Nguruvi3, I don't know what is more painful, kuangalia picha ya mabaki ya Daudi Mwangosi au kusoma hii report ya Nchimbi? Report inaonesha ni jinsi gani Jaji Ihema na wapambe wake wanavyoona watanzania ni mazuzu! Na inaelekea walichokifuata Iringa ni eneo la kukaa na kuandika mambo ambayo walishakubaliana.
Nimesoma kwa kurukaruka sehemu maana report imejaa upuuzi wa viwango vya juu sana. Inaharibu kabisa taswira ya majaji wetu pamoja na mwandishi wa habari Theophil. Yaani pamoja na vielelezo vyote (stilll and moving pictures) bado wanaleta habari za kutunga? Kama sio madharau kwa watanzania ni nini?
Kama huyu Jaji na wenzake walikuwa na nia njema wangeanza kwa kuuliza amri ya vyama vya siasa kutofanya mikutano wakati wa sensa ilihusu chama kimoja au vyote? Na amri hiyo ilihusu mikutano ya hadhara au mikutano ya ndani? Na CHADEMA walikuwa na mkutano wa hadhara au wa ndani?
Pili, maaskari waliokuwa kwenye eneo la tukio wote ni wa mahali hapo? kama jibu ni hapana, walikuja lini, na kwa sababu zipi?
Lakini kuna mambo kwenye hii report yanatia kichefuchefu. Jaji Ihema anaonekana ku-suggest kuwa Daudi Mwangosi aliuwawa na mtu/watu wengine mbali na polisi! Na anaenda mbele zaidi na kutoa maoni kuwa vikundi vya ulinzi kama Green guards, blue, guards and red guards viangaliwe upya. Moja kwa moja utaona kuwa anachosema jaji ni kwamba Daudi Mwangosi aliuliwa na moja ya hivyo vikundi?
Yote tisa, kumi Jaji anatoa mapendekezo ya kufuta shughuli za siasa nje ya bunge!
Kwa maoni yangu, hii tume ilikuwa na kazi maalum, kazi ya kuungaunga habari ili wapate nafasi ya kuchomekeza mapendekezo 'maalum' kama kuweka sheria ya kukandamiza vyama 'vya msimu' na kumpa msajili wa vyama vya siasa nguvu ya kuburuza vyama vinavyosumbuwa wakubwa.
Kwa zama tunazoishi sasa, ni kituko tena kituko kweli kweli kuandaa report chafu kama hiyo. Watanzania wengi wanajua mkanda mzima wa mauaji ya Daudi Mwangosi. Kamati ingejiwekea heshma kwa kuleta report inayoeleka na sio hizo ngonjera za mwaka 47. Yaani wameingiza mpaka points za Shibuda?!
-Kuhusu operesheni ya uzuiaji wa mkutano wa CHADEMA usio halali Kijijini Nyololo tarehe 02 Septemba 2012, Jeshi la Polisi lilitekeleza wajibu wake ipasavyo na kutumia nguvu sahihi. Operesheni iliyoandaliwa na kufanyika ilikamilika kwa kuwatawanya watu waliofika kwenye mkutano, kukamata baadhi ya Viongozi na wafuasi wa CHADEMA na hali ya utulivu ilirejea kwenye eneo husika. "
nimewatukana tusi kubwa kuliko yote hapa duniani na ahera,nchimbi na kamati yako wote!
mods tunaomba ruhusa ya lugha chafu japo dk 5 tu kwa hili liripoti la kik..
report ni nzuri nadhani imejaribu kutoa picha halisi ya kilichotokea siku ya tukio
Kwa minajili hii basi Kamati imeshindwa kubaini baada ya kumalizika operesheni na askari Polisi kuanza kuondoka, kwa nini Mwangosi alishambuliwa kwa kipigo kabla ya kulipuliwa na bomu la kishindo?
Mods, naomba kwa mara ya kwanza toka nijiunge na JF nitukane mtu. Walioandika hii ripoti ingefaa wakamatwe mara moja na kufikishwa wanakostahili kwa uwongo na wizi wa kujipatia hela kwa njia ya udanganyifu bila kuifanyia kazi. Hawana tofauti na mlevi aliyeshiba pombe ya pingu na kama ilivyo kawaida kalowa na bila akili anajipitisha pitisha mbele za watu bila kujitambua kuwa anatoa harufu kali ya kunuka hadi hata nzi wanamkwepa. Naapa na nasema wazi kuwa kama moja wa hawa watu angekuwa ndugu yangu, nisingeongea naye tena katika maisha yangu...ni aibu, ni aibu na ni aibu. Halafu moja wao anajiita Jaji na mwingine anajiita Mwandishi, what? Hivi tumemkosea nini Mungu? Naomba niishie hapa!FJM, yapo mengi sana yanyotia uchungu kama kifo cha Mwangosi aliyekuwa anatafuta mkate wa familia.
Yapo yanayoudhi sana na kutia hasira:
1. Kutumia kifo cha Mwangosi kuficha 'wahalifu' wakubwa akina Chagonja, Kamuhanda n.k.
2. Kutumia kifo cha Mwangosi kuficha wahuni wa siasa kama akina Nchimbi
3. Kutumia kifo cha Mwangosi kuudanganya umma
4. Kutumia kifo cha mwangosi kukaa mahali na kutunga uongo
Kinachosikitisha sana ni kuelewa kuwa wapo watu wengi waliohukumiwa na Jaji Ihema. Watu hawa wahawakutendewa haki kwasababu Jaji Ihema ameonyesha uelewa kidogo (in fact kutoelewa) anachokifanya.
Ameandika ripoti ambayo mtoto wa kidato cha sita angeweza kuiandika vizuri zaidi kama insha.
Kinachotia kichefu chefu ni Theophili Makunga, mtu anayedhaniwa kuwa mwandishi na mwenye weledi kukaa pamoja na Jaji Ihema na kutunga upuuzi usiolingana na taaluma yoyote isipokuwa kama ipo ya wapuuzi.
Tunaichambua habari hiyo na tutarejea na kipengele kimoja baada ya kingine ili kuonyesha kuwa hatumtukani wala kumdhalilisha Ihema na Makunga, bali wamejidhalilisha wenye.
Tanzania bwana! sasa kwanini report ni ya kiingereza?
Nani bigwa hapo?duh ukisoma ripoti ya MCT na ya Nchimbi --- BIG DIFERENCE
Ya MCT mpaka nimepata shule ya jinsi ya kuandika vitu. Good one.
Watu 3 vs watu 7 akiwamo Jaji....