SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010
SEHEMU YA MIA NA SITA
Hali ilikuwa tete mle ndani kwa upande wa Dokta Kilumba. Vijana wale wawili makini walikuwa wamembana Dokta Kilumba kisawasawa. Mwanasheria mlevi nae alitoka pale mlangoni na kusogea pale walipokuwa Dokta Yusha na Dokta Kilumba. Siku hiyo Mwanasheria alikuwa hajatia hata tone moja la pombe, lakini mwendo wake ulikuwa wa kilevi. Sauti yake ilikuwa ya kilevi. Ama hakika Mwanasheria mlevi alikuwa ameathiriwa sana na pombe, pombe ilikuwa imeweka kambi katika mishipa yake ya damu. Mwanasheria alikuwa akikanyaga mguu mmoja hapa anakanyaga mguu mwengine kule, alikuwa anayumba ndani ya chumba, alikuwa anakwenda mtindo wa zigzag, lakini Mwanasheria alifika alipopakusudia. Pale walipokuwa wale mahasimu wawili, Dokta Yusha na Dokta Kilumba.
"Dokta Kilumba, daktari mkuu wa hospitali ya Kinyonga. Daktari msomi uliyekabidhiwa dhima kubwa katika wilaya hii. Dhima ya kuokoa uhai wa wagonjwa. Daktari makini sana, uliyepata mafunzo yako ya udaktari huko katika jiji la Mumbai, India. Daktari mzalendo, uliyekataa kufanya kazi mjini, na kuamua kuja huku wilayani, porini eti kuja kusaidia wananchi maskini wa huku kama ulivyodai mbele ya jopo la madaktari bingwa. Unakumbuka ulikataa kufanya kazi Muhimbili? Ulikataa kufanya kazi katika hospitali ya Taifa, hospitali iliyopo jijini Dar es salaam, unakumbuka Dokta?
Ulikataa dokta, inamaana ulikuwa na mpango huu kabla ndomana uliamua kuja huku kujificha ili ufanye kwa amani ufarauni wako? Una roho mbaya sana Dokta Kilumba,
Zaidi John Kilumba sindo jina lako, nakufahamu vizuri Dokta. Si ulisoma shule ya msingi Kigoma wewe? Au nikwambie mwaka uliomaliza? Jua nakufahamu vizuri sana kabla hujajifahamu.
But to make story short, Dokta Kilumba maisha yako yapo mikononi mwangu, ni bahati mbaya sana kwako kwakuwa maisha yako yapo mikononi mwa mlevi, mlevi niliyekubuhu, mlevi niliyopitia mengi sana katika maisha yangu, kuishi na kifo kwangu ni sawa tu, kwa hiari yako na hii hasa kama bado unatamani kuishi naomba ujibu swali langu kwa ufasaha bila kunidanganya....." Mwanasheria mlevi kwa sauti ya kilevi aliweka nukta na kumeza mate, huku akimwangalia Dokta Kilumba kwa umakini mkubwa. Kiukweli Mwanasheria mlevi aliongea maneno yaliyowashangaza wote mle ndani....
Swali gani hilo analotaka kuuliza Mwanasheria mlevi..Mwanasheria mlevi ni nani mbona anayajua mengi..
ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA