Riwaya: I died to save my President

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
I DIED TO SAVE MY PRESDANT

Mtunzi Patrick Ck

Simu 0764294499

Season 1

Sehemu 1


hughuli zote zilizopangwa
kufanyika katika kikao
cha bunge zilikamilika na
kabla ya kusitisha shughuli za
bunge kwa siku hiyo hadi siku
inayofuata,spika wa bunge
akamuita waziri anayeshughulika
na bunge mheshimiwa William
Kangoga ili aweze kutoa hoja ya
kutengua kanuni
“Meshimiwa Spika, naomba
kwa ruhusa yako sasa nitoe hoja
kwamba bunge lako tukufu
litengue kanuni ya bunge ili
kuwaruhusu vijana wetu
wanafunzi waliofanya vizuri katika
mithani yao ya kidato cha nne
waweze kuingia bungeni hapo
kesho.Mheshimiwa spika naomba
kutoa hoja”
Baada ya hoja ile kutolewa
wabunge wote wakasimama na
kuiunga mkono halafu spika
akawahoji na wote wakakubalianana hoja ile kwamba kanuni ya
bunge itenguliwe na kuwaruhusu
wanafunzi ishirini waliofanya
vizuri katika mitihani yao ya
kidato cha nne waweze kuingia
bungeni ili waweze kupongezwa na
bunge.
“Ahsanteni sana waheshimiwa
wabunge kwa kukubali watoto
wetu waje bungeni tuwapongeze
na kuwatia moyo ili waweze
kufanya vizuri zaidi huko mbele
waendako.” Akasema spika wa
bunge halafu akasitisha shughuli
za bunge hadi siku inayofuata saa
tatu za asubuhi
*********************
Ni saa tano za usiku sasa
lakini bado Patricia hakuwa na
usingizi.Yeye na mama yake
walikuwa katika chumba kilichoko
ghorofa ya nne ndani ya hoteli hii kubwa mjini Dodoma ijulikanayo
kama Dodoma view hotel.Ni moja
kati ya hoteli yenye hadhi ya juu
kabisa mjini Dodoma na ambayo
wabunge wengi wa bunge la
jamhuri ya muungano wa
Tanzania hupenda kufikia .
“Patricia mbona hulali?Si
unajua siku ya kesho itakakuwa
ndefu? Jitahidi ulale ili usije
ukasinzia katika ukumbi wa
Bunge” akasema Bi Doroth
Mwaukala mama mzazi wa Patricia
“Mama nashindwa kabisa
kupata usingizi siku ya leo.Usiku
nauona mrefu sana” akasema
Patricia binti aliyejaaliwa uzuri wa
kipekee mno
“Una wasi wasi?
“Ndiyo mama lakini si
sana.Nawaza kuhusu kesho sijui
itakuaje pale nitakaposhikana
mkono na mheshimiwa waziri
mkuu huku nikionekana katika
televisheni nchi nzima.Mama sikuwahi kuota siku kama ya
kesho itakuja kunitokea katika
maisha yangu.Bado siamini hadi
hapo nitakaposhikana mkono na
waziri mkuu ndipo nitaamini ni
kweli.Mama kesho ni siku yangu
kubwa mno” akasema
Patricia.Mama yake aliyekuwa
akimtazama mwanae
akatabasamu na kusema
“Usiwe na hofu Patricia.Hii si
ndoto bali ni kitu cha kweli
kinachokwenda kutokea hapo
kesho.Kama ingekuwa ni ndoto
tusingekuwa hapa Dodoma mida
hii katika hoteli kubwa na nzuri
kama hii.Patricia unapaswa
kujivunia mafanikio yako haya
makubwa uliyoyapata.Mwanangu
umenitoa kimaso maso mimi
mama yako kwani hakuna
aliyetegemea kama mwanafunzi
aliyeshika namba moja nchini
Tanzania atakuwa ni kutoka
katika familia masikini kama ya kwetu.Umeidhihirishia nchi na
dunia kwamba hata mtoto wa
masikini anaweza akafanya
mambo makubwa na ya
kushangaza.Umelipandisha
kileleleni jina la familia yetu na
kwa sasa sisi si watu wa
kudharaulika tena kama
ilivyokuwa hapo awali.Laiti baba
yako angekuwa hai kushuhudia
tukio hili sipati picha angekuwa
na furaha ya namna gani…”
akasema Bi Doroth.
“Mama sifa na shukurani
zimwendee mwenyezi Mungu kwa
neema na Baraka zake nyingi
kwangu lakini sifa na shukrani za
pekee pia ni kwako wewe
mama.Wewe ndiye kila kitu
kwangu na ndiye uliyefanikisha
haya yote yakawezekana.Umenipa
ushirikiano mkubwa.Maongozi na
maelekezo yako yameniweka
katika nafasi hii nilipo sasa.Mama
unastahili sifa za kipekee kwa kunijali na kuwa nami na
kunivumilia hata katika nyakati
zile ngumu kabisa.Umejinyima
mambo mengi ili mwanao niweze
kusoma na haya ndiyo matunda
yake” akasema Patricia halafu
akainuka na kuelekea dirishani
,akalifungua na kuutazama mji wa
Dodoma ulivyokuwa usiku hii.
“ Huu ni mwanzo wa safari
yangu ndefu ya maisha.Nina ndoto
nyingi sana za kutimiza maishani
na ndoto ya kwanza ni kuiondoa
familia yangu katika umasikni
huu mkubwa tulionao.Namuonea
huruma mama yangu namna
anavyohangaika
kunisomesha.Lazima nikiri
kwamba si kazi rahisi kwake lakini
amejitahidi kwa kila namna na
kuhakikisha kwamba hakuna siku
nimekosa shule.Huyu ni mama
anayestahili sifa za pekee kabisa.”
Akawaza Patricia halafu akalifunga dirisha na kurejea
kitandani
“ Patricia jitahidi ulale.Muda
umekwenda sana.Kesho
tunatakiwa tuamke asubuhi na
mapema” akasema Bi Doroth
“ Mhh ! mama sijui kama
nitaweza kupata usingizi.Sijazoea
kulala sehemu laini kama hii”
akasema Patricia na wote
wakacheka
“ Patricia unatakiwa uanze
kuzoea vitu kama hivi.Huu ni
mwanzo wako wa safari ndefu ya
maisha yako.Siku moja vitu kama
hivi utaviona vya kawaida.Jitahidi
ulale” akasema Mama yake halafu
akamfunika shuka vizuri akaenda
kuzima taa wakalala.
*********************

Ilikuwa ni mara ya kwanza
kwa Patricia kuingia katika
viwanja vya bunge.Aliustaajabia uzuri wa eneo hili.Hakukaukiwa
na tabasamu.Siku hii alikuwa
amependeza mno.Alivaa gauni
lenye rangi nyeupe chini na juu
likiwa na rangi nyeusi.Miguuni
alivaa viatu virefu vilivyoendana
na gauni alillolivaa.Mavazi haya ya
gharama alizawadiwa na Juliana
mwanamitindo maarufu hapa
nchini ambaye alifurahishwa mno
na matokeo ya Patricia.
Wanafunzi bora ishirini
walipokewa na katibu wa bunge
halafu wakakabidhiwa kwa
wafanyakazi wa bunge ambao
walianza kuwatembeza sehemu
mbali mbali za bunge .Patricia
alionekana kuwa na furaha
pengine kuliko wengine wote kwa
sababu hakujua kama siku moja
angeweza kufika mahala pale.Kati
ya wanafunzi ishirini waliofanya
vizuri mtihani wa kidato cha nne
wengi walionekana kutoka katika
familia bora zenye kujiweza kifedha.Ni Patricia pekee ambaye
alitoka katika familia iliyo masikini
zaidi lakini pamoja na umasikini
wa familia yake iliyokuwa ikiishi
katika chumba kimoja tu cha
kupanga ,aliweza kuwaongoza
wanafunzi wote nchini waliofanya
mtihani wa kidato cha nne na
kushika nafasi yakwanza.
Kwa siku ya leo ingekuwa
vigumu kuamini kwamba Patricia
anatoka katika familia duni
kwanamna alivyokuwa
amependeza kwa mavazi
aliyozawadiwa na mwanamitindo
Juliana.Wakati amekaa na
wenzake wakisubiri kuingia katika
ukumbi wa bunge mara akatokea
mama yake na kumuita pembeni
“ Mama kuna nini mbona
umefurahi namna hiyo?
“ Patricia huwezi
amini.Juliana amekuja .”
“ Juliana?! Patricia akastuka
“ Ndiyo “ Amekuja kufanya nini?
“ Amekuja kukusapoti katika
siku yako kubwa.”
“ Kweli mama ?!! akauliza
Patricia huku akiruka ruka kwa
furaha
“ Ndiyo Patricia.Anasema
kwamba hakutaka kukutaarifu
mapema kwamba atakuja alitaka
akushangaze”
“ mama yuko wapi dada
Juliana? Nipeleke nikaonanane
naye” akasema Patrcia na kwa
haraka wakatembea hadi katika
maegesho ya magari ambako
Juliana alikuwa garini na rafiki
yake aishiye mjini Dodoma.Mara
tu Patricia alipotokea,Juliana
akatoka garini na kumkumbatia
“Wow ! Dada Juliana sikujua
kama utakuja Dodoma”akasema
Patrcia.Juliana akatabasamu na
kusema
“Sikutaka kukutaarifu
mapema kama nitakuja Dodoma.I wanted to surprise you.Siwezi
kukosa katika siku yako kubwa na
muhimu kama hii ya leo.Patricia
najua una wasi wasi sana na
nimeona katika orodha ya watoto
ambao utaambatana nao leo
bungeni ,wote ni kutoka katika
familia zenye uwezo
mkubwa.Usiwe na wasi wasi you
have a huge support” akasema
Juliana na kumshika mkono
Patricia wakaingia
garini,akafungua mkebe mkubwa
wa poda na kuanza kumremba
halafu akavua heleni zake nzuri za
dhahabu
akamvisha.Akamuangalia na
kutabasamu.
“Now you look like a
princes.Go now.Tutaonana
baadae” akasema Juliana ,
Patricia akakimbia kwenda
kuungana na wenzake.Uso wake
ulikuwa na tabasamu zito.Baada
ya Patricia kuondoka,Juliana akaagana na Bi Doroth kwa ahadi
ya kuonana jioni ya siku hiyo
katika sherehe ya kuwapongeza
akina Patricia .
“Juliana nakushukuru sana
kwa msaada wako
mkubwa.Umeweza kunifuta aibu
kubwa siku ya leo. Bila wewe sijui
Patricia angeonekanaje leo.Lakini
kwa saabu yako leo Patricia
ameng’aa na kupendeza kuliko
wenzake wote” akasema Bi Doroth
“ Mama hupaswi
kunishukuru .Patricia ni kama
mdogo wangu.Mimi ni mmoja wa
watu walioguswa sana na matokeo
yake mazuriNinathamini sana
elimu hasa kwa mtoto wa kike na
ndiyo maana nimeamua kwa moyo
wangu kujitolea kumsaidia
Patricia ili aweze kutimiza malengo
yake.Bado ana safari ndefu sana
na ili afikie malengo yake
anahitaji sana sapoti yetu sisi
sote” akasema Juliana halafu akaagana na Bi Dprpth na
kuondoka kwa ahadi ya kukutana
jioni .
***************

Kipindi cha maswali na
majibu kilimalizika , Spika wa
bunge akasoma baadhi ya
matangazo ikiwa ni pamoja na
kuwatambulisha wageni waliofika
hapo bungeni kwa mafunzo halafu
akamuita katibu ili aweze kusema
ni kitu gani kilichokuwa
kinaendelea.Katibu akasimama na
kulitaarifu bunge kwamba ni
wakati wa kuwaruhusu wanafunzi
waliofanya vizuri waingie bungeni
wakabidhiwe vyeti na waziri
mkuu.Spika wa bunge akasimama
na kusema
“Waheshimiwa wabunge ,jana
tulitengua kanuni ya bunge ili
kuwaruhusu watu ambao si
wabunge kuingia ndani ya ukumbi wetu huu.Wageni tuliowaalika ni
wanafunzi ishirini bora katika
mtihani wa kidato cha nne
.Naombeni wakati vijana wetu
wakiingia humu
ukumbini,muwashangilie kwa
makofi kwani wamefanya kazi
kubwa sana” Akasema Spika na
kumuamuru askari wa bunge
awaongoze wanafunzi kungia
ukumbini .Lango kuu
likafunguliwa na wanafunzi
wakaingia wakiwa katika mistari
miwili,mmoja wa wanaume na
mwingine wa wanawake.Makofi
mengi ,vigere gere pamoja na meza
kugongwa vikasikika.Kilikuwa
kipindi cha furaha sana kwa
wabunge kuwashuhudia
wanafunzi wale ishirini bora.Spika
wa bunge akaomba utulivu halafu
akamkaribisha waziri mkuu ili
aweze kusema machache kabla ya
kuwakabidhi vyeti.Waziri mkuu
wa Tanzania mheshimiwa Thobias Kangeba kengaiza akasogea mbele
na kusema
“ Mheshimiwa spika naomba
nikushukuru sana kwa kunipa
nafasi hii niweze kusema
machache kuhusiana na tukio
hili.Napenda nikushukuru wewe
na bunge lako kwa kukubali
kutengua kanuni ili wanafunzi
hawa waweze kukaribishwa
bungeni na kupongezwa.Binafsi
ninafuraha kubwa sana kuwaona
wanafunzi hawa ingawa
ningefurahi zaidi kama
kungekuwa na uwiano sawa baina
ya wavulana na wasichana kwa
sababu naona kati ya wanafunzi
bora ishirini wasichana ni nane tu
na kumi na mbili ni
wavulana.Kuna haja ya kuendelea
kuwekeza zaidi katika elimu ya
mtoto wa kike ili kuwe na uwiano
sawa wa ufaulu.Pamoja na hayo
,kwa niaba ya serikali napenda
kutoa pongezi zangu nyingi kwenu wanafunzi kwa ufaulu huu
mzuri.Haikuwa kazi rahisi
.Yalikuwa ni mapambano na leo
hii mmeibuka
vinara..Nawapongeza pia walimu
na wazazi wenu kwa ushirikiano
wao wa kuwasaidia kuwafikisha
hapa mlipofika.”
“Mheshimiwa spika,mfumo
wetu wa elimu bado unakabiliwa
na changamoto nyingi kama vile
uhaba wa walimu,vitabu,vifaa vya
kufundishia na kujifunzia,lakini
serikali imekuwa ikjitahidi kutatua
changamoto hizi na leo hii
tunashuhudia mwanafunzi wa
kwanza Tanzania ametoka katika
shule ambazo zimejizolea
umaarufu kama shule za kata
ambazo zimekuwa na changamoto
nyingi.”
Makofi mengi yakapigwa
halafu waziri mkuu akaendelea
Mheshikiwa spika,ninaomba
niseme kwamba hata kama tukifanikiwa kutatua changamoto
zote zinazoikabiili sekta ya elimu
hapa nchini lakini bila juhudi
binafsi za wanafunzi wenyewe
kamwe hakutakuwa na ufaulu
mzuri.Kuna shule zenye walimu
wa kutosha na vifaa vya
kufundishia na kujifunzia lakini
hazikufanya vizuri .Kwa hiyo basi
naomba niwaase wanafunzi
waongeze kasi ya kujisomea
.Mwalimu ana nafasi yake lakini
mwanafunzi pia ana nafasi yake.Ni
vyema kila mmoja akaitumia
vyema nafasi yake.”
“Mheshimiwa spika naomba
nimalizie kwa kutoa pongezi zangu
nyingi kwa niaba ya serikali na
kuwatakia kila la heri wanafunzi
hawa katika safari yao
ndefu.Someni kwa bidii na taifa
linawasuri mje
kulitumikia.Hongereni sana”
akamalizia nasaha zake
mheshimiwa waziri mkuu,wabunge wakamshangilia
kwa kugonga meza halafu spika
wa bunge akasimama
“Tunakushukuru sana
mheshimiwa waziri mkuu kwa
nasaha zako.Natumai wanafunzi
wote wamekusikia na
watayafanyia kazi yale uliyowaasa
Waheshimiwa wabunge
kinachofuata sasa ni mheshimiwa
waziri mkuu kuwakabidhi vyeti
vijana wote ishirini.” Akasema
Spika na zoezi la kutoa vyeti
likaanza.Wa kwanza kuitwa
kwenda kupokea cheti alikuwa
Patrcia.Ukumbi wote wa bunge
ukalipuka kwa makofi na
kushangilia wakimpongeza
msichana huyu kwa kushika
namba moja.Zoezi lilipomalizika
baadhi ya wabunge walipata nafasi
ya kusema machache na kuwaasa
wanafunzi kusoma kwa bidii.Kila
aliyesimama hakuacha
kumpongeza na kumtolea mfano
 
I DIED TO SAVE MY PRESDANT

Mtunzi Patrick Ck

Simu 0764294499

Sehemu 2

Patrcia.Kila mbunge alikunwa
vilivyo na uwezo wa kipekee
aliouonyesha binti huyu
Hatimaye shughuli zote
zilzopangwa kufanyika katika
kikao cha asubuhi zikamalizika na
spika akasitisha shughuli za
bunge hilo hadi saa kumi na moja
za jioni.
Nje ya ukumbi wa bunge ,kila
mbunge alitaka kumpa mkono na
kumpongea Patricia.Waandishi wa
habari hawakubaki nyuma katika
kumuhoji Patricia na wenzake
kuhusu siri ya ushindi wao.Baada
ya zoezi lile kukamilika Patricia na
mama yake wakaingia katika gari
na kurudishwa hotelini ambako
walipata chakula cha mchana
kisha wakaenda chumbani kwao
kupumzika na kujiandaa kwa ajili
ya sherehe za pongezi
zitakazofanyika jioni .
“ Nimepokea simu nyingi toka
kwa majirani zetu wote pale mtaani wakisema kwamba
wamekuona katika teleisheni.Dah
! Sikutegemea kama lingekuwa ni
tukio kubwa namna hii” akasema
Bi Doroth mama yake Patricia.
“ Mama siku ya leo ni siku
yangu ya furaha sana.Nashindwa
niielezaje furaha niliyo nayo.Leo
nimeshikaka mkono kwa mara ya
kwanza na waziri mkuu.Ninaona
ni kama muujiza.Nahisi ni kama
ndoto” akasema Patrcia akiwa
amekishika cheti alichopewa na
waziri mkuu.Mama yake
akatabasamu na kusema
“ Haya pumzika Patricia .Bado
kuna shughuli nyingine leo jioni.”
akasema bi Doroth
*******************
Saa kumi na mbili za jioni
mrembo Juliana akawasili katika
hoteli waliyofikia Patrcia na mama
yake Wow !Patricia my dear …!!!”
akasema Juliana kwa furaha na
kumkumbatia Patricia
“Karibu sana dada Juliana.”
Akasema Patricia
“ Ahsante sana
Patrcia.Congraturations.It was
your first time to enter that
building and you showed a great
confidence.Nilikuwa nakuangalia
kupitia Luninga.Everybody is
talking about you.Congraturations
again” akasem Juliana
“ Ahsante sana dada
Juliana.Jumba lile ndiyo maana
likaitwa tukufu.Linatisha kwa
ndani kama ni mara yako ya
kwanza kuingia” akasema Patricia
“ Unavaa nini jioni ya leo?
akauliza Juliana.Patricia
akamuonyesha nguo ambayo
alipanga kuivaa jioni hiyo Hapana usivae hiyo.You
have to look like a queen .All eyes
must be on you tonight” akasema
Juliana na kufungua begi alilokuja
nalo akatoa gauni refu jeusi lenye
k u m e r e m e t a
“Utavaa hili” akasema halafu
akatoa vifaa vya urembo na
kuviwe ka me zani akaanza
kumremba Patricia.Baada ya
k u m a l i z a k u m r e m b a
akamuangalia na kutabasamu.
Patricia you are blessed with
the natural beauty.You deserve a
miss world crown” akasema
Juliana na wote wakacheka
Baada ya kumaliza kumremba
Patricia Juliana akaanza
kumremba na Bi Doroth
“ Ahsante sana Juliana kwa
kuja kwako.Bila wewe sijui tungeonekana vipi” akasema Bi
Doroth
“ Usihofu mama.Nisingeweza
kukosa tukio kubwa kama hili
kwa ajili ya mdogo wangu “
akasema Juliana
Saa moja na nusu za jioni
tayari walikwisha
jiandaa,wakaingia garini na
kuelekea mahala inakofanyikia
sherehe ya kuwapongeza akina
Patricia.Endapo ungebahatika
kumshuhudia Patricia jioni ya leo
ungedhani ni mwanamitindo
maarufu sana hapa nchini kwa
namna alivyokuwa amependeza
Waliwasili ukumbini
wakapokelewa na kuelekezwa
sehemu za kukaa. Patricia
akawaacha mama yake na Juliana
kwa ajili ya kwanda kukaa katika
sehemu waliyokuwa wameandaliwa kwani Kulitengwa
sehemu maalum ya wanafunzi
kukaa .
“ Patricia don’t be
nervous.Always put a smile on
your face.” Juliana
akamnong’oneza Patricia sikino
wakati akienda kuungana na
wenzake katika sehemu
waliyoandaliwa.Kama alivyokuwa
ametazamia Juliana ndivyo
ilivyokuwa ,Patrica alikuwa
anameremeta na kila mtu
alimtupia jicho.
Bado waheshimiwa wabunge
na wageni mbali mbali waliendelea
kuwasili.Aliyekuwa akisubiriwa ni
mgeni rasmi ambaye ni waziri
mkuu wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania.Katika sherehe hii
alikuwepo pia mke wa rais bi
Bernadetha Jumbo ambaye ni mwanamke anayepambana sana
kuhusiana na elimu ya mtoto wa
kike.
“ Hi” Patricia akasalimiwa na
kijana mmoja mweupe mtanashati
aliyevaa suti nzuri nyeusi
iliyomkaa vyema.Kijana Yule
alikuwa ni moja kati ya wanafunzi
waliofanya vizuri.Patricia
akageuza shingo na kumuangalia
kijana Yule .Wote wawili
wakatabasamu na kisha Patricia
akasema
“ Hi”
Kijana Yule aliyekuwa na sura
nzuri na vishimo mashavuni
anapotabasamu akamnyooshea
mkono Patricia na kusema
“ Hongera sana”.
Patricia akatabsamu na kusema
“ Hongera nawe” Sisi sote tunapaswa kukupa
wewe hongera kwani ndiye
uliyetuongoza.” Akasema Yule
kijana na kumfanya Patricia azidi
kutabasamu
“ Sote tumeshinda.Sote tuko
katika kundi moja la ishirini bora”
akasema Patricia halafu kikapita
kimya kifupi Yule kijana akasema
“ By the way I’m Elvis.”
“ I’m Patricia.” Akajibu
Patricia.
“ Huna haja ya kujitamblisha
Patricia.Hakuna mtu
asiyekufahamu kwa sasa hapa
nchini.Wewe ni mmoja wa watu
maarufu sana hapa nchini”
akasema Elvis na kumfanya
Patricia atabasamu.Kabla
hajasema kitu mwanamama
mmoja ambaye ni mbunge
akamsogelea na kusema Patricia nilikutafuta mchana
pale bungeni sikukuona.Kuna
jambo ambalo nilitaka
nikufahamishe. Ni kwamba
umechaguliwa kutoa neno la
shukrani kwa niaba ya wenzako
wote”
“ Mimi ..?!! Patricia akauliza
kwa mshangao
“ Ndiyo wewe”
“ Mheshmiwa sidhani kama
nitaweza kuongea mbele ya umati
huu mkubwa wa
viongozi.Tafadhali naomba
utafute mtu mwingine afanye
hivyo mimi sintaweza”
“ Hapana Patricia utaweza
tu.Wewe ndiye uliyeshika namba
moja kati ya wenzako wote kwa
hiyo unapaswa kuwaongoza
wenzako pia katika kutoa
shukrani.” Patricia akafikiri kidogo na
kusema
“ Nitaenda kusema kitu gani?
Akauliza Patricia kwa wasi wasi
“ Say anything.Ili mradi liwe
ni neno la shukrani.You can do it
Patricia.Show all these people that
you deserve to be number one”
akasema Yule mbunge na mara
Elvis aliyekuwa kimya akifuatilia
maongezi kati ya Patricia na Yule
mbunge akaingilia kati na kusema
“ Madam usihofu
nitamsindikiza mimi ili kumpa
sapoti na kumfanya asiogope”
akasema Elvis
“ Good.Hilo ni jambo
zuri.Patricia atakapoitwa
utamshika mkono na kumuongoza
mpaka pale mbele” akasema
mbunge na kumgeukia PatriciaStart preparing
yourelf.Itumie vyema nafasi hii”
akasema Yule mbunge na
kuondoka.Patricia alionekana
kuingiwa na woga mwingi
“ Usiogope Patrcia.You can do
it” akasema Elvis.
“ Sijawahi kuongea mbele ya
hadhira kubwa kama hii tena
kukiwa na viongozi wa juu wa
serikali.” Akasema Patricia
“ Patricia kama umeweza
kuwazidi akili wanafunzi wote wa
Tanzania na ukashika namba
moja ,huwezi kushindwa kuongea
neno pale mbele.Just say anything
you want to say”
“ C’mon Elvis,ule ulikuwa ni
mtihani na hatufanyi kwa
kuongea.I don’t know what I have
to say” Elvis akamtazama Patricia
usoni akatabasamu na kusema
“ Unataka nikuandikie kitu
cha kwenda kuongea pale mbele?
“ No ! don’t do that” akasema
Patrcia na kuinuka akaelekea
katika meza waliyokuwa wamekaa
mama yake pamoja na
Juliana.Akamuita Juliana
pembeni
“ Patricia whats wrong? Naona
sura yako imebadilika.Unaogopa
nini?
“ Dada Juliana kuna kitu
nimeambiwa muda huu ambacho
kimenistua kidogo”
“ Kitu gani Patrcia?
“ Nimeambiwa kwamba mimi
ndiye nitakayetoa neno la
shukrani kwa niaba ya wenzangu
.Nimestukizwa na sijafanya
maandalizi yoyote.Sielewei nitasema nini pale mbele ya
viongozi hawa wakubwa wa
kiserikali.” Akasema Patrcia
“ Kwa nini hawakukutaarifu
toka mapema ukafanya
maandalizi? Akauliza Juliana
“ hata mimi sielewi ni kwa
nini wamefanya hivi .This is
unfair.Wangenieleza toka mapema
ili nijiandae akalalama
Patricia.Juliana akatabasamu
akamshika bega na kusema
“ Relax my dear.Relax.Put
back your smile .Usikwazike na
hilo.Wamekuchagua kwa sababu
wanajua una uwezo mkubwa kwa
hiyo ukiitwa pale mbele nenda
kawaonyeshe kwamba unaweza
na unastahili kuwa namba moja
Tanzania.Waonyeshe kwamba
hukubahatisha kushika nafasi
hiyo.Jambo lingine jihadhari na matumizi ya lugha.Usichanganye
lugha.Ongea Kiswahili fasaha na
kilichonyooka.I believe in you
Patrcia.You can do it.Go and make
your mom proud.make us all
proud my dear” akasema Juliana
na kumfanya Patricia atabasamu.
“ dada Juliana nitaenda
kusema nini pale mbele? I’m a bit
scared” Akauliza Patricia
“ say anything you want to
say.Ongea neno lolote la shukrani
unalolijua.This is your
time.Waandishi wa habari wako
hapa na wote watayaelekeza
macho yao kwako.Wamekupa
nafasi hiyo makusudi ili kukupima
kwa hiyo wadhihirishie kwamba
unastahili” akasema Juliana na
mara ikasikika sauti ya muongoza
shughuli akiwataka watu wote
walio nje ya ukumbi kuingia ndani kwani muda wowote sherehe
zinarajia kuanza.
“ Watu waliokuwa nje
wakaingia ukumbini na sherehe
zikaanza.Ilikuwa ni sherehe nzuri
iliyoambatana na hotuba za
viongozi mbali mbali akiwemo
waziri mkuu na mke wa
rais.Baada ya hotuba za viongozi
kikafuata kipindi cha utoaji wa
tuzo na zawadi kwa wanafunzi
wote na shule zilizofanya vizuri
zikatolewa.
Baada ya zoezi lile kukamilika
,muongoza shughuli
akawafahamisha watu kwamba ni
wakati wa chakula na baada ya
chakula Patricia akaitwa mbele ili
aweze kutoa neno la shukrani kwa
niaba ya wenzake.Ukumbi wote
ukalipuka kwa shangwe baada ya
Patrcia kuinuka na kuanza kuelekea mbele ya ukumbi akiwa
ameongozana na kijana
mtanashati sana Elvis.Uso wake
haukukaukiwa tabasamu.Akafika
mbele na kukabidhwa kipaza
sauti.Ilikuwa ni mara yake ya
kwanza kukishika na
kukitumia.Mikono ilikuwa
inamtetemeka na midomo
kumcheza kiasi kwamba
alishindwa aanze vipi.Watu wote
wakakaa kimya tayari kumsikiliza
.Mara maneno ya Juliana
yakamjia kichwani.
“Wamekuchagua kwa sababu
wanajua una uwezo mkubwa kwa
hiyto ukiitwa pale mbele nenda
kawaonyeshe kwamba unaweza
na unastahili kuwa namba moja
Tanzania.Waonyeshe kwamba
hukubahatisha kushika nafasi
hiyo” I have to do it..I can do it”
akasema moyoni na kwa ujasiri
akakishika vizuri kipaza sauti
akakohoa kidogo kurekebisha koo
na kusema
“ Mheshimiwa waziri
mkuu,mpendwa mama yetu mke
wa rais,waheshimiwa mawaziri
,wabunge na viongozi wengine wa
serikali,walimu ,wazazi ,
wanafunzi wenzangu,wageni
waalikwa mabibi na
mabwana,ninapenda kumshukuru
sana mwenyezi Mungu mwingi wa
rehema kwa kutujalia wote
kuwepo hapa usiku huu.”
Maneno haya ya utangulizi
yakazidi kumpa ujasiri
.Akaendelea
“ Waheshimiwa viongozi
,wageni waalikwa mabibi na
mabwana nimesimama mbele yenu kwa unyenyekevu mkubwa
ili kutoa neno la shukrani kwa
niaba ya wanafunzi wenzangu
wote tulioko hapa usiku huu”
Akatulia kidogo halafu
akaendelea
“ Baba yangu alifariki nikiwa
darasa la tano.Alifariki kwa ajali
ya gari.Kifo chake kiliacha pengo
kubwa sana kwangu na kwa
familia yangu .baba yangu
hakuwa tajiri kwa hiyo alipofariki
hakutuachia mali yoyote hali
iliyomlazimu mama yangu ashike
nafasi zote mbili yaani kama baba
na kama mama.Mama yangu Bi
Doroth ambaye niko naye hapa
usiku huu,hakuwa na kazi ya
maana zaidi ya kufua nguzo katika
majumba ya wahindi.Pamoja na
kazi hiyo yenye ujira mdogo lakini
bado alielekeza nguvu zake zote katika kuhakisha kwamba hata
hicho kidogo alichokuwa akikipata
katika kazi zake za ufuaji
anakitumia katika kuniendeleza
kielimu.Aliamini kwamba elimu
pekee ndiyo itakuwa mkombozi
wangu.”
Patricia akanyamaza na
kuitazama hadhira ile iliyokuwa
kimya ikimsikiliza halafu
akaendelea
“Nilichaguliwa kuendelea na
elimu ya sekondari katika moja ya
shule zile zenye umaarufu kama
shule za kata.Ni shule yenye
changamoto nyingi,hatukuwa na
walimu wa kutosha,vifaa vya
kutosha vya kujifunzia n.k.Pamoja
na hali hiyo bado mama yangu
aliendelea kuniunga mkono katika
kila hatua niliyopiga.Alininunulia
vitabu na kunilipia masomo ya ziada.Kuna nyakati ilimlazimu
kukaa nami hadi usiku katika
sehemu niliyokuwa nikijisomea
aidha na wenzangu au masomo ya
ziada ili kuhakikisha kwamba
ninarudi nyumbani nikiwa salama
.Alikuwa mkali sana kila pale
ambapo sikufanya vizuri shuleni
jambo ambalo lilinifanya niongeze
bidii sana katika masomo na
hatimaye leo hii nimesimama
mbele yenu enyi waheshimiwa
sana nikiwa mwanafunzi
niliyeshika namba moja katika
mtihani wa kidato cha nne nchini
Tanzania”
Makofi mengi na vigere gere
vikapigwa.Bi Doroth mama yake
Patricia alishindwa kujizuia
kutokwa na machozi..Patricia
akaendelea
 
Kulubule the tale teller Shukrani sana!!

Nasubiri nasubiri viwii vya kulalia
 
I DIED TO SAVE MY PRESDANT

Mtunzi Patrick Ck

Simu 0764294499

Sehemu 3

Najua mtajiuliza ni kwa nini
nimeyasema haya
yote.Nimeyasema haya yote
kwanza kutoa shukrani zangu za
kipekee kwa mama yangu kipenzi
,walimu wangu na walezi wangu
walionisaidia mimi binafsi kufika
hapa nilipofika.Ni wengi
wamenisaidia na sintaweza
kuwataja wote kwa majina lakini
kwa ujumla wao ninasema
ahsanteni sana” makofi mengi
yakapigwa
“ Pili nimeyasema haya yote ili
kuonyesha wazi kwamba
mafanikio ya mtoto yanachangiwa
na mambo mengi lakini kubwa ni
ushiriki wa mzazi.Pamoja na
umaskini wake mama yangu
ameshirikiana nami katika kila
hatua niliyopiga.Pale
nilipoanguika alikuwa mtu wa
kwanza kunipa moyo nikainuka
nikasonga mbele.Mama huyu ni
mfano wa kuigwa na wazazi
wote.Kushindwa kwa wanafunzi
wengi kunachangiwa kwa kiasi
kikubwa na ushirikiano mdogo wa
wazazi .Sisi wanafunzi ishirini
tulioko hapa tulioko hapa usiku
huu tumepata mafanikio haya
kwa juhudi za wazazi
wetu.Ahsanteni sana wazazi wote
mlioko hapa kwa juhudi zenu na
ushirikiano mnaowapa watoto
wenu.Kwa wale wazazi na walezi
ambao hawako karibu na watoto
wao,ni wakati wenu wa
kubadilika.Watoto wenu
wanawahitaji sana.Kwa niaba ya
wenzangu wote tunawashukuru
nyote kwa mapokezi
mazuri,pongezi mlizotupa na
zawadi nzuri mlizotuzawadia.Tumejifunza
mengi toka kwenu na tutasoma
kwa bidii sana kwani tumetambua
nchi yetu inatuhitaji
sana.Tunawatakia nyote afya
njema na mafanikio katika
kufanikisha majukumu mliyonayo
kwa taifa.Ahsanteni na Mungu
awabariki.” Patricia akamaliza na
kumkabidhi muongoza shughuli
kipaza sauti.Watu wote
walikuwawamesimama wakipiga
makofi.Wote walikunwa na
maneno yale na kuduwazwa kwa
uwezo mkubwa aliokuwa nao
Patricia.Patriciai akaongozwa
akaenda kupeana mkono na waziri
mkuu ,kisha mke wa rais na
viogozi wengine wa meza kuu
halafu akageuka na kuanza
kupiga hatua kurejea kitini lakini
muongoza shughuli akamzuia Ndugu wageni waalikuwa
,mabibi na mabwana,nadhani
nyote mmeshangazwa na uwezo
mkubwa alio nao binti yetu
Patricia.Ameongea maneno mazito
sana na nina imani kila mmoja
wetu hapa ameguswa .Miongoni
mwa watu walioguswa ni mama
Bernadetha Jumbe mke wa rais
wetu ambaye anataka kusema
neno.Karibu sana mama”akasema
muongoza shughuli na makofi
mengi yakapiga.Bi Bernadetha
Jumbo mke wa rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
akasimama na kuelekea mbele
akapewa kipaza sauti.
“ Waheshimiwa wageni
waalikwa mabibi na
mabwana,nimesimama mbele
yenu tena kutokana na kuguswa
na maneno mazito aliyoyasema binti yetu Patricia.Ni maneno
yenye ukweli na ametukumbusha
wajibu wetu sisi kama wazazi,
ambao wengi wetu
tumeusahau.Napenda kuchukua
nafasi hii kumpongeza kwa namna
ya pekee kabisa Patricia kwa
ufaulu wake mzuri.Ameonyesha
njia na kuwa mfano wa kuigwa na
wengine hasa watoto wa
kike.Ninampongeza kwa namna ya
pekee pia kwa sababu amepitia
changamoto nyingi sana katika
maisha yake hadi hapa
alipofika,changamoto ambazo
zingepelekea yeye ashawishike
kuingia katika mambo yasiyofaa
na kumuharibia kabisa muelekeo
mzima wa maisha yake lakini yeye
hakuanguka na alielekeza akili
yake katika kitu kimoja tu
,kusoma.Watoto wengi wa kike hushawishika kuingia katika
mambo yasiyofaa kutokana na
changamoto mbali mbali
wanazokutana nazo katika maisha
yao ya kila siku na wakati
mwingine ni tamaa tu ya kutaka
kuishi maisha yasiyolingana na
uwezo wao .
“Binafsi nimeguswa sana na
historia ya Patricia na kuanzia
sasa ninatangaza kwamba
nitagharamia mimi gharama zote
za masomo yake hadi
atakaposema imetosha.”
Makofi mengi na vigere gere
vikapigwa halafu akaendelea
“Mama yake Patricia ni mama
wa mfano.Ametufundisha namna
bora ya kulea watoto wetu.Pamoja
na changamoto kubwa ya kipato
inayomkabili ,ameweza kufahamu
umuhimu wa elimu kwa mtoto wake na akaelekeza nguvu zake
zote katika kuhakikisha kwamba
mwanae anasoma.Hongera sana
mama Patricia na ninakuomba
kokote ulipo sogea hapa mbele.
Tafadhali”
Mama yake Patricia
akasimama na kuanza kusogea
mbele huku akishangiliwa kwa
nguvu.Akakumbatiana na mke wa
rais kwa furaha
“ Hongera sana mama
Patricia.Juhudi zako
zimeonekana.Wazazi wote natumai
wataiga mfano wako na kuwekeza
kila walichonacho katika elimu ya
watoto wao.” Akasema Bi
Bernadetha huku akimpa mkono
wa pongezi mama Patricia halafu
akaendelea
“ waheshimiwa wageni
waalikwa mabibi na mabwana,mimi pia ni mama na
ninaufahamu ugumu uliopo katika
ulezi wa familia na hasa ukiwa
peke yako.Kwa maana hiyo
ninamuunga mkono mwanamke
mwenzangu kwa kumpatia mtaji
wa biashara wa shilingi milioni
tano ili aachane na kazi ya ufuaji
anayoifanya na afungue biashara
ambayo itamuwezesha kujikimu
yeye na familia yake.” Bi
Bernadetha akashangiliwa kwa
nguvu sana na kelele zilipopungua
akaendelea
“ Najua wengi wenu hapa
mmeguswa kama nilivyoguwa
mimi kwa hiyo kama nawe
unajisikia kumsaidia chochote
mama Patricia unakaribishwa
kufanya hivyo.Pita hapa mbele
umpongeze mama huyu ambaye
ninaweza kumuita ni jasiri” Kauli ile ya mama Bernadetha
ilikuwa ni kama imewasha moto
kwa waheshimiwa wabunge kwani
ndani ya dakika chache Patricia
na mama yake walikuwa wanaoga
pesa.Elvis na Juliana walikuwa na
kazi ya kukusanya fedha
walizotunzwa Patricia na mama
yake.
Baada ya zoezi lile kumalizika
mama Patrcia akapewa kipaza
sauti ili aweze kutoa neno la
shukrani kwa niaba ya wazazi
wote
“ Sina maneno mengi ya
kusema ila ninaomba nimshukuru
sana mama Bernadetha Jumbo
kwa moyo wake wa huruma na
kwa msaada wake mkubwa
kwangu.Kwa kweli changamoto ni
nyingi sana ukiwa kama mzazi
mmoja na kubeba majukumu yote ya ulezi peke yako lakini
namshukuru Mungu nimeweza
kuvuka vikwazo vyote na
mwanangu ameweza kusoma japo
kwa shida.Naomba nikiri kwenu
kwamba haikuwa kazi rahisi lakini
kwa kuwa ninaamini kwamba
elimu ndiyo urithi pekee
ninaoweza kumpatia mwanangu
basi nilijifunga mkanda
kuhakikisha kwamba mwanangu
anasoma.Kuna nyakati ilinilazimu
kusoma pamoja naye japokuwa
nilikuwa nafunua tu vitabu na
kutazama picha bila kuelewa
chochote”
Watu wote ukumbini
wakaangua kicheko
“ Nawasihi wazazi wenzangu
wote mlioko hapa na wale walioko
majumbani,tujenge urafiki na
watoto wetu na tuwe nao karibu katika kuwapa msaada
wanaouhitaji kila mara.Tuwasaidie
hawa watoto hasa wa kike ambao
wanakabiliwa na vishawishi vingi
sana.Mwisho napenda
kuwashukuru nyote kwa
michango yenu wote.Mungu
awabariki sana” akasema mama
Patricia na kwa mara nyingine
tena akashikana mkono na mke
wa rais halafu akarejea kukaa
mahala pake akifuatana na
Juliana aliyekuwa amebeba pochi
lililojaa fedha.
Zoezi lililofuata lilikuwa ni
burudani toka katika kikundi cha
sanaa za ngoma za asili.
“ Hongera sana Patricia
ulifanya vizuri..Usiku wa leo
umedhihirisha kwamba unastahili
kuwa namba moja..” akasema
Elvis wakati burudani ya ngoma ikiendelea.Patricia akatabasamu
na kusema
“ Ahsante sana
Elvis.Ulinisaidia sana kuniondolea
uoga” akasema Patricia.
“ Usijali Patricia .Ni jambo la
kawaida kuwa na uoga
unaposimama mbele ya hadhira
kubwa kama hii.Pamoja na uoga
wote uliokuwa nao lakini umeweza
kuongea maneno mazito
yaliyomgusa kila mmoja na hata
mimi niliguswa
pia.Umenikumbusha baba yangu
alikuwa ni rafiki yangu
mkubwa.Ilikuwa ni ndoto yake
siku moja nifike mbali sana
kielimu.”akasema Elvis
“ Alikuwa ?! ..Patricia
akashangaa Ndiyo.Baba yangu alifariki
mwaka juzi.Mimi na wewe sote
tumebakiwa na mzazi mmoja tu”
“ Dah ! pole sana Elvis”
“ Ahsante.Pole nawe” akasema
Elvis halafu kimya kikapita
“ Patricia unaishi wapi kwa
sasa? Akauliza Elvis
“ Naishi Kimara Baruti Dar es
salaam.Wewe unatokea wapi?
“ Mimi natokea Arusha
.Ninaishi Njiro.Karibu sana
Arusha uje utembee siku
moja.Karibu uje utembelee mbuga
za wanyama na vivutio mbali
mbali vya kitalii” akasema Elvis na
kumfanya Patricia atabasamu
“Nitakuja kutembea siku
moja.Natamani sana kufika
Arusha”
“ Ukija nitakuwa mwenyeji
wako” akasema Elvis Ahsante ila naomba nikupe
tahadhari mapema kwamba
sintakuwa na hela ya kukulipa
kama muongozaji watalii”
Elvis akacheka sana na kusema
“ Sintakutoza fedha nyingi
kwa kuwa wewe ni mtalii wa
ndani.Tuna nyumba Dar es
salaam Mbezi,na mimi siku moja
nitakuja Dar na wewe utakuwa
mwenyeji wangu”
“ Usijali kuhusu
hilo.Nimezaliwa na kukulia Dar
kwa hiyo ninalifahamu vyema jiji”
akasema Patricia.
Baada ya burudani ya ngoma
za asili kumalizika mheshimiwa
waziri mkuu akafungua muziki na
watu wote wakajumuika ukumbini
kulisakata rhumba.
“ wakati wa muziki sasa.Can
we dance? Akauliza Elvis.Patricia alionekana kuogopa na kuona
aibu.Wanafunzi wenzao walikuwa
wanainuka na kujumuika na
wabunge katika kuusakata muziki
“Ninaogopa sijawahi kucheza
hata mara moja.” Akasema
Patricia
Wakati Elvis akimuomba
Patricia waende wakacheze muziki
mara akatokea mama yake akiwa
ameongozana na ndugu wengine
watano.
“ Elvis sherehe imemalizika.Ni
wakati wa kuodnoka
sasa.Tunatakiwa tupumzike kwani
kesho tuna safari ndefu ya kurejea
Arusha.Sitaki kuendesha gari
nikiwa nimechoka. Akasema
mama Elvis
“ Mama kabla ya yote kutana
na Patricia.Yeye ndiye
aliyetuongoza wote na kushika namba moja.Ni rafiki yangu wa
kwanza kukutanana naye ambaye
nitakuwa naye pale J.Y.Makamba
school of science.” Elvis
akamtambulisha Patricia kwa
mama yake
“Patricia huyu ni mama yangu
anaitwa Mrs Tarimo na hawa
wengine ni ndugu zangu
walionisindikiza kwa ajili ya
sherehe hii”
Patricia akainuka na kwa
adabu akamsalimu mama Elvis.
“ Shikamoo mama”
“ Marahaba Patricia.Nafurahi
kukutana nawe.Hongera sana kwa
kufanya vizuri”
“ Ahsante sana mama.Hata
mimi nafurahi kukutana
nawe.Hongera pia kwa Elvis kwani
naye amefanya vizuri sana” Amejitahidi ameshika
namba nane.Nilitegemea labda
angekuwepo katika nafasi tatu
bora.Kwa kuwa mtakuwa wote
shule moja naomba umkazanie
sana mwenzio aongeze juhudi na
kidato cha sita nyote muwe katika
nafasi tatu za juu” akasema mama
Elvis.
Usihofu mama.Kidato cha sita
Patricia hatanishinda
tena.Nitamshusha toka namba
moja” akasema Elvis na wote
wakacheka
“ Patricia unaishi wapi?
“ Mimi natokea Dar es
salaam”
“ Ouh vizuri sana.Sisi
tunaishi Arusha japokuwa hata
Dare s salaam tuna nyumba
pia.Karibu sana Arusha
ututembelee siku moja” Ahsante sana mama.Tayari
Elvis ameshanialika nije Arusha
siku moja na nitakuja pale
nipatapo nafasi”
“Ouh kumbe
ameshakukaribisha.Huyu naye
huwa hachelewi.Haya ukipata
nafasi tafadhali njoo ututembelee”
“ Ahsante sana mama
nitakuja siku moja”
“ Haya Patricia sisi
tunaondoka,tunatakiwa
tukapumzike kesho asubuhi tuna
safari ya kurejea
Arusha.Nakutakia safari njema ya
kurejea Dar es salaam”
“ Nashukuru sana
mama.Nami nawatakia safari
njema ya kurejea Arusha”
akasema Patricia.
“ Mama tangulieni katika gari
nitakuja baada ya muda mfupi.Nataka kuagana na Patricia
“ akasema Elvis na mama yake
huku akitabasamu akaondoka
kuelekea garini
“ Mama yako mcheshi sana”
akasema Patricia
“ Usimuone akiongea kwa
upole namna ile.Ni mkali sana
akiwa nyumbani.Tuachane na
hayo,Patricia nashukuru sana
kukutana nawe .Kwa kuwa sote
tunakwenda kuendela na masomo
katika shule moja,nina imani
tutazidi kuwa marafiki sana.”
“ Hata mimi nafurahi sana
kukutana nawe Elvis.” Akasema
Patricia
“Patricia najua hatutaonana
tena hadi tutakapokutana
shuleni.Unaweza ukanipa namba
yako ya simu ili mara moja moja niwe nikikupigia simu na
kukujulia hali”
Patricia akatabasamu na
kusema
“ Sina simu Elvis”
“ Huna simu?!....Elvis
akashangaa
“ Ndiyo sina simu” akajibu
Patricia.
“ C’mon Patricia ina maana
hufanyi mawasiliano?
“Nikitaka kuwasiliana na mtu
hutumia simu ya mama”
“Ok..! Ok ! ..Nipe basi namba
ya simu ya mama”
“ Hapana Elvis.Nipe wewe
namba zako na nitakupigia simu
mimi nikipata nafasi.”
Elvis akaandika namba zake
za simu na kumpatia Patricia
halafu wakaagana na
kuondoka.Watu bado waliendelea kujimwaga ukumbini wakilisakata
rhumba.Patricia akamfuata mama
yake aliyekuwa amesimama na
kundi la wabunge wanawake
wakimpongeza
Sherehe zilipomalizika
Patricia na mama yake
wakarejeshwa hotelini
“Dah ! ilikuwa ni siku ndefu
sana” akasema mama Patricia.
“ Ilikuwa siku ndefu lakini
nzuri.Mama nimefurahi sana
leo.Hii ni siku kubwa katika
maisha yangu” akasema Patricia
“ Hata mimi nimefurahi
sana.Unajua pale ulipoitwa uende
mbele kuongea neno la shukrani
nilistuka sana kwani nilijua
hujajiandaa kitu cha kuongea
lakini Juliana alinitoa wasi wasi
na kuniambia nisihofu.Ulipoanza
kuongea kijasho kilikuwa
kinanitoka lakini mwishowe
nilijikuta nikitoa machozi.Patricia Mungu amekujalia akili ya kipekee
kabisa.Ahsante sana kwa maneno
yale mazito ambayo yalichoma
mioyo ya kila mmoja pale
ukumbini.Ni kwa maneno yale
mazito tumefanikiwa kupata kiasi
hiki cha fedha.Bado siamini
macho yangu.” Akasema mama
Patricia na kulifungua pochi lake
kubwa na kumwaga pesa
kitandani.
“ Wow ! ..Patricia
akatabasamu
“ Patricia tunapaswa
kumshukuru sana Mungu kwa
muujiza huu mkubwa.Jana
tulikuwa hatuna hata fedha ya
kununua sukari lakini leo hii tuna
fedha hizi nyingi.Ouh Mungu
ahsante sana kwa jambo hili
kubwa” akasema mama Patricia
na kuanza kuzihesabu fedha
zile..Jumla zilikuwa ni shilingi
million mbili laki saba na sabini.Bi
Doroth hakuamini macho yake.Machozi ya furaha
yakamtoka.Akakumbatiana na
mwanae
“ Basi usilie mama.Ni wakati
wetu wa kufurahi na kumshukuru
Mungu kwani maisha yetu
yanaanza kuonyesha nuru.Pesa
hizi na zile alizokuahidi mama
Bernadetha zinatosha sana
kuanzisha mradi wowote ambao
utatuwezesha kujikimu na
kututoa katika lindi hili la
umasikini mkubwa” akasema
Patricia
“ Patricia mwanangu lazima
nilie kwa sababu nikikumbuka
taabu nilizozipata katika
kukusomesha.Mungu pekee ndiye
anayejua.Ninawashukuru wote
waliotuchangia fedha hizi ambazo
ni nyingi na zinatosha kabisa
kuanzisha bashara.Tunatakiwa
tukae na tubuni biashara ya
kufanya.Mimi nina wazo
moja.Siku ya jumatano
 
I DIED TO SAVE MY PRESDANT

Mtunzi Patrick Ck

Simu 0764294499

Sehemu 4


nitakapokwenda kuonana na
Mama Bernadetha katika taasisi
yake kama
alivyonitaka,nitamuomba anisaidie
nipate walau shamba au kiwanja
ili niweze kuanzsha mradi wa
ufugaji kuku.Unaonaje kuhusu
wazo hili?
“ Hilo ni wazo zuri sana mama
lakini nina imani utakapoonana
naye na kumweleza hali yako ,yeye
mwenyewe anaweza akatafuta njia
bora zaidi ya kukusaidia” akasema
Patricia huku akiuvua mkufu wa
dhahabu na mara akamkumbuka
Juliana
“ Dada Juliana amefanya
kazi kubwa sana na amenifanya
nipendeze na kusifiwa na kila mtu
leo ” akasema
“ Ni kweli Patricia.Tunapaswa
kumshukuru mno Juliana kwa
wema wake kwetu.Amesafiri toka
Dar es salaam hadi huku Dodoma
kuja kuungana nasi.Ana moyo wa huruma sana Yule binti.” Akasema
mama Patricia halafu akanyamaza
kana kwamba kuna kitu
anakikumbuka,akauliza
“ Patricia Yule kijana
aliyekusindikiza pale mbele
ulipokwenda kutoa shukrani
,mnafahamiana?
Swali lile likamstua kidogo
Patricia
“ Unasema Elvis?
“ Simfahamu kwa jina
.Umesema anaitwa Elvis?
“ Ndiyo mama anaitwa
Elvis.Nimefahamiana naye pale
pale katika sherehe.Yeye ameshika
namba nane na anatokea
Arusha.Kitu ingine ni kwamba
wote tumechaguliwa kuendelea na
kidato cha tano katika shule
moja.Kuna tatizo lolote mama?
“ Hapana hakuna tatizo
lakini kama unavyofahamu
kwamba sitaki ulewe sifa na
kubadilika.Safari yako ndiyokwanza imeanza.Masuala ya
vijana mimi sitaki kuyasikia.Kama
ni urafiki uwe ni wa kusaidiana
katika masomo tu na si
vingnevyo.Nitakuwa mkali sana
katika hilo na ninakuomba
usinione mbaya.Nataka ufahamu
kwamba utakapokwenda huko
shuleni utakuwa peke
yako.Hautakuwa na mimi
tena.Kwa hiyo zingatia yale yote
ambayo nimekuwa nikikuelekeza
japokuwa una uwezo wa kufanya
maamuzi yako mwenyewe kwa
sababu wewe ni binti mkubwa
sasa na unafahamu jema na
bayaa.Unazifahamu ndoto zako
kwa hiyo pambana ili kuzitimiza.”
Akasema mama Patricia.Patricia
akatabasamu na kumsogelea
mama yake.
“ Mama usiwe na hofu na
mimi hata kidogo.Ninajitambua
mimi ni nani na malengo yangu ni
nini kwa hiyo nakuomba usiwe na wasi wasi hata
kidogo.Sintakuangusha mama
yangu.Naomba uniamini” Patricia
akasisitiza
“ Nakuamini Patricia lakini
lazima nikukumbushe mara kwa
mara kwamba kwa sasa wewe ni
binti mkubwa na unazidi kuwa
mrembo.Urembo wako ni kama ua
lenye harufu nzuri ambalo huvutia
nyuki wengi kulifuata.Urembo
wako ukichanganya na jina
ambalo umelipata hivi sasa ni
vichocheo tosha kabisa
kuwafanya wanaume wengi ,vijana
kwa wazee kuanza kukuzengea na
katika umri huu mwili nao
hukumbana na vichocheo na
vishawishi vingi.Wasichana wengi
huanguka vishawishini katika
kipindi hiki. Patricia
mwanangu,umeweza kujilinda kwa
miaka minne na nina imani
utaweza pia kwa hiyo miaka miwili
na mingine mingi utakayokuwa masomoni.Kamwe usikubali
kuanguka vishawishini.Mapenzi
yapo na utaondoka
utayaacha.Tengeneza kwanza
maisha yako na mambo mengine
yatafuata baadae.Naomba
usiyasahau maneno haya ambayo
ni kwa faida yako wewe
mwenyewe” akasema Bi Doroth
“ Mama siwezi kuyasahau.Siku
zote maneno yako yamekuwa ni
dira na ngao
yangu.Nakuhakikishia mama
kwamba siwezi kuanguka na
nitamuweka Mungu mbele siku
zote.Usichoke kuniombea”
“ Mimi nitakuombea bila
kuchoka lakini hata wewe pia
unatakiwa usimame imara katika
maombi”
Ulikuwa ni usiku mrefu sana
kwa Bi Bernadetha na binti
yake.Waliongea mambo mengi
sana kuhusiana na maisha
yao.Walikumbushana mambomengi kuhusu waliyoyapitia katika
maishayao na ilipotimu saa tisa za
usiku wakalala.
**********************
Siku sita zimekwisha pita toka
Patricia arejee toke
Dodoma.Maisha yao yalianza
kuwa na mabadiliko.Tayari Bi
Doroth amekwisha onana na mke
wa rais na akampatia kiasi cha
fedha alichomuahidi.Mke wa rais
pia alikwenda mbali zaidi na
kuahidi kumpatia kiwanja ili
aweze kujenga nyumba walau
nyumba ndogo ya kushi yeye na
mwanae Patricia pamoja na
kufanya kazi ya ufugaji kama
alivyokuwa amepanga.Mwanga
ulianza kuonekana katika maisha
yao
Ni siku ya Ijumaa saa nne
asubuhi mrembo Juliana
akawasili nyumbani kwa akina Patricia.Akashuka toka ndani ya
gari lake aina ya Mercedece Benz
jeusi na kuwasalimu akina mama
waliokuwa kibarazani wakiendelea
na shughuli za usafi halafu
akanyoosha hadi katika chumba
cha akina Patricia akagonga na
mama Patricia ndiye aliyefungua
mlango
“ Ouh ! Juliana ! Karibu sana”
akasema Bi Doroth
“ Ahsante sana
mama.Shikamoo” akajibu Juliana
“ Marahaba Juliana.karibu
sana.Karibu ndani” akasema
mama Patricia huku akiweka vitu
vizuri ili Juliana aweze kupita
“ Karibu sana Juliana.Habari za
toka majuzi?
Habari nzuri mama .Habari za
hapa?
“ habari za hapa nzuri.Sijui
huko kwenu”
“ Kwetu kwema mama.Vipi
Patricia hajambo? Hajambo ,nimetuma hapo
dukani atarejea muda si mrefu”
“ Mama leo ndiyo ile siku
niliyokuwa nimeamuandalia
Patricia ile sherehe ndogo ya
kumpongeza nyumbani
kwetu.Watakuwepo marafiki
wachache tutakaojumuika
pamoja” akasema Juliana
“ Juliana ahsante sana lakinu
utanisamehe kwani sintaweza
kuhudhuria.Hivi unavyoniona
nina miadi ya kuonana na mama
Imelda Kulangwa ambaye
ameelekezwa na mke wa rais
aende akanionyeshe kiwanja
alichoninunulia.Utakwenda na
Patricia”
Patricia akatabasamu na
kusema
“ Ouh hizo taarifa njema sana
mama.Kama umepata kiwanja
tutasaidiana masuala ya
ujenzi.Nina rafiki yangu mmoja
ana duka la vifaa vya ujenzi tutamtumia huyo kupata vifaa vya
ujenzi”
“ ahsante sana Juliana” akajibu
Bi Doroth na mara mlango
ukafunguliwa Patricia akaingia
“ wow ! Dada Juliana” akasema
kwa furaha na kumkumbatia
Juliana
“ Karibu sana dada Juliana”
akasema Patricia
“ Ahsante sana Patricia” akajibu
Juliana halafu akamfahamisha
Patricia kwamba amekuja
kumchukua ili aende akashinde
nyumbani kwao ambako
kuliandaliwa sherehe ndogo ya
kumpongeza.Patricia alijiandaa
haraka haraka halafu akapanda
katika gari la Juliana
wakaondoka.Breki ya kwanza
ilikuwa Sabina beauty saloon
ambako Patricia alirembwa
“ Wow ! Patricia you are so
beautifu.You are amazing”
akasema Juliana baada ya Patricia kumaliza kurembwa.Toka hapo
walielekea katika maduka ya nguo
na urembo ambako Juliana
alimnunulia Patricia vitu mbali
mbali halafu wakaelekea
nyumbani kwa akina Juliana
Geti kubwa jeusi lilifunguliwa
wakaingia katika jumba kubwa
lenye rangi nyeupe.Patricia
akatabasamu kwa uzuri wa jumba
lile.
“ Patricia hapa ndipo
ninapoishi.Kwa sasa ninaishi
mimi, mdogo wangu Godson
pamoja na binamu zetu
wawli.Baba mama na mdogo wetu
wa mwisho wanaishi nchini Afrika
kusini ambako baba nafanya kazi
katika shirika moja la kimataifa.”
Akasema Juliana kabla ya
kushuka garini
“ Nafurahi kupafahamu
nyumbani kwenu dada Juliana.Ni
nyumba nzuri sana nimeipenda”
akasema PatriciaLaiti mama angeweza
kukubali ningekuchukua tukaishi
wote hapa kwetu lakini mama
katu hawezi kukuachia” akasema
Juliana huku akicheka halafu
wakashuka na kwa kupitia mlango
wa nyuma wakaingia ndani na
moja kwa moja wakaelekea
chumbani kwa Juliana.Patricia
akapatwa na mshangao baada ya
kuingia katika chumba kile
kikubwa na kizuri.
“ Patricia hiki ni chumba
changu cha kulala.Nimekuleta
huku moja kwa moja ili mtu
yeyote asikuone kabla ya sherehe
kuanza.” Akasema Juliana huku
akitabasamu
“ Dada Juliana una chumba
kizuri mno.Sijawahi kuingia katika
chumba kikubwa na kizuri kama
hiki katika maisha yangu”
“ Usijali Patricia.Hivi ni vitu vya
kawaida tu na utakapovizoea
utaviona ni vya kawaida .Kwa sasa usiwaze kuhusu maisha kama
haya.Una kazi ngumu ya kusoma”
akasema Juliana halafu
akafungua kabati kubwa la nguo
na kuanza kumchagulia Patricia
nguo nzuri itakayompendeza kwa
jioni ya siku ile.Alimchagulia suti
nzuri nyeupe na kumpa aijaribu
Patricia hakuna nguo
utakayoiweka mwili mwako
isikupendeze.Kama isingekuwa
bado ni mwanafunzi
ningekushauri uingie katika
ulimwengu wa mitindo.Una umbo
la kiuanamitindo na nina hakika
ungeweza kufika mbali sana lakini
usiwaze mambo kama haya kwa
sasa.Elekeza akili yako katika
masomo” akasema Juliana halafu
akamuacha Patricia mle chumbani
akaenda kuungana na rafikize
katika kuandaa sherehe ile ndogo
ya kumpongeza Patricia.Bado
maandalizi yalikuwa
yanaendelea.Wengine walikuwa jikoni wakiendelea kupika na
wengine walikuwa bustanini
wakipamba sehemu
itakapofanyikia sherehe
“ Wakati pilika pilika zikiendelea
huko nje, Patricia yeye alikuwa
chumbani kwa Juliana akiendelea
kutazama filamu.Wakati
akiendelea kuifurahia filamu ile
nzuri mara mlango ukafunguliwa
taratibu.Patricia alidhani ni
Juliana ndiye aliyeufungua
mlango ule lakini ghafla akapatwa
na mshangao alipoelekeza macho
yake mlangoni.Kijana mmoja
mweupe mwenye sura nzuri na
aliyefanana sana na Juliana
alikuwa amesimama
akitabasamu.Walitazamana kwa
sekunde kadhaa Patricia
akaingiwa na woga.Kijana yule
akaanza kupiga hatua taratibu
kumuendea Patricia.
“ helo Patricia” akasema Yule
kijana huku akinyoosha mkono wake na kumsalimu Patricia
ambaye alipatwa na uoga
mkubwa.Alimtazama kijana Yule
mwenye sura nzuri aliyekuwa
akitabasamu naye akajilazimisha
kutabasamu na kunyoosha mkono
akasalimiana na Yule kijana
“ I’m Godson” akasema kijana
Yule halafu akakaa katika sofa
lililoelekeana na lile alilokaa
Patricia
“ Tafadhali usiogope Patricia
Juliana hawezi kuja sasa
hivi.Nimemsikia akiwaambia
wenzake kwamba uko huku
chumbani kwake amekuficha na
kwa kuwa nilikuwa na hamu ya
kukuona nikaona ninyate ili nije
nikusalimie.Nimefurahi sana
kukuona na kukufahamu”
akasema Godson
“ dada Juliana aliniambia ana
mdogo wake anaitwa Godson ndiye
wewe? Akauliza Patricia.
“Ndiye mimi” akajibu Godson. Nimefurahi kukuona
Godson.Umefanana sana na
Juliana.Nilipokuona tu nilijua
lazima utakuwa ndugu yake”
akasema Patricia na kumfanya
Godson atabasamu.Kimya kifupi
kikapita .Patricia akaendelea
kumtupia jicho la wizi Godson
akimchunguza.Alikuwa ni kijana
mwenye sura nzuri sana na ya
kuvutia sana.Alikuwa na mwili
uliojengeka vyema.Fulana ile
aliyovaa iliyokatwa mikono
ilionyesha michoro aliyojichora
katika mabega yake.Kwa ujumla
alikuwa ni kijana mwenye kuvutia
mno ambaye kila binti angetamani
kuwa naye.Kwa mara ya kwanza
katika maisha yake Patricia
akajikuta akisisimka mwili
“ Patricia ! ..akaita Godson na
kumstua Patricia
“ Juliana ameniambia kwamba
umeshika namba moja katikamatokeo ya mtihani wa kidato cha
nne”
“ Ndiyo Godson” akajibu Patricia
“ Hongera sana
Patricia.Unastahili pongezi”
“ Ahsante sana
Godson.Namshukuru sana Mungu
kwa hilo”
“ By the way,umekwisha
pangiwa ni shule gani unakwenda
kuendelea na kidato cha tano?
“ Ndiyo.Nimechaguliwa
kuendelea na kidato cha tano na
sita katika shule ya J.Y.Makamba
school of science iliyoko Bumbuli
Tanga.Ni shule mpya kabisa na
nzuri.”
“Safi sana kama umechagua
mchepuo wa sayansi.Katika dunia
ya sasa sayansi ndiyo
inayoongoza.Hata mimi napenda
sana masomo ya sayansi
.Unafikiria kuwa nani huko
mbeleni? Napenda niwe daktari” akajibu
Patricia
“ That’s great.Mimi pia nilisoma
shule ya sayansi lakini nimejikita
zaidi katika teknolojia ya
kompyuta.”
“ Ouh safi sana.Hata mimi nina
hamu sana ya kujua kompyuta “
“ Katika shule uliyosoma
hakukuwa na somo la kompyuta?
“ Somo la kompyuta lilikuwepo
lakini hakukuwa na kompyuta
hata moja shuleni kwa hiyo
ilikuwa vigumu
kuelewa.Nafahamu kuna vitu
vinaitwa keyboard,monitor lakini
sijawahi kuvitumia
“ Uko tayari nikufundishe
kompyuta walau kwa siku hizi
chache kabla ya kwenda shuleni?
Nina hakika itakusaidia sana
katika masomo yako.”
“ Niko tayari Elvis.Natamani
sana kujua kompyuta” Basi usihofu kuhusu
hilo.Nitakufundisha katika kipindi
hiki kifupi kabla ya kuelekea
shuleni.” Akasema Godson na
mara mlango ukafunguliwa
akaingia Juliana.Alishikwa na
mshangapo mkubwa baada ya
kumkuta Godson mle chumbani
“ Godson !!!!!..akasema Juliana
“Nini kimekuleta chumbani
kwangu?Please get out of here
now” akafoka Juliana.
Huku akitabasamu Godson
akainuka na kumsogelea dada
yake.
“ Calm down big sister.Nilikuja
kumsalimu Patricia.Nimeshindwa
kuvumilia hadi jioni” akasema
Godson.
“ Ok go out now” akasema
Juliana na Godson akageuka na
kumtazama Patricia
“ Bye Patricia.See you later”
akasema Godson na kutoka mle
chumbani. sorry Patricia.Huyu mdogo
wangu ni mtundu
sana.Hajakwambia neno lolote la
kukukwaza?
“ Hapana dada
Juliana.Hajanitamkia neno lolote
baya.Alitaka kunisalimu tu na
tulikuwa tukiongea mambo ya
kawaida ya masomo.Godson ni
mcheshi sana” akasema Patricia
“ Sikutaka mtu yeyote akuone
kabla ya muda haujawadia.I
wanted to surprise them.Lakini
huyu Godson kajipenyeza mpaka
amekuja kukuona.” Akasema
Juliana na kumfanya Patricia
acheke kidogo
“ Dada Juliana ,Godson
ameniambia kwamba yuko tayari
kunifundisha kompyuta” akasema
Patricia na kumstua Juliana
“ Godson anataka kukufundisha
kompyuta?
“ Ndiyo dada JulianaAmesema atakufundishia wapi
na lini?
“ Bado hajasema ni lini na
wapi.Mbona umestuka hivyo dada
Juliana? Hana uwezo wa
kunifundisha? Akauliza Patricia
Juliana akavuta pumzi ndefu na
kusema
“ Godson amesoma kompyuta
na anaifahamu vyema .Ni hivi
majuzi tu amerejea toka nchini
Marekani alikokuwa akisomea
sayansi ya kompyuta.” Akasema
Juliana na kumtazama Patricia .
“ Are you sure you want to learn
computer? Akauliza Juliana.Huku
akitabasamu Patricia akajibu
“ Ndiyo dada Juliana”
“ Ok hakuna shida .Nitaongea
naye ili tuone namna
tutakavyoweza kufanya kuhusu
somo hilo lakini kabla ya yote
lazima mama akubali” Mama hatakuwa na shida
,mara zote huwa hana shida
linapokuja suala la masomo.”
“ Nitaongea naye jioni ya leo
nitakapokurudisha” akasema
Juliana
Ilikuwa ni siku nzuri sana na ya
kupendeza kwa Patricia na kwa
wote waliohudhuria sherehe ile
ndogo ya kumpongeza .Chakula
kitamu kiliandaliwa na vinywaji
vya kila aina vilikuwepo
Ilipotimu saa mbili za usiku
Juliana akamuomba Patricia
ajiandae ili aweze kumrejesha
kwao.Patricia akaagana na wote
waliohudhuria sherehe ile
,akawashukuru kwa kufika kwao
na kwa zawadi walizomzawadia
halafu akaingia garini yeye
Patricia na Godson ambaye
aliomba akapafahamu nyumbani
kwa akina Patricia
Waliwasili nyubani kwa akina
Patricia lakini mama yake bado alikuwa hajarejea.Juliana na
Godson hawakukaa sana
wakaondoka huku Juliana
akiahidi kuongea na mama yake
Patricia simuni kuhusu suala la
mafunzo ya kompyuta
“ Ilikuwa ni siku nzuri sana
kwangu kiasi kwamba ninaiona
kama imekuwa fupi mno.Sijui
nitamlipa nini dada Juliana kwa
wema wake huu
mkubwa.Ametokea kunipenda
sana na kunijali kama ndugu yake
wa damu.Ana roho nzuri sana ya
upendo na ndiyo aana
anafanikiwa.” Akawaza Patricia na
mara picha ya chumba kikubwa
cha Juliana ikamjia kichwani
akatabasamu
“ Nimekipenda sana chumba
cha Juliana.Kina kila kitu
ambacho mwanamke
anakihitaji.Natamani siku moja na
mimi niishi maisha kama yale ya
Juliana lakini yote haya yatawezekana tu kama nitaongeza
juhudi katika masomo.Familia
yangu ni masikini na haina uwezo
wa kunifanya niishi maisha kama
yale ya Juliana.Kitu pekee
kitakachonifanya niishi maisha
kama yale ni elimu..” akawaza
Patricia huku akiendelea
kufungua zawadi alizopewa picha
ya Godson ikamjia kichwani
“ What a handsome guy.Kusema
kweli sijawahi kuona kijana wenye
sura nzuri kama Godson.Uzuri
wake hata mimi umenigusa.Ana
sura nzuri,mwili laini na na hata
tabia yake inaonekana ni nzuri
japokuwa Juliana alisema
kwamba ni mtndu.Alikuwa
akiongea nami kwa lugha
laini.he’s so sweet” akawaza
Patricia huku akitabasamu na
kuendelea kuzifungua zawadi zake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom