'Ripoti' ya Mziray na Mabadiliko ya Chadema kuelekea 2010

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,530
Political structure of Chadema resembles CCM! It stinks!

For CHADEMA to be effective on its drive to bring mageuzi, it needs to revamp its leadership structure and organization.

What Chadema has done is to follow the leadership structure and organization blue print of CCM inch by inch. As a result of this, it has failed to separate itself from CCM and thus being ineffective to bring solid changes to political spectrum fo Tanzania!

Mageuzi si kuingia Ikulu pekee, bali ni mabadiliko ya mfumo mzima wa siasa na uendeshaji wake. Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, kinabidi kiwe cha kwanza kufanya hivyo,ndipo wengine watafuatilia na Wananchi wanweza kuanza kutofautisha Pumba na Mchele.

Nimewahi kuhoji miaka kadhaa iliopita kuwa siasa za Tanzania ni za mrengo gani baada ya Azimio la Zanzibar na kuja Mageuzi, sikupata jibu la maana zaidi ya watu kudai sisi sasa ni Mabepari na tuna Siasa za vyama vingi!

Mwanzo wa kweli wa mageuzi ya Siasa za Tanzania, utaanzia kwenye mabadiliko ya mfumo na miundo ya vyama vya siasa.

Chadema kiwe cha kwanza kuondokana na mfumowa ki-CCM ambao umelea tabaka la kundi maalum kutawala daima na kufanya maamuzi kwa Taifa zima (wanachama wake)!

Mbowe alipata bahati kuja Marekani wakati wa Uchaguzi wa 2004, je alijifunza yapi? je aliona mkutano mkuu wa chama kupitia kamati kuu na halmashauri kuu za Republican au Democrats zikipanga ni nani awe mgombea uwakilishi wa jimbo u uraisi? Nope!

Structure ya kwetu ni ya Kikomnisti, ile ile ya Wachina, Korea na hata Urusi. Sasa ni vipi mifumo hii ya utendaji italeta maendeleo na demokrasia ya kweli ikiwa Wenyeviti wa Vyama na wale "wateule wakuu" wanapewa nguvu za kufanya maamuzi makubwa kwa kutumia nyadhifa zao?

Kwa mnaoishi Marekani, mwaelewa mfumo wa siasa za vyama. Nguvu za chama na wawakilishi zipo majimboni na si Mkutano Mkuu au Kamati na Halmashauri Kuu!

Ikiwa Chadema itakubali mawazo yangu na kubadilisha mfumo wake ambao umeanza kuleta migooro na ulalamishi wa upendeleo, ukabila, udini na udugu na kuachia nguvu za wawikilishi kukamilishwa na wanachama wake katika ngazi za kata, wilaya hata mkoa, hapo ndipo mageuzi ya kweli katika siasa za Tanzania yatatoka na hiyo itakuwa njia pekee ya kuleta Demokrasia na Maendeleo kwa Taifa.

Mbowe, Slaa, Zitto, Mnyika, Makani, nasubiri vitendo!
 
Last edited by a moderator:
Rev. Kishoka

Kuhusu mageuzi ndani ya CHADEMA tulishaitika mwito huo tayari; mara baada ya uchaguzi mkuu 2005 tulifanya tathmini ya kina na hatimaye tukaandaa Mpango Mkakati(Strategic Plan) ya miaka mitano. Kama sehemu ya Mpango huo tukaamua kubadili Katiba ya chama na kuchukua muundo tofauti kidogo(unaweza kuitazama kupitia www.chadema .net) na kuilinganisha na ya CCM. Ndio maana baada ya hapo tuliamua kuzindua chama upya( bonyeza hapa utapata maelezo yangu kuhusu uzinduzi huo na ni kwa vipi unakifanya CHADEMA kuwa chama tofauti na CCM):

http://www.chadema.net/blogu/mnyika/2006/09/dokezo-kuhusu-uzinduzi-mpya-wa-chadema.html

Kwa hiyo uliyoyaona yametokea 2007 ni matokeo ya mipango na malengo sio bahati nasibu.

Mwaka 2008 ni mwaka wa uchaguzi ambapo tutaunda oganizesheni ya chama kuanzia ngazi ya msingi mpaka taifa, na hata kimataifa; na tutafanya hivi mijini na vijijini. Ni changamoto kwa wanaCHADEMA sasa kuifahamu ratiba husika na kushiriki michakato hii ya uchaguzi na kujenga chama katika maeneo yao.

Kwa kweli tumeamua kabisa kupeleka nguvu zaidi majimbo na hata kupanua uwakilishi wa majimbo kwenye baraza kuu; lakini nguvu za kichama sasa ni katika vitovu vya kimapambano.

Ni hatua nzuri; naamini mabadiliko yanayofuata ya katiba yatatoa mamlaka zaidi kwa ngazi za chini katika kujitawala; ila katiba hii mpya ya mwaka 2006 naamini itawezesha kuwa na muundo na mfumo bora zaidi. Haionekani sasa kwa kuwa mpaka sasa bado tunatumia katiba ya mwaka 2004. Katiba mpya itaanza kutumika mwaka 2008 mara baada ya uchaguzi. Kwa meneno mengine, uchaguzi utakaonza mwezi Februari utaendeshwa kwa katiba mpya ya CHADEMA ambayo imeshazingatia sehemu ya ushauri ambao umeutoa.

Lakini kazi hii si ya kina Mbowe, Makani, Zitto na Mnyika pekee. Ni yako pia wewe na yule. Pamoja tutashinda.

JJ
 
Mnyika,

Kwa mtaji huu wa uamsho mpya unaniambia kuwa mtaondokana na Kamati na Halmashauri Kuu kufanya maamuzi yote ya kiutendaji katika kata, wilaya na Mikoa?

Jee wnaotaka kugombea uchaguzi katika Kata, Wilaya na Mikoa hawatakuwa na hofu ya majina yao kuchujwa kwenye kikao cha siri cha "Wateule"?

Ni nguvu gani wenyeviti wa Chama wa Mikoa walizonazo katika maamuzi ya Kitaifa na uongozi wa Chama Kitaifa?

Je Watendaji wa Chama katika Wilaya na Mikoa watakuwa huru kuchaguliwa na wanachama wao au watakuwa ni Wateule wa Mwenyekiti na kamati yake?

Je Katiba yenu inasemaje kuhusu kutenganisha kofia? Does the Chairman have to be Presidential Candidate? je Kutafuta Ugombea uraisi, maamuzi ni ya wanachama kupitia nguvu zao za kata, wilaya na mikoa au kila kitubado kitakuwa rolled up to Kamati na halmashauri Kuu ambazo zitawasilisha majina ya mchujo kwa Mkutano Mkuu?

Je hata kama mtabakia na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, mchujo wa wagombea uwakilishi kupitia Chadema utaachwa kwa ngazi husika au kwa wagombea waliopita michujo yote kujinadi mbele ya Mkutano Mkuu na si "Wateule" kuchuja na kuweka watu wanaowataka?

Tuendelee kuelimishana!
 
Simfahamu huyu Mnyika isipokuwa tu kwa kumsoma hapa, lakini kwa ambayo nimeshasoma toka kwake tayari naona ni mtu makini sana katika anayoyafanya. He sounds intelligent, organised and very well composed.

Kila siku zinavyoenda na ninavyosoma post zake humu ndani, namwona anavyozidi kukua siku baada ya siku, yani ukisoma alichoandika mwezi huu utaona kina ukomavu kuliko mwezi uliopita, ni hazina ya ajabu huyu jamaa. Sijui umri wake huyu jamaa, lakini natamani kuona CHADEMA ikikua kwa rate ya huyu jamaa, na kama hili likitokea kuna matumaini mazuri mbeleni ya kupata mifumo mbadala ya kuongoza nchi.

Sijajua pia kama yuko hivyo kwa sababu ya uzuri wa chama (maana yake na wanachama wengine wengi wako hivyo pia), au ni personal attributes na qualities zake (ambazo pia CHADEMA inaweza kuzitumia vizuri kujenga chama chao).

Kwa ujumla namtakia heri ndugu Mnyika, na kumtaka aendelee kutumia kipaji alichojaliwa pamoja na wenzie huko kwenye CHADEMA, watupatie matumaini kuwa mabadiliko ya serikali yanawezekana na mbadala upo (maana wako wengi wanaochagua CCM kwa kukosa viable alternatives).
 
Mnyika,

Kwa mtaji huu wa uamsho mpya unaniambia kuwa mtaondokana na Kamati na Halmashauri Kuu kufanya maamuzi yote ya kiutendaji katika kata, wilaya na Mikoa?

Jee wnaotaka kugombea uchaguzi katika Kata, Wilaya na Mikoa hawatakuwa na hofu ya majina yao kuchujwa kwenye kikao cha siri cha "Wateule"?

Ni nguvu gani wenyeviti wa Chama wa Mikoa walizonazo katika maamuzi ya Kitaifa na uongozi wa Chama Kitaifa?

Je Watendaji wa Chama katika Wilaya na Mikoa watakuwa huru kuchaguliwa na wanachama wao au watakuwa ni Wateule wa Mwenyekiti na kamati yake?

Je Katiba yenu inasemaje kuhusu kutenganisha kofia? Does the Chairman have to be Presidential Candidate? je Kutafuta Ugombea uraisi, maamuzi ni ya wanachama kupitia nguvu zao za kata, wilaya na mikoa au kila kitubado kitakuwa rolled up to Kamati na halmashauri Kuu ambazo zitawasilisha majina ya mchujo kwa Mkutano Mkuu?

Je hata kama mtabakia na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, mchujo wa wagombea uwakilishi kupitia Chadema utaachwa kwa ngazi husika au kwa wagombea waliopita michujo yote kujinadi mbele ya Mkutano Mkuu na si "Wateule" kuchuja na kuweka watu wanaowataka?

Tuendelee kuelimishana!

Rev. Kishoka

Nimeambatanisha Katiba ya CHADEMA- isome halafu tuendelee kuelimishana.

Utaona kwa katiba hii mamlaka ya maamuzi yapo kwenye chama ngazi husika kuhusiana na yale mambo ambayo yanahusu ngazi hiyo. Utanona kwamba hapo kwamba chama hakiendeshwi na 'wateule wachache'! Chama ni cha wananchama kupitia vyombo vyao vya maamuzi. Ngazi ya juu inaingilia ngazi ya chini kama tu kuna masuala yamekiukwa.

Hii katiba kuna mambo yapo humo ni ya mpito, naamini siku za baadaye tutafanya mabadiliko mengine makubwa zaidi- baadhi ya miundo ipo kama hatua za awali za kuitambulisha na baadaye itakuja kupewa nguvu zaidi katika mabadiliko yajayo. Katika mabadiliko ya mwaka 2006 tulikuwa makundi matatu ya mawazo(sio kambi): wapo waliokataa mabadiliko, wapo waliotaka mabadiliko kiasi na wapo waliotaka mabadiliko makubwa kupindukia.

Katiba unayoiona ni compromise ya makundi yote matatu; ukiona katiba ya 2004 ukalinganisha na hii utaelewa nasema nini. Na kwa kweli ilikuwa kazi ngumu kufanya haya mabadiliko kwa kuwa binadamu wengi kwa asili ni watu wa mazoea na hivyo kuhofia mabadiliko- karibu mchakato huu utuzalishie migogoro lakini kwa kuwa tulihusisha wanachama kwa kupata maoni yao kuanzia chini tulipata uhalali wa hoja za kufanya yaliyofanyika!

Hivyo wazo la local parties kuwa autonomous kama ilivyo baadhi ya nchi duniani nalo lilijitokeza, lakini zingine zilionekana ni radical reforms sana ukilinganisha na mazingira ya kisiasa ya Tanzania- hivyo ililbidi kuwa makini kuepuka institutional crush! Unaweza kujiuliza ilikuwaje tukaweza kukubaliana kubadili rangi za bendera na kuzindua chama upya?

Against uniforms and bendera ambazo tayari zilikuwa zimesambaa? Kwa hiyo, kwangu mimi huu ulikuwa mwazo mzuri wa reforms- tutaendelea zaidi katika awamu itakayofuata ya mabadiliko ndani ya chama.

Kwa katiba hii watu wako huru kuchaguliwa na wanachaguliwa na wengi. Katiba iko kimya kuhusu kutenganisha kofia kwa hiyo si lazima uwe mwenyekiti kuwa mgombea Urais na si lazima Rais awe Mwenyekiti.

Katiba imedokeza mchakato wa mchujo; lakini haijaingia kiundani sana. Kuna mambo mengine yapo kwenye taratibu- kwa mfano, kabla ya kamati kuu, baraza kuu na mkutano mkuu- tunafanya kwanza primaries kama ilivyo Marekani ili kushindanisha wanaotaka kugombea Urais ambao wanachama wana haki ya kuchagua wampendae- kwa hiyo mapendekezo ya jina kwa National Congress yanategemea Primaries- So far ni CHADEMA pekee ndio inatumia mfumo huu Tanzania!

Kuna nyaraka nyingine muhimu ambazo ni vyema zikasomwa baada ya kusoma katiba: Kanuni, Itifaki na Maadili; Taratibu za Mabaraza ya Wanawake, Wazee na Vijana Nk. Ukisoma mambo yote haya utabaini kwamba CHADEMA ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Karibu

JJ
 
Attachments

  • katiba_2006.pdf
    76.9 KB · Views: 385
Simfahamu huyu Mnyika isipokuwa tu kwa kumsoma hapa, lakini kwa ambayo nimeshasoma toka kwake tayari naona ni mtu makini sana katika anayoyafanya. He sounds intelligent, organised and very well composed. Kila siku zinavyoenda na ninavyosoma post zake humu ndani, namwona anavyozidi kukua siku baada ya siku, yani ukisoma alichoandika mwezi huu utaona kina ukomavu kuliko mwezi uliopita, ni hazina ya ajabu huyu jamaa. Sijui umri wake huyu jamaa, lakini natamani kuona CHADEMA ikikua kwa rate ya huyu jamaa, na kama hili likitokea kuna matumaini mazuri mbeleni ya kupata mifumo mbadala ya kuongoza nchi. Sijajua pia kama yuko hivyo kwa sababu ya uzuri wa chama (maana yake na wanachama wengine wengi wako hivyo pia), au ni personal attributes na qualities zake (ambazo pia CHADEMA inaweza kuzitumia vizuri kujenga chama chao).

Kwa ujumla namtakia heri ndugu Mnyika, na kumtaka aendelee kutumia kipaji alichojaliwa pamoja na wenzie huko kwenye CHADEMA, watupatie matumaini kuwa mabadiliko ya serikali yanawezekana na mbadala upo (maana wako wengi wanaochagua CCM kwa kukosa viable alternatives).

Kithuku

Heshima yako, naamini kabisa utakuwa umenizidi umri- nimefarijika na maneno yako.

Maisha ni kukua katika kila pumzi tunayoendelea kuvuta. Maisha ni kujifunza toka kwa kila mtu- kujifunza mazuri na mabaya, na kufanya maamuzi sahihi. Maisha pia ni kufundisha kwa maneno na vitendo. The golden rule!

Wengine kwa sasa tumeamua kujitoa kafara kwa muda kujenga chama mbadala, uongozi mbadala, sera mbadala, siasa mbadala na Tanzania mbadala. Tunapoteza mengi kwa kufanya hivi kwa sasa, lakini tunajaribu kutazama mbali zaidi. Tunafanya hivyo kwa kuwa tunaamini hivyo vya binafsi tunavyovipoteza kwa sasa, tuna uwezo wa kuvipata wakati ujao- pamoja na kuwa wakati ni ukuta. Lakini hivi tunavyovifanya sasa, ndivyo umma una hitaji kwa sasa. Taifa letu liko katika mtanziko, linahitaji mfumo mbadala. Kama kila mtu atakimbia kutekeleza wajibu huu, hakika historia itakuja kutuhukumu. Lakini kama tukitimiza jukumu hili vizuri, hakika historia itakuja kutuheshimu.

Niliona chama mbadala kupitia CHADEMA, na sasa naliona Tumaini Jipya. Lakini ni wazi chama hiki mbadala inabidi kiboreshwe kuwa mbadala uliobora, na kazi hii haiwezi kufanywa tu kwa kunyoosha vidole kwa mbali. Hatupaswi tu kuomba mambo yatokee ama kushabikia yakitokea, tunapaswa kufanya yatokee. CHADEMA inahitaji kuungwa mkono na wewe na wengine, bahari ni muunganiko wa matone ya maji. Kama matone hayo ya maji yasingekuwa pamoja asingekuwa bahari!

Kwangu mimi yote ninayofanya sasa ni wito, nafanya yote kwa nia ya kutumikia na kutumia vizuri talanta kwa ajili ya mridhiko wa nafsi na maslahi ya wengi. Nayaweza yote haya katika yeye anitiaye nguvu. Bado kitambo kidogo nitatoweka, lakini ni baada ya kutimiza wajibu kwanza. Na kweli hata kutoweka kwangu kutakuwa kimwili tu, roho yangu itaendelea kusimama kidete kuona chama mbadala kinachukua dola Tanzania ili viongozi bora waunganishe nguvu ya umma kutumia rasilimali ambazo Mungu ametujalie kwa manufaa ya kizazi chetu na vijavyo. Nashukuru, tuendelee kuombeana kila la kheri

JJ
 
Mnyika kweli anajitahidi, lakini namshauri akae na wazee karibu sana hata wa CCM/TANU/ASP/HIZZIB/ZPPP/CUF/PPT/MAKINI kupata uzoefu namna ya kulainisha mambo,,, kwa kuwa CHADEMA kikiwa chama kikubwa ukumbuke misuguano haitaepukika,,, sasa wanatakiwa walioandaliwa kuweza kulainisha na kwenda mbele!!!

Kuna Moja tu ninalo liona, siasa sio Rocket Science,,, kijana yeyote mzuri, mwenye exposure kama ya Mnyika kwenye mambo ya Kitaifa na Kimataifa anaweza kushaini kwenye siasa za sasa ambazo zimekuwa chini ya Wazee kama Kingunge, na wengineo mradi tu akubali kwamba primary occupation yake iwe siasa!!! hapa utaonekana Kipanga...

Sina ufahamu zaidi wa Historia ya Mnyika other than,,, kujichanganya kwenye mambo ya Vijana wa kitaifa na Kiafrika na ile issue ya Ubungo!!!

Mtu ambaye mimi binafsi namkubali bila matatizo yoyote ni Kitila Mkumbo,,, unapokuwa President kwenye institution yenye demokrasia ya hali ya juu hapa nchini kama ile ya DARUSO,,, pale ni sehemu nzuri sana ya kujua huyu ni Kiongozi au La... Najua hashaini kwa kuwa Kitila inaonyesha anakazi nyingine Primary na Siasa ni by the way, au kazi ya Pili,,, lakini Lau siasa ingekuwa his primary JOB... mambo yangekuwa mengine!!!

Infact mtanisamehe lakini nina haki ya kutoa maoni yangu!!! Kitila Mkumbo ni Zaidi ya hata Zitto, as I said ni kwa kuwa mguu ndani, mguu nje!!! na wakati mwingine ni vyombo vimekujenga?

Kuna siku moja mchangiaji mmoja alisema Pro. Issa Shivji apewe kesi,,, anasahau kwamba kufundisha na ku-practise ni vitu viwili tofauti,,, Maprofessa ni watu wanaamini kwenye taaluma na nadharia,,, lakini kwenye vitendo/practises mara nyingi ni Vilaza wa hali ya juu sana. Ndio maana kwenye makampuni yanayotafuta faida, hata kwenye idara zao za R&D unakuta ni mara chache sana kuna maprofessa huko!!!!

Kwa hiyo Mnyika na Zitto waanapractise ndio maana wanaonekana kazi zao, kuna vijana wengi vipanga kwa maana hata shuleni hawajaunga unga na pia vichwani wako fiti sana but hawana platform ya kutokea,,, kwenye taifa makini huwa wanatafutwa na kupelekwa sehemu stahiki!!!
 
Kaka Kilitime

Naomba turejee kwenye mjadala mama "CHADEMA Must Reform". Naona sasa tunaelekea kujadili nani ana 'pua ndefu' kati ya Kitila, Mnyika na Zitto....(mzaha)

Tuendelee kujadili.

Nasubiri Rev. Kishoka na wengine waje na hoja za ziada kuhusu maboresho ya CHADEMA.

Kweli kaka Alaa! kumbe nimetoka nje ya mstari!!! Mdogo wetu, tukipata fursa ya kufunda na kusema ukweli tunamwaga hapo hapo!

Nimesoma katiba yenu kwa kuanzia nzuri only that itahitaji several frequent reviews, kwa kuwa imeingiza mambo mengine ambayo si lazima yawe kwenye katiba!mengine yanakuwa kwenye ilani za uchaguzi tu! au kwenye program za chama! Katiba nzuri ni ile ambayo inabeba makubwaya ujumla na kuacha details kanuni, ilani na program mbalimbali kwenye.

Mna pakuanzia, sasa tafuteni viongozi wa kukipeleka chama mbele!! Hakikishesheni chama kinakuwa real taasisi, maadili ya wanachama na viongozi. yanaheshiwa.!
 
Mnyika, Kilitime

Nafikiri ni wakatiumewadia kuwa tunabadilisha mwelekeo wa fikira zetu na nguvu za ushawishi na kuwa ni nguvu za kujenga Taifa na si kuhoji tuu yaliyotokea.

Nimeipitia katiba ya Chadema jana ni nzuri. Nikajiuliza mfumo wake na kama Mnyika navyoelezea hapa inaelekea ni mzuri. Sasa tatizo ni lipi kuwa haina wafuasi wengi hasa vijana na wanataaluma? au ni kwa kuwa wengi wanaogopa mkono wa dola (CCM)?

Kikubwa ambacho kinakera ni kwa Chama cha upinzani chenye nguvu kama Chadema kuonekana kina kosa uadilifu kama CCM. Na hii inatokana na hisi azilizojengeka tangu awali eti n Chama cha Wachaga na kuna ukabila na undugunization.

Ndio maana nikasema, ili Chadema kiwe kamilifu (at least 85%) inabidi kibadili mfumo wake wa kiutendaji na utawala na isionekane kuwa hiki ni chama cha Mtei na mkwewe Freeman.

Nimefurahia jinsi Mnyika ulivyo na uamsho na imani katika chama chako, swali ni jee ni wangapi katika chama Chako wenye mtazamo kama wako?

Jumuiya yenu ya vijana ina nguvu kiasi gani kupambana na Nchimbi na wafuasi wake? Nguvu ninazoulizia ni za mfumo wa utandawazi, mawazo, kujitolea na uhamasishaji si nguvu za fedha ambazo najua Chadema haina kufananisha na Chama Cha Machotaji!

Ni tumaini langu kuwa kama Chadema itaongeza mwendo kasi wake wa reforms and si kusua sua, basi mnaweza kupata japo 15% ya viti vya Bunge.

Reformation ya Chadema ni lazima iende kwa slogan ya Kikwete, Ari, Kasi na Nguvu mpya. Nafikiri mkiendelea kuchelea kufanya kweli ili kwenda na wakati na kupambana na ufidhuli wa CCM, basi itawachukua miaka 46 kufika mahali CCM ilipo leo kimuundo na kiutandawazi.
 
Mnyika,
Pamoja na maelezo mazuri yaliotolewa hapo juu kukusifia- na wewe kujitetea kuwa kwa sasa umejitoa kutengeneza 'Tz Mbadala'- hii ni 2007 na uchaguzi ni 2010- pamoja na kuwa hili ni jukumu binafsi- je una nia gani ya kusoma zaidi ili kupata exposure ktk Party politics? International Relations? n.k?

Tunaona Mbowe anasoma kwa sasa Hull- na elimu haina mwisho- kumbuka elimu ya ngazi fulani ni tam na ina manufaa sana ktk umri fulani!

Una maoni gani kwa hilo?
 
Mnyika,
Pamoja na maelezo mazuri yaliotolewa hapo juu kukusifia- na wewe kujitetea kuwa kwa sasa umejitoa kutengeneza 'Tz Mbadala'- hii ni 2007 na uchaguzi ni 2010- pamoja na kuwa hili ni jukumu binafsi- je una nia gani ya kusoma zaidi za kupata exporure ktk Party politics? International Relations? n.k?

Tunaona Mbowe anasoma kwa sasa Hull- na elimu haina mwisho- kumbuka elimu ya ngazi fulani ni tam na ina manufaa sana ktk umri fulani!

Una maoni gani kwa hilo?

Nashukuru. Nia ninayo. Soma maelezo yangu katikati ya mstari, ndio maana nimesema bado kitambo kidogo nitatoweka. Tuendelee kujadili "CHADEMA must reform"

JJ
 
Mnyika, Kilitime

Nafikiri ni wakatiumewadia kuwa tunabadilisha mwelekeo wa fikira zetu na nguvu za ushawishi na kuwa ni nguvu za kujenga Taifa na si kuhoji tuu yaliyotokea.

Nimeipitia katiba ya Chadema jana ni nzuri. Nikajiuliza mfumo wake na kama Mnyika navyoelezea hapa inaelekea ni mzuri. Sasa tatizo ni lipi kuwa haina wafuasi wengi hasa vijana na wanataaluma? au ni kwa kuwa wengi wanaogopa mkono wa dola (CCM)?

Kikubwa ambacho kinakera ni kwa Chama cha upinzani chenye nguvu kama Chadema kuonekana kina kosa uadilifu kama CCM. Na hii inatokana na hisi azilizojengeka tangu awali eti n Chama cha Wachaga na kuna ukabila na undugunization.

Ndio maana nikasema, ili Chadema kiwe kamilifu (at least 85%) inabidi kibadili mfumo wake wa kiutendaji na utawala na isionekane kuwa hiki ni chama cha Mtei na mkwewe Freeman.

Nimefurahia jinsi Mnyika ulivyo na uamsho na imani katika chama chako, swali ni jee ni wangapi katika chama Chako wenye mtazamo kama wako?

Jumuiya yenu ya vijana ina nguvu kiasi gani kupambana na Nchimbi na wafuasi wake? Nguvu ninazoulizia ni za mfumo wa utandawazi, mawazo, kujitolea na uhamasishaji si nguvu za fedha ambazo najua Chadema haina kufananisha na Chama Cha Machotaji!

Ni tumaini langu kuwa kama Chadema itaongeza mwendo kasi wake wa reforms and si kusua sua, basi mnaweza kupata japo 15% ya viti vya Bunge.

Reformation ya Chadema ni lazima iende kwa slogan ya Kikwete, Ari, Kasi na Nguvu mpya. Nafikiri mkiendelea kuchelea kufanya kweli ili kwenda na wakati na kupambana na ufidhuli wa CCM, basi itawachukua miaka 46 kufika mahali CCM ilipo leo kimuundo na kiutandawazi.

Rev. Kishoka

Vijana wanataaluma na vijana wa kawaida wanazidi kuongezeka CHADEMA, changamoto ni jinsi ya kuwafanya kila mmoja atimize wajibu wake kama mwanachama. Mwaka huu mipango ya chama haikiruhusu kuunda oganizesheni ya Baraza La Vijana wa CHADEMA(BAVICHA), kuanzia mwakani hii ndio kazi tunayoifanya kama vijana. Hivyo, natarajia wanataaluma vijana nao watachukua majukumu katika mkondo wa BAVICHA badala ya kukaa pembeni na kushabikia tu. Ikifika mwisho wa mwaka utaweza kupima vizuri uwezo wetu wa kupambana na UVCCM. Lakini kwa upande wa PR, na kusimamia masuala haki za vijana kwa kweli CHADEMA tuko mbele.

CHADEMA imekosa uadilifu kama CCM kivipi? Kwa kweli CHADEMA si chama cha mafisadi! Hizo hisia ulizozitaja naamini nimezitolea ufafanuzi katika thread zingine, unajua hisia zikiachwa zikatawala mwishowe huaminika kuwa ni ukweli wenyewe- ni wajibu kuzikabili kwa hoja.

Kwa kweli tunaendeleza reforms kwa misingi ya "Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke". Ujumbe wa hizi reforms ni 'CHADEMA- Tumaini Jipya'. Na kauli mbiu yake ni "CHADEMA: Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli"

Ari, NGUvu na KAsi Mpya bila maudhui yanayoeleweka ni mhemko, mabavu na mbio za kufukuzana na upepo, inaweza kuwa ni kwenda mbele au kurudi nyuma ama kujikwaa kabisa na ku- A.NGU.KA.

JJ
 
Nashukuru. Nia ninayo. Soma maelezo yangu katikati ya mstari, ndio maana nimesema bado kitambo kidogo nitatoweka. Tuendelee kujadili "CHADEMA must reform"

JJ

Mnyika,

Hivi unaweza kuturushia CV yako? Au kama iko kwenye mtandao basi ninaiomba link yake. Samahani kwa usumbufu.
 
Mnyika,

Hivi unaweza kuturushia CV yako? Au kama iko kwenye mtandao basi ninaiomba link yake. Samahani kwa usumbufu.

Kaka

Sijui ni CV kwa ajili gani kwa kweli, maana zipo za namna mbalimbali. Ila kama ni kwa lengo la kupata wasifu tu unaweza kubonyeza hapa: http://www.chadema.net/uongozi/taifa/mnyika.php au hapa: http://www.esrftz.org/BUDGET/CORU_out2_inc_archive.asp?Id=1066&Year=2005 , japokuwa naona zote ni za nyuma kidogo lakini naona zinaweza kukusaidia. Alternatively, just google search.

I hope i has nothing to do with "CHADEMA must reform"

JJ
 
Mwe! kumbe we Mnyika dogo namna hii??

Hata hivo nadhani unakipaji fulani, kweli wazo la kwenda shule ni zuri sana isije kuwa kikwazo mbele yako. Good job, na Mungu akufanikishe.

Back to CHADEMA nadhani inakwenda vyema, la msingi ni kujiimarisha hasa huko maeneo ya pepmbezoni kwani wapiga kura wapo huko, na hata wenye uelewa mdogo wa kinacho endelea!
 
Mnyika,

Samahani nilishindwa kuwasiliana nawe tena kwa ajili ya dharura, nitakutafuta baada ya Krismas.

Air, Kasi na Nguvu ya Reforms ni muhimu. Naamini kuwa Chadema ni chama makini, hivyo woga wa kuanguka usiwepo. Kuanguka ni kawaida katika safari, waamka pukuta mavumbi na kuendelea huku ukijiuliza ni vipi ulianguka?

Kama kuanguka, mmeshaanguka, mmejipukutisha, lakini inabidi muongezo kasi ya mageuzi ambayo itawasaidi kung'ara 2010!

Sualal nililoliongelea kuwa ni la ki CCM ni lile la Ukabila na Ukoo ambalo limekuwa likiliandama Chadema tangu kuundwa kwake. Hisia za Watanzania pamoja na kuwa ni kweli si Chama cha Wachaga pekee au ukoo wa Mtei zimetapakaa kwenye mawzo ya Watanzania na CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhakikisha hisia hizo bado zipo na kuaminika.

Ndio maana nasema, mabadiliko ya haraka yanahitajika ambayo yataondoa ukungu wote ambao umekitia chama chenu doa.

CUF wanatatizo moja ambalo ni la wazi na kamwe hawataweza kufanikiwa mpaka wabadilike. Kwa wengi, CUF ni chama cha Kizanzibari na Udini! Ushahidi ni mkubwa hata katika uwakilishi wao katika Bunge na hoja wanazopigania.

Chadema has opportunity to be the only party that will reform the political spectrum of Tanzania and change the structure of Political systems that could lead to real solutions to critical things such as Katiba ya nchi na Muungano.

CCM had that opportunity, lakini they have decided to focus on their tummies and being a big bully who oppresses everytghing under democracy.

I am looking forward to work with you and share our passion for Taifa letu.
 
Mnyika
Chama chenu vilevile kinatakiwa kuwa na financial muscle, mmejiandaa vipi kuhakikisha kuwa chama chenu kina pesa za kutosha? au ndio mnategemea tu michango ya wanachama na membership fee.

2010 inaonekana kama iko mbali, lakini kwa uchaguzi iko karibu, mmeangalia weakpoints (zipo nyingi) ambazo mnaweza kucapitalize kwenye viti vya udiwani na ubunge, walau mkaongeza idadi ya wabunge?

Au lengo lenu ni kuendelea kuwa na wabunge hawahawa wachache waliopo?
 
Kaka

Sijui ni CV kwa ajili gani kwa kweli, maana zipo za namna mbalimbali. Ila kama ni kwa lengo la kupata wasifu tu unaweza kubonyeza hapa: http://www.chadema.net/uongozi/taifa/mnyika.php au hapa: http://www.esrftz.org/BUDGET/CORU_out2_inc_archive.asp?Id=1066&Year=2005 , japokuwa naona zote ni za nyuma kidogo lakini naona zinaweza kukusaidia. Alternatively, just google search.

I hope i has nothing to do with "CHADEMA must reform"

JJ

JJ,

Chama ni wanachama na viongozi, na wasifu wa viongozi na wanachama wanafanya chama kiwe na sura fulani, hivyo kuwajuwa wanachama/viongozi ni haki ya wananchi ambao wataongozwa na viongozi na wananchama hao especially pale chama husika kitakapochukua dola!!!

kwa hiyo niruhusu kidogo niulize swali kwenye wasifu wako!!!
Kuna disconnect moja kidogo pale kwenye form six kwenda chuo kikuu... kama ulivyoweza weka vizuri matokeo yako ya Darasa la Saba na Darasa la Kumi na mbili tunaomba ugusie kidogo matokeo ya darasa la kumi na nne!!! naona kuna-ka-disconnect kidogo mkuu... natanguliza msamaha...

Baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka 2001,alijiunga na chuo cha diplomasia cha jijini Dar es salaam katika kozi ya itifaki na mahusiano ya jamii. Baadaye aliajiriwa na Redio Tanzania Dar es salaam (RTD) katika kitengo cha PRT na kufanya kazi ya utangazaji kwa mwaka mmoja. Akiwa RTD bado aliendelea na harakati za vijana kupitia NYF mpaka taasisi hiyo ilipofutwa na serikali. Aliendelea pia na harakati za utetezi wa wanafunzi kupitia mtandao wa wanafunzi Tanzania 'TSNP'ambayo yeye ni mmoja wa waanzilishi wake.

Alijiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) mwaka 2002 kusoma shahada ya kwanza ya utawala wa biashara (BBA) katika programu ya jioni. Sambamba na masomo ya jioni katika chuo kikuu cha Dar es salaam, ameendelea kuwa muajiriwa wa United Nations Association (UNA) kama mratibu msaidizi wa mradi wa ushiriki wa vijana unaotekelezwa na kitengo chake cha vijana (YUNA) katika wilaya kumi nchini Tanzania.
 
JJ,

Chama ni wanachama na viongozi, na wasifu wa viongozi na wanachama wanafanya chama kiwe na sura fulani, hivyo kuwajuwa wanachama/viongozi ni haki ya wananchi ambao wataongozwa na viongozi na wananchama hao especially pale chama husika kitakapochukua dola!!!

kwa hiyo niruhusu kidogo niulize swali kwenye wasifu wako!!!
Kuna disconnect moja kidogo pale kwenye form six kwenda chuo kikuu... kama ulivyoweza weka vizuri matokeo yako ya Darasa la Saba na Darasa la Kumi na mbili tunaomba ugusie kidogo matokeo ya darasa la kumi na nne!!! naona kuna-ka-disconnect kidogo mkuu... natanguliza msamaha...

Kilitime

Mbona yote yapo hapo hapo? Ni vyema ukasoma vizuri tu- unaweza pia kutembelea hiyo link nyingine mwandishi ameandika kwa undani zaidi http://www.esrftz.org/BUDGET/CORU_out2_inc_archive.asp?Id=1066&Year=2005 , . Asante.

Turejee saa kujadili reforms za CHADEMA maana naona sasa mnakaribia kugeuza huu mjadala kuwa "Mnyika Must reform"(Mzaha).

Tutazame picha kubwa zaidi! Mnyika ni tone dogo tu katika CHADEMA kama taasisi- tujadili masuala, badala ya watu ama matukio- chambelecho cha simple, ordinary and great minds.

JJ
 
Back
Top Bottom