EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,357
Binafsi si mtaalam wa mambo ya Sheria, bali ni Mwanasayansi. Sidhani kama weledi wangu kwenye kuichambua sheria hasa neno hadi neno utakua sahihi sana.....
Ni kweli kuwa "kwa nia ya kuchafuana" inaweza kuwa ngumu kueleweka moja kwa moja.
Labda tuanze kwa tafsiri ndogo tu, kwa jinsi nielewavyo neno "NIA" ni ule utayari wa kutaka kutekeleza wazo fulani, laweza kuwa baya au zuri.
NOTE: n shabaha, lengo, kusudi, azma. (tafsiri kutoka TUKI)
Kwa mantiki hiyo basi, Daktari baada ya kuchukizwa hakupaswa kuyaleta huku, kwa kufanya hivyo kwa kiasi fulani anaiweka wazi azma(nia) yake. Kumbuka mawasiliano ya PM ni binafsi baina ya pande mbili, kwa mtazamo wangu suluhisho lolote la kutofautiana lilipaswa kumalizwa huko huko PM.
Kitendo cha kuyaleta huku kwetu, binafsi ndio naweza kuamni kuwa kuna mtu hapa anadhalilishwa(tayari jambo limehusisha kadamnasi na si binafsi tena kama ilivyo PM).
Kwa bahati nzuri na hekima ya daktari ni kwamba hakumtaja moja kwa moja muhusika kwa jina.
Kumbuka hapo awali ulipoanza kuniquote, kuna mtu nilikua najaribu kumuelekeza kuwa sheria hairuhusu kutajana majina.
Hapa inabidi tutofautishe kati ya "nia" na "kusudio". Unless I am wrong, nahisi kama ni vitu viwili vile.
Nahisi neno "nia" ni kama "motive" - sababu iliyomsukuma Riwa kuanzisha hii thread.
Hii inaweza kuwa tofauti na "kusudio" ambayo ni kama "intent"
Kwa kawaida motive ni irrelevant kwenye makosa mengi. Kinacho-matter zaidi ni intention.
Lakini as JF Members hasa tunaochangia kwenye hii thread tufikie sehemu tu-reconcile our fellow members. Wote Riwa na aliyemtumia PM are our fellow members na watu muhimu sana kwa JF na tusingependa wapotee hivi hivi simply because of this.
Inawezekana kabisa aliyetuma PM hakuwa na bad intention. Gaijin kaghusia huko nyuma kuwa wabongo tuna bad communication skills. Pia inawezekana kabisa Riwa hakuwa na bad intention dhidi ya aliyemtumia PM. May be he was so upset na kushindwa kuji-control. This shit happens sometimes.
Kama uliyemtumia Riwa hiyo PM unasoma haya, unless kweli ulikuwa na bad intention, send Riwa a PM kuwa you regret what your PM have caused and that it was not your intention to cause any harm. Pia Riwa unless he had intention to damage the reputation of the person who sent the PM, aijibu hiyo PM huko kwa huko, mambo yaishe.