RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George IronMosenya
Wapita njia waliongezamwendokasi walivyokaribia eneo lile. Wengine waliziba pua zao kwakutumia viganja vya mikono yao kuepukana na hewa hiyo chafu.
Baadhiyao walijiziba na magazeti, wengine kwa bahasha zao. Ilikuwa ni jionina kila mmoja alikuwa anarejea kutoka katika mizunguko yake.
Kwajinsi watu walivyokuwa wametingwa na mambo vichwani mwao hawakuwezakulishuhudia kundi la viumbe hai ambalo halikubabaishwa na moshi huomzito. Na hata kama wangeona wasingekuwa na la kusaidia zaidi yakupata la kuongea na kujisahaulisha suluba ya siku nzima hukowalipotoka.
Ardhi iliyobeba uchafu wa kila aina iliyopewa jina lajalala ilikuwa katika mahangahiko ikifukuliwa kwa fujo na watotowanne wa rika moja huku mkubwa akikadiriwa kuwa na miaka kumi namitano
Macho yao yalikuwa mekundu, matambala ambayo zamaniyaliitwa nguo yalifunika miili yao.
Wengine walikuwa wameinamawengine wakiwa wamepiga magoti, mikono yao ikiwa 'bize' kuchimbaardhi na kutoka na vyuma chakavu.
Matambala waliyovaa yaliwafanyawote wafanane, na ilikuwa ngumu kutambua iwapo wana jinsiatofauti.
Hakuna aliyezungumza na mwenzake, nyuso zaozilizotiririka jasho zilitangaza njaa kali na chuki.
Mtoto mmojaalivyojiridhisha kuwa eneo lile vyuma vilikuwa vimekwisha alinyanyukana mfuko wake wa chumvichumvi, akachukua mkono wake mchafuakajipangusa jasho. Tambala alilokuwa amevaa lilisomeka kwa shidamaandishi 'I LOVE TANZANIA', lilikuwa kubwa kumpita na lilikuwalimetatuka na kuruhusu matiti yake yaliyokuwa yameanza kujifunzakusimama yachungulie nje. Huyu pekee alikuwa mkubwa kupitawenzake.
Alijikongoja na fuko lake hadi akalifikia jalala jingine.Hapo pia alipapasa bila kupata chochote. Akasimama wima akiwa amekatatamaa. Alipopiga hatua nne kuliacha jalala macho yake yalivutiwa nakifurushi cha uchafu wa siku nyingi, akatua tena fuko lake akachukuakimti kigumu akaliendea lile furushi na kuanza kupekenyua.
Lahaula!Tabasamu pana likachanua usöni mwake, akayapongeza macho yake kwakuvutiwa na furushi lile. Akavuta kwa nguvu, akatoka na jembechakavu.
Biashara nzuri kwa siku hiyo!
Wakati anasimamakuliendea fuko lake, akasita kabla ya kupiga hatua. Hakuwa pekeyake!
"Siso yangu hiyo!" sauti ya kiume ilikoroma. Bintiakamtazama yule chokoraa mwenye nywele zinazotaka kufanana namwarabu, ngozi nyeusi yenye ukurutu unaotiririka jasho.
"Sisoyangu hiyo uliyoshika" sauti ya mvulana haikuwa na mzaha.Alimaanisha!
Yule binti akashtuka na kulitazama lile jembemkononi kana kwamba hakutambua kama amelishikilia.
Kisha akapuuziaakapiga hatua kadhaa kuliendea fuko lake, yule kijana akamfanyiashambulizi la kushtukiza, akamnyakua lile jembe. Alipotaka kukimbiayule binti akawa mwepesi akakamata shati chakavu la yule kijana. Kamavile wembe mkali unavyokutana na karatasi laini ndivyo lilivyoachanatambala lile.
"Mamaa! Umenichania shati we malaya!"
"Nanimalaya? Malaya mama yako aliyekuzaa akakutupa jalalani mwanahizayamkubwa nipatie jembe langu!" binti naye alijibu mapigo kwa sautikali.
Pasipokutegemea alivamiwa na kuchabangwa teke tumboni kwanguvu, akajipindua na kuanza kuugulia maumivu. Tambala lililokuwalinamuhifadhi likakosa umakini, chupi yake ambayo zamani ilikuwanyeupe lakini sasa ikiwa kama ina kutu ilichungulia nje. Mbavu zakezilizohesabika kutokana na wembamba zilitokeza nje.
Yule mhanga wakuchaniwa shati akiwa hajaridhika na pigo lile alimrukia tenaakamchabanga teke kali katika zile mbavu zilizokuwa nje kimakosa,sasa binti akanyoosha mikono kuomba msamaha huku maumivu yakiukunjauso wake.
Hakuupata msamaha bali kukaribisha kipigo kingine.Tumboni tena!
"Mariaa! Mariaa!" sauti ilisikika kutokeakatika ule moshi mzito.
Maria aliyekuwa amekumbatia uchafu wajalalani alisikia lakini hakuweza kugeuka. Mbavu zilikuwa zinamuumana alipumua kwa shida sana.
Vishindo vya miguu vikafika karibuyake.
"Kwanini unampiga?
"Kwanini unampiga?"sauti ya kitoto ililalamika kwa uchungu.
"Kwani na wewe dogounasemaje?" alijibu kwa ubabe na jeuri yule mhanga wa kuchaniwashati.
Maria alisikia kila kitu lakini hakuweza kuongea. Alitamaniyule mtoto angekuwa mtu mzima huenda angemsaidia.
Yule kijanaambaye alikuwa kama amepandwa na mori ya kimasai, alijitazama tenashati lake lililoachana, hasira ikapanda upya!
Akampuuzia yulemtoto. Akamrukia Maria. Sasa aliamua kutumia mikono.
"Utalipashati langu utalipa we malaya." maneno hayo hayakutoka bure,yalisindikizwa na mdundo wa mapigo ya ngumi na vibao katika uso waMaria, ambaye naye tambala lake lilikuwa limeuacha mwili. Matitimawili madogo yakitazamana na mbingu za bluu.
Hapa likatokea tukiolisirotarajiwa na wote mpiga na mpigwa.
Yule mtoto mwenye umri wamiaka tisa aliyekulia katika kundi maarufu na hatari jijini Mwanza la'watoto wa wakoma' alichomoka mbiombio akamfikia mpigaji.
Kitendocha sekunde tatu hali ikabadilika. Maria akabaki huru, yule mpigajiakatua chini akiwa anagalagala, damu ikiruka kwa fujo mgongoni mwake.Mtoto wa wakoma alikuwa anatoweka kuelekea mashariki.
Wembe wenyemakali ulikuwa umepenya katikati ya mgongo wa yulempigaji.
****
Chumvi chumvi ilipenya katika koo lakealivyojaribu kumeza mate. Akatambua kuwa midomo ilikuwa imepasuka.Mbavu zilikuwa zinauma sana lakini hakuwa na budi kusimama.Akaunganisha tambala lake, kidogo likamstiri. Yule mpigaji hakuwepotena eneo lile. Zilisalia damu nzito pale ardhini.
Maria alibakikatika sintofahamu, hakujua ni kwa namna gani yule mtoto alimuokoa.Sasa alikuwa amesimama wima, mwili wote ukiwa unauma na giza lilikuwalimeanza kutanda.
Upepo uliokuwa unavuma kutokea jalalani, jaamaarufu la 'mchafu kuoga' jijini Mwanza. Uliileta harufu mbaya katikapua zake.
Kwa mara ya kwanza katika maisha yake akajuta kuzaliwa.Akaupata ukiwa maradufu, ukiwa wa kutengwa na dunia
Taswira yamama yake mzazi ikakimeza kichwa chake, japo alilelewa naye kwakipindi kifupi lakini anakumbuka amani aliyokuwanayo kwa kuyapatamalezi yale bora.
Akiwa na miaka tisa pekee, mama yake (MamaMaria) baada ya kutoka masomoni katika chuo cha Kigurunyembe Morogoroanapatwa na maswaibu ya kuchekesha, baada ya kuyakwepa magari mjiniMorogoro na jijini Dar es salaam alipokwenda katika mafunzo yavitendo. Anakuja kugongwa na baiskeli mjini Singida. Aliyemgonga nimwanamke. Badala ya kukasirika mama Maria alicheka.
Alicheka maanahakuumia!
Hata alivyomsimulia mumewe na mtoto wao wa pekee Maria.Wote walimcheka na kumtania!!
Siku iliyofuata hakuwezakuamka!
Mguu ulikuwa umevimba! Mguu ule uliogongwa nabaiskeli.
Baba Maria alishangaa. Maria alikuwa shuleni wakatihuo!
Kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo mguu ulizidikuvimba!
Huduma za hospitali zikahitajika.
Akakimbizwaupesi.
Ile tamthilia ya kuchekesha iliyoanzia kwa kugongwa nabaiskeli, ikamalizikia kwa huzuni kuu. Mama Maria akaaga dunia hatakabla hajafika hospitali.
Maria alimngojea mama yake aendekumchukua shuleni lakini hakutokea! Siku hiyo akajiunga na rafikizake wakarejea nyumbani ambapo alikuta kundi la watu
Wengi wakiwawameizunguka nyumba yao. Ulikuwa msiba!
Maria akiwa na miaka kumina tatu akabakiwa na malezi ya baba pekee baada ya kuwa amerushaudongo kumfukia mama yake kaburini.
Mzee Paul alivyorejea katikabiashara zake. Yule mama aliyemgonga marehemu Mama Maria na hatimayekupoteza uhai kimaajabu akawa haishi kufika pale nyumbani. Wakatimwingine alikuwa akimpeleka Maria shuleni, anampikia chakula.
Baadaya miezi sita, Maria akatambulishwa rasmi kuwa yule ni mama yakempya.
Muuaji wa mama yake sasa anakuwa mama yake!
Angefanyanini angali ni mdogo!
Akakubali!
Mambo yakabadilika, yulemwanamke akaanza manyanyaso kwa Maria. Akamfanyisha kazi nzitokumzidi.
Cha ajabu mzee Paul hakujali.
Baada ya kuyazoea yalemanyanyaso. Miaka miwili baadaye alikuja mgeni ambaye Mariaalitmbulishwa kama kaka yake.
Hili nalo hakupinga walahakuuliza!
Ule ukaka ukawa na utata ndani yake.
Mara leoanamtekenya, mara amkumbatie.
Maria hakuwa na pa kulalamika.
Sikumoja walipobaki wawili nyumbani yule kaka akambaka! Kishaakatoweka.
Siku aliyomweleza mama yake wa kambo ndiyo sikualiyofukuzwa nyumbani.
Maajabu! Baba akabariki uamuzi huo!
Mariaakiwa na miaka kumi na tano anapokelewa na mtaa wenye ndugu wachachewasiojali.
Mapokeo hayo mabovu kutoka kwa ndugu anaowafahamuyanamfadhaisha!
Baadaye akiwa kwa shangazi yake anagundulika kuwani mjamzito. Hakuna aliyetaka kumsikiliza, akalazimishwa kurudinyumbani kwa baba yake.
Akarejea kwa shingo upande. Siku hiyoaliyofika hakukuta mtu lakini funguo ulikuwa juu ya mlango. Mariaakafungua na kuzama ndani!
Akapokelewa na fungu la pesa katikameza ya kulia chakula. Akili ikakimbia maili mia mbele. Akawaza juuya kutoa mimba, alihitaji pesa, kama vile kunguru anyakuapo vifarangandiyo naye alivyonyakua zile pesa zilizokuwa zimeigandamiza karatasi,yenye maandishi.
Laiti kama angefikiria walau kuisoma ile barua,angegundua kuwa baba yake amejirudi anamtafta yeye (Maria) kwa udi nauvumba na barua ile ilikuwa ya kumfukuza yule mwanamke mwenye rohombaya!
Na zile zilikuwa pesa kwa ajili yake.
Mariahakuisoma
Laiti angeisoma asingefikia pale ambapoalifikia!!
***
Doreen alilipokea tatizo la Mariakama la kwake. Ni msichana huyu pekee ambaye Maria alikuwa anamuaminikati ya rafiki zake. Kwa kuwa pesa likuwepo kila kitukingewezekana.
Vyuma vikapenya katikati ya miguu ya Maria, matusiya nguoni mfululizo kutoka kwa daktari mwenye kipara ambaye tayarialikuwa amepokea shilingi elfu hamsini kwa ajili ya kufanya dhambihii ya utoaji mimba. Hatimaye mabonge mabonge ya damu yaliyoanzakujikusanya katika mji wa uzazi wa Maria yakaharibiwa maksudi, mimbaikawa imetolewa kwa uchungu mkubwa.
Ni Doreen aliyemshawishiMaria kukimbilia jiji la Mwanza kutafuta maisha. Maria hakufikirimara mbili akakubali.
Huku akapokelewa na mtaa, mtaa ukamsulubu nasasa amepigwa vibaya na chokoraa wa kiarabu, amevimbausoni.
Anamkumbuka mama yake mzazi.
Anamkumbuka mamaMaria.
Nani kama mama???
***MARIA ametengwa na dunia sasaameangukia mtaani…mtaa unamsulubu!!! Nini hatma yake??
***Je!!Nini kitaendelea katika RIWAYA hii ya CHOKORAA!!!
culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata Moderator binti kiziwi Nicas Mtei korino Sukula aniceth mzahula Khantwe kelcie Meljons
MTUNZI: George IronMosenya
SEHEMU YA KWANZA
Moshimweusi uliokuwa unatoka katika jalala lililokuwa linachomwa ulifanyamfano wa ukungu usiopendeza machoni.