Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Mnyika,
Kwa mtaji huu wa uamsho mpya unaniambia kuwa mtaondokana na Kamati na Halmashauri Kuu kufanya maamuzi yote ya kiutendaji katika kata, wilaya na Mikoa?
Jee wnaotaka kugombea uchaguzi katika Kata, Wilaya na Mikoa hawatakuwa na hofu ya majina yao kuchujwa kwenye kikao cha siri cha "Wateule"?
Ni nguvu gani wenyeviti wa Chama wa Mikoa walizonazo katika maamuzi ya Kitaifa na uongozi wa Chama Kitaifa?
Je Watendaji wa Chama katika Wilaya na Mikoa watakuwa huru kuchaguliwa na wanachama wao au watakuwa ni Wateule wa Mwenyekiti na kamati yake?
Je Katiba yenu inasemaje kuhusu kutenganisha kofia? Does the Chairman have to be Presidential Candidate? je Kutafuta Ugombea uraisi, maamuzi ni ya wanachama kupitia nguvu zao za kata, wilaya na mikoa au kila kitubado kitakuwa rolled up to Kamati na halmashauri Kuu ambazo zitawasilisha majina ya mchujo kwa Mkutano Mkuu?
Je hata kama mtabakia na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, mchujo wa wagombea uwakilishi kupitia Chadema utaachwa kwa ngazi husika au kwa wagombea waliopita michujo yote kujinadi mbele ya Mkutano Mkuu na si "Wateule" kuchuja na kuweka watu wanaowataka?
Tuendelee kuelimishana!
Simfahamu huyu Mnyika isipokuwa tu kwa kumsoma hapa, lakini kwa ambayo nimeshasoma toka kwake tayari naona ni mtu makini sana katika anayoyafanya. He sounds intelligent, organised and very well composed. Kila siku zinavyoenda na ninavyosoma post zake humu ndani, namwona anavyozidi kukua siku baada ya siku, yani ukisoma alichoandika mwezi huu utaona kina ukomavu kuliko mwezi uliopita, ni hazina ya ajabu huyu jamaa. Sijui umri wake huyu jamaa, lakini natamani kuona CHADEMA ikikua kwa rate ya huyu jamaa, na kama hili likitokea kuna matumaini mazuri mbeleni ya kupata mifumo mbadala ya kuongoza nchi. Sijajua pia kama yuko hivyo kwa sababu ya uzuri wa chama (maana yake na wanachama wengine wengi wako hivyo pia), au ni personal attributes na qualities zake (ambazo pia CHADEMA inaweza kuzitumia vizuri kujenga chama chao).
Kwa ujumla namtakia heri ndugu Mnyika, na kumtaka aendelee kutumia kipaji alichojaliwa pamoja na wenzie huko kwenye CHADEMA, watupatie matumaini kuwa mabadiliko ya serikali yanawezekana na mbadala upo (maana wako wengi wanaochagua CCM kwa kukosa viable alternatives).
Mnyika kweli anajitahidi, lakini namshauri akae na wazee karibu sana hata wa CCM/TANU/ASP/HIZZIB/ZPPP/CUF/PPT/MAKINI kupata uzoefu namna ya kulainisha mambo,,, kwa kuwa CHADEMA kikiwa chama kikubwa ukumbuke misuguano haitaepukika,,, sasa wanatakiwa walioandaliwa kuweza kulainisha na kwenda mbele!!!
Kuna Moja tu ninalo liona, siasa sio Rocket Science,,, kijana yeyote mzuri, mwenye exposure kama ya Mnyika kwenye mambo ya Kitaifa na Kimataifa anaweza kushaini kwenye siasa za sasa ambazo zimekuwa chini ya Wazee kama Kingunge, na wengineo mradi tu akubali kwamba primary occupation yake iwe siasa!!! hapa utaonekana Kipanga...
Sina ufahamu zaidi wa Historia ya Mnyika other than,,, kujichanganya kwenye mambo ya Vijana wa kitaifa na Kiafrika na ile issue ya Ubungo!!!
Mtu ambaye mimi binafsi namkubali bila matatizo yoyote ni Kitila Mkumbo,,, unapokuwa President kwenye institution yenye demokrasia ya hali ya juu hapa nchini kama ile ya DARUSO,,, pale ni sehemu nzuri sana ya kujua huyu ni Kiongozi au La... Najua hashaini kwa kuwa Kitila inaonyesha anakazi nyingine Primary na Siasa ni by the way, au kazi ya Pili,,, lakini Lau siasa ingekuwa his primary JOB... mambo yangekuwa mengine!!!
Infact mtanisamehe lakini nina haki ya kutoa maoni yangu!!! Kitila Mkumbo ni Zaidi ya hata Zitto, as I said ni kwa kuwa mguu ndani, mguu nje!!! na wakati mwingine ni vyombo vimekujenga?
Kuna siku moja mchangiaji mmoja alisema Pro. Issa Shivji apewe kesi,,, anasahau kwamba kufundisha na ku-practise ni vitu viwili tofauti,,, Maprofessa ni watu wanaamini kwenye taaluma na nadharia,,, lakini kwenye vitendo/practises mara nyingi ni Vilaza wa hali ya juu sana. Ndio maana kwenye makampuni yanayotafuta faida, hata kwenye idara zao za R&D unakuta ni mara chache sana kuna maprofessa huko!!!!
Kwa hiyo Mnyika na Zitto waanapractise ndio maana wanaonekana kazi zao, kuna vijana wengi vipanga kwa maana hata shuleni hawajaunga unga na pia vichwani wako fiti sana but hawana platform ya kutokea,,, kwenye taifa makini huwa wanatafutwa na kupelekwa sehemu stahiki!!!
Kaka Kilitime
Naomba turejee kwenye mjadala mama "CHADEMA Must Reform". Naona sasa tunaelekea kujadili nani ana 'pua ndefu' kati ya Kitila, Mnyika na Zitto....(mzaha)
Tuendelee kujadili.
Nasubiri Rev. Kishoka na wengine waje na hoja za ziada kuhusu maboresho ya CHADEMA.
JJ
Mnyika,
Pamoja na maelezo mazuri yaliotolewa hapo juu kukusifia- na wewe kujitetea kuwa kwa sasa umejitoa kutengeneza 'Tz Mbadala'- hii ni 2007 na uchaguzi ni 2010- pamoja na kuwa hili ni jukumu binafsi- je una nia gani ya kusoma zaidi za kupata exporure ktk Party politics? International Relations? n.k?
Tunaona Mbowe anasoma kwa sasa Hull- na elimu haina mwisho- kumbuka elimu ya ngazi fulani ni tam na ina manufaa sana ktk umri fulani!
Una maoni gani kwa hilo?
Mnyika, Kilitime
Nafikiri ni wakatiumewadia kuwa tunabadilisha mwelekeo wa fikira zetu na nguvu za ushawishi na kuwa ni nguvu za kujenga Taifa na si kuhoji tuu yaliyotokea.
Nimeipitia katiba ya Chadema jana ni nzuri. Nikajiuliza mfumo wake na kama Mnyika navyoelezea hapa inaelekea ni mzuri. Sasa tatizo ni lipi kuwa haina wafuasi wengi hasa vijana na wanataaluma? au ni kwa kuwa wengi wanaogopa mkono wa dola (CCM)?
Kikubwa ambacho kinakera ni kwa Chama cha upinzani chenye nguvu kama Chadema kuonekana kina kosa uadilifu kama CCM. Na hii inatokana na hisi azilizojengeka tangu awali eti n Chama cha Wachaga na kuna ukabila na undugunization.
Ndio maana nikasema, ili Chadema kiwe kamilifu (at least 85%) inabidi kibadili mfumo wake wa kiutendaji na utawala na isionekane kuwa hiki ni chama cha Mtei na mkwewe Freeman.
Nimefurahia jinsi Mnyika ulivyo na uamsho na imani katika chama chako, swali ni jee ni wangapi katika chama Chako wenye mtazamo kama wako?
Jumuiya yenu ya vijana ina nguvu kiasi gani kupambana na Nchimbi na wafuasi wake? Nguvu ninazoulizia ni za mfumo wa utandawazi, mawazo, kujitolea na uhamasishaji si nguvu za fedha ambazo najua Chadema haina kufananisha na Chama Cha Machotaji!
Ni tumaini langu kuwa kama Chadema itaongeza mwendo kasi wake wa reforms and si kusua sua, basi mnaweza kupata japo 15% ya viti vya Bunge.
Reformation ya Chadema ni lazima iende kwa slogan ya Kikwete, Ari, Kasi na Nguvu mpya. Nafikiri mkiendelea kuchelea kufanya kweli ili kwenda na wakati na kupambana na ufidhuli wa CCM, basi itawachukua miaka 46 kufika mahali CCM ilipo leo kimuundo na kiutandawazi.
Nashukuru. Nia ninayo. Soma maelezo yangu katikati ya mstari, ndio maana nimesema bado kitambo kidogo nitatoweka. Tuendelee kujadili "CHADEMA must reform"
JJ
Mnyika,
Hivi unaweza kuturushia CV yako? Au kama iko kwenye mtandao basi ninaiomba link yake. Samahani kwa usumbufu.
Kaka
Sijui ni CV kwa ajili gani kwa kweli, maana zipo za namna mbalimbali. Ila kama ni kwa lengo la kupata wasifu tu unaweza kubonyeza hapa: http://www.chadema.net/uongozi/taifa/mnyika.php au hapa: http://www.esrftz.org/BUDGET/CORU_out2_inc_archive.asp?Id=1066&Year=2005 , japokuwa naona zote ni za nyuma kidogo lakini naona zinaweza kukusaidia. Alternatively, just google search.
I hope i has nothing to do with "CHADEMA must reform"
JJ
Baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka 2001,alijiunga na chuo cha diplomasia cha jijini Dar es salaam katika kozi ya itifaki na mahusiano ya jamii. Baadaye aliajiriwa na Redio Tanzania Dar es salaam (RTD) katika kitengo cha PRT na kufanya kazi ya utangazaji kwa mwaka mmoja. Akiwa RTD bado aliendelea na harakati za vijana kupitia NYF mpaka taasisi hiyo ilipofutwa na serikali. Aliendelea pia na harakati za utetezi wa wanafunzi kupitia mtandao wa wanafunzi Tanzania 'TSNP'ambayo yeye ni mmoja wa waanzilishi wake.
Alijiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) mwaka 2002 kusoma shahada ya kwanza ya utawala wa biashara (BBA) katika programu ya jioni. Sambamba na masomo ya jioni katika chuo kikuu cha Dar es salaam, ameendelea kuwa muajiriwa wa United Nations Association (UNA) kama mratibu msaidizi wa mradi wa ushiriki wa vijana unaotekelezwa na kitengo chake cha vijana (YUNA) katika wilaya kumi nchini Tanzania.
JJ,
Chama ni wanachama na viongozi, na wasifu wa viongozi na wanachama wanafanya chama kiwe na sura fulani, hivyo kuwajuwa wanachama/viongozi ni haki ya wananchi ambao wataongozwa na viongozi na wananchama hao especially pale chama husika kitakapochukua dola!!!
kwa hiyo niruhusu kidogo niulize swali kwenye wasifu wako!!!
Kuna disconnect moja kidogo pale kwenye form six kwenda chuo kikuu... kama ulivyoweza weka vizuri matokeo yako ya Darasa la Saba na Darasa la Kumi na mbili tunaomba ugusie kidogo matokeo ya darasa la kumi na nne!!! naona kuna-ka-disconnect kidogo mkuu... natanguliza msamaha...