Riwaya: Code x 3

Riwaya: Code x 3

Riwaya gani nyingine iko jikoni madamS?
 
RIWAYA: CODE X 3:
THE REAL ME
MTUNZI: Tariq Haji

SEHEMU YA 15

"Muheshimwa raisi tutahitaji msaada wako" Alex aliongea na kumsogelea kisha akamnong'oneza kitu sikioni. Raisi alitabasamu na kuashiria amemuelewa, "basi hakuna shida wacha mimi niondoke niwaache muendelee na majukumu mengine" Raisi aliongea na kusimama kisha akaondoka. Waliendelea kupanda mipango yao kwa makini sana, walifanya hivo kuhakikisha hatoki mtu hata mmoja kati ya waasi.
Mipango ilipokamilika Alex aliondoka na kikosi chake, walikuwa wamejipanga kisawa sawa. kila mtu alibeba ile silaha ambayo aliamini ni rafiki yake mkubwa. Walipanda ndege na safari ikaanza, kila mtu kwenye ndege alisali anavyojua yeye. "baada ya vita hii,kutakuwa na mambo mazuri sana" aliongea Alex huku akicheka na kuwafanya wenzake wote kumuangalia kwa sintofahamu.
Ndege ilifika karibu na eneo la waasi kushuka usawa wa bahari, Alex na kikosi chake waliruka na kuingia kwenye maji. Waliogelea mpaka nchi kavu, "tutasubiri kikosi cha Jeff na Darling kifike" aliongea Alex na kila mmoja akatafuta kicha cha kujificha. Nusu saa baadae waliibuka watu kadhaa kutoka maji, walianza kutembea taratibu mpka juu kabisa kwenye mchanga. Mmoja wao aliweka silha chini na kuinyanyua mara tatu, Alex alitoka na kikosi chake. "nimefurahi kukuona tena Allen jr" Alex aliongea baada kumuona Christine, "Jeff nashkuru kwa kufika" aliongea tena na kumpa mkono Jeff ambae aliupokea kwa tabasamu.
"tunaanzia wapi?" aliuliza Jeff, "tusubiri kama dakika kumi hivi" tutapata pa kuanzia. Alex aliongea na wote wakatoa ishara ya kuelewa. Walianza kuongea utasema hawako hatarini, baada ya dakika kumi zilipita ndege kadhaa zinazojulikana kwa jina la DRONE au ndege isio na rubani. Zilianza kushambulia kambi ndogo ndogo zote ambazo zimezunguka kambi kubwa. "natumai tushapata pakuanzia" Alex aliongea na kushika mtutu wake vizuri.
Kazi ilianza huku wakijitahidi kuwaondoa wale walibahatika kupona mavamizi ya ndege zile zisizo na rubani. Walipohakikisha wamesafisha njia, Alex alitoa radio na kuongea "miba yote imeendoka", "rodger" alijibiwa upande wa pili. Vilianza kutoka vifaru kwenye maji pamoja na jambizi amabzp zilishusha magari na vifa vingine vya kivita. Walifika mpaka walipo kina Alex na Jeff, "kazi nzuri kijana" aliongea general Griffin. Waliingia kwenye gari na safari ikaanza, sasa walikuwa wamebakiwa na kambi kubwa tu.
"mkuu kitumbua kimeingia mchanga" Kamanda Willy alirpoti, wakati huo kulikuwa na kikao kinaendelea. "inavyoonekana Alex amekucheza akili mkuu" aliendelea kuongea Willy, "kivipi" aliuliza General David. "alijua akishambulia kambi ndogo ungeita wakuu wote ili kujadili mstakbali wa dhamira yenu na inaonekana amelenga ndipo" alifafanua Kamanda Willy. "ndio yuko sahihi kabisa" walisikia sauti, "msishtuke sana, kwasababu hivi punde tu tutakutana. Na nasikitika sana kukwambia General David, kosa lako kubwa ulolifanya ni kucheza na familia yangu. Kosa hilo litakugharimu vile inavyostahiki" aliongea Aex kwa sauti nzito na kukata mawasiliano.
"mkuu tumevamiwa" aliingia mwanajeshi mwengine na kuongea, sasa wale wote waiokuwepo katika kikao hicho walianza kuhisi tumbo la kuharisha. "sasa tnafanyaje" aliuliza mzee mmoja alieonekana muoga kidogo. "hapa hakuna la kufanya tumezungukwa na mjeshi ya serekali, mimi niliwaambia tufanye mapema mukaniona mjinga" aliongea General David. "sasa kila mtu hapa atatoka kwa nguvu zake" aliendelea kuongea na alipomaliza aliinuka na kuondoka.
Huko nje moto ulikuwa si wa kitoto, mkali Alex na Jeff na vikosi vyao walikuwa wakitembeza dozi. "Scarlet achana nae huyo kashakufa" Adrian alimwambia Scarlet baada kumuona akimuamsha mwenzake mmoja ambae amepigwa risasi. Mpambano ulizidi kuwa mkali, maana hiyo kambi haikuwa na wanajeshi kidogo. Wakati mpambano unaendelea Scarlet alizembea kidogo na kuna mtu alikuwa kashamlenga mlenga, ghafla General Griffin alipita mbele yake na kukinga kifua. Risasi iliopigwa kwa lengo la kumuua Scarlet ilipenya kifuani mwa General na kuanguka chini. Alipotaka kuongea nae alimpa ishara aendelee kupambanaa.

Huko ufukweni ziliibuka nyambizi nyinngine zikiongozwa na raisi mwenyewe, mambo sasa yalizidi kunoga maana waasi hawakutegemea kama jeshi kubwa kama vile lingekwenda kupambana nao. Jeshi hilo lilokuwa chini ya raisi liliekea uwanjani na kuendeleza mapigano, general David alifanikiwa kufika mpaka kwenye helicopter. "tuondoke haraka" aliongea na hapo aliongezeka mwanajeshi mmoja kwa ajili ya ulinzi na helicopter ikaondoka. Ilipofika kwenye ufukwe ilianza kushuka, "mbona unaishusha hapa" aliuliza. "ulidhani unaweza kututoroka" sauti ya Alex ilisikika kutoka mbele, "general mzima unaacha wanajeshi wako wanakufa wewe unakimbia" sauti ya kike ilisikika pembeni yake na ilikuwa ni ya Agent Darling.
Helicopter ilikanyaga fukwe na papo hapo ikazungukwa na wanajeshi, "wekeni silaha chini" ilikuwa sauti ya raisi. "mheshimiwa raisi mkuu wa waasi huyu hapa" Alex aliongea huku akimshusha general David kwa nguvu. "kazi nzuri kijana" raisi alimpongeza, "Agent Darling nahisi mimi nikuachie wewe huyo mpuuzi, mfanye unavotaka na hakuna atakae kuuliza" Raisi aliongea na kurudi nyuma. Masikini General David alichokutana nacho nahisi atamsimulia Allen huko kwa alipokwenda. Agent Darling alipohakikisha General David hajiwezi tena, alimchapa risasi ya kichwa na kummaliza kabisa.
Vita hiyo ilikwisha na waasi wote waliokamatwa waliuliwa huko huko, lakini hali ya general Griffin ilikuwa mbaya mno. Aliwaita Scarlet na Adrian na kuongea nao kitu kidogo, baada ya hapo raisi alifika "mheshimiwa nasikitika sitokuwepo karibu yako tena na kukusaidia katika kufanikisha malengo yako" aliongea japo kwa tabu kidog. "siku zote utakuwa karibu yangu, najivunia kuwa na General kama wewe katika nchi yangu" aliongea raisi na kumshika General mkono. "una ombi lolote la mwisho kabla hujasafiri safari ya milele" raisi alimuuliza.
"ndio mkuu, naomba Alex aongoze kikosi cha THE PIRATES. Ana mbinu nyingi sana za kivita na uwezo wa kipekee, atasaidia katika kiwango kikubwa sana katika kuimarisha ulinzi wa nchi yetu" aliongea General na kukohoa damu. "kwa mamlaka niliokuwa nayo kama raisi wa nchi hii, Bwana Alex Jr umepandishwa cheo na kuwa General wa nchii hii. Kuanzia sasa utakuwa mkuu wa kikosi cha The Pirates" raisi alimuapisha Alex mbele ya General Griffin ambae alikata roho huku ametabasamu.
Maiti yake ilibebwa a safari ya kurudi ufukweni ikaanza, lakini kabla hajaingia kwenye nyambizi Alex alimnongoneza kitu raisi nae akaonesha kama kukumbuka kitu. "Adrian, Ariella, Jeff na Christine nomba musogee hapa" alitoa amri rais, nao walisogea lakini walikuwa hawajui kitu gani kinaendelea. Ghafla kwenye nyambizi alishuka mchungaji akiwa amembatana na watu kadhaa. Walifungishwa ndoa hapo hapo katika uwanja wa vita, "Alex asante na naomba unisamehe" aliongea Christine na kumkumbatia. "usijali mdogo wangu, Allen alinambia nikulinde mpaka pale utakapopata wa kukulinda mwengine" Alex alimjibu huku akicheka.
Waliigia kwenye nyambizi na safari ya kurudi ikaanza, siku hiyo iliwekwa katika kumbukmbu za nchi hiyo kama siku ya mashujaa. Mazishi yalikamilika huko Adrian na Scarlet wakianza maisha yao nje ya jeshi, Jeff na Christine walielekea Qatar kwa ajili ya kuwasalimu ndugu wa Christine. Alex alirudi katika kambi ya the pirates kwa lengo la kukikuza kikosi hicho na kuwa hatari kuliko wanajeshi wa Project CODE X. Amani ilirejea nchini na hofu ilipotea, na kila mwaka waliadhimisha siku ya mashuja katika nchi hiyo.

UZALENDO NI NGAO PEKEE YA KUIKOMBOA NCHI KUTOKA KATIKA MAJANGA, JIVUNIE KUWA RAIA WA NCHI YAKO MAANA KUWEPO KWA NCHI NDIO KUNATAFSIRI UTAIFA WAKO.
IN GOD WE TRUST

MWISHO.

Inapendeza sana...
Chapter Closed


Cc: mahondaw
 
Shunie acha
Naona marefu refu tu zipo episode ngapi yaan nikute story imeshaanza nguvu zote zinaniisha
shunie acha uvivu. Mimi hadithi ikiwa nzuri hainitii uvivu nitaisoma mpaka nitaifikia. Ila hii kidogo imenivuruga. Sijaielewa kivile
 
Shunie acha
shunie acha uvivu. Mimi hadithi ikiwa nzuri hainitii uvivu nitaisoma mpaka nitaifikia. Ila hii kidogo imenivuruga. Sijaielewa kivile
Ndugu yangu naona uvivu wangu umezidi yaan huwezi amini nipo hivyo ukiona haunioni kwenye story nyingine ujue nimeikuta kati na episode nyingi zimepita
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom