Serikali yaagizwa kufuatilia kwa haraka mgogoro Kati ya Wananchi na Taasisi ya Efatha uliosababisha watu kadhaa kupigwa risasi

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Bunge limeagiza Serikali kwenda haraka katika Jimbo la Kwela mkoani Rukwa kwa ajili ya kusaidia mgogoro kati ya wananchi na taasisi ya kidini ya Ephata Ministry ambao umesababisha watu kadhaa kupigwa risasi.

Agizo hilo limetolewa bungeni leo Junanne Novemba 7, 2023 na Mwenyekiti wa Bunge, Daniel Sillo baada ya Mbunge wa Jimbo hilo, Deo Sangu (CCM) kuomba shughuli za bunge zisimame ili wabunge wajadili vurugu za jana katika jimbo hilo ambazo zilipelekea wafugaji watatu kupigwa risasi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, jana nilisema kuhusu mgogoro huo wa muda mrefu na nikaomba Serikali iingilie kati ambapo Waziri wa Ardhi aliahidi kuja Novemba 17, lakini jana hiyo hiyo kumetokea machafuko kwa wafugaji watatu kupigwa risasi, naomba bunge lako liahirishe shughuli zake ili kujadili jambo hili kwa dharura,” amesema Sangu.

Katika hoja yake ambayo iliungwa mkono na wabunge wengi amesema kabla ya mgogoro wa jana, kuna ubakaji kwa wanawake ambapo 10 walisharipoti wake, wananchi kukatwa masikio na walinzi, mwanamke mjamzito alianguka na kupoteza maisha wakati akiwakimbia walinzi na vitendo vya kinyama wanavyofanyiwa watu ni vingi.

Akijibu tuhuma hizo, Naibu Waziri wa Ardhi, Geofrey Pinda amekiri kuwa jambo lilitokea jana na kwamba wanazo taarifa watu wawili walikimbizwa hospitali za rufaa mmoja Mbeya na mwingine hospitali ya rufaa ya Sumbawanga na kwamba hali zao kwa mujibu wa taarifa, zinaendelea vizuri ingawa mmoja wa majeruhi hao hakwenda hata hospitali.
 
Back
Top Bottom