RIWAYA: CODE X 3:
THE REAL ME
MTUNZI: Tariq Haji
SEHEMU YA 14
Alex akiwa usingizini alishtuka ghafla na kuinuka, moja kwa moja hadi cumba cha rubani. Alipofungua mlango alipigwa na bumbuwazi baada ya kukuta wawili hao wakiwa wamekumbatiana. "samahanini kwa kuingilia kati starehe zenu" aliongea, "hapana tena bora ulivyokuja maana huyu bibie hataki kuniacha" alijibu Adrian na kujaribu kumtoa Scarlet KIfuani. "Ariella tafadhali punguza basi, najua ni muda mrefu lakini wacha tumalize ili kwanza halafu nitakuacha unikumbatie mpaka uridhike" Adrian aliongea kwa sauti ya chini lakini Alex alifanikiwa kusikia jina la Ariella. "Adrian" aliita Alex, "ndio mimi" Adrian alijibu.
"Ni hivi kwa sasa hatuwezi kuelekea kambini, si kwetu wala si kwako. Hii ni kwasababu katika kambi zote mbili kuna kunguni wamepandikizwa na waasi" aliongea Alex, "unasemaje?" Scarlet aliropokwa kwa nguvu. "natumai umenisikia bila shaka, kuna vikunguni vimepandikizwa na ile kambi kwa sasa sio siri tena kwasababu waasi wanajua ilipo na kila kinachofanyika humo" alijibu Alex na kufafanua. "Adrian sasa hivi tuko wapi" aliuliza Alex, Adrian alisoma rada "tunakaribia New York".
"hii ndege inabidi tuiangushe majini ili tusijulikane tulipo, Scarlet kawaambie wavae makamanda wavae parashute kabisa" Alex aliongea na Scarlet alitoka katika chumba hicho na kuelekea walipo wengine na kuwapa taarifa. Bila kuchelewa walianza kujiandaa, "Adrian igeuze ndege na uielekeze chini" Alex aliongea na kutoka chumbani humo. Adrian aliigeuza na ufanya kama alivyoelekezwa. Kisha alitoka humo nakwenda kuungana na wengine.
Walipohakikisha kila mtu amejiandaa, walifungua mlango wa nyuma wa ndege hiyo na wote wakaruka na kuiacha ndege ikielekea baharini na kulipuka. Alex akiwa kama kiongozi kwa sasa, aliongoza msafara huo unaoelea angani kuelekea mjini New York. Baada kama dakika ishirni hivi walifungua maparachute na kushuka nje ya mji kidogo. Walipohakikisha wote wakosalama, Alex aliwapa ishara wamfuate. Walitembea kwa nusu saa mpaka walipofika katika nyumba moja ambayo ilikuwa imejitenga sana na nyingine.
Alex alisogea mlangoni na kubonyeza sehemu, kilitoka kitu kama keyboard ndogo. alibonyeza bonyeza na mlango ukafunguka, "karibuni nyumbani" Alex aliongea na kuingia ndani huku nyuma akiafatiwa na makamanda wengine. "Alex hii nyumba ni ya nani?" aliuliza Scarlet, "ni ya mwalimu wangu Allen James" Alex alijibu na kukaa kwenye kochi. Kila mtu alionekana kuchoka kivyake vyake, baada muda kidogo kupita Alex aliinuka na kuelekea katika chumba chake. Alikaa kwa muda kabla ya kusikikia vitu vikivunjika. Wote walikimbilia chamba ambcho alikwenda Alex, walimkuta akimeshika picha mschana huku akilia kwa majonzi ya hali ya juu. "najua bado amani hujaipata lakini nakuahidi kuwa muda si mrefu utaipata" Alex aliongea huku akifuta machozi.
Scarlet alipoona vile aliwaambia wenzake watoke na wamuache peke yake, afanye analotaka. Dakika ya saa kupita Alex alirudi ukumbini akiwa anatabasamu sana, "Scarlet wasialiana na general mwambie aondoke kambini hapafai tena" aliongea Alex na kumkabidhi simu maalum lakini kila Scarlet alipojaribu namba ya General haikupatikan kabisa. Alijaribu zaidi ya mara kumi lakini hali ilikuwa ndio ile ile. Alijikuta akiingiwa na baridi ghafla, wenzake walijaribu kumtuliza na kumwambia kuwa atakua salama. "labda amezima simu kwa sababu za kiusalama zaidi" aliongea Adrian.
"jamani leo pumzikeni maana kuanzia kesho kutakuwa na kazi kubwa sana ya kufanya" Alex aliongea na kuwaomba wamfuate, aliwaonyesha vyumba vya kulala na mwisho alibaki yeye, Scarlet na Adrian. "nyinyi chumba chenu kile pale, maana hueda baada ya leo msipate tena usiku wa kuwa pamoja" Alex aliongea na kuwafanya wote wacheke. Waliagana na kuelekea vyumbani mwao, huko chumbani kwa Scarlet na Adrian kulikuwa ni peponi kwa usiku huo.
Baada ya kuingia chumbani kwake Alex alitoa computer ndogo inayojulikana kama master computer. Aliichezea na kuingiza code anazojua yeye mwenyewe na akili yake kisha akatuma ujumbe "Allen Jr za siku nyingi" ndivyo ulivyosomeka ujumbe huo. "Christine kuna ujumbe wako huku" Martina alimuita Christine, macho yalimtoka baada kugundua kama ujumbe huo umetoka kwa Alex. Na hilo halikumpa tabu kutokana na kuwa ni Alex pekee ndie anaemuita Allen Jr. "unataka nini?" alijibu, "wakati huu ni wakati wa kueka tafauti zetu pembeni" Alex alijibu. "unamaanisha nini?" Christine alihoji.
"wewe unataka kulipa kisasi cha babaako na mimi nataka kulipa cha mwalimu wangu, sasa kwanini mimi na wew tuwe maadui?" alex alijibu na kuuliza swali. "sihitaji msaada wako" Christine alijibu kuonesha jeuri, "bado hujakua kumbe, au unaringa kwasababu uko na Jeff" alijibu pigo na kuwafanya wote washtuke. "musishituke sana na wala musihangaike kutafuta ni wapi ninapo waonea" Alex alijibu. "sasa ni hivi mimi najua ulipo nakupa nafasi ya mwisho, aidha tueke tafauti pembeni au tuendelee kuwa maadui" Alex alituma tena ujumbe.
"na kama nikikata kushirikiana na wewe" Christine alijibu, hapo hapo computer zao zilizima na zilipo waka tu ilionekana picha ya Alex akicheka. "naona kukuandikia kwa ujumbe hutaki kunielewa na natumai sasa tutaelewana vzuri" aliongea kisha akaendelea "ukikataa, hao wote waliouwa pembeni yako watakufa mmoja baada ya mwengine". "Christine hebu kaa pembeni kwanza" aliongea Jeff, "Alex tuongee kiume maana huyu mtoto wa kike anaonekana hajakua bado" Jeff aliongea jambo lilimkera sana Christine.
"Mambo si hayo sasa, Allen Jr kaa pembeni kaka zako tuongee" aliongea Alex na kucheka kidogo. "Sasa ni hivi hawa jamaa wanakambi nyingi sana na ili kuwapunguza makali tuanze kuteketeza kambi moja moja mpaka zibakie chache ambazo tutaweza kuzimudu" Aliongea Alex. "kwa makadirio zinafika kambi ngapi" Jeff aliuliza, "mia moja na hamisini na kidogo hivi lakini hazifiki mia mbili" Alex alijibu. "hizo nyingi kweli" Jeff alijibu na kuendelea "sasa una mpango gani?" aliuliza, "hizo kambi zimegawanyika sehemu tatu, kuna za baharini, za msituni na za jangwani. Nyingi ziko jangwani na baharini na hizo ndio rahisi kuziangamiza" alifafanua Alex na kuendelea "kwa vile sisi tuko makundi mawili, inabidi tugawane kundi moja lichukue kamba za baharini na kundi la pili lichukue za jangwani. Tukizimaliza hizo tushirikiane kuzimalizia za msituni maana hizo ndio kambi kubwa kuliko zote".
"sawa hakuna shida mimi na timu yangu tutachukua za jangwani, kesho usiku tutahakikisha zimekweisha zote" Jeff aliongea na kutabasamu. "ok sis huku tutachukua za baharini, tukutane tena kesho usiku kwa ajili ya mipango mengine" Alex alimaliza kuongea na kukata mawasiliano. Sekunde chache tu baada ya kukata mawasiliano hayo, uliingia ujumbe kambini kwa Jeff. Ilikuwa ni ramani ya kambi za janngwani, "kwa nini unataka kushirikiana nae?" Christine alifoka. "tatizo lako wewe hutaki kuwa muelewa, unadhani pekeetu tungewezaje kupata taarifa zote hizi. Kuna baadhi ya wakati inabidi ukubali tu kama umeshindwa, na kuanzia sasa jina langu ni Ghost na sio Jeff" Jeff aliongea huku akikunja sura. Christine alitaka kumjibu lakini Talbot alimuwahi na kumziba mdomo kisha akamwambia "kumjibu ni wazo baya sana na utalijutia, ni bora unyamze tu maana ushamvuruga. Akibadilisha jina na kujiita Ghost ujue tayari yupo katika maandalizi ya kuuwa au kutoa dozi isio na kipimo maalum"
Christine alipoambiwa hivo alinyamaza kimya, Jeff alielekea chumbani kwake na kujichimbia. Alianza kupanga na kupangua mipango yake, mpaka muda huo alishaelewa kusudio la Alex. "kwanini yule mwanamke anakuwa kichwa ngumu" alijiuliza swali hilo, wakati akiendelea kuwaza mlango ulifunguliwa na alieingia alikuwa ni Christine. "Jeff nimekukwaza?"aliuliza, "hivi kwanini unaweka sana vinyongo, we hujaona maana ya Alex kukutafuta" aliongea Jeff au Ghost kama anavyojulikana na wakiuka sheria wengi.
"kinachoniuma ni babaangu kufa kwaajili ya mtu mwengine" Christine alitoa donge hilo moyoni, "wewe kwani leo unavyopambana na majambazi sugu, unapigania maisha ya familia yako au?" alifoka Jeff. "hapana napigania maisha ya watu wa nchi yangu" alijibu huku akiona aibu, "sasa babaako kufa kwa ajili ya mtu mwengine huoni kama alikuwa akitimiza wajibu wake" Jeff aliongea. "basi yaishe nimejifunza" ilibidi Christine akubali sasa, "sio kujifunza unatakiwa kuwa mwanajeshia aliekomaa, yaani pamoja na kuwa na cheo kikubwa kama cha THE ONE AND THE ONLY. Unashindwa na mtu mwenye cheo cha ukomando tu kweli mpenzi wangu" Jeff alionekana kukereka sana na tabisa alioinesha Christine mbele ya Alex na mbele ya kikosi chake chote.
Ilibidi Christine atumie nguvu ya ziada kuomba msamaha, kwasababu alielewa ni kiasi gani amekidhalilisha cheo chake. Baada kuomba msamaha muda mrefu, Jeff alisamehe na kumona ikiwa atarudia tena basi atamvua cheo. Hilo lilikuwa onyo kali sana ambalo Christine tokea anze kulitumikia jeshi hakuwahi kupewa. Jeff alirudi ukumbini na kukiita kikosi chake chote "kesho kutakuwa na kazi ngumu sana ya kufanya, na kazi hiyo ndio itatupa muelekeo wa nchi zetu. Tukae tukijua kuwa tukiharibu basi tumeziumiza nchi zetu. Kufa vitani ni ushujaa kuliko kurudi nyumbani na mkia katikati ya mapaja eti tumeshindwa. Tunasimama pamoja hadi mwisho, hadi tujue mbivu na mbichi" Jeff alimaliza kuongea na kuweka mkono kati, ilifata mikono mingine juu na kwa pamoja wakasema "pamoja hadi mwisho".
Upande wa Alex huko nako mambo yalikuwa yameiva sana, "sisi tuko tisa na ndege zipo tano, sasa ni hivi kila ndege itakuwa na watu wawili kasoro moja. Hiyo moja ntakuwa pekeangu, kumbukeni kuwa kuifanikisha kazi hii ni muhimu sana hata kama itatugharimu maisha yetu" aliongea Alex na alionekana kuwa makini sana na anacho kiongea. "nifateni" aliwaambia na kuanza kuongoza njia, aliingia katika chumba chake na kufungua kabati ambako kulikuwa na mlango wa siri. Waliingia wote, mlango ulifungwa na lift ikaanza kushka chini. Kumbe ilie ni lifti, iliposimama na mlango kufuguka wote walipgwa na bumbuwazi baada kkutana na ndege za kipekee za kivita.
"sijawahi kuona ndege kama hizi zaidi ya kwenye filamu" aliogea Adrian, "basi leo utarusha kabisa" Alex alijibu na kutabasamu. walichagua wawili wawili na kila kikundi kikaelekea kwenye ndege moja, "kabla ya kuondoka, kila mtu aombe mungu wake kutokana na imani yake. Maana huenda tusionane tena baada ya leo" alimaliza kuongea Alex na kila mtu akasali anavojua yeye. Waliingia kwenye ndege zao, mlango mkubwa ulifunguka na kuonesha njia ndege kwa uzuri zaidi. Zilianza kutoka moja moja, Alex ndie aliekuwa wa mwisho. Zilifuatana kwa dakika tano kisha kila ndege ikashika njia yake, haikuwa shida kwa sababu ramani walikua nazo wote.Wakati huo huo upande wa kina Christine walitoka na ndege zao, na kuelekea katika kambi zilizokuwa jangwani.
***********************
ITAENDELEA