RIWAYA: CODE X 3:
THE REAL ME
MTUNZI: Tariq Haji
SEHEMU YA 10
Basi Alex alikaa katikati ya duara la watu kumi na kutabasamu kisha akajisemea "like old days". kipenga kilipulizwa na wote kumi kwa wakati mmoja walimvamia, Alex hakuwa na papara kabisa kwani alikuwa akijiamini vya kutosha. Taratibu alianza kupambana nao na kadiri muda ulivyokwenda ndio mpambano ulizidi kupamba moto. Alipigana nao kwa muda wa dakika kumi na tano tu na wote kumi walikuwa chini hoi bi taabani.
Baada ya mpambano huo alikwenda mpaka kwenye meza maalum ya maji na kuchukua chupa mbili za maji na kurudi nazo mpaka walipo wengine. Alimkabidhi mwanajeshi mmoja na kumwambia azipeleke umbali wa mita mia mbili kisha azifukie nusu. Baada alimuomba mtunguaji (sniper) aliechaguliwa, "umeziona zile chupa mbili, moja ni yako na moja ni yangu na unatakiwa upige sehemu ya kifuniko" Alex aliongea na kuchukua bastola aina ya Riffle huku yule kijana akichukua bastola maalum ya masniper.
Kila mmoja alitafuta sehemu yake na kulala chini, kumbuka bastola ya Alex haikuwa hata na darubini na kuvutia kitu na kukiona kwa ukaribu zaidi. Kipenga kilipulizwa na wote kwa pamoja wakafyetua risasi, "kijana hujapiga kifuniko, umepiga kwenye shingo ya chupa" Alex aliongea huku akiikabidhi bastola yake kwa mwanajeshi mwengine. Yule aliepeleka zile chupa alirudi huku akiwa haamini kabisa kilichotokea.
Alizikabidhi zote mbili kwa generel na hapo sasa wote walitoa macho, chupa iliopigwa na Alex ilikuwa umetawanyika sehemu ya kifunikio tu na ile nyingine ilikuwa imetawanyika katika shingo. Baada ya hapo Alex alimuomba mtu aliechaguliwa upande wa utmiaji silaha, Scarlet aliingia uwanjani akiwa na bastola maalum zenye risasi za mpira wenye rangi. Alex alichuku bastolo yenye vigololi maalum ambavo hata vikimpat mtu hawezi kuumia sana. Kwa pamoja waliingiwa uwanjani kwa ajili ya kuonyeshana nani ni mkali zaid.
Kama kawaida yake General lipuliza penga na mmpambano ukaanza, na mpaka unaisha nguo za Alex zilikuwa kama wa walivyoanza ila nguo za Scarlet zikuwa zimejaa madoa ya risasi. "natumai general utakuwa umpeta jibu lako"Alex aliongea baada kuikabidhi bastola yake. "kijana hivi wewe ni mtu au mashine" General aliuliza kwa sintofahamu. "hahaha, mimi ni mtu wa kawaida mbona" Alex alijibu. "hapana wewe huwezi kuwa mtu wa kawaida kwa mambo ulioyafanya hapa leo hakuna atakae amini kama wewe ni mtu wa kawaida" General alijibu huku akionekana kutoamini kilichoyokea muda mfupi ulipita.
"Sasa subiri niwaeleza maana ya CODE X" Alex aliongea na wote walisogea karibu kusikiliza kwa umakini wa hali ya juu. "kirefu cha CODE X ni CINDREX OLTIVIASO DECA ENDROLINE X, hii chemical maalumu imetengenezwa kwa ajili kuwafanya wanajeshi kuwa hatari zaid. Ni project ambayo ni hatari sana kuliko watu wengi wanavyoifikiria, na mtu wa kwanza ambae ilitumika kimikali hii na kufanikiwa alikuwa naitwa Alen James. Huyo ndie aliekuw hatari zaidi lakinu ameshafariki tayari, mtu wa kwa hatari ni mimi Alex Jr au Project 75".
Alex alinyamaza kidogo na kuwaangalia kisha akaendelea "Mimi nina uwezo wa kupiga risasi mita mia mbili bila kutumia darubini, pia nina uwezo wa kukwepa risasi na natumai mumeona baada ya pamabano na Scarlet. Na katika ubora wangu nina uwezo wa kupambana na makomando zaidi ya kumi na tano, sasa jiulizeni kambi ya kawaida ya vibaka naifanyaje. Na kwa wakati huu siko peke yangu, kuna wanajeshi wengine wengi wanaandaliwa na kikundi kinachojulikana kama WANAMAPINDUZI. Na harakati zote zile za kusakwa ilikuwa ni kuhakikisha wananizuia siingilia kati katika kufanikisha hilo" Alex alimaliza kuwaeleza kwa ufupi kuhusiana na Project CODE X.
Alex aliwaangalia wote kwa umakini wa hali ya juu sanana kugundua wasiwasi waliokuwa nao. "Kijana asante kwa kutifmbua macho maana ni muda mrefu sasa tumadili na kikosi fulani xha watu ambao hatuwajui" general aliongea huku akimshika bega Alex. "chochote kwa taifa langu" Alex alijibu kisha akapia salute kama ishara ya heshim. Walirudi ndani na kila mtu akaelekea upande wake, general alielekea katika chumba cha mawasiliani kwa ajili ya kuzifikisha taarifa hizo kwa raisi.
"habari yako muheshimiwa" General aliongea baada kuunganishwa ikulu na rais, "nzuri tu, pole na majukumu" Raisi alijibu. "asante mkuu, kuna video nitakutumia naomba uiyangalie kwa makini kisha tujadii kitu mkuu"."ok, hakun shida", General akampa ishara mtalamu wa computer na hapo akaituma video ambayo ilirikodiwa wakati Alex anaonyesha uwezo wake. Raisi aliiangalia mpaka mwisho, "naam general unataka tujadili kitu" Raisi aliongea baada kumaliza kuangalia video hiyo.
"Mi nashauri huyu kijana tumuunge na kikosi hichi kwa sababu atakuwa ni msaada mkubwa sana kwetu", "wewe umeamuamini?". "ndio mkuu, huyu ni mzalendo na haina haja ya kumtilia mshaka kabisa", "basi hakuna shida juu ya hilo, andaa taratibu zote zinazohitajika kuapishwa kwa kijana huyo. Mimi kesho asubuhi nitakuwa hapo kwaajili ya kumkabidhi gwanda zake". Walimaliza kuongea na kuagana, General alitoka katika chumba hicho na kumuita mtu maalum wa kuchora tattoo na kuongozana nae mpaka katika ukumbi maalum.
Aliamuru wanajeshi wote waitwe, haukupita muda mrefu wote walikuwa katika eneo hilo. "msishangae kwanini nimewaita wakati sio muda mkusanyiko, lakini ni hivi nimeongea na raisi muda si mrefu na kumtumia video ambayo ilirikodiwa wakati wa mazoezi ya Alex. Hivyo basi ametoa agizo kuwa Alex awe miongoni mwetu katika kulitumikia taifa" General aliongea na uwanja mzima ulilipuka kwa sauti za kushangilia.
Alex alipewa amri atoke mbele kwaajili ya kuchorwa tattoo la kikosi hicho, bila kupinga alivua fulana yake na kusogea. Mchoraji alianza kazi yake huku watu wakishuhudia tukio hilo, "ebwana unajua huyu ndugu habari nyingine". "huyu jamaa ana hatari kwakweli, sasa ikiwa huyu mmoja tu yuko hivi hao wengie sijui wakoje". "lakini si mbaya, tunae mmoja wao kati yetu hivyo tutajifunza kupitia yeye jinsi ya kukabiliana nao katika mpambano" hayo ni baadhi ya yaliokuwa yakiongelewa na baadhi ya wanajeshi wakati zoezi la uchoraji likiendelea.
**************
"may day, may day mimi ni rubani wa kikosi cha KING's SQUAD (K.S)" Alisikika kijana mmoja akiongea kupitia kifaa maalum, "rodger, tunaomba nambari yako tuhakikishe" upande wa pili ulimjibu. "Nambari yangu KS099" alijibu rubani huyo, "tueleze kuna nini". "nimefanikiwa kuupata mzigo lakini sidhani kama nitafika nao, kuna ndege nyingine nne za waasi zinani fukuza na mpaka muda huu tunaongea wenzangu wawili wameshatung....." kabla hajamaliza mawasilino yalikata na kila control tower ilivojaribu hakupatina.
Ripoti ya kutunguliwa ndege hiyo ilifikishwa kwa raisi, wakati huo alikuwa anajianda kuelekea katika kambi ya THE PIRATES kwaajili kumuapisha kijana Alex. Baada ya kupewa taarifa hiyo alitoa amri kuwa iandikwe haraka na apewe hiyo document aondokea nayo. Hazikupita hata dakika kumi ilikuwa imeshakamilika na raisi aliichukua na kuondoka nayo. Safari ilianza huku raisi akiwa na wasiwasi sana kutokana na tarofa muhimu alizokuwa nazo rubani aliepotea.
Baada ya masaa kadhaa hatimae ndege ilikanyaga uwanja wa PIRATES, raisi alishuka na kuelekea ndani. Haikuchukua muda mrefu kumuapisha kutokana na maandalizi yalikuwa yamekamilika. Baada shughuli hiyo fupi, Alex alikabidiwa gwanda zake rasmi na kupewa amri akazivae muda huo huo. Raisi alimwita General na kumkabidhi ile bahasha yenye ile document, kisha yeye akaaga na kuondoka. General aliifungua bahasha ile na kusoma kilichokuwemo ndani na aliporidhika alibofya kitufe fulani hivi ikaanza kusikika honi ya dharura.
Muda huo huo kikosi chote kikasanyika katika ukumbu wa vikao, Scarlet na timu yake akaambiwa ajiandae. Alex pia alijumuishwa katika kikosi hicho chenye jumla ya wati saba hivyo na yeye akawa mtu wa nane. Baada kukamilisha maandalizi walirudi katika ukumb huo na kupewa maelekezo "kuna rubani mmoja ametunguliwa na alikuwa amebeba taarifa muhimu sana, tunaamini ametunguliwa maeneo hayo" General aliongea na kuonyesha sehemu katika ramani.
Alex alishtuka kidogo baada general kuonesha hio sehemu, ni kama kwamba anaifahamu. "samahani general, hiyo kambi ni kambi ya watu gani?" aliuliza. "mpaka sasa hatujahakikisha ni kambi ya wtu lakini nahisi ni kambi ya ncho amabazo hatupatani nazo General alijibu kisha akauliza "kwani vipi". Alex alikaa kimya kwa muda kama mtu amabe alikua anajaribu kukumbuka kitu, alishtuka tena na hapo akijipa uhakika kuwa hajakosea. "hiyo ni kambi nambari ishirini ya jangwani, ni moja kati ya kambi kubwa sana Project CODE X" Alex alijibu kwa uhakika.
Wote waliokuwepo pale walishtuka baada ya kusikia hivo, "basi vizuri kwasababu sasa tumeshaifahamu, basi hakuna shida" General alijibu na kuendelea kutoa maelezo. Kikosi cha Scarlet kiliingia katika chumba maalum cha kuchukua silaha na hapo ndipo alipozidi kuonyesha maajabu. "hivi katika kikosi hichi kuna sniper wangapi?" aliuliza Alex, "wawili tu" alijibu Scarlet. "ok, sasa inatakiwa kuwe na wanne" Alex aliongea na kuwafanya wote wamuangalie.
" Na wote hao wanatakiwa wakae masafa yenye umbali zaidi ya mita mia mbili, na bastola ziwe zile ambazo ni nzito sana" Alex aliongea na wote wakakubaliana nae. Walimaliza maandalizi na kuondoka kambini hapo kwa chopa maalum amabyo iliandaliwa kwa kazi hiyo tu.
"kijana unaleta jeuri sio" aliongea mtu mmoja kwa hasira sana, "narudia tena kwa mara ya mwisho, jina lako nani na ni nani aliekutmuma". "huna haki ya kujibiwa na mimi, mimi najibu wakubwa zangu tu" aliongea kijana huyo ambae alikuwa amerowa damu baada ya kuchezea kichapo kikali sana. "naona wewe hujafunzawa kwenu"aliogea tena kwa hasira yule mtu na kumtandika ngumi ya tumbo. "P102 (project 102) unaitwa na mkuu" aliingia kijana mwengine na kutoa taarifa.
P102 aliondoka na kuelekea ofisini kwa mkuu wake "umepata chochote kutoka kwa yule rubani?" aliuliza mkuu wake, "hapana anaonekana amekaza kweli kweli" P102 alijibu. "sawa muache apumzike kwanza utaendelea kumhoji baadae maana huyo mtu ni muhimu sana" aliongea mkuu huyo na kumpa ishara aondoke. P102 alifunga mguu na kuondoka huku akiwa mechukiwa kwa kitendo cha kuambiwa amuache.
ITAENDELEA