HARUFU
Platinum Member
- Jan 21, 2014
- 31,704
- 48,141
Kote umepatia mkuu ila hapo kwenye Elimu nitapishana na wewe, unajua Elimu si chanzo cha kumfanya mtu awe na moyo wa kikatili.Duh! kwa mpango huo sijui tuweke tumaini letu wapi?
Tunapokosa imani na vyombo vyetu vya dola sijui tutafanyaje?
Nahisi jamaa wanalipwa mshahara kiduchu ndo maana wanakuwa na vijitamaa vikubwa vikubwa!?
Ama wanaamua kutumia rungu walilopewa!?
Ama jamaa hawajafundwa vizuri juu ya somo la uzalendo!?
Ama jamaa elimu yao ni hafifu kwa hiyo wanaona dhuruma kwao ni sawa!?
Dah! kwa kweli sijielewi elewi!
Maana kuna wakati nilisikia mkuu wao sijui anaitwa nani? naye alihusika na uporaji na akakaa jela muda kadhaa.
Mh! hii ni fedheha kaka.
Kuwa na Elimu au kutokuwa na Elimu sio tija, ni hulka za tamaa na kukosa ubinaadamu. Mtu anaweza akawa ameelimika na tabia ya unyama akawa bado yupo nayo na mtu anaweza akawa hajaelimika hata kidogo lakini akawa amejawa na ubinaadamu na hawezi fanya jambo lolote baya kumdhuru mwingine iwe kwa kutapeli, kudhulumu, kunyang'anya, kuua au kufanya baya lolote kuhusiana na cha mtu