Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Siku ya leo sijui tuuiteje huko; Mbaya? Au nzuri sana?

Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali inayoendelea kusomwa muda huu si kwamba tu inawaweka CCM na watetezi wa mwendazake kwenye wakati mgumu sana, lakini tayari imechefua wananchi wengi kwa kiwango kisichomithilika.

Madudu ya SHUJAA WA AFRIKA yanatisha na kutia kinyaa.

Madudu ya MTETEZI WA WANYONGE Yanatia hasira sana.

Chukulia hili moja BILIONI 3.9 kwenye matengenezo ya ndege moja ambayo HAIKUFAA!

Upinzani uliwahi kusema upigaji wa awamu hii utavunja rekodi, watu wakabeza sana. Lakini wakati ni hakimu mzuri. Uongo hupanda lift lakini ukweli hukwea ngazi. Mahakama ya mafisadi inaweza kuanzia pale kwenye nyumba ya milele ya mwendaAzakwe marehemu hayati.

Huu uozo uliendelea kuwekwa wazi peupe hivi tusishangae kuona siku moja marehemu akalikimbia kaburi lake. N itokee kuna kitu kinaitwa maandamano kifanyike Bila udhibiti imara si ajabu kuwakuta waandamanaji wakilicharaza bakora kaburi la shujaa wa Afrika na kuipopoa mawe picha yake.

Baada ya kusomwa hii ripoti, masikio yote yako kwa Bimkubwa. Je, atasemaje? Watu wamefura kwa hasira. I hope hatawazingua
Mahabusu ziandaliwe za kutosha sasa. Ni zamu ya kubadilisha wapangaji. Karibia kila wizara ina vimeo vya kutisha.
 
Shida yetu kubwa ni kwamba tunapojadili haya mambo hatuji na masuluhisho. Na kila mwaka ni yale yale. Upigaji wa kutisha!

Kama jamii tufanye nini ili kuikomesha hali hii? Tunawezaje kuukomesha ufisadi? Kwa nini viongozi wetu wanakuwa hivi? Tufanye nini?

Mwendazake keshalala. Hata tukipopoa mawe na kucharaza bakora kaburi lake hatatusikia. Kimbembe ni kwetu tuliobakia. Ni kweli hatuwezi kuikomesha hali hii?
 
Mada ya 2018

Awamu ya tano imetupa pembeni utaratibu wa zabuni na sasa inaamua na kufanya manunuzi au kuingia mikataba wenyewe kwa amri toka juu...

Rejea hii itatukumbusha siku za usoni na hasa kwa Miradi hii.

1. Uwanja wa ndege chato
2. Vitambulisho vya utaifa
3. Fly overs
4. Bombadier
5. Tenda za ujenzi za TBA n.k
6. SGR
7. Bwawa la umeme

Kwa kumalizia tuu.... nimeandika hayo nikiwa full detailed. Kuna vitu duniani havichiki navyo ni Jua mwezi na ukweli.

MUDA NI HAKIMU WA YOTE!!

Credit kwako Lusungo
 
Ripoti ya CAG ni sawa na repoti ya matokeo ya final exams
Sio wote wanapata A, B, C wapo pia wa D, E....... na yote hayo ni matokeo

Tusubiri hati safi na chafu tujue wale walioPass na walioDisco
Screenshot_20210408-152546.jpg
 
Aibu kubwa sana!
Spika wa Bunge Job Ndugai amewaasa wbunge kuchangia kwa uwazi bila kuogopa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022 na sio kusubiri serikali ifeli kisha walaumu

Spika amesemakwa mfano Taarifa ya CAG imeonyesha ATCL imepata hasara ya bilioni 60 na kuuliza je ni sahihi kuendelea kununua ndege nyingine?

Pia ameshauri sekta binafsi kuhusishwa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa kama kununua mabehewa ya treni za kisasa zitakazokuja na sio kila kitu kufanya Serikali huku akisema wabunge nao inabidi washiriki na sio kuwaachia wawekezaji wa kutoka nje pekee japo nayo ni vizuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom