mapengo junior
JF-Expert Member
- Jun 28, 2011
- 1,135
- 276
- Thread starter
- #41
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
Usiku uleule Tano alienda Kilwa Masoko. Kummaliza Mwanasheria. Alijua kumuacha hai Mwanasheria basi habari juu ya kidonda kilichoibuka ghafla katika kifua cha mama Mpaukha itaendelea kusambaa. Ilikuwa ni lazima kumuuwa Mwanasheria ili kumziba mdomo milele !
Usiku wa saa nne usiku ulimkuta Mwanasheria akinywa bia katika baa ya Tiga Tisa. Alikunywa bia nyingi sana. Tangu saa kumi na mbili jioni alikuwa hapo akipata ulabu.
Meza ya tatu toka pale alipokaa Mwanasheria kulikuwa na mgeni. Mgeni aliyewasiri pale majira ya saa tatu usiku. Mgeni huyo alikuwa makini kwa kila alichokuwa anakifanya Mwanasheria. Mgeni huyo hakuwa mwengine ila ni Tano wa Six Killers. Alikuwa anamsubiri mwanasheria anyanyuke ili akamfanye alichotaka kwenda kumfanya.
Saa tano usiku Mwanasheria alinyanyuka pale kwenye kiti. Tayari kuelekea nyumbani kwake. Alisogea taratibu kwenye gari yake, alipanda na kuliwasha. Safari kwenda nyumbani kwake ilianza. Tano naye alitoka pale Tiga Tisa. Alichukua pikipiki yake na kulifuata gari la Mwanasheria kwa nyuma.
Mwanasheria alikuwa amelewa hasa. Alipoteza kabisa umakini na hakutambua kabisa kama alikuwa anafuatwa. Alifika nyumbani kwake na kuingia ndani. Kutokana na ulevi Mwanasheria alijikuta amelala katika sofa pale sebuleni.
Tano alipaki pikipiki yake kwa nje. Alifika hadi mlangoni katika nyumba ile ya Mwanasheria. Kwa bahati mbaya nyumba ile haikuwa na fensi.
Kwa kutumia funguo malaya alifungua mlango wa sebule wa Mwanasheria. Ilikuwa ni kazi ndogo sana, kazi iliyodumu kwa dakika tatu. Alifungua mlango na kumkuta Mwanasheria amelala pale sebuleni kama mzoga. Alichomoa kisu chake mkononi. Kwa mwendo wa kunyata akawa anamsogelea pale sofani.
Akamtikisa kidogo, Mwanasheria hakuamka, alikuwa amelewa sana pombe. Alimtikisa tena. Nia ya Tano ni kumuamsha Mwanasheria ili kumjua mtu wa pili aliyedakia ile simu wakati yeye anaongea na Dokta Yusha. Lakini Mwanasheria hakuamka.
Tano aliamua kuua tu, akijipa moyo atamjua tu huyo mtu. Alirudisha nyuma ule mkono uliishika kisu, kwa nguvu aliungiza katika tumbo la Mwanasheria, akatoa akaingiza tena. Alirudia mara nne.Mwanasheria akakata roho akiwa amelewa.
Tano alitoka nje huku akiwa na furaha tele. Bila kujua kama alimuua mtu asiye sahihi. Yeye alimuua Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Ndugu Juma Ngozi. Wakati Mwanasheria aliyeongea na Dokta Yusha, Mwanasheria mlevi alikuwa kilabuni wakati ule, akinywa pombe na kupigizana kelele na kina mama Kindumba...
ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA.