Zaidi ya wiki tatu sasa kuna zoezi la kukamatwa ngombe katika manispaa za Zanzibar katika mkoa wa mjini Magharibi Unguja.
Imeelezwa kuwa lengo la zoezi hilo ni kukamatwa ngombe wanaozurura ovyo. Hata hivyo habari zinasema Vikosi vya SMZ kwa kushirikiana na Manispaa vinaendesha kazi hio ambayo imegeuka kuwa kadhia.
Zipo taarifa za zoezi hilo kuvuka mipaka na sasa vikosi hivyo vinakamata ngombe hata wanaofugwa wakiwa mazizini na sehemu maalumu. Athari mbali mbali zimetokea ikiwa ni pamoja na watu kuchukuliwa ngombe wao na kutakiwa kulipa faini.
Zoezi linalalamikiwa kuwa Vikosi vimepitiliza maelekezo ya kukamata ngombe wanaozurura na hatimae kuleta mivutano na wafugaji. Hapo jana katika eneo la Tomondo nje kidogo ya mji kulizuka sintofahamu hiyo baina ya wafugaji na Vikosi na kupelekea watu watatu kujeruhiwa kwa risasi(Mwananchi leo).
Mifugo kadhaa imechukuliwa maeneo tofauti na hata sehemu za ndani ambapo ngombe hao wanatunzwa sehemu maalum.
FAINI.
Ili kukombowa ngombe mmoja unatakiwa kulipa 300,000 (laki tatu). Zipo taarifa kuwa kuna wafugaji wamechukuliwa ngombe zaidi ya nane na vikosi kutumia ubabe mwingi kuchukuwa ngombe hao.
(Sorce magazeti ya Leo na vyanzo binafsi)