopa kifo, mafunzo ya kutumia bunduki za
aina mbalimbali, na tayari akiwa huko
alishatekeleza mashambulizi mbalimbali Somalia
na Sudani, sasa alipewa kazi yake ya mwisho
kuja kuifanya Tanzania maana mkataba wake
ulikuwa mwishoni.
Masaa machache nyuma
Farjah alitafakari sana alipokuwa njiani kutoka
Somalia kuja Tanzania, alifanya mashambulizi
mengi sana ya mauaji lakini yalikuwa tofauti
sana na haya anayotakiwa kufanya Tanzania.
Akiwa ameketi kwenye kochi kubwa la kisasa
alionekana kuwa na mawazo mengi sana, kiasi
kwamba iliwatia shaka mabosi wake.
“Farjah, mzima au?” aliuliza Shailan.
“Hapana, nipo vizuri tu” alijibu huku akiwa
ameangalia chini, akitafakari kifo chake
kinachofuata baada ya masaa machache.
“Farjah najua wazi kuwa una mawazo lakini
wewe tayari hitima yako tumekwishaifanya,
haupo duniani kama mkataba wetu ulivyo,
tunakushukuru kwa kazi yote uliyotufanyia, na
sasa unakwenda kumalizia na roho yako
itapumzika mahali pema huko peponi” Shailan
alikuwa akimwambia Farjah ambaye alionekana
wazi kuvujwa jasho japo kiyoyozi cha LG kilikuwa
kikitengeneza baridi kali ndani ya chumba hicho,
Farjah alishusha pumzi ndefu na kujitupa kwenye
kiegemeo cha sofa hilo. Mbele yake aliletewa
ramani kubwa ya jengo la JM MALL.
“Ok, tazama hapa Farjah, jengo tunalolitaka ni
hili, hapa ni floor ya saba, unapotoka tu katika
lifti, kunja kushoto kuna milango kadhaa,
utazipita ofisi zingine na wewe unatakiwa ufanye
mlipuko wako ndani ya ofisi hii, pale utamkuta
kijana mmoja matata sana na binti ambaye ni
katibu wake, hakikisha unanionana na huyu
kijana na mlipuko huu ufanyike ukiwa na huyo
kijana, jihadhari huyu kijana ni mjanja sana na
IQ ya hali ya hali ya juu, usipoteze muda.
Mwisho wako ndiyo huo. Ole wako ulete ujinga
na uzembe,” Shailan alimaliza kumuelekeza
Farjah kisha akanyanyuka na kuelekea chumba
fulani, Farjah akiwa katika kutafakari hili na lile
mlango mwingine ulifunguliwa na kijana jalali
akaingia akiwa na begi jeusi mkononi, Farjah
alishtuka kumuona kijana huyu, alimfahamu,
alinyanyuka na kumkumbatia kwa bashaha,
Shakrum Shakran hakuwa na muda wa
kukumbatia msichana, aliitazama saa yake na
kuushusha ule mkono.
“Tunachelewa, vua hilo baibui lako,” ilikuwa sauti
tulivu ya Shakrum, Farjah alipoisikia sauti hiyo
aliikumbuka jinsi ilivyokuwa ikimbembeleza
katika chumba kimoja cha hoteli huko Mombasa
ikimwambia ‘vua mpenzi nataka nione umbo lako
zuri, jeupe, lenye mvuto,’ lakini leo iliongea kwa
mkato tu.
Farjah hakuwa na lakusema alivua lile baibui
lake na kiblauzi kidogo ndani yake, chuchu
zilizosimama zilikuwa zikimtazama Shakrum,
kwa shida kidogo alimeza mate lakini haikuwa
kazi iliyokusudiwa. Begi jeusi likafunguliwa na
kitu kama mkanda kikatolewa na mbele yake
kulikuwa na kitu kilichotunatuna, Shakrum
akakizungusha kile kitu tumboni mwa Farjah na
kuzunguka mgongoni mwake akakikutanisha na
kufunga sawia kwa kutumi namba za siri (code
number) ambazo ni yeye tu alikuwa akizijua.
Akarudi upande wa mbele wa msichana huyu,
akafungua kifuniko Fulani kidogo na kubonyeza
vitufe kadhaa, mara kukawaka vinamba
vilivyojiandika sifuri sifuri kama sita hivi na
kutengenishwa na nukta mbili zilizobebana kila
baada ya siruri mbili (colon), kisha akaseti
vijinamba fulani, na alipoachia vikaanza
kujihesabu, bomu la saa! Shakrum alimwangalia
usoni Farjah aliyekuwa amelowa jasho mwili
mzima akitetemeka kwa hofu, akamshika kwa
viganja vyake vya mikono mashavuni na
kumbusu kwa kumnonya ulimi, usaliti!
“Farjah, fanya unalotakiwa kufanya na si
vinginevyo” Shakrum alisema hayo na kuchukua
ile baibui na kumvesha, kisha akamchukua hadi
chini kulikokuwa na Prado nyeupe ikiwasubiri,
wote wakaingia ndani na kuondoka eneo hilo.
≈ ≈ ≈
KATIKA kijibarabara cha watembea kwa miguu
eneo la Buguruni Chama kuelekea Y2K bar,
msichana mmoja alikuwa akitembea kwa hatua
za haraka haraka huku akiangalia nyuma mara
kwa mara, na kukibana kipochi chake kwa mbele,
sketi fupi aliyoivaa ilimnyima uhuru wa kuongeza
kasi, jioni hiyo watu wengi walikuwa katika
harakati za kurudi majumbani, hivyo kijibarabara
hiko kilikuwa na kazi ngumu ya kukanyagwa na
ymati huo. Alipokaribia katika lango la kuingia
kati ile bar, aliitoa simu yake katika pochi na
kubofya namba fulani kisha akaiweka sikioni na
kuonekana akiongea na mtu fulani huku akiwa
hana amani kabisa, mara akairudisha simu ile na
kuingia ndani ya ile bar, alipokelewa na
mhudumu wa bar hiyo aliyevalia nadhifu kabisa,
akamuongoza mpaka meza Fulani iliyokuwa na
mtu mmoja tu, mwanaume aliyevalia kaunda suti
kuukuu na kichwani akiwa na kofia aina ya
pama, mezani kwake kulikuwa na safari bia
iliyokua nusu na nyingine ikiwa katika bilauri.
Yule msichana aliketi kwa woga akimwangalia
mtu yule ambaye alihisi hajapata kumuona kabla,
yule mtu akatoa kadi ya kibiashara nyingine na
kumuwekea mezani, yule msichana alipoisoma
jina akalikumbuka lakini mbona hafanani ndiyo
swali alilojiuliza.
“Stephen Amalutwa!” alitamka kwa upole huku
akiisukuma juu ile kofia yake, “Nilipata simu
yako ndo maana nikakwambia tuonane hapa,
ningependa kukujua kwanza kwa jina, kisha
ndiyo unambie shida yako”
“Naitwa Mwada, mwadawa, naishi Magomeni
Makuti nyumba namba 12C, mi nimekutafuta
nikuulize kitu, ulipokuja ofisini na ulipoondoka
bosi wangu kanikaripia sana kwa kukukaribisha,
kisha kanipa likizo ya muda, hii hapa barua na
kanilipa cheki ya millioni mbili, mi nimeshindwa
kuelewa nini kimejificha” alijieleza Mwadawa
“Nafikiri mimi ningepaswa kukuuliza swali hilo,
sivyo? Kama bosi wako kaupa likizo kwa kitendo
cha mimi kuja kuandika habari kutoka ofsini
kwenu, nini kimejificha hapo?” kamanda Amata,
Stephen Amalutwa wa bandia aliligeuza lile
swali, Mwadawa alitulia tuli akitafakari
anachoulizwa,
“Mi kaka sijui, ninachoshangaa ni boss hatua
aliyoichukua,” alijibu, Amata alimwangalia kwa
jicho la chini,
“Ina maana wewe kama secretary wa ofisi
hujagundua kitu tofauti siku hizi ofisini kwenu au
nyendo tofauti na zile za kawaida za boss
wako?” Amata alirusha swali, na ukimya
ulitawala kati yao.
“Hapana zaidi ya wageni wengi wanaokuja siku
hizi, ambao tunatambulishwa kuwa ni ndugu
zake”
“Wageni wa namna gani?” kamanda aliuliza
“Ni hao ndugu zake, huja na kukaa hapa wiki au
mwezi, wakibadilishana na kuwa na vikao
visivyokwisha” alijibu Mwadawa.
Baada ya mazungumzo marefu na kamanda
Amata kuridhika kiasi na majibu ya dada huyo
waliagana.
“Kwa sababau umechelewa sana basi ngoja
nikufikishe nyumbani” Amata alimwambia
“Oh, no acha tu bwana nitafika mwenyewe”
“Ok, take care!” Amata alimuaga Mwadawa,
akabaki kasimama akimwangalia mwanadada
huyo anavyopotelea nje ya bar hiyo maarufu
hapo Buguruni ambayo daima huzungukwa na
akina dadapoa wengi wanaofanya kuwavuta
watu kufika hapo kila jua lilalapo.
Kamanda Amata, alimalizia kinywaji chake na
kutoka katika bar hiyo, moja kwa moja aliiendea
gari yake aina ya LandRover 110 TDI na kuingia
ndani yake kisha kuelekea mitaa ya kati ya jiji la
Dar es salaam, aliifuata barabara ya Uhuru
mpaka katika mataa ya Karume na kukunja
kushoto kuelekea Magomeni kupitia barabara ya
Kawawa, pale Magomeni alinyoosha moja kwa
moja na breki ilikuwa katika bar nyingine
maarufu Kinondoni kwa Manyanya. Mara tu
baada ya kusimamisha gari yake binti mmoja
aliisogelea na kuzunguka upande wa kushoto
kisha kuingia kiti cha mbele.
“Mungu anakupenda mrembo” Amata alianzisha
mazungumzo
“Kwa nini wasema hivyo honey?” ilikuwa sauti
tamu ya Gina, sauti inayoweza kumtoa nyoka
pangoni, sauti yenye mtetemo wa kutatanisha
inayoweza kukufanya kijana kupoteza network ya
kichwa chako hata ukiambiwa uandike cheki ya
milioni kadhaa utatii tu maana uatakosa la
kufanya.
“Kwani sakata la leo hulijui? Yaani hapa nyaraka
zote zimelowa huko ofisini,” Amata alieleza kisha
akatulia kwa muda na kumtazama Gina,
“Ungekuwa saa hii unalia mpaka unazimia
maana tayari ningekuwa hata sura haijulikani,
hawa jamaa ni hatari sana lazima nihakikisha
nawafutilia mbali katika uso wa dunia kwa
mkono wangu huu”. Ilionekana wazi hasira ya
Amata ilikuwa moyoni mwake, kijana mcheshi
anayependa kucheka muda wote hata na
asiyemjua.
Gina alimtazama Amata usoni kisha akauweka
mkono wake begani mwa kijana huyo,
“Pole!” alimtuliza.
“Ok, nipe tafutishi zetu” Amata alimwambia Gina.
Gina akatoa bahasha ndogo na kuchambua
karatasi fulani Fulani na kumpatia, Amata
alizichukua na kuzisoma kwa makini akatikisa
kichwa kukubaliana na kilichoandikwa ndani
yake.
“Shakrum!” Amata alitamka hilo jina, “Asante
sana mpenzi, umefanya kazi kubwa,”
Alizikunja zile karatasi na kuziweka katika droo
ya dashboard na kuwasha gari na kuondoka na
binti huyo.
“Wapi Amata jamani?” Gina aliuliza huku
akiuvuta mkanda wa usalama na kuufunga
vizuri.
“Hapo tu mbele unisindikize, kwa chakula cha
jioni”
≈ ≈ ≈
Addis in Dar, jioni hiyo watu wengi walikuwa
wakiingia katika hoteli hiyo kwa mlo wa jioni,
wengi walionekana na wapenzi wao wakishikana
kimahaba kuingia ndani ya hotel hiyo nzuri yenye
vyakula vya kuvutia vya tamaduni tofauti hasa
vile vya Ethiopia. Amata alishuka garini
akiongozana na Gina mpaka ghorofani na kuketi
katika meza moja iliyopo katika kona ya ukumbi
huo nadhifu, waliagiza vinywaji na vyakula
kadhaa na kuwa wakila huku wakibadilishana
mawazo.
“Gina, nisubiri hapa nakuja muda si mrefu!”
alimwambia Gina
“Wapi tena Amata?” kuna rafiki yangu nina miadi
naye nakuja, nipe lisaa limoja tafadhali”
akanyanyuka na kumpa funguo za gari na
kumuacha hela za kulipia chakula kisha yeye
akateremka chini na kuondoka. Kwa hatua za
harakaharaka aliifuata barabara ya Ursino
kuelekea upande wa barabara ya Bagamoyo,
aliikatisha na kupita mbele ya Kanisa la Kristo
kisha akakunja kulia na kusimama karibu na mti
wa mnazi ambaye ulilingana naye kimo,
alitazama huku na huko hakuona dalili ya mtu,
tayari ilitimu saa tano usiku, alitembea tena
haraka haraka na kulipita geti lililosomeka FK
Security na kuzunguka upande wa nyuma wa
ukuta wa uzio, aliangali kama kuna usalama
wowote akaona hamna shida, kwa kutumia mti
wa mwarobaini ulioota upande huo aliukwea na
kufika juu ya ukuta huo mrefu kisha kujirusha
ndani na kutua kwa utulivu kwenye ardhi tifutifu,
kishindo hafifiu kilimfanya mlinzi wa upande huo
kusogea, Amata alitulia kwa mtindo uleule na
kumsubiri, alipomkaribia kwa haraka aliruka na
kumpiga karate moja ya nyuma ya shingo kisha
kumdaka na kumshusha chini taratibu na
kumvutia karibu na pipa la takataka,
akamuhifadhi hapo na kuvuta hatua kwenda
upande wa pili, pale alikuta magari kadhaa
yamewekwa na mojawapo likiwa gari kubwa la
zimamoto ndani yake kulikuwa na watu sita
waliojilaza, akanyata taratibu akatoa mfukoni
kichupa chake kidogo chenye dawa kali ya
usingizi iliyochanganywa na dawa ya Halcion na
kupuliza kwa kupitia dirishani, haikupita sekunde
kumi wote walikuwa hoi kwa usingizi, Amata
akauendea mlango mmoja ulio pembeni mwa
jingo hilo na kutia funguo yake maalum mlango
ule ulikubali na kufunguka, akaingia ndani na
kuurudishia nyuma yake, kisha akaiendea korido
ndefu kidogo yenye milango michache lakni yeye
aliuchagua ule uliondika Director na kuutomasa
kidogo kwa funguo zake ukafunguka akaingia
ndani
NINI KILIMPATA FARJAH?
JE KAMANDA AMATA ATAFANIKIWA LENGO LAKE
NDANI YA JENGO HILO...
 
mwendelezo kidi kudi tafadhali. niko nyuma yako
 
EPISODE 06

ALIIANGALIA ile ofisi nadhifu ambayo mchana
wake tu alikuwa pale, kwa tahadhali aliizunguka
na kuketi juu ya kiti kile cha bwana Scolleti,
akaanza kuvuta droo moja baada ya nyingine
huku akisaidiwa na tochi yake ndogo mfano wa
peni yenye mwanga unaomulika pale tu
upatakapo. Alipofungua kabati alikaribishwa na
mafaili mengi sana ila alivutiwa na moja tu,
akalishusha na kuliweka mezani kisha
kuchambua nyaraka moja baada ya nyingine na
hii ilimvutia, kadi za gari, sasa uongo ulijulikana.
Kamanda Amata aligundua wazi kuwa lile lori la
zimamoto lililotumika kumuokoa yule binti
lilikuwa ni lao, walichokifanya ni kuibadilisha
namba ya usajili, alipoendelea kuichunguza ile
namba ya usajili akagundua kuwa ni namba ya
Toyota Premio, Amata akatikisa kichwa kuashiria
kuwa ameridhika kwa hilo, alitoa mashine yake
ndogo yenye uwezo mkubwa wa kutoa
photocopy , mashine ambayo huweza hata
kuiweka katika mfuko wa shati na usiijue, akatoa
vivuli vya kadi zile na kuzihifadhi vyema kisha
akarudisha lile kabrasha mahala pake. Akavuta
hatua kuliendea kabati lingine na kutoa faili
lililoandikwa ‘ Wageni’ ndani yake kulikuwa na
faili moja tu lililolazwa kana kwamba
limesahaulika mle ndani, alilivuta na kuliweka
mezani, akalifungua, kopi za hati za kusafiria
zilikuwa humo za watu ambao labda atawahitaji
wakati Fulani, nazo alifanya vilevile. Akavuta
hatua za tahadhari kuuelekea mlango lakini kitu
kilimvutia, kabla hajatoka, katika chano moja
iliyoandikwa IN kulikuwa na kijimemo kidogo,
akakirudia na kukinyanyua, ilikuwa ni miadi tu
‘Tuonane saa tisa alasiri kesho, White Sand
hotel’ kisha kufuatiwa na namba Fulani ya simu.
Amata aliirudisha ile kadi mahali pake na
kuuendea mlango kisha kutoka na kuufunga
nyuma yake. Alitoka nje taratibu kwa kufuata
njia ileile, alipofika kwenye ule mlango wa
kutokea kwenye ule uwanja alisikia mngurumo
wa gari kubwa na watu wakiwa wanazungumza,
akawasikiliza kwa makini.
“Wamesema kulekule Kunduchi” sauti moja
ilisema.
“Kunduchi ni mbali kwa nini isiwe jirani tu, si
kesho wataokota” sauti nyingine ilijibu, kisha ule
mlango ukafunguliwa, Amata akajibanza kwa
nyuma yake, vijana wawili wenye sare ya
kisecurity wakashuka na kuchukua kitu kama
mfuko wa saruji na kutoka wakisaidiana huku na
huku.
“Aaahapo safi, kesho mtainjoy jioni,” ilisema
sauti ingine ikifuatiwa na sauti ya lile gari
iliyoonesha wazi kuwa dereva alikuwa
amekanyaga pedeli ya mafuta, kutoka pale alipo,
kwa kasi alaijitupa chini na kujiviringa mpaka
uvungu wa lile lori, ijapokuwa kulikuwa na
walinzi eneo lile kwa muda huo lakini hakuwa
aliyemuhisi, sembuse kumuona. Amata alijishikia
vizuri sana kwenye chuma imara cha chessis
huku akiwa mbali kidogo na lile propeller Shaft
lililokuwa likizunguka kwa kasi. Ile lori ikatoka
getini na kuiendea barabara ya New Bagamoyo,
wakati likijiandaa kuingia barabara kubwa Amata
alitoka na kuliacha liende peke yake.
Akajinyanyua pale alipojitupia na kujikung’uta
vumbi na nyasi kavu zilizonasa mwilini.
≈ ≈ ≈


3
Asubuhi ilofuata
KIKOMBE cha chai kilishindikana kufikishwa
kinywani mwa Madam S wakati macho
yalipogongana na habari ya kipolisi kuwa mwili
wa mwanamke mmoja mwenye asili ya Kihabesh
umeokotwa kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi
huko maeneo ya Kunduchi. Kisha picha kadhaa
zilipitishwa kwenye luninga, na wakaomba kama
kuna mtu aliyepotelewa na ndugu yake basi
akautambue mwili huo katika chumba cha maiti
pale Muhimbili.
Madam S, aliendelea kunywa chai huku
akisikiliza watu wanaohojiwa juu ya tukio hilo,
kwake yeye halikuwa na uzito sana kwani mara
nyingi imetokea matukia kama hayo kusikika,
labda tu watu wameuana kwa wivu wa mapenzi,
hivyo hakufuatilia lolote. ‘Kazi za kipolisi’,
alijiwazia.
Aliinuka kitini na kukusanya vifaa vyake kisha
kuondoka kuelekea kazini, kama kawaida alikuwa
kwenye foleni ndefu ya magari ya kuingia
barabara ya Ally Hassan Mwinyi ili aelekee
upande wa Posta, alifungua redio na kusikia tena
habari ile ile aliyoiacha kwenye televishen, lakini
katika redio hii kitu fulani kilimvutia, habari
iliyosema kuwa marehemu ametupwa usiku
uliotangulia na watu wasiojulikana. Alijaribu
kuchanganya kichwa kama kuna lolote muhimu
kwake lakini hakuona hilo, aliendelea na safari
yake.
Mwananyamala hospitali
“YEAH, huu ni mwili wa mwanamke
anayekadiriwa kuwa na miaka 25 hadi 30,
ameuawa kwa kuvunjwa shingo,” Dr Semeni
alikuwa akimueleza Amata aliyekuja kujua
kilichojiri juu ya mwili ule uliookotwa kule
Kunduchi Beach siku hiyo asubuhi. Aliufunua ile
shuka iliyofunikwa mwili mzima na kuruhusu uso
kuwa wazi, akatingisha kichwa kuashiria
ameelewa kitu.
“Vipi?” Dr Semeni aliuliza.
“Hapana, nimekubaliana na uchunguzi wako”
Amata alijibu. Amata aliugundua mwili ule, mwili
wa msichana aliyekuja na bomu jana yake pale
katika jengo la JM MALL kwa minajiri ya
kujilipua, tena ofisini kwa Amata. ‘Inaonekana
wamemuua baada ya kushindwa kutekeleza lile
jaribio,’ alijiwazia Amata, huku akiandika andika
katika kitabu chake cha kumbukumbu.
≈ ≈ ≈
“Mheshimiwa Rais ametuachia hilo jukumu sisi,
kama tunaona ni vyema kumuachia huyu jamaa
au la!” waziri wa ulinzi aliongea huku
akiwaangalia mjumbe mmoja mmoja katika
kikao hicho waliokaa kwa mtindo wa nusu duara,
wakiwa katika majadiliano hayo na utayari wa
kuandaa remove order, mara mlango ulifunguliwa
na Amata akawa amesimama nyuma ya wale
wajumbe wengine akitazamana na waziri uso
kwa uso, wajumbe wote waligeuka nyuma
kumtazama kijana huyu aliyeingia hapo bila
kualikwa. Madam S alimtazama kijana wake kwa
macho makali sana.
“Amata! Unafanya nini hapa, kikao hakikuhusu,”
madam S aliongea huku akiinuka kitini kumkabili
Amata.
“Mnisamehe kwa kuingia ghafla lakini imebidi
nifanye hivyo kwani ningechelewa kidogo tu
mngefanya kile nisichokitaka” Amata
alizungumza kwa kujiamini.
“Kipi hicho?” waziri aliuliza.
“Swala la kumuachia huru Jegran Grashan,
siliungi mkono hata kidogo, najua mna nia nzuri,
lakini mimi naona mkifanya hivyo mtakuwa
mmeharibu sana na watu watawashangaa kwa
hatua hiyo, mimi suing mkono hata kama sina
uwezo wa kuwazuia kufanya maamuzi yenu”
Amata aliongea kwa hasira iliyomfanya kila mtu
kutulia, “Wenyewe mnajua nilivyompata kwa
shida hata kuhatarisha maisha yangu, halafu
aachiwe kirahisi namna hiyo! Haiwezekani,
kumuacha yule tutakuwa tumeonesha udhaifu
mkubwa sana wa kiutendaji katika ngazi ya
kiusalama. Sitakubaliani na hilo, yule akae ndani
kama ilivyo sasa na hawa washirika wake ndiyo
tutawapata kiurahisi, kitendo cha kumuachia ni
kuwaweka mbali maadui zetu, sikubaliani na
mnalotaka kufanya,” Amata alimaliza na kutoka
ofisini mle kisha kuufunga mlango nyuma yake.
Aliingia katika gari yake na kuketi nyuma ya
usukani akionekana wazi kupoteza network kiasi
Fulani.
Mara kioo cha dirisha la upande wake
kikagongwa, alipogeuka akagongana macho kwa
macho na madam S, walitazamana kwa nukta
kadhaa kisha Amata akashusha kioo.
“Nione Ofisini,” Madam S akaongea kwa kifupi na
kuielekea gari yake. Amata akawasha gari yake
na kuondoka eneo lile.
Baada ya dakika kadhaa alikuwa tayari ofisini
mwa madam S akiwa ameketi kwa mtindo wa
kutazamana na mwanamama huyu, mkuu wake
wa kazi.
“Umefanya nini Amata?” madam S aliuliza,
“Unadiriki kuingia katika kikao kama kile bila
idhini yoyote! Amata,”
“Ilibidi iwe hivyo kwani nilijua mnalolizungumzia
mimi nalipinga kadiri ya mwenendo wa kazi hii”
Amata alimjibu.
“Hukutakiwa kufanya vile, kwa nini hukusubiri
kikao kiishe, kisha utoe rufani yako?”
“Isingewezekana ukizingatia nyote mliokuwa pale
tayari mlikuwa na adhma moja tu, kumuacha
huru Jegran, mimi hilo siwezi kulivumilia,
nilimpata kwa tabu sana yule mtu, kumbuka
mwenyewe madam jinsi ile kazi ilivyokuwa
ngumu…”

Miaka minne iliyopita …
“HATA kama nimejeruhiwa, hakika siwezi
kumuachia hayawani huyu aondoke aende
akadhuru watu wengine, sambaza picha yake
mipakani na mijini labda tutapata fununu juu
yake,” Amata alizungumza kwa uchungu huku
machozi yakimtiririka, mkono wake wa kushoto
ulikuwa ukivuja damu baada ya kujeruhiwa na
risasi na kusababisha jeraha katia nyama zake
za juu ya kiwiko, lakini uzuri ni kuwa hakuna
mfupa uliovunjika.
“Pole kamanda” Madam S alimpa pole huku
akimwangalia kwa huzuni pale kitandani
alipokuwa akipata tiba.
Baada ya kila kitu kukamilika, kamanda Amata
na madam S walitoka hospitalini hapo na kurudi
mjini, jua lilikuwa tayari likiuacha mji wa Dar es
salaam na kupotelea Maghalibi kama ilivyo
desturi mji ulianza kuchangamka wengine
wakirudi nyumbani ilhali wengine wakiingia mjini
kuanza kazi zao haramu na halali.
“Kumpata huyu jamaa ipo kazi kamanda” madam
S alizungumza.
“Yeah, ni kazi ngumu sana lakini lazima tumpate,
na atapatikana tu” alijibu kamanda Amata.
“Unafikiri tufanye nini ili tumtie mkononi?”
“Kwanza kabisa mpaka sasa sitegemei kama
yupo Dar, kwa vyovyote atakuwa ameshatoka
mji huu ili kutaka kukimbia”
“Ni ngumu, makachero wengi tumewasambaza
katika sehemu muhimu ili kumnasa ama yeye au
aliyefanana naye”
“Tutumaini, jamaa alitaka kufanya kitu kibaya
sana pale uwanja wa ndege, tumshukuru Mungu
niliwahi kuokoa lakini sasa hivi tungeongea
mengine.” Amata alisema
“Ah, kwa kweli unastahili pongezi” madama S
alimpongeza Amata
“Aah, tuwapongeze wale waliotufahamisha
kuhusu Jegan kuwa pale, maana alijua wazi
kuwa tumebana kila kona hivyo atumie njia ya
kawaida kuondoka, ka kujibadili sura yake kiasi
fulani”
Masaa machache yaliyopita
Uwanja wa ndege wa kimataifa Dar es
salaam, DIA
JASMINE aliinua kichwa chake kumtazama mtu
aliyekuwa mbele yake, alipata shaka na hati
yake ya kusafiria, alimtazama kwa makini usoni
kisha akarudisha macho katika hati ile,
mashaka.
Aliichukua ile hati na kumkabidhi mwenzake
aliaitazame upya.
“Samahani subiri pale kwenye kiti,” alimwambia
mtu yule aliyekuwa na mandevu mengi kidevuni
mwake. Yule mtu aliketi kitini na kuuweka mfuko
wake wa plastiki pembeni yake, akisubiri kuona
kinachojiri.
“Mh! Hii hati mbona yanitia mashaka?” mtumishi
mwingine wa idara ya Uhamiaji alimuuliza
Jasmine.
“Ndiyo maana nikakupa” Jasmine alijibu. Yule
bwana akaiweka kwenye mtambo maalum na
kuifanyia scan kisha akamrudishia le Hati
Jasmine.
“Samahani kwa kukuchelewesha, tulikuwa
tunaikagua kidogo hati yako, wakati mwingine
unapoingia nchini kumbuka kupata kibali (visa)
cha muda mrefu, maana hapa inaonekana kibali
chako kimeisha tangu juzi,” Jasmine alimueleza
yule bwana mwenye mandevu kisha akampa hati
yake na kumruhusu kuendelea na utaratibu
mwingine baada ya kumgongea mihuri kadhaa,
kilichomshangaza juu ya huyu Bwana alikuwa
haongei wala hajibu chochote isipokuwa
kukutazama tu kwa macho yake mekundu.
Baada ya kuiscan ile hati, aliichukua kielektroniki
ile picha ya mtu huyo na kuingiza kwenye
mtandao maalum wa usalama wa taifa
unaoweza kuitambua sura yoyote ya mtu na
kukupa taarifa zake. Chiba akiwa nyuma ya
kompyuta yake maalum kwa kazi hiyo, safari hii
akiwa ndani ya sare za ofisa uhamiaji pale
uwanja wa ndege alitulia tuli, akisubiri ule
mtandao ufanye kazi huku akimtazama yule mtu
asipotee machoni mwake.
Mlio fulani ulisikika kwenye kompyuta yake na
alipoitazama, kwenye kioo kulikuwa na picha
mbili, ile aliyoiscan na pembeni yake kulikuwa na
nyingine iliyoletwa kwa msaada wa mtandao na
maelezo kadhaa chini yake.
Jegan Grashan, mzaliwa wa Yemen; kisha
zikafuatili tarehe za kuzaliwa na maelezo
mengine mengi, lakini katika ile hati kulikuwa na
maelezo tofauti kabisa. Jasmine aliitilia shaka
kutokana na mihuri ya kibali chake cha kuwapo
nchini ilifanana sana na ile ya idara ya uhamiaji
isipokuwa kitu kimoja kidogo sana ambacho kwa
raia wa kawaida huwezi kukitambua
hakikuonekana katika mihuri ile.
Chiba alibofya vitufe Fulani kwenye hiyo
kompyuta yake kisha akaandika ujumbe na
kuutuma mahali. Alinyanyuka kutoka alipoketi na
kuiweka tayari bastola yake kicha kuipachika
katika mkanda wake wa suruali na kujitupia koti
lake la buluu liliofunika vyema bastola ile.
≈ ≈ ≈
Akiwa kitandani na msichana mrembo, Kumbuka,
kamanda Amata alikuwa akiendelea na shughuli
hiyo nyeti ambayo haistahili kusimuliwa mbele
ya watoto, alikuwa akitoa miguno
iliyochnganyika na sauti nyembamba ya mahaba
yaliyosindikizwa na raha kutoka kwa msichana
huyu aliyeonekana wazi kuipagawisha roho ya
Amata mchana huo wa jua kali katika hoteli
fulani hapo Dar.
Kumbuka alimsukumia upande wa pili Amata na
kujinasua katika mikono ya dume hilo lililokuwa
bado likiendeleza libeneke wakati mwenzake
alikuwa amekwishamaliza mizunguko yake.
Kamanda Amata alitulia kitandani akimwangalia
Kumbuka alipokuwa akikimbilia bafuni huku
nyama zake za nyuma zikitisika kwa mpangilio
hadimu ambao huwezi kuuona kirahisi kama
hukumpembua mavazi binti huyu wa kihehe.
Akiwa katika butwaa hilo mara saa yake ilimfinya
kwa meno maalum yaliyo chini ya mfuniko.
Akabofya kitu fulani na kutulia, mara mkanda
mdogo ukatoka katika ile saa, Amata aliusoma
ujumbe uliokuwamo katika kijimkanda hicho.
‘Mzigo wetu upo hapa Airport, njoo haraka, Tena
Sana Aisee’
HAYA MVUTANO UMENOGA JE JEGAN
GRASHAN ATAACHIWA HURU?
NIMEKURUDISHA NYUMA ILI UPATE KUMJUA
VIZURI GAIDI HUYU.....
USIKOSE EPISODE IJAYO YA SHOW HII....
 
‘Mzigo wetu upo hapa Airport, njoo haraka,
Tena Sana Aisee’

CHAPISHO LA 7

KAMANDA AMATA, alikurupuka kitandani na
kukimbilia bafuni, alijiswafi haraka haraka na
kuvaa nguo zake.
“We vipi mbona hueleweki?” ilikuwa ni sauti ya
Kumbuka, akimuuliza Amata wakati akiwa
kwenye harakati hizo.
“Nitakutafuta baadae kuna dharula hospitalini”
alimdanganya. Alipomaliza kujiweka tayri alitoka
na kumuachia noti zenye thamani ya elfu
hamsini kisha yeye kuliendea gari lake na
kupotelea.
Madam S nae alikuwa njiani kuelekea hapo
sambamba na kamanda Amata. Dakika chache
Amata aliingia uwanja wa ndege na kuiwiweka
maegeshoni gari yake, ulinzi tayari uliimarishwa
na askari waliovaa kiraia, madam S naye
aliteremka na kuongoza moja kwa moja katika
mlango wa kuingilia wasafiri wenye kibao
kilichoandikwa ‘Departure’.
“Geti namba 38” sauti ya Chiba ilifika masikioni
mwa madam S aliyeonekana kuwa kikazi zaidi,
tayari alikwishavuka huo mlango na kusimama
mahali Fulani akipepesa macho yake huku na
kule, kwa mbali alimuona Amata naye akiwa
amebana kwenye kona Fulani.
“Chiba! Nenda pale alipoketi mwambie kuwa hati
yake ya kusafiria ina mashaka kisha akikufuata
tumtie nguvuni” Amata alimwambia Chiba kwa
kutumia saa yake maalum inayoweza kusafirisha
ujumbe wa sauti.
“Amata, nipe mpango wako!” Madam S alipeleka
ujumbe wa sauti ka Amata.
“Chiba atakwenda kumueleza kuwa hati yake ina
shida hivyo amfuate ofisini, kisha tutambana
huko, najua lolote linaweza kutokea madam,
watu wameshakaa kila kona kwa tahadhari”
Amata alimjibu madam S.
“Ok, kamanda nakuaminia, hakikisha hasitoroke
mshenzi huyo” madam S alimaliza kuongea kwa
kutumia ile saa yake na kujiweka tayari. Amata
akiwa kona ya upande wa pili aliweza kuona kila
kinachoendelea.
Jegan Grashan alikuwa ameketi huku akisoma
gazeti la Daily News, alionekana kutokuwa na
utulivu maana kila wakati alikuwa akiiangalia
saa yake. Chiba alivuta hatua ndogondogo
mpaka pale alipoketi Jegan na kusimama mbele
yake.
“Mheshimiwa!” Chiba aliita, na Jegan aliinua uso
wake kumuangalia, “Samahani kwa usumbufu
kuna tatizo dogo kwenye hati yako ya kusafiria,
naomba unifuate ili tukairekebishe.” Jegan
alimtazama Chiba kwa tuo,
“Mimi?” alimuuliza
“Ee ndiyo wewe bwana Hassanail Hussein” Chiba
aliongeza na kumtaja kwa jina alilotumia katika
hati yake. Jegan, gaidi la kimataifa, lilianza
kuhisi harufu mbaya ya hatari, alitazama huku
na huku na kwa mbali alimuona Amata
amejibanza kwenye kona Fulani, akamtambua
akaona hatari na janja inayotumika. Jegan
alimkazia macho Chiba na Chiba akafanya vivyo
hivyo huku akizisoma hisia za gaidi huyo, Chiba
aliona wazi kuwa sasa kazi imeamka kazi
ambayo hakuitarajia alitamanai Kamanda Amata
awe jirani. Amata aliona kila kitu na akamtupia
signal madam S, taarifa zikafika kwa
wanausalama wa nje ya uwanja kujiweka tayari
kwa lolote muda wowote.
“Ok twende,” Jegan alijibu, kisha akanyanyuka
na kuongoza, hatua chache alimuona Amata
akitoka kwenye ile kona aliyosimama. Jegan
akasimama na kujifanya anafunga kamba ya
kiatu, teke moja la nyuma lilimtoka na
kumpepesua Chiba ambaye alienda chini bila
pingamizi, kelele za wasafiri zikaamsha vurugu
kwenye chumba cha kusubiria safari, Chiba
alinyanyuka na kuchomoa bastola yake.
“Freeze!!!” alipiga kelele, lakini Jegan alijirusha
kwa ustadi na kutua juu ya ngazi za umeme
zilizokuwa zikielekea chini.
“Watu wote lala chini !” sauti ya Amata ilisikika
na kila aliye ndani ya ukumbi ule alijitupa
sakafuni. Polisi mmoja alimjia mbele Jegan,
kosa. Jegan aliruka sarakasi na kutua miguu
yake kifuani mwa polisi huyo na kumpeleka chini
huku bunduki yake aina ya SMG ikimtoka
kiurahisi mikononi na kudondokea pembeni,
alipotaka kunyanyuka teke moja kali lilitua
shavuni na kumvunja taya, Jegana sasa alikuwa
na ile bunduki mikononi mwake, akaiondoa
usalama tayari kwa mashambulizi.
‘Mambo yashaharibika’ Amata alijisemea akiwa
anaelekea kule kwenye mapigano. Jegan
alifyatua risasi kadhaa hewani na watu wote
walitulia chini, alipoona Amata anamkaribia
alimuinua mama mmoja wa Kihindi na
kumuweka ngao.
“Ukiniletea shida namuua huyu mama” Jegan
alimueleza Amata aliyekuwa kasimama mbele
yake tayari na bastola mkononi. Jegan
aliididimiza mtutu wa ile bunduki kwenye shingo
ya yule mama, “weka silaha yako chini”
alimuamuru Amata, Amata akaiweka chini
bastola yake, “Vizuri, sasa isukumie kwangu kwa
kutumia mguu wako” alitoa amri nyingine, Amata
akatii na kuipiga kwa teke ile bastola nayo
ikaseleleka kumuelekea Jegan, Jegan
alimsukuma yule mama na kuiwahi ile bastola
baada ya kufyatua magazine ya SMG na
kutengeanisha na ile bunduki, alipogeuka kwenda
uapande wa pili, alikutana na ngumi nzito toka
kwa Chiba, kabla hajakaa sawa Chiba aliruka
double kick na kumfanya ayumbe, wakati huo
tayari Amata alikuwa jirani, Jegan alipanda ngazi
haraka kuelekea upande wa juu akageuka na
kufyatua risasi moja iliyotawanya vyoo kila
upande,
“Kamanda…!!!!” ilikuwa sauti ya madam S, Amata
aligeuka upande ule na kumuona madam S
akimrushia bastola, Amata akaidaka kwa ustadi
na kugeuka upande alipo Jegan hakumuona, kwa
hatua za kunyata alipanda ngazi kuelekea juu na
kufika tena pale kwenye sehemu ya kusubiria
wasafiri, alisimama kwa utulivu akitazama huku
na huku, ‘Uko wapi hayawani?’ alijiuliza
mwenyewe huku akitembeza bastola yake huku
na kule. Amata alijikuta akipigwa karate moja
kali kutoka nyuma yake, akajirusha sarakasi na
kutua mbele kama hatua tatu hivi kisha kugeuka
kumkabili adui, aliruka juu na kuichanua miguu
yake kwa mtindo wa kujizungusha na kumpata
sawia Jegan ambaye hakutetereka bali
alisimama kidete akamsubiri Amata kutua
sakafuni, kama alivyotarajia, Amata alitua kwa
mguu mmoja lakini kabla hajakaa sawa, Jegan
alipiga teke kali na kuufyatua ule mguu, sasa
Amata alianguka vibaya sakafuni lakini alipotua
tu naye alipiga teke moja sehemu ya nyuma ya
magoti na kumfanya Jegan apige magoti, teke la
pili lilitua usoni na kumfanya aanguke chali.
Amata alijinyanyua na kumuendea huku Chiba na
madam S nao wakija kwa kasi, Jegan
alinyanyuka na kumpiga dafrao Amata kisha kwa
kasi ya ajabu alikimbi na kujirusha kwenye kioo
kikubwa na kutoka nje huku milio na risasi
vikimfuati kwa kasi lakini havikufanikiwa, Jegan
alikuwa tayari nje ya jingo chini kabisa na
kukimbia kuelekea pande za Kipawa, walinzi wa
nje walipata wakati mgumu kumkamata
haikuwezekana.
Amata alibaki kasimama huku kajishika kiuno
pembeni yake madam S akionekana wazi
kukasirika kwa kumkosa hayawani huyo. Amata
alisonya na kuelekea pale kwenye lile tundu
kubwa la kioo alipopitia Jegan.
“Amkeni, poleni kwa usumbufu” madam S
aliwaambia abiria. Kisha akifuatana na kamanda
Amata na Chiba waliteremka ngazi mpaka nje ya
jengo hilo ambapo walikuta polisi wakiwa kwenye
kibarua kizito cha kumsaka Jegan wakiwa na
mbwa maalum kwa kazi hiyo.
Katikati ya vichaka vya eneo hilo ambalo wakazi
wake walikwishahamishwa ili kupisha upanuzi
wa uwanja huo, mbwa wote waliishia kwenye
kiatu kilichokuwa hapo, hawakuendelea zaidi,
Jegan hayupo….
“Sasa mtu kama huyo kweli, ee! Madam,
tumuachie? Watanzania takriban saba
wamepoteza maisha pale ubalozini mwaka ule,
na Wakenya zaidi ya mia mbili, hapana
mkimuachia mi namuua, naapa!” Amata
alimwambia madam S, akasimama na kutaka
kuondoka.
“Kamanda hebu rudi kwanza hapa!” madam S
alimuita, Anata akarudi na kusimama
akimtazama boss wake, kisha madam S
akaendelea, “Unalosema ni sahihi, lakini we
unafikiri tufanyeje? Kwa maana hata
mheshimiwa amelibariki hilo.”
“Sikatai, lakini si kwamba tumeshindwa
kuliangamiza hili genge?” Amata aliuliza
“Hilo niachie mimi, nitaongea na wadau tuone
njia mbadala,” Madam alimpoza jazba Amata.
Amata akatoka nje na kuiacha ofisi ya madam S
akiwa mwenye mawazo mengi sana.
≈ ≈ ≈
KAMANDA AMATA aliingia kwenye gari yake na
moja kwa moja alielekea ofisini kwake pale
kwenye jingo la JM MALL, aliegesha gari na
kuteremka, huku na huku aliangalia usalama na
kuufunga mlango kisha kuingia ndani kupitia
mlango mkubwa wa mbele, mlango wenye watu
wengi wanaoingia na kutoka kwa kuwa ndani
yake kulikuwa na supermarket kubwa ya
Shoprite, alipiga hatua chache na kutulia kusubiri
lift ya kumpeleka ghorofa ingine ambamo ofisi
yake ilikuwamo, alifika na kubonyeza kengele
kwa mtindo ule waliowekeana na Gina, mlango
ulifunguliwa na akaingia moja kwa moja akaenda
kujitupa katika kiti chake akiwa mwenye mawazo
lukuki, Gina kama kawaida yake, aliandaa
kahawa ya kiitaliano inayojulikana kama
‘Capucino’ na kumpelekea pale mezani,
“Karibu kamanda” alimkaribisha huku akitoa
tabasamu pana lililomrudishia nguvu Amata,
“Asante mrembo, ndiyo maana nilikuajiri ofisini
kwangu” alimsifia huku akijiweka sawa kitini, na
kumkaribisha Gina kiti cha pili yake, kisha akatoa
camera yake ndogo na kuiwasha sehemu ya
kuangalia picha zilizokwishapigwa ambazo
zimehifadhiwa humo, akachagua akachukua na
waya wake wa USB na kuuchomeka kutoka
kwenye camera mpaka kwenye kompyuta yake,
sekunde chache zile picha zikaanza kuonekana
pale katika kioo cha kompyuta.
“Gina, unamjua huyu?” Amata alimuuliza Gina,
Gina alikodoa macho kuangalia ile picha, picha
ya mtu asiye na uhai, mwana dada mweupe
mwenye nywele ndefu zilizoijaza machela ya
chuma ya chumba cha kuhifadhia maiti cha
Mwananyamala.
“Hapana, simfahamu” Gina alijibu
“Huyu ndiye aliyekuja hapa kufanya ule mlipuko,
lilikuwa bomu hai,”
“Umempataje hadi kumuua?” Gina alisaili
“Hapana, sijamuua, wamemuua wenyewe, unajua
hii ni mikataba, unapokwenda kujitoa mhanga
maana yake wameshakulipa na
wameshakuwekea matanga kwamba wewe nai
marehemu hivyo uende ukaue na wewe ufe
ukohuko, sasa huyu inaonekana kafeli hivyo
wamemuua, wamemnyonga shingo” Amata
aliposema hayo alimuona Gina akisisimka mwili.
“Watu wabaya!” Gina aliongea
“Sio kidogo!” Amata akaongeza, aliinua kikombe
chake na kunywa ile kahawa kisha akakishusha
n kujiweka vyema kitini.
“Nipe mrejesho, maana tangu juzi ile hatujakaa
kuongea, nilikupa kazi, unakumbuka?” Amata
aliuliza.
“Nakumbuka sana, nitakuwa sekretari gani kama
nasahau kazi ninazopewa na boss?!” aliuliza
kwa kejeli
“Na utakuwa mke gani kama utakuwa unasahau
majukumu unayopewa na mumeo?” kisha wote
wakacheka. Gina akanyanyuka na kuiendea meza
yake na kuivuta saraka, akatoa kabrasha moja
na kuja nalo pale mezani, akalifungua na kumpa
karatasi moja Amata, aliipokea na kuisoma kwa
makini.
“Ok! Gina nakupa kazi ingine, nenda ofisi ya
Idara ya uhamiaji pale makao makuu waulizie
jina hili Shakrum Shakran, yuko nchini kwa
shughuli gani na wakupe anuani ya wapi kafikia,”
Gina alitikisa kichwa kuwa amekubali, lakini
kabla hajaondoka, “Gina, tafadhali usitumie simu,
sawa?”
“Sawa Bro,” alijibu kisha akarudi katika meza
yake na kufungafunga, akahakikisha anakariri lile
jina kichwani kisha akaaga na kuondoka, Amata
akaendelea kufanya kazi zilizopo kwa wakati huo
ikiwa ni kupanga mipango mabalimbali ya
kuhakikisha anamaliza mchakato huo mapema ili
ikiwezeka akamsaidie Chiba huko China kwenye
sakata lile la Watanzania waliokamatwa na
madawa ya kulevya na kuchafua jina la nchi hii
tukufu yenye unono wa maziwa na asali.

WHITE SANDS HOTEL

KIJUA cha alasiri kilikuwa kinaendelea kuchoma
ardhi katika mchanga wa pwani ya White Sand,
kila mtu alikuwa na hamsini zake, wengine
wakiogelea, wengine wakipata vinywaji, wengine
wakicheza mpira wa mikono kwenye mchanga
ilimradi tu kwamba kila mtu alikuwa na shughuli
ya kufanya.
Mawimbi makali yalikuwa yakipiga huku na huko,
hali ile watoto wa Kihindi waliifuarahia sana na
iliwafanya hata wengine kutoka katika madimbwi
ya kuogelea na kukimbilia huko baharini wakiwa
na furaha ya ajabu.
Kamanda Amata, aliibuka kutoka katikati ya
mawimbi makali akiwa ni mmoja na wale
waogeleao kwa furaha, kwa hatua za kujivuta
kidogo alijaribu kupingana na maji ya bahari
huku akielekea pwani akiwa ndani ya bukta ya
kuogelea, mwili wake ulioonekana wazi sehemu
kubwa uliwavuta watoto wengi kumshangaa jinsi
alivyojaza misuli kimazoezi na kujijenga mwili
mithili ya ‘Daniel Craig’, alitoka mpaka pwani
akasimama kidogo na kuangalia huku na huku
kisha akakatiza katika ule mchanga kuiendea
meza moja iliyo chini ya msonge maridadi, pale
palikuwa na msichana mmoja wa kihindi ameketi
akijisomea kitabu cha riwaya ‘ISABEL’
kilichoonekana kumkuna kwelikweli, Amata
hakumuacha msichana huyu hapo, lakini
alishangaa kumkuta ameketi pale bila wasiwasi
wowote, Amata alichukua taulo lake na
lilitengenezwa kwa mfano wa koti na kulivaa,
“Waoh!” yule msichana alitoa mshangao.
“Vipi mbona unashangaa?” Amata alimuuliza
“Aaaa, mmmm! Umejazia mbaba mpaka
napata..”
“Unapata nini?” Amata alimkatisha, yule
msichana wa kihindi akaita mhudumu na
kuagiza juice mbili, mara zikaja, akachukua glass
moja na kumpa nyingine Amata, Amata alitupa
jicho la wizi kwa msichana huyu hasa kiuno
chake kilichojengeka vyema na makalio ya
kubinuka kidogo, ‘Huyu Mhindi au Mbantu?’
alijiuliza,
“Cheers!” alitamka yule msichana huku akigonga
glass yake na ile ya Amata zikalia nge! Yule
mdada akapiga funda, Amata alipokaribia
mdomoni mara alimuona Gina kafika na
kusimama katikati yao, Gina akaichukua ile glass
na kuirudisha mezani, kisha akamgeukia yule
msichana wa Kihindi na kumsonya,
“Mxiuuuuu! Acha waume za watu,” kisha
akamvuta mkono Amata na kuongozana nae
upande wa malocker maalum ya kuhifadhi nguo
na vifaa vingine kabla hujaenda kuogelea,
akamgeuza Amata mbele yake na kumuoneshea
ishara ya kimya yaani kidole chake cha shahada
akakiweka kukatisha midomo yake,
“Shhhhhhhh!!!!!!, ile juice ina sumu Amata,
ungekunywa tu umekwisha” Gina alimwambia.
“Asante sana, Malaika wangu mlinzi, umefikaje
hapa na umejuaje niko hapa?” Amata aliuliza.
“Usichezee mtoto wa kike wewe!” nilijua wazi
huku kunaweza kuwa na hatari ndiyo maana
nikaja kukuchunga. Gina alimuachia Amata,
wakatazamana, “Nipo ghorofa ya juu kwenye
ukumbi wa chakula, nenda kaendelee na mpenzi
wako” Gina alipokwishakusema hayo akageuka
kuondoka, Amata akamdaka mkono kabla
hajafika mbali,
“Gina, njoo, upo na nani?”
“Nipo mwenyewe tu, usijali swahiba nakulinda,”
akafungua pochi yake kumuonesha ndani
mlikuwa na bastola mbili zilijoaa vizuri na
magazine nyingine tatu za akiba, “Hapa kitanuka
Amata, utaniona mi nani leo, lete ujinga na huyo
Malaya wako.” Gina akaondoka akamuachia
Amata kifaa maalum cha kunasa sauti kati yao
wawili.
Dakika tano zilikuwa nyingi, kamanda Amata
akawa ndani ya suti nadhifu ya kijivu
iliyotanguliwa na shati la buluu bahari safari hii
hakuweka tai aliuruhusu upepo wa pwani upite
kwenye shingo yake na kuingia mpaka kifuani.
Kwa hatua za kibrotherman alitembea kuielekea
tena meza ileile akiwa na shauku ya kujua ni
nani yule mrembo na alikuwa akitaka nini kwake,
aliifikia ile meza, peupe! Hakuna mtu, mezani
kulibaki na juice glass moja na ile nyingine ipo
nusu, kitabu cha riwaya ‘ISABEL’ alichokuwa
akisoma yule dada kilikuwa kimefunguliwa
kurasa Fulani na kulaziwa kisu juu yake, kwenye
ile kurasa kulikuwa na tone moja la damu na
sentensi Fulani ilipigiwa mstari kwa wino
mwekundu, akaisoma harakaharaka iliandikwa
…“Kamwe hamtoweza kufisha juhudi za
kimataifa, mpango huu umesukwa na kusukika”…
…“Mimi ni mwanamapinduzi halisi, nipo hapa
kwa kazi moja tu ya kuondoka na roho yako”…
Kamanda Amata akatoa kifaa chake cha
mawasiliano na kupachika earphone sikioni
mwake,
“Umewahiwa kijana” sauti ya Gina
ilimnong’oneza
“Kaelekea wapi?” Amata aliuliza lakini kwa kuwa
alikuwa akipigwa na upepo mkali wa bahari
alijisika sikio ili asikilizane vizuri na anayeongea
naye,
“Amata!, toa mkono sikioni haraka” sauti ya
Gina ilimkaripia, Amata akashusha mkono wake
na kubaki hajui afanye nini.
JEGAN GRASHAN AMETOROKA KATIKA MIKONO
YA WANAUSALAMA, JE; WALIMPATA VIPI?
NI NANI MWANAMKE ALIYEMHUSUDU KAMANDA
AMATA PALE WHITE SANDS HOTEL?
USIKOSE CHAPISHO LIJALO
 
CHAPISHO LA 08

GINA binti Komba Zingazinga, akiwa ghorofa ya
juu katika ukumbi wa chakula wa hoteli aliweza
kuona matukio mengi yanayoendelea pale chini
akiwa kavaa miwani yake maalu yenye auto
focus ambayo si yo rahisi mtu mwingine kujua,
pindi unapotua jicho kwenye kitu Fulani na
kutulia miwani ile iliweza kukisogeza karibu
uweze kukiona kwa usahihi zaidi. Gina aliiba
miwani hii ofisini mwa Amata pindi tu aliporudi
na kutomkuta ofisini alijua wazi kuwa atakuwa
ameelekea White Sand kwani alimpa habari hiyo
tangu usiku uliopita kuwa atafanya hivyo ili
akajue nini na nani wanakutana, Gina alishaona
hali hiyo ya hatari, hivyo alimua kufuatilia kwa
mbali ili kumsaidia boss wake inapowezekana,
alifika pale hotelini na moja kwa moja akapanda
ghorofa ya juu na kutega mambo yake huko.
“Geuka nyuma uketi kiti cha upande huo!” Gina
akamueleza, Amata akatii akageuka na kuketi,
alipotazama mbele akamuona Scolleti akiwa
amekaa kitini peke yake akijisomea gazeti,
Amata aliitazama saa yake, ilikuwa imetimu saa
tisa kasoro dakika kumi, aliishusha na kujituliza,
alimwita mhudumu na kumuagiza soda baridi
lakini kabla akamuomba aondoe vile vitu pale
mezani.
Soda ilipokuja akawa anakunywa taratibu, mara
kutoka lango kuu akaona gari moja aina ya
Toyota V8 nyeupe ikiingia na kusimama jirani
kabisa na banda lile aliloketi Scolleti watu wawili
wakashuka. Mara hiyo muuza magazeti alipita
jirani na Amata, akamwita na kununua gazeti
Mwananchi na kuliafungua kisha kuanza kusoma
lakini bado aliweza kuona kinachoendelea. Watu
wawili walioteremka katika ile prado waliielekea
ile meza ya Scolleti na kusalimiana kabla ya
kuketi. Shakran Shakrum alikuwa amefuatana
pamoja na Shailan boss wake. Amata alikuwa
akiwatazama tu na kuhakikisha wasije
kumtoroka, mara kwa mbali alimuona binti yule
wa Kihindi akitokea kwenye bwawa la kuogelea
akiwa na nguo za kuogelea, Amata alimtaza kwa
shauku na kusahau kilichomleta, msichana yule
alitembea kwa madaha akipita mchangani
mpaka pale alipoketi Amata, akageuka na kumpa
mgongo Amata, “Mmmm, magnificent view”
Amata alitamka, yule msichana akageuka na
kutoa tabasamu la wizi na kuchukua taulo lake
kama lile la Amata na kulivaa, kisha akageuka
na kutoka eneo lile,
“Shiiiit!” sauti ya Gina ilimgutua Amata
alipotazama pale mezani hakuona mtu,
wameondoka.
“Gina, wameelekea wapi?”
“Sijui, mi nilikuwa nakuangali wewe na huyo
Malaya wako nageuza macho siwaoni” Gina
akajibu.
“Ok, shuka twende, hapa si salama tena” Amata
akiwa katika kuongea hilo, Nissan cedric ya
kijivu ilipita mbele yake na kufunga breki kali
kama mita ishirini hivi, watu wawili wenye sox
zilizoficha nyuso zao wakachomoza kama
umeme na kumdaka yule dada wa kihindi na
kumvutia ndani ya gari kisha ile Nissan ikatoka
kwa kasi na kusugua ile barabara kwa nguvu,
Amata aliichomoa bastora yake na kujaribu
shabaha, risasi ya kwanza ilivunja kioo cha
nyuma, ya pili ikalikosa tairi, lo tayari
ilikwishachukua barabara ya kuelekea barabara
kubwa ya Bagamoyo, Amata alikimbilia pale
alipoegesha gari yake na kuingia ndani akafunga
mkanda, na kuitia moto kabla ya kuiweka
barabarani, na kuondoka kwa kasi,
“Amataaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!” Gina aliita kwa
sauti kali, Amata alifunga breki kali na Gina
aliingia kwa kupitia dirishani kisha gari ilitolewa
kasi huku watu wakishuhudia miguu ya Gina
ikimalizikia kuingia ndani ya gari ile. Wakiwa
karibu na barabara kubwa ya kuelekea
Bagamoyo, aliiona ile Nissan ikisaga lami
kuelekea upande wa Bagamoyo, Amata naey
akaingia barabarani na kuzifanya daladala kupiga
honi ovyo, akakunja kulia na kuifukuza kwa kasi,
barabara ilikuwa nyembamba kiasi kwamba
ilikuwa ni vigumu kuwafikia, Gina alikuwa
ameketi nyuma akiwa ametulia tuli kwa woga
akiangalia jinsi kamanda anavyofanya ovateki za
hatari huku akiacha ajali nyingi nyuma yake.
“Kamanda polepole” Gina alipiga kelele
Kamanda Amata kama hakumsikia, bastola
mkono wa kulia, usukani mkono wa kushoto,
ngoma ipo 110 Km/h, baada ya dakika kadhaa
alikipita kiwanda cha saruji cha Wazo na kuipita
Tegeta, sasa walibaki wawili tu barabarani
mwendo mkali wakielekea Boko. Ile Nissan
ilikuwa ikienda kasi sana kiasi kwamba Amata
aliona wazi hatoweza kuipata, akamtazama Gina
kwenye kioo cha ndani akamuona kajikunyata
kama kifaranga cha kuku.
“Gina! Njoo uendeshe hapa nimalizie kazi!”
alimwita
“No! kamanda mi siwezi,” Gina alijibu kwa kelele
“Come on, Gina, njoo haraka” Amata alipiga
kelele huku akipigapiga usukani wa gari ile. Gina
alipita katikati ya viti huku gari ikiwa kasi sana,
Amata alhamia kiti cha abiria huku mkono
mmoja wa kulia sasa ukiwa umeshika usukani,
Gina alipenya chini ya mkono wa Amata na
kuketi nyuma ya usukani na kuikamata gari ile
barabara kabisa.
“Uuuuuuuuuuuuiiiiiiiiiiiiiii Kamandaaaaaa!!!!!!” Gina
alipiga kelele baada ya Amata kumuachia
usukani alijikuta akishindwa kuimudu na gari ile
ikayumba vibaya kisha akairudisha barabarani.
Amata akavuta saraka katika dashboard ya gari
yake na kutoa sortgun aina ya Double Barrel na
kuivunja katikati, ndivyo inavyowekwa risasi
hivyo jamani, akatumbukiza risasi mbili, kwa
maana aina hii ya short gun inabomba mbili na
lazima uweke risasi mbili na unapopiga hutoka
zote mbili. Kamanda Amata alipohakikisha
ameiweka vizuri akarukiti cha nyuma na
kutokeza dirisha la kulia nyuma akitanguliza ule
mtutu, kichwa nje alibana jicho moja sawia na
kulitafuta tairi la ile Nissan, alipohakikisha lipo
kwenye shabaha, alipotaka kufyatua trigger
tayari kupiga, alihisi gari yao ikiyumba nakisha
ikazunguka mchoro wa S, barabara yote ikitoa
harufu ya mipira na kusimama ikiangalia
ilikotoka, katikati ya barabara. Kamanda Amata
aliangukia kwenye kiti cha nyuma na kukaa,
damu zilikuwa zikimtoka pembeni kidogo ya pua
yake, shortgun yake ikiwa mapajani.
“Gina umefanya nini sasa? Tumepoteza nafasi
nzuri sana ya kutegua kitendewili chetu” Amata
alimueleza Gina amabaye alikuwa anatetemeka
kama mgonjwa mwenye homa kali, “Gina, Gina!”
Amata aliita na alipojinyanyua kuangalia kule
kwa Gina, “Shiiiiiiit!!!!”….
Nyoka mkubwa aina ya black mamba alikuwa
akitoka chini ya kiti cha dereva na taratibu
akawaakijizungusha karibu na mguu wa Gina,
Kamanda Amata alimtazama huku akiuma meno,
aliichomoa bastola yake na kumlenga sawia na
kukifumua kichwa chake, risasi ile
ilisambarataisha kichwa cha nyoka yule. Gina
alishusha pumzi na kufungua mlango, akatoka
nje akiwa hajiamini. Kamanda Aamata alitoka na
kwa kutumia mtutu wa ile shotgun kamtoa nje
yule nyoka, alikua nyoka mkubwa sana, kisha
akavaa miwani yake na kuchungulia chini ya kiti
kimoja baada ya kingine na kuhakikisha hakuna
hatari yoyote.
“Washenzi sana, saa ngapi walituwekea huyu
nyoka?” alijisemea huku akiizunguka gari yake
na kutoa sonyo refu kisha akamuendea Gina
aliyekuwa bado kasimama hajielewi, akamshika
mkono na kumvutia upande wa pili, “Pole
mrembo, panda twende,” alimsihi na kisha
kumfungulia mlango, naye akaingia upande wa
dereva kisha akageuza gari na kurudi mjini.
≈ ≈ ≈
“Siku ya nne sasa inaisha, deni letu kwa serikali
linabakia siku tatu, mnafikiri watatekeleza ombi
letu?” Shailan aliwaeleza wenzake.
“Hata kama siku zimebaki tatu, tena tuseme
mbili kwa sababu hii ya nne inaisha, bado
tuendelee kuwasubiri kwa maana hatujui wana
lengo gani.” Shakrum akajibu.
“Hata hivyo, lazima tuanze kuandaa mazingira
ya shambulizi la mwisho, shambulizi baya kuliko
yote ambalo dunia lazima itetemeke kwa hofu na
Afrika iishi kwa wasiwasi, wakati Tanzania
itajutia uamuzi wake,” Shailan alimjibu Shakrum.
Scollet muda wote alikuwa akiwasikiliza, alikuwa
kimya kabisa kama mtu ambaye hayupo pale,
kisha kama aliyegutushwa kutoka usingizini,
“Sasa mnataka kufanya nini?” aliuliza.
“Hilo kwa sasa hatuwezi kuzungumzia kwa
sababu kuna mawili, maana hili jukumu inabidi
limalizwe Julai 7 na mtu wetu awe mikononi kwa
njia yoyote ile, lakini kama watakuwa na shingo
ngumu kama ya Firauni basi watajua sisi ni nani,
kesho watapata ujume wao wa mwisho,” Shailan
alimalizia kauli yake, alikuwa akiongea kwa jazba
sana wakiwa wamesimama pwani karibu kabisa
na bahari ya mti kwenye mchanga mweupe wa
White Sand Hotel baada ya kuhama pale
walipokuwa wameketi kwanza baada ya kupewa
taarifa ya kujihami na walinzi wao waliokuwa
eneo lile.
“Itabidi tuombe silaha mbili za kutumia kwa
mara nyingine, silaha hai,” Shakram alimwambia
Shailan.
“Yeah, huo ndiyo mpango!”
Mazungumzo ya watatu hawa yaliendelea kwa
takriban nusu saa kisha wakiwa kulekule pwani,
boti moja ndogo ilikuja na kusimama umbali
kama wa mita hamsini, wote wakaingia majini na
kuingia kwenye hiyo boti kisha wakaondoka zao
eneo lile. Walifanya hivyo kadiri ya maelekezo ya
walinzi wao waliowaweka pale tangu mapema
kuangali kama kuna lolote baya juu yao, hivyo
wakawashauri waondoke kutumia usafiri wa maji
kwani hakuna usalama barabarani kwa wakati
ule, hivyo waliliacha gari lao pale kwa minajiri ya
kuja watu maalumu kwa kazi hiyo na kuliondoa
eneo lile.
Shakrum, alichukua simu yake ya upepo na
kubofya kitufe Fulani, “Vipi mzigo umefika
salama?”
“Yeah, umefika salama japokuwa tulipata
msindikizaji njiani” alijibiwa.
“Msindikizaji?! Mliweza kumng’amua
hakuwaletea shida?” Shakrum aliuliza
“Yeah, na kama si mbinu aliyotumia Staina saa
hizi tungeongea mengine,”
“Atakuwa nani huyo?”
“Nafikiri ni kachero wa serikali”
Shakrum alishusha simu yake na kupumua kwa
nguvu, Shailan alimtazama na kumtupia swali,
“Vipi?”
“Jamaa wanasema walipata msindikizaji njiani,”
Shailan alishtuka kidogo kwa jibu hilo. Mpaka
dakika hiyo hawakugundua uwepo wa Amata
eneo lile hivyo wao walizitazama hatari nyingine
tu.
≈ ≈ ≈
GETI KUBWA lilifunguliwa na gari ndogo aina ya
Subaru iliingia taratibu ndani ya yadi hii kubwa
iliyosheheni malori ya mafuta yasiyopungua mia
moja, gari ile iliegeshwa pembeni na milango
yake kufunguliwa, vijana wane walishuka na
msichana yule wa Kihindi,
“Huku tafadhali,” mmoja aliwaongoza, na
wengine wakafuatia wakiwa wamemshika yule
mwanamke uku na huku ijapokuwa walimfunga
kamba za katani mikono yake. Walitembea nae
mpaka kwenye jengo lingine lililoonekana
kutumiwa kama ofisi, wakaingia na kumtupia
yule dada wa Kihindi na kumfunsia ndani ya
kijichumba fulani.
“Aaah, Mungu mkubwa, sikutegemea kama
tutafika salama,” mmoja wao aliyekuwa ndiye
dereva aliwaambia wenzake, aliliendea jokofu
kubwa lililokuwa katika ofisi hiyo ndogo na
kuchukua konyagi ndogo kisha akaifungua na
kupiga funda moja na kuirudisha jokofuni.
4
KAMANDA Amata alijitupa kwenye kochi kubwa
na kuvuta chupa ya maji iliyokuwa mezani na
kuigugumia yote kama mtu aliyetoka jangwani na
kuteseka kwa jua na vumbi.
“Gina, unaendeleaje?” alimuuliza Gina aliyekuwa
hoi katika kochi lingine upande wa pili.
“Sijiamini kama nimefika hapa salama, Amata
naogopa sana nyoka, leo sijui kama ntaweza
kulala nyumbani peke yangu” alijibu.
“Usijali utalala hapa kwangu kama shida ni uoga,
angalau hata jiko langu leo liwashwe” kisha wote
wakacheka.
“Gina, asante kwa kuniokoa, hivi yule mwanamke
wa Kihindi ni nani?”
Gina badala ya kujibu akacheka kwanza na
kumtazama Amata usoni.
“Amata, siku yako ya kufa utakuwa umelala na
mwanamke kitandani, maana ndiyo udhaifu wako
huo. Ile juice haikuwa na sumu ni mimi tu
nilitaka uwe makini na lililokupeleka na siyo
kufuatilia wanawake wa watu,” Gina alijibu.
Amata akasonya na kujiweka vizuri, “Na we
ulikujaje kule?”
“Ha, mi si ni secretary wako, lazima nijue
uendako na nikuandalie kila kinachotakiwa
ikiwamo usalama. We mwenyewe ulinambia
kuwa utaenda kule kwa sababu hizi, lakini
sikuweza kutulia kwa kuwa naona wivu,
wanawake wengine wakafaidi na mi nipo hapa
nakula kwa macho. Nikatangulia, nikachukua tax
na kuja kisha nikaketi juu ghorofani nikiangalia
mazingira, tangu unaingia nilikuona na kila
ulichofanya, ulipokwenda kuogelea ndipo yule
mwanamke wa Kihindi alikuja pale ulipoketi
kwanza, ulipoacha taulo lako naye akaketi.
Kiukweli sijui alikuja wakati gain na ni nani lakini
nilimuona pindi tu alipokuja pale ulipoketi.
Mwanzoni nilijua wamekuwekea mtego ndiyo
ulikuwa wasiwasi wangu lakini nimeshangaa kwa
nini wale jamaa wamemteka tena, ina maana si
mwenzao?” Gina alieleza na kuuliza.
“Mi sijui, maana nimeona wakiondoka nae, ndiyo
maana niliwafukuza ili niujue ukweli,” Amata
alijibu na kubaki kimya kwa muda.
Mara pale kwenye kochi simu ya Amata ikaanza
kuita kwa fujo, akaangalia namba haijui, akatulia
na kuiacha, baada ya muda meseji ikaingia,
akaichukua nakuisoma
‘…Natafutwa, nafuatiliwa na watu nisiowajua,
naomba msaada… Mwad…”
Kamanda Amata akashusha pumzi na kuisoma
tena ile meseji, kisha akampa simu Gina naye
akasoma.
“Nani huyo?” akauliza Gina
Amata akamsimulia Gina kisa chote cha
msichana Mwadawa, tangu walipokutana pale
ofisini na kisha kuachishwa kazi.
“Mh! Itakuwa wanamuwinda sana” Gina alijibu.
Kamanda Amata alijaribu kuipigia ile namba
lakini mara ya kwanza haikupatikana, alipojaribu
mara kadhaa aliipata na kuongea naye.
Mwadawa alikuwa akiongea kwa sauti ya chini.
“Bwana Stephen, nipo matatizoni unisaidie
tafadhali” sauti ya Mwadawa ilisema
“Uko wapi sasa?” Amata (Stephen wa bandia)
aliuliza.
“Nimejificha huku Kariakoo shimoni” alijibu
“Ok, subiri hapo nakuja” alimueleza, “ Gina
twende,”
“Aah we nenda mwenyewe, saa hizi muda wa
kazi umeisha” Gina aliongea na kucheka.
Kamanda Amata alijiweka tayari bastola zake
mbili kiunoni, akaenda stoo na kuchukua pikipiki
lake kubwa kisha kutokomea mjini.
******
MTAA wa Tandamti ulikuwa na shughuli nyingi
kama kawaida yake, watu wengi wakubwa kwa
wadogo walionekana wakitafuta hiki na kile,
magari ya lioegeshwa bila mpangilio
yalisababisha msongamano na kufanya mtaa ule
kuwa vigumu kupita, achilia mbali wale
walioweka bidhaa zao chini nao walileta tabu
kwa watumia njia hiyo.
Kamanda Amata aliiacha barabara ya Msimbazi
na kuchukua ile ya Swahili kuelekea soko kuu la
Kariakoo, kwa mwendo wa wastani alipita huku
akingalia huku na kule, watu walilishangaa sana
pikipiki lile na jinsi lilivompendeza muendeshaji
wake, punde kidogo alisimama mbela ya posta
ndogo karibu na kituo cha daladala za Mwenge,
akatulia kidogo akijaribu kupanga na kupangua
ili ajue aanzie wapi. Aliitazama saa yake, muda
ulikuwa unamtupa mkono, akaondoa pikipiki lake
na kuzunguka upande wa pili wa soko hilo
kubwa mpaka pale kwenye foleni ya malori
yanayosubiri kuingia shimoni ili kushusha mazao
yaliyobeba kutoka mikoani na sehemu
mbalimbali za nchi, akachukua simu yake na
kubonya namba Fulani Fulani kisha akaiweka
sikioni,
“…yeah, niko hapa kwenye lango la kuingilia
magari, njoo utanikuta…” kisha akatega sikio
kusikia sauti ya upande wa pili,
“…naogopa kutoka wananifuata…” alijibiwa
“…njoo nakusubiri hapa hakuna lolote
litakalotokea…” alimhakikishia usalama kisha
akasubiri pale nje bila kushuka kwenye lile
pikipiki lake.
Mwadawa Said alitokeza taratibu kwenye lile
lango na kuanza kupandisha kuelekea huko
yalikopaki yale malori. Kamanda Amata alitulia
pembeni mwa lori mojawapo akiwa bado kavalia
ile kofia ngumu na mikono ikiwa mfukoni
akiangalia wote watokao na waingiao, kwa mbali
alimuona yule binti akiwa anakuja kwa mwendo
wa uwoga uwoga, alipokaribia kumaliza lile lango
vijana wawili walitokea kwa nyuma yake na
kumfuata taratibu, walizidi kumkaribia, kabla
Mwadawa hajamaliza ule muinuko wa ile njia
kuyafikia yale malori wale vijana walimshika
mmoja mmoja mkono huu na mwingine mkono
mwingine kisha wakbadili uelekeo na kupita kati
ya malori yaliyokuwa yameegeshwa hapo.
Kamanda Amata alizunguka upande wa nyuma
wa malori yale na kupita kati yake, uso kwa uso
akiwa anatazamana na wale vijana walikuwa
wakielekea kukutana kati ya malori yale. Hatua
kama tano hivi walikutana katikati, Amata
alisimama, na wale vijana walifanya vivyo hivyo,
akakisukuma juu kioo kilichozuia macho yake
cha lile kofia gumu la kuendeshea pikipiki,
akawatazama wale vijana waliomshika
Mwadawa, wakabaki wakitazamana na hakuna
aliyeongea kati yao, Kamanda Amata
akawaoneshea ishara kuwa wamuachie yule
msichana, lakini amri hiyo hakuna aliyeitii badala
yake wakageuka naye na kurudi walikotoka,
mara nyuma yao wakasikia mlio wa bastola
inayoondolewa usalama tayari kwa kazi,
wakageuka na kutazamana na domo la bastola
iliyofungwa kiwambo cha sauti ikiwa kwenye
mikono imara ya Amata, bastola yenyewe, sura
ya aliyeishika vyote viwili havikuonekana kuwa
na masihara hata kidogo, hawakuwa na ujanja,
walijikuta mikono yao ikilegea na kumuachia yule
msichana, Mwadawa akatoka kwa hatua za
haraka na kujificha nyuma yake, bado wakiwa
katikati ya malori yale hakuna mtu yoyote eneo
lile aliyejua kinachoendelea, Amata hakuona haja
ya kuanzisha timbwili katika eneo lile kwa kuwa
kungeweza kuleta madhara kwa Watanzania
wengi ambao amani imewafanya wajinga hata
kupenda kushangaa matukio ya hatari kama
hayo kana kwamba wanaangalia sinema.
Alimchukua Mwadawa, na bastola yake mkononi
na kugeuka kuanza kuondoka huku akionesha
kuwa hajali nyuma kuna nini, wale viajana
walimtazama mpaka alipoishia katika yale malori akiwa na windo lao.
******
MTAA wa Tandamti ulikuwa na shughuli nyingi
kama kawaida yake, watu wengi wakubwa kwa
wadogo walionekana wakitafuta hiki na kile,
magari ya lioegeshwa bila mpangilio
yalisababisha msongamano na kufanya mtaa ule
kuwa vigumu kupita, achilia mbali wale
walioweka bidhaa zao chini nao walileta tabu
kwa watumia njia hiyo.
Kamanda Amata aliiacha barabara ya Msimbazi
na kuchukua ile ya Swahili kuelekea soko kuu la
Kariakoo, kwa mwendo wa wastani alipita huku
akingalia huku na kule, watu walilishangaa sana
pikipiki lile na jinsi lilivompendeza muendeshaji
wake, punde kidogo alisimama mbela ya posta
ndogo karibu na kituo cha daladala za Mwenge,
akatulia kidogo akijaribu kupanga na kupangua
ili ajue aanzie wapi. Aliitazama saa yake, muda
ulikuwa unamtupa mkono, akaondoa pikipiki lake
na kuzunguka upande wa pili wa soko hilo
kubwa mpaka pale kwenye foleni ya malori
yanayosubiri kuingia shimoni ili kushusha mazao
yaliyobeba kutoka mikoani na sehemu
mbalimbali za nchi, akachukua simu yake na
kubonya namba Fulani Fulani kisha akaiweka
sikioni,
“…yeah, niko hapa kwenye lango la kuingilia
magari, njoo utanikuta…” kisha akatega sikio
kusikia sauti ya upande wa pili,
“…naogopa kutoka wananifuata…” alijibiwa
“…njoo nakusubiri hapa hakuna lolote
litakalotokea…” alimhakikishia usalama kisha
akasubiri pale nje bila kushuka kwenye lile
pikipiki lake.
Mwadawa Said alitokeza taratibu kwenye lile
lango na kuanza kupandisha kuelekea huko
yalikopaki yale malori. Kamanda Amata alitulia
pembeni mwa lori mojawapo akiwa bado kavalia
ile kofia ngumu na mikono ikiwa mfukoni
akiangalia wote watokao na waingiao, kwa mbali
alimuona yule binti akiwa anakuja kwa mwendo
wa uwoga uwoga, alipokaribia kumaliza lile lango
vijana wawili walitokea kwa nyuma yake na
kumfuata taratibu, walizidi kumkaribia, kabla
Mwadawa hajamaliza ule muinuko wa ile njia
kuyafikia yale malori wale vijana walimshika
mmoja mmoja mkono huu na mwingine mkono
mwingine kisha wakbadili uelekeo na kupita kati
ya malori yaliyokuwa yameegeshwa hapo.
Kamanda Amata alizunguka upande wa nyuma
wa malori yale na kupita kati yake, uso kwa uso
akiwa anatazamana na wale vijana walikuwa
wakielekea kukutana kati ya malori yale. Hatua
kama tano hivi walikutana katikati, Amata
alisimama, na wale vijana walifanya vivyo hivyo,
akakisukuma juu kioo kilichozuia macho yake
cha lile kofia gumu la kuendeshea pikipiki,
akawatazama wale vijana waliomshika
Mwadawa, wakabaki wakitazamana na hakuna
aliyeongea kati yao, Kamanda Amata
akawaoneshea ishara kuwa wamuachie yule
msichana, lakini amri hiyo hakuna aliyeitii badala
yake wakageuka naye na kurudi walikotoka,
mara nyuma yao wakasikia mlio wa bastola
inayoondolewa usalama tayari kwa kazi,
wakageuka na kutazamana na domo la bastola
iliyofungwa kiwambo cha sauti ikiwa kwenye
mikono imara ya Amata, bastola yenyewe, sura
ya aliyeishika vyote viwili havikuonekana kuwa
na masihara hata kidogo, hawakuwa na ujanja,
walijikuta mikono yao ikilegea na kumuachia yule
msichana, Mwadawa akatoka kwa hatua za
haraka na kujificha nyuma yake, bado wakiwa
katikati ya malori yale hakuna mtu yoyote eneo
lile aliyejua kinachoendelea, Amata hakuona haja
ya kuanzisha timbwili katika eneo lile kwa kuwa
kungeweza kuleta madhara kwa Watanzania
wengi ambao amani imewafanya wajinga hata
kupenda kushangaa matukio ya hatari kama
hayo kana kwamba wanaangalia sinema.
Alimchukua Mwadawa, na bastola yake mkononi
na kugeuka kuanza kuondoka huku akionesha
kuwa hajali nyuma kuna nini, wale viajana
walimtazama mpaka alipoishia katika yale malori
akiwa na windo lao....
NANI ANAMTAFUTA MWADAWA, KWA NINI?
 
CHAPISHO LA 09

Mwendo wa dakika kumi na tano, Kamanda
Amata alimfikisha Mwadawa nyumbani kwake,
na kumkuta Gina amekwishaandaa chakula,
akawakaribisha na wote wakaketi vitini.
“Asante Stephen,” ilikuwa ni sauti ya Mwadawa
iliyoongea katika hali ya kutojiamini.
“Karibu sana, hebu nambie hawa jamaa
wamekufuata tangu lini?” Kamnda aliuliza,
wakati huo alikuwa ameiwasha simu yake yenye
uwezo wa kurekodi sauti.
“Jana jioni niliwaona watu hawa karibu na
nyumba ninayoishi, lakini sikuwafuatilia
ijapokuwa walikuwa eneo lile karibu siku nzima,
leo asubuhi nilikuwa nina shughuli zangu mjini
ndipo nilipowaona kila ninapokwenda mpaka
mchana huu nilipoona sasa hali inakuwa zaidi,
walijaribu kunikamata mara mbili lakini nikawa
nawakwepa kwa kujichanganya na makundi ya
watu, mara ya mwisho hii nilijifanya nanunua
matunda pale soko dogo nikawaona mmoja
kushoto na mwingine kulia, nikaondoka
nikakimbilia kule shimoni, nikaikumbuka kadi
yako ulonipa ndo nikakupigia.” Mwadawa
alieleza.
“Kabla ya hapa uliwahi kuwaona hawa watu?”
lilikuwa swali lingine zuri kutoka kwa Amata.
“Kwa kweli hapana sijawahi kuwaona kabisa,”
alijibu mwadawa.
“Ok, hebu leo niambie ukweli bila kuficha,
kampuni yenu ya ulinzi na matukio ya milipuko
ya mabomu vina uhusiano wowote?”
“Aah kwa kweli bwana Stephen, mi sina uhakika
sana, ila tu siku ile ulipokuja ofisini nilisikia
jambo moja likiongelewa ambalo lilinitia
wasiwasi,” aliposema hayo Amata akajiweka
vizuri, “Enhe, jambo gain hilo?” aliuliza.
“Nilisikia wakiongelea sana lile jengo la JM MALL
kwa sababu mimi nilikuwa nawapelekea chain a
kahawa kule ofisini nilikuwa nasikia hilo pia
walikuwa na ramani nahisi ni ya jengo hilo,”
Mwadawa alieleza kwa kusitasita, Amata
akaingiza mkono mfukoni na kutoa simu
nyingine aina ya Nokia Lumia na kufungua
sehemu ya picha, “Huyu unamjua?” ilikuwa ni
picha ya msichana aliyeonekana kama chotara
wa kiarabu na kiswahili, Mwadawa aliichukua ile
simu na kuangalia vizuri, akawa kama anajaribu
kumgusa mwanadada huyo pichani, “Niambie
unamjua?” swali la Amata lilimshtua Mwadawa,
“Ndiyo namjua, nilimuona siku moja kabla yaw
ewe kuja ofisini, alikuja pale ofisini kwetu
akiongozana na kijana mmoja wa kiarabu lakini
ni raia wa Kazakhistan,” alijibu kwa ufasaha.
“Ok, unaweza kunambia ana uhusiano na boss
wako bwana Scolleti?”
“Bwana Scolleti, alinitambulisha hawa watu wote
kuwa ni business partiners wake kutoka mbali,
hivyo wana vikao vya kubadilishana mawazo juu
ya biashara zao,” Mwadawa alieleza. Kamanda
Amata akaichukua ile simu na kutafuta picha
ingine akamuonesha Mwadawa, “Huyu
unamjua?” lilikuwa swali lingine kwa Mwadawa.
“Uuuuuuhhhhh!!!! Yeah, si ndiyo yule dada au?”
alijibu kwa swali na kushusha pumzi ndefu.
Amata akaizima ile simu na kuiweka mfukoni
mwake, akajiweka vizuri pale alipoketi.
“Ameokotwa amekufa jana, una habari na hilo?”
Amata alimuuliza Mwadawa ambaye alijibu kwa
kutikisa kichwa chake kushoto kulia kwamba
hajui chochote, kisha akabaki ameduwaa, na
mara machozi yakaanza kumdondoka.
“Unalia nini?” Amata aliuliza
“Dah, Stephan, huyu dada wakati anaondoka
pale na wale vijana alinipa noti ya dollar mia
moja ya Kimarekani akanambia, hatutaonana
tena hela hii itakuwa kumbukumbu yako na
msaada mkubwa kwa watakaohitaji, akanikabidhi
na kuondoka,” Mwadawa aliangusha machozi ya
haja kwa kilio. Kamanda Amata akainuka kutoka
alikoketi kwenda kwenye kikabati kidogo na
kutoka na kitu kama kitambaa laini akampatia
Mwadawa kwa ajili ya kufuta machozi yake.
Amata akatazamana na Gina aliyekuwa ameketi
pembeni akijinywea coca cola yake huku akingali
runinga kubwa iliyokuwa mbele yake. Baada ya
kunyamaza kulia kule wote watatu walienda
mezani na kupata chakula cha mchana, lakini
Amata bado alikuwa kaidadisi huku na kule.
“Boss wako Scolleti, ana biashara gain au
kampuni ngapi?”
“Kwa hapa Tanzania ana huu mradi wa
zimamoto na pia ana kampuni kubwa ya
kusambaza mafuta, ananunua mafuta Uarabuni
na kuyaleta hapa, ana tanker zake zaidi ya mia
mbili zinapeleka karibu nchi zote za SADC”
“Du, amejiimarisha kweli, na yard yake ipo
wapi?” Amata aliendelea kuchimbachimba
“Yadi moja ipo pale External Mabibo karibu na
hostel za chuo kikuu, lakini ile ni ndogo, kubwa
kabisa ambayo pia ina matank makubwa ya
mafuta ipo Bunju njia ya Bagamoyo, pale ndiyo
kila kitu”
≈≈≈
“HARAKATI za ukombozi zinaendelea huko
duniani na tunaamini ndani ya masaa sabini na
mbili yajayo utakuwa huru ijapokuwa bado
wamekaakimya hadi sasa” Mtu mmoja wa
makamo alikuwa amesimama upande wa pili wa
nondo za gereza akiongea na Jegan Grashan
kwa lugha ambayo watu waliokuwa hapo
hawakuelewa.
“Itapendeza kuona taifa letu linakuwa huru dhidi
ya utawala wa kibeberu wa Maghalibi, wao ni
nani hata watake kuitawala dunia, ndugu
piganeni kwa nguvu zote, na siku ya kiyama
mtapata thawabu yenu, mimi nimepigana kadiri
ya uwezo wangu na sasa niko hapa gerezani ila
naamini wazi kuwa nitakuwa huru na nitaendelea
na mapambano mpaka tulikomboe taifa nyonge
ambalo Wamaghalibi hawataki kuliona duniani,
Mungu mkubwa ndugu,” Jegan aliongea kwa
hisia huku akiwa ameishika mikono ya ndugu
yake huyo aliyeonekana kuwa ni mtu wa
makamo kwa jinsi uso wake ulivyoonekana
ukiwa na mikunjo michache na ngozi iliyoanza
kuchoka kwa mbali.
“Usichoke kuomba, ndugu zako tutapigana
mpaka mwisho,” alimalizia mazungumzo yake na
kuziachia zile nondo, alipopiga hatua kadhaa
alisimama na kugeuka nyuma kumwangali ndugu
yake huyo Jegan Grashan ambaye pamoja na
kukimbia katika mikono ya vyombo vya usalama
nchi mbalimbali za dunia hatimaye alijikuta
akinasa katika idara makini ya usalama ya
Tanzania, idara isiyofanya mzaha kwenye kazi
kama hiz, ikiongozwa na viongozi makini na
ikifanya kazi na watu makini walio makini katika
mambo yanayohitaji umakini. Ijapokuwa mara ya
kwanza alijaribu kutoroka pale JNIA (Julius
Nyerere International Airport) lakini mwisho wa
yote alitiwa mkononi na vikosi mahiri vya
usalama hapo Handeni Tanga akiwa mbioni
kutoroka nchini shida ilikuwa ni jinsi gani ya
kuvuka mpaka kwa maana kila uchochoro
ulidhibitiwa kuhakikisha kiumbe huyu hatari asiye
na chembe ya huruma hatoki nchini labda
ageuke njiwa au upepo. Kila mtu alikuwa makini
na kitengo chake mpaka pale walipopata fununu
kutoka Mkoa wa Tanga kuwa inasadikiwa gaidi
huyo amejichimbia huko.

Rudi Miaka Mitatu nyuma
Handeni Tanga
BAADA ya msako na uchunguzi mkali wa
makachero wa serikali, takribani ya mwaka
mmoja iliwachukua kupata fununu kuwa Jegran
Grashan alikuwa huko Tanga katika eneo la
Handeni, kwenye moja ya nyumba ambayo
inasadikiwa huwa hakuna mtu anayeishi
isipokuwa hutumiwa kama stoo ya kuhifadhia
makorokoro kutoka katika kiwanda cha mkonge.
Iliposadikiwa hilo mmoja wa makachero ambaye
alipanga chumba eneo hilo la makazi ya watu ila
ni mbali kidogo na lile shamba la mkonge
ambako kunai le stoo tajwa. Baada ya kuishi
eneo hilo na kuzoeleka na waenyeji alianza
kufuatilia kwa umakini wote juu ya lile eneo na
kuchukua kila kilichokuwa kikiongelewa kwenye
vijiwe vya vijana au vilabu vya pombe, mara
kadhaa amekuwa akienda kule shambani kwa
ajili ya kujipatia kibarua cha siku moja au mbili,
mara nyingine alipata na mara nyingine
hakupata. Ndipo wakati Fulani zilipotangazwa
nafasi za vibarua wenye ujuzi, naye alijitokeza
akiwa na ujuzi wa kuendesha trekta, Mungu si
Athumani akajipatia kazi ile na hapo ndipo
alipoanza kwa umakini juu ya kazi yake
iliyompeleka pale.
Siku moja alipangwa kupeleka takataka huko
katika ile stoo, kwake ilikuwa ni nafasi nzuri
kwake. Kijana huyu ambaye daima aliizowesha
jamii kuwa yeye ni mpenda miwani siku hiyo
kama kawaida alikuwa na miwani yake nzuri,
daima alipokuwa kazini miwani ile aliivua na
kuiweka mahala ili aweze kufanya kazi zake,
hata mabosi wake wale maburushi walimzoea
kwa hilo. Ilikuwa ni mchana kama wa saa nane
hivi alipoegesha treat lake karibu kabisa na
mlango wa ile stoo, wale vibarua alokuwa nao
wakafungua geti naye akaingiza lile trela la
trekta kisha akashuka na kuingia mle ndani kwa
minajiri ya kuwasidia wale wenzake kushusha
zile takataka, akaivua miwani yake na kuiweka
juu kwenye kidirisha Fulani ambacho
kilitazamana na mlango mmoja ulioonekana
katika jumba hilo. Baada ya kushusha takataka
zote walionsoka na kurudi kazini. Muda
ulipotimu wakafunga kazi na kuondoka, akiwa
tayari keshaliacha lile eneo na wenzake
akajifanya kukumbuka miwani yake, kwa kweli
alionekana kuchanganyikiwa kwa namna moja au
nyingine lakini walimpoza kuwa asijali siku ya
pili ataiona miwani hiyo.

Siku iliyofuata…
KAMA kawaida vibarua waliingia kazini na jambo
la kwanza yule kijana aliivua miwani nyingine
aliyoivaa siku hiyo, hakuonesha kujali juu ya ile
miwani aliyoiacha kule. Ilipotimu saa nane kama
kawaida alikuwa juu ya trekta na wenzake
wakienda kule stoo, walipofika jambo la kwanz
ayule kijana akaiendea miwani yake nakuikuta
kama ilivyo akaichukua na kuwaonesha wenzake
kuwa ameikuta salama, kila mtu alifurahi. Baada
ya kila kitu kumalizika walirudi kazini na kufunga
ofisi kisha kutawanyika kila mmoja na anakoishi.
Yule kijana aliketi chumbani kwake na akiwa
kajifungia mlango, akaichukua ile miwani na
kubetua kioo kimoja ambacho kilitoka katika ile
fremu yake, akamisnya sehemu Fulani palepale
alipotoa kioo kile na mara memori kadi ndogo
ikatoka, akaichomoa na kuchukua dvcam yake
kisha akaipachika ile kadi na kuwasha ile dvcam,
sekunde kadhaa ikaonekana kwenye kile kioo
kidogo picha ya watu watatu walioingia eneo lile
jioni wakiwa na bunduki nzito zilizosheheni
risasi, waliongea mambo mengi ambayo yote
yalisikika vyema katika mashine ile, watu wale
watatu aliwatambua vyema kwa kuwa mara
nyingi aliwaona hata pale kiwandani, picha
ikaendelea, mtu wa nne alionekana kuongezeka
baada ya kama nusu saa ya ile picha kuendelea,
huyu hakumjua, alimzoom mara kadhaa lakini
sura yake haikuonekana vizuri kutokana na
mwanga hafifu wa mbala mwezi, wasiwasi
ulimjaa na kuamini maneno ya watu kuwa ndani
ya stoo ile kuna watu wanaishi. Tafutishi yake
ya pili ilimpa jibu sahihi la kuwa kuna mtu zaidi
ya walinzi hujumuika usiku, lakini bado hakuwa
na uhakika ni nani mtu huyo, taarifa hizo zenye
kila dalili ya mafanikio zilifika makao makuu ya
idara ya usalama wa Taifa, Kamanda Amata
aliyekuwa akifuatilia na ndiye aliyemtuma kijana
yule mbichi kabisa katika kazi hiyo alifurahi
kuona majibu anayoyapata kuwa yalikuwa na
uelekeo chanya.
Jegan Grashan, mara baada ya kutoroka pale
uwanja wa ndege mwaka mmoja uliopita, na
kuwaacha Kamanda Amata, Madam S na Chiba
hoi alipotelea mitaa ya Kujichanganya na wakazi
wa eneo hilo waliokuwa kwenye pilikapilika
nyingi, hakuna aliyemtilia shaka kwani utulivu
wake ulikuwa na ngao tosha ya kujifunika,
alikodi tax na ikampeleka moja kwa moja mpaka
Posta kwenye bandari ndogo ya Zanziba na
kuiwahi boti iliyokuwa inaondoka muda huo,
wakati taarifa zinasambazwa kubana kila mahali
tayari ile boti ilikuwa kilomita moja kutoka
kwenye gati hiyo, Jegan Grashan aliiona Dar es
salaam ikizidi kuwa ndogo na mara ikamezwa na
maji ya bahari, baada ya dakika tisini ile boti ya
Sea Express ilikuwa tayari ikiingia katika bandari
ya Zanzibar, akiwa kama gaidi mzoefu alielewa
wazi kuwa lazima pale langoni kutakuwa na
ulinzi wa kumnasa, hivyo aliposhuka tu hakupita
katika mlango mkuu bali alishuka na kuyaelekea
madau yaliyoegeshwa mahali hapo na kukodi
moja limpeleke Pemba, kutokana na pesa
aliyolipa dau lile lilimpeleka mpaka Pemba usiku
huo, masaa nane yaliisha wakiwa baharini
kwenye mawimbi na dhoruba kali, Jegan Grasha
alikaa Pemba kwa muda mfupi na kuondoka kwa
dau lingine mpaka Tanga alipopokelewa na
swahiba zake ambao walikuwa wkijua kila
kinachoendelea na wakaja kumuhifadhi hapo
wakimpatia kila kitu, walinzi waliokuwa
wakiendelea kulinda stoo ile kubwa walielewa
mchezo mzima, na daima walipoketi walikuwa
wakijua kuwa mtu huyo anatafutwa hivyo
walimshauri akae hapo kwa muda mpaka
mambo yatakapotulia kumbe hawakujua kuwa
kimya kingi kina mshindo mkuu.
Katika idara ya utambuzi ya usalama wa Taifa,
Picha zilizopigwa na ile camera ya kisasa
iliyofungwa katika miwani aliyokuwa akiitumia
yule kijana zilifanyiwa uchunguzi wa hali ya juu
katika vifaa vya kisasa kabisa vilivyoweza
kufananisha picha za mtu zaidi ya mia moja na
baada ya kufanya utafiti huo uliochukua takribani
siku nne jibu lililokuja lilikuwa lilelile kuwa mtu
huyo si mwingine bali ni Jegan Grashan. Kazi
ikawa ni jinsi gani ya kumtia mkononi mtu huyo
hatari ambaye bila shaka yoyote lazima atakuwa
na silaha za kujihami ambazo hazitojali kukuua
iloimradi yeye aokoke, mkakati ukapangwa,
wanajeshi watatu mahili wakaungana na
Kamanda Amata kufanya kamato hilo usiku wa
manane.
Chopa la kijeshi liliandaliwa na usiku huo liliruka
kutoka uwanja wa ndege wa jeshi majumba sita
ukonga na kuelekea Handeni Tanga,
wakiongozwa na signal maalum iliyowekwa
katika jengo lile katikati ya takataka na yule
kijana alipoenda kumwaga taka siku ile.
“Heyyyyyy!” zilikuwa kelele za rubani wa chopa
ile akiwashtua wapiganaji wake, kisha
akawaonesha ishara kuwa tayari wamekaribia.
Kila mtu akajiandaa kwa kuvaa gas mask zao
zilizowaficha sura zao, bunduki kubwa za kivita
na silaha ndogondogo zilikuwa sambamba nao,
rubani wa chopa ile aliishusha pembeni kidogo
ya stoo ile, walinzi walipoona hayo
wakahamainika na kuanza kutaka kuishambulia
ile chopa, yule rubani akawasha taa kali sana
iliyofungwa mbela ya chopa hiyo na kuwanya
wale walinzi kushindwa shabaha na kuficha
macho yao, Kamanda Amata na wale wapiganaji
wa jeshi waliteremka kwa kuruka na kuvamia
moja kwa moja jengo hilo, upinzani ulionekana
dhahiri, kwani wale walinzi walionekana kumudu
hasa mapigano ya silaha, walipoamuriwa
kusalimu amri walibisha vikali na kushambuliwa
kwa risasi ma kuuawa, moja kwa moja msako
uliamia ndani ya jengo hilo huku askari wawili
wakibaki nje kulinda usalama, Kamanda Amata
na mmoja waliingi ndani, hawakutegemea kukuta
jumba kubwa la kifahari lililojengwa chini ya
ardhi, ndani ya chumba kimoja walimkuta Jegan
Grashan akiwa ameketi bila wasiwasi wowote,
hakuonesha upinzani wowote kama
ilivyotegemewa, Kamnda Amata alitulia kwanza
kuona mtu huyo katulia namna ile, akamwita
Jegan asimame kutoka pale alipokaa na asogee,
lol Jegan alikuwa amekalia bomu ambalo lilibaki
muda mchache kulipuka, hakuna kulala. Yule
mwanajeshi alimshika mkono Jegan na kumvuta
kutoka naye nje, walipofika nje hawa kumaliza
hata geti,
NINI KILITOKEA?
USIKOSE CHAPISHO LIJALO...
 
CHAPISHO LA 10

...ishara waliyoitoa kwa rubani ndiyo iliyosaidia
rubani yule kuelewa na kuligeuza lili chopa
haraka kuliondoa eneo lile, “Chiniiiiiiii !!!!!!” yule
mwanajeshi alipiga kelele na wote wakalala chini
pamoja na wale walioimarisha ulinzi walilala
chini, mlipuko mkubwa ulitokea ile stoo yote
ikateketea. Kamanda Amata alinyanyuka akiwa
na maumivu makali mkononi mwake, kipande
cha chuma kilimchoma na kumuumiza,
walimkokota Jegan umbali kidogo na kuifikia ile
chopa ambayo sasa ilikuwa imesimama kwenye
mikonge wakampakia na kumfuga pingu na
minyororo ya miguu, kisha wakaondoka zao.
5
DUNIANI kuna mvutano mkubwa sana juu ya
utwala na tawala zenyewe, huyu anasema hili
juu ya mwenzake na huyu anatamka vile dhidi
yake. Mvutano mkubwa unaonekana waziwazi
kati ya taifa la Marekani na washirika zake wa
Ulaya dhidi ya mataifa machache ya Mashariki
ya kati, mataifa yanayosadikiwa kwa mbinu
chafu za kigaidi za kuteketeza mamia ya
wanadamu katika sehemu mbalimbali za
ulimwengu kwa njia tofauti wanazozijua wao.
Mataifa yanayojiita makubwa duniani yana ndoto
za kufutilia mbali enzi na ujeuri wa mataifa haya
machache ambayo yamejidhatiti na hayatetereki
na vitisho kama hivyo, ambayo leo kesho yako
tayari kuingia vitani dhidi ya mabeberu hawa wa
maghalibi.
Kitendo cha Marekani na washirika wake
kuivamia ardhi ya Mashariki ya kati kwa minajiri
ya kukomesha tawala za kidekteta zinazonyima
watu haki zao kiliwachukiza watawala wa
mataifa haya na ndipo walipoanza kujitutumua
na kuendesha vita yao dhidi ya mataifa
makubwa popote yalipo duniani, yalizalisha
magaidi wakubwa, watu hatari ambao kwa
namna moja au nyingine walijifunza mbinu zote
za medani za kivita ndani ya mataifa yao na
kufundishwa na wao wenyewe kisha wakageuka
kuwa silaha mbaya zenye akili ya ajabu na
kuitikisa dunia. Vichwa vinauma, mioyo
inadunda, akili hazitulii, vikao vya mara kwa
mara vinaitishwa vya kuangalia jinsi ya
kukomesha hali hii, na muda huohuo vikao
vingine vinaitishwa kuona jinsi gani ya
kutengeneza shambulio lingine, la namna gani na
wapi wakalitekeleze. Ni akili mbili
zisizochangamana zilikuwa zikizungukana pande
mbalimbali za sayari hii na kuwafanya watu
kuishi pa si na amani. Wkati wao wanaanzisha
kambi za jeshi kila kona ya dunia ndani ya ardhi
za nchi za wengine hasa wanyonge kama Afrika,
na wenzao waliimarisha makundi yao kila kona
hasa Afrika.
≈≈≈
Kikao kizito kilikuwa kikiendelea katika ofisi moja
nyeti ya serikali, hoja ilikuwa ni ileile ya
kuachiwa kwa Jegan Grashan au la, mara hii
muda ulikuwa umekwisha sana hivyo kufanya
kikao hicho kuwa na mvutano mwingine wa
kipekee. Zilikuwa zimebaki siku tatu tu ili zile
siku saba walizopewa kumuachia huru mtu huyo
zitimie na endapo hatoachiwa basi shambulizi
kubwa na lisilotegemewa lilikuwa limepangwa.
Vikosi vya usalama havikulala, usiku kucha
vilijipanga hapa na pale kuhakikisha wanansa
kila aina ya milipuko inayosadikiwa kubebwa au
kuwekwa mahali Fulani. Mitambo ya kisasa
ilifungwa katika sehemu mbalimbali za
mikusanyiko ya watu kama kwenye supermarket,
vituo vya mabasi kama Ubungo, uwanja wa
ndege na sehemu nyinginezo nyingi, askari
kanzu walizagaa kila eneo kuhakikisha
wananusa kila aina ya mazungumzo, usiku ndo
usiseme, ilikuwa tabu sana kwa wale wapenda
giza, vibaka, machangudoa, walevi, wazururaji na
wote wanaofanana na hao. Idara ya uhamiaji
nayo ilikuwa makini kuchunguza kila anayeingia
nchini iwe kwa ndege, meli, gari au hata pikipiki
kama sio baisikeli, vibali vya kusafiria
vilipekuliwa kwa umakini wa hali ya juu kwa
mitambo ya kisasa iliyoweza kugundua alama
fichwa mbalimbali katika vijitabu hivyo, wapo
waliokamatwa na hati feki lakini walipoonekana
hawana dalili ya wale wanaowatafuta basi
waliwaacha na adhabu kubwa kwao ilikuwa ni
kuwarudisha kwao tu. Computer maalum
iliyounganishwa na zile za usalama za mataifa
ya maghalibi zilifanya kazi kubwa maana
ziliweza kutambua mtu mpaka kijiji ulichozaliwa
hata kama wewe ulikisahau kwa kuwa zilikuwa
zimelishwa kumbukumbu nyingi.
Muafaka ulikuwa mgumu sana katika kikao hicho
lakini ukweli ni kwamba wengi walionekana
kukubali bwana huyo kuachiwa ili kukomesha
mauaji yanayofanyika na kupoteza maisha ya
Watanzania wasio na hatia. Madam S bado
alikuwa na ushawishi mkubwa wa kuwafanya
wajumbe wa kikao hicho kubadili mawazo na
kuytomuachia huru Jegan, kila alipokumbuka
kauli na mifano ya kijana wake Amata au
Kamanda kama ilivyozoeleka kuitwa alijikuta ana
dei la kuzuia kuachiwa kwake, lakini wengine
wote walitaka aachiwe. Waziri mwenye dhamana
alijaribu kuwasihi jambo hilo lifanyike haraka
maana ni masaa sabini na mawili yalikuwa
yakijihesabu ili lile wasilolijua lifanyike. Walibaki
kizani, kiza kinene kwa kuwa walipigana na adui
wasiyemjua wala kumuona, ilikuwa ni kama
kupiga ngumi gizani.
Kikao kilifikia tamati, uamuzi wa kusubiri masaa
ishirini na nne ulipitishwa na kila mjumbe alirudi
katika majukumu yake wakati waziri mwenye
dhamana alikwenda kuonana na mkuu wa nchi
kujadili swala ilohilo.
≈≈≈
Upande wa pili nako kikao kiliendelea.
“Hawataki kumuachia mpiganaji wetu,” yalikuwa
maneno manne ya Shailan, aliyaongea huku
akiwa akishikashika zile ndevu zake nyingi.
“Kama hawatii tunachotaka basi tufanye yetu,
hapa tuna masaa yasiyopungua sabini tu so
hatuna budi kuanza kazi, nimeongea na Beishal,
tayari amesema kuna watu wako njiani kuingia
hapa wao watakuja kumaliza kazi kwa jinsi
ambayo watabaki na hofu kuu maana
hataitegemea kutokea.” Shakrum alizungumza
kwa kujiamini sana huku taratibu akiwa
anakunywa ile kahawa yake chungu kabisa
ambayo upendwa kunywewa na watu wa Pwani.
“Wasipotekeleza itakuwa ni kaburi lao sasa,
kama wanakumbuka septemba 11 pale New York
sasa wataona kwa macho yao kitachotokea
hapa mbele ya macho yao,” Shailan aliijibu hoja
ya Shakrum. Wakiwa katika kikao chao cha watu
wachache mara simu ya mezani iliita na Shailan
akampa ishara Shakrum aipokee naye akafanya
hivyo. Baada ya dakika kadhaa alirudi kitini na
kutazamana na Shailan, muda wote huo Scolleti
alikuwa kimya bila hoja.
“Vipi?”Shailan aliuliza
“Mzigo tayari, Beishal kasema tusubiri, kutoka
upande tusioujua jamaa watatokea na watakua
hapa ndani ya masaa ishirini na nne,” Shakrum
aakajibu.
“Ok! Tuwasubiri tufanye kazi”
Kimya cha ghafla kikapita kwa sekunde kadhaa,
kisha wote wakacheka pamoja.
“Shailan, kumbuka tuna yule Malaya wa jana,
lazima ashughulikiwe,” Shakrum alikumbusha
“Ooh gud, nenda ukamfanyie kama yule
mwingine kisha nipe ripoti, na hakikisha
Mwadawa anapatikana kuna mabo anayajua yule
binti asije akayatapika,” Shailan akasisitiza.
Shakrum akainuka kitini na kuvuta droo iliyokuwa
kwenye kikabati kidogo na kuchukua bastola na
kisu chenye urefu wa futi moja. Kisha akaondoka
zake na kumuacha Shailan na Scolleti.
≈≈≈
MALAWI
Uwanja wa ndege wa Karonga
KARONGA, mji mdogo ulio katika mkoa wa
kaskazini katika nchi ya Malawi, maghalibi mwa
ziwa Malawi au ziwa Nyasa kama linavyoitwa
hapa kwetu.Ndege ndogo aina ya Sessna ilitua
subuhi na mapema katika uwanja huo,
ilipokwishaegeshwa mahali pake, mlango
ukafunguliwa, watu wawili wanaume waliteremka
na kuelekea eneo la mapokezi ambako watu wa
uhamiaji walikuwa pale tayari kuwapa msaada
wanaouhitaji. Haikuwa na shaka wala haikuwa
na tabu, ndani ya dakika ishirini walikuwa nje ya
uwanja huo tayari kuelekea kule wanakokutaka.
Tax, ilikuwa ni usafiri pekee uliowapeleka moja
kwa moja mpaka katika moja ya hotel za
kawaida na kujipatia chakula huku wakipanga
mikakati yao jinsi ya kuingia Tanzania,
walishatahadaharishwa kuwa huko waendako
kuna ulinzi wa hali ya juu hivyo watumie mbinu
zote wawezazo kufanikisha adhma hiyo.
Ndani ya lisaa limoja walikuwa kwenye Pwani ya
Ziwa Malawi, pale walikuta shughuli nyingi za
wavuvi zikiendelea, wakatazama huku na kule,
wakaona boti moja iliyofungwa injini, wakaona
ndiyo iwafaayo, wakaiendea na kumkuta kijana
mmoja aliyekuwa akisuka nyavu zake tayari
kujiandaa kwenda kuvua. Wakamwita na
kuzungumza nae kuwa wanaomba awafikishe
katika kijiji kingine mbele katika mwambao huo,
alipotaka kuleta ubishi wakampatia pesa za
kimarekani, akakubali, lakini akaomba wakubali
aene na mwenzake, hawakupinga.
Watu wanne walikuwa botini na safari ikaanza,
boti ile ya mti ilikuwa ikikata maji kwa mwendo
wa kasi kwani injini yake iliruhusu hilo.
Walipofika mbali na pale walipotoka ndipo
walipofanya lile walilopanga, waliwaua wale
vijana na miili yao wakaitupa majini kisha wao
wakamiliki ile boti, na kwa kuongozwa na dira
waliyokuwa nayo, waliongoza chombo hicho
kuelekea kaskazini maana kiliwapa uelekeo
sahihi. Masaa manne hayakuwa haba wao
kufika katika mapori Ludewa ambako
walikitelekeza chombo hicho na wao kupotelea
katika misitu hiyo mpaka Ludewa mjini, sasa
wakagawana kila mtu kutumia usafiri wake na
miadi ilikuwa ni kukutana Dar es salaam, mahala
walipoelekezwa, kwa muda waliopanga.
≈≈≈
Shakrum aliingia katika stoo kubwa
waliyomfungia yule binti wa kihindi, akapigwa na
butwaa kukuta mlango mdogo wa chumba cha
siri walimomficha yule binti uko wazi, akasita,
akasimama na kaungali kwa makini, kisha
akanyata hadi kwenye ule mlango na kuangalia
ndani yake, hakuna mtu, kamba waliyotumia
kumfunga yule binti walizikuta pale chini, si
kwamba zimekatwa bali zimefunguliwa na
aliyefungwa ametoroka kwa amani. Shakrum
hakuamini kilichotokea, akatazama huku na kule,
juu na chini hakugundua kitu, ‘Ametokea wapi
mwanaharamu huyu?’ alijiuliza lakini hakuna jibu
alilopata, akiwa kashika kisu chake kwa mkono
wa kulia na ule wa kushoto akiwa kama
anajaribu kujua makali ya kisu kile kwa
kugusagusa kwa vidole vyake, kijasho
chembamba kilimtiririka na kurusu mvujo
uliokuwa ukilowesha fulana yake aliyovaa,
alipogutuka, alitoka nje haraka na kuwaendea
walinzi kuwaliza kama wamemuona mtu yeyote
kupita eneo hilo, lakini walidai hawakuona,
Shakrum alisikitika sana lakini pia alijilaumu kwa
kuwa hakuwaambia walinzi tangu kabla kama
kuna mtu aliyefungiwa ndani ya jengo hilo.
Hakuwa na la kufanya aliinua simu yake na
kupiga kwa Shailan ambaye alishtushwa na
habari hiyo pia. Wote walibaki midomo wazi
hakuna aliyeamini kama binti yule angeweza
kutoroka katikla mazingira kama yale, lakini
ndiyo ilikuwa tayari imetokea.
≈≈≈
ShaSha, alijificha nyuma ya kibanda kidogo
ambacho hakikuwa mbali na geti la mlinzi, jirani
kabisa na tenki kubwa la mafuta lililowekwa
hapo, aliweza kuwaona Shakrum na wale walinzi
walipokuwa wakiongea pale karibu na geti,
alipoondoka na kuwaacha pale, ShsSha alinyata
huku akiambaa na ukuta mpaka nyuma ya
kibanda cha mlinzi na kutulia hapo,
akawaangalia walivyokaa kizembe wakicheza
draft hali silaha zao wameziweka chini,
akakizunguka kile kibanda upande wa geti na
kuona limefungwa akatazama huku na kule
hakuna mtu akajitokeza, na kwa kasi ya ajabu
akaruka teke lilitoa kisogoni mwa mmoja wao na
kumsukuma mbele ambako aligongana kichwa
na yule mwingine na wote kuanguka, kabla
hawajakaa sawa, aliruka na kutua pale walipo,
pigo moja la nguvu lilitua nyuma ya shingo ya
mmoja wao na kumpotezea fahamu kisha yule
mwingine alimpiga kwa kumkanyaga na
kumrudisha chini sakafuni kwa kishindo, kwa
jinsi alivyopiga kisogo pale chini alipoteza
fahamu pia, ShaSha akawasachi na kutoa funguo
kisha akajifungulia geti na kutoka nje, akachukua
tax haraka na kumuamuru dereva amfikishe Ilala
Hotel.
Walipofika alimwambia amsubiri pale chini, kisha
akaja na kumpatia pesa yake. ShaSha akaona
wazi kuwa hapo sasa si mahala salama
akafunga mabegi yake na kuondoka, akabadili
hotel na kuhamia Kinondoni kwa Manyanya
kwenye hotel ya kawaida ya Manyanya Hotel na
kuweka kambi hapo.
ShaSha, kama anavyojiita, msichana wa kihindi
kwa umbo lake dogo lakini ni mtu mzima
aliyestahili kuitwa mwanamke, alikuwa nchini
kwa kazi moja tu aliyotumwa na serikali yake,
kuja kumchunguza Scolleti na mambo yake
maana katika nchi nyingi bwana huyu alimopita
serikali nyingi zimelalamikia uwepo wake kwa
kusaidia kutekeleza ama ujambazi au
kuhatarisha hatari ya nchi hiyo kwa namna moja
au nyingine. Mara hii serikali yake ya India
iliamua kuingia kazini kumchunguza kila aendako
ni nini anakifanya, sasa Tanzania, Scoletti
anawasaidia freedom fighters kutekeleza lile
taraja lao la kudai haki ya kufunguliwa ndugu
yao, wakitekeleza milipuko mikubwa na mibaya
na kuuwa mamia ya watu.
ShaSha alikuwa pale White Sands hotel katika
nyendo zake za kumfuatilia tajiri huyu,
alipokutana na Amata na kumkaribisha juice,
Amata alivutwa na uzuri wa sura ya binti huyu
na macho yake yasiyo na pazia hayakuweza
kuinyima raha roho yake iliyofungiwa ndani ya
kifua chake kwa kuutalii mwili mdogo, shupavu
wenye umbo la kuvutia. Angekosa kuwapo Gina
katika eneo lile basi tayari labda mapenzi
yangeamka, ama kweli, Inzi hufia kwenyew
kidonda.
HIZO NDIZO CHECHE ZA SHASHA.....
AKIKUTANA TENA NA AMATA KIKAZI ZAIDI
ITAKUWAJE?
 
CHAPISHO LA 11

KAMANDA AMATA alikunja nne kwenye kiti chake
cha kuzunguka, huku akimwangalia Gina
aliyekuwa bize na kuchapa kazi mbalimbali
alizopewa siku hiyo. Akiwa na mawazo mengi
hakuna kingine alichofanya kwa siku hiyo zadi
ya kushinda ofisini tu akitega skio huku na kule
kuona kama atasikia lolote kat i ya yale
anayoyahitaji, lakini mpaka muda huo haluna
kilichojiri kabisa.
Magazeti yote alikwishayapitia, hakuna jipya.
Redio zote alshasikiliza lakini habari zilkuwa
zilezile, hakuna kigeni. Alivuta kjitabu chake
kidogo cha kumbukumbu na kutazama kurasa
chache za kufanyia kazi, akajikohoza kdogo na
kuendelea kusoma kumbukumbu zake.
“Gina,” aliita, Gina akagutuka na kumwangalia
Amata.
“Niambie,” akatika kwa mtindo huo wa kipekee.
“Nataka nikutume sehemu wewe kama katibu
wangu muhtasi ukaniombee miadi ya kukutana
na manager wa eneo hilo,” Amata alimueleza.
“Bila shaka, ni wapi huko?” Gina akauliza.
“Unakumbuka Mwadawa alitueleza juu ya ile
kampuni ya Scolleti ya kusafirisha mafuta?”
“Ndyo,”
“Hapo sasa, uende, uombe miadi, nataka
kukutana na manager ili tuongee maswala ya
kibiashara,” akavuta mtoto wa meza na kutoa
kadi ya kibiashara na kumpa Gina, “Hilo ndilo
jina langu,” alongeza. Gina aliisoma kwa makini
ile kadi huku akigeuzageuza kwa jinsi livyokuwa
nzuri, yenye kuvutia kwa rangi rangi anuai, JOHN
SIZIMBA, ilisomeka hivyo kwa maandishi ya
rangi ya dhahabu.
“Kijana una majina mengi ! hivi unayakumbuka
yote?” Gna aliuliza huku akiiweka ile kadi katika
mkoba wake.
“Yote nayakumbuka,” akajibu. Baada ya kumaliza
kazi yake, Gina alinyanyuka na kumuaga Amata
kuwa anaenda huko alikomtuma, “Tunaenda
wote. Mi nakuacha uingie utanikuta nje.”
Baada ya kupambana na foleni za jiji la Dar hasa
ile barabara ya Bagamoyo, iliwachukua lisaa
limoja na nusu kufika Bunju, mbele kidogo ya
Baobab Sekondari na moja kwa moja kwenye
maegesho ya yadi kubwa lililoshehen malori
kadhaa ya mafuta. Amata alegesha gari nje na
kumtaka Gina kuwenda huku akiwa
amemuunganisha na kinasa sauti katika sidiria
yake. Gina alishuka na kuanza mwendo wake wa
mikogo kulielekea get kuu, akagonga na
kufunguliwa, akajitoma ndani.
Kamanda Amata akajiweka sawa, na kukiwasha
kiredio maalumu ambacho kingempatia
mawasiliano yote yanayotoka humo ndani.
“Karibu mrembo!” ilikuwa ni saut nene na nzto
kutoka kwa pande la mtu alyekuwa ameketi
nyuma ya meza kubwa iliyostahili kuwapo ndani
ya ofisi hiyo nadhfu ilipambwa na kunukia udi.
“Asante sana, nimekaribia,” Gina aliitikia, “Naitwa
Gina Zingazinga, kutoka kampuni ya SCOTT,”
alijtambulisha na kueleza kwa kifupi juu ya kazi
wafanyayo. Yule bwana alionekana akifuatilia kila
kitu kwa makin kabisa, Gina akamaliza
utambulisho wake na kueleza kile kilchomleta.
“Ok nimekuelewa, haina tatizo, tuna nafasi nzuri
sana ijumaa baada ya swala ya mchana, tena
utakutana na mkurugenzi mkuu atakuwepo,
natumaini atafurahia ujio wenu,” Yule bwana
alyejitambulisha kwa jina la Aidan,a alieleza kwa
kirefu.
“Asante sana,” Gina alishukuru na kuaga,
akasindkizwa na Aidan mpaka katika uwanja ule
ambao ni maegesho ya yale malori, wakaagana
na kutoka. Akiwa anatoka katika geti lle kubwa
alipishana na gari moja aina ya Prado nyeupe
iliyokuwa ikiingia ndani ya yadi ile, aliitazama
kwa jicho la wizi na kukumbuka vizuri gari ile.
“Aidan!” Amata allitaja hilo jina mara tu Gina
alipoketi kitin katka ile gari. Akageuza na
kuondoka eneo lile na kurudi mjini. “Tutakuja
ijumaa mchana,” Amata alirudia maneno yale yai
le miadi.
≈≈≈
“Karibuni sana Tanzania,” Shailan aliwakaribisha
vijana wawili walioonekana kuchoka sana kwa
safari. Vijana waliosafiri kutoka nchi ya mbali
kuja kuungana na wenzi wao katika kile
wanachokiita ‘kupigania uhuru’, hawakuja
kufanya starehe bali walikuja kufanya kazi, kazi
ya hatari ambayo kishindo chake kila mtu
atashtuka na dunia itazizima kwa hofu kuu,
walipania, walidhamiria, waliamua kufanya kile
kinachoitwa mauaji ya kimbari, lakini
wangeikumbusha vipi serikali kuwa wanamhitaji
ndugu yao, kaka yao, aliyeko gerezani? Yote
ilikuwa ni mipango inayosukwa chini kwa chini
na watu hao hatari katika uso wa dunia.
“Tumeshapata la kufanya, kabla ya lile
tulilodhamiria, lazima tuwape tashwishwi kwanza
kwa tukio dogo tu halafu watakapokuwa
wameshtuka sasa tunawapa onyo kisha
wasipojibu tunafunga kazi kabisa,” mmoja wa
wale vijana alieleza.
“Sasa tukiwashtua, huoni tutakuwa tumewapa
mwanya wa kuongeza ulinzi?” Shailan aliuliza.
“Hapana, lipi tumefikiria kufanya kama hitimisho
kwa ndugu yetu hata wafanye vipi hawawezi
kufikiria hilo, wataspigwa na mshangao tu,
limetokeaje, watabaki midomo wazi
wakishuhudia mamia ya wananchi wao
yakiteketea kikemikali, hapo hawatakuwa na
ujanja tena zaidi ya kutupatia kaka yetu na wao
kubaki wakiomboleza, na hili litatokana na
ugumu wa shingo zao,” aliongea kijana wa pili
kwa sauti ya upole.
“Ok, tumebaki na masaa 48 hivi, nina wasiwasi
mmoja hivi, kuna spy wao mmoja hatari sana,
huyu jamaa nashindwa kumuelewa ni intelijensi
kiasi gani, tusipomwangalia atakuwa kikwazo
katika mkakati wetu,” Shailan alieleza kwa
masikitiko, akadakiwa na Scolleti, “Yeah ni kweli
kabisa, anaitwa Kamanda Amata, mwanzoni wa
mission yetu amewaua vijana wetu na sasa
amekuwa ni kikwazo kikubwa sana.”
“Nipe picha yake kama mnayo,” yule kijana
aliomba. Shailan akachukua laptop yake ndogo
na kufungua picha Fulani, kisha akamuonesha
yule kijana.
“Sasa, huyu tuachieni sisi, kabla ya tukio hili
atakuwa tayari marehemu, na mipango yote
itaenda kama ilivyopangwa, tutahahakisha kabla
ya jua la jioni kesho mwili wake upo mikononi
mwetu,” walijigamba.
“Muwe waangalifu sana, Amata si mtu wa
kuchezea hata kidogo, one mistake one goal,
ameshakwamisha mambo mengi sana aisee,”
Scolleti alizungumza.
“Hamna shaka, Shakrum, endelea na ule mpango
wetu kama tulivyoongea, hakikisha ile kemikali
imesogea eneo la tukio hilo ndilo la maana, mimi
na huyu swahiba tunamfungia kazi Amata ndani
ya masaa kumi tu,” yule kijana aliongea kwa
majigambo. ‘Unamjua Amata au unamsikia?’
alijiuliza Shakrum moyoni mwake. Kikao
kikaendelea na mikakati mibaya ikapangwa dhidi
ya Watanzania wasio na hatia, hali tete.
≈≈≈
Mlango wa chumba cha Mwadawa uligongwa na
watu wawili wakajikaribisha wenyewe mpaka
ndani. Mwadawa alikuwa amejilaza kitandani
akiangali habari kupitia runinga yake ya kisasa
iliyofungwa sambamba na ukuta, alikurupuka
kuwaona watu hao wawili waliojikaribisha baada
ya kugonga mara moja tu, akaketi kitandani na
kuwatazama, “Ninyi ni akina nani? Mbona
mnaingia kwa mtu kibabe hivyo?” akawauliza.
“Usijali utatujua tu, umejaribu kutukimbia lakini
sasa tumekupata, sasa, sisi na wewe tuondoke
mguu kwa mguu jioni hii,” mmoja wao alisisitiza
“Mnipeleke wapi?” Mwadawa aliuliza kwa woga.
“We utajua ukifika, fanya tunalotaka kabla
hatujatumia nguvu,” walimuamuru. Mwadawa
aliwatazama kwa zamu watu wale ambao
hawakuwa hata na chembe ya tabasamu, mmoja
wao alipoona msichana Yule anataka kuleta
ubishi, akachomoa bastola na kumuoneshea,
“Sasa unaondoka na sisi au tukubakishe ukae
hapa ndani mpaka watu wasikie harufu ya uozo
wako?” aliuliza mwingine huku akiifunga
kiwambo cha sauti ile bastola. Mwadawa alijawa
na woga, alitetemeka mwili mzima.
“Tunayasitisha maisha yako kwa kuwa
umejifanya kimbelembele na kumpatia siri
usiyoijua Kamanda Amata, sasa hizi ni salamu
kutoka kwa bosi wako Scolleti,” Yule mwenye
bastola akailengesha kwenye paji la uso wa
Mwadawa na kuifyatua mara kadhaa, Mwadawa
alijibwaga kitandani akiwa chapachapa kwa
damu, kisha wale vijana wakaondoka zao na
kuufunga mlango kwa mtindo wa kuurudishia.
Kamanda Amata aliitazama simu yake mara kwa
mara hakuona ujumbe wowote kutoka kwa
Mwadawa ambaye walikuwa wakichati muda si
mrefu, alishangazwa na ukimya huo, akabofya ile
namba na kupiga lakini wapi, haikupokelewa
kabisa, akaishusha taratibu na kuitazama tena,
akafungua meseji ya mwisho ; ‘Magomeni
Makuti, nyumba namba 434B, ukifika nishtue,’
ilikuwa ni moja kati ya meseji za miadi iliyokuwa
ikipangwa kati ya wawili hao yaani Mwadawa na
Kamanda Amata. Mwili wa Amata ulikuwa
ukisisimka mara kwa mara, akhisi kuna jambo la
hatari lakini hakuwa na uhakika ni jambo gani,
alijinyanyua na kuifuata gari yake huku akiwa
hajui ni wapi anakoelekea.
Ilikuwa yapata saa mbili na nusu usiku
alipoegesha gari yake mbele ya nyumba namba
434B, Magomeni Makuti, akashuka na kuzipanda
ngazi chache zilizo kwenye kibaraza cha nyumba
hiyo, alipoukaribia mlango mkubwa alikuta na
mbibi mmoja akiwa anatoka ndani, akamsabahi
na kumuuliza chumba cha Mwadawa, Yule bibi
akamtazama Kamanda na kumtupia swali, “Na
we nani tena? He huyu binti ana hatari huyu, hivi
magonjwa yote haya haogopi?” Amata akacheka
na kurudisha swali, “Bibi, kwa nini unasema
hivyo, mimi ni bnamu yake bwana.”
“Aaaaa binamu ndiyo hana maana kabisa,
binamu nyama ya hamu wenyewe mwasema,
haya bwana anaishi mlango huo wa tatu kulia,
uwe mwangalifu kijana kuna madume mawili
yameingia muda si mrefu,” Yule bibi alijibu huku
akitoka nje na kumuacha Kamanda akiwa
anaelekea ndani ya nyumba ile. Korido ndefu
ilimkaribisha, akaipita na alipoukaribia ule
mlango alihisi mwili ukisisimka na nywele
kumsimama, akasita kidogo, akautazama na
kugonga, haukufunguliwa, akainua simu yak e na
kupiga, akaisikia ikiita ndani ya chumba hicho,
akagonga tena na tena lakini hakupataa jibu,
kengele za hatari zikamgonga kichwani,
akatazama kupitia tundu la ufunguo, la haula,
hakuamini akionacho, mwili wa Mwadawa
ulijilaza kitandani, akagonga tena mlango lakini
haukufunguliwa, wala Yule Mwadawa
hakutikisika, akaufungua nao ukafunguka bila
ubishi, hakuamini akionacho, sura wa Mwadawa
aliyokuwa ikimwangalia ililowa damu na kisogoni
mwake ndio kabisa, damu ilitapakaa na kuchafua
shuka yote, Kamanda Amata alishikwa na ganzi,
hakuamini kilichotokea na anachokiona, akavuta
hatua zaidi na kuutazama mwili ule, alitikisa
kichwa kuonesha masikitiko, hasira ikamtawala,
alipotaka kugeuka, akagundua kitu, katika
kiganja cha mkono wa Mwadawa, kipande cha
karatasi, akakichomoa taratibu kana kwamba
hataki kumuamsha huyo aliyelala, akakifungua
na kukisoma kiliandikwa JULAI 7, hakuelewa
maana ya ujumbe huo lakini pia hakuupuzia,
akakiweka mfukoni na kutoka nje, akamuona
tena Yule bibi.
“Mbona watoka kwa masikitiko, vipi, amekusaliti
huyo, unaona!” Yule bibi aliendelea na swaga
zake, Amata alipitiliza katika gari yake na
kuondoka kwa kasi mpaka Yule bibi akabaki
kushangaa. Alipotulia akapiga simu ya dharula
kituo cha polisi na kuongea askari wa zamu pale
Mgomeni, akawapa taarifa ya kutokea mauaji
hayo na kuwaelekeza nyumba. Haukupita muda
polisi wale walifika na gari yao mpaka katika ile
nyumba, wakateremka na kuangalia hali halisi ya
tukio lile, vipimo vya kitaalamu kama alama za
vidole zilichukuliwa katika maeneo mbalimbali na
walipomaliza, waliubeba mwili wa marehemu,
huku nyuma wakiacha askari wakiendelea na
mahojiano na wapangaji wengine. Kamanda
Amata aliifuatili gari ya polisi kwa nyuma mpaka
ilipofika Muhimbili na kuhifadhi mwili ule,
walipoondoka, yeye akaingia na kukutana na Dr
Jasmine ambaye alikuwa zamu siku hiyo, yeye
kama daktari pia alibobea katika maswala ya
uchunguzi wa maiti.
Kamanda Amata aliutazama mwili wa msichana
Mwadawa uliokuwa umelala katika kitanda cha
mochwari pale Muhimbili, pembeni yake akiwepo
Dr Jasmin, aliutazama tena na tena hakuamini
kilichotokea lakini ukweli ulibaki kuwa uleule tu,
Mwadawa ameuawa.
“Vipi Kamanda?” Dr Jasmin aliuliza
“Ah! Nilikuwa sijamaliza kazi na huyu msichana,
alinisaidia katika sakata hili lakini najua
wameshajua hilo ndo maana wamemmaliza,”
Kamanda alimjibu Jasmin huku akijifuta kamasi
jembamba lilioashiria uchungu wa ndani kwa
ndani, akaufunika mwili ule na kuongoza nje ya
chumba hicho kisichopendwa na watu akimuacha
Dr Jasmin aendelee na uchunguzi wake wa
kitabibu.
»»»
Gina aliegesha gari katika maegesho ya kampuni
ile ya uchukuzi na usambazaji mafuta,
wakateremka wote wawili akitangulia Kamata
Amata, JOHN SIZIMBA wa bandia.
Wakakaribishwa na walinzi na kuongozwa hadi
kwenye ofisi ya secretary, pale walimkuta
mwanadada mrembo, mweupe, mwenye asili ya
kiarabu aliyewakaribisha kwa heshima ya hali ya
juu, “ Karibuni, bila shaka ni ugeni kutoka
SCOTT,” Amata akatikisa kichwa kuashiria kuwa
yuko sahihi, wakaongozwa mpaka kwa meneja
mkuu, kutokana na Amata jinsi alivyojibadili
ilikuwa vigumu kumgundua. Ndani ya ofisi ile ya
meneja walikutana na mtu mnene mwenye tumbo
kubwa aliyejaa vema katika kiti chake cha
magurudumu kinachokuruhusu kuweza
kuzunguka ufanyapo kazi ya hapa na pale. Mtu
huyo ambaye nae alikuwa na asili isiyojulikana,
mhindi si mhindi, mwarabu si mwarabu,
tukimwita chotara tunakosea, tukimwita
mwafrika tunajidhalilisha. Aliwapokea na
kuwakaribisha viti, kisha yule sekretari
akachukua kiti kingine na kuketi akiwa na
makabrasha machache mkononi mwake.
“Naitwa Mr John Sizimba, na huyu ni katibu
wangu, kutoka kampuni ya Scott,” Amata alitoa
utambulisho upande wake na baada ya hapo
ukafuatia utambulisho wa upande wa pili, ndipo
mazungumzo mengine yalipoendelea juu ya
mambo ya kibiashara, baada ya hapo yule
meneja aliwachukua Amata na Gina na
kuwapeleka kwenye chumba maalum ambacho
waliweza kuona uwekezaji huo jinsi ulivyojikita
nchini na nje ya nchi, marafiki zao wa kibiashara
sehemu mbalimbali za ulimwengu hasa katika
bara Hindi. Kamanda Amata hakuwa akisikiliza
kwa makini ila alikuwa akikichunguza chumba
kile kila kona jinsi kilivyoweka nakshi na ile
screen kubwa ambayo iliweza kuwaonesha
mambo mengi sana, wakiwa katika chumba
hicho, kijana mmoja aliingia ndani na
kumnong’oneza kitu yule meneja.
“Oooh Mr John, uniwie radhi, kuna dharula
imejitokea sina budi kuagana nanyi, lakini
karibuni wakati mwingine,” yule meneja aliagana
na Kamanda Amata na Gina. Akili ya Kamanda
Amata ikafanya kazi haraka sana, akagundua
kwa vyovyote watakuwa wamemgundua, nae
akaagana nae kisha yule sekretari akawaongoza
nje, walipofika kwenye uwanja wa yadi ile,
kulikuwa na wafanyakazi ambao kila mmoja
alionekana kuwa na shughuli yake, wakapita
mpaka geti kubwa pale wakakutana na kijana
mmoja mwenye asili kama ya yule meneja,
Amata akayasoma haraka macho ya yule mtu
ambayo yalimpa majibu ya jambo alilolifikiria,
hatari. Akatoka nje ya geti hilo na hapo pia
akakutana na kijana mwingine mithiri ya yule wa
kwanza, nywele za Amata zikasimama kuashiri
kuna jambo si jema. Gina alilielekea gari lakini
Kamanda Amata alimshika mkono na kumvutia
upande wa pili kisha wakakodi tax mojawapo
kati ya nyingi zilizopo nje ya eneo hilo na
kuondoka zao. Hakuna aliyeongea katika tax
hiyo mara kwa mara, Amata alikuwa akiangalia
nyuma kuhakikisha kama kuna anayewafuata
lakini hali ilikuwa shwari, hakukuwa na jipya.
NINI KILIENDELEA?
 
CHAPISHO LA 12

6
SHAILA Shavrij ‘ShaSha’ aliendelea kutulia
palepale njiapanda ya Ursino Road akisubiri kile
alichokuwa akikisubiri, akiwa ndani ya gari ya
kukodi kutoka kampuni Fulani ya jijini Dar,
hakushusha hata kioo kimoja bali kiyoyozi
kilifanya kazi yake ya kumrejeshea ubaridi, hali
iliyo hadimu katika jiji la Dar es salaam. Akiwa
gari yake kaitazamisha kule kwenye jingo la
Kanisa la Kristo, macho yake hayakutaka
kupoteza hata sekunde kuisubiri ile gari
aliyoifuatilia ambayo ilikuwa imeingia pale
kwenye ile barabara.
Ama kweli, subira huvuta heri, dakika cache tu,
ile gari ilitokea njia ileile na kuchukua barabara
ya Bagamoyo kuelekea Mwenge. ShaSha naye
akafanya hivyo hivyo, kati yake na lile gari
aliruhusu magari mawili tu kumpita. Taa za
barabarani zililipendezesha jiji hasa katika njia hii
ielekeayo Bagamoyo.
“Hakikisha hajui uwepo wako, maana
malalamiko ya watu yamekuwa mengi, kwani
Scoleeti ni nani au anafanya nini zaidi ya ufanya
biashara aliyonayo?” ShaSha aliikumbuka sauti
ya bosi wake siku alipokuwa akimpa majukumu
ya kumfuatili tajiri huyu muuza mafuta.
»»»
Scoletti Ramjo, mzaliwa wa Bombay, lakini
alipitisha maisha yake ya ujana huko Mumbai,
India, muumini wa dini ya Kiboora aliondokea
kuwa mfanya biashara maarufu sana
aliyewekeza katika nchi mbalimbali ndani na nje
ya Asia, daima alikuwa ni mtu wa kubadilisha
makazi kutoka haya kwenda yale, hakutulia
mahali pamoja. Kila nchi aliyokaa mfanya
biashara huyu, haikuchukua muda ama
alifukuzwa au alisababisha matatizo ya
kidiplomasia kati ya nchi hizo, alituhumiwa
kushirirkiana na vikundi vya kigaidi, kutekeleza
mipango michafu dhidi ya binadamu na
ubinadamu wenyewe, kuhifadhi wahamiaji
haramu ambao hata hawakujulikana kazi yao
katika nchi enyeji. Baada ya kufukuzwa huku na
huko, Bwana Scolleti aliingia Africa Mashariki
miaka kadhaa, akaishi Nairobi na baadae
kuhamia Dar es salaam ambako alianzisha
kampuni mbili kubwa, moja ya kusafirisha
mafuta kwenda nchi za SADC na nyingine ni ile
ya zimamoto iliyopo Dar es salaama na kueneza
matawi yake katika mikoa mikubwa mingine.
Kama kawaida ya Tanzania, taifa la amani, huwa
alimfuatilii mtu, linaamini kuwa kila mtu ni
mwema, kumbe wapo chui katika ngozi ya
kondoo.
Alipokutana na waziri wa Viwanda na Biashara
katika moja ya mikutano ya kimataifa ya
kibiashara uliofanyika huko Tokyo, Japan, ndipo
alipopitisha ombi lake la kuja kuwekeza katika
nchi hii tulivu, wakati huo akiwa ametimuliwa
kutoka Thailand baada ya kugundulika kuwa
alikuwa akfadhili kikundi cha Tamir Tiger kwa
kuwapa silaha kupigana na serikali huku yeye
akifanya biashara zake haramu. Akakubaliwa,
mipango ikawekwa mezani, mimi na wewe
hatujui, labda kuna kiasi kilitolewa kama takrima
kwa mabwanyenye, akaingia nchini, haikuchukua
muda akaanzisha kampuni yake ya zimamoto na
uokoaji yenye vifa vya kisasa kabisa, ilikuwa ni
mapinduzi kwani tangu hapo huduma hiyo
ilitolewa na kampuni ya jiji tu iliyobaki na gari
noja lilichoka kila idara. Baada ya hapo
akaanzisha ile ya uchukuzi na usafirishaji wa
mafuta, akiwa mbioni kuiomba serikali wampe
moja ya visiwa vya Mafia kunakosadikika kuna
mafuta ili achimbe. Scolleti pamoja na washirika
wake wakajikita katika mwamvuli huo na wakati
wa mlipuko wa ubalozi wa USA hapa Dar na
Nairobi, alishiriki kikamilifu katika kuwahifadhi na
kuwapa kila wanalohitaji wataalamu hao mpaka
wakafanikiwa.
“Tumechoka, kila nchi inatulaumu sisi juu ya
huyu mtu,” aliongea bwana Premji, afisa usalama
wa India, akimweleza ShaSha.
“Uende Tanzania, maana tumeshajua kuwa yuko
huko kwa muda sasa, hakikisha ukishajua
anachofanya, haina haja ya kuwa hai, utajua
utafanya nini, sisi tunataka ripoti tu.”
ShaSha, mwanausalama mtukutu anayejulikana
natika kazi, kwa kujiamini kwake na utendaji
bora. Alikabidhiwa kabrasha la Scolleti
ahakikishe anamtia mkononi kwa hali yoyote ile.
shaSha baada ya kukabidhiwa jukumu lile
alianza moja kwa moja kwanza kwa kutafuta ni
mahali gani katika dunia hi alipojificha, haikuwa
kazi ndogo, ilimbidi kusafiri sana kila nchi
apitayo, mwisho akajikuta ndani ya Tanzania,
akikabiliana na Scolleti, mtu ambaye hajawahi
kumuona live isipokuwa kwenye picha tu. Katika
chunguzi zake sasa anajikuta anagundua mambo
mbalimbali yafanywayo na Scolleti, sasa
akaanza kumfuatilia kila mahali akichukua picha
mpaka za maswahiba zake, mara ya kwanza
alimuona pale White sands Hotel alipokuwa na
kikao na swahiba zake wenye ule mpango halifu,
lakini Scoletti katika kujilinda ana macho mengi,
alishajua uwepo wa SaSha eneo lile hivyo vijana
wake wakaweza kumteka na kutoweka nao.
SaSha aliitazama saa yake ya kwenye gari,
ilimuonesha kuwa ni saa nne usiku na dakika
kadha wa kadha, aliiacha ile gari ikiingia kwenye
yadi kubwa pale Bunju na yeye akapiliza kama
mtu yoyote asiye na shughuli na eneo lile,
alipakumbuka sana kwa kuwa alishawahi
kutekwa na kuhifadhiwa ndani ya yadi hiyo. Kwa
mwendo wa taratibu akaegesha gari yake katika
moja kilabu kikubwa cha pombe za kizungu mita
kama mia nne kutoka ile yadi, akashuka na
kujichanganya na wanywaji wengine, kila mtu
alimuonea kijicho mtoto huyo wa Kihindi
aliyeingia eneo kama hilo, wakware mate
yaliwadondoka, wazinzi mioyo ilienda mbio na
suruali kupata shida. SaSha, msichana mfupi,
mwenye mwili wa wastani kadiri ya kilo 65 hivi,
aliyevali fulana nyeusi iliyopambwa na maandishi
‘Mtoto wa Bongo’ ilifunika vijititi vidogo kama
vya msichana ambaye hajavunja ungo, jeans
nyeusi yenye kigozi ‘Lee’ ilisitiri eneo la chini la
mwili wake likiyaficha makalio manene kidogo
yaliyoning’inia kwenye kiuno chembamba kabla
ya kubebwa na miguu iliyoonekana mikakamavu
ingawaje ilikuwa ndani ya suruali.
Hatua chache zilimfikisha katika kaunta ya bar
hiyo na akaagiza kinywaji aina ya Savanna, kwa
kuwa aliona jinsi alivyokuwa akitolewa macho na
midume ile, akawaagizia pombe kila mmoja.
Muda ulienda na masaa mawili yakakatika, binti
yule akapita njia ya kwenda chooni na kuruka
ukuta kutokea nje, upande wa pili wa bar hiyo,
akapenyapenya mpaka akatoke barabara kubwa
na kuiendea ile yadi. Mwanga mkali wa taa za
pikipiki ulimmulika usoni, akajificha macho huku
akiipa mgongo ilipompita alishangaa kuiona
ikisimama eneo Fulani si mbali sana na pale,
hakulifuatilia hilo, aliendelea na yake.
»»»
SHAILAN na watu wake walikuwa katika meza ya
duara ndani ya ukumbi mdogo wa mikutano
katika yadi ndogo ya Mabibo, walikuwa
wakihesabu masaa arobaini yaliyowabakia tangu
kuishinikiza serikali imuachie huru ndugu yao
mpigania uhuru, Jegan Grashan aliyefungwa na
serikali ya Tanzania katika gereza kuu la Ukonga
kwa miaka kadhaa.
“Unafikiri watamuachia?” mmoja wa wale vijana
wageni aliyejulikana kama Tajan aliuliza.
“Tajan, unakata tama au vipi?” Shakrum
alimtupia swali.
“Hapana kaka maana sioni jibu lolote kutoka
kwao,”
“Wasipomuachia sisi kuanzia kesho ni kama
tulivyoongea na tulivyopanga,”
“Na kuhusu Amata?” Tajana aliuliza tena,
“Maana tulitega bomu kwenye gari yake ila
jamaa yule ana machale sana, akapanda tax,
tukamkosa,” aliendelea.
Shailan akawakatisha, “Na hakikisheni Kamanda
Amata anadhibitiwa vyema, hivi tunavyoongea ni
kumzingira nyumbani kwake, haina haja
kumkamata bali kumpoteza kabisa,”
“Ila Shailan, usikumbuke kupambana na Amata
ukamsahau yule msichana wa Kihindi, hawa
wawili wakiungana , maana sijui kama bado au
tayari, tutakuwa na hali ngumu,” Shakrum
akadakia.
“Usijali, kesho nchi hii itatetema kwa hofu na
viongozi wao watapumua hewa ya mauti, dunia
itazizima maana yale ya Nigeria, Somalia na
Kenya ni cha motto, tutawaonesha patgazeti
kisha picha lenyewe linakuja,” Shailan alijitamba
huku akiipuliza kahawa yake ipoe kidogo,
akainywa na kuagana na maswahiba zake,
wakiwa tayari kila mmoja kachukua majukumu
yake usiku huo.
Tajan na kijana mwingine waliondoka na gari
yao kueleka Kinondoni kwa Kamanda Amata,
wakati Shakrum aliingia katika chumba kidogo
cha mawasiliano.
Giza lilikuwa limetawala, hakuna hata mbala
mwezi iliyong’aa usiku huo isipokuwa nyota za
mbinguni tu.
Tajan aliegesha gari yake karibu na geti la
nyumba ya Amata, akashuka pamoja na yule
mwingine, wakaizunguka nyumba kila mtu
upande wake, hakukuwa na njia nyingine zaidi ya
ukuta mrefu ambao kuukwea ulitakiwa ujasiri wa
hali ya juu, lakini hiyo haikuwa kazi kubwa kwa
Tajan, alirudi nyuma hatua kadhaa na kuupanda
kwa kasi kama ambavyo buibui apandavyo, na
dakika moja tu alikuwa ndani ya wigo huo.
Alitulia tuli, akisubiri kusikia kama kuna
mchakacho wowote, alipoona kimya alitembea
taratibu huku akiwa ameinama na bastola yake
mkono ikiwa tayri kufuata amri itakayopewa na
mshikaji, alilifikia dirisha kubwa la mbele,
akajinyanyua kidogo kurusu paji la uso wake
litangulie na macho yafuatie, hakukuonekana
dalili ya mtu ndani mle. Akauendea mlango,
akautazama kwa jicho lake kali, akachomoa
funguo yenye uwezo wa kufungua loki kadhaa za
ulimwengu huu, alipoitumbukiza tu, mlango
ukajibu, akausukuma taratibu na kujitoma ndani.
Hakuruhusu kelele yoyote isikike, akalivuta vazi
lake na kufunika uso wote akabaki macho tu,
mikono yake iliyovikwa gloves iliikamata bastola
kwa ustadi, kwa mwendo wa kunyata, mwendo
wa kininja, aliipita sebure na kukuta milango
kadhaa, kati ya milango ile, mmoja ulikuwa
unawaka taa hafifu na sauti ya muziki laini
ilisikika kwa mbali. Tajan akajua sasa windo
lake kalipata, akataka kuufungua mlango wa
chumba kile, akasita, akabadili mawazo,
akaiendea switch kuu ya umeme na kuiweka off,
nyumba nzima ikawa giza, akatulia dakika kama
mbili ili aone kama kuna mchakacho wowote
baada ya giza hilo, hakuna. Akavuta hatua
mpaka kwenye ule mlango, akanyonga kitasa,
kikanyongeka, mlango ukajiachia kuruhusu nafasi
ya mtu kupita, Tajan akaingia ndani na kutulia
karibu na kabati paliponing’inizwa makoti na
suruali kadhaa, alimuona mtu aliyelala kitandani
na kujifunika mwili wote isipokuwa kichwa tu,
alitulia palepale na kutoa kikopo kidogo chenye
dawa kali ya usingizi, akanyunyiza, hewa ile
ikajaa chumba kizima. Alipohakikisha zoezi hilo
tayari, akakiedea kitanda na kumsukasuka
aliyelala hapo, hakuwa Amata, bali Gina alikuwa
kajipumzisha, hakuona haja ya kumuua, ‘huyu
nikimchukua, Amata atakuja mwenyewe’
≈≈≈
Utulivu wa ndani ya jengo hilo usiku ule
ulimfanya ShaSha afanye upekuzi wake taratibu
sana, akichunguza kila droo na kila karatasi aone
kama atapata vile avitakavyo, alivuta hili
akavuta lile, alifunua hiki akafunua kile, lakini
alihakikisha anarudisha katika mtindo ambao
wewe au mimi si rahisi kugundua kuwa hapa
pamepekuliwa. Taratibu akatoka ndani ya ofisi
hiyo ambayo aliona wazi kuwa haina tija kwake,
akavuta hatua chache za kunyata katika kigiza
cha koridoni na kuufikia mlango mwingine,
akautazama kwa makini hata jinsi ambavyo
alikuwa anautazama ni kiintelijensia zaidi,
akashika kitasa chake na kukinyonga,
akashangaa kikiachia na mlango ule kufunguka
taratibu. ShaSha akatulia kwanza, akavuta
pumzi, akajua huu kwa vyovyote ni mtego,
akavuta hatua fupi fupi za tahadhari huku
akaingalia pande zote kwa makini mkubwa,
akauachia mlango na kukamata bastola yake
mkononi, kwa harakaharaka alikikagua chumba
kile na kugundua kuwa pia ilikuwa ofisi nyingine
kubwa ya kifahari, alihisi kuwa ile itakuwa ndiyo
hasa anayoitafuta, alitulia kidogo, ukimya wa
ndani ya ofisi hiyo ulimpa faraja ya kujua kuwa
hakuna tatizo lolote kama sio shida, akairejesha
bastola yake mahala pake nay eye kuiendea
meza kubwa iliyopo hapo ambayo juu yake
ilibeba kibao chenye maandishi mazuri ya
kupendeza yaliyochorwa kwa nakshi safi ya
rangi ya dhahabu ‘Managing Director’ na chini
ya hiyo ‘Mr Scolleti’, maandishi haya yalimvutia
sana ShaSha. Moja kwa moja alianza na motto
wa meza akavuta taratibu na kuangali
makabrasha kadhaa yaliyopo hapo,
akayachambua kwa harakaharaka, alipoona
hayana tija akaamia upande mwingine na
kufanya vilevile, lakini hapa alipata kitu tofauti,
kabrasha moja inaonekana lilimfurahisha zaidi,
aklichambua harakaharaka na katika baadhi ya
kurasa zake alitumia kamera yake ndogo lakini
yenye nguvu sana kupiga picha baadhi ya kurasa
hasa mle anamomuhitaji. Alipojiridhisha
akarudisha kama vilivyo, na kuweka kamera yake
mahali husika kisha akatoka taratibu katika
chumba hicho na kuurudishia mlango kama
ulivyokuwa.
≈≈≈
Kamanda Amata alijua moja kwa moja
anchokwenda kukifanya katika jengo hilo
lililojengwa ndani ya yadi kiubwa ambayo mchan
wake tu alikuwa hapo. Kwa kupitia nyuma ya
ukuta wa yadi ile Amata aliweza kuruka na
kuingia ndani kwa utulivu, akajibanza kando
kidogo ya tenki bovu la mafuta lililotelekezwa
hapo, akatulia akiangalia ustaarabu, alipotaka
kutoka eneo lile alisikia mchakacho wa hatua
zikija upande wake, akazisikiliza kwa makini ili
agundue kama ni za mnyama au binadamu,
lakini aligundua kuwa ni za miguu miwili, za
binadamu, akatulia palepale bila kujitikisa, mara
mtu aliyemkuwa akivuta hatua hizo akafika eneo
lile, akasimama karibu kabisa na alipo Kamanda
Amata lakini hakugundua kama kuna mtu. Yule
mlinzi alitazama huku na huku, kimya, akaamua
kuondoka, kabla hajavuta hatua ya pili, Kamanda
Amata kama umeme aliibuka na kumpiga karate
moja ya shingo iliyomfanya alegee na kuanguka,
fahamu zikimtoka, Amata akamdaka na
kumuweka chini taratibu asilete kokolo wala
kelele. Akamruka na kuelekea upande wa pili,
akajificha karibu kabisa na choo, akitazama
walinzi jinsi walivyojipanga katika eneo lile.
Ilikuwa ngumu kwake kuvuka kuelekea jengo lile
lenye ofisi kwa sbabu kati yake na lile jengo
palikuwa na uwazi mkubwa sana na taa
zilizomulika kwa mwanga mkali, hivyo alitulia
akipiga mahesabu jinsi ya kuvuka eneo hilo bila
kuonekana na walinzi aliyoweza kuwahesabu na
idadi yao kufikia kama sita hivi, wazo la haraka
likamjia, akamkumbuka yule aliyemzima kwa
karate kule nyuma, akageuza kurudi ili afanye lile
alilolikusudia
Tajan akajua sasa windo lake kalipata, akataka
kuufungua mlango wa chumba kile, akasita,
akabadili mawazo, akaiendea switch kuu ya
umeme na kuiweka off, nyumba nzima ikawa
giza, akatulia dakika kama mbili ili aone kama
kuna mchakacho wowote baada ya giza hilo,
hakuna. Akavuta hatua mpaka kwenye ule
mlango, akanyonga kitasa, kikanyongeka, mlango
ukajiachia kuruhusu nafasi ya mtu kupita, Tajan
akaingia ndani na kutulia karibu na kabati
paliponing’inizwa makoti na suruali kadhaa,
alimuona mtu aliyelala kitandani na kujifunika
mwili wote isipokuwa kichwa tu, alitulia palepale
na kutoa kikopo kidogo chenye dawa kali ya
usingizi, akanyunyiza, hewa ile ikajaa chumba
kizima. Alipohakikisha zoezi hilo tayari,
akakiedea kitanda na kumsukasuka aliyelala
hapo, hakuwa Amata, bali Gina alikuwa
kajipumzisha, hakuona haja ya kumuua, ‘huyu
nikimchukua, Amata atakuja mwenyewe’
GINA AMETEKWA....
USIKOSE SEHEMU YA 13 YA JULAI 7... UJUE
HATIMA YA KISA HIKI
 
CHAPISHO LA 13
≈≈≈
Kamanda Amata alijua moja kwa moja
anchokwenda kukifanya katika jengo hilo
lililojengwa ndani ya yadi kiubwa ambayo mchan
wake tu alikuwa hapo. Kwa kupitia nyuma ya
ukuta wa yadi ile Amata aliweza kuruka na
kuingia ndani kwa utulivu, akajibanza kando
kidogo ya tenki bovu la mafuta lililotelekezwa
hapo, akatulia akiangalia ustaarabu, alipotaka
kutoka eneo lile alisikia mchakacho wa hatua
zikija upande wake, akazisikiliza kwa makini ili
agundue kama ni za mnyama au binadamu,
lakini aligundua kuwa ni za miguu miwili, za
binadamu, akatulia palepale bila kujitikisa, mara
mtu aliyemkuwa akivuta hatua hizo akafika eneo
lile, akasimama karibu kabisa na alipo Kamanda
Amata lakini hakugundua kama kuna mtu. Yule
mlinzi alitazama huku na huku, kimya, akaamua
kuondoka, kabla hajavuta hatua ya pili, Kamanda
Amata kama umeme aliibuka na kumpiga karate
moja ya shingo iliyomfanya alegee na kuanguka,
fahamu zikimtoka, Amata akamdaka na
kumuweka chini taratibu asilete kokolo wala
kelele. Akamruka na kuelekea upande wa pili,
akajificha karibu kabisa na choo, akitazama
walinzi jinsi walivyojipanga katika eneo lile.
Ilikuwa ngumu kwake kuvuka kuelekea jengo lile
lenye ofisi kwa sababu kati yake na lile jengo
palikuwa na uwazi mkubwa sana na taa za
helogene zilimulika kwa mwanga mkali, hivyo
alitulia akipiga mahesabu jinsi ya kuvuka eneo
hilo bila kuonekana na walinzi aliyoweza
kuwahesabu na idadi yao kufikia kama sita hivi,
wazo la haraka likamjia, akamkumbuka yule
aliyemzimishaa kwa karate kule nyuma,
akageuza kurudi ili afanye lile alilolikusudia.
Aliusukasuka ule mwili uliolala, akaona hakuna
dalili ya mtu huyo kuamka muda huo, akatazama
nguo zake, na kuona suruali inashahabiana na ile
aliyovaa, akamvua koti na kulivaa kisha
akachukua ile bunduki yake kubwa, gobole,
akalipachika mgongoni, taratibu akatoka kwa
kupitia upande ule alikotokea yule mlinzi,
alipofika kwenye kona akasimama, kidogo, kama
aliyekumbuka kitu, kweli alisahau kitu kimoja,
sigara, yule mlinzi alikuwa anavuta sigara,
akaenda na kuinyofoa kinywani mwake kisha
akaipachika kati ya vidole vyake viwili cha kati
na cha shahada, mkono mwingine ukiwa na
tochi, akajitokeza.
Mwendo wa kama mita mia akapishana na kundi
la walinzi watatu, akajikausha na kujifanya
mmoja wao, akapita katikati yao bila
kuwaogopa.
Baada ya kuyapita malori kadhaa, alilifikia jingo
ambalo alilidhamiria, akauendea mlango mdogo
ulio upannde wa nyuma nakufanya vitu vyake,
sekunde chache alikuwa ndani ya jingo hilo,
akatulia kutazama usalama kwa maana alijua
wazi kuwa mle ndani kuna camera za usalama
kwa kuwa aliziona mchana ule. Ndani ya
kijichumba alimokuwamo hakukuwa na kitu
kingine zaidi ya mandoo ya takataka, akasonya
kwa hasira ya kuwa amekosea mlango,
akageuka kutoka lakini akasita, aliporudisha
macho ukutani kwa juu kidogo akakuta kuna
kamera ndogo mfano wa taa iliyopachikwa
kiufundi sana, akatikisa kichwa kuashiria kuwa
chumba hicho si bure, kuna jambo, chumba cha
takataka kiwekwe camera. Akatuliza akili na
kuendea kwa upande wa pili ile camera ili
isiweze kupata picha yake alipoifikia alifyatua
kiwaya kidogo kilichokuwa kikipeleka
mawasiliano kwenye chumba kingine.
Akautazama ule ukuta kwa makini ulikuwa
umepigwa chuping, akayasukuma sukuma
magudulia ya uchafu, akagundua kuwa kumbe
kilikuwa choo, choo cha kutumia maji, lakini
hakuona kijitenki cha maji isipokuwa bomba
dogo pembeni, haina mana. Kamanda Amata
hakuelewa hata kwa nini chumba hicho ambacho
kilikuwa choo, mara cha takataka kiliwekwa
camera, akaachana nacho akaamua kutoka,
alipotikisa mlango umefungwa, lo! Yeye
hakuufunga, ‘Nani kaufunga mlango?’ alijiuliza,
‘Au wameujua uwepo wangu?’ hakupata jibu.
Akiwa katika mawazo, alijiegemeza ukutani,
mara akahisi kitu kama msumari kikimchoma,
akageuka na kupapasa akakutana na kitu hicho,
akakitazama kisha akageuka upande wa kulia na
kugundua kuwa ile camera ilikuwa ikitazama
pale, akatikisa kichwa, akajaribu kukibonyeza,
mara ukuta wa mbele yake ukagawanyika
taratibu na kuacha uwazi mkubwa, Kamanda
Amata akatabasamu na kuvuka kwa tahadhari
eneo lile mpaka upande wa pili. Sasa likiona kile
chumba anachokitaka, akakijongea na kuufanyia
kazi mlango wake kisha akaingia, na kuanza
upekuzi wake, ofisi ya ‘Managing Director’, akiwa
amefanikiwa kupata kabrasha alitakalo ambalo
lilikuwa kwenye sefu ya siri sana ambayo si
rahisi kuigundua kwa mtu wa kawaida, aliamua
kuitoa fotokopi yote katika mashine iliyopo
hapohapo ofisini na kisha kuhifadhi vivuli vyake.
Akiwa anajiandaa kutoka akaona mlango
ukifunguliwa taratibu, akarudi nyuma na kujificha
pembeni mwa kabati karibu kabisa na ua la
plastick, hakuamini macho yake alipomuona
mwandada yule wa Kihindi akiingia, naye
akichakurachakura makabrasha lakini alishangaa
kuona yeye kachukua kabrasha lingine, hakujua
kwa nini.
»»»
Barabara ya Mandela
“Hakikisha unachomea vizuri, usiruhusu hewa
hata kidogo kutoka,” Shakrum alikuwa
akimwambia kijana mchomeaji aliyekuwa
akifanya kazi ya kutengeneza kitu mfano wa tank
la mafuta lakini likiwa na umbo la wastani.
Ilikuwa usiku mnene kazi hiyo ilipokuwa
ikifanyika, haikuwa kazi rahisi kwa jinsi ambavyo
kijitanki hicho kilikuwa kikiendelea kusukwa.
“Hapa vipi braza?” aliuliza Shakrum.
“Hapa poa, sasa watatia akili, lazima taifa
liteteme kwa hofu,” sauti ya Shailan ilikuwa
ikijibu swali la Shakrum.
Kazi iliendelea mpaka karibu na alfajiri, wakiwa
mezani wanakunywa kahawa mara gari moja
ndogo ikaingia
Shakrum aliiacha meza na kuiendea hiyo gari,
akafungua mlango na kukuta mwanamke
aliyelazwa katika kiti cha nyuma, akamtazama
na kutikisa kichwa.
“Tajan, Amata yuko wapi?” akamuuliza.
Tajan akafungua kitambaa kilichokuwa shingoni
mwake akachukua sigara na kuiwasha,
akaipachika kinywani na kupiga pafu kama nne
za nguvu, kisha akamtazama Shakrum, “Amata
hayupo nyumbani kwake, nimemchukua Malaya
wake huyo, najua kwa vyovyote atamtafauta
ndipo tutakapomkamata na yeye kiurahisi,”
akajibu.
“Ok, wazo zuri sana,” Shakrum alimpongea
Tajan, akawaita walinzi na kuwaamuru
wampeleke kwenye chumba maalum, wakafanya
hivyo.
≈≈≈
Kamanda Amata alitoka kwa upole wa hali ya
juu katika ngome ile kwa kufuata ujia mrefu
ambao hakujua hata ni wapi ulikoelekea,
alijua wazi kuwa kurudia njia aliyoingilia ni
hatari kubwa hivyo akaamua kutafuata njia
nyingine kuweza kuwa huru nje ya jumba
lile. Akiwa katika kupitapita ndipo
alipokutana na kitu kama kivuli kikitua
nyuma yake mita kadhaa kutoka yeye alipo,
hisia zake zilimtuma hivyo akaamua kugeuka
ili akubaliane na hisia hizo, kosa, alipogeuka
tu kabla hajakaa sawa alijikuta akipata
mateke mawili yaliyotua usoni mwake kwa
mtindo wa round kick, Kamanda Amata
alijitahidi kukwepa ijapokuwa lilikuwa ni
shambulizi la ghafla lakini hakufanikiwa,
aliyumba kidogo lakini mara akawa sawa na
kuangalia uelekeo wa adui yake ambaye sasa
alimuona akijiviringa chini kwa ufundi
mkubwa, akajua kuwa adui yake si mtu wa
mchezo hata kidogo, akajiweka sawa. Yule
mtu akajiinua kwa kasi ya upepo lakini kabla
hajakaa wima alijikuta akipata pigo takatifu
lililotua kifuani mwake na kumpotezea
uelekeo, Kamanda Amata baada ya kutoa
shambulizi lile, kwa mguu wake wa kulia
alikanyaga ukuta na kujizungusha hewani
alipotua chini mikono yake mikakamavu
ilitua na karate safi katika shingo ya adui
yake na kumpeleka chini. Kamanda Amata
alitulia wima akiwa kajipanga kwa
shambulizi linguine lakini hakumuona adui
yake pale mbele yake, kabla hajageuka
kuangalia nyuma alihisi akipigwa ngwala
kutokea upande wa nyuma, akaruka juu kwa
sentimeta kadhaa, hakukosea kucheza na
hisia zake katika kigiza kile kilichomfanya
kila mmoja apambane na adui yake kwa
tahadhari. Adui wa Amata alikua ni mjanja
kupita maelezo, alijizungusha na kupiga
ngwala ya miguu miwili ule uliotangulia
ulipita sentimeta kadhaa kutoa sakafuni na
Amata aliukwepa kwa kuruka lakini ule wa
pili ulifuatia juu kidogo ya ule wa kwanza,
huu ulimpata sawia kabisa katika visigino
vyake na kutokana na kasi ya mguu ule,
Amata alijikuta akikosa umakini hivyo kwa
wakati huo akili yake ilifanya kazi haraka na
kujirusha samasoti lakini alisahau kuwa eneo
hilo ulikuwa ni ujia mdogo ambao haukuzidi
mita moja na nusu kwa upana, so kwa
uamuzi wake huo akajikuta akijigonga
kichwa ukutanni na kitendo hicho kilifanya
kengele za tahadhari za siri katika jingo lile
kupata uhai, alipotua chini kama mzigo taa
kali ziliwaka katika ujia ule na hakuna
aliyeweza kujivuta hata sentimeta kumi,
ndipo Amata kwa shida sana aliweza
kumuona adui yake, akagundua kuwa
alikuwa akipambana na mwanamke wa
Kihindi, ShaSha, alimtazama kwa shida huku
akiona taswira inayofifia machoni pake,
akajitahidi kupambana na hali hiyo lakini
haikuwezekana hata kidogo, akapoteza nuru
kutokana na kupiga kicha chake kwa nguvu
ukutani.
≈≈≈
“Kazi imekamilika bila kuitolea jasho
kiongozi,” Shakrum alikuwa akimueleza
Shailan huku usoni akionesha furaha ya wazi
kabisa isiyofichika, “kamanda Amata, Yule
Malaya wa kihindi na mwanamke wa Amata,
wote tunao mikononi bila tabu, ni sisi tu wa
kutoa hukumu juu yao, nikiwa na maana
kuwa siku hizi mbili tulizobaki nazo tuna
uwezo wa kuitikisa dunia katika mhimili
wake kupitia nchi hii nyonge na dhaifu,”
aliendelea kuongea. Shailan alibaki
katumbua macho tu kwani hakuamini
anachoambiwa kuwa watu hao wote ambao
walikuwa wanatishia juhudi za kazi zao sasa
wapo mikononi mwao, bado ilikuwa ni kama
simulizi ya alfu lela ulela, Shalan hakuamini
kama Kamanda Amata wanae.
“Shakrum, unalolisema lina ukweli au ndio
sikukuu yua wajinga?” Shailan aliuliza.
“Tangu lini nakutaniaga wakati wa kazi
muhimu kama hii? Nimepewa ripoti kutoka
yadi kubwa kule Bunju hawa jamaa
wamejiingiza wenyewe katika mtego huo, na
hivi sasa wapo katika chumba cha chini na
pingu mbilimbili kila mmoja kuhakikisha
hawatoroki,” Shakrum alizidi kusisitiza.
“Habari njema, basi kwa ujumla tumemaliza
kazi yetu kwa urahisi ambao
hatukuutegemea. Haya mpe taarifa balozi
tukutane pale yadi kubwa haraka
iwezekanavyo,” Shailan hakuweza kuificha
furaha yake, muda uohuo alituma fax haraka
kule Mombasa kwa mkubwa wao naye
aliwapongeza kwa hilo akaamuru watu hao
wachinjwe mara moja na miili yao
ihifadhiwe kwenye kaburi la siri ambalo
limejengwa ndani ya yadi kubwa kupitia
chumba maalum kilicho ndani ya chini ya
ardhi.
Haikupita hata lisaa limoja timu yote ya
kikosi kazi cha ‘Freedom Fighters’ pamoja na
balozi wao hapa nchini Mr Scolleti walikuwa
wamekusanyika katika chumba maalumu
pale yadi kuu, Bunju.
“Tumepewa Baraka zote, za kuwakata vichwa
hawa mabwana, na mi sioni haja ya kupoteza
muda kwani kama kutusumbua
wametusumbua sana hasa huyu Amata, na
huyu nahitaji kumuua kwa mkono wangu
huu,” Shailan aliongea kwa jazba mbele ya
jopo lote hilo, akatulia kidogo akimtazama
mmoja baada ya mwingine kisha akaendelea
kusema, “Sasa hakuna po, kukipambazuka ni
onyo la mwisho kwa serikali kwani sasa
tayari ni wakati muafaka, afunguliwe kaka
yetu, mpigania uhuru mwenzetu, anayejua
kile anachokifanya, Jegan Grashan, awe huru
na keshokutwa turudi naye nyumbani
ambako atapokelewa kwa furaha,”
akamalizia.
Baada ya majadiliano machache, wote
wakashuka kwa chombo maalum mpaka
chini ya ardhi ambako walifika kwenye
chumba hicho cha siri, chumba madhubuti
kwani mlango wake ulifungwa kwa namba
maalum ambazo ni mtu mmoja tu aliyezijua,
Shakrum.
“Ah ha ha ha ha !!!!” lilikuwa cheko la
Shailan, cheko la dharau ambalo lilifika moja
kwa moja masikioni mwa Kamanda Amata
aliyekuwa amelala chini na pingu mbili
mkononi mwake, alisikia kwa uzuri kila
lizungumzwalo na watu hao lakini alijifanya
bado hana fahamu ilhari akijua hila zao,
ShaSha yeye alikuwa katulia tuli, hana la
kufanya katika hilo maana pingu zile
zilikuwa zimeimaban mikono na miguu yake
pale chini, alikutana mzcho kwa mzcho na
adui yake Scolleti, alyetumwa kwake kuja
kuichukua roho yake tu baada ya serikali ya
India kuchishwa na malalamiko ya mataifa
mbalimbali yaliyopelekea mengine kuwa na
mgogoro wa kidiplomasia na taifa hilo.
Scolleti, alivuta hatua chache sana na
akamfikia ShaSha pale alipoketi,
akamsukuma kwa mguu wake, ShaSha
akainua kichwa na kumtazama mtu huyo.
“Hivi wewe mwanamke, nchi yako
imekutuma na kukuamini kuja
kunichunguza mimi, we unanijua mimi
wewe, wenzako wote walionifuatilia mpaka
sasa hawajulikani walipo, na wewe leo ndio
zamu yako kuwafuata, kifo chako
hakitakuwa na maazishi, wala maiti yako
haitakuwa na mapambo yoyote, nani
aliyekwambia binadamu anaweza kufuata
nyayo za samba pa si kudhurika? Karibu
sana katika himaya ya Shetani, na sisi sote ni
wafuasi wake watiifu,” Scolleti aliongea kwa
sauti yake nzito, huku akimsukasuka ShaSha.
Bila kutegemea, Scolleti alijikuta akitemewa
mate usoni na mwanamke huyo jeuri,
aliyejiamini hata ndani ya pingu na
minyororo ya watesi wake.
“Hata ukiniua mimi bado wapo wanaokuja
kukutafuta, yupo ambaye atakutia mkononi
na kuivunja shingo yako hata kama si mimi,
Shetani mkubwa wewe, unayepoteza masiha
ya watu kwa kufadhili na kuhifadhi magaidi
sehemu mbalimbali duniani, ilahali kule
kwetu India unajifanya mwema kuwasaidia
masikini na kuwajengea mashule na
mahospitali ili kuilagha serikali, sasa umefika
wakati, msaada wako ni takataka mbele ya
wanaokujua na sasa kinachopangwa na
kutenganisha roho yako na mwili wako
ambao tungewapa ndege wa angani wafaidi
nyama iliyojaa damu ya ibilisi ndani yako,”
ShaSha hakumaliza kauli yake kwani teke la
nguvu lilitua ubavuni mwake, na kumlete
maumivu makali, hajakaa sawa teke lingine
na lingine, kisha Scolleti akaenda kwa
Shakrum na kumvua mkanda wa kijeshi
uliofungwa kiunoni mwake, vichapo kadhaa
vilimuacha ShaSha hoi hajitambui, damu
zikimtoka puani na kinywani, hasira
zilizotawala damu yake zilimfanya ajaribu
kujitikisa labda pingu zile zingemuachia
huru amuoneshe kazi mzee huyu lakini
haiku hivyo alibaki kuuma meno tu.
Shakrum akamuendea Scolleti na kumvuta
pembeni, “Braza, usifanye kazi ambayo bado
muda wake,” alimwambia
JE NINI KITATOKEA? SHASHA ATACHINJWA?
USIKOSE CHAPISHO LA 14
 
asante sana kid kud naomba na hii ujitahidi kuimaliza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom