Risasi na uporaji muda huu hapa Ukonga

Risasi na uporaji muda huu hapa Ukonga

Kova na vijana wake walikuwa busy uwanja wa taifa wanashangaa

Ulitaka wafanye nini? Tayari walishasema yeyote anayesafirsha fedha nyingi aombe ulinzi toka kwao na atapewa. Tatizo watu wanafanya mambo kwa mazoea. Kuna kampuni zinatoa hufuma za kusafirisha fedha, kwa nini hawatumii huduma hizo? Unaweza kukuta gharama ni reasonable kulinganisha na pesa anazosafirisha. Tuache tabia ya kuwalaumu polisi kwa uzembe wetu
 
baadhi ya watu wana uelewa mdogo sana...
wanaleta siasa kwenye masuala ya kutumia akili yako mwenyewe?eti unauliza polisi walikuwa wapi?...jukumu la msafirishaji wa fedha kutoa taarifa ili kupata escort ya polisi na sio ujinga wanaofanya kubeba fedha kama mandazi ukipasuliwa za kichwa wajinga waanze ooo polisi walikuwa wapi? kwani polisi ni mungu
 
Umenena yaliyo ya busara na ukweli.
Watu wamekuwa wakisafirisha fedha kimazoea ile hali zipo kampuni za ulinzi na za usafirishaji fedha.
Kwa mtu mwenye kufikiria vyema hawezi kukurupuka kulaumu polisi labda iwe ni mazoea tu ya kuropoka kutokana na mihemko ya ujinga
 
jambazi ni hero uswazi....vunja ukimya....if u keep silence u be next target.
 

however,they did a clean robbery.no one was injured or killed.kwa uhalifu kama huo,ingekuwa ni wakora wa nairobi lazima wangeuwa au kujeruhi watu si chini ya watano.kwa huko kwenyu,mhalifu wa kawaida anaweza akakupeleka kaburini kwa ksh500 tu.
 
Last edited by a moderator:
Hatari sana..ila tujipende kwa kuacha tabia za kubeba hela nyingi...solution pale ni kuomba usalama wa polisi tu..tushukuru jamaa hakupata madhara..
 
Ila lazima hata mie niamnin kuna mkono wa wanandani katka matukio ya jana na leo.
Hawa majambawaz nani anawajulisha kuwa boss flan anachukua fedha sehem.?? maana hawajawah kuvamia UDA waibe smartphone za abiria, ni boss kuibiwa mamilion.
Pia jaman, polis tunawalaum bure, ilishatangazwa ukiwa na kiwango kikubwa cha pesa, waite walinzi, watu hawakubali.
Teknolojia inakuwa, unaweza hamisha fedha kwenda na kutoka benk muda wowote online, kwann tunabebana na hiz karatas mwishowe wanipige hata mie maskini choka mbaya sina hata 10,000 kisa nawachelewesha kumuibia tajiri kwenye eneo la tukio.
CHANGE TANZANIA,.... STOP BLAMING
 
Suala la watu kubeba pesa nyingi halitaisha leo wala kesho kutokana na mfumo wa uchumi wetu ambao umejikita kwenye Cash Transactions. Ni jukumu La serikali kuhakikisha usalama wetu wakati wote na sio Jeshi La Polisi kujivua lawama.

Pengine tunahitaji kuangalia jirani zetu Kigali, Rwanda wamedhibiti vipi hali hii. Kigali ni jiji pekee ambalo mtu unaweza kutembea pasipo na hofu ya kukabwa au kuibiwa. Ikifika saa 12 jioni Serikali ya Kagame ina-deploy wanajeshi kwenye barabara kuu na major intersections kwa ajili ya kusimamia ulinzi...

Tatizo letu Tz tunapenda sana kujificha nyuma ya pazia la lawama. Matokeo yake kila mtu anamtupia mwenzie lawama na mwisho wa siku hakuna kinachofanyika. Walioko madarakani pengine wanahofia kuthubutu ku-upset the current system; lkn inafikia mahali viongozi wetu wawe na ujasiri wa kuthubutu ili kunusuru maisha yetu. Hainiingii akilini Dar, Arusha, na Mwanza kuna kambi za Jeshi zisizopungua 3 kila mji na bado wanajeshi wako makambini huku usalama wetu ukitishiwa kila kukicha. Wapo mtakaosema kwamba Jeshi ni kulinda mipaka yetu nk...lkn nafikiri bado serikali inaweza kupata 'baraka' bungeni or through presidential order na kuimarisha ulinzi ndani ya nchi kwa kutumia Jeshi.

Polisi, Tigo ni wazi wameelemewa na Hivyo jitihada za maksudi zinahitajika kukabiliana na mijizi inayoongezeka na kuua raia hadharani. Nawasilisha
 
Polisi hawawezi kujua kama unasafirisha fedha. Ni jukumu lako kuwapa taarifa ili wakupe ulinzi. Watu waache kufanya mambo /vitu kwa mazoea

Samahani endapo nikiomba ulinzi wa Polisi natakiwa kumlipa?


||Tomorrow will say its a memory and we have enjoyed our lives for couple of days||
 
Tatizo wa Tanzania somo la Insurance atujalipata kwahiyo kulipia gari la kubeba pesa zikifika salana tunaona ni hasara kwetu bila kufikiri madhara amabayo yangepatikana kama umevamiwa.

Polisi tupe elimu na hao wasafirishaji watoe elimu wati wajue umuhimu wa kutobeba pesa wenyewe.
 
Tunasisitiza kila siku kwenye vikao na wadau wa usalama pamoja na taasisi zote za fedha na Jeshi la Polisi kuwa usalama au hatari yyte huanzia ofisini kwako au nyumban. Wa kwanza kuhisi au kujua kuwa pesa inatoka leo nyumbani au ofisini ni mfanyakaz mwenzio,mwanafamilia au mlinzi ama wewe mwnyw.
Tunasisitiza kila trip ya kusafirisha pesa kutoka sehem moja had nyngne omba escort ya polisi. Inakugharim nn kutoa 20,000/- kuwalipa askar wawili mzigo wako ufike au bank branch yako iwe safe? CRDB walisema wanataka bank zao zote zilindwe na FFU..tukasema poa,then ujambaz kwny bank zao umepungua. Benki zngne na bureau de change pamoja na nyie ndo bado mnasumbua. Tujifunze kutokana na hayo matukio.
 
Ashukuru kapona nadhani siku nyingine atakumbuka kuomba ulinzi wa Askari,mzembe mwenzake kafa jana Mlimani City...

Mkuu ngoja nikuulize swali, unadhani sahihi kwa Watanzania kuishi kwa uoga?

Mathalani watu wanaoporwa na vibaka pesa ndogo ndogo, je ni uzembe wa mtu anayeporwa?
 
Si bure..., ni mawili either haujui unachoongea au unashirikiana na hawa majambazi

Mkiambiwa ukweli mnaumia sana??!!!
Kuporwa pesa ambayo haikuwa na ulinzi ni uzembe tu au kujiamini kulikopitiliza ambao pia ni uzembe
 
Tatizo wa Tanzania somo la Insurance atujalipata kwahiyo kulipia gari la kubeba pesa zikifika salana tunaona ni hasara kwetu bila kufikiri madhara amabayo yangepatikana kama umevamiwa.

Polisi tupe elimu na hao wasafirishaji watoe elimu wati wajue umuhimu wa kutobeba pesa wenyewe.

Wabeba pesa wote wanajua hatari wanayoifanya, basi tu mazoea mabaya na uzembe!!!!
 
Back
Top Bottom