Wanaume wengi huwa hawana uvumilivu kwenye ndoa hasa akiona anafanya usaliti mwenzie anaona afu anapuuzia, alafu mjue mwanamke aliyeamua kuolewa akazaa watoto zaidi ya wawili afu eti awe msaliti wa mapenzi labda kama alikuwa malaya kama malaya wengine!
Speaking from my experience mume wangu alivoona nampotezea na mambo zake hata akae wiki huko simuulizi, akipiga simu ntapokea kama kuna hitaji lolote ntamwambia bila kumuuliza uko wapi au kwanini haurudi alipata hasira sana akaanza wasiwasi bila sababu kuna wakati atakuja apark gari paleee anakuja ananyata anaruka ukuta anakaa dirishani kusikilizia lakini waaapi😀😀 akaanza kuniambia kuna mwanaume anakudanganya nkamuuliza ni yupi yule? Ananiambia haiwezekani usiniulizie hata usiwe na wivu na mimi😀😀 heee nkasema we kaka yaani mie niumie kwa maamuzi uloamua mwenyewe? Alikuwa akipiga simu usiku wa manane hapo yuko kwa mchepuko akiskia sauti ya usingizi anauliza unalalaje hujui mumeo yuko wapi😡
Nikamzoea kabisa wakati mwingine atakuja hadi na condoms zimetumika kaekewa mfukoni nazikuta namuwekea pale akija anazikuta ayayaaa siku hiyo alisema ntakuua humu ndani iweje ukute yote haya na usiniulize nkamwambia ya nini nijisumbue kukupigia simu na akati ukirudi utakuta mzigo wako?
Hasira zilizidi neno kukuua lilikuwa haliishi mdomoni anatishia naenda wanaeka lock up asubuhi anatoka nkaona hii bastola itaja niua ivi ivi aaghhhr ni mengi yalienda hata ntajaza kitini nikachoka nkaondoka zangu huyooo saivi ndo sasa anaanza kujirudisha natalaka tushapeana ndo kuniambia ivi kweli
Sweet16 ulishindwa kunisamehe mpaka kunipea talaka🤣🤣🤣
Ngeng'ang'ania ndoa nahisi ngeshakufa afu wakati huo akiwa humu mjini hana safari ya kuhitaji silaha mie ndo nabaki najua naieka wapi humo chumbani afu ije iniue woooii.
On top of that kuna ka ugomvi kalijitokeza pia japo yeye hakutaka umiliki ila alinishawishi nibebee mkopo nyumba yangu (hii alinikuta nayo) nkamuiliza how come nikuchukulie mkopo kwa nyumba yangu na unazo zako? Hapo hasira ilizidi ila nia yake niliigundua ilikuwa baaada ya hapo mkopo usingerejeshwa nyumba iuzwe.
Akani shawishi sana uza viwanja basi afu tununue kwa pamoja nkatia kamgomo ila si kwa kisirani ni kwa ujanja wa kukwepa kwepa tuuu coz nshaona red flags kama zote ikaishia ivo sasa kwenye ugomvi alikuwa lazima ataje unajidai kwakuwa una hiki, namuuliza mume wangu mbona akati naolewa vilikuwepo na katika ugomvi tulionao ni wapi nimetaja kumiliki kitu flani? Yaani ilikuwa gubu tu mtindo mmoja....