Risk ya mchawi kujigeuza mnyama...!

Risk ya mchawi kujigeuza mnyama...!

Hii ni kaliba iliyojaa upweke na mateso japo kuna watu eti wanatamani wanatamani kuwa wachawi...
Mojawapo ya advertise ya kuwa mchawi ni uwezo wa kujigeuza umbo la kibinadamu na kuwa mnyama... Na binadamu wengine wasikujue kabisa kama wewe sio mnyama halisi.. Japo wanyama huwa wana hisia na maranyingi watajitenga na wewe ama kukufukuza...
Unapokutana na kundi la wanyama lakini kuna mmoja kajitenga na wenzake... Tambua tu kwamba huyo si mnyama halisi kwa asilimia kubwa
Kwenye mikusanyiko ya watu ukifanikiwa kuwa na jicho la tatu utaona mengi sana.. Pale kariakoo pale Ilala sokoni, buguruni nknk kuna wanyama wengi sana katikati ya makundi ya watu
Kujigeuza umbo la kibinadamu kuwa mnyama ni uthubutu wa hali ya juu japo ni sifa kwa mtendaji ila anapaswa kuwa na msingi mzuri kwenye taaluma yake kwakuwa akikutana na nguvu kubwa kuliko yeye atapigwa dafrau na kupoteza maisha
Kuna wanga hupenda kujigeuza paka na kuingia kwenye majumba ya watu, sometimes panya au hata nyoka nk.. Sasa hawa ukiwavizia ukawalia timing ukawapa mkong'oto... Asubuhi yake utapata tu habari
Utasikia mzee fulani kaumia bega au kichwa au mkono nknk.. Na ukija kurudisha kumbukumbu nyuma unakuta pale ulipompiga yule mnyama ndio hapo hapo anapoumwa huyo mzee.. Na haendi hospital ataugulia nyumbani mpaka apone...
Risk kubwa ni pale wanapopata kipigo mpaka kupoteza maisha. Siku ya pili mtaani utaona turubai
Mheshimiwa huwa unaandika unachokijua au una hisi tu? Maana kunawatu tumesha onyeshwa dibaji Na babu zetu eneohilo huwasikuelewi
 
Miaka mingi iliyopita mjomba wangu aliingiliwa na nyoka ghafla huko kijijini. Cha kushangaza, yule nyoka alipofika mlangoni tu kutaka kuingia ndani akalipuka kama bomu kisha vile vipande vyake vikaanza kugeuka katika ubinadam, akamwagia unga fulani hivi na akaacha kugeuka. Mjomba akajipaka dawa fulani mwilini kujikinga na yatakayojiri baadaye.
moto ulikutana na fire
 
Hivi kwa nini mimi hizi story za uchawi haziniingii na wala siamini kama huo uchawi ni real
 
Ukishamuua atarudije sasa nyumbani kesho muone turubai???
 
Ukishamuua atarudije sasa nyumbani kesho muone turubai???
Unapiga kivuli... Hicho kivuli kimebeba roho yake huyo mnyama ni coumaflage Tuu... Unatandika huku maumivu anayapata huko aliko
 
Mshana unavyofichua aya mambo hakikisha na ww uko vzr
 
Back
Top Bottom