RITA badilikeni ili mambo yafanyike kimtandao

KALABASH

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
493
206
Hivi karibuni jirani yangu huku mkoani alipata msiba wa kufiwa na mke wake. Kifo kilitokea hospitali iliyoko Dar es Salaam. Kwa kuwa kifo kilitokea Dar shughuli zote inabidi zifanyikie katika za ofisi za RITA Wilaya kulikotokea kifo. Hii ndiyo sheria ya RITA.

Alimtumia wakili aliyepo(Advocate) documents zote zinazohusika na tukio hilo la kifo ili aweze kupata Hati ya kifo(Death Certificate) kutoka RITA. Zoezi halikuweza kufanyika mpaka aje ama Mume, mtoto, au ndugu wa karibu wa marehemu.

Sasa fikiria gharama za kumtoa mtu huku mkoani ili aje kushughulikia hiyo hati. Ni usumbufu na ni kukosa ubunifu kwa upande wa RITA. Mbona wenzao wa BRELA wanafanikisha maswala ya wateja wao bila mteja kufika makao makuu ya BRELA? AMKENI.
 
Back
Top Bottom