Risasi yamkwama shingoni mtangazaji

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
CANADA: Mwandishi wa habari wa Kituo cha ABC nchini Canada, Adam Harvey amepigwa na risasi kwa makosa shingoni wakati akiripoti mapigano yanayoendelea chini Ufilipino.

Licha ya kunusurika, lakini risasi hiyo imenasa shingoni mwa mwanahabari huyo.

Leo, Harvey ametupia picha yake ya X-ray katika mtandao wa Twitter ikionyesha risasi ilivyokwama ndani ya shingo lake.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Kituo cha ABC, amesema jeraha hilo sio la kumtishia maisha.

Harvey amesema alipigwa risasi wakati akiinama kuchukua chakula kutoka kwenye gari.

“Ingawa nilikuwa nimevalia mavazi ya kujikinga dhidi ya risasi, lakini nilisikia nikigongwa na kitu nilichohisi ni kama mpira wa kriketi,” amesema Harvey.

Chanzo: Mwananchi
 
Risasi anasema kaisikilizia kama mpira wa cricket je angepigwa bomu si angeona kama kapigwa dafu changa
 
_96499872_009ad5c3-8a40-45ba-867c-1de2529d7ab4.jpg
 
Huyo ndiye muandishi wa habari, sio wangojea press releases za Msigwa.

Give that man medal already.
 
Back
Top Bottom