Ripoti ya PCCB yafichwa kulinda familia kuu

Pasco

Endelea kulinda mafisadi, siku ya uzinduzi wa Kampeni za Ukawa majina yote na kiasi kilichochotwa Stanbic kitawekwa hadharani.

Kuanzia yule aliyebeba 9bilion na kisha kumuua yule kijana aliyetumwa na Noah nyeusi namba..... Kwenda Stanbic kubeba hizo hela na kupewa asante ya 40mililion kisha akauwa Airport masaa macheche tu baada ya kukabidhi mzigo ule.


Wee nawe kutuning'iniza roho...haya ngoja tusubiri hiyo siku mtakapoamua kutumia 'mtaji' wenu...
 
Hiyo ripoti ya PCCB imefichwa makusudi kumlinda Jk kwenye huo mgao wa escrow naye anahusika
 
PascoEndelea kulinda mafisadi, siku ya uzinduzi wa Kampeni za Ukawa majina yote na kiasi kilichochotwa Stanbic kitawekwa hadharani.Kuanzia yule aliyebeba 9bilion na kisha kumuua yule kijana aliyetumwa na Noah nyeusi namba..... Kwenda Stanbic kubeba hizo hela na kupewa asante ya 40mililion kisha akauwa Airport masaa macheche tu baada ya kukabidhi mzigo ule.
Mkuu Yeri, sio kwamba natetea mafisadi, mimi nazungumzia kitu kinachoitwa sheria, taratibu na kanuni!, nothing more, nothing less!.

Sina tatizo kabisa kwa Ukawa kuyatumia majina ya Stanbic kama mtaji wake mpya wa kunadia ilani yake ya uchaguzi!, haswa kwa kuzingatia ile single ya 'list of shame' imechuja!, cha muhimu ni this time muwe mmepewa the real thing!, naikumbuka ile story ya makotena ya kura zilizopigwa!, au ile story ya prince wetu kushikwaq China!.

Cha muhimu ambacho ningependa watu wafahamu ni kuwa majina ya miamala ya Mkombozi was a mistake!, Stanbic did the right thing kuyahifadhi!, vyombo vya uchunguzi vina access na majina hayo, hivyo kama kuna wa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, then watafikishwa tuu lakini sio kuanza kutajana majina na kuishia kuchafuana tuu!.

Pasco
 
Sioni maana ya hizi taasisi
Bora tuwe bila serikali kila mtu afanye yake tu
Kazi kula pesa zetu tunazonyonywa kodi tu
 
umechambua fresh bado swali ni jepesi mno.wanufaika wa account ya stanbic ni kina nani?
why double standards tujue tu ya mkombozi?
tukisema wakubwa wamefichwa tunakosea?
hivi nani mkubwa zaidi ya waziri????
Mkuu Ndevu Mzazi, nakuunga mkono kuwa majina yaliyotoka ni yale ya Mkombozi tuu na sio ya Stanbic, hivyo kuonekana kama ni double standard!. Ukweli ni kuwa Mkombozi kuweka wazi yale majina was a mistake!, Stanbic ndio wanafanya the right thing kwa disclosure ya account numbers tuu bila majina, ila vyombo vya uchunguzi vina access na majina!. Hatuwezi kuendelea kufanya makosa simply kwa sababu tulianza na makosa!.

Kuna kitu kinaitwa 'the right to privacy' vs 'disclosure!', benki haikutakiwa kutoa too much details hadi majina ya wateja wao,
na sio benki tuu, hata hospitali, mwalimu na mwanafunzi, daktari na mgonjwa, lawyer na mteja wake, coll records etc, access ya private information inaruhusiwa kwa maombi rasmi, na vyombo vya ulinzi na usalama vinayo hiyo access, mbona hawataji ?!. Majina yapo Tiss, Takukuru, CAG, Ikulu na BOT, ila hawawataji simly because its not right!.

Pasco
 
Ahadi ya Report ya PCCB kujadikiwa bungeni ilitolewa na waziri mkuu akihitimisha kikao cha bunge lililopita.

Waziri mkuu ni mtendaji mkuu katika muhimili ambao PCCB ipo chini yake.
Bahati nzuri au mbaya mimi sikuwahi kumsikia PM akiliahidi bunge kuileta ripoti ya PCCB bungeni!, japo nilikuwa nalifuatilia bunge ila unaweza kufuatilia na usisikie!, ninachojua bunge lilikuwa linasubiri ripoti ya CAG tuu, hiyo ripoti ya PCCB ni kama nyongeza tuu!.

umesoma sheria lkn hujui kuitafsi sheria na ndilo tatizo sugu la wanasheria wetu wengi na ndio maana wanawa mislead sana watawala.
Kwenye hii issue, hakuna hoja za kisheria ni hoja za kikanuni tuu na kiutaratibu, Bunge kama msimamizi wa serikali, lina full access ya kujua kila kitu kuhusu serikali zikiwemo confidential information au mikataba mbalimbali, vitu hivi vinaombwa kwa utaratibu maalum, lakini sio kwa lengo la kuviweka public, ndio maana Zitto kupitia kamati yake ya PAC, alilazimisha kupewa mikataba ya gesi toka TPDC, TPDC walimgomea, akawapeleka polisi, viongozi wakashikwa na kisha kuachiwa simply because Zitto hakufuata taratibu!. Serikali inaendeshwa kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni!.

Kusoma sheria ni jambo moja, kuielewa hiyo sheria ni jambo jingine, kuitafsiri nalo ni jingine na kuitekeleza nalo ni jingine kabisa!.

Pasco
 
Mkuu baada ya maelezo na maswali kadhaa uliyoulizwa na wadau mbalimbali akiwemo Yeriko Nyerere, nadhani ni busara sasa ukafuta hapo kwenye red (Watanzania tuna tatizo kubwa ya elimu ya civics!),na andika tatizo lako wewe binfsi na akina Lizaboni, Msalani and the likes.
Mkuu Chintu, nimekusikia na kuitikia wito wako, hivyo sasa nakiri wazi, Pasco wa jf, ana tatizo kubwa la elimu ya civics!.
Pasco
 
Ndo maana ukawa wako kimya hiyo ni moja ya kete wkt wa uchaguzi mwaka huu.
Itafahamika tu
 
Pasco

Makosa yaliyofanywa na mkombozi ya kutoa majina ya wanufaika wa Escrow account, Je inaweza kuwagharimu kama wahusika watakwenda mahakamani kama alivyafanya Mzee Mengi?
 
mkuu pasco unafiki unamfanya anakuwa kichwa maji wakati mwingine

RED:
Pale 'wajina' wake wa kipindi cha KITI MOTO alivyoyumbishwa..Yeye (Pasco), ilibidi amfuate ili ampe kisa kizima kilichopelekea kipindi chake hicho 'kikafa'. Alichokipata huko ni kuunganishwa kwenye kundi maalumu kwa masurufu ambayo yanamfanya aweze kutoa hoja unazoziona hapa JF.

Pasco huyu alikuwa na 'tabia sawa' na wajina wake wa kipindi cha KITI MOTO. Lakini toka 'kufa' kwa kipindi hicho, Pasco amekuwa na endelea kuhusishwa na tabia za ajabu ajabu ikiwemo na hiyo uliyompachika.
 
mkuu huyu Pasco laana ya hela aliyopewa na Lowassa inamsumbua labda naye Lowassa amemuahidi ka uwaziri siku akibahatisha kuwa raisi japo haiwezekani Lowassa kuwa Raisi
Mkuu Abdala Hasani, sikujua kumbe na wewe uliujua ule mgao wangu wa hela niliyopewa na Lowassa?!, mimi nilidhani ni siri!. Sasa imeishajulikana sijui nitafanyaje?!.

Kumbe kuna watu wameahidiwa uwaziri?!, kumbe urais wa Tanzania ni wa kubahatisha?!, pia sikujua kumbe tuna miungu watu humu jf wanaoweza kusema kwa uhakika kuwa haiwezekani fulani kuwa rais!.

Pasco
 
Pasco
Makosa yaliyofanywa na mkombozi ya kutoa majina ya wanufaika wa Escrow account, Je inaweza kuwagharimu kama wahusika watakwenda mahakamani kama alivyafanya Mzee Mengi?
Kama nilivyoeleza mwanzo, kitendo cha Mkombozi kuonyesha majina ya miamala was a mistake, waathirika wanaweza kabisa kuifungulia mashitaka Mkombozi bank wakadai fidia kwa bank ya Mkombozi kutotimiza wajibu wake kwa kukiuka vipengele vya fiduciary relationship by unnecessary disclosure hivyo kuchafuliwa majina ya baadhi ya wateja wao!.

Streng ya kesi hiyo ni yale majina ya Mkombozi yameorinate wapi, yaani ni nani aliyeya leak kwenye public domain!. Kama Mkombozi bank waliya release kwa lengo la kuvisaidia vyombo vya uchunguzi, then hii itakuwa ni defence kwao kwa sababu pale BOT kuna kitengo cha FIU ambacho kina mamlaka ya kufuatilia miamala yoyote, hivyo kama wao ndio waliomba taarifa na kui leak kwenye media, then sio kosa la Mkombozi, bali ni ujinga tuu wa Mkombozi kupeleke majina bada la accont numbers only!.

Wanashitakika, kesi inashindika na fidia inalipika!.

Pasco
 
RED:
Pale 'wajina' wake wa kipindi cha KITI MOTO alivyoyumbishwa..Yeye (Pasco), ilibidi amfuate ili ampe kisa kizima kilichopelekea kipindi chake hicho 'kikafa'. Alichokipata huko ni kuunganishwa kwenye kundi maalumu kwa masurufu ambayo yanamfanya aweze kutoa hoja unazoziona hapa JF.

Pasco huyu alikuwa na 'tabia sawa' na wajina wake wa kipindi cha KITI MOTO. Lakini toka 'kufa' kwa kipindi hicho, Pasco amekuwa na endelea kuhusishwa na tabia za ajabu ajabu ikiwemo na hiyo uliyompachika.
Duu!, Mkuu Tuji, , hapa mimi ndiye mhusika mwenyewe na sijaelewa!, jee wasiohusika?!.

Pasco
 
Yericko Nyerere

Mkuu kwa jinsi ulivyoeleza na kwa namna ninavyotambua michango yako humu jamvini, naamini usingetaka kupoteza heshima yako kwa kuambiwa umeleta habari za kizushi usizo na ushahidi nazo.
Basi mkuu kwa kudhihirisha ukweli wa habari yako na kuthibitisha kwamba ripoti umeiona mwenyewe na kuisoma taarifa zake, basi tuwekee hapahapa jamvini nasi tujiridhishe na kuwa katika wakati muafaka wa kutoa mawazo na maamuzi yetu sisi kama watanzania na wenye nchi hii.
Tuwekee haraka mkuu uepuke kejeri na dharau za kina Lizbon, Pasco nk

Huyo kishadanganya humu JF kuwa baba'ke ni Mzee Nyerere aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania. Mpaka mtoto wa Nyerere wa ukweli akaja kukana hilo. Ushahidi umo humu humu.

Pia juzi juzi alikuwa na kashfa lie humu humu JF ya kumtapeli kijana pesa laki mbili.

Huyo anaejiita Yericko Nyerere hana zaidi ni kiwanda cha uongo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Pasco,

Watu wanahoji kwa kuwa PM mtoto wa Mkulima Mzee Mizengo Pinda alisimama bungeni na kudai wameagiza CAG na PCCB kufanya uchunguzi na report zitawasilishwa na kujadiliwa bungeni. Sasa ingekuwa vizuri wewe kama mwandishi wa kuaminika ungemkosoa that time na sisi tungeemini hayo unayoyasema.

On the other hand, haiingii akilini MP aagize uchunguzi hadharani halafu report ije iwe siri. hatukuwahi kusikia uchunguzi wa escrow wa BOT, TISS au Ikulu hivyo itakuwa vigumu sana kuhoji report zao.

Maadamu Wadanganyika tushakubali kuwa kila kitu ni siri ya serikali basi na tuache iwe hivyo. Wenzetu enquiry kama hiyo huwa inakuwa live kwenye TV .......................... no wonder mpaka leo Chenge ana ubavu wa kututengenezea katiba. Bongo hiyo!!
Mkuu Zero, ni kweli Pinda aliiagiza CAG na PCCB wafanye uchunguzi ila sijui kama aliahidi kuziwasilisha ripoti zote bungeni, ila nijuavyo mimi, ripoti ya CAG ndio imewasilishwa bungeni na ripoti ya PCCB imepelekwa kwa Pinda kamati ya PAC ikapewa kama rejea!.

Kumeundwa tume ngapi za uchunguzi, ripoti zao zote umewahi kuziona au kuzisikia?!. NB, usichangale kitu kinachoitwa Kamati Teule ya Bunge na Tume za Uchunguzi!, kamati teule ripoti zake ni wazi na zinawasilishwa bungeni, ripoti nyingine zote za uchunguzi matokeo yake huwa siri na zinawasilishwa kwa aliyehitaji huo uchunguzi, kisha yeye ndie aamue aweke wazi au laa!.

Pasco
 
Lakini inaleta tija gani kwa Taifa kama wizi ni CONFIDENTIAL? Ripoti inayohusu ubadhirifu ni Confidential kwa maslah ya nani? Wewe leo ukiiba million 2 halafu ukachunguzwa je hutapelekwa mahakamani? Lakini hili la Stanbic Bank linatia mashaka.

Lakini siku moja najua itakuja kujulikana who were actual beneficiaries katika muamala wa Stanbic. Tuepuke kuishi katika maisha ya Double Standard.
Mkuu Chaza, kwenye escrow hakuna wizi wowote ndio maana hakuna aliyepelekwa mahakamani kwa wizi!.
Banking transaction ni confidential kama ilivyo call record kwenye simu yako. Vyombo husika vina all the access na all classified information, hivyo majina ya Stanbic yako ila not for public consumption!.

Pasco
 
Pasco: [PCCB ni chombo cha dola sambamba na jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi na usalama, hivyo ripoti zake hazijadiliwi bungeni!. Ripoti inayojadilika bungeni ni ripoti ya CAG!. Ripoti ya PCCB ni 'closed document', yaani ni confidential!./QUOTE]

Ripoti ya CAG imejadiliwa bungeni, Je CAG si chombo cha dola? Tofauti kati ya CAG na Jeshi la Polisi ni ipi? Kama ripoti ya PCCB haiwezi jadiriwa bungeni wakati ripoti yake imetokana na msukumo na maamuzi ya bunge then Yooooote ni ubatili. Uwazi na Utawala bora havipo!
 
Pasco: [PCCB ni chombo cha dola sambamba na jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi na usalama, hivyo ripoti zake hazijadiliwi bungeni!. Ripoti inayojadilika bungeni ni ripoti ya CAG!. Ripoti ya PCCB ni 'closed document', yaani ni confidential!./QUOTE]

Ripoti ya CAG imejadiliwa bungeni, Je CAG si chombo cha dola? Tofauti kati ya CAG na Jeshi la Polisi ni ipi? Kama ripoti ya PCCB haiwezi jadiriwa bungeni wakati ripoti yake imetokana na msukumo na maamuzi ya bunge then Yooooote ni ubatili. Uwazi na Utawala bora havipo!
Jitume, serikali ina mihimili mitatu inayojitegemea, kila mmoja ukiwa na wajibu na mamlaka yake ambayo haipaswi kuingiliwa na mhimili mwingine!. Kuna Bunge, Serikali na Mahakama. Vyombo vyote vya dola viko chini ya serikali, ikiwemo PCCB, Ofisi ya CAG, Jeshi, Polisi, Tiss etc. Kwa vile moja ya majukumu ya Bunge ni kuisimamia serikali, hivyo Bunge lina manlaka ya kuuliza chochote kuhusu chombo chochote cha serikali, ila haliwezi kuuliza direct to PCCB kwa sababu PPC ni answerable kwa serikali na sio answerable kwa bunge!. Serikali ndio iko answerable kwa bunge, hivyo bunge au mbunge yoyote anao uhuru wa kuuliza swali lolote kwa serikali kuhusu jambo lolote na wanajibiwa kupitia mawaziri husika!.

Ripoti za vyombo vya serikali Polisi, PCCB, Tiss, zinaishia serikalini, haziwasilishwi bungeni!, ripoti zinazowasilishwa bungeni ni ripoti ya CAG!. Hata hivyo serikali inaweza kuamua kuwasilisha bungeni contents za ripoti yoyote ya uchunguzi kuhusu jambo lolote kupitia kauli za mawaziri, hivyo serikali ikiamua contents za ripoti ya PCCB ziwasilishwe bungeni, then waziri husika angetoa "kauli za mawaziri".

Hoja ya kukataliwa kujadiliwa tena kwa escrow ni kwa mujibu wa kanuni kuwa jambo likiisha jadiliwa na bunge na kukamilishwa kwa azimio la bunge, utekelezaji ni kwa serikali na haipangiwi lini or how, ila kanuni zinalizuia bunge kuibua tena jamba hilo chini ya muda wa mwaka mmoja!. Na maazimio ya bunge kwa serikali yanahesabiwa tuu kama maoni su ushauri, they are not binding kuilazimisha serikali kutekeleza!.

Watanzania tunapaswa tufunzwe ipasavyo "The doctrine of separations of powers and checks and balances!" between state organs!.

Pasco
 
Back
Top Bottom